KUOTA UMEFUNGA NDOA.

KUOTA UMEFUNGA NDOA.

Kuota umefunga ndoa  kuna maanisha nini?


Ndoto ya namna hii mara nyingi inaangukia katika kundi la ndoto zinazozotokana na shughuli nyingi..

Mhubiri 5:3 “Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi; na sauti ya mpumbavu kwa njia ya wingi wa maneno”.

Na hii inatokana na kwamba pengine umekuwa ukiwaza kuoa au kuolewa hivi karibuni, au umekuwa ukitamani sana  kuoa au kuolewa kwa muda mrefu lakini bado malengo yako ya ndoa hujayafikia, au umehudhuria ndoa nyingi, au umezitazama, n.k. 

 Hivyo siku zote zile unachokifanya sana, au unachokiwaza sana, ni lazima kitajirudia tu katika ndoto zako, kama sio mara moja basi ni mara kwa mara, hilo ni jambo la kawaida.

Kwa mfano utakuta mwingine amekuwa akitafuta sana ajira kwa muda mrefu, au amekuwa akiwaza sana  ajira kwa muda mwingi, hivyo mtu kama huyu kuota yupo kwenye interview litakuwa ni jambo la kawaida kwake..

Na ndivyo vivyo hivyo katika kuota umefunga ndoa..mara nyingi ni ndoto itokanayo na shughuli za kila siku.


Lakini pia lipo jambo lingine la rohoni unapaswa ujue. Kumbuka kuwa Mungu huwa anazungumza pia na watu  katika ndoto kwa kupitia Maisha ya kawaida kabisa ya siku zote. Hivyo Ikiwa ndoto hii ya kuota umefunga ndoa imekujia kwa uzito wa kitofauti..

Na ukaifarahia hiyo ndoa na ukatamani ingekuwa hivyo kweli, Fahamu kuwa Mungu anakuonyesha kuwa ipo HARUSI ILIYO BORA NA KUU kuliko hiyo, inayokuja huko mbele. Na hiyo si nyingine Zaidi ya mwanakondoo (Yesu Kristo na kanisa lake)

Hilo usilisahau hata kidogo, katika Maisha yako. Kwasababu biblia inatuambia itakuwa ni Harusi ya pekee sana, ambayo karamu yake itafanyika mbinguni. Wakati huo wapo watu watatamani kuingia lakini waseweze, kitakachobakia kwao ni kilio na kusaga, kwa kuikosa tu.

Harusi hiyo ya Bwana Yesu na kanisa lake sio kama hii ya kimwilini, hapana, bali itakuwa ni ya rohoni, ambapo ndoa inaanzia hapa hapa duniani, na karamu itakuwa ni mbinguni.

Huko ndipo tutakapokutana na mambo ambayo jicho halijawahi kuona wala sikio kusikia..ili kufahamu vizuri jinsi karamu hiyo itakavyokuwa..Fungua hapa >>>>> KARAMU YA MWANAKONDOO

Fahmu kuwa Hizi ni nyakati za mwisho, Unyakuo upo karibu, Yesu yupo mlangoni kurudi, kulinyakua kanisa lake Je! Umeokoka? Umemkabidhi Maisha yako? Kama bado ni vizuri ukafanya uamuzi huo sasa, kukutana na ujumbe huu sio bure.Bali Mungu anayo malengo makubwa na wewe maishani mwako… Fanya hima nawe pia usionekane umeikosa siku ile ya Harusi kuu ya mwana-kondoo.

Ufunuo 19:7 “Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari.

8 Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing’arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu.

9 Naye akaniambia, Andika, Heri walioalikwa karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo. Akaniambia, Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu”

Shalom.

Group la whatsapp Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi

Mada Nyinginezo:

KUOTA UPO UCHI.

KUOTA UNAPAA.

KUOTA UNAOLEWA/UNAOA.

KUOTA UNATOKA DAMU YA HEDHI.

KUOTA UNAOLEWA/UNAOA.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments