Swali: Kutawa kwa Elisabeti miezi mitano maana yake nini?
Jibu: Turejee..
Luka 1:24 “Hata baada ya siku zile mkewe Elisabeti alichukua mimba AKATAWA miezi mitano, akisema, 25 Hivi ndivyo alivyonitendea Bwana katika siku zile alizoniangalia ili kuniondolea aibu yangu mbele ya watu”.
Luka 1:24 “Hata baada ya siku zile mkewe Elisabeti alichukua mimba AKATAWA miezi mitano, akisema,
25 Hivi ndivyo alivyonitendea Bwana katika siku zile alizoniangalia ili kuniondolea aibu yangu mbele ya watu”.
Tafsiri ya “Kutawa” ni “kujitenga”.. hivyo Kiswahili kingine cha mstari huo ni hiki… “Hata baada ya siku zile mkewe Elisabeti alichukua mimba AKAJITENGA miezi mitano”
Hivyo Elisabeti alijitenga na jamii ya watu pengine kwasababu za kumshukuru MUNGU kwa muujiza aliomtendea wa kubeba mimba uzeeni, au kwa nia ya kuepusha uadui kutoka kwa watu ambao ungetokana na wivu, au pengine kwasababu nyingine za kupumzika na kumtafakari MUNGU kwa faragha!. Mojawapo ya hizo au zote zaweza kuwa sababu za kujitenga kwake.
Na tunaona lilikuwa ni jambo jema kwa Elisabeti kwani baadaye alipokutana na Mariamu ndugu yangu, alijazwa Roho Mtakatifu na kuzungumza kiusahihi habari za Mariamu na Bwana Yesu aliye tumboni mwa Mariamu.
Hiyo inatufundisha nini?
Si kila Baraka kutoka kwa MUNGU inapokuja ni wakati wa kutangaza na kushuhudia wakati huo huo, wakati mwingine ni vizuri kujitenga/kutawa kwa muda ili kutumia kumshukuru MUNGU, na kuomba ulinzi wa Baraka ile,..kuwahi kutangaza Baraka za MUNGU au mlango MUNGU aliokufungulia kabla ya kupata utulivu ni hatari kwako na kwa utakaoenda kuwaambia.
Hivyo ni vizuri kutokuwa mwepesi wa kuzungumza bali ni vizuri kuwa mwepesi wa kupata faragha na MUNGU na kutafakari fadhili zake kabla ya kuzungumza au kushuhudia.
Bwana atusaidie.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
MARIAMU AKUTANA NA ELISABETI.
Yohana aliwatiaje waasi akili za wenye haki? (Luka 1:17)
KWA VILE ALIVYOKUWA MTU WA HAKI.
JE BIKIRA MARIAMU ALIZAA WATOTO WENGINE?
UWEZA WA MUNGU UNAONEKANA WAPI?
Print this post
Jibu: Turejee kuanzia ule mstari wa 11..
Luka 1:11 “Akatokewa na malaika wa Bwana, amesimama upande wa kuume wa madhabahu ya kufukizia. 12 Zakaria alipomwona alifadhaika, hofu ikamwingia. 13 Lakini yule malaika akamwambia, Usiogope, Zakaria, maana dua yako imesikiwa, na mkeo Elisabeti atakuzalia mtoto mwanamume, na jina lake utamwita Yohana. 14 Nawe utakuwa na furaha na shangwe, na watu wengi watakufurahia kuzaliwa kwake. 15 Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za Bwana; hatakunywa divai wala kileo; naye atajazwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye. 16 Na wengi katika Waisraeli atawarejeza kwa Bwana Mungu wao. 17 Naye atatangulia mbele zake katika roho ya Eliya, na nguvu zake, ili kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto, NA KUWATILIA WAASI AKILI ZA WENYE HAKI, NA KUMWEKEA BWANA TAYARI WATU WALIOTENGENEZWA”.
Luka 1:11 “Akatokewa na malaika wa Bwana, amesimama upande wa kuume wa madhabahu ya kufukizia.
12 Zakaria alipomwona alifadhaika, hofu ikamwingia.
13 Lakini yule malaika akamwambia, Usiogope, Zakaria, maana dua yako imesikiwa, na mkeo Elisabeti atakuzalia mtoto mwanamume, na jina lake utamwita Yohana.
14 Nawe utakuwa na furaha na shangwe, na watu wengi watakufurahia kuzaliwa kwake.
15 Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za Bwana; hatakunywa divai wala kileo; naye atajazwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye.
16 Na wengi katika Waisraeli atawarejeza kwa Bwana Mungu wao.
17 Naye atatangulia mbele zake katika roho ya Eliya, na nguvu zake, ili kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto, NA KUWATILIA WAASI AKILI ZA WENYE HAKI, NA KUMWEKEA BWANA TAYARI WATU WALIOTENGENEZWA”.
Haya ni maneno ya Malaikaa aliyokuwa anamwambia mzee Zakaria kuhusu mtoto atakayezaliwa (ambaye ni Yohana Mbatizaji), kwamba mtoto huyo atajazwa Roho Mtakatifu tangu akiwa tumboni, na atatembea na roho (yaani huduma) ya Eliya, lakini pia atawatejeza wengi wa Mungu, na kumwekea Bwana tayari watu waliotengenezwa, na zaidi sana KUWATILIA WAASI AKILI ZA WENYE HAKI!
Sasa kabla ya kutazama ni kwa namna gani Yohana Mbatizaji “aliwatilia waasi akili za wenye haki” hebu kwanza tutazame alimwekeaje Bwana tayari watu waliotengenezwa..
Ikumbukwe kuwa baadhi ya wanafunzi wa Bwana YESU kabla ya kuwa wanafunzi wa Bwana Yesu walikuwa kwanza wanafunzi wa Yohana mbatizaji.. baadhi ya hao walikuwa ni Andrea na nduguye Petro (Soma Yohana 1:35-41).
Kwahiyo akina Andrea na wengine ni watu waliotengenezwa kiroho kabla ya kuanza kutembea na Bwana, hivyo kwao haikuwa ngumu kumwamini Bwana au kumwelewa.. (hiyo ndio maana ya kumwekea tayari Bwana watu waliotengenezwa)
Sasa terejee sehemu ya Pili ambayo ni “Kuwatilia waasi akili za wenye Haki”
Hapa kuna mambo mawili, 1. Waasi, 2.Akili za wenye haki.
Waasi wanaozungumziwa hapo ni Wana wa Israeli ambao wameiasi sheria ya MUNGU na kumwacha Mungu (Soma 2Nyakati 29:6), Na anaposema “akili za wenye haki”.. maana yake zipo “akili za wasio haki” maana yake akili za watu wasiomjua MUNGU, Lakini akili za watu wanaomjua MUNGU/wenye haki ni zile zinazomfanya Mtu amwangalie Muumba wake katika jicho la usafi na utakatifu, ndio zile alizowaambia katika Luka 3:8-14..
Luka 3:7 “Basi, aliwaambia makutano ya wale waliomwendea ili awabatize, Enyi wazao wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja? 8 Basi, toeni matunda yapatanayo na toba; wala msianze kusema mioyoni mwenu, Tunaye baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba katika mawe haya Mungu aweza kumwinulia Ibrahimu watoto. 9 Na sasa hivi shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni. 10 Makutano wakamwuliza, Tufanye nini basi? 11 Akawajibu akiwaambia, Mwenye kanzu mbili na ampe asiye na kanzu; na mwenye vyakula na afanye vivyo hivyo. 12 Watoza ushuru nao wakaja kubatizwa, wakamwuliza, Mwalimu, tufanye nini sisi? 13 Akawaambia, Msitoze kitu zaidi kuliko mlivyoamriwa. 14 Askari nao wakamwuliza, wakisema, Sisi nasi tufanye nini? Akawaambia, Msidhulumu mtu, wala msishitaki kwa uongo; tena mtoshewe na mshahara wenu”.
Luka 3:7 “Basi, aliwaambia makutano ya wale waliomwendea ili awabatize, Enyi wazao wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja?
8 Basi, toeni matunda yapatanayo na toba; wala msianze kusema mioyoni mwenu, Tunaye baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba katika mawe haya Mungu aweza kumwinulia Ibrahimu watoto.
9 Na sasa hivi shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni.
10 Makutano wakamwuliza, Tufanye nini basi?
11 Akawajibu akiwaambia, Mwenye kanzu mbili na ampe asiye na kanzu; na mwenye vyakula na afanye vivyo hivyo.
12 Watoza ushuru nao wakaja kubatizwa, wakamwuliza, Mwalimu, tufanye nini sisi?
13 Akawaambia, Msitoze kitu zaidi kuliko mlivyoamriwa.
14 Askari nao wakamwuliza, wakisema, Sisi nasi tufanye nini? Akawaambia, Msidhulumu mtu, wala msishitaki kwa uongo; tena mtoshewe na mshahara wenu”.
Akili za wasio haki, zinafundisha DINI tu, kwamba wao ni wayahudi wanaye Baba ambaye ni Ibrahimu, kwahiyo ni uzao mteule, lakini akili za wenye haki zinafundisha kwamba pamoja na kwamba wanaye Baba ambaye ni Ibrahimu bado wanapaswa kujitakasa maisha yao ili wakubaliwe na MUNGU, kuwa tu mwana wa Ibrahimu haitoshi, inahitaji matendo yanayoendana na hiyo Imani.
Hivyo wengi walipojua hilo walitubu na kumrudia Mungu kwa matendo yao.
Hali kadhalika hata leo tunahitaji hizi akili za wenye haki.. hatuwezi kusema sisi ni wakristo wenye madhehebu makubwa, na majina mazuri ya kibiblia halafu matendo yetu hayaendani na asili ya imani yetu, ni lazima tupate akili za wenye haki.
Je kuna Yohana wangapi katika biblia?
Je biblia inajichanganya kwa habari za Yohana kuwa Eliya?
YOHANA MBATIZAJI
Nini maana ya “SAA INAKUJA” na “SASA IPO” (Yohana 4:23).
MGAWANYIKO WA ISHARA ZA UJIO WA BWANA YESU KRISTO.
WhatsApp
Mwanzo 3:15
[15]nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa..
Kitu pekee Ambacho kilitabiriwa kuweza kuvunja vichwa vya majoka(shetani), ni uzao wa mwanamke tu. Aliyetabiriwa kwenye (Mwanzo 3:15)
Uzao huu wa mwanamke ni Yesu Kristo.. kwasababu ni yeye tu pekee ndiye aliyezaliwa Bila mwanamume, sisi wote ni uzao wa mwanamume…kwasababu mbegu yetu imetoka kwa Baba zetu, lakini Kristo ni mbegu iliyoshuka Kutoka mbinguni, ndio maana hapo anatajwa Kama uzao wa mwanamke.
Yeye kwa ushindi alioupata dhidi ya nguvu za giza kwa kufufuka kwake kutoka kwa wafu na kupaa mbinguni..ni pigo Kubwa sana kwa shetani, ambalo lilimlenga moja kwa moja katika kichwa chake.
Kwasababu kwa njia hiyo wanadamu tumevuka kutoka mautini kwenda uzimani…
Lakini habari njema ni kuwa yeyote amwaminiye, anakuwa sehemu ya uzao huo kwa imani. Na hivyo anapokea mamlaka ile ile ya kuvunja mafuvu ya majoka…mpaka ufalme wa giza kutokomea kabisa katika uso wa ulimwengu..
Wagalatia 3:29
[29]Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.
Luka 10:19
[19]Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.
Kumbuka uwezo huu, hakuna uzao mwingine wowote unaoweza kumuharibu shetani, waafrika hawawezi, wazungu hawawezi, wachina hawawezi, waarabu hawawezi, ukoo wa kiyahudi hauwezi, familia za kichifu, haiwezi, wanadamu wote hawawezi kuponda majoka, hata waungane kwa vifaru vyao na makombora ya nyuklia, bado hawawezi kinyume chake wao ndio watafanyika chakula cha hao majoka.Ni uzao mmoja tu wa Yesu Kristo ndio wenye nguvu hizo..
Swali ni je! Tunapondaje vichwa vya majoka.
Ni kwa kuendelea kuhubiri. Ukikaa tu bila kushuhudia habari za Kristo kwa wenye dhambi, kukaa bila kujishughulisha na shamba la Bwana..Fahamu kuwa ‘mabuti’ yako uliyopewa huko miguuni huyatendei Haki..yapo tu!
Unamridhia shetani, unafurahishwa na uwepo wake shambani mwa Bwana, ndugu njia pekee inayomdosha shetani kwa wepesi ni wewe kukutana na mwenye dhambi mmoja na kumshuhudia habari za wokovu.
Mitume walipoenda kuhubiri baada ya kutumwa na Yesu, waliporudi na ushindi, Yesu aliwaambia nalimwona shetani akianguka kutoka mbinguni kama umeme..
Luka 10:18
[18]Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme.
Simama tumia mabuti yako vizuri, endeleza kuponda, ponda kweli kweli, haribu kisawasawa, kwa njia ya injili.
Sio kwa kuimba “nakuponda shetani” au
Kusema “toka shetani” bali kwa injili
Kuponda kwingine ni maombi na kuishi maisha ya utakatifu, huku nako kunahubiri injili ya Kristo na hivyo shetani anaumizwa vibaya sana.
Amka tumia buti zako, kila kichaka katika shamba la Bwana ambacho majoka yamejificha Ni kwenda kuponda tu, mpaka habari njema za ufalme zifike ulimwenguni kote.
Bwana awe nawe.
Amen.
IHUBIRI INJILI, KILA MAHALI KWASABABU AKUZAYE NI MUNGU.
INJILI NI UWEZA WA MUNGU, UULETAO WOKOVU.
MBONA MMESIMAMA HAPA MCHANA KUTWA BILA KAZI?
Ni vema kufahamu Kanisa ni nini?
Kanisa sio jengo, au mahali, bali ni watu, walioitwa Na Mungu, waliookolewa wanakusanyika pamoja katika nia moja kumwabudu na kumtumikia yeye.
Hivyo watu hawa wanaweza kukusanyika maeneo yaliyo rasmi, lakini pia maeneo yasiyo rasmi kwa shughuli zao za kiibada..maadamu tu wamekidhi vigezo hivyo vya kiroho.
Kanisa la kwanza lilikusanyika Hekaluni (mahali rasmi kwa shughuli za kiibada tu). Lakini pia lilikusanyika majumbani…wakati mwingi pembezoni Mwa mito na kwenye madarasa..
Matendo ya Mitume 2:46
[46]Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe,
Matendo ya Mitume 5:42
[42]Na kila siku, ndani ya hekalu na nyumbani mwao, hawakuacha kufundisha na kuhubiri habari njema za Yesu kwamba ni Kristo.
Kama tunavyojua majumbani mahali ambapo, pana shughuli nyingi wakimaliza ibada huwenda sherehe zinafanyika hapo, au vikao vya kijamii, lakini hilo halikuwazuia kutimiza makusudi ya Mungu yaliyoyakusudia.
Hivyo yaweza kuwa ni sahihi endapo, hakuna mahali rasmi bado, ibada zinaweza kufanyika kwenye majengo ya shule, kwenye mabwalo, kwenye kumbi,.viwanjani, hata chini ya miti maadamu tu umoja huo upo na nia ni Kristo..hata hivyo yapo makanisa makubwa na yamefanikiwa lakini bado hayana maeneo yao rasmi ya kukutanikia…lakini kanisa Limesimama.
Mambo tu ya kuzingatia, ni nidhani yenu, adabu na utulivu wa mazingira ya kiroho kwa wakati huo,..ikiwa haya yapo hapo Mnapokusanyikia basi Mungu yupo nanyi..wala si dhambi.
Lakini ni busara na vema zaidi kanisa likatafuta eneo rasmi la kukusanyikia litakalokuwa ni kwa shughuli zao tu za kiibada.
Shalom.
Nini maana ya kumwabudu Mungu katika Roho na kweli?
MAISHA YA UVUGUVUGU, YANAMFANYA MUNGU AUMWE.
UNAWAZA NINI SASA, JUU YA UFALME WA MBINGUNI?
1Petro 1:12 Mwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa.
Siku ya kujiliwa ni wakati ambao, Mungu anashuka ulimwenguni, aidha kwa kuokoa au kuhukumu.
Zote mbili ni siku za kujiliwa.
Kwa mfano kwa lengo la kuokoa. Upo wakati ambao neema ya Mungu humjia mtu, au taifa, na hivyo wakati huo mara nyingi uamsho mkubwa huwa unapita, Kwamfano, kipindi cha Kristo, kilikuwa ni kipindi maalumu cha Israeli kujiliwa lakini hawakukubali ..isipokuwa wachache..(Luka 19:41-44)
Lakini kwa lengo la hukumu ni siku ambayo kila mmoja wetu atahukumiwa kulingana na matendo yake.
Hivyo tukirudi kwenye 1 Petro 1:12, inayosema ‘Mwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa’.
Maana yake, matendo mema ya mwamini, hupelekea watu kuupokea wokovu na kumtukuza Mungu,siku neema yao inapowafikia, kwamfano wapo watu ambapo kwa kukuangalia, kwa kipindi kirefu, siku ya kujiliwa inapowafikia inakuwa ni rahisi kuamini na kumtukuza Mungu, kwasababu walishawahi kuona watu waliokoka walivyo na sifa zao njema, mfano upendo, amani, uadilifu..Lakini ukiwa na mwenendo mbovu, siku yao ya kujiliwa inapowafikia, wakikumbuka mwenendo mbovu waliouna kwako , ni ngumu sana kumtukuza Mungu,
Ndicho ambacho mtume Petro alikuwa anakieleza hata mbeleni kidogo, kuhusiana na Wanandoa, kwa upande wa wanawake, akasema, ikiwa mtu ana mume asiyeamini, anao uwezo wa kumvuta ndani ya Kristo kwa mwenendo wake tu.. (1Petro 3:1).
Kwa ufupi ni kuwa mwenendo wako mwema hulainisha njia ya neema ya Kristo Kutenda kazi vema juu ya mtu.
Mungu akubariki.
Biblia inamaana gani inaposema “Mungu wa neema yote” (1Petro 5:10)
Nini maana ya ombeni kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi wala siku ya sabato?.
MILANGO YA KUZIMU.
Isaya 61: 1-3
1 Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta …3 kuwaagizia hao waliao katika Sayuni, WAPEWE TAJI YA MAUA BADALA YA MAJIVU, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito; wapate kuitwa miti ya haki, iliyopandwa na Bwana, ili atukuzwe.
Kitu kikishachomwa na kuteketea kabisa, kinachosalia cha mwisho kabisa huwa ni majivu. Majivu hayana thamani yoyote, ni vumbi jembamba, ambalo likikanywagwa, hutoweka kabisa.
Hivyo zipo nyakati ambazo, watu wanakuwa kama majivu mbele ya macho yao wenyewe, au kwa wengine. Yaani Kila kitu kimekufa na kuteketea kabisa, yale maono aliyokuwa nayo yamefutika, wengine afya zao zimekuwa jivu,hawana matumaini ya kupona tena, wengine maisha yamevurugika, akiangalia muda aliochezea moyo unapoa kabisa, wengine mahusiano yao yametafunwa, haoni kuendelea mbele.. Rohoni akijiangalia ni jivu tu, kila mahali ni jivu hajasaliwa na chochote, isipokuwa kukata tamaa na kupotea kabisa..
Ndio maana katika enzi za biblia mtu aliyekuwa katika maombolezo Makali, alijimwagia majivu mwilini kama ishara kuwa umepukutika kabisa..Mfano wa hawa ni Ayubu na Mordekai (Ayubu 2:8, Esta 4:1 )
Lakini Mungu afufuaye matumaini, alitoa unabii huu juu ya mwanawe atakayekuja kuukomboa ulimwengu, akasema..
Amemtia mafuta, “ili awape watu wake taji ya maua badala ya majivu..”
Tafsiri yake, ni kuwa sio tu atamwondoa kwenye majivu na kumwacha, Hapana, bali anambadilishia na kumpa taji la maua.
Maua huwakilisha heshima, cheo, hadhi, baraka, afya.
Hivyo haijalishi utakuwa katika hali isiyoeleweka kiasi gani, Yupo Yesu wa kukuondoa majivuni na kukuvika maua, ‘Majivu yako leo ndio maua yako baadaye, lakini ikiwa tu utakuwa ndani ya Kristo’.
Usihofu wala usiogope, wala usikate tamaa..Magonjwa hugeuzwa afya.
Yusufu alikuwa majivu gerezani, lakini Mungu alimfanya maua katika kiti cha Farao. Petro alikuwa jivu kwa kumkana Bwana wake, lakini ndiye alikuwa mjenzi wa kanisa la Kristo. Ruthu alikuwa mjane kwa kufiwa na mumewe, lakini Bwana alimwekwa kama mama wa uzao wa kifalme, Haijalishi hutafaa kwa jinsi gani leo, Kristo yupo kukugeuza, na kukuondoa majivuni.
Lakini hii inahitaji kumpokea na kuendelea kuishi ndani yake. Je upo tayari kuyakabidhi leo maisha yako kwake?
Kwanini mkono wa Musa uingie ukoma?
UMESAMEHEWA DHAMBI ZAKO.
Siku moja Yesu alipokuwa anahubiri katika nyumba fulani, watu wengi walikusanyika mahali pale, na ghafla wakamletea mtu aliyepooza mwili mzima hawezi kufanya lolote, wakamweka Mbele yake ili amponye. Lakini tunaona mwitikio wa Yesu ulikuwa ni tofauti na matarajio yao. Bwana Yesu hakumwekea mikono na kumwambia simama uende, bali alimwambia..
Rafiki, umesamehewa dhambi zako.
Luka 5:17-20
[17]Ikawa siku zile mojawapo alikuwa akifundisha, na Mafarisayo na waalimu wa torati walikuwa wameketi hapo, waliotoka katika kila kijiji cha Galilaya, na Uyahudi, na Yerusalemu; na uweza wa Bwana ulikuwapo apate kuponya. [18]Na tazama, wakaja watu wanamchukua kitandani mtu mwenye kupooza; wakataka kumpeleka ndani na kumweka mbele yake. [19]Hata walipokosa nafasi ya kumpeleka ndani kwa ajili ya lile kundi la watu, walipanda juu ya dari wakampisha katika matofali ya juu, wakamshusha yeye na kitanda chake katikati mbele ya Yesu. [20]Naye alipoiona imani yao, alimwambia, Ee rafiki, umesamehewa dhambi zako.
[17]Ikawa siku zile mojawapo alikuwa akifundisha, na Mafarisayo na waalimu wa torati walikuwa wameketi hapo, waliotoka katika kila kijiji cha Galilaya, na Uyahudi, na Yerusalemu; na uweza wa Bwana ulikuwapo apate kuponya.
[18]Na tazama, wakaja watu wanamchukua kitandani mtu mwenye kupooza; wakataka kumpeleka ndani na kumweka mbele yake.
[19]Hata walipokosa nafasi ya kumpeleka ndani kwa ajili ya lile kundi la watu, walipanda juu ya dari wakampisha katika matofali ya juu, wakamshusha yeye na kitanda chake katikati mbele ya Yesu.
[20]Naye alipoiona imani yao, alimwambia, Ee rafiki, umesamehewa dhambi zako.
Jicho la mwanadamu linaona uponyaji ni kutendewa muujiza wa nje, lakini kwa Mungu Uponyaji hasaa ni kusamehewa dhambi. Mtu akishasamehewa dhambi, mengine yote hufuata..
Tunasamehewaje dhambi?
Kwa kumwamini Bwana Yesu na kumaanisha kumfuata kwa toba ya kweli. Hapo ndipo tunapopokea Msamaha Wa dhambi zetu, na hatimaye uponyaji Wa mambo yetu mengine yote.
Wakolosai 1:13-14
[13]Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake; [14]ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi;
[13]Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake;
[14]ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi;
Matendo ya Mitume 26:18
[18]uwafumbue macho yao, na kuwageuza waiache giza na kuielekea nuru, waziache na nguvu za Shetani na kumwelekea Mungu; kisha wapate msamaha wa dhambi zao, na urithi miongoni mwao waliotakaswa kwa imani iliyo kwangu mimi.
Ni ajabu Kuona, watu wanakwenda kwa Yesu na mapooza Yao, wengine katika afya zao kama huyu, wengine mapooza ya shughuli zao, wengine katika familia Zao n.k. wakitarajia Yesu awaponye kwa njia zao.
Lakini wanapokutana Na injili za wokovu na kuacha dhambi.. wanazikwepa wanakimbilia kwenye maombezi na mafuta Ya upako.
Ndugu fahamu kuwa asili ya kila tatizo ni dhambi..Mahali ambapo maisha yako yanawekwa wazi, yanamulikwa hapo ndipo uponyaji wako halisi upo. Usikimbie, usitange-tange.
Pokea kwanza msamaha wa dhambi mengine yafuate…kubali wokovu, kubali uzima, uponywe. Itakufaidia nini upate ulimwengu wote, afya yote, amani yote kisha ukateketee tena jehanamu milele baadaye?
Ikiwa bado hujaokolewa (yaani hujapata msamaha wa dhambi zako) basi wakati ndio huu.. wasiliana nasi kwa namba hizi kwa mwongozo wa kumpokea Yesu.
Shalom
NITAACHAJE DHAMBI?
MAFUNZO YA BIBLIA KWA WATOTO
Swali: Kwanini MUNGU aliufanya mkono wa Musa kuwa na ukoma kama ishara kwa wana wa Israeli? (Kutoka 4:6).
Kutoka 4:6 “Bwana akamwambia tena, Sasa tia mkono wako kifuani mwako. Akautia mkono wake kifuani mwake; naye alipoutoa, kumbe! Mkono wake ulikuwa una ukoma, umekuwa mweupe kama theluji. 7 Akasema, Tia mkono wako kifuani mwako tena. Akautia mkono wake kifuani mwake tena, na alipoutoa kifuani mwake, kumbe! Umerudia hali ya mwili wake. 8 Basi itakuwa, wasipokusadiki, wala kuisikiliza sauti ya ishara ya kwanza, wataisikiliza sauti ya ishara ya pili”.
Kutoka 4:6 “Bwana akamwambia tena, Sasa tia mkono wako kifuani mwako. Akautia mkono wake kifuani mwake; naye alipoutoa, kumbe! Mkono wake ulikuwa una ukoma, umekuwa mweupe kama theluji.
7 Akasema, Tia mkono wako kifuani mwako tena. Akautia mkono wake kifuani mwake tena, na alipoutoa kifuani mwake, kumbe! Umerudia hali ya mwili wake.
8 Basi itakuwa, wasipokusadiki, wala kuisikiliza sauti ya ishara ya kwanza, wataisikiliza sauti ya ishara ya pili”.
Sababu kuu ya BWANA MUNGU, kuutia mkono wa Musa ukoma na kisha kuuponya ni kutoa ujumbe kwa wana wa Israeli kuwa yeye ni Mungu awaponyaye.. Kwa hivyo wana wa Israeli walipoiona ile ishara walitambua kuwa Mungu wao ni Mungu anayeponya na kuondoa maradhi, misiba, mateso na hata utumwa..
Jambo hilo tunalithibitisha mbele kidogo katika ile sura ya 15 alipowaambia jambo hilo pale alipoyaponya maji yaliyokuwa machungu..
Kutoka 15:22 “Musa akawaongoza Israeli waende mbele kutoka Bahari ya Shamu, nao wakatokea kwa jangwa la Shuri; wakaenda safari ya siku tatu jangwani wasione maji. 23 Walipofika mahali palipoitwa Mara hawakupata kuyanywa yale maji ya Mara, kwa kuwa yalikuwa machungu; kwa ajili ya hayo jina lake likaitwa Mara. 24 Ndipo watu wakamnung’unikia Musa, wakisema, Tunywe nini? 25 Naye akamlilia Bwana; Bwana akamwonyesha mti, naye akautia katika hayo maji, maji yakawa matamu. Basi akawawekea amri na hukumu huko, akawaonja huko; 26 akawaambia, Kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya Bwana, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yo yote niliyowatia Wamisri; KWA KUWA MIMI NDIMI BWANA NIKUPONYAYE. 26 kawaambia, Kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya Bwana, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, MIMI SITATIA JUU YAKO MARADHI YO YOTE NILIYOWATIA WAMISRI; KWA KUWA MIMI NDIMI BWANA NIKUPONYAYE”.
Kutoka 15:22 “Musa akawaongoza Israeli waende mbele kutoka Bahari ya Shamu, nao wakatokea kwa jangwa la Shuri; wakaenda safari ya siku tatu jangwani wasione maji.
23 Walipofika mahali palipoitwa Mara hawakupata kuyanywa yale maji ya Mara, kwa kuwa yalikuwa machungu; kwa ajili ya hayo jina lake likaitwa Mara.
24 Ndipo watu wakamnung’unikia Musa, wakisema, Tunywe nini?
25 Naye akamlilia Bwana; Bwana akamwonyesha mti, naye akautia katika hayo maji, maji yakawa matamu. Basi akawawekea amri na hukumu huko, akawaonja huko;
26 akawaambia, Kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya Bwana, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yo yote niliyowatia Wamisri; KWA KUWA MIMI NDIMI BWANA NIKUPONYAYE.
26 kawaambia, Kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya Bwana, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, MIMI SITATIA JUU YAKO MARADHI YO YOTE NILIYOWATIA WAMISRI; KWA KUWA MIMI NDIMI BWANA NIKUPONYAYE”.
Na hata sasa bado MUNGU wetu ana sifa hiyo hiyo, “YEYE NI MUNGU ATUPONYAYE”… Ikiwa tutasikiliza kwa bidii sauti yake na kufanya yale anayotuelekeza.. Magonjwa yote hayatakuwa sehemu yetu, mateso yote hayatakuwa sehemu yetu na kila aina ya mabaya ya ibilisi hayatatutawala.
Je umempokea YESU KRISTO kama Bwana na Mwokozi pekee wa maisha yako?
Kama bado unasubiri nini?.. mwamini leo uokolewe na kuponywa.
FANYIKA SIPORA WA KRISTO, UNYAKUO UPO KARIBU.
FIMBO YA HARUNI!
MAMBO SITA, AMBAYO MUNGU HUTUMIA KUONDOA UOVU NDANI YA MTU.
Kwanini Mungu alimchagua Musa, na si mtu mwingine?
NABII MUSA.
Mathayo 20:6
[6]Hata kama saa kumi na moja akatoka, akakuta wengine wamesimama, akawaambia, Mbona mmesimama hapa mchana kutwa bila kazi?
Bwana Yesu alizungumza mfano ambao unagusia kabisa uhalisia wa kiroho uliopo sasa katika kazi ya Mungu (Ushuhudiaji).
Mfano huo unahusu mtu mmoja aliyetoka asubuhi sana kuajiri wafanyakazi ili kwenda kulilima shamba lake ambalo lilihitaji watu wengi kulihudumia.
Hivyo akatoka alfajiri sana, kuwatafuta na kwa bahati nzuri akawakuta, akawapeleka shambani mwake, akatoka tena saa tatu, akawakuta wengine wamekaa bila kazi, akawatuma shambani, akaenda tena saa sita na saa tisa vivyo hivyo akafanya…Mpaka ilipofika saa kumi na moja akatoka na kuwakuta watu wengine wamesimama tu toka asubuhi mpaka jioni…hawafanyi chochote wapo “Idle”
akawaambia, Mbona mmesimama hapa mchana kutwa bila kazi?
