Swali: Kuna tofauti gani kati ya Ahadi na Nadhiri, kwa mujibu wa Biblia?
Jibu: Ahadi ni Neno/tamko la hiari mtu analolitoa kwa mtu mwenzake, kwamba atalitenda katika wakati mfupi au mrefu ujao.
Kwamfano mtu anaweza kuahidi kuwa kesho atawasili katika hafla, na hiyo kesho kweli akafika kama alivyoahidi, hapo anakuwa ameitimiza ahadi yake, lakini asipowasili kama alivyoahidia anakuwa hajaitimiza ahadi, na ni dhambi ikiwa hakuwa na sababu za msingi za kuivunja ahadi yake.
Lakini katika upande wa Nadhiri, hii ni ahadi (yaani tamko ya hiari) mtu analolitoa kwa MUNGU, na si kwa mtu.
Kwamfano mtu anaweza kuahidi kuwa endapo akipona ugonjwa unaomsumbua atamtolea MUNGU sadaka ya shukrani, au endapo Mungu akimtendea jambo Fulani basi atamtolea MUNGU sadaka Fulani, hiyo inakuwa ni nadhiri.
Na mtu asipotimiza Nadhiri aliyomwekea MUNGU inakuwa ni dhambi..
Mhubiri 5:4 “Wewe ukimwekea Mungu nadhiri, usikawie kuiondoa; KWA KUWA YEYE HAWI RADHI NA WAPUMBAVU; BASI, UIONDOE HIYO ULIYOIWEKA NADHIRI.
5 Ni afadhali usiweke nadhiri, Kuliko kuiweka usiiondoe.
6 Usikiache kinywa chako kuukosesha mwili wako; wala usiseme mbele ya huyo malaika ya kwamba umepitiliwa; kwani Mungu akukasirikie sauti yako, na kuiharibu kazi ya mikono yako?”
Kwahiyo ni muhimu kuitimiza ahadi tunazozitoa na pia Nadhiri uliomwekea MUNGU.
Ikiwa kuna sababu zozote za msingi zilizojitokeza za kutotimiza ahadi basi ni vizuri kufanya mapatano na uliyemhadi mapema ili isigeuke kuwa uongo.
Bwana atusaidie.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
JE! USIPOTIMIZA NADHIRI ZAKO ZOTE KWA BWANA. HAWEZI KUKUSAMEHE?
About the author