SWALI: Kwanini yule mtu hakukutwa na vazi la arusi wakati naye pia alialikwa?. Inamaana wale wengine walipewa mavazi siku ile ya kuingia karamuni?
Mathayo 22:1 “Yesu akajibu, akawaambia tena kwa mithali, akisema,
2 Ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyemfanyia mwanawe arusi.
3 Akawatuma watumwa wake wawaite walioalikwa kuja arusini; nao wakakataa kuja.
4 Akatuma tena watu kwa wengine, akisema, Waambieni wale walioalikwa, Tazameni, nimeandaa karamu yangu; ng’ombe zangu na vinono vimekwisha kuchinjwa, na vyote vimekuwa tayari, njoni arusini.
5 Lakini hawakujali, wakaenda zao, mmoja shambani kwake, mmoja kwenye biashara yake;
6 nao waliosalia wakawakamata watumwa wake, wakawatenda jeuri, na kuwaua.
7 Basi yule mfalme akaghadhibika; akapeleka majeshi yake, akawaangamiza wauaji wale, akauteketeza mji wao.
8 Kisha akawaambia watumwa wake, Arusi i tayari, lakini wale walioalikwa hawakustahili.
9 Basi enendeni hata njia panda za barabara, na wote mwaonao waiteni arusini.
10 Watumwa wale wakatoka wakaenda njia kuu, wakakusanya wote waliowaona, waovu kwa wema; arusi ikajaa wageni.
11 Lakini alipoingia yule mfalme ili kuwatazama wageni wake, akaona mle mtu mmoja asiyevaa vazi la arusi.
12 Akamwambia, Rafiki, uliingiaje humu nawe huna vazi la arusi? Naye akatekewa.
13 Mfalme akawaambia watumishi, Mfungeni mikono na miguu, mchukueni mkamtupe katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
14 Kwa maana waitwao ni wengi, bali wateule ni wachache”
JIBU; Ndio wote waliolikwa pale walipewa vazi la arusi, kulikuwa na utaratibu walioupitia kwanza kabla ya kuingia kule harusini, kila aliyefika pale alihakikiwa kwanza na alipoonekana amekidhi vigezo ndipo akapewa vazi lile la Harusi, lakini yule mwingine alidhani ni kuingia tu, na yeye akajichanganya katikati ya kundi kinyemelewa..Na mwisho wa siku atakambulikana kwa mavazi yake yaliyotofauti na wengine….
Ndio makundi mawili yaliyopo katika kanisa la Kristo leo hii…wote wanasema yanasema nimeokoka nitakwenda mbinguni!! Lakini lipo linalotii na kufuata maagizo yote Kristo aliyoliekezeka..lakini lipo lingine linadhani maadamu tayari limeshakuwa mshirika wa kanisa basi hiyo inatosha, maadamu linatoa zaka, basi inatosha, maadamu linaimba kwaya inatosha, hakuna haja ya kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi, hakuna haja ya kuishi maisha matakatifu, hakuna haja ya kuomba, hakuna haja ya kujikana nafsi na kumfuata Kristo, hakuna haja ya kuhakiki ni nini kimpendezacho Bwana, na ni kipi hakimpendezi, lenyewe halina mzigo wowote na dhambi, linachopenda ni kuhubiriwa mafanikio tu, na kubarikiwa, lakini likigusiwa habari za toba halipendi.
Kufanya uzinzi ni kitu cha kawaida kwao, kuvaa nguo za nusu uchi si jambo ajabu pia, kuvaa suruali (wanawake) linaona ni sawa, kunywa pombe ni sawa, kwenda disko ni sawa, kukaa kwenye kampani za kidunia hakuna shida yoyote..
Sasa hawa katika ulimwengu wa roho, ni kweli waliitwa na Bwana lakini hawakuteuliwa…kwasababu hawakuwa tayari kulitwaa vazi jeupe la harusi ambalo ndio kama tiketi ya kuingia mbinguni.
Ufunuo 19:7 “Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari.
8 Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing’arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu.
9 Naye akaniambia, Andika, Heri walioalikwa karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo. Akaniambia, Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu”.
Unaona?, hiyo kitani nzuri, ing’arayo safi ya kuingia karamuni ni matendo ya haki ya watakatifu…Hivyo na sisi hatutaingia mbinguni kwenye karamu ya mwanakondoo kama matendo yetu hayatakuwa ya haki hata kama tutajiita tumeokoka vipi… Haijalishi Bwana Yesu alitutokea, au tuliona maono, au tulitubu mwanzoni na Mungu akasikia toba yetu, kama hatutajizoeza kuishi maisha matakatifu biblia inasema hatutaweza kumwona Mungu pasipo huo (Waebrania 12:14)
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii 0789001312
Mada Nyinginezo:
Naomba kujua watakaoenda mbinguni je! ni wengi au wachache?
Kuna ufufuo wa aina ngapi?
Kuna hukumu za aina ngapi?
Ule mfano wa wanawali 10 (Mathayo 25), wale watano hawakuwa na mafuta ya ziada katika chupa zao je yale mafuta ya ziada yanawakilisha nini?
KILA MTU ATATOA HABARI ZAKE MWENYEWE.
SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?
JUMA LA 70 LA DANIELI
MPINGA-KRISTO
MKUU WA ANGA.
About the author