Mathayo 20:1-7
[1]Kwa maana ufalme wa mbinguni umefanana na mtu mwenye nyumba aliyetoka alfajiri kwenda kuajiri wakulima awapeleke katika shamba lake la mizabibu. [2]Naye alipokwisha kupatana na wakulima kuwapa kutwa dinari, aliwapeleka katika shamba lake la mizabibu. [3]Akatoka mnamo saa tatu, akaona wengine wamesimama sokoni wasiokuwa na kazi; [4]na hao nao akawaambia, Enendeni nanyi katika shamba langu la mizabibu, na iliyo haki nitawapa. Wakaenda. [5]Akatoka tena mnamo saa sita na saa kenda, akafanya vile vile. [6]Hata kama saa kumi na moja akatoka, akakuta wengine wamesimama, akawaambia, Mbona mmesimama hapa mchana kutwa bila kazi? [7]Wakamwambia, Kwa sababu hakuna mtu aliyetuajiri. Akawaambia, enendeni nanyi katika shamba la mizabibu.
[1]Kwa maana ufalme wa mbinguni umefanana na mtu mwenye nyumba aliyetoka alfajiri kwenda kuajiri wakulima awapeleke katika shamba lake la mizabibu.
[2]Naye alipokwisha kupatana na wakulima kuwapa kutwa dinari, aliwapeleka katika shamba lake la mizabibu.
[3]Akatoka mnamo saa tatu, akaona wengine wamesimama sokoni wasiokuwa na kazi;
[4]na hao nao akawaambia, Enendeni nanyi katika shamba langu la mizabibu, na iliyo haki nitawapa. Wakaenda.
[5]Akatoka tena mnamo saa sita na saa kenda, akafanya vile vile.
[7]Wakamwambia, Kwa sababu hakuna mtu aliyetuajiri. Akawaambia, enendeni nanyi katika shamba la mizabibu.
Embu jiulize swali moja.. Je! Unadhani watu hawa wa saa kumi na moja hawapo leo?
Kukaa bila kufanya kazi ya Mungu, wakati Kazi ipo kubwa kwa kisingizio kuwa hakuna wa kukuajiri ni ulegevu kiroho… yule Bwana hakuwa na muda wa kusikiliza sababu zao, kwamba waendelee kukaa na kumalizia tu siku kwasababu muda umeenda, bali aliwatuma haraka sana shambani.
1) Hofu ya kutumika
Kusema mimi siwezi, Mimi bado mchanga kiroho, sijui biblia vizuri, Mimi bado mdogo kiumri, mimi siwezi Kuongea nina aibu, nina kigugumizi..sina fedha, sina elimu n.k…haya ndio mambo yanayowakawiisha watu wengi wasimtumikie Mungu..
Ndugu fahamu kuwa Mungu hategemei ukamilifu wetu, kutimiza kusudi lake kamilifu, bali hututumia katika hali zetu hizi hizi, hivyo usingojee siku fulani utakuwa mzoefu ndio umtumikie Mungu..haitafika, anzia na hali yako hiyo hiyo.(1Wakoritho1:26-29)
2) Kungojea muda fulani sahihi.
Kudhani Kuwa upo muda fulani maalumu utaitwa na Bwana rasmi umtumikie, hilo pia limewafanya wengi, kungoja muda mrefu na hatimaye kutoona mafanikio.. saa ya kutumika ni sasa..tayari Wote tulishaitwa tumtumikie yeye tangu siku tulipookoka..ukishaokoka umepewa na vibali vyote na mamlaka ya kumtumikia Bwana..usingoje utokewe na Yesu kama Paulo Dameski, Usingoje usikie sauti fulani ikikwambia nenda kawafundishe watu. Anza sasa na Bwana ataungana na wewe mbele ya safari.
3) Masumbufu ya maisha
Mizigo mingi ya kimaisha, utakula nini, utavaa nini, utaishije, linawapunguza watu kasi ya kufikiria kwamba wanahitaji kwanza kuyaandaa maisha yao yawe safi ndipo waamke kwenda kumuhubiri Kristo.
Ndicho walichokifanya wayahudi walipokuwa wanajenga hekalu la pili, ilifika wakati wakaacha ujenzi kila mmoja akaenda kwenye mambo yake, Kwasababu tu, ya kujiangalia hali zao.
Hagai 1:2-4
[2]BWANA wa majeshi asema hivi, ya kwamba, Watu hawa husema, Huu sio wakati utupasao kuja, huu sio wakati wa kujenga nyumba ya BWANA. [3]Ndipo neno la BWANA lilikuja kwa kinywa cha nabii Hagai, kusema, [4]Je! Huu ndio wakati wa ninyi kukaa katika nyumba zenye mapambo ya mbao, iwapo nyumba hii inakaa hali ya kuharibika?
[2]BWANA wa majeshi asema hivi, ya kwamba, Watu hawa husema, Huu sio wakati utupasao kuja, huu sio wakati wa kujenga nyumba ya BWANA.
[3]Ndipo neno la BWANA lilikuja kwa kinywa cha nabii Hagai, kusema,
[4]Je! Huu ndio wakati wa ninyi kukaa katika nyumba zenye mapambo ya mbao, iwapo nyumba hii inakaa hali ya kuharibika?
Usingoje ufanikiwe, uoe, uwe na maisha ndio sasa uanze kuifanya kazi ya Mungu, ukijitazama Sana, hutamtumikia Mungu ndugu.. fahamu kuwa wengi wanaokuletea wewe habari njema sio wenye mafanikio, lakini Bwana hawaachi.
4) Ulegevu.
Kupendelea mambo ya kirahisi rahisi, zaidi ya kujitoa..wakati mwingine kukataa kutaabika kwa ajili ya injili..kutaka ijiendeshe Yenyewe, bila kuwa mfuatiliaji na mwombaji, pia hukawiisha utendaji kazi wa injili.
Hivyo, ndugu muda ni mfupi sana, tupo katika saa la kumi na moja yetu, usihudhurie tu kanisani, kuwa sehemu ya utumishi kanisani, usisikilize / kusoma tu mahubiri, hubiri na kwa wengine unachojifunza, Shamba la Bwana linatuhitaji wote.
Ni wakati wa kuamka usingizini, bado hatujachelewa, ikiwa tutatimiza kusudi la Mungu vema, basi tutalipwa sawasawa tu na wale waliowahi..Hivyo amka sasa.. anza kushuhudia.
Shiriki injili kwa kushea na wengine habari hizi
Bwana akubariki
Siku moja nilikuwa nakatiza eneo fulani la biashara ambalo limechangamka sana, Ni eneo ambalo watu wengi wanapishana..ghafla kwa mbele nikamwona kijana mmoja ameinama, baada ya muda kidogo akachuchumaa, na mara akaanza kutapika matapishi mengi sana.. Uso wake ulionekana kuumwa, hivyo moja kwa moja nilipomwangalia moyoni mwangu, niliguswa sana na ile hali aliyokuwa anapitia..
Kikawaida zipo hali ambazo ukiumwa Unaweza kuzivumilika mpaka ufike mahali fulani pa matibabu..lakini kuumwa mpaka kutapika Hakuzuiliki, na kama ulishawahi kutapika unaelewa nguvu inayotumika, hali unayoisikia wakati huo.. ni kama nusu ya kufa..
Sasa sisi ndivyo tunavyomfanya Mungu, ajisikie muda wote tunapokuwa Na aina ya mwenendo wa uvuguvugu maishani mwetu, .alisema hivi;
Ufunuo wa Yohana 3:15-19
[15]Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. [16]Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu. [17]Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi. [18]Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona. [19]Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.
[15]Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.
[16]Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.
[17]Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.
[18]Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.
[19]Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.
Uvuguvugu ni ile hali ya kuwa mtu wa kidini na sio wa kiroho, unahudhuria ibada lakini mabadiliko huna, unavaa vizuri kanisani lakini ukiwa nje unavaa nguo zisizo na adabu, unaimba kwaya, lakini wakati huo huo unasikiliza nyimbo za kidunia, ni mtumishi mzuri wa kanisani lakini bado unaishi na mume wa mtu..
Maisha ya uvuguvugu, yanamtesa Kristo isivyo kawaida..Ikiwa wewe hupendi kutapika- tapika Kwanini wewe umfanye Mungu kuwa na hali hiyo?
Ukristo ni mwendelezo sio tukio…eti mimi nimeshamkiri Yesu kwa Kinywa..inatosha nimeokoka, hapana…bali ni ukuaji wa kiroho.. ni lazima uonyeshe ukuaji…kitu chochote kilicho hai kinakua…lakini kuwa mtu yule yule kila siku wewe ni vuguvugu.
Kanisa La Laodikia, lilikuwa na sifa ya kujiona ni tajiri Kisa Lina vyombo vizuri vya miziki, lina Makongamano makubwa ya nje, lina mwonekano wa kuvutia, lina umaarufu, Lakini Yesu aliliona si la kiroho hata kidogo..Linamheshimu Mungu kwa nje tu, lakini ndani limepoa zaidi ya barafu..
Hizi ni nyakati ambazo watu wengi wanazisahau ibada za kweli, wanatafuta fedha na Midundo inayovutia masikio ya watu lakini hawajali ujumbe wa rohoni au ‘uzuri Wa utakatifu’.
Na watu ambao wakiwaona wengine wamesimama kikamilifu mbele za Mungu wanawaita “walokole” …
Embu tubu, rafiki…uzuri wako, mwonekano wako, Sifa zako, udunia wako, havina ushirika na Kristo, hizo status zisizo na staha na elimu, unampostia nani mitandaoni? Hiyo mitandao ya kizinzi unayoitembelea kila siku, na kujichua unakoendelea nako kwa siri na wakati huo huo unasema umeokoka, nini unakiunda kama sio kumfanya Bwana atapike?…maanisha kumpokea Kristo. Simama katika imani, ili umwone Mungu wa kweli na sio sanamu.
Kumbuka hizi ni nyakati za kusimama kikamilifu, kwasababu mwisho umekaribia..Unyakuo Ukipita watakaokwenda na Bwana ni walio moto tu, na sio vuguvugu.
Kutubu ni kugeuka…Geuka tu leo kwa kumaanisha na Bwana atakusamehe kabisa na kuanza na wewe..Ikiwa hujaokoka na upo tayari leo kufanya hivyo…Basi wasiliana nasi kwa mwongozo wa sala ya Toba..
NAYAJUA MATENDO YAKO.
Nini maana ya kumwabudu Bwana katika uzuri wa utakatifu?