MAOMBI NI NINI

MAOMBI NI NINI

Maombi ni nini?


Neno maombi limetokana na neno kuomba, Kwamfano mtu unapokuwa na hitaji ya kitu Fulani, labda tuseme kazi, basi huwa unatuma maombi yako kwanza kwenye ofisi husika au shirika, kisha wanapitia  wasifu wako na kule wakisharidhiwa na maombi yako ndio wanakurudishia  majibu ya kile ulichokiomba.

Kamwe huwezi ukapeleka maombi ya kazi,  halafu yakarudi majibu ya mkopo, ya ufadhili, au ya kupewa bima badala yake..Hilo jambo halipo, kwa namna ya kawaida chochote kile unachokiomba ndicho utakachopewa, ukiomba ajira utarudishiwa majibu ya ajira, ukiomba mkopo utarudishiwa majibu ya mkopo, ukomba zabuni utarudishwa majibu ya zabuni, kamwe haiwezi ikavuka hapo.

Maombi ni nini katika ukristo?

Lakini katika Ukristo Maombi, yanavuka hiyo mipaka, hayalengi tu kupeleka hitaji na kujibiwa, halafu basi.. Bali yanakwenda mbele Zaidi na kufanya kazi nyingine nyingi kuliko hizo, na ndio maana maombi ni nyenzo muhimu sana kwa mtu yeyote anayejiita mkristo. Bila maombi umekwisha.

Watu wengi wanadhani, Mungu anakitazama tu kile  tunachokwenda kumwomba kwa wakati huo halafu atujibu iwe imeisha..ni vizuri tukafahamu kuwa kabla hata hatujamwomba Mungu chochote, tayari alishajua ni nini tunachokwenda kumwomba..

Mathayo 6:7  “Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi. 8  Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba”.

Hivyo mbele za Mungu, maombi ni ziadi ya kile tunachokifikiria. Ikiwa anajua tayari tunachokwenda kumwomba, unaweza ukajiuliza ni kwanini sasa atusumbue tuende tukamwombe?..Hapo ndipo utakapojua kuwa maombi kwa Mungu ni Zaidi ya kupeleka mahitaji.

Maombi ni nini..

Pale unapopiga magoti na kumwambia Mungu hiki na kile, hafamfikii tu kama mahitaji peke yake, bali yanajitafsiri kama kitu kingine pia..yanafika kwake kama harusi nzuri ya manukato, kama sauti ya upole ya kumwita aje ndani yako, kuku rehema, kukupa  neema zake, kukuponya n.k. Na hiyo inamfanya Mungu ashuke, na kuanza kuifanya kazi yake ndani ya maisha yako, ambayo hata wewe usiyoyajua..zaidi ya yale aliyokuwa anayaomba.

Na kwa jinsi unavyodumu zaidi katika maombi, ndivyo Mungu anavyotenda kazi zaidi ndani yako.

Mtu ambaye ni mwombaji mzuri, kamwe hawezi kushindwa na majaribu ya shetani, Bwana Yesu alishasema hivyo. Mtu ambaye ni mwombaji mzuri, huwa  nyingi maishani mwake zza mambo ya ajabu ambayo Mungu amemtendea..Vilevile mtu ambaye ni mwombaji mzuri huwa unakutana na Mungu sana katika njia zake.

Tofauti na Yule ambaye haombi kabisa.. Huyo ni sawa na gari linalotembelewa miaka 20 halipelekwi gereji.

Biblia inasema..

1Wathesalonike 5:16  “Furahini siku zote; 17  ombeni bila kukoma;”

Maombi  ni nini? Maombi ni kama karakana ya Mungu ndani ya moyo wa mwanadamu, pale tunapokwenda kuomba, anashuka kuyakarabati Maisha yetu..Hivyo suala la maombi ni jambo linalotakiwa liwe sehemu ya Maisha yetu na sio pale tu tunapojisikia.

Bwana wetu Yesu japo alikuwa ni Mungu katika mwili mkamilifu lakini alikuwa ni mwombaji mkubwa sana..

Luka 6:12  “Ikawa siku zile aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha katika kumwomba Mungu. 13  Hata kulipokuwa mchana aliwaita wanafunzi wake; akachagua kumi na wawili miongoni mwao, ambao aliwaita Mitume”;

Na ndio huyo huyo alituambia..

Marko 14:38  “Kesheni mwombe, msije mkaingia majaribuni, roho i radhi ila mwili ni dhaifu”

Hivyo kama wewe umeokoka na sio mwombaji ni vizuri ukaanza sasa. Na Bwana alitupa kiwango cha kuomba cha siku ambacho walau kila mwaminio anapaswa akifanye..Nacho ni SAA MOJA kwa siku. Luka 14:37..Unaweza ukaona ni kirefu lakini ukijua kuwa yapo mambo mengi ya kuombea hutaona ni kirefu.

Maombi ni nini

Lakini ikiwa bado upo nje ya Kristo, Mungu hawezi kuyaumba Maisha yako vile anavyotaka, Lakini kama leo upo tayari kumkaribisha katika Maisha yako, basi uamuzi unaoufanya ni sahihi..

Bofya hapa kwa ajili ya sala ya toba..>> SALA YA TOBA

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

FAIDA ZA MAOMBI YA USIKU

MAOMBI YA VITA

ZIFAHAMU HOJA SABA ZENYE NGUVU MBELE ZA MUNGU.

DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.

UTAWALA WA MIAKA 1000.

NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE.

UTOE MWILI WAKO KWA BWANA KWASABABU SI MALI YAKO.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments