Jini Mahaba yupo kibiblia?, Mtu mwenye jini mahaba anakuwaje?
Moja ya elimu inayowachanganya wengi na inayopotoshwa ni Elimu juu ya mapepo..
Mapepo kwa lugha nyingine wanaiwa majini…Ni kitu kimoja kinachojulikana kwa majina mawili tofauti, ni kama MWANADAMU na MTU. Hayo ni majina mawili tofauti lakini yanaelezea kitu kimoja.
Sasa mapepo ni roho za malaika walioasi mbinguni, ambao walitupwa chini pamoja na kiongozi wao mkuu shetani. Baada ya kutupwa chini ndio yakaitwa mapepo.
Mapepo hayo yanaweza kumwingia mtu na kumfanya awe na tabia yoyote ile wanayotaka wao. Mapepo haya yanaweza kumwingia mtu na kumfanya awe mwizi, mengine yanaweza kumfanya mtu awe mlevi, mengine yanaweza kumfanya mtu awe mzinifu au mwenye tabia ya zinaa.
Sasa mapepo ambayo yanawafanya watu wabadilike tabia na kuwa wazinifu au kuhisi wanafanya mapenzi na watu wakati wa kulala ndio hayo WATU wanayoyaita MAJINI MAHABA. Lakini kiuhalisia mapepo hayo hayana jinsia yoyote kwasababu ni roho. Na haya yanapomwingia mtu yoyote ambaye hajaokoka.(yaani ambaye hajampokea Yesu Kristo kama Bwana na mwokozi wa maisha yake) yanamfanya anakuwa mtumwa wa dhambi hiyo ya zinaa katika ndoto au katika maisha yake ya kawaida..Kwa mtu wa kawaida huwa hayamtokei kwa wazi lakini kwa wale ambao wamekufa kabisa kiroho na wamejiuza kwa shetani huwa yanaweza kujidhihirisha kwa macho kabisa..
Lakini kumbuka shetani siku zote ni mwongo pamoja na mapepo yake yote, biblia inasema shetani anao uwezo wa kujigeuza na kuwa hata malaika wa Nuru (Kasome 2Wakoritho 11:14), hivyo sio ajabu kuweza kujigeuza na kuwa hata mwanamke mzuri au mwanamume mzuri wa kuvutia, lakini ndani yake ni pepo mbaya na mchafu. Watu wengi wanadanganyia na kufikiri kuna mapepo ya kike..Ndugu usidanganyike hakuna kitu kama hicho…hayo ni maroho tu hayana jinsi, shetani ni baba wa uongo siku zote.
Kwa asili roho hizi za mapepo huwa hazimtokei mtu kwa wazi kama tulivyotangulia kujifunza hapo juu, isipokuwa kwa mtu ambaye tayari amejiuza kwa shetani moja kwa moja, hususani kama mtu ni mshirikina, au mganga au mchawi kabisa, huyu anaweza kuziona kwa macho..Lakini kwa wengine ambao wapo nusunusu, vuguvugu..roho hizi zinawaendesha katika ndoto tu na katika tabia zao. Katika ndoto wanakuwa wanaota wanafanya zinaa na katika tabia wanakuwa wanatabia zilizokithiri za uasherati mpaka wengine kuwafanya kuwa mashoga au wasagaji, au walawiti au wafiraji.
Na zifuatazo ni njia mapepo haya yanayozitumia kuingia ndani ya watu.
Kujitazama kwenye kioo hakuna uhusiano wowote na kuingiwa na roho hizo..Isipokuwa mtu mwenye tabia ya kujipamba, na kujichubua, kusuka suka, kuchonga nyusi anakuwa na tabia ya kujiangalia kwenye kioo mara kwa mara..hivyo hiyo tabia ya kujipamba na kuchonga nyusi ndio mlango wa mapepo hayo kuingia lakini sio kujitazama kwenye kioo.
Biblia inasema katika..
Ufunuo 21:27 “Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo”.
Kilicho kinyonge kinachozungumziwa hapo ndio hicho chenye roho ya mapepo ndani yake..Kwasababu mtu mwenye roho ya mapepo atakuwa na tabia tu fulani chafu ambazo watu wenye tabia hizo biblia inasema hawataurithi uzima wa milele. Mtu mwenye pepo la zinaa/jini mahaba ni lazima atakuwa mzinifu na mbinguni hawataingia wazinifu..Mtu mwenye pepo la ulevi ni lazima atakuwa tu mlevi na mbinguni hawataingia walevi.
Ufunuo 21:8 “Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili..”
Mbinguni wataingia tu watu wenye Roho Mtakatifu..ambao ni watakatifu.
Waebrania 12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao; “
Kwanza ni kwa kumpa Yesu Kristo maisha yako, unatubu kwa kudhamiria kabisa kuacha dhambi na kisha unajiepusha na milango kujitenga na milango hiyo sita hapo juu tuliyoiona ambayo ndio mlango ya kuingiwa na roho hizo chafu. Na roho hizo zitakuacha kabisa na utakuwa huru.
Bwana akubariki
Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
dungu, vioo havifaikabisa tena kujitizima pindi ukiwa hunanguo pia majini wana wake wapo, majini,waliumbwa kwa moto ,binadamu waliumbwa kwa udongo na malaika waliumbwa kwa nuru,pia ukisema majini ni malaika walio asi hiyo siyo kweli, bali majini ndio walio asi hivyo mwenyezi mungu akatuma kundi la malaika kuangamiza koo zakijini na pindi operation ilipokuwa ikiendelea ndipo kiongozi wa malaika alikikuta kitoto cha kijini kiki sali hivyo akaamua kukichukua hadi kwa mwenyezi mungu, ila mwenyezi mungu hakuwa ladhi naalicho kifanya mkuu wa malaika kwa kumchukua huyo jini, basi mtoto wakijini aliendelea kukuwa akiwa pamoja na kundi la malaika ndipo mwenyezi mungu akawaambia malaika kuwa anataka kuumba binadamu ambae atakuwa kiongozi katika dunia ndipo malaika wakamuuliza mwenyezi mungu je? unataka kuleta atakae kuasi kama walivyo kuasi hao wa kabla? natena sisi niwenye kuku abudu wewe? mwenyezi mungu akawajibu kuwa mimi nayajua nyinyi msio yajua ,hivyo uumbaji wa adam ukaanza pia tukumbuke kuwa adam aliumbwa akiwa mrefu sana naakawekwa kwenye uwazi hivyo yule jini alie kuwa miongoni mwa malaika alikuwa akienda kuangalia na kupita katika mwili wa adam pindi haja pulizwa roho hivyo alifanya atakavyo nakuujua uzaifu wa adam siku zilikwenda ndipo mwenyezi mungu aka upulizia roho mwili wa adam, napia mwenyezi mungu akamfundisha majina yavitu na ya wanyama pia nahata mwenyezi mungu alipo wauliza malaika jina ya wanyama, ndege hawakuwa wenye kuyafahamu ndipo mwenyezi mungu akawaambia malaika msujudieni adam malaika wakatii amli ya mwenyezi mungu ila yujini hakutii amri ya mwenyezi mungu ndipo mwenyezi mungu akamwambia mkuu wa malaika nilikuambie muangamize koozote za kijini ila nyinyi hamkufanya hivyo je? mmeona kibuli cha huyu? ila tukumbuke kuwa ilikwisha andikwa kuwa huo uta kuwa nimtihani kwa wanadamu na ndipo mwenyezi mungu alipo amua kumfukuza huyojini katika pepo nakumwambia adam kuwa hakika huyu niadui kwako hiyo kwa ufupi broo?
About the author