Kicho ni hali ya hofu. Kwamfano pale biblia inaposema kicho cha Bwana, inamaanisha hofu ya Bwana.
Hivi ni baadhi ya vifungu vinavyolitaja neno hilo katika biblia;
Matendo 9:31 “Basi kanisa likapata raha katika Uyahudi wote na Galilaya na Samaria, likajengwa, likiendelea na kuongezeka katika kicho cha Bwana, na faraja ya Roho Mtakatifu”.
Waefeso 5:20 “na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo;
21 hali mnanyenyekeana katika kicho cha Kristo”.
Waebrania 12:28 “Basi kwa kuwa tunapokea ufalme usioweza kutetemeshwa, na mwe na neema, ambayo kwa hiyo tumtolee Mungu ibada ya kumpendeza, pamoja na unyenyekevu na kicho”;
Kumbukumbu 7:21 “Usiingiwe na kicho kwa sababu yao; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yu katikati yako, Mungu mkuu, mwenye utisho”.
Kumbukumbu 28:67, 2Samweli 23:3, Ayubu 15:4
Hivyo nasi pia tunapaswa tuwe na kicho cha Mungu ndani yetu, hicho ndicho kitakachotufanya tuishi maisha yampendazayo yeye hapa duniani, tukikosa hofu ya Mungu, hatutaona hata shida kuua, au kuiba, au kuzini, kwasababu hatumwogopi Mungu. Lakini ikiwa kicho chake kinakaa ndani yetu,tutaogopa kufanya mambo yasiyompendeza kwasababu tunajua Mungu wetu ni mkuu sana, anaweza kutenda lolote juu ya maisha yetu.
Yeremia 5:22 “Je! Hamniogopi mimi? Asema Bwana; hamtatetemeka mbele za uso wangu; mimi niliyeweka mchanga kuwa mpaka wa bahari, kwa amri ya daima, isiweze kuupita? Mawimbi yake yajapoumuka-umuka, hayawezi kushinda nguvu; yajapovuma sana, hayawezi kuupita.
23 Lakini watu hawa wana moyo wa kuasi na ukaidi; wameasi, wamekwenda zao.
24 Wala hawasemi mioyoni mwao, Basi, na tumche Bwana, Mungu wetu, aletaye mvua, mvua ya mwaka, na mvua ya vuli, kwa wakati wake; na kutuwekea juma za mavuno zilizoamriwa”.
Bwana atusaidie kicho chake kiumbike ndani yetu.
Shalom.
Angalia maana ya maneno mengine ya biblia chini.
Na ikiwa utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
About the author