Kutabana ni nini? (Mika 5:12)

Kutabana ni nini? (Mika 5:12)

Kutabana ni kitendo kinachofanywa na wachawi cha kutabiri mambo yajayo kwa kutazama vitu fulani. Kwamfano wasomaji nyota, wasomaji viganja, watazamaji wa nyakati mbaya n.k. wote wanatabana

Utalisoma neno hilo kwenye kifungu hiki;

Mika 5:12 “nami nitakatilia mbali uchawi, usiwe mkononi mwako; wala hutakuwa tena na watu wenye kutabana;

13 nami nitakatilia mbali sanamu zako na nguzo zako, zitoke kati yako; wala hutaiabudu tena kazi ya mikono yako”.

Ukweli ni kwamba hakuna kiumbe chochote duniani, mbinguni au kuzimu chenye uwezo wa kutabiri au kujua mambo yajayo isipokuwa Mungu tu peke yake. Alishaliweka hilo wazi kuwa hakuna kitu chochote kinachoweza kujua hatma ya mtu isipokuwa yeye peke yake. Anasema;

Isaya 41:21 “Haya, leteni maneno yenu, asema Bwana; toeni hoja zenu zenye nguvu, asema mfalme wa Yakobo.

22 Wayatangaze na kutujulisha yatakayokuwa; watuonyeshe mambo ya zamani, ni mambo gani, tukapate kuyatia moyoni, tukajue mwisho wake; au wamdhihirishie yatakayotokea baadaye.

23 Tujulisheni yatakayokuwa baadaye, nasi tutakiri ya kuwa ninyi ni miungu; naam, tendeni mema au tendeni mabaya, ili tujipime, tukaone pamoja.

24 Tazameni, ninyi si kitu, tena kazi yenu si kitu; awachaguaye ninyi ni chukizo”.

Hivyo hatupaswi kufiriki kutabana kunaleta matokeo yoyote, zaidi ni kudanganywa  kama sio kurushiwa mapepo. Shetani sikuzote ni mwongo.

Isaya 46:9 “kumbukeni mambo ya zamani za kale; maana mimi ni Mungu, wala hapana mwingine; mimi ni Mungu, wala hapana aliye kama mimi;

10 nitangazaye mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado; nikisema, Shauri langu litasimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote”.

Kama ukiwa ndani ya Kristo, yeye mwenyewe atakufunulia hatma njema ya maisha yako ya sasa na ya baadaye. Lakini ikiwa utatafuta ujuzi au maarifa yoyote ya mambo yajayo kutoka kwa wasoma nyota ujue unapotezwa.

Hivyo kama hujaokoka,  na upo tayari kutubu na kumkabidhi Kristo maisha yako, akufanye kiumbe kipya ni uhakika kuwa mbele yako ipo salama. Je! Upo tayari kufanya hivyo leo? Kama jibu ni ndio basi fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba na kupata maelekezo mengine ya kiroho  >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Tazama maana za maneno mengine ya biblia chini;

Na kama  utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Fumbi ni nini?(Ayubu 6:15)

Chamchela ni nini kwenye biblia?(Zaburi 58:9, Amosi 1:14)

Zaburi maana yake nini, katika Biblia?

Hori ni nini kibiblia (Waamuzi 5:17, Luka 2:7)?

JINSI WATU WANAVYOZAMA KATIKA USHIRIKINA NA UCHAWI.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments