Majaribu matatu Yesu aliyojaribiwa na shetani akiwa njikani siku 40, yanaweza yakachukuliwa kivyepesi lakini ukiyachunguza kwa undani yana tafsiri kubwa sana na maana kubwa sana katika maisha ya kila mkristo akiwapo hapa duniani, na yanahitaji uongozo wa Roho Mtakatifu kuyaelewa yale majaribu yana maana gani kama yalivyoandikwa pale.
Wengi wetu tunafikiri kuwa Yesu alipandishwa nyikani siku 40, kujaribiwa na ibilisi, na alipomaliza kujaribiwa alirejea katika maisha yake ya kawaida halafu basi yaliishia pale. Watu pia wanafikiria kuwa shetani alimtokea Yesu kwa mfano wa nyoka au vinginevyo na kuanza kumjaribu kumpa yale majaribu matatu.
Lakini hiyo sio kweli dhumuni kuu la Yesu kupandishwa nyikani ni kwenda kukutana na Mungu wake kwa dhumuni la kupokea maagizo fulani au ufunuo fulani, Tunaona sehemu fulani kristo aliwaambia wanafunzi wake mwenyewe Mathayo 17:21 [Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.] Yesu Kristo hakuongozwa na Roho na kufunga siku 40 nyikani kwenda kukutana na shetani hapana bali ni kwenda kukutana na Mungu wake.
Tunaweza tukaona mfano mwingine kama Musa alivyoitwa na Mungu mlimani kwenda kuchukua zile amri 10, alifunga siku 40 usiku na mchana, na alikuja kufunga tena siku nyingine 40 mchana na usiku kuwaombea wana wa israeli kwa makosa waliyoyafanya ya kuabudu sanamu. Kwahiyo Bwana Yesu Kristo kufunga nyikani siku 40 ilikuwa ni kwa ajili ya huduma yake iliyokuwa inakaribia kwenda kuanza, ndipo huko Mungu alipomfunulia huduma yake itakavyokuwa pamoja na yale majaribu makuu matatu atakayokutana nayo katika maisha yake ya huduma.
JARIBU LA KWANZA:
Tunasoma katika luka 4:1-4 “1 Na Yesu, hali amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani, 2 akijaribiwa na Ibilisi. Na siku hizo alikuwa hali kitu; hata zilipotimia, aliona njaa. 3 Ibilisi akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, liambie jiwe hili liwe mkate. 4 Yesu akamjibu, Imeandikwa ya kwamba mtu hataishi kwa mkate tu.”
Hapa tunaona Bwana Yesu baada ya siku 40 kuisha aliona njaa na alipoona njaa akiwa kama mwanadamu alitamani chakula, lakini safari yake ya nyikani ilikuwa bado haijakwisha kwahiyo shetani alipoona kuwa huyu mtu anauhitaji wa chakula alimletea ushawishi moyoni wa kugeuza jiwe kuwa mkate kwasababu alifahamu kuwa anaweza kufanya hivyo.
Sasa hapa inadhaniwa kuwa shetani alimtokea akamwambia hivyo la! hakumtokea bali alimletea ushawishi moyoni kufanya vile, biblia inasema mtu anajaribiwa kwa tamaa zake mwenyewe,(yakobo 1:14 ). Yesu kama asingeona njaa asingejaribiwa, njaa ilipokuja shetani naye akapata nafasi lakini pamoja na hayo Bwana alishinda kwa kuwa aliyajua maneno ya Baba yake kuwa “mtu hataishi kwa mkate tu bali kwa kila neno litakalotoka katika kinywa cha Mungu”, aliona sio vema kuyakatiza mapenzi ya Mungu kwa sababu ya chakula, alitambua kuwa ni Mungu ndiye aliyempeleka kule kwa hiyo hata kama siku za kukaa kule nyikani zingeongezeka mpaka kufikia 60,au 70 au 100. angeendelea kuishi kwasababu anaishi kwa neno linalotoka katika kinywa cha baba yake na sio kwa chakula cha mwilini tu. Kwahiyo tunaweza kuona Yesu Kristo aliweza kushinda kwa namna hiyo.
Lakini jaribu hili sio kwamba liliishia pale nyikani tu, ule ulikuwa kwake ni kama ufunuo wa mambo atakayokwenda kukutana nayo mbeleni katika huduma yake, Mungu alimuonyesha ni moja ya jaribu kuu ambalo shetani atampelekea katika maisha yake ya huduma.
Maana ya kugeuza jiwe kuwa mkate ni ipi? kugeuza jiwe kuwa mkate inatokea pale mtu anayopitia hali ya uhitaji au shida ya kitu fulani na anafahamu kuwa ni Mungu ndiye aliyempitisha katika hiyo hali, lakini yeye anatafuta njia mbadala ya kujing’amua na hiyo shida angali iko katika uwezo wako wa kufanya hivyo, mfano Yesu Kristo alitambua kuwa anapitia katika hali ya taabu na alikuwa na uwezo wa kugeuza lile jiwe kuwa mkate lakini hakufanya vile kwasababu alijua kuwa angeenda nje ya mapenzi ya Mungu sio kana kwamba hakuwa na njaa au alikuwa anajinyima au hakuweza kufanya la! bali alijinyenyekeza chini ya Mungu katika hali ngumu aliyokuwa nayo..
Tunaona jaribu kama hili liliwapata wana wa Israeli lakini walilishindwa pale walipopitishwa miaka 40 nyikani wakaanza kumnung’unikia Mungu wakitaka watimiziwe matakwa yao wenyewe na sio matakwa ya Mungu. Tunaona katika hali ngumu waliyokuwa nayo nyikani ukafikia wakati wakasikia njaa kama Yesu Kristo alivyosikia njaa, na kwajinsi Yesu alivyokuwa na uwezo wa kubadilisha jiwe kuwa mkate vivyo hivyo na wao pia walikuwa na uwezo huo huo wa kubadilisha jiwe kuwa mkate mfano huu tunawaona badala ya kujinyenyekeza chini ya mapenzi ya Mungu wakaanza kumnung’unikia Mungu wakitaka nyama nyikani na Mungu aliwapa nyama, alikuwa akiwapa chochote walichokuwa wanakihitaji(huku ndio kugeuza jiwe kuwa mkate)..
Kumbuka wana wa israeli walikuwa wanajua kuwa lolote watakalomwomba Mungu atawapa kama vile Yesu alivyojua kuwa lolote atakalomwomba Baba yake atampa, tunaona wana wa israeli walikuwa wanashushiwa mana kule jangwani kwa hiyo wakatumia kigezo hicho kwa tamaa zao kutaka vitu ambavyo sio sawasawa na mapenzi ya Mungu kwa kisingizio kuwa wanasikia njaa lakini hawajui kuwa shetani ameshawashinda kwa kutoweza kulishinda hilo jaribu.
kumbukumbu 8:1-5″Amri hii ninayokuamuru leo mtaishika kuitenda, mpate kuishi na kuongezeka, na kuingia katika nchi ile ambayo Bwana aliwaapia baba zenu; nanyi mtaimiliki. 2 Nawe utaikumbuka njia ile yote Bwana, Mungu wako aliyokuongoza miaka hii arobaini katika jangwa, ili akutweze, kukujaribu kuyajua yaliyo moyoni mwako, kwamba utashika amri zake, au sivyo. 3 Akakutweza, akakuacha uone njaa, akakulisha kwa mana, usiyoijua wewe wala baba zako hawakuijua; apate kukujulisha ya kuwa mwanadamu haishi kwa mkate tu, bali huishi kwa kila litokalo katika kinywa cha Bwana. 4 Mavazi yako hayakuchakaa, wala mguu wako haukuvimba, miaka hiyo arobaini. 5 Nawe fikiri moyoni mwako, ya kuwa kama vile baba amrudivyo mwanawe, ndivyo Bwana, Mungu wako, akurudivyo.”
Vivyo hivyo kristo katika huduma yake ambayo Mungu alikuwa akimtuma alijifunza kutokutazama vitu vya nje kama mali,chakula, mavazi hakujali hata sehemu ya kulala japokuwa alikuwa na uwezo wa kupata mali, kula na kunywa, na sehemu za kulala kwasababu alihesabu kutenda mapenzi ya Mungu kwanza ni bora kuliko njaa ya vitu vya nje
yohana 4:30-34 Basi wakatoka mjini, wakamwendea. 31 Huko nyuma wanafunzi wakamsihi wakisema, Rabi, ule. 32 Akawaambia, Mimi ninacho chakula msichokijua ninyi. 33 Basi wanafunzi wake wakasemezana, Je! Mtu amemletea chakula? 34 Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake.”
Kwahiyo alifahamu eneo shetani atakalomtesea katika maisha yake ya huduma ni hapo kwenye njaa ya mambo ya nje, lakini kwa kujua ufunuo huo alikuja kuweza kuyashinda yote. Na ndio maana aliwaambia mahali fulani wanafunzi wake
mathayo 6:26″ Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi? 26 Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao? ” aleluya!!
Jambo hili hili linajirudia kwa Mkristo anayesema ameamua kumtumikia Mungu, kumbuka haya majaribu matatu kila mkristo lazima ayapitie na hakuna majaribu makubwa zaidi ya hayo shetani anaweza akamjaribu mtu, vivyo hivyo kwa mkristo aliyeamua kumtumikia Mungu atambue kuwa ni lazima akutane na hili jaribu, pale shetani anapokuona upo karibu na Mungu wako sana na upo katika hali ya nyikani(kumbuka nyikani ndipo Mungu anaposhushia mana, na nyikani ni sehemu yoyote isiyokuwa na tumaini lolote,
Inawezekana katika maisha sana sana katika safari ya wokovu mtu anapoanza kumwangalia Kristo) hapo ndipo shetani analeta ushawishi kama huo alioupata Bwana ili uache njia yako, anatumia Neno kukufanya wewe utimize tamaa yako ambayo sio sawasawa na mapenzi ya Mungu, atakwambia fanya hivi au fanya vile ili uishi vizuri ndipo umtumikie Mungu, atakwambia acha hicho unachokifanya fanya kwanza hichi ujikwamue kimaisha..
Atakwambia sasa tafuta kwanza maisha ndipo uje kumtumikia Mungu baadaye, tafuta pesa kwanza maana unashida ya pesa sasa hivi halafu Mungu utamtafuta baadaye, atakwambia jiweke vizuri kiuchumi kisha utaenda baadaye kuhubiri injili, atakwambia huoni watumishi wote wanafanya hivyo,?? na atakupa sababu zote kwamba una uwezo wa kufanya hayo yote na ni kweli ukiangalia unao huo uwezo lakini nia yake yeye sio wewe kuyakidhi mahitaji yako bali ni kukufanya utoke katika kusudi la Mungu la kumtazama yeye, anakufanya usilifahamu neno la “mtu hataishi kwa mkate tu,”
kwahiyo anatumia tamaa zako kukufanya uende kinyume na mapenzi ya Mungu. kumbuku wana wa israeli walivyokuwa Mungu kuwapitisha nyikani ilikuwa sio kwenda kuwakomoa, lakini wangejuaje kama Mungu anaweza kuwalisha pasipo kazi ya mikono? wangelifahamu vipi hilo neno la MTU HATAISHI KWA MKATE TU ?? kama wasingepitishwa nyikani. unaona ni kusudi kabisa la Mungu kumpitisha mtoto wake nyikani ili ajifunze kumtegemea lakini shetani anavumbua njia mbadala kumchonganisha na Mungu haya ndiyo yaliyowakuta wana wa Israeli.
Jambo hili hili linawatokea wakristo wengi wanapopitishwa nyikani(kumbuka kila mkristo lazima apitishwe nyikani) wanashindwa na hili jaribu la shetani wanashindwa kufahamu kuwa mtu hataishi kwa mkate tu bali kwa kila neno litakalotoka katika kinywa cha Mungu, mtu hataishi kwa pesa tu, mtu hataishi kwa kazi tu, mtu hataishi kwa mifumo tuliyoizoea tu, mtu hataishi kwa gari na nyumba tu, mtu hataishi kwa umaarufu wala chochote cha ulimwengu huu, bali mtu ataishi kwa neno la Mungu tu!! Mungu ni zaidi ya mali na kila kitu Kristo anasema .
(Mathayo16:25-26..”Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona. 26 Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake? ).
(Mathayo16:25-26..”Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona.
26 Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake? ).
kila siku unasema ngoja nisubirie kidogo, nisubirie kwanza nifanye kitu fulani nikishakipata ndipo nianze kumtafuta Mungu, mwingine yupo katika taabu anasema ngoja kwanza nitafute pesa nitoke katika hii tabu ndipo nianze kumtafuta Mungu huko ndiko kugeuza jiwe kuwa mkate, unadhania kuwa mtu ataishi kwa pesa tu pasipo pesa huwezi kuishi(wana wa israel hawakuwa na fedha lakini walilishwa miaka 40 jangwani), unasema pasipo nyumba huwezi kuishi(yesu alilala milimani ambaye ndiye tunayemwita Bwana wetu na mfalme wetu),
Yesu alisema
mathayo 6:31-34″ Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini? 32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. 33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. 34 Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.”
mathayo 6:31-34″ Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?
32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.
33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
34 Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.”
Na pia Yesu alisema chakula changu ni kuyatenda mapenzi ya baba yangu (yohana 4:34) vivyo hivyo na sisi tuseme hivyo chakula chetu ni kuyatenda mapenzi ya baba yetu na kuyamaliza. Tusigeuze jiwe(vitu visivyo na uhai) kuwa mkate. Mungu anapotuita tuwe tayari kutii na kusema ndio pasipo kuangalia mambo mengine ya kando kando, kwa kufanya hivyo ndivyo tutakavyoshinda hilo jaribu la mkate vinginevyo hatutaweza.
JARIBU LA PILI:
Luka 4:5-6″ Akampandisha juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja. 6 Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo. 7 Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake. “
Luka 4:5-6″ Akampandisha juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja. 6 Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo.
7 Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake. “
Kwenye Jaribu hili tunaona Kristo akihamishwa kutoka nyikani mpaka kwenye milki zote za ulimwengu akaonyeshwa fahari zote za ulimwengu. Hapa sio shetani alimchukua katika mwili bali ni alichukuliwa na Mungu katika maono kuonyeshwa lile jaribu la shetani litakavyokuwa katika maisha yake ya huduma”. Kwa namna ya kawaida ni vigumu adui yako akuambie nisujudie halafu nitakupa vitu vyote, unafahamu kabisa huwezi kumsujudia kwasababu unajua kabisa anakujaribu kwahiyo ni wazi kabisa shetani hakumtokea Yesu bali ni Mungu ndiye aliyemwonyesha yale maono, na hili jambo lilikuja kutimia katika maisha yake kule mbeleni pale huduma yake ilipoanza kuwa kubwa, alipojulikana kila mahali na watu wote mfano huu tunaona alipokwenda Samaria wale watu wa ule mji walitaka kumshika na kumfanya mfalme
(Yohana 6:14-15 “Basi watu wale, walipoiona ishara aliyoifanya, walisema, Hakika huyu ni nabii yule ajaye ulimwenguni. 15 Kisha Yesu, hali akitambua ya kuwa walitaka kuja kumshika ili wamfanye mfalme, akajitenga, akaenda tena mlimani yeye peke yake. “)
(Yohana 6:14-15 “Basi watu wale, walipoiona ishara aliyoifanya, walisema, Hakika huyu ni nabii yule ajaye ulimwenguni.
15 Kisha Yesu, hali akitambua ya kuwa walitaka kuja kumshika ili wamfanye mfalme, akajitenga, akaenda tena mlimani yeye peke yake. “)
Jaribu kufikiria leo hii kama Bwana Yesu angekuwa mfalme wa wasamaria msalaba tungeujulia wapi, kwahiyo tunaliona hilo ni jaribu shetani alilomletea lakini alikumbuka alionyeshwa na baba yake akiwa jangwani, ya kwamba utamsujudia Bwana Mungu wako yeye peke yake, sasa kusujudia pale sio kwenda kumpigia magoti shetani bali ni kukubaliana na jambo lolote shetani atakalokuletea mbele yako kinyume cha mapenzi ya Mungu, tunaona hata leo hii watu wanamsujudia shetani pasipo hata wao kujua pale wanapotenda dhambi, unadhani shetani angemtokea mtu na kumwambia nisujudie nani angekubali?? yeye siku zote anatumia hila kuabudiwa anamfanya mtu adhani kuwa anamwabudu Mungu kumbe anamwabudu shetani.
Vivyo hivyo shetani alivyokuwa anajaribu kufanya kwa Bwana Yesu Kristo kwa kutaka kusujudiwa kwa kupitia ufahari,lakini Kristo alishinda, aliona ni vyema kuiendea njia ya msalaba aliyowekewa na baba yake kuliko kukubali sifa na heshima na vyeo na ukuu na ufalme kutoka kwa watu.Lakini leo hii angeonekana ni mtu anayechezea bahati.
Vivyo hivyo jaribu hili pia linawakuta wakristo sana sana watumishi wa Mungu walio katika huduma, mwanzoni wataanza vizuri katika huduma na Mungu atatembea nao lakini shetani anapoona hivyo ili kumwaribu anamletea jaribu kama hili lililomkuta Bwana Yesu, anaanza kwa kumpa umaarufu wa ghafla, watu watakuja kumwambia njoo uwe kiongozi wetu tutakupa pesa, nyumba, magari, tutakufanya kuwa maarufu kushinda hapo ulipo, tutaikuza huduma yako zaidi ya hapo ilipo, ila acha tu huo mtindo wako wa kale wa kuhubiri, punguza ukali wa maneno tutakupa kila kitu, we hubiri tu kama sisi tunavyohubiri, wengine wanaitwa na wanasiasa wawasaidie katika siasa zao na wanaahidiwa kupewa pesa nyingi.
Kwahiyo mtu huyu badala ya kukaa chini na kutafakari kama huduma yake itaathirika au la! yeye anakubali bila kufahamu kuwa hizo ni hadaa za shetani kutaka asujudiwe. Na watumishi wengi wa Mungu wameshindwa hili jaribu wameacha kusudi lao la kufundisha, na kuiendea njia ya msalaba, wakaiendea njia ya watu wa mataifa ili kupata umaarufu na heshima. luka 6:26″ Ole wenu ninyi watu wote watakapowasifu, kwa kuwa baba zao waliwatenda manabii wa uongo mambo kama hayo. “ JARIBU LA TATU:
Luka 4:9-12″ Akamwongoza mpaka Yerusalemu, akamweka juu ya kinara cha hekalu, akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini; 10 kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake wakulinde; 11 na ya kwamba,mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe. 12 Yesu akajibu akamwambia, Imenenwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako. “
Katika jaribu la tatu tunaona Yesu Kristo akipelekwa katika kinara cha hekalu, unaweza ukajiuliza kwa nini alipelekwa Yerusalemu, na ni kwanini kwenye kinara cha hekalu na sio penginepo?
Ono hili alipewa kuonyeshwa mwisho wa safari yake ya huduma, kwamba mwishoni atawekwa kwenye kinara cha hekalu ambacho ni msalaba, Yesu Kristo safari yake ya mwisho ilikuwa ni msalabani(hata sio ajabu kuyaona makanisa yakiwa na msalaba juu, hii inaleta picha kuwa pale juu ya kinara cha hekalu alipowekwa Yesu ni msalabani) na kumbuka hata pale msalabani shetani alikuwa akimjaribu kwa maneno hayohayo kama tunayoyaona hapo juu, shetani alimwambia kipitia vinywa vya wale watu
Mathayo 27: 39-44″ Nao waliokuwa wakipita njiani wakamtukana, wakitikisa-tikisa vichwa vyao, wakisema, 40 Ewe mwenye kulivunja hekalu na kulijenga kwa siku tatu, jiokoe nafsi yako; ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, shuka msalabani. 41 Kadhalika na wale wakuu wa makuhani wakamdhihaki pamoja na waandishi na wazee, wakisema, Aliokoa wengine, hawezi kujiokoa mwenyewe. 42 Yeye ni mfalme wa Israeli; na ashuke sasa msalabani, nasi tutamwamini. 43 Amemtegemea Mungu; na amwokoe sasa, kama anamtaka; kwa maana alisema, Mimi ni Mwana wa Mungu. 44 Pia wale wanyang’anyi waliosulibiwa pamoja naye walimshutumu vile vile. “
Lakini kama Bwana Yesu Kristo asingetambua hayo majaribu ambayo alionyeshwa na baba yake akiwa nyikani angejishusha chini msalabani na watu wote wangeamini kwasababu alikuwa anao huo uwezo, picha hii hii tunaiona pale usiku ule walipokuja kumshika Yesu na petro alipotaka kumwokoa Bwana alimwambia (mathayo 26:52-54 ”
Ndipo Yesu akamwambia, Rudisha upanga wako mahali pake, maana wote waushikao upanga, wataangamia kwa upanga. Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumsihi Baba yangu, naye ataniletea sasa hivi zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika? Yatatimizwaje basi maandiko, ya kwamba hivyo ndivyo vilivyopasa kujiri?” ) Kwahiyo tunaona Yesu Kristo alikuwa ana huo uwezo wa kujishusha msalabani lakini je! angejishusha msalabani mapenzi ya baba yangetimizwaje? na sisi tungepataje wokovu?.
Vivyo hivyo na kwa mkristo yeyote anayeipenda njia ya msalaba(japo sio wote watakayoipitia ) jaribu kama hili atakutana nalo ndilo la mwisho kumbuka shetani hatakuacha hata katika dakika ya mwisho ya wewe kukata roho atakuwa karibu yako kukufanya uanguke. Msalaba ndio hatua yetu ya mwisho, Yesu alisema mimi ndimi njia na kweli na uzima mtu haji kwa baba isipokuwa kwa njia ya mimi, njia hapo anayoizungumzia ni maisha yake yeye sasa tunayaamishia kwetu, na alisema pia mtumwa sio mkuu kuliko Bwana wake, kama yeye walimwita belzebuli, mwenye pepo, alienda msalabani kufa kifo cha aibu je! inatupasaje sisi? hatupaswi kuionea haya njia ya msalaba, watazame mitume na manabii na wakristo wa kale kwa kuitetea kweli na kuisimamia kweli hawakupenda maisha yao hata kufa, walihesabu kuwa utukufu wa Mungu ni bora kuliko utukufu wa wanadamu, Kristo alisema mtu yeyote akitaka kunifuata ajikane nafsi yake, ajitwike msalaba wake anifuatae kila siku (mathayo 16:24),na unajua msalaba ni nini?, mwisho wake ni golgotha.
Kwahiyo utakapofikia katika jaribu la tatu na la mwisho ambalo shetani atakuacha ni pale utakapoona unaenda kutiwa mikononi mwa shetani kama Yesu Kristo na mitume na manabii. walivyofanyiwa, angali una uwezo wa kujiepusha nalo kama Yesu tunaweza kuona shetani alimvaa hata Petro akijaribu kumshawishi Yesu asiipitie njia ya msalaba, lakini Yesu alimwambia nenda nyuma yangu shetani huyawazi ya Mungu bali ya wanadamu, lakini Yesu alijinyenyekeza kama kondoo aendaye kuchinjwa na ndivyo walivyofanya mitume watu wa Mungu kama stephano, yohana n.k huko ndiko kulishinda hilo jaribu( na kumalizia kusema Baba wasamehe kwa kuwa hawajui watendalo).
Yesu Kristo anasema
(ufunuo 3:20-22″ Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. 21 Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi. 22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. ). kwahiyo kushinda ni nini?? kushinda ni kule kushinda yale majaribu matatu kama Bwana Yesu alivyoyashinda.”
Sio kwamba usipopitia hiyo njia itakufanya usiende mbinguni la! Labda utaenda lakini utakuwa hujashinda kwasababu hujapigana kikamilifu, thawabu yako itapunguzwa kama utashindwa na majaribu hayo ya shetani,
1wakorintho 9:24″ Je! Hamjui, ya kuwa wale washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, ili mpate. 25 Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote; basi hao hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi tupokee taji isiyoharibika. 26 Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitaye; napigana ngumi vivyo hivyo, si kama apigaye hewa; 27 bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.
1wakorintho 9:24″ Je! Hamjui, ya kuwa wale washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, ili mpate.
25 Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote; basi hao hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi tupokee taji isiyoharibika.
26 Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitaye; napigana ngumi vivyo hivyo, si kama apigaye hewa;
27 bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.
Na pia mtume Paulo anasema,
2timotheo 2:5″4 Hakuna apigaye vita ajitiaye katika shughuli za dunia, ili ampendeze yeye aliyemwandika awe askari. 5 Hata mtu akishindana katika machezo hapewi taji, asiposhindana kwa halali. “
2timotheo 2:5″4 Hakuna apigaye vita ajitiaye katika shughuli za dunia, ili ampendeze yeye aliyemwandika awe askari.
5 Hata mtu akishindana katika machezo hapewi taji, asiposhindana kwa halali. “
mtume Paulo pia aliandika..
wafilipi 3:10-14″10 ili nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake; 11 ili nipate kwa njia yo yote kuifikia kiyama ya wafu. 12 Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu. 13 Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele; 14 nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu. “
wafilipi 3:10-14″10 ili nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake;
11 ili nipate kwa njia yo yote kuifikia kiyama ya wafu.
12 Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu.
13 Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele;
14 nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu. “
mwisho mtume Paulo aliandika
2timotheo 4:6-8″ Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika. 7 Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; 8 baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake. “
2timotheo 4:6-8″ Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika.
7 Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda;
8 baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake. “
Mungu akubariki sana ndugu yetu mpendwa.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
NI KWA NAMNA GANI TUTASHINDA MAJARIBU?
JE! DAMU INA UMUHIMU WOWOTE KATIKA MAISHA??
ZIFAHAMU NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE SABA
KWANINI KUNA WATU WANAFANYIWA DELIVERANCE (MAOMBI YA KUFUNGULIWA), LAKINI BAADA YA MUDA WANARUDIWA TENA NA HALI ILE ILE SABABU NI NINI?
Rudi Nyumbani
Print this post
Mathayo 24:32-35 ” Basi kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake likiisha kuchipuka na kuchanua majani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno u karibu; 33 nanyi kadhalika, myaonapo hayo yote, tambueni ya kuwa yu karibu, milangoni. 34 Amin, nawaambia, KIZAZI HIKI HAKITAPITA, hata hayo yote yatakapotimia. 35 Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
Mathayo 24:32-35 ” Basi kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake likiisha kuchipuka na kuchanua majani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno u karibu;
33 nanyi kadhalika, myaonapo hayo yote, tambueni ya kuwa yu karibu, milangoni.
34 Amin, nawaambia, KIZAZI HIKI HAKITAPITA, hata hayo yote yatakapotimia.
35 Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
Mambo haya Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake walipokuawa wameketi katika mlima wa Mizeituni, akiwaonya mambo yatakayokuja kutokea siku za mwisho kabla ya kurudi kwake, yakaandikwa kwaajili yetu sisi tusiwe gizani ili wakati huo ukifika mambo hayo yasitujie kama mwivi. Yapo mambo mengi Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake kama tunavyoyaona katika vitabu vya injili na vitabu vingine kuhusu siku za mwisho zitakavyokuja kuwa.
Lakini katika kitabu cha Mathayo 24 Bwana Yesu alisema katika siku za mwisho kutatokea vita na matetesi ya vita (mathayo 24:6), Hii ni sahihi hivi vita tumekuwa tukiviona vikipiganwa kwa karne na karne kati ya mataifa na mataifa, lakini vita vingi na vikubwa vimekuja kukithiri zaidi katika karne ya 20 na 21,tunaona mfano wa vita vya kwanza (1914-1918) na vya pili vya dunia (1939-1945) ambavyo vimesababisha mauaji ya mamilioni ya watu ulimwenguni kote, kitu ambacho hata hakijawahi kuonekana katika historia ya vizazi vyote vya nyuma., lakini Bwana alieleza wazi yatakapoanza kutokea haya msitishwe ule mwisho bado,alisema kuwa huo ndio mwanzo wa utungu.
Bwana Yesu alisema pia siku za mwisho kutakuwa na njaa (mwilini na rohoni), matetemeko ya nchi, kutakuwa na magonjwa mengi, mambo ambayo tumekuwa tukiyaona kila kukicha matetemeko kila mahali, magonjwa mapya yanazuka kila siku((kama cancer, kisukari,presha,zika,ukimwi,ebola,sars,kimeta, n.k) ambayo hayakuwepo katika vizazi vya zamani, lakini haya yote Bwana Yesu pia alisema ni mwanzo wa utungu, kwamba ule mwisho unakaribia lakini bado haujafika.
Jambo lingine Bwana Yesu alilolisema ni kuwa manabii na makristo wengi wa uwongo watatokea na kuwadanganya wengi, Kila mtu anafahamu kama tunavyowaona leo mafundisho mengi ya uwongo yamezagaa kila mahali, alisema pia upendo wa wengi utapoa, ni dhahiri kabisa upendo(shauku) ya watu kumpenda Mungu na kupendana wao kwa wao imetoweka,na tamaa mbaya za ulimwengu huu zimewasonga watu na kumsahau Muumba wao, alisema pia watu watakuwa wakijipenda wenyewe, wakisalitiana na kuchukiana.
Aliwaambia wanafanzi wake pia,
luka 21:20-24 “ Lakini, hapo mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, ndipo jueni ya kwamba uharibifu wake umekaribia. 21 Ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani, na walio katikati yake wakimbilie nje, na walio katika mashamba wasiuingie. 22 Kwa kuwa siku hizo ndizo za mapatilizo, ili yatimizwe yote yaliyoandikwa. 23 Ole wao wenye mimba na wanaonyonyesha katika siku hizo! Kwa kuwa kutakuwa na shida nyingi katika nchi, na hasira juu ya taifa hili. 24 Wataanguka kwa ukali wa upanga, nao watatekwa nyara na kuchukuliwa katika mataifa yote; na Yerusalemu utakanyagwa na Mataifa, hata majira ya Mataifa yatakapotimia.”.
luka 21:20-24 “ Lakini, hapo mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, ndipo jueni ya kwamba uharibifu wake umekaribia.
21 Ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani, na walio katikati yake wakimbilie nje, na walio katika mashamba wasiuingie.
22 Kwa kuwa siku hizo ndizo za mapatilizo, ili yatimizwe yote yaliyoandikwa.
23 Ole wao wenye mimba na wanaonyonyesha katika siku hizo! Kwa kuwa kutakuwa na shida nyingi katika nchi, na hasira juu ya taifa hili.
24 Wataanguka kwa ukali wa upanga, nao watatekwa nyara na kuchukuliwa katika mataifa yote; na Yerusalemu utakanyagwa na Mataifa, hata majira ya Mataifa yatakapotimia.”.
Hili jambo lilitimia kama lilivyo mwaka 70 BK pale majeshi ya Rumi yalipouzunguka mji wa Yerusalemu na kuharibu mji na hekalu kuliteketeza kwa moto, na wayahudi wote waliokuwa wamesalia Yerusalemu walitawanywa katika mataifa yote duniani hivyo basi Israeli wakawa wageni katika mataifa mengine, mpaka Mungu alipowarejesha tena nchini kwao mwaka 1948 kuwa kama taifa huru tena linalojitegemea.
Mwisho Bwana Yesu alisema habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.
Lakini hapa kuna jambo kuu na la muhimu sana tunatakiwa tulione,
Tukisoma katika
Luka 21:29-33 inasema “29 Akawaambia mfano; Utazameni mtini na miti mingine yote. 30 Wakati iishapo kuchipuka, mwaona na kutambua wenyewe ya kwamba majira ya mavuno yamekwisha kuwa karibu. 31 Nanyi kadhalika, mwonapo mambo hayo yanaanza kutokea, tambueni ya kwamba ufalme wa Mungu u karibu. 32 Amin, nawaambieni, KIZAZI HIKI HAKITAPITA, HATA HAYO YOTE YATIMIE. 33 Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
Alisema kwa mtini jifunzeni, “Mtini” siku zote kwenye biblia unawakilisha Taifa la Izraeli,(soma yeremia 24), na aliposema utazameni mtini na miti mingine,hii miti mingine ni mataifa mengine, sasa aliposema mtini utakapoanza kuchipua alikuwa na maana Taifa la Israel kuzaliwa tena upya baada ya kukaa katika mataifa mbalimbali kwa muda mrefu. Tunaona jambo hili lilitimia mwaka 1948 pale Izraeli waliporejea katika nchi yao wenyewe kama ilivyotabiriwa na Bwana, hiyo ndiyo maana ya kuchipuka kwa Israeli. Hivyo basi kuanzia huo mwaka wa 1948 mpaka sasa tunaona mataifa mengi yalianza kupata uhuru wao ikiwemo mataifa karibu yote ya Afrika, baadhi ya Asia na Marekani ya kusini hii inatimiza ule unabii Yesu aliosema mjifunze pia kwa miti mingine (miti mingine ni sisi mataifa mengine mbali na Israeli).
Sasa baada ya mtini kuchipuka(Izraeli) hapo ndipo Bwana aliposema “Amin, nawaambieni, Kizazi hiki hakitapita hata hayo yote yatimie. Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.”
Hichi kizazi kinachozungumziwa hapa sio kile kizazi cha Yesu alichokuwa anazungumza nacho, bali ni kile kizazi kilichoshuhudia Izraeli ikichipuka yaani Izraeli kuwa Taifa huru tena kama ilivyokuwa hapo mwanzo zaidi ya miaka 2500 iliyopita.
Na kizazi kilichoshuhudia hayo ni kuanzia watu waliozaliwa mwaka 1948 na kuendelea hadi sasa, kwahiyo tumeshafahamu kuwa kizazi cha wale waliozaliwa mwaka 1948 Bwana Yesu ndicho alichosema hakitapita. Na tunajua kizazi mpaka kitoweke kabisa katika dunia ni miaka 100,kwa dunia ya sasa, tukiangalia tangu mwaka 1948 hadi leo ni miaka 69 imeshapita, na hapa Bwana Yesu alisema kizazi hiki hakitapita hakusema kitatimia ndio mwisho uje bali alisema hakitapita,
Kwahiyo hii ina maanisha hapa hapa katikati kabla ya kufikia hicho kipindi cha kizazi kutoweka Bwana Yesu Kristo atakuwa ameshakuja, ni wazi kabisa wengi waliozaliwa chini ya mwaka 1948 ni asilimia 7% tu inayoishi duniani sasa (kwa mujibu wa takwimu za dunia), kwahiyo hili rika la hawa watu linakaribia kupotea, lakini Bwana Yesu Kristo aliapa kuwa hili rika halitapita,
aliweka msisitizo kabisa akasema Amin, nawaambieni, Kizazi hiki hakitapita hata hayo yote yatimie. Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.”..
Na baada ya hapo ndipo Bwana Yesu aliposema mtakapoona hayo yanaanza kutokea tambueni ya kwamba ufalme wa Mungu u karibu, kwa hiyo ndugu tambua hilo wewe unayesema bado sana Yesu kurudi, wewe ambaye unasitasita kwenye mawazo mawili, maneno haya yanaonyesha wazi kabisa kuwa kuja kwa Bwana kuko mlangoni, Baada ya hayo maneno Bwana Yesu Kristo alimalizia kwa kusema
“ Basi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafula, kama mtego unasavyo; 35 kwa kuwa ndivyo itakavyowajilia watu wote wakaao juu ya uso wa dunia nzima. 36 Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu.”
“ Basi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafula, kama mtego unasavyo;
35 kwa kuwa ndivyo itakavyowajilia watu wote wakaao juu ya uso wa dunia nzima.
36 Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu.”
Bwana Yesu Kristo hakutoa muda wala saa ya kuja kwake lakini alitupa majira kwamba yatakapokuja yasitujie kama mwivi au kama mtego unasavyo, je! wewe ambaye unatambua kabisa tunaishi katika kizazi ambacho tutashuhudia kuja kwa Yesu Kristo mara ya pili, umejiwekaje tayari, umebatizwa kweli kwa Roho Mtakatifu?? umeufanya imara kweli uteule wako na wito wako? Bwana Yesu akija leo una uhakika wa kwenda naye??.
Huu ni wakati wa wale wanawali werevu kutengeneza taa zao kwenda kumlaki Bwana Yesu, je! na wewe una uhakika kuwa taa yako iko sawa?? Tambua ya kuwa Bwana akija leo na taa yako haipo sawa utabaki hapa na kuingia katika ile dhiki kuu? Kumbuka ujumbe huu unakuhusu wewe mkristo unayesema umeokoka, kumbuka wale walikuwa wote ni wanawali na wote walikuwa wanamsubiria Bwana wao isipokuwa watano walikuwa werevu na watano walikuwa wapumbavu (mathayo 25)
kwahiyo hao wanawali 10 wote ni wakristo na sio watu wasioamini, fahamu tu uchungu utakuwa kwa wale ambao walidhani wangeenda katika unyakuo lakini wakabaki, na sio wale wasioamini, hivyo ndivyo itakavyowakuta wakristo wote ambao ni vuguvugu sasa wanachofahamu tu ni madhehebu yao lakini hawataki kumjua Kristo katika neno lake, hawataki kujazwa Roho Mtakatifu ili awaongoze katika kweli yote uteule wao uwe wa uhakika, Roho Mtakatifu ndio muhuri wa Mungu (waefeso 4:30) pasipo Roho Mtakatifu hakuna unyakuo. je! wewe ni mmoja wa wanawali mwerevu au mpumbavu? wanawali wote werevu wanajivunia kuwa wakristo wa NENO na sio wakristo wa madhehebu, wanawali wapumbavu wanaona aibu kuitwa wakristo, wanajivunia madhehebu ukimwuliza yeye ni nani atakwambia mimi nimlutheri,mkatoliki,msabato,mbranhamite,m-eagt,morovian., hawafahamu jambo lingine lolote nje ya madhehebu yao, ukiwaambia biblia inasema hivi wanasema dhehebu letu halifundishi hilo,
Lakini BWANA YESU KRISTO leo anatuita tuwe WANAWALI WEREVU(SAFI)…..na ujumbe tulionao sasa kwa wakati wetu ni
Ufunuo 18:4 “Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake. Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake.”
Jihadhari na mafundisho ya uongo.
Ndugu tubu, mgeukie Bwana muda ndio huu, usidanganyike na mafundisho yanayosema kuwa Kristo bado sana kurudi.
Mungu akubariki!
[embedyt] https://www.youtube.com/watch?v=9K3Zsu-btLs[/embedyt]
NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE
CHUKIZO LA UHARIBIFU.
KITABU CHA UZIMA.
UTAWALA WA MIAKA 1000.
JE! KUFANYA MASTURBATION (PUNYETO) NI DHAMBI?
Mwanzo 2:8-9 “Bwana Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya. 9 Bwana Mungu akachipusha katika ardhi kila mti unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa; na mti wa uzima katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na mabaya”.
Mwanzo 2:8-9 “Bwana Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya.
9 Bwana Mungu akachipusha katika ardhi kila mti unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa; na mti wa uzima katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na mabaya”.
Tukisoma katika mistari hii hapa juu, tunaona kabisa mwanzoni Mungu alipopanda bustani mashariki mwa Edeni Mungu aliiweka miti ya aina tatu bustanini nayo ni:
Hapa usichanganye hii ni miti aina tatu tofauti yenye tabia tatu tofauti tofauti, tukianzana na mti wa kwanza,
Sasa mti wa aina hii unaozungumziwa hapa biblia inasema Mungu alichepusha katika ardhi ”KILA” mti unaofaa kwa chakula, tunaona hili neno “KILA” linamaanisha ni miti mingi na sio mti mmoja, mfano wa miti hii ni mapeasi, matofaa, maembe,mananasi, ndizi, mapasheni,mapapai n.k. hii ni miti aina ya kwanza ya mti ambayo Mungu aliichepusha katika ardhi kwa ajili ya chakula cha mwanadamu kumfaa kwa ajili ya mwili wake na mahitaji yake akiwa bustanini, yeye pamoja na wanyama wake wote Bwana aliompa. Adamu hakupewa masharti juu ya miti hii alikuwa na uhuru wa kula jinsi apendavyo na jinsi atakavyo kama biblia inavyosema.
2. Mti wa uzima katikati ya bustani.
Huu ni mti aina ya pili ambao Bwana aliuweka bustanini, tunaona kuwa mti wa pili na watatu imebeba tabia, na hii miti miwili ya mwisho ipo mmoja, mmoja tu. sio mingi kama ile aina ya kwanza ya mti, sasa huu mti wa uzima. Huu mti ulikuwa hauonekani kwa macho, kama miti mingine, na ulikuwa ni mti ambao ukila matunda yake (sio kula kwa mdomo) unapata uzima ambao umebeba ule uzima wa milele. Kwahiyo huu mti Mungu aliuweka kama hazina kwa Adamu endapo ikitokea wameupoteza ule uzima, waende kula matunda yake wapate uzima tena, Mungu kwa kujua kuwa mwanadamu baadaye atapoteza uzima aliuumba huu mti kuwa kama akiba ya tiba baadaye. Na huu mti Adamu hakuwa na matumizi nao kwasababu tayari alikuwa na uzima wa milele ndani yake.
Lakini tunaona baadaye Adamu alipodondoka kwenye dhambi na kupoteza uzima ndani yake alitamani kwenda kula matunda ya mti wa uzima lakini njia yake ilikuwa imeshafungwa ikilindwa mpaka wakati ulioamuriwa wa hiyo njia kufunguliwa ufike.kwahiyo ilipasa mwanadamu aijue hiyo njia ni ipi. soma mwanzo 3:24. kuanzia hapo wanadamu ndipo walipoanza kufa na kuanza kutafuta suluhisho la kuishi milele tena, na ndipo hapo wanadamu walipoanza kuliitia jina la BWANA, mwanzo 4:26
Lakini sasa sisi tunaoishi wakati huu wa neema tunajua NJIA ni ipi?… na huo MTI WA UZIMA ni nani?… na MATUNDA yake ni nini?..na tunajua sio mwingine zaidi ya BWANA wetu YESU KRISTO mwokozi wetu Haleluya!! .Kwa ufafanuzi mfupi wa jambo hili tusome maandiko yafuatayo…
Yohana 14:6″ Yesu akamwambia, Mimi ndimi NJIA, na KWELI, na UZIMA; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.” Unaona hapo!?? hakuna njia yoyote sisi tunaweza kumfikia Baba kama ilivyokuwa hapo mwanzo kabla ya Adamu kuasi isipokuwa kwa njia ya YESU tu! na pia tena ukisoma
Yohana 6:47-51″ Amin, amin, nawaambia, Yeye aaminiye yuna UZIMA WA MILELE. 48 Mimi ndimi chakula cha uzima. 49 Baba zenu waliila mana jangwani; wakafa. 50 Hiki ni chakula kishukacho kutoka mbinguni, kwamba mtu akile wala asife. 51 Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; mtu akila chakula hiki, ATAISHI MILELE. Na chakula nitakachotoa mimi ni mwili wangu, kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.”
Yohana 6:47-51″ Amin, amin, nawaambia, Yeye aaminiye yuna UZIMA WA MILELE.
48 Mimi ndimi chakula cha uzima.
49 Baba zenu waliila mana jangwani; wakafa.
50 Hiki ni chakula kishukacho kutoka mbinguni, kwamba mtu akile wala asife.
51 Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; mtu akila chakula hiki, ATAISHI MILELE. Na chakula nitakachotoa mimi ni mwili wangu, kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.”
Maandiko hayo hapo juu yanaonyesha wazi kabisa kuwa hakuna uzima wa milele mahali pengine popote nje ya BWANA YESU KRISTO, matunda ya porini siku zote hayajawahi kumpa mtu uzima wa milele, kwahiyo mtazamo wa kuwa matunda ya mti wa uzima ni matunda yafananayo na ya mwituni sio sahihi,(ni kukosa tu Roho ya mafunuo) kwasababu matunda ya kawaida hayawezi kutupa sisi uzima wa milele, biblia inasema hakuna wokovu wowote nje ya Yesu Kristo, Hivyo basi maana ya kula matunda ya mti wa uzima ni kulitafakari na kuliamini NENO la Bwana Yesu tu, na kusafishwa kwa damu yake ambaye yeye ndiye huo mti wa uzima. Na hili NENO la Mungu ndilo liletalo Utii,Upendo,Amani,Uvumilivu,Fadhili,Kiasi,Utakatifu,Utu wema,Hekima,Haki n.k.
Wagalitia 5:22″ Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, 23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria”.
3.Mti wa ujuzi wa mema na mabaya.
Kama tulivyouona mti wa pili, haukuwa mti wa kawaida kama ule wa kwanza, ndivyo ulivyo na huu pia, mti huu nao upo mmoja na umebeba tabia ya kipekee kwamba ukila matunda yake, utapata maarifa ya ujuzi wa mema na mabaya na ndio mti pekee Mungu aliomkataza mwanadamu asiule, alimwambia kabisa siku atakapokula tu matunda ya mti ule atakufa hakika. Lakini mwanadamu alikaidi akala na ikapelekea hata sisi wote tukaingia katika hali ya laana ambayo tunayo mpaka sasa, lakini ashukuriwe Mungu njia ya mti wa uzima (YESU KRISTO) imeshafunguliwa tunao ukombozi wetu.
Huu mti asili yake ni mauti, na mauti inaletwa na shetani, kama vile uzima unavyoletwa na Yesu Kristo vivyo hivyo mauti inaletwa na shetani. Kwahiyo huu mti alikuwa ni “shetani” mwenyewe, na matunda yake ni “kwenda kinyume na NENO la Mungu” ndio huko unazaliwa uongo,uasherati,uuaji,ulevi,wizi,ulafi,sanamu,ufisadi,wivu, usengenyaji, n.k. ambayo mwisho wake ni mauti.
sasa kilichotendeka Edeni. shetani ambaye ndio ule mti wa ujuzi wa mema na mabaya, alimwingia nyoka. na nyoka akaenda kumdanganya Hawa kwa mafundisho yake ya uongo aliyoyatoa kwa baba yake shetani. kumbuka Mungu alimwonya mwanadamu adumu katika maagizo yake, asitafute maarifa mengine nje na Neno lake, lakini kwa kuwa shetani alijua mwanadamu anapenda maarifa ambayo Mungu alimkataza mwanadamu asiyatafute, na shetani siku zote ni mpingamizi wa Mungu hivyo alimjaribu katika hayo hayo, ndipo alipomwingia nyoka, na kumshawishi Hawa kutokumtii Mungu. na njia shetani aliyotumia ni ushawishi wa kufanya uasherati, kwa maana nyoka alimwambia ukila matunda haya utafanana na Mungu ukijua mema na mabaya. kumbuka kuwa nyoka hakuwa mnyama “reptilia” kama tunavyomwona leo, bali alikuwa ni mnyama anayekaribiana sana na mwanadamu, alikuwa na uwezo wa kuongea, kutafakari, alikuwa anatembea kwa miguu miwili, kwa ufupi alikuwa kama mtumwa wa mwanadamu.Baada ya kulaaniwa ndipo alipotembea kwa matumbo, na kula mavumbi.
Kwahiyo baada ya nyoka kuingiwa na shetani na kwenda kufanya uzinzi na Hawa, Hawa naye akaenda kumpa tunda (kuzini) na mumewe, ikapelekea Hawa kubeba mimba ya mapacha wawili wasiofanana, akamzaa Habili na Kaini kila mmoja akiwa na baba yake. Baba yake Habili alikuwa ni Adamu na baba yake Kaini alikuwa ni nyoka. kumbuka nyoka hakuwa kama nyoka tunayemwona leo.(kwa ufafanuzi mrefu fuatilia somo langu liitwalo UZAO WA NYOKA.)
Tujue kuwa kitendo cha kula matunda ya porini kama peasi, embe au papai, hakuwezi kumfanya mtu ajione kuwa uchi, na kama walikula matunda yale kwa midomo hiyo midomo ndiyo ingetakiwa ilaaniwe na sio viungo vya uzazi, tunaona kabisa baada ya kula tunda (kuzini) walikimbilia kwenda kujifunika sehemu zao za siri, kiashirio kuwa hizo sehemu zao ndizo zilizohusika katika tendo lile.
Ni dhahiri kabisa kuwa mwanadamu ni vigumu kushawishika kwa matunda ya porini, kwa sababu alikuwa na matunda mengine mengi kwanini sasa aende kula lile la katikati ya bustani ya Edeni? Jibu ni dhahiri kuwa ni dhambi ile ile ya asili ambayo shetani alifahamu atampata nayo mwanadamu kirahisi na ndiyo hiyo hiyo anayowapata nayo wanadamu hata leo na hii sio nyingine bali ni dhambi ya uasherati.
Mungu ni yeye yule jana, na leo na hata milele, alichokichukia Edeni ndio hicho hicho anakichukia hata leo. Kama ilikuwa kula tunda kama tunda la kawaida ni makosa angeendelea kukichukia na kukikemea hicho kitu mpaka leo. lakini ni dhambi ya uasherati Mungu anayoichukia hata leo na ndiyo inayowaangusha watu wengi, kwa wanaojiita wakristo na wasio wakristo. kwahiyo hili tunda la kutokuliamini neno la Mungu (ambalo kwa mara ya kwanza shetani alilitangaza kwa kivuli cha uzinzi) hadi leo watu wanalila hili tunda. kama vile tu watu wa Mungu wanavyoendelea kula matunda ya mti wa uzima (kama tulivyosema ni kuliamini na kuliishi Neno la Mungu) ili wapate uzima wa milele vivyo hivyo hadi leo watu wanaendelea kula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya kama uasherati, n.k. kwa ajili ya mauti yao wenyewe. Akipandacho mtu ndicho atakachovuna.
Kwahiyo ndugu jambo lile lile lililotendeka Edeni linaendelea kutendeka hadi leo, je! unakula matunda ya ule mti wa ujuzi wa mema na mabaya huku ukijua kabisa Mungu amekataza usiyale ambayo tunayajua matunda yake ndiyo haya, uasherati, na mengine ni uongo, ulevi,ufisadi, usengenyaji, ushoga, ulafi, anasa, kuupenda ulimwengu, wizi, rushwa, tamaa mbaya, chuki, wivu, n.k. unafahamu kabisa mwisho wa haya ni mauti kama Mungu alivyosema pale Edeni, siku utakapokula matunda hayo utakufa hakika. Apple haliwezi likakufanya ufe! na biblia inasema mshahara wa dhambi ni mauti. Kimbilia kwa Yesu sasa ukale matunda ya Mti wa uzima, upate uzima wa milele, Bwana Yesu alisema itakufaidia nini uupate ulimwengu mzima na kupata hasara ya nafsi yako au utatoa nini badala ya nafsi yako. Kuzimu ipo, tazama miti miwili ipo mbele yako, chagua moja MTI WA UZIMA au MTI WA MAUTI.
Warumi 6:16 Hamjui ya kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake katika kumtii, mmekuwa watumwa wake yule mnayemtii, kwamba ni utumishi wa dhambi uletao mauti, au kwamba ni utumishi wa utii uletao haki.
Chaguo lipo kwako. Wakati umekwenda sana na mlango wa neema unakaribia kufungwa, je! umejiweka tayari.?? Umejazwa Roho Mtakatifu,??
Neema ya Mungu iwe pamoja nawe.
UZAO WA NYOKA.
JE! NYWELE ZAKO ZINAOTA AU ZIMESIMAMA?
UNAFANYA NINI HAPO?
Moja ya maagizo muhimu ambayo Bwana wetu Yesu Kristo aliyatoa kwa wanafunzi wake na kwa kanisa kwa ujumla ni kitendo cha kushiriki meza ya Bwana, pamoja na wakristo kutawadhana miguu na mengineyo yakiwemo ubatizo , na wanawake kufunika vichwa vyao wakiwemo ibadani. lakini leo tujifunze hayo mawili ya kwanza.
MEZA YA BWANA:
Mathayo 26:26 ” Nao walipokuwa wakila Yesu alitwaa mkate, akabariki, akaumega, akawapa wanafunzi wake, akasema, Twaeni, mle; huu ndio mwili wangu 27 Akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akisema, Nyweni nyote katika hiki; 28 kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi. “
Mathayo 26:26 ” Nao walipokuwa wakila Yesu alitwaa mkate, akabariki, akaumega, akawapa wanafunzi wake, akasema, Twaeni, mle; huu ndio mwili wangu
27 Akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akisema, Nyweni nyote katika hiki;
28 kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi. “
Tukisoma pia…
Yohana 6:52-56″ Basi Wayahudi walishindana wao kwa wao wakisema, Awezaje mtu huyu kutupa sisi mwili wake ili tuule? 53 Basi Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu. 54 Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho. 55 Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli. 56 Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake. 57 Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, nami ni hai kwa Baba; kadhalika naye mwenye kunila atakuwa hai kwa mimi. “
Yohana 6:52-56″ Basi Wayahudi walishindana wao kwa wao wakisema, Awezaje mtu huyu kutupa sisi mwili wake ili tuule?
53 Basi Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu.
54 Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.
55 Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli.
56 Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake.
57 Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, nami ni hai kwa Baba; kadhalika naye mwenye kunila atakuwa hai kwa mimi. “
Tunaona kuwa haya ni maagizo ya Bwana kwa kila mkristo kushiriki meza ya Bwana kikamilifu.
1wakoritho 11:26 inaeleza umuhimu wa jambo hili kwamba tunapoumega mkate na kukinywea kile kikombe tunaitangaza mauti ya Bwana katika miili yetu wenyewe, hii inamaana kuwa tunakubaliana na lile jambo la kufa na kufufuka kwa Bwana Yesu pale msalabani vivyo hivyo na sisi tunayachukuwa yale mateso ya Bwana Yesu katika miili yetu( kwamba tunakubali kudharauliwa, kuchukiwa na hata kuuawa kwa ajili yake kama yeye alivyouawa).hivyo picha ya Kristo inajengwa ndani yetu
Wafilipi 1:29″Maana mmepewa kwa ajili ya Kristo, si kumwamini tu, ila na kuteswa kwa ajili yake;
“2Timotheo 2:12″ Kama tukistahimili, tutamiliki pamoja naye; Kama tukimkana yeye, yeye naye atatukana sisi; ” Kwahiyo Huko pia ndiko kutangaza mauti ya Kristo.
1Wakoritho 10:16″ Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, je! Si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo? 17 Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja. 18 Waangalieni hao Waisraeli walivyokuwa kwa jinsi ya mwili; wale wazilao dhabihu, je! Hawana shirika na madhabahu? 19 Basi niseme nini? Ya kwamba kile kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu? Au ya kwamba sanamu ni kitu? 20 Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani. 21 Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani. “
1Wakoritho 10:16″ Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, je! Si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo?
17 Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja.
18 Waangalieni hao Waisraeli walivyokuwa kwa jinsi ya mwili; wale wazilao dhabihu, je! Hawana shirika na madhabahu?
19 Basi niseme nini? Ya kwamba kile kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu? Au ya kwamba sanamu ni kitu?
20 Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani.
21 Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani. “
kwa mistari hii inaonyesha kabisa kuna mahusiano makubwa ya rohoni kati ya mtu na Bwana, pale anaposhiriki meza ya Bwana. Kama tu vile mtu anapokwenda katika madhabahu za mashetani na kula vitu vya mashetani ni dhahiri kabisa nguvu za giza zitamwandama huyo mtu, vivyo hivyo pia na kwa mtu anayeshiriki meza ya Bwana anashiriki pia neema ya Bwana na baraka za Bwana, na roho za unyemelezi za shetani kama roho za magonjwa, hofu, n.k. Mungu anazifukuzia mbali maana Bwana Yesu alisema mtu asipokula mwili wangu na kuinywa damu yangu hana uzima ndani yake.(yohana 6:53). kwahiyo tunapoula mwili wake na kuinywa damu yake tunakuwa na uzima ndani yetu kila siku.
Luka 24:13″13 Na tazama, siku ile ile watu wawili miongoni mwao walikuwa wakienda kijiji kimoja, jina lake Emau, kilichokuwa mbali na Yerusalemu kama mwendo wa saa mbili. 14 Nao walikuwa wakizungumza wao kwa wao habari za mambo hayo yote yaliyotukia. 15 Ikawa katika kuzungumza na kuulizana kwao, Yesu mwenyewe alikaribia, akaandamana nao. 16 Macho yao yakafumbwa wasimtambue. 17 Akawaambia, Ni maneno gani haya mnayosemezana hivi mnapotembea? Wakasimama wamekunja nyuso zao. 18 Akajibu mmoja wao, jina lake Kleopa, akamwambia, Je! Wewe peke yako u mgeni katika Yerusalemu, hata huyajui yaliyotukia humo siku hizi? 19 Akawauliza, Mambo gani? Wakamwambia, Mambo ya Yesu wa Nazareti, aliyekuwa mtu nabii, mwenye uwezo katika kutenda na kunena mbele za Mungu na watu wote; 20 tena jinsi wakuu wa makuhani na wakubwa wetu walivyomtia katika hukumu ya kufa, wakamsulibisha. 21 Nasi tulikuwa tukitumaini ya kuwa yeye ndiye atakayewakomboa Israeli. Zaidi ya hayo yote, leo ni siku ya tatu tangu yalipotendeka mambo hayo; 22 tena, wanawake kadha wa kadha wa kwetu walitushitusha, waliokwenda kaburini asubuhi na mapema, 23 wasiuone mwili wake; wakaja wakasema ya kwamba wametokewa na malaika waliosema kwamba yu hai. 24 Na wengine waliokuwa pamoja nasi walikwenda kaburini wakaona vivyo hivyo kama wale wanawake walivyosema, ila yeye hawakumwona. 25 Akawaambia, Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii! 26 Je! Haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia katika utukufu wake? 27 Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe. 28 Wakakikaribia kile kijiji walichokuwa wakienda, naye alifanya kama anataka kuendelea mbele. 29 Wakamshawishi wakisema, Kaa pamoja nasi, kwa kuwa kumekuchwa, na mchana unakwisha. Akaingia ndani kukaa nao. 30 Ikawa alipokuwa ameketi nao chakulani, alitwaa mkate, akaubariki, akaumega, akawapa. 31 Yakafumbuliwa macho yao, wakamtambua; kisha akatoweka mbele yao. 32 Wakaambiana, Je! Mioyo yetu haikuwaka ndani yetu hapo alipokuwa akisema nasi njiani, na kutufunulia maandiko? “
Luka 24:13″13 Na tazama, siku ile ile watu wawili miongoni mwao walikuwa wakienda kijiji kimoja, jina lake Emau, kilichokuwa mbali na Yerusalemu kama mwendo wa saa mbili.
14 Nao walikuwa wakizungumza wao kwa wao habari za mambo hayo yote yaliyotukia.
15 Ikawa katika kuzungumza na kuulizana kwao, Yesu mwenyewe alikaribia, akaandamana nao.
16 Macho yao yakafumbwa wasimtambue.
17 Akawaambia, Ni maneno gani haya mnayosemezana hivi mnapotembea? Wakasimama wamekunja nyuso zao.
18 Akajibu mmoja wao, jina lake Kleopa, akamwambia, Je! Wewe peke yako u mgeni katika Yerusalemu, hata huyajui yaliyotukia humo siku hizi?
19 Akawauliza, Mambo gani? Wakamwambia, Mambo ya Yesu wa Nazareti, aliyekuwa mtu nabii, mwenye uwezo katika kutenda na kunena mbele za Mungu na watu wote;
20 tena jinsi wakuu wa makuhani na wakubwa wetu walivyomtia katika hukumu ya kufa, wakamsulibisha.
21 Nasi tulikuwa tukitumaini ya kuwa yeye ndiye atakayewakomboa Israeli. Zaidi ya hayo yote, leo ni siku ya tatu tangu yalipotendeka mambo hayo;
22 tena, wanawake kadha wa kadha wa kwetu walitushitusha, waliokwenda kaburini asubuhi na mapema,
23 wasiuone mwili wake; wakaja wakasema ya kwamba wametokewa na malaika waliosema kwamba yu hai.
24 Na wengine waliokuwa pamoja nasi walikwenda kaburini wakaona vivyo hivyo kama wale wanawake walivyosema, ila yeye hawakumwona.
25 Akawaambia, Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii!
26 Je! Haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia katika utukufu wake?
27 Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe.
28 Wakakikaribia kile kijiji walichokuwa wakienda, naye alifanya kama anataka kuendelea mbele.
29 Wakamshawishi wakisema, Kaa pamoja nasi, kwa kuwa kumekuchwa, na mchana unakwisha. Akaingia ndani kukaa nao.
30 Ikawa alipokuwa ameketi nao chakulani, alitwaa mkate, akaubariki, akaumega, akawapa.
31 Yakafumbuliwa macho yao, wakamtambua; kisha akatoweka mbele yao.
32 Wakaambiana, Je! Mioyo yetu haikuwaka ndani yetu hapo alipokuwa akisema nasi njiani, na kutufunulia maandiko? “
tunaona hapa umuhimu wa jambo lingine tena kuwa watu hawa wasingemtambua Bwana kama wasingeumega mkate, vivyo hivyo na sisi kwa kufanya hivyo Mungu anaachilia Roho ya kumjua yeye na Neno lake vizuri siku baada ya siku pale ambapo tulikuwa hatumuelewi vizuri tunapata ufahamu mpya wa kumwelewa vizuri, hivyo ni muhimu kwa kila mkristo kushiriki meza ya Bwana.
Vitu vinavyohitajika ni mkate usiotiwa chachu (yaani usiotiwa hamira), na uwe ni unga wa ngano, Ni vizuri kutumia ngano ambayo haijakobolewa iliyosagwa japo kwa mazingira ya sasa hivi ni ngumu kupata ngano ambayo haijakobolewa isiyochanganywa na chochote hivyo unaweza ukaenda tu masokoni kununua ngano na kwenda kuisaga mwenyewe mashineni kama wanavyosaga unga wa mahindi nusu kilo/kilo moja inatosha kwa matumizi ya muda mrefu, kwahiyo wakati unaanza kuandaa chukua unga mkono mmoja (sasa inategemea na idadi mnaokutanika kushiriki) idadi inapaswa iwe ni watu wawili na kuendelea haiwezekani kushiriki peke yako, kanisa ni kuanzia watu wawili na kuendelea.
ukishapima unga mkono mmoja, tia mafuta yoyote mazuri ya kupikia kama kijiko kimoja (wengi wanapenda kutumia mafuta ya mizeituni), lakini kwa huku kwetu yanayopatikana sana ni ya alizeti, kisha tia chumvi kidogo, kisha weka maji kidogo halafu kanda kama vile unavyokanda chapati, (angalizo : usitie hamira wala vyombo unavyotumia visiwe na hamira vioshe kabla haujatumia).
ukishamaliza kukanda sukuma kama unavyosukuma chapati, usipoteze muda mwingi katika kukanda na kutengeneza umbo, maana unavyozidi kukawia unga utaumuka kutokana na hamira ya asili hivyo jitahidi kuwa haraka kidogo. ukishamaliza tia jikono usiweke chochote tena baada ya kuuweka jikoni, acha kama dakika mbili tatu, ili uwe mgumu wa kuvunjika ukishaiva toa. Na mkate wako utakuwa upo tayari.
Tumia “Divai isiyo na kilevi”. Zipo Divai zenye kilevi, maandiko hayajaonyesha moja kwa moja kwamba Divai iliyokuwa inatumika enzi za Bwana YESU, “ilikuwa na kilevi au haikuwa na kilevi”, lakini tunajua mambo yote tunapaswa kuyafanya kwa uangalifu, na kwa ushuhuda mwema, kwahiyo Divai ni vyema ikatumika “ile isiyo na kilevi”.
Kwahiyo baada ya kuandaa mkate wako na divai mkishakwisha kushukuru mnaweza mkaumega kama Bwana alivyoagiza muda wa jioni ni mzuri zaidi.
KUTAWADHANA MIGUU:
Yohana 13:3-17″ Yesu, hali akijua ya kuwa Baba amempa vyote mikononi mwake, na ya kuwa alitoka kwa Mungu naye anakwenda kwa Mungu, 4 aliondoka chakulani; akaweka kando mavazi yake, akatwaa kitambaa, akajifunga kiunoni. 5 Kisha akatia maji katika bakuli, akaanza kuwatawadha wanafunzi miguu, na kuifuta kwa kile kitambaa alichojifunga. 6 Hivyo yuaja kwa Simoni Petro. Huyo akamwambia, Bwana! Wewe wanitawadha miguu mimi? 7 Yesu akajibu, akamwambia, Nifanyalo wewe hujui sasa; lakini utalifahamu baadaye. 8 Petro akamwambia, Wewe hutanitawadha miguu kamwe. Yesu akamwambia, Kama nisipokutawadha, huna shirika nami. 9 Simoni Petro akamwambia, Bwana, si miguu yangu tu, hata na mikono yangu na kichwa changu pia. 10 Yesu akamwambia, Yeye aliyekwisha kuoga hana haja ila ya kutawadha miguu, bali yu safi mwili wote; nanyi mmekuwa safi, lakini si nyote. 11 Kwa maana alimjua yeye atakayemsaliti; ndiyo maana alisema, Si nyote mlio safi. 12 Basi alipokwisha kuwatawadha miguu, na kuyatwaa mavazi yake, na kuketi tena, akawaambia, Je! Mmeelewa na hayo niliyowatendea? 13 Ninyi mwaniita, Mwalimu, na, Bwana; nanyi mwanena vema, maana ndivyo nilivyo. 14 Basi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu, nimewatawadha miguu, imewapasa vivyo kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi. 15 Kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo. 16 Amin, amin, nawaambia ninyi, Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake; wala mtume si mkuu kuliko yeye aliyempeleka. 17 Mkiyajua hayo, heri ninyi mkiyatenda. “
Yohana 13:3-17″ Yesu, hali akijua ya kuwa Baba amempa vyote mikononi mwake, na ya kuwa alitoka kwa Mungu naye anakwenda kwa Mungu,
4 aliondoka chakulani; akaweka kando mavazi yake, akatwaa kitambaa, akajifunga kiunoni.
5 Kisha akatia maji katika bakuli, akaanza kuwatawadha wanafunzi miguu, na kuifuta kwa kile kitambaa alichojifunga.
6 Hivyo yuaja kwa Simoni Petro. Huyo akamwambia, Bwana! Wewe wanitawadha miguu mimi?
7 Yesu akajibu, akamwambia, Nifanyalo wewe hujui sasa; lakini utalifahamu baadaye.
8 Petro akamwambia, Wewe hutanitawadha miguu kamwe. Yesu akamwambia, Kama nisipokutawadha, huna shirika nami.
9 Simoni Petro akamwambia, Bwana, si miguu yangu tu, hata na mikono yangu na kichwa changu pia.
10 Yesu akamwambia, Yeye aliyekwisha kuoga hana haja ila ya kutawadha miguu, bali yu safi mwili wote; nanyi mmekuwa safi, lakini si nyote.
11 Kwa maana alimjua yeye atakayemsaliti; ndiyo maana alisema, Si nyote mlio safi.
12 Basi alipokwisha kuwatawadha miguu, na kuyatwaa mavazi yake, na kuketi tena, akawaambia, Je! Mmeelewa na hayo niliyowatendea?
13 Ninyi mwaniita, Mwalimu, na, Bwana; nanyi mwanena vema, maana ndivyo nilivyo.
14 Basi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu, nimewatawadha miguu, imewapasa vivyo kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi.
15 Kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo.
16 Amin, amin, nawaambia ninyi, Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake; wala mtume si mkuu kuliko yeye aliyempeleka.
17 Mkiyajua hayo, heri ninyi mkiyatenda. “
Maagizo hayo yanajitosheleza kabisa kwamba yatupasa sisi kutawadhana miguu hii inaonyesha picha ya unyenyekevu na kujishusha jambo hili linapuuziwa sana na watu wengi na katika makanisa lakini ni la muhimu sana na faida zake ni nyingi, unaposhika miguu ya mwenzako na kuiosha mambo yote na sababu zote mbaya ambazo shetani ameziweka za uadui baina yako na ndugu yako zinayeyuka, utashangaa ghafla chuki na ndugu yako inapotea, wivu, masengenyo, kutokumjali kunapotea na jinsi utakavyofanya mara kwa mara ndivyo upendo na mahusiano yanavyozidi kuongezeka zaidi na zaidi.
si ajabu leo tunakosa umoja wa Roho kanisani baina ya ndugu, kwasababu tumeyaacha maagizo kama hayo kila mmoja na mambo yake, mkristo mmoja hamjui mwumini mwenzake kanisani. matabaka kati ya maskini na matajiri yanakuwepo kanisani ni kwasababu hakuna mtu anayetaka kujinyenyekeza kwa mwenzake, Bwana Yesu alisema mkiyajua hayo heri ninyi mkiyatenda, kama Bwana wetu alituosha sisi miguu inatupasaje sisi?? tunapaswa tufanye haya zaidi na zaidi.
Kwahiyo mambo haya mawili makuu (kushiriki meza ya Bwana na kutawadhana miguu), sio lazima yatendeke tu kanisani hata nyumbani tunapokusanyika katika Bwana iwe ni wawili au watatu au wanne, n.k. jambo hili linaweza likatendeka. Na tukizingatia haya hali zetu za kiroho zitazidi kuimarika pamoja na upendo kati ya ndugu na ndugu.
Mungu akubariki.
Kwa mawasiliano/Ushauri/kuokoka/Whatsapp. Namba zetu ni hizi
+255693036618/+255789001312
MWILI NA DAMU YA YESU KRISTO.
HADITHI ZA KIZEE.
JE! NI SAHIHI KUMUITA MARIA MAMA WA MUNGU?
UBATIZO WA MOTO NI UPI?
Bwana YESU ni yeye yule jana, na leo na hata milele hajabadilika wala hana kigeugeu, na NENO lake ni lile lile. Kama maandiko yanavyosema mwanamke wa kikristo anapaswa avae mavazi ya kujisitiri.(1Timotheo 2:9) hilo Neno hata leo bado linaendelea kufanya kazi kwa binti za Mungu.
Leo hii vichaa wapo wengi mitaani tunawaona, lakini ni mara chache sana kumuona kichaa mwanamke akitembea uchi barabarani, ingawa vichaa wanaume ni rahisi kuwaona wakiwa uchi, lakini sio kwa wanawake vichaa utawakuta wamevaa matambara na kujisitiri mwili mzima japo ni vichaa. Je! ni kwanini iwe hivi?? Jibu ni Kwasababu uchi wa mwanamke ni wathamani zaidi kuliko wa mwanamume hivyo unastahili muda wote usitiriwe.
Lakini leo hii mwanamke mwenye akili timamu ambaye uchi wake unathamani ambaye angepaswa afunikwe, ndiye anayeongoza kwa kutembea uchi barabarani, SASA HAPO KICHAA NI NANI? lakini mwanamume ambaye uchi wake usiokuwa na thamani nyingi utakuta kajisitiri, kafunika shingo yake kwa shati na tai, huwezi kuona mgongo wake uko wazi wala mapaja yake wazi akitembea barabarani, miguu yake imesitiriwa yote kwa viatu na soksi, ni mtu huyo ambaye uchi wake hauna thamani sana, Leo hii huwezi kuona mwanaume anaenda na vesti kazini, lakini hili jambo ni la kawaida kwa wanawake kutembea migongo wazi na vifua wazi hata sasa imekuwa kawaida mpaka kwenye sehemu za ibada.
Swali ni Je! roho gani ipo hapo katikati? jibu ni rahisi ni ile ile roho iliyokuwa kwa mwanamke Yezebeli wa kwa maana yeye ndiye mwanamke pekee aliyekuwa anapaka uso rangi katika biblia.Lakini tuna wadada hao hao ambao Bwana Yesu amewaambia yeye mwenyewe wasifanye mambo kama hayo na wametii yaani, kujipodoa uso, kupaka wanja, kuvaa vimini, suruali, kaptura, vesti, tight, pedo, kupaka lipstick, kupachika kucha, wigi n.k. lakini cha ajabu utamkuta mdada mwingine anajiita mkristo na anadai amepokea Roho Wa Mungu lakini bado anajiona salama kufanya vitu hivyo.
Jiulize ni roho gani iliyoko ndani yako? kwanini YESU yule yule amkataze dada yule kufanya hivyo vitu na wewe asikukataze? jiulize sana, kama Roho wa Mungu kweli anakaa ndani yako atakushuhudia kwamba haya mambo hayafai na yanakupeleka kuzimu.
Lakini kaa ukifahamu tu, wanawake wote wanaofanya hivyo sehemu yao ni katika lile ziwa la moto HIVI ASEMA BWANA.. (warumi 1).
MAVAZI YAPASAYO.
CHACHU YA MAFARISAYO NA CHACHU YA HERODE
BWANA YESU ALIKUWA ANAMAANISHA NINI KUSEMA MARKO 2:19″WALIOALIKWA HARUSINI WAWEZAJE KUFUNGA MAADAMU BWANA-ARUSI YUPO PAMOJA NAO?”
PAULO ALIMWAMBIA TIMOTHEO ATUMIE MVINYO KIDOGO KWA AJILI YA TUMBO LAKE, JE! TUNARUHUSIWA NA SISI PIA KUTUMIA POMBE?
WhatsApp
Tukisoma kitabu cha mwanzo 1, Biblia inasema Hapo mwanzo, Mungu aliziumba mbingu na nchi. Lakini tunaona hakueleza aliumbaje umbaje hii mbingu na nchi yaani, miti, jua, mwezi, milima, wanyama, mwanadamu n.k.
Lakini tukija kusoma kwenye kitabu cha waebrania 11:3 tunaona
” Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri. “
Kwahiyo siri inaonekana hapo ni kwamba mbingu na nchi ziliumbwa kwa NENO la Mungu.
Sasa swali linakuja hili NENO ni nini?
Tukisoma Yohana 1:1-3″
1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. 2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. 3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. “
1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.
3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. “
Kwahiyo kulingana na mstari huu biblia inaeleza kuwa Neno lilikuwapo kwa Mungu, na lilikuwa ni Mungu, maana halisi ya “Neno” kulingana na tafsiri ya Kigiriki iliyotumika ni WAZO au NIA. Kwahiyo wazo lilikuwapo ndani ya Mungu, Na hivyo vitu vyote vilivyoumbwa vimetoka katika hilo wazo la Mungu mfano dunia, malaika, wanadamu, sayari, miti n.k.
Mfano mzuri ni kama wewe kitu chochote ulichokitengeneza kama nyumba, kiti, meza, nguo, vilitoka kwanza katika wazo lako au nia yako. Hii ikiwa na maana kwamba kama usingekuwa na hilo wazo usingeviumba vitu hivyo vyote, Vivyo hivyo na kwa Mungu pia kama WAZO lake (ambalo ni Neno lake) asingekuwa nalo hapo mwanzo asingeweza kuumba chochote.
Kwahiyo kabla ya mwanadamu kuasi hili NENO lilikuwa pamoja na mwanadamu, Mtu alikuwa na ushirika na Mungu kwa asilimia zote, kwasababu NENO lilikuwa ndani yake kama lilivyokuwa ndani ya Mungu kitu kilichomfanya mpaka mwanadamu kuonekana kuwa kama mfano wa Mungu, Adamu alikuwa na mamlaka yote duniani, kama vile YESU leo alivyo na mamlaka yote duniani na mbinguni biblia inasema hivyo. Na ndio maana utajua sababu ya Mungu kutuita sisi ni miungu duniani, Na yeye ni MUNGU WA miungu.
Lakini baada ya anguko Adamu aliyapoteza yote aliyokuwa nayo kwasababu alijitenga na NENO la Mungu kwa kutokutii. Hivyo yeye na NENO (nia ya Mungu) vikawa ni vitu viwili tofauti. Kuanzia wakati huo baada ya anguko, lile NENO likaanza kumtafuta tena mwanadamu limrudishe tena katika ile hali ya kuwa na mahusiano na Mungu na mamlaka yote aliyokuwa nayo kabla hajayapoteza. Na ndio maana kuna mahali Yesu alisema sio ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua nyinyi.
Sasa tangu huo wakati lile NENO likaanza kutafuta njia nyingi za kumrejesha mwanadamu, likaanza kuzungumza na wanadamu kwa kupitia MBINGU, nyota,sayari na kwa vitu vya asili, kwa dhumuni la kumrejesha tu, lakini mwanadamu bado hakutaka kutega sikio lake kusikia.
Baadaye lile NENO likaanza kuzungumza kupitia watu, mfano manabii wa Mungu, tunaona manabii kama Henoko, Nuhu, Ibrahimu, Musa, Eliya, Danieli, Yeremia, Isaya n.k..lilisema nao kwa nguvu na kwa udhihirisho mwingi liliwapigia kelele wanadamu wamrudie Mungu, warudi katika ule ushirika waliokuwa nao kwanza na Mungu. Lakini wanadamu bado hawakutega sikio lao kulisikia, zaidi ya yote waliwaua manabii waliotumwa kwalo.
Lakini japokuwa NENO hili limezungumza mara zote hizi kwa vizazi na vizazi kupitia vitu vya asili na manabii, bado ule uhusiano uliokusudiwa mwanadamu awe nao na Mungu wake haukufanikiwa kurejeshwa kwasababu ya ugumu wa mioyo ya wanadamu.
Ndipo wakati ulipofika lile Neno likaona liuvae mwili, lije lenyewe katika mwili,liishi na wanadamu, lihubiri mambo yote lililohubiri ndani ya manabii na vitu vya asili kwa kusudi lile lile la kumrejesha mwanadamu kwa muumba wake. Hili jambo linazungumziwa kwenye..
Waebrania 1:1-2″ Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu. ”
Sasa umeona mwisho wa yote Neno limekuja kuzungumza na sisi kupitia nini? sio kanisa wa chochote bali mwana.
Hili NENO likajichagulia mwili unaoitwa YESU KRISTO, Haleluya! ni furaha kiasi gani Mungu alivyojirahisisha kwetu sisi ili tukae na hilo NENO kwa jinsi ya kimwili, likiongea, likifundisha, likijibu maswali, likitembea na sisi wazi kabisa, linafurahi na sisi, kitu ambacho hapo mwanzo ilikuwa ni ngumu kulielewa lizungumzapo lakini hapa lipo pamoja nasi (IMANUELI)..Embu tutazame mstari ufuatao;
1 Yohana 1:1-3″
1 Lile lililokuwako tangu mwanzo, TULILOLISIKIA, TULILOLIONA kwa macho yetu, TULILOLITAZAMA, na mikono yetu IKALIPAPASA, kwa habari ya NENO la uzima; 2 (na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu); 3 hilo tuliloliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo.”
1 Lile lililokuwako tangu mwanzo, TULILOLISIKIA, TULILOLIONA kwa macho yetu, TULILOLITAZAMA, na mikono yetu IKALIPAPASA, kwa habari ya NENO la uzima;
2 (na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu);
3 hilo tuliloliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo.”
Habari hiyo inaelezea lile NENO ambalo zamani lilikuwepo lakini sasa limefanyika mwili na lipo katikati yetu kama mwanadamu.
Hivyo basi BWANA YESU KRISTO alipokuja akaanza kutufundisha na kuturejesha katika utimilifu wote na Mungu tuliokuwa nao pale Edeni hata na zaidi ya pale.,Jambo la kwanza alilolifanya ni kutupatanisha sisi na Mungu kwa kumwaga damu yake kwa ajili ya ondoleo la dhambi zetu maana biblia inasema pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo (waebrania 9:22).
Na jambo la pili ni kutufanya sisi kuwa wana wa Mungu (miungu) Yohana 1:12 “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; “
Tukisoma
2 Wakoritho 5:18-19 “Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, naye alitupa huduma ya upatanisho; yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu NENO la upatanisho. “
Kama tulivyosema lile NENO ni wazo/nia ya MUNGU nalo ni Mungu, ikiwa na maana usiipotii nia ya Mungu haujamtii Mungu. Na nia ya Mungu ni nini? Ni kuturujesha sisi tuwe na mahusiano naye kama ilivyokuwa hapo mwanzo ili tumwabudu MUNGU katika Roho na Kweli. Na ndio maana WAZO/NIA yake iliuvaa mwili kwa dhumuni la kutuhubiria sisi tumgeukie Baba.
Kwasababu hiyo basi Yesu Kristo ndiye NJIA, NA KWELI, NA UZIMA, MTU HAFIKI KWA BABA ISIPOKUWA KWA NJIA YAKE YEYE.(Yohana 14:6), alisema aliyeniona mimi amemwona BABA, usipomtii YESU KRISTO na kumwamini umeukataa mpango wa Mungu kwa wanadamu na viumbe vyake vyote kama shetani alivyofanya.
Natumaini utakuwa umeshaiona sababu ya YESU KRISTO Kutokea ni nini?, ni hiyo hapo juu, Neno la Mungu liliuvaa mwili, kutuhubiria sisi na kuturejesha kwa Mungu wetu ili tumwabudu yeye katika roho na kweli.
Wakolosai 2:9 “Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili. “
Kwahiyo Mungu hana nafsi tatu, Nafsi ya Mungu ni moja tu. Mungu kuonekana katika mwili hakumfanyi yeye kuwa na nafsi tatu. Alifanya hivyo tu ili kutupatanisha sisi na yeye. Kama tusingeanguka katika dhambi kulikuwa hakuna haja ya yeye kuuvaa mwili na kuja duniani, Yeye ni Roho nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.
NEEMA YA BWANA YESU KRISTO IWE PAMOJA NAWE!
BADO KITAMBO KIDOGO HAMNIONI
VIUNO VYENU VIWE VIMEFUNGWA NA TAA ZENU ZIWE ZINAWAKA
VIUMBE VINATAZAMIAJE KUFUNULIWA KWA WANA WA MUNGU?
NINI MAANA YA MSIMWITE MTU BABA DUNIANI?
KAINI ALIPATIA WAPI MKE?
Je! Manabii wa uongo ni wapi?
Mathayo 7:15 “Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali. 16 Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti? 17 Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya. 18 Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri. 19 Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni. 20 Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua. 21 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. 22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? 23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu. “
Kuna watu wanasema usizihubiri hizi habari, we fundisha TU watu watubu wawe wakristo inatosha ndiyo kazi yako!. Swali ni je! ukishakuwa mkristo ndio mwisho wa safari?, unahitaji kukua na ndio safari inapoanzia na sio inaishia. Hivyo basi unahitaji chakula ili ukue, na ujue ni chakula gani unapaswa ukile, maana vyakula ni vingi vijengavyo na vibomoavyo, Hivyo ni kuwa makini kujua ni chakula kipi ule na kipi usile kwa usalama wa roho yako na hatma yako ya milele.
Tunaishi katika kipindi cha hatari ambacho hakijawahi hata kutokea katika vizazi vyote vya nyuma, ambacho kina mchanganyiko mkubwa wa MANABII WA UONGO NA MANABII WA KWELI, Na wote wanafanya kazi moja ya KUVUNA ROHO ZA WATU, aidha kuzipeleka kuzimu au mbinguni, ni kipindi cha hatari sana tunachoishi. Ni muhimu kufahamu unavunwa upande gani, ili usije ukajikuta unadondokea sehemu ambayo haujatarajia.
Jambo kubwa linalowachanganya watu wengi ni kuona pale mtu anayejiita mtumishi wa Mungu halafu bado ni mwasherati, mtukanaji, mlevi, anapenda anasa, na bado miujiza inatendeka na yeye, anafufua wafu, anaombea watu wanaponywa, anatabiri na unabii unakuja kutimia, ananena kwa lugha n.k.
Kiasi ambacho kinamfanya mtu mchanga ashindwe kuelewa inawezekanikaje huyu mtumishi anafanya mambo ya kidunia lakini bado ishara na miujiza zinatendeka na yeye, Na wala hatumii uchawi ila anatumia jina la YESU na nguvu za Mungu zinashuka. “HII NI SIRI” na ni jukumu kwa kila mkristo anayethamini maisha yake ya kiroho kufahamu..kumbuka (kuna wanaotumia nguvu za giza kutenda miujiza, siwazungumzii hao, hao ni rahisi kuwagundua lakini nawazungumzia wale wanaotumia nguvu za Mungu ambao ni ngumu kuwatambua.)
Tusome, mstari ufuatao unawazungumzia hao wanaotumia nguvu za Mungu ; Kumb.13:1-5″
1 Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu, 2 ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo; 3 wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda Bwana, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote. 4 Tembeeni kwa kumfuata Bwana, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye. 5 Na yule nabii, au yule mwotaji wa ndoto, na auawe, kwa kuwa amesema yaliyopotoka juu ya Bwana, Mungu wenu, aliyewatoa katika nchi ya Misri, akakukomboa katika nyumba ya utumwa, apate yule mtu kukupotoa katika njia aliyokuamuru Bwana, Mungu wako, uiendee. Ndivyo utakavyouondoa uovu utoke katikati yako. “
Unaona hapo? Huyo nabii hapo katoa unabii kwa uweza wa nguvu za Mungu na ikatokea, lakini anawafundisha watu waende kinyume na maagizo ya Mungu. Vivyo hivyo na hata sasa katika kipindi hichi cha mwisho Mungu ameamua kuachia mvua yake (UPAKO) kwa watu wote waovu na wema kutujaribu sisi kama TUNAMPENDA BWANA NA KUYASHIKA MANENO YAKE AU LA!.
Mtu anaweza akaja kwako na kutoa unabii na ukatimia na kufufua wafu, na kuponya wagonjwa lakini akafundisha injili nyingine akakwambia ulevi ni sawa, wanawake kwenda na mitindo ya kisasa ni sawa (anasema Mungu haangalii mavazi anaangalia roho ), akakufundisha kuupenda ulimwengu ni sawa, kuoa wake wengi ni sawa, Dunia haiishi leo wala kesho kula maisha, kuwa na pesa nyingi ndio kigezo cha kubarikiwa na Mungu, Mungu siku zote ni Mungu mzuri na hawezi kuwahukumu watu aliowaumba. n.k. na bado mtu huyo akatoa mapepo na kufufua wafu.
Na wewe kwasababu NENO na kumpenda Mungu hakupo ndani yako, ukadhani anazungumza ukweli au katumwa na Mungu kwasababu tu! ametoa unabii ukatokea, NDUGU USIDANGANYIKE UMEPOTEA!! . Biblia inasema jiepushe na huyo mtu, CHUKUA TAHADHARI KWA USALAMA WA MAISHA YAKO..KIMBIA! HARAKA SANA NI BWANA NDIYE ANAYEKUJARIBU KUONA KAMA UNAMPENDA KWELI NA KULIFUATA NENO LAKE AU LA!
Leo hii wewe unayejiita mkristo unapenda injili za kufarijiwa tu! siku zote unapendwa kuambiwa “ALL IS WELL” ulimwengu hautakuja kuteketezwa,tunaishi chini ya neema, mafundisho unayoyapenda wewe ni KUTABIRIWA MAFANIKIO TU!. Lakini fahamu jambo moja BWANA YESU hakuacha enzi na mamlaka mbinguni ili aje kutufia sisi mlabani tuwe MABILIONEA, bali kwa ajili ya dhambi zetu.(hicho ndicho kiini cha injili) yeye mwenyewe alizungumza ..Mathayo 16:24-27
” Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate. 25 Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona.26 Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?
Leo mkristo anadai anamfuata YESU, lakini kigezo cha kumfuata YESU ni kuwa na MSALABA wako, sasa wewe MSALABA WAKO UKO WAPI?, Jihadhari na haya mafundisho ya uongo yanawapeleka maelfu wa waaminio kuzimu kila siku pasipo wao kujua.
Hawa manabii wa uongo, Bwana Yesu alisema tutawatambua kwa MATUNDA YAO na sio kwa upako wao, kwasababu Mungu anaweza akamtumia mtu kama chombo tu cha kuazima akishamaliza shughuli nacho anakiacha, mfano tunaona Mungu alimtumia Punda kuongea na Nabii Balaamu kumpa ujumbe, lakini baada ya punda kutoa ujumbe alirudia katika hali yake ya kawaida ya upunda, vivyo hivyo na Balaamu mwenyewe alikuwa ni MCHAWI lakini Mungu alimtumia yeye kuwabariki Israeli, (hesabu 22:21-29),
Na pia Mungu aliwatumia wale manabii 400 kumdanganya mfalme Ahabu kwasababu Mungu alikuwa amekusudia mabaya juu yake. (1 wafalme 22:6). Kwahiyo kuwa na upako mtu kuona maono, au kuwa nabii, au kunena kwa lugha au kuponya au kufanya miujiza yoyote ile, sio kigezo cha huyo mtu kuwa NABII WA MUNGU. Tutatawatambua kwa matunda yao (AMBAYO NI NENO LA MUNGU). Nabii wa ni yule anayekuja na ishara pamoja na NENO lakini lililokuu ni NENO.
Kipime mtu anachokuambia je! kinaendana na NENO la Mungu? kama hakiendani na NENO la Mungu weka kando haijalishi anawashirika wengi kiasi gani, au anakubalika kiasi gani, au kanisa ni kubwa kiasi gani, au anaupako kiasi gani. KIMBIA! HILO NI SINAGOGI LA SHETANI!..
Jiulize Wewe unayejiita mkristo tangu ulipoamini, maisha yako ya kiroho yamesonga mbele kiasi gani. utakuwaje mkristo halafu biblia husomi!?? sasa utawatambuaje manabii wa uongo au manabii wa ukweli kwa namna hiyo watakapokujia na mafundisho yao??. Utakuwa unapelekwa na kila upepo unaokuja wa elimu yoyote. Maana njia pekee ya kumpima nabii wa uongo au Nabii wa ukweli ni kwa NENO TU!.
Na sio kitu kingine. Jijengee kila siku tabia ya kusoma NENO na kuomba. Hizi ni nyakati za hatari tunaishi zile zilizotabiriwa kuwa watatokea manabii na makristo wengi wa uongo nao watawadanganya wengi yamkini hata walio wateule. Kumbuka ni wateule ndio wanaozungumziwa hapo kuwa wanaweza wakadanganywa sasa jiulize wewe ambaye sio mteule utaonekania wapi? wewe ndio hautaelewa chochote kinachoendelea utaishia kuwashangilia na kuwasifia kama Bwana Yesu alivyotabiri juu ya manabii wa uongo.
2 Petro 1:10″ Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe.”
KWAHIYO NDUGU HUU NI WAKATI WA MUNGU KUTUJARIBU SISI KAMA TUNAMPENDA YEYE NA KULISHIKA NENO LAKE AU LA!. Biblia inasema, MPENDE BWANA MUNGU WAKO, KWA MOYO WAKO WOTE, KWA ROHO YAKO YOTE, KWA NGUVU ZAKO ZOTE, NA KWA AKILI ZAKO ZOTE.
Mungu hadhihakiwi usipoweza kufanya hivyo jua tu utaangukia kwenye huu mstari ufuatao;
2 Thesalonike 2:10-12″… na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa. 11 KWAHIYO MUNGU AWALETEA NGUVU YA UPOTEVU, WAUAMINI UONGO;12 ILI WAHUKUMIWE WOTE ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu. “
MARAN ATHA!
Masomo Mengineyo
UPENDO NI NINI NA JE! KUNA AINA NGAPI ZA UPENDO?
UNYAKUO.
Nini maana ya “Roho za manabii huwatii manabii?
HUJAPEWA MBAWA ZA KUKIMBIA MATATIZO
Kutoka 21:2-6 ” Ukimnunua MTUMWA wa Kiebrania, atakutumikia muda wa miaka sita; mwaka wa saba atatoka kwako HURU bure. 3 Kwamba aliingia kwako peke yake tu, atatoka hivyo peke yake; kwamba ameoa, mkewe atatoka aende pamoja naye. 4 Kwamba ni bwana wake aliyempa huyo mke, naye amemzalia wana, wa kiume au wa kike; yule mke na wanawe watakuwa ni mali ya bwana wake, naye mume atatoka peke yake. 5 Lakini huyo mtumwa AKISEMA WAZIWAZI, Mimi nampenda bwana wangu, na mke wangu na watoto wangu; SITAKI MIMI KUTOKA NIWE HURU; 6 ndipo hapo huyo bwana wake atamleta mbele ya Mungu na kumleta mlangoni, au penye mwimo wa mlango; na bwana wake ATALITOBOA SIKIO LAKE KWA UMA; ndipo ATAMTUMIKIA SIKU ZOTE. “
Kutoka 21:2-6 ” Ukimnunua MTUMWA wa Kiebrania, atakutumikia muda wa miaka sita; mwaka wa saba atatoka kwako HURU bure.
3 Kwamba aliingia kwako peke yake tu, atatoka hivyo peke yake; kwamba ameoa, mkewe atatoka aende pamoja naye.
4 Kwamba ni bwana wake aliyempa huyo mke, naye amemzalia wana, wa kiume au wa kike; yule mke na wanawe watakuwa ni mali ya bwana wake, naye mume atatoka peke yake.
5 Lakini huyo mtumwa AKISEMA WAZIWAZI, Mimi nampenda bwana wangu, na mke wangu na watoto wangu; SITAKI MIMI KUTOKA NIWE HURU;
6 ndipo hapo huyo bwana wake atamleta mbele ya Mungu na kumleta mlangoni, au penye mwimo wa mlango; na bwana wake ATALITOBOA SIKIO LAKE KWA UMA; ndipo ATAMTUMIKIA SIKU ZOTE. “
Biblia inaeleza wazi kabisa kulingana na maandiko hayo hapo juu, Mtumwa yule aliyetangaziwa uhuru wake baada ya kutumika miaka 6 akakataa (Yaani akaona ni vyema kuendelea katika utumwa wake.). Jambo linalotokea ni hili bwana wake huyo mtumwa atachukua sindano na kutoboa SIKIO lake, kuwa kama MUHURI wa kukataa kuwekwa huru, Hivyo basi huyo mtumwa atamtumikia bwana wake milele, Na kama tunavyofahamu sikio likishatobolewa haliwezi kurejea tena katika hali yake ya kwanza. Na ndio maana ilikuwa inatumika kama ISHARA YA MAPATANO(MUHURI).
Vivyo hivyo kwa wanadamu wa leo, Kristo alikuja kututangazia uhuru wetu kutoka katika UTUMWA WA DHAMBI kulingana na
Mathayo 11:28-29 (Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; “),
Kwasababu Bwana Yesu alisema Yohana 8:34-36″ ….Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.Wala mtumwa hakai nyumbani sikuzote; mwana hukaa sikuzote. Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli. “
Bwana Yesu pia alisema maneno haya luka 4:18-19″ Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma KUWATANGAZIA WAFUNGWA KUFUNGULIWA KWAO, Na vipofu kupata kuona tena, KUWAACHA HURU WALIOSETWA,Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa. “
Kwahiyo injili ililetwa kwetu mahususi kwa kutuweka HURU mbali na dhambi. Hapo anaposema
“kuutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa” akiwa na maana kuwa ndio mwaka wa maachilio, ule mwaka wa saba ( Kwa maana mahali pengine anasema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia; tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa.
2 Wakoritho 6:2). Kwahiyo tunaona MBIU YA MAACHILIO IMESHAPIGWA watu wote wawe HURU kwa YESU KRISTO BWANA. Lakini cha kusikitisha wapo baadhi ya watumwa (watumwa wa dhambi), wanakataa kuupokea uhuru WAO waliotangaziwa na Bwana wanapenda kuendelea kumtumikia bwana wao shetani ambaye hapo mwanzo alikuwa anawatumikisha na kuwatesa. Embu tuitazame hii mihuri inampataje mtu.
Mungu anao MUHURI wake, na shetani pia anao muhuri wake kwa watoto wake. Wale waliokubali kuwekwa huru na BWANA wanatiwa MUHURI WA MUNGU nao ni ROHO MTAKATIFU kulingana na
waefeso 4:30″(Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa MUHURI hata siku ya ukombozi). , na pia biblia inasema katika
2 Wakoritho 3:17 .. walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru. “.
Kwahiyo unaona unapoukubali UHURU Mungu anakupa zawadi ya kupokea Roho Mtakatifu kama Muhuri wa uhuru wako. Lakini kama hauna Roho wa Mungu wewe bado ni mtumwa wa dhambi na UNAJUA MSHAHARA WA DHAMBI NI MAUTI. Warumi 8:9″….Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake. ”
Kwa wale waliokataa uhuru kwa makusudi angali wakijua kabisa wapo kwenye utumwa na wangepaswa wawe huru, lakini wakapenda kumtumikia bwana wao shetani katika dhambi zao kuliko kumtumikia Mungu nao pia wanatiwa MUHURI. Na mihuri hiyo YA SHETANI wanatiwa katika MASIKIO YA MIOYO YAO, maana yake ni hii HAWATAKUWA TENA NA NEEMA YA MUNGU JUU YA MAISHA YAO!,baada ya kuisikia injili na kuikataa Haiwezekani wao kumgeukia Mungu tena, Hata waelezweje injili hawawezi kusikia tena wageuke hao wameshakuwa mali halali ya shetani. Hii ni hatari sana tuwe makini tunaposikia wito wa Mungu.
Na huu muhuri wa shetani mpaka sasa hivi unaendelea kuwapiga watu,
leo hii umeshaisikia injili mara ngapi, umehubiriwa uache uzinzi mara ngapi ewe kijana ewe binti,? umehubiriwa utubu dhambi zako mara ngapi? lakini umekuwa wa kwanza kufanya mizaha? umehubiriwa uache ulevi mara ngapi? unavuta sigara, unaangalia pornoghaphy, unafanya mustarbation, binti unasagana, umekuwa shoga kijana, unaenda kwa waganga, unajifurahisha katika anasa na miziki ya kidunia,
Mwanamke unavaa suruali, vimini, unapaka rangi kucha, kijana unanyoa mitindo isiyofaa na kusuka nywele ,na tatoo kwenye mwili wako, wanawake usengenyaji na umbea, mtukanaji, unajichanganya na watu waovu kwa jinsi isivyopasa, unachati nao mambo maovu, huku ukijua kabisa watu wanaoyafanya hayo wataishia katika jehanum ya moto, JE! UNADHANI NEEMA YA MUNGU ITAENDELEA KUDUMU JUU YAKO MILELE?.
Mungu hadhihakiwi apandacho mtu ndicho atakachokivuna. Tutawezaje kupona tusipouthamini wokovu mkuu namna hii?.
Unashindwa kuona jinsi unavyozidi kutiwa ule MUHURI wa shetani? kwa kuukataa uhuru wako ambao BWANA aliokutangazia pale KALVARI?. Maana kama unasikia sauti ya Mungu kila siku ikisema moyoni mwako UTUBU lakini unaipuuzia nakwambia ukweli utafika wakati HAUTAKAA UISIKIE TENA NDANI YAKO!!,
Na unajua ni kitu gani kitaenda kukutokea? Ni kwamba utafika wakati utaona mambo yote kuwa ni sawa, kuwa ulevi ni sawa,utaona uasherati hauna ubaya wowote, Mungu aliyetuumba hawezi kutuhukumu, hautaamini tena kama kuna jehanamu, utaishia kuwaona watumishi wote wa Mungu ni waongo, utaishia kuukosoa kila siku ukristo na biblia ukisema hayo mambo ni ya kale.
Utaanza kujiona kuwa ni haki yako kuishi unavyotaka hata kujichubua, kubadili maumbile, kuvaa unavyotaka ni sawa, Utajiona kutukana ni sehemu tu ya maisha ya binadamu hakuna kosa lolote kwasababu Roho Wa Mungu hayupo tena ndani yako kwasababu UMESHATIWA MUHURI, utaanza kuona kujipenda mwenyewe ni sawa, Kutazama pornography na kufanya musturabation ni sehemu maisha ya kila mwanadamu ukijidanganya kuwa Mungu hawezi kumuhukumu mtu kwa kufanya hivyo, unajikuta unaanza kupenda kufuatilia mafundisho ya mashetani kuliko mafundisho ya Mungu, Biblia hutaki kusoma kusoma lakini habari za freemasons, na zi kichawi, na filamu pamoja na vitabu kama , harryporter, twightlight, vampires,n.k. ndivyo vinavyokuvutia kusoma na kuangalia, jiulize ni roho gani inakuendesha? n.k.
Ndugu ukishaanza kuona dalili ya mambo kama hayo yanakuja ndani yako, jua kabisa neema ya Mungu ndivyo inavyoondoka kwako kidogo kidogo na ndo unavyoupokea MUHURI wa shetani hivyo, maana jua tu wewe unayeisikia injili kila siku unaambiwa utubu hautaki, neema yako haiwezi kuwa sawa na mtu yule ambaye hajawahi kusikia injili kabisa. soma mstari ufuatao;
2 Wathesalonike 2:10-12 ” na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa. 11 KWAHIYO MUNGU AWALETEA NGUVU YA UPOTEVU, WAUAMINI UONGO; 12 ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu. “
Kwahiyo ndugu maneno hayo hayakuogopeshi?? TUBU! yamkini hii sauti ya upole inayokuambia kila siku utubu bado inaendelea KULIA NDANI YAKO! ..itii na ugeuke maana upo katika HATARI, Maana hiyo sauti haitadumu milele ndani yako. Na ikishaondoka hakutakuwa na njia ya kurudi tena. YAANI MOYO WA KUTUBU hautakuwepo tena ndani yako utafanana na hao watu unaowaona huko ulimwenguni watendao matendo ya giza si kana kwamba hawasikii au hawakusikia injili hapana lakini mioyo yao imeshatiwa MUHURI, hawatakaa wasikie tena na kubadilika, ndugu usifanane nao. Mtii Mungu tubu dhambi zako muda umeenda sana kuliko unavyofikiria.Yesu yupo mlangoni kurudi. Maana biblia inasema…
Ufunuo 22:10 “Akaniambia, Usiyatie muhuri maneno ya unabii wa kitabu hiki, kwa maana wakati huo umekaribia. MWENYE KUDHULUMU NA AZIDI KUDHULUMU; na MWENYE UCHAFU AZIDI KUWA MCHAFU; na MWENYE HAKI AZIDI KUFANYA HAKI; na MTAKATIFU NA AZIDI KUTAKASWA.Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. “
Naomba umalizie kwa kuyatafakari maneno yafuatayo ujue hatma ya WALIOUKATAA UHURU WAO KUTOKA KWA BWANA;
Warumi 1:24” Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao. 25 Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina. 26 HIVYO MUNGU ALIWAACHA WAFUATE TAMAA ZAO ZA AIBU, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili; 27 wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, WAKAPATA NAFSINI MWAO MALIPO YA UPOTEVU WAO YALIYO HAKI YAO. 28 NA KAMA WALIVYOKATAA KUWA NA MUNGU KATIKA FAHAMU ZAO, MUNGU ALIWAACHA WAFUATE AKILI ZAO ZISIZOFAA, WAYAFANYE YASIYOWAPASA. 29 Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya, 30 wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao, 31 wasio na ufahamu, wenye kuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema; 32 AMBAO WAKIJUA SANA HUKUMU YA HAKI YA MUNGU, YA KWAMBA WAYATENDAYO HAYO, WAMESTAHILI MAUTI, WANATENDA HAYO, WALA SI HIVYO TU, BALI WANAKUBALIANA NAO WAYATENDAYO. Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Warumi 1:24” Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao. 25 Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina. 26 HIVYO MUNGU ALIWAACHA WAFUATE TAMAA ZAO ZA AIBU, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili; 27 wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, WAKAPATA NAFSINI MWAO MALIPO YA UPOTEVU WAO YALIYO HAKI YAO. 28 NA KAMA WALIVYOKATAA KUWA NA MUNGU KATIKA FAHAMU ZAO, MUNGU ALIWAACHA WAFUATE AKILI ZAO ZISIZOFAA, WAYAFANYE YASIYOWAPASA. 29 Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya, 30 wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao, 31 wasio na ufahamu, wenye kuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema; 32 AMBAO WAKIJUA SANA HUKUMU YA HAKI YA MUNGU, YA KWAMBA WAYATENDAYO HAYO, WAMESTAHILI MAUTI, WANATENDA HAYO, WALA SI HIVYO TU, BALI WANAKUBALIANA NAO WAYATENDAYO.
UMETEKWA NA UPENDO WA KRISTO?
WAKATI WA JIONI KUTAKUWAKO NA NURU.
NUHU ALIWALETAJE LETAJE WANYAMA KWENYE SAFINA?
NINI TOFAUTI KATI YA 1) KUOKOKA, 2) WOKOVU, 3) KUONGOKA?
UAMSHO MKUU UMEKARIBIA!!
Yoeli 2:28-32″ Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono; 29 tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu. 30 Nami nitaonyesha MAMBO YA AJABU KATIKA MBINGU na KATIKA DUNIA, DAMU, na MOTO, na MINARA YA MOSHI. 31 JUA LITAGEUZWA KUWA GIZA, na MWEZI KUWA DAMU, kabla haijaja hiyo siku ya Bwana iliyo kuu na itishayo. 32 Na itakuwa ya kwamba mtu awaye yote atakayeliita jina la Bwana ataponywa; kwa kuwa katika mlima Sayuni na katika Yerusalemu watakuwako watu watakaookoka, kama Bwana alivyosema; na katika mabaki, hao awaitao Bwana.
Yoeli 2:28-32″ Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono;
29 tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu.
30 Nami nitaonyesha MAMBO YA AJABU KATIKA MBINGU na KATIKA DUNIA, DAMU, na MOTO, na MINARA YA MOSHI.
31 JUA LITAGEUZWA KUWA GIZA, na MWEZI KUWA DAMU, kabla haijaja hiyo siku ya Bwana iliyo kuu na itishayo.
32 Na itakuwa ya kwamba mtu awaye yote atakayeliita jina la Bwana ataponywa; kwa kuwa katika mlima Sayuni na katika Yerusalemu watakuwako watu watakaookoka, kama Bwana alivyosema; na katika mabaki, hao awaitao Bwana.
Tukisoma mistari hiyo Nabii Yoeli alionyeshwa maono ya uvuvio mkubwa wa Roho ya Mungu ambao ungekuja katika siku za mwisho, Na ni dhahiri kabisa kwa wasomaji wa biblia wanafahamu sehemu ya huo unabii ulitimia wakati wa PENTEKOSTE, pale Roho wa Mungu alipowashukia wale watu 120 kwa mara ya kwanza, na kuwapa vipawa vikubwa na vya ajabu, ishara na miujiza mingi ikifanywa na mitume na wale wote waliojazwa Roho Mtakatifu.
Mvua hii ya Roho Mtakatifu Mungu aliyoiachilia kwa mara ya kwanza pale Pentekoste inajulikana kama “MVUA YA AWALI/MASIKA” ( kwa kiingereza former Rain). Lakini pia Mungu aliahidi kuileta mvua nyingine tena ambayo ni “MVUA YA BAADAYE/ VULI” ( kwa kiingereza Latter Rain). Kwa ufafanuzi wa maelezo haya tusome;
Yoeli 2:23 “Furahini, basi, enyi wana wa Sayuni, mkamfurahie Bwana, Mungu wenu; kwa kuwa yeye huwapa ninyi MVUA YA MASIKA, kwa kipimo cha haki, naye huwanyeshea mvua, MVUA YA MASIKA, na MVUA YA VULI, kama kwanza.”
Kwahiyo hii mvua ya pili (MVUA YA VULI) mbali na ile ya kwanza iliyotokea wakati wa Pentekoste, Tukisoma katika historia ya ukristo Bwana aliishusha tena mwaka 1906, kwenye uamsho uliotokea mtaa wa AZUSA, huko Calfornia Marekani ambapo Bwana alimwaga ROHO wake na kushusha vile vipawa tena vya Roho Mtakatifu kama ilivyokuwa katika Pentekoste ya kwanza baada ya kanisa la Kristo kukaa muda mrefu bila uamsho kwa muda wa karne nyingi, lakini kuanzia huu mwaka 1906 tunaona vipawa vyote vilirejeshwa watu wakaanza kunena kwa lugha, kutabiri, kuponya magonjwa, ishara na miujiza, unabii n.k. vitu ambavyo havikuwahi kutenda tangu wakati wa kanisa la kwanza.
Hivyo basi Mungu alimtuma mjumbe wake William Branham kama mjumbe wa kanisa la mwisho LAODIKIA, ufunuo 3, Mungu alimtumia kwa ishara nyingi na miujiza ya ajabu ambayo haikuwahi kufanyika hapo kabla ikiwemo na utambuzi wa siri za mioyo ya watu, tafsiri za ndoto kama ilivyokuwa kwa Nabii Danieli, na ishara zilizoweza kuonekana wazi na kunaswa katika picha za kimagnetiki, n.k.
Ndipo Mungu akaendeleza kuimwaga hiyo roho kwa watumishi wake wengi waaminifu duniani kote kwa mfano wa William Branham kama oral Robert, Billy Granham, TL Osborn, nk..
( tazama ushuhuda mfupi juu ya huduma na maisha ya William Branham,)
Mvua hii ya mwisho itatimizwa katika huu wakati wa mwisho Bwana aliahidi sehemu hii ya maandiko itaenda kutimia
Yoeli 2:29 “tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu. 30 Nami nitaonyesha mambo ya ajabu katika mbingu na katika dunia, damu, na moto, na minara ya moshi. 31 Jua litageuzwa kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla haijaja hiyo siku ya Bwana iliyo kuu na itishayo.
Yoeli 2:29 “tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu.
30 Nami nitaonyesha mambo ya ajabu katika mbingu na katika dunia, damu, na moto, na minara ya moshi.
31 Jua litageuzwa kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla haijaja hiyo siku ya Bwana iliyo kuu na itishayo.
Kumbuka katika mvua iliyoachiliwa mara ya kwanza, tuliona unabii, lugha, maono, ndoto, ishara, n.k. lakini hatukuona mambo ya ajabu katika dunia na katika mbingu kama jua kutiwa giza, mwezi kuwa damu, moto, minara ya moshi, n.k. tumezoelea kuona unabii na uponyaji, lakini haya mambo mengine yaliyosalia yanaenda kutimilika katika hii mvua ya mwisho na yatakuja na hukumu sio kwa kuwaburudisha watu, Tunaona mfano uliotokea kwa mapigo ya Musa na Eliya. Ni mambo ya kutisha yanakuja. Na ishara ambazo hata hazijawahi kurekodiwa wala kufanywa mahali popote pale katika historia ya dunia.
Kumbuka hakuna ishara isiyokuwa na ujumbe nyuma yake. Hivyo hizi ishara zitakuja na ujumbe, na ujumbe wake utakuwa ni wa kipekee, ukisoma kitabu cha ufunuo 10:4-11″ Inaelezea zile NGURUMO SABA ambazo Yohana aliambiwa asiziandike, ni siri zilizofichwa tangu zamani nazo hazijaandikwa mahali popote katika biblia.
Zipo siri nyingi ambazo hazijulikani kwamfano “Tutakapofika kwenye utawala wa miaka 1000 ni shughuli gani zitakuwa zinaendelea , na tukienda mbinguni tutakuwa tunafanya nini huko, siri za kwenda kwenye unyakuo na siri za kurudi kwa pili kwa Yesu, kuanguka kwa shetani, na mambo yaliyokuwa yanatendeka kabla ya Adamu kuumbwa nk,(huu ni mfano tu, zinaweza zikawa nyingine tofauti ya hizo au zaidi ya hizo ) .Siri hizi zitakuja kufunuliwa katika wakati huu ambao upo karibu katika mvua hii inayokuja kunyesha.
Ndugu William Branham kabla ya kufariki kwake alionyeshwa na Bwana huu uvuvio mkubwa jinsi utakavyokuja kuwa kiasi kilichomfanya yeye mwenyewe atamani kuwepo katika huo uamsho. Katika hilo ono alionyeshwa uponyaji wa kiungu wa ajabu ukitendeka watu wengi walikuwa wakiponywa kabisa kabisa.
lakini tukisoma
Mathayo 24:14″Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.”
Mstari huu unaelezea jambo litakalofanyika kwanza kabla ya Bwana YESU kurudi, Huu uamsho unaokuja ndio utakaokuwa wa mwisho na utapita duniani kote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote, kwasababu mambo dhahiri na ishara za ajabu zitaonekana kwa watu wote na bibi-arusi naye atakusanyika pamoja kwa ajili ya unyakuo na ndipo ule mwisho utakapokuja.
Ndugu hizi siku zipo karibu, wakati huo utakapofika kama leo haujajiweka tayari kule hautaweza kwasababu zitakuja na hukumu kutoka kwa Bwana, utaishia kupinga na kusema ni vya shetani, kwasababu utasikia mambo ambayo pengine hayajarekodiwa mahali popote kwenye biblia, na hautapata uhakiki wa mambo hayo sehemu yeyote kama hauna ROHO MTAKATIFU kwasababu ni mambo mapya kabisa na hautaweza kupambanua utabakia kuwa mtu wa nia mbili kama unyasi utikiswao na upepo hutajua wapi usimame, ikiwa leo tu huwezi kumtambua yupi nabii wa kweli na yupi nabii wa uongo, utawezaje kuelewa yatakayokuja huko mbele ambapo mambo mapya yatakuja kuhubiriwa??.
Tafakari ndugu tunaishi katika siku za mwisho, ijue kalenda ya Mungu katika maisha yako na wakati tuliopo, usije ukafanana na wale wanawali wapumbavu ambao hawakuwa na mafuta ya ziada katika taa zao. Maana ya yale mafuta ya ziada ni roho ya mafunuo ambayo mkristo wa dini tu hawezi kuwa nayo.
Ndugu kaa ukifahamu Huu uamsho utaanza duniani kote hivi karibuni, na mambo ya ajabu yataenda kutendeka na kuhubiriwa, kwa waovu itakuwa ni hukumu bali kwa wenye haki itakuwa ni kwa kuandaliwa kwa ajili ya unyakuo. Maandalizi ni sasa.
“Tumeandika makala hii kuwakumbusha bibi arusi wa Kristo wote popote walipo kuwa kuna uamsho mkuu unakuja mbeleni na kuna baadhi ya watumishi wa Mungu waaminifu wachache wamekwisha anza kuonyeshwa katika maono na Bwana Yesu, jinsi utakavyokuwa. Tazama chini shuhuda chache za watu hawa;”
USHUHUDA WA STEPHEN POWELL’S
Stephen Powell’s ni muhubiri wa kimarekani hivi karibuni tarehe 21 April 2017. Bwana alimwonyesha maono yafutayo na haya ni maneno yake yaliyonukuliwa;
Kulingana na historia, “NEMBO” (Coat of Arms) ni ishara muhimu ya utaratibu wa urithishaji uliotumika katika zama za kati huko Ulaya, Ilitumika mahususi kama utambulisho katika vita, Nembo zilianzishwa kuashiria ukoo wa familia fulani, urithi, umoja, umiliki, na pia katika taaluma fulani .
Bwana kwasasa anaenda kupitisha NEMBO hii ya thamani sana kwa kizazi chenye utukufu anachokinyanyua leo duniani!, Mungu anaenda kuachilia uhalali fulani, ujuzi fulani, na urithishwaji katika roho!. Nisikilize kwa makini kitu ninachokwenda kusema sasa…
Hivi karibuni katika mfululizo wa maono niliyopewa, nilichukuliwa mbinguni nikaonyeshwa vitu vingi. Mara ya mwisho nilijikuta nimerudi katika hali yangu ya kawaida nikiwa na akili zangu juu ya kitanda changu katika hotel moja huko west Virginia. Na nilipokuwa nimelala pale nilisikia BWANA akisema ” NINARUDISHA TENA NEMBO YA VITA ALIYOKUWA AMEIVAA WILLIAM BRANHAM “. Kisha nikaona ono Bwana akishika bega la askari mmoja ambaye kwenye nguo yake kulikuwa na kitu kama NEMBO hivi ingawa sikuweza kuikariri jinsi ilivyokuwa. Kisha Bwana akaniambia ataenda kuachia vipawa vya miujiza katika mikono ya wana wake na binti zake katika hichi kipindi, kama ilivyokuwa kwa William Branham alivyopewa sio tu kuona maono bali pia kipawa katika viganja vyake.
Katika vita askari huwa wanavaa vazi fulani la nje (surcoat) kuzuia dirii isipate kutu. Hichi ndicho nilichokiona usiku ule, na ninaamini NENO la Bwana kuwa ni hili: Bwana anaenda kuendeleza haya katika roho mwaka huu hapa Marekani na itakuwa ni kwa mwendelezo wa William Branham. Dirii ya huyu mtu haitaendelea kushika kutu itatokea tena kwa mara nyingine Marekani katika huu mwaka, wamekwisha vikwa hawa matenda miujiza wapya ambao wataanza kutenda kazi mwaka huu.
Kama vile Mungu alivyoweka fimbo katika mkono wa Musa na kumwambia aende kufanya miujiza kule Misri, vivyo hivyo Mungu ataenda kufanya miujiza kupitia mikono ya hawa mashujaa ambao watatokea katika mwendelezo wa William Branham.
Branham alipewa maagizo mwaka 1946, Mungu alimwambia “miujiza itafanyika kupitia mikono yake”. Moja ya hii miujiza ilifanya kazi katika mkono wake wa kushoto na akapewa uwezo wa kupambanua roho hata kuweza kugundua uwepo wa magonjwa ya kipepo au udhaifu. Ishara ya pili aliyopewa ni kipawa cha ajabu cha maono aliweza kutambua siri za mioyo ya watu kwenye mimbari na kuwasaidia watu kuishinda roho ya kutokuamini (kitu ambacho kinazuia miujiza mingi isitendeke hapa Marekani). Mungu aliyafanya haya yote kupitia maisha ya huyu mtu na huduma yake, Hata hapa Marekani Mungu anaenda tena kufanya haya katika wakati wetu. Anaendeleza Nembo iliyokuwa kwa William Branham.
Bwana alisema msiwe na mitazamo hafifu juu ya uvuvio unaokuja wa Mungu, kwasababu ikiwa haupo katika sehemu ya huo uamsho, ni rahisi wewe kuingia katika hatari ya kumruhusu shetani aufanye moyo wako kuwa mgumu kama hautakuwa makini.
“Kuweni makini sana katika huu wakati mchunge laana mnazotoa katika midomo yenu juu ya huo uamsho unaokuja na kuuita kazi ya Mungu kuwa ni ya shetani. Kwasababu hata mafarisayo walisema maneno hayo hayo japo walikuwa wanauona uwepo dhahiri wa Mungu ukitembea katika dunia. Sio mara zote ni rahisi kufahamu kipi kinatoka kwa Mungu na kipi kinatoka kwa shetani kwahiyo usiwe mwepesi kuhukumu kimakosa huo uvuvi unaokuja. Jinyenyekezeni viongozi wangu, ” Bwana anasema ” Na kwa utulivu hukumuni kazi ya Mungu hichi kipindi kinachokuja, sana sana kama katika kazi za kanisa”
“Kwasababu mimi BWANA nitaijaribu mioyo ya viongozi wangu katika huu uvuvio unaokuja; kwasababu uvivio unaokuja unahitaji kuujaribu uongozi. Mimi BWANA nitafichua siri za mioyo yenu, na kuyakemea mawazo yenu kwa vitu ambavyo hamjawahi kusikia wala msivyovielewa. Lakini kama mkijinyenyekeza na kuwa wavumilivu katika hukumu zenu katika hichi kipindi, Mimi Bwana nitawafunulia kazi zangu ni zipi na za shetani ni zipi.
“Mimi Bwana nitawafanya mtambue tofauti kati ya mwanga na giza. Lakini hawatapewa ujuzi huo viongozi wote wenye majigambo na wenye kujikweza na kujidhani kuwa wana mamlaka yote. Hawatapewa watu wanaojiona wanajua vitu vya Mungu. Siri za Mungu hawatapewa watu wale waliowepesi kuhukumu bali wale wanyenyekevu ndio watakaopewa kuzijua hizi siri.
Katika huu uamsho unaokuja kutafunuliwa vitu vya ajabu, siri zilizojificha, na vitu ambavyo huwezi kuvitegemea, Mimi Bwana nitaleta watenda miujiza na sio tu waponyaji, hawa watafanya miujiza ambayo hamjawahi kusikia wala kuona. Lakini msiogope kwa hivyo vitu msivyovielewa, Kwa kuwa mimi Bwana nitakuwa pamoja nanyi nami nitawapa uwezo wa kutambua. Nitaenda kuwasaidia, viongozi wangu, Mitume wangu, Manabii wangu, Wachungaji wangu, lakini muwe wanyenyekevu na msiwe wepesi kuhukumu. Hili ndilo Neno nalowapeni leo kuwaanda ninyi katika huo uvuvio unaokuja.
Love & Blessings,
Stephen Powell,
Lion of Light Ministries.
Hivi karibuni ndugu Sadhu ambaye ni nabii mwenye asili ya India Bwana amekuwa akimtumia kutoa nabii nyingi na kuja kutimia ikiwemo ushindi wa Obama 2008 na Donald Trump 2016 , mafuriko na matetemeko ya ardhi, mengi pamoja na tetemeko litakalokuja kutokea Calfornia Marekani hivi karibuni, Alionyeshwa na Bwana Yesu Katika maono kwamba nguvu ya uvuvio iliyokuwepo juu ya nabii William Branham itarejeshwa tena ikiwa na nguvu mara saba”, kwa vijana wadogo ambao Mungu ataenda kuwanyanyua. Bwana alimwonyesha katika maono mengine mengi kuwa nguvu ambayo itaenda kuachiliwa katika huu wakati ukifika itakuwa ni kubwa sana na miujiza isiyokuwa ya kawaida itatendeka alisema. bofya hapa kutazama video .
Na kuna manabii wengi wameonyeshwa uamsho huo utakao kuja duniani, baadhi yao ni Rick jonyer, Kenneth Hagin, Neville Johnson, Vincent selvakumar n.k.
Kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno litathibitika. Katika neema tulionayo sasa hivi umejiwekaje tayari umepokea Roho Mtakatifu?. Jitahidi utubu ndugu injili zinazokuja huko mbele sio za kuwafanya watu watubu tena bali ni kwa ajili ya hukumu na ushuhuda kwa watu tu , wakati wa kutubu ndio sasa, wakati wa kupita katika mlango ulio mwembamba ndio sasa, Tafuta mahusiano yako binafsi na Mungu epuka kamba za madhehebu uwe tayari maana Bwana yupo mlangoni kurudi. Ndugu huu ni wakati wa kukaa chini na kumtafuta muumba wako, kalenda ya Mungu isikupite usilemewe na mambo ya ulimwengu huu, Bwana Yesu alisema tukeshe ili siku hiyo isitujie kama mwivi maana ndivyo itakavyoujia ulimwengu mzima. Kukesha sio kujizuia kulala bali ni kuwa macho rohoni, ujumbe wa Mungu unapokushukia uufahamu.
Luka 13:23-28″ Mtu mmoja akamwuliza, Je! Bwana, watu wanaookolewa ni wachache? Akawaambia, 24 Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze. 25 Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako; 26 ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu. 27 Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu. 28 Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje”.
Luka 13:23-28″ Mtu mmoja akamwuliza, Je! Bwana, watu wanaookolewa ni wachache? Akawaambia,
24 Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.
25 Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako;
26 ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu.
27 Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu.
28 Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje”.
HATUA ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUTUONGOZA
ACHENI MJUE YA KUWA MIMI NI MUNGU.
NINI MAANA YA HUU MSTARI “NIMEVIPIGA VITA VILIVYO VIZURI, MWENDO NIMEUMALIZA, IMANI NIMEILINDA”?
HISTORIA YA WILLIAM BRANHAM
Hii neema tulionayo leo itafika mwisho, kuna baadhi ya misemo imekuwa ikisemwa kuwa Mungu wa agano la kale leo hii hayupo, kama yupo zile ishara alizokuwa anatenda agano la kale ziko wapi leo?. Lakini SIKU YA BWANA inakuja ndugu usitamani uwepo! USITAMANI UWEPO! ni mambo ya kuogopesha ambayo usingetamani hata adui yako yampate, Mungu kuzuia ghadhabu yake ni kwa ajili yetu sisi tutubu lakini tusipotubu hukumu itatukuta.
vitasa saba
Kuna vitu vitatu vinavyokuja huko mbeleni, 1) DHIKI KUU, 2) SIKU YA BWANA, 3) ZIWA LA MOTO. Leo tutaitazama hii SIKU YA BWANA ni ipi, itakuja lini na itakuwa inamuhusu nani.
Kwa ufupi ndugu, DHIKI KUU itakuja na tunafahamu itakuwa kwa wakristo watakaokataa kuipokea ile alama/chapa ya mnyama. Hii itamuhusu mpingakristo akiwatesa wakristo wale waliokataa kuipokea ile chapa ya mnyama wale ambao hawakwenda kwenye unyakuo, Ambapo mwishoni mpinga-kristo atafanikiwa kuwaua kikatili wote wasioipokea chapa. Na hii dhiki itadumu kwa muda wa miaka mitatu na nusu, ni wakati wa kutisha sana unakuja mbeleni. Kwahiyo wakati wakristo wachache wanapitia dhiki kuu, wengine wote waliosalia watakuwa wanaendelea kujifurahisha na mambo yao ya dunia wakimfurahia mpinga kristo na utawala wake.
Sasa SIKU YA BWANA itaanza mara tu baada ya DHIKI KUU kuisha ambapo wale wanawali wapumbavu wote watakuwa wameshaondoka,(wameuliwa na mpingakristo) na unyakuo utakuwa umeshapita wakati huo, lakini hao waliobakia walioipokea chapa ya mnyama itawapasa waingie kwenye adhabu kali sana ya Mungu mwenyewe, Kwasababu wameshirikiana na mpinga kristo kuwaua watu wa Mungu na kwasababu wamekataa kumcha Mungu na kuzishika amri zake, ndugu Hii SIKU YA BWANA usitamani uwepo. Kumbuka haitakuwa jehanamu ya moto, bali itakuwa ni adhabu ya hapa hapa duniani.
maandiko yanasema:
Amosi 5:18 “Ole wenu! Ninyi mnaoitamani SIKU YA BWANA; kwani kuitamani siku ya Bwana? Ni giza, wala si nuru. 19 Ni kama mtu aliyemkimbia simba, akakutana na dubu; au aliingia katika nyumba akauegemeza mkono wake ukutani, nyoka akamwuma. 20 Je! Siku ya Bwana haitakuwa giza, wala si nuru? Naam, yenye giza sana, wala haina mwanga.“
Amosi 5:18 “Ole wenu! Ninyi mnaoitamani SIKU YA BWANA; kwani kuitamani siku ya Bwana? Ni giza, wala si nuru.
19 Ni kama mtu aliyemkimbia simba, akakutana na dubu; au aliingia katika nyumba akauegemeza mkono wake ukutani, nyoka akamwuma.
20 Je! Siku ya Bwana haitakuwa giza, wala si nuru? Naam, yenye giza sana, wala haina mwanga.“
Pia tukisoma…
Isaya 13:6″ Pigeni kelele za hofu; maana SIKU YA BWANA i karibu; itanyesha kama maangamizi yatokayo kwa Mwenyezi Mungu. 7 Kwa sababu hiyo mikono yote italegea, na moyo wa kila mtu utayeyuka. 8 Nao watafadhaika; watashikwa na utungu na maumivu; watakuwa na utungu kama mwanamke aliye karibu na kuzaa; watakodoleana macho; nyuso zao zitakuwa ni nyuso za moto. 9 Tazama, siku ya Bwana inakuja, siku kali, ya hasira na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake. 10 Maana nyota za mbinguni na matangamano havitatoa nuru yake; jua litatiwa giza wakati wa kucha kwake, na mwezi utaacha nuru yake isiangaze. 11 Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayaangusha chini majivuno yao walio wakali; 12 nitafanya wanadamu kuadimika kuliko dhahabu safi, na watu kuliko dhahabu ya Ofiri.”
Isaya 13:6″ Pigeni kelele za hofu; maana SIKU YA BWANA i karibu; itanyesha kama maangamizi yatokayo kwa Mwenyezi Mungu.
7 Kwa sababu hiyo mikono yote italegea, na moyo wa kila mtu utayeyuka.
8 Nao watafadhaika; watashikwa na utungu na maumivu; watakuwa na utungu kama mwanamke aliye karibu na kuzaa; watakodoleana macho; nyuso zao zitakuwa ni nyuso za moto.
9 Tazama, siku ya Bwana inakuja, siku kali, ya hasira na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake.
10 Maana nyota za mbinguni na matangamano havitatoa nuru yake; jua litatiwa giza wakati wa kucha kwake, na mwezi utaacha nuru yake isiangaze.
11 Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayaangusha chini majivuno yao walio wakali;
12 nitafanya wanadamu kuadimika kuliko dhahabu safi, na watu kuliko dhahabu ya Ofiri.”
Maandiko yanaposema SIKU YA BWANA hayamanishi ni siku kama siku moja, bali inamaanisha ni kipindi fulani cha WAKATI ambacho Bwana amekitenga kwa kusudi fulani. Kama maandiko yanavyotueleza ni kipindi ambacho kimetengwa cha GHADHABU NA HASIRA ya Mungu kulipiza kisasi kwa wanadamu wote wasiomcha Mungu.
Kipindi Hichi cha SIKU YA BWANA kitadumu kwa muda wa siku 75, Hizi zimepatikana kutoka katika kitabu cha Nabii Danieli 12:12, ambapo tunaona kipindi cha ile dhiki kuu kitadumu kwa muda wa siku 1260, na hapo zimeongezeka siku nyingine kutoka siku 1260 mpaka kufikia siku 1335, kwahiyo ukichukua hizo siku 1335-1260=75.
Kwahiyo hizi siku 75 zilizoongezwa ni mahususi kwa ajili ya BWANA kujilipizia kisasi kwa wanadamu wote waliosalia juu ya uso wa nchi.
Kabla ya SIKU hiyo ya BWANA kuanza Kutakuwa na baragumu saba zitakazopigwa kuitangulia , Hizi Zitabeba hukumu kwa watu wote, kama onyo watu watubu kumgeukia Mungu, Dunia itapigwa kwa mapigo mengi ya ajabu ukisoma Ufunuo 8 utaona hili, ikiwemo, theluthi moja ya maji kuwa damu, theluthi ya maji duniani kutiwa uchungu,theluthi ya mwezi na jua na nyota kupigwa,hebu tafakari kutakuwaje duniani wakati huo mchana kutakuwa kama jioni, giza litakuwa nene usiku na baridi kali sana, nzige wa ajabu watapandishwa kutoka kuzimu, maumivu yao ni kama ya kung’wata na nge, na meno yao ni kama meno ya simba, n.k.
Biblia inasema watu watakitamani kifo lakini hawatakiona, kumbuka hapo bado SIKU YA BWANA haijaanza huo ni mwanzo wa utungu tu, unatangaza hukumu KUU ya Bwana inayokuja mbeleni kwa urefu soma ufunuo sura ya 8 na ya 9. inaelezea haya mapigo ya baragumu saba za Mungu.
Lakini pamoja na mapigo yote hayo ya baragumu biblia inasema watu watakaokuwa juu ya uso wa nchi hawatatubu maovu yao kwasababu roho ya uovu imeshakaa juu yao kwa kuwa wote wamekwisha ipokea ile chapa ya mnyama neema ya Mungu imeondoka juu yao hawawezi kutubu tena.
Kwahiyo mara baada ya dhiki kuu ya mpinga-Kristo kuisha hapo tayari unyakuo ulishapita siku nyingi na wanawali wapumbavu kuuliwa, Sasa Hawa wanadamu waliobaki ndio watakaoingia katika mapigo ya vitasa Saba vya Mungu , katika hayo ghadhabu ya Mungu imetimia : Hebu tutazame vitasa hivi kimoja baada ya kingine.
Ufunuo 16:1 ” Nikasikia sauti kuu kutoka hekaluni, ikiwaambia wale malaika saba, Enendeni, mkavimimine vile vitasa saba vya ghadhabu ya Mungu juu ya nchi. 2 Akaenda huyo wa kwanza, akakimimina kitasa chake juu ya nchi; pakawa na JIPU BAYA, BOVU, juu ya wale watu wenye chapa ya huyo mnyama, na wale wenye kuisujudia sanamu yake.”
Ufunuo 16:1 ” Nikasikia sauti kuu kutoka hekaluni, ikiwaambia wale malaika saba, Enendeni, mkavimimine vile vitasa saba vya ghadhabu ya Mungu juu ya nchi.
2 Akaenda huyo wa kwanza, akakimimina kitasa chake juu ya nchi; pakawa na JIPU BAYA, BOVU, juu ya wale watu wenye chapa ya huyo mnyama, na wale wenye kuisujudia sanamu yake.”
Sasa adhabu hizi zitakuwa ni kwa Dunia nzima na sio theluthi tena ya dunia kama ilivyokuwa kwa zile baragumu saba. Majipu haya tunaona ni mfano wa yale yale waliopigwa wamisri, Kutakuwa na majipu ya ajabu usidhani ni haya ya kuwaida uliyoyazoea, biblia imeyaita ni MAJIPU MABOVU bado hajatokea kabisa duniani, huo ugonjwa bado haujazuka, Tuna magonjwa mengi ya hatari duniani lakini biblia haijayataja yote hayo, lakini ni huu ugonjwa wa MAJIPU tena jipu bovu ndio umetabiriwa utakuja, homa yake itakuwa sio kama hizi za kawaida tulizozizoea. Ndugu usitamani kuwepo huko wewe unayesema Mungu wa agano la kale haishi, siku hiyo utayaona haya wazi wazi.
Ufunuo 16:3 “Na huyo wa pili akakimimina kitasa chake juu ya bahari, ikawa damu kama damu ya mfu, na vitu vyote vyenye roho ya uhai katika bahari vikafa.” .
Duniani kutakuwa na harufu kama ya damu ya mtu aliyekwisha kufa, fikiria jambo hilo dunia nzima kutoa uvundo, hakutakuwa na kiumbe chochote baharini chakula kitapungua duniani, maji yataisha, shughuli za usafirishaji baharini nk. vitakwama, mvua zitaacha kunyesha duniani kutakuwa sio sehemu ya kuishi tena mwanadamu, taabu itaongezeka duniani, hofu kuu itawaingia watu wakitazama ni mambo gani haya yameipata dunia?.. lakini bado mapigo yatakuwa yanaendelea,
Ufunuo 16:4-7 ” Na huyo wa tatu akakimimina kitasa chake juu ya mito na chemchemi za maji; zikawa damu. 5 Nami nikamsikia malaika wa maji akisema, Wewe u mwenye haki, uliyeko na uliyekuwako, Mtakatifu, kwa kuwa umehukumu hivi; 6 kwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu na ya manabii, nawe umewapa damu wainywe; nao wamestahili. 7 Nikaisikia hiyo madhabahu ikisema, Naam, Bwana Mungu Mwenyezi, ni za kweli, na za haki, hukumu zako. “
Baada ya bahari kugeuzwa kuwa damu ya mizoga, watu wote tunajua wangekimbilia kutafuta maji katika mito na kwenye chemchemi za maji, kutokana na kiu kikali, lakini Bwana atayapiga pia maji ya mitoni na chemchemi, wakati huo fedha itakuwa haifanyi kazi tena, Mtu tajiri atakuwa ni mwenye kikombe cha maji safi mkononi mwake na sio fedha, Kwahiyo Bwana atawalazimisha kuyanywa hayo maji ya DAMU kwasababu walishirikiana na yule mnyama kumwaga damu ya watakatifu wa Mungu, hivyo nao Bwana amewapa wainywe. Na kwasababu ya kiu kali watakunywa hiyo damu, na wanadamu wengi wataangamia na kufa kwa pigo hilo.
Ufunuo 16:8-9 “Na huyo wa nne akakimimina kitasa chake juu ya jua, nalo likapewa kuwaunguza wanadamu kwa moto. 9 Wanadamu wakaunguzwa maunguzo makubwa, nao wakalitukana jina la Mungu aliye na mamlaka juu ya mapigo hayo; wala hawakutubu wala kumpa utukufu.”
Baada ya pigo la maji kuwa damu, jua litashushwa chini, maunguzo yatakuwa ni makubwa sana, joto litaongezeka duniani kwa nyuzi joto kubwa kuliko kiwango cha kawaida. Mimea yote itakauka, dunia itafanana na jangwa ndani ya muda mfupi sana, jaribu kutafakari jipu linapigwa na jua kali halafu hakuna maji hata kidogo ya kujipooza,ni dhiki kiasi gani? ni mambo ambayo huwezi dhania yatatokea lakini yapo mbioni kutokea. Lakini pamoja na hayo mapigo yote biblia inasema watu watamtukana Mungu hawatatubu. Mfano tu wa kizazi chetu hichi watu wanapopatwa na majanga badala wageuke na kumuuliza Mungu ni kwanini na kutubu, wao wanalaani.
Ufunuo 16:10-11 “Na huyo wa tano akakimimina kitasa chake juu ya kiti cha enzi cha yule mnyama; ufalme wake ukatiwa giza; wakatafuna ndimi zao kwa sababu ya maumivu, 11 wakamtukana Mungu wa mbingu kwa sababu ya maumivu yao, na kwa sababu ya majipu yao; wala hawakuyatubia matendo yao. “
Sasa pigo hili linamuhusu sana sana yule mnyama aliyewakosesha wanadamu wote kuipokea ile chapa, mahali kiti chake cha enzi kilipo ambapo ni VATICAN, Roma, Mungu ataachilia laana kwa mataifa ya ulaya ambayo ndio zile pembe kumi, zitamchukia na kumwangamiza yule mwanamke kahaba (Kanisa Katholiki) ambalo makao yake makuu ni VATICAN.
Hii ni kutokana na kwamba yale mataifa ambayo yalimtumaini mpinga kristo ayaletee amani duniani, hayajaletewa zaidi ya yote mpingakristo (PAPA) ameiongezea dunia matatizo hivyo basi watamchukia na kumwangamiza, tangu wakati huo utawala wa Roma, pamoja na mpinga kristo (PAPA) na Vatican yake hawatakuwepo tena ufalme wao umekwishatiwa giza.
Soma
ufunuo 17:16″ Na zile pembe kumi ulizoziona, na huyo mnyama, hao watamchukia yule kahaba, nao watamfanya kuwa mkiwa na uchi, watamla nyama yake, watamteketeza kabisa kwa moto. ”
Ufunuo 16:12 “Na huyo wa sita akakimimina kitasa chake juu ya mto ule mkubwa Frati; maji yake yakakauka, ili njia itengenezwe kwa wafalme watokao katika maawio ya jua. 13 Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo. 14 Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi. 15 (Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.) 16 Wakawakusanya hata mahali paitwapo kwa Kiebrania, Har-Magedoni.”
Ufunuo 16:12 “Na huyo wa sita akakimimina kitasa chake juu ya mto ule mkubwa Frati; maji yake yakakauka, ili njia itengenezwe kwa wafalme watokao katika maawio ya jua.
13 Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo.
14 Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.
15 (Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.)
16 Wakawakusanya hata mahali paitwapo kwa Kiebrania, Har-Magedoni.”
Kitasa hichi kunazungumzia ile vita kuu ya HAR MAGEDONI ambayo itakuwa ni vita kati ya Mungu mwenyezi akilipigania taifa la Izraeli dhidi ya wafalme wote wa dunia. karibu kila taifa litaunga mkono vita hii wakiongozwa na mataifa kutoka mawio ya jua. Haya mataifa ya mawio ya jua ni mataifa ya mashariki, nayo ni CHINA,JAPAN, KOREA n,k. Wakati huo Vatican itakuwa haipo, Marekani itakuwa haipo, Urusi itakuwa haipo yatatoweshwa katika vita vilivyoelezwa katika ezekieli 38 & 39,
Kwahiyo zile roho chafu ambazo zilikuwa zinaendesha Vatican na Marekani zitahamia kwenye haya mataifa ya mashariki yaliyosalia kwa ajili ya vita dhidi ya Izraeli. Wakati huo ndio Bwana YESU atakapotokea kuwapigania watu wake Izraeli. Ndugu wakati huo dunia itakuwa mfano wa sayari ya Zebaki, hakutakuwa na maji, chakula, magonjwa, joto litakuwa juu sana,maji yote damu, machafuko pamoja na vita, usitamani ndugu yangu uwepo nakuombea Mungu usiwepo itakuwa ni vilio na kusaga meno, siku hiyo watu watatamani siku hizi za neema tulizonazo leo hawataziona.
Ambacho ndio hasaa kinaizungumzia ile siku ya Bwana..
Ufunuo 16:17-21 ” Na huyo wa saba akakimimina kitasa chake juu ya anga. Sauti kuu ikatoka katika hekalu, katika kile kiti cha enzi, ikisema, Imekwisha kuwa. 18 Pakawa na umeme na sauti na radi; na palikuwa na tetemeko la nchi kubwa, ambalo tangu wanadamu kuwako juu ya nchi hapakuwa namna ile, jinsi lilivyokuwa kubwa tetemeko hilo. 19 Na mji ule mkuu ukagawanyikana mafungu matatu, na miji ya mataifa ikaanguka; na Babeli ule mkuu ukakumbukwa mbele za Mungu, kupewa kikombe cha mvinyo ya ghadhabu ya hasira yake. 20 Kila kisiwa kikakimbia, wala milima haikuonekana tena. 21 Na mvua ya mawe kubwa sana, ya mawe mazito kama talanta, ikashuka kutoka mbinguni juu ya wanadamu. Wanadamu wakamtukana Mungu kwa sababu ya lile pigo la mvua ya mawe; kwa maana pigo lake ni kubwa mno.”
Ufunuo 16:17-21 ” Na huyo wa saba akakimimina kitasa chake juu ya anga. Sauti kuu ikatoka katika hekalu, katika kile kiti cha enzi, ikisema, Imekwisha kuwa.
18 Pakawa na umeme na sauti na radi; na palikuwa na tetemeko la nchi kubwa, ambalo tangu wanadamu kuwako juu ya nchi hapakuwa namna ile, jinsi lilivyokuwa kubwa tetemeko hilo.
19 Na mji ule mkuu ukagawanyikana mafungu matatu, na miji ya mataifa ikaanguka; na Babeli ule mkuu ukakumbukwa mbele za Mungu, kupewa kikombe cha mvinyo ya ghadhabu ya hasira yake.
20 Kila kisiwa kikakimbia, wala milima haikuonekana tena.
21 Na mvua ya mawe kubwa sana, ya mawe mazito kama talanta, ikashuka kutoka mbinguni juu ya wanadamu. Wanadamu wakamtukana Mungu kwa sababu ya lile pigo la mvua ya mawe; kwa maana pigo lake ni kubwa mno.”
Hili ni pigo la mwisho, na katika hili ghadhabu ya Mungu imetimia tukisoma pale muhuri wa sita ulipofunguliwa ulitoa picha halisi jinsi hii siku itakavyokuwa soma Mathayo 24:30-31 na pia Ufunuo 6:12-17
Ufunuo 6:12-17 ” Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu, 13 na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi. 14 Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake. 15 Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima, 16 wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo. 17 Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?”
Ufunuo 6:12-17 ” Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu,
13 na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi.
14 Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake.
15 Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima,
16 wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo.
17 Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?”
Pigo la saba la mwisho kama tunavyosoma ni baya kuliko yote yaliyotangulia maana jua linaondolewa, mwezi utakuwa damu, nyota zitatoweka, unaweza kuona kutakuwa na giza kiasi gani duniani, na baridi kiasi gani,litakuwaa ni giza zito sana, hakutakuwa na chanzo chochote cha umeme, shughuli zote za kimaendeleo zilishamalizwa katika mapigo yaliyotanguliwa, hadi kufikia hapa watu wachache sana watakuwa wamesalia duniani, kumbuka hapo bado ziwa la moto linasubiri watu, Hichi ni kisasi cha hapa hapa duniani.
Mvua ya mawe kubwa sana itanyesha, mawe kama talanta,(talanta 1 ni kama kg 34), Huwezi kujificha kwenye nyumba yako ya bati au ya kigae, kg 34 ni uzani mkubwa sana itaambana na tetemeko ambalo halijawahi kutokea, kiasi cha kwamba visiwa vitahama, kisiwa cha zanzibar kitapotea, Milima itatapika volkano, kumbuka hayo yote yatafanyika katikati ya giza nene, hakuna mawasiliano. hapo hakuna mfalme wala mtumwa, raisi wala mwananchi wote waliosalia watatamani wafe kuliko kuishi, watatamani milima iwaangukie waikwepe ghadhabu ya Mungu, Hapo ndipo itakapoonekana ishara ya mwana wa Adamu mawinguni.
Mathayo 24:29 “Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika; 30 ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi. “
Rafiki haya mambo ni kweli yatatokea, ndivyo yatakavyokuja kuupata ulimwengu na dalili zote zinaonyesha kuwa yatatokea katika kizazi chetu tunachoishi mimi na wewe, Bwana amekwisha kutuonya mbele, Nia yake ni sisi tuiepuke hiyo ghadhabu na ndio maana kuna mahali alisema alipokuwa katikati ya kitasa cha sita (Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake). Kwahiyo ametuonya tukeshe na kuyatunza mavazi yetu, maana hii siku ya ghadhabu itakuja ghafla.
Ndugu kimbia injili ambazo zinakufanya usifikiri hatma ya maisha yako ya milele badala yake inakupeleka kutazama mambo ya ulimwengu huu. Hii ni roho ya shetani inawapumbaza wengi wafikiri mambo hayo yatakuja kutokea baada ya miaka 2000 mbele, usidanganyike ni uongo wa shetani, ndugu dalili zote zinaonyesha, unabii wote umetimia kwamba tunaishi katika kizazi cha hatari sana.
Chunguza maisha yako angali neema ipo, mambo hayatakuwa hivi siku zote, pale mlango wa neema utakapofungwa kutakuwa hakuna kurudi nyuma itakuwa ni vilio na maombolezo, kimbilia kalvari sasa tubu dhambi zako, uoshwe kwa damu ya Yesu, na Upokee Roho Mtakatifu kabla ya huo wakati kufika. Kumbuka adhabu ya hii SIKU YA BWANA, sio jehanamu ya moto, baada ya mapigo hayo ndipo ziwa la moto ziwa la moto litafuata.
Ikiwa unataka kumpa Bwana Yesu maisha yako na kugeuka leo tubu mwenyewe moyoni mwako au fuatiliza sala hii kwa imani:
Sema:
“Bwana Yesu, Leo hii nasogea mbele zako nikiwa mwenye dhambi, natubu makosa yangu yote niliyokukosea, naomba unisamehe, nimeamua kugeuka leo, nisaidie Bwana Yesu, neema yako iwe juu yangu, nikuishie wewe, siku zote za maisha yangu, asante Bwana Yesu kwa kunisikia na kunisamehe. AMEN! “.
Baada ya kutubu unahitaji kubatizwa, Hivyo basi tafuta kanisa linalobatiza ubatizo sahihi nao ni kwa kuzamishwa kwenye maji mengi na ni kwa jina la YESU KRISTO, Kwa kufanya hivyo Bwana atakupa kipawa cha Roho Mtakatifu na utakuwa umekamilisha wokovu wako.
MUNGU AKUBARIKI.
Kwa msaada zaidi, wa kanisa, au mafundisho, au ushauri, piga namba hizi
+255693036618/ +25578901312
KIKOMBE CHA GHADHABU YA MUNGU KINAJAA…TUBU UMGEUKIE MUNGU
NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE.
JE! SISI NI WAFALME NA MAKUHANI KWA NAMNA GANI?
PETRO ALIAMBIWA NA BWANA YESU UKIONGOKA WAIMARISHE NA NDUGU ZAKO. JE! KUONGOKA MAANA YAKE NINI?