Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe, karibu tujifunze biblia.
Kama tunavyojua adui yetu wa kwanza na wa mwisho ni shetani, ambaye biblia inasema anazunguka huko na huko kama simba akitafuta mtu wa kummeza 1Petro 5:8, hivyo ni wajibu wetu kujua kuwa tupo katika shabaha ya adui.
Sasa ipo milango ambayo shetani anaitumia sana kuleta mashambulizi kwa mtu, na mashambulizi hayo yanaweza kuwa ni magonjwa ya kimwili, na ya kiroho (mfano kusumbuliwa na roho za mapepo, ikiwemo hofu, na mashaka, na madhaifu mbali mbali). Ukiona unazo dalili hizo basi kuna uwezekano mkubwa umeshambuliwa na adui.
Ifuatayo ni milango mikubwa ambayo inafungua fursa ya mashambulizi ya kiroho na kimwili, kutoka kwa adui.
UASHERATI NA ZINAA.
Huu ndio mlango wa kwanza na mkubwa, unaoharibu maisha ya watu wengi kiroho na kimwili. Mlango huu ndio wa kwanza hata zaidi ya ushirikina, mtu yeyote anayefanya uzinzi/ uasherati..katika roho ni kama ametangaza kuwa yeye ni nyumba ya kila roho chafu..Ni mlango tosha wa pepo la aina yeyote kumwingia huyo mtu.
Milango mingine ni pamoja na ushirikina, ibada za sanamu, kutokusamehe, chuki, uuaji n.k
Sasa unaweza kuwa hufanyi zinaa, wala sio mshirikina,huabudu sanamu, wala sio mlevi, wala muuaji..wala hufanyi mambo mengine yote yasiyompendeza Mungu, lakini bado unaona kuna mashambulizi unayapata..
Ukiona unapitia hali kama hiyo, basi fahamu kuwa shetani amekushambulia kwa mlango mwingine ambao huujui wewe wala hukuidhania.
NA HUO SI MWINGINE ZAIDI YA MLANGO WA MAOMBI.
Kumbuka maombi tunayoyazungumzia hapa sio maombi ya kuombewa, kwamfano kuwekewa mikono na mtumishi au mtu fulani, Hapana!, bali ni yale maombi ya mtu binafsi kumwomba Mungu juu ya mambo yake, na ya wengine. Na hayo sio ya dakika 5, wala 10…bali ni yale yasiyopungua saa moja. Na sio lisaa limoja kwa wiki au mwezi, bali angalau lisaa limoja kwa siku.
Shetani kawapotosha wengi na kufikiri ukishamwamini Yesu tu, basi hakuna sababu ya kuomba mara kwa mara, kwani tumeshafunikwa na damu, pale tulipompokea. Yanini kuomba kila siku?. Usidanganyike!..Bwana Yesu pamoja na ukamilifu wake wote, lakini alikuwa anaomba dua nyingi tena kwa machozi mengi kila siku. (Soma Waebrania 5:7).
Na Bwana Yesu huyo huyo alisema..
Luka 22:46 “Akawaambia, Mbona mmelala usingizi? Ondokeni, mkaombe, msije mkaingia majaribuni”
Mtu anayeomba kila siku ni kama vile mtu anayeoga kila siku, maana yake nafasi ya kupata magonjwa katika mwili wake anaipunguza kila siku, lakini mtu asiyekuwa mwombaji, lakini anaendelea kuwa msomaji wa Neno, ni sawa na mtu aliyeacha kuoga kabisa lakini anaendelea kula mlo kamili, na kupiga mswaki. Ni kweli mlo ule unaweza kumfanya afya yake ikawa thabiti, lakini hiyo itakuwa kwa kitambo tu, ule uchafu wa mwili unapozidi kujilundika juu ya mwili wake, utamletea magonjwa tu siku moja!..hata kama atakuwa anakula vizuri kiasi gani.
Ndivyo hivyo ivyo na mtu asiyeomba na huku anajitumainisha kwamba anasoma Neno tu, au hafanyi dhambi hii wala ile, (mashambulizi yake yatamjia kwa ghafla na wala hatajua yanakotokea)…Kwa kitambo kifupi sana roho yake itakuwa na afya na salama, lakini siku si nyingi tatizo litaingia kupitia kipengele hicho cha maombi alichokipuuzia au kizembea.
Lakini kama vyote vikienda pamoja, kusoma Neno,kujitenga na dhambi, pamoja na kusali kwa bidii…ni sawa na mtu anayekula mlo kamili, na pamoja na kula mlo kamili pia unausafisha mwili wake kila siku kwa kuoga, mtu wa namna hiyo ni ngumu kushambuliwa na magonjwa..Kwasababu milango yote yote kaifunga.
Mathayo 26:40 “Akawajia wale wanafunzi, akawakuta wamelala, akamwambia Petro, Je! Hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja? 41 Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.
Mathayo 26:40 “Akawajia wale wanafunzi, akawakuta wamelala, akamwambia Petro, Je! Hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja?
41 Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.
Hivyo ndugu kama ni wewe bado unapata shida ya kusumbuliwa na mashambulizi ya kiroho, hebu tazama tena eneo lako la Maombi. Jiulize mara ya mwisho kuomba angalau lisaa limoja ni lini?, inawezekana hufanyi uasherati, wala mambo mengine ya kidunia ambayo ni milango ya mashambulizi ya kiroho, lakini katika kipengele hichi cha maombi umekizembea… Basi jua tatizo lipo hapo.
Yakobo 4: 4b “..Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi!
Na hata kama husali na bado hujaona madhara yake, fahamu kuwa yanakuja…hivyo usisubiri mpaka shida zikupate ndipo ukumