SWALI: Je Mungu alipomwumba Adamu kwa sura yake na mfano wake alikuwa na kitovu?..Kwasababu kazi ya kitovu ni kumlisha mtoto tumboni chakula kutoka kwa mama yake…..Sasa Adamu na Hawa hawakupitia hiyo hatua ya kukaa tumboni kwa mama zao je!..ingewezekanikaje wao kuwa na vitovu?…
JIBU: Mungu alipomwumba Adamu alimwumba akiwa kamili..Hakuna chochote kilichokuwepo kwa Adamu ambacho hakikuwepo kwa watoto wake. Umbile lake lote kuanzia kichwani mpaka miguuni lilikuwa ndio hilo hilo kwa uzao wake wote.
Sasa tukirudi kwenye swali linalouliza…je Adamu alikuwa na kitovu?..Jibu ni ndio alikuwa nacho!…Mungu alimuumba akiwa na kitovu..Sasa Mungu alipokiweka kitovu kwa Adamu na Hawa visingekuwa na kazi kwao lakini vingekuja kuwa na kazi kubwa kwa wanao ambao watawazaa hapo baadaye..kwani wanao watavitumia kupata chakula wakiwa tumboni.
Ni sawa na Adamu Mungu alipomwumba na chuchu mbili ndogo kifuani mwake…Mungu aliziweka vile kwa utukufu wake, ambapo Adamu pengine zisingekuwa na kazi yoyote kubwa kwake….kama leo tunavyoziona sizivyo na kazi kwa wanaume…Lakini umuhimu wa kuwepo zile chuchu mbili kifuani kwa Adamu tunakuja kuziona pale Hawa alipotoka ubavuni mwake….Kwani Hawa alizirithi zile chuchu kutoka kwa Adamu na zilikuja baadaye kutumika kama chanzo cha chakula kwa watoto wao.
Kadhalika na kitovu. Adamu alikuwa nacho lakini hakikuwa na kazi yoyote kwenye mwili wake…lakini kazi kubwa ilikuja kuonekana kwa wanawe aliokuja kuwazaa…kwani kitovu hicho walichokirithi kutoka kwa Adamu kimekuja kutumika kama njia ya kupitishia chakula kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa ujauzito.
Hivyo Adamu alikuwa na kitovu pale alipoumbwa na Mungu. Na wanawe aliowazaa walikuwa kama yeye wote wana vitovu..Biblia inasema Adamu alizaa mwana kwa sura yake na mfano wake….Ikimaanisha kuwa kama Adamu angekuwa hana kitovu halafu mtoto aliyemzaa awe nacho basi biblia ingekuwa inasema uongo pale iliposema Adamu alizaa mwana wenye sura yake na mfano wake.
Mwanzo 5:1 “Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya Mungu alimfanya; 2 mwanamume na mwanamke aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa. 3 Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi”. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mwanzo 5:1 “Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya Mungu alimfanya;
2 mwanamume na mwanamke aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa.
3 Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi”. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
Adamu alikuwa na watoto wangapi?
BUSTANI YA NEEMA.
Je! Adamu aliwasaliana na Mungu kwa lugha ipi pale bustanini?
Je! mwanadamu wa kwanza kuumbwa ni yupi Mzungu mwafrika au Mchina na kama ni mmojawapo kati ya hao je hao wengine wametoka wapi?
Je! taratibu za kufunga ndoa [yaani harusi] ni agizo la Mungu au ni mapokeo tu ya kibinadamu?
Uzao wa Mwanamke ni upi? Unaozungumziwa katika Mwanzo 3:15?
Mungu alikuwa anaongea na nani aliposema na “Tumfanye mtu kwa mfano wetu”,(Mwanzo 1:26)?
JE! Kaini alimpatia mke wake wapi?
Rudi Nyumbani:
Print this post