Jibu: Neno Utakatifu linatokana na Neno “utakaso”.. kitu lilichotakasika kinaitwa “kitakatifu”.. na kitu kilichotakasika/takata maana yake hakina uchafu.
Kwahiyo utakatifu kwa tafsiri rahisi maana yake ni “kuwa safi, (kutokuwa na uchafu)”.. Mtu anaweza kuwa msafi (mtakatifu) mwilini na rohoni.
Sasa kikawaida kitu chochote kinapokuwa safi, huwa kinatoa Mng’ao unaopendeza.. sasa ule mng’ao unaotafsiri usafi wa kitu kile ndio unaoitwa UTUKUFU, kwamfano dhahabu inaposafishwa na kuwa safi huwa inatoa mng’ao mzuri wa kipekee, sasa ule mng’ao ndio utukufu wa ile dhahabu au kito, na vitu vingine vyote ni hivyo hivyo.
Hali kadhalika mtu aliyetakaswa dhambi zake kwa damu ya YESU, na yeye mwenyewe kujilinda na kujitenga na uchafu wote wa rohoni na mwilini, basi mtu huyo ni mtakatifu na anao utukufu, ambao ni NURU inayong’aa, ambayo shetani na mapepo yake hayawezi kustahimili mwako wake.
Lakini zaidi sana MUNGU wetu aliyetuumba ndiye mwenye utukufu MKUU, ambao huo unatokana UTAKATIFU alionao, uzidio viumbe vyake vyote.. Mng’ao wa utukufu wake hata malaika wanainama mbele zake na kujifunika kwa mbawa zao, na utukufu wake unang’aa mpaka duniani.
Isaya 6:1 “Katika mwaka ule aliokufa mfalme Uzia nalimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu sana na kuinuliwa sana, na pindo za vazi lake zikalijaza hekalu.
2 Juu yake walisimama maserafi; kila mmoja alikuwa na mabawa sita; kwa mawili alifunika uso wake, na kwa mawili alifunika miguu yake, na kwa mawili aliruka.
3 WAKAITANA, KILA MMOJA NA MWENZAKE, WAKISEMA, MTAKATIFU, MTAKATIFU, MTAKATIFU, NI BWANA WA MAJESHI; DUNIA YOTE IMEJAA UTUKUFU WAKE”.
Naam nasi tuliompokea YESU ni lazima tufanane naye, na hatuwezi kuwa na utukufu bila kuwa watakatifu, na hatuwezi kukosa utukufu tukiwa watakatifu, na kuwa mtakatifu duniani inawezekana..
Zaburi 16:3 “Watakatifu waliopo duniani ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao”.
Bwana atusaidie.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
JE UMEUFIKIA ULE UTUKUFU HALISI WA MANA?
NYUMBANI MWA BABA YANGU MNA MAKAO MENGI.
About the author