WATASHINDANA LAKINI HAWATAKUSHINDA

WATASHINDANA LAKINI HAWATAKUSHINDA

Watapigana nawe lakini hawatakushinda maana yake ni nini?


Yeremia 1:18 “Maana, tazama, nimekufanya leo kuwa mji wenye boma, na nguzo ya chuma, na kuta za shaba, juu ya nchi yote; juu ya wafalme wa Yuda, na juu ya wakuu wake, na juu ya makuhani wake, na juu ya watu wa nchi hii.

19 Nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamoja nawe, asema Bwana, ili nikuokoe”.

Haya ni maneno ambayo alipewa Yeremia baada ya kuitwa na Mungu katika huduma. Lakini kwa hofu ya labda atakapokwenda kuwaeleza  watu juu ya hukumu za Mungu, watakasirika na kumletea madhara ya ghafla labda watampiga mawe, hapo ndipo hapo Mungu akamuhakikishia kuwa ni kweli watakuja kupigana na yeye, lakini hawatamshinda, kwasababu yeye yupo pamoja naye.

Hata sasa adui hawezi kuja kupigana na mtu kama huna huduma ya  Mungu mkononi mwake, mstari huu unapendwa kutamkwa na watu wengi kirahisi rahisi hata watu ambao wapo katika dhambi, wanajidanganya wakisema..

watashindana lakini hawatakushinda

Huo ni uongo, shetani hashindani na watu waovu,hata mara moja, kwasababu tayari alishawashinda siku nyingi. Hivyo ukijiona unapitia vita visivyokuwa na maana angali wewe ni mwenye dhambi ujue hayo sio mapambano.

Lakini ili Neno hili liwe na nguvu ndani yako, ni sharti kwanza, uokoke, umkabidhi Yesu maisha yako kweli kweli, kisha uwe na kazi ya kufanya katika injili yake, ndipo hapo hata shetani akinyanyuka na majeshi yake yote kutaka kukuangusha wewe ni sawa na kazi bure, kwasababu Mungu yupo pamoja na wewe daima.

Wakati huo hata ulimwengu mzima uungane vipi kutaka kukupindua usisonge mbele, watakuwa ni kama wanapoteza Muda kwasababu Mungu yupo upande wako.

Hivyo kama upo tayari leo kuokoka, ili maneno haya yawe na nguvu kwako, basi uamuzi huo ni wa busara, fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Shalom.

Mada Nyinginezo

MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA WARAKA WA TATU WA YOHANA.

Historia ya wimbo wa tenzi – Ndio dhamana Yesu wangu

KWANINI TUNAOMBA KWA JINA LA YESU?

NAO WATAKAOUAWA NA BWANA WATAKUWA WENGI.

YEREMIA

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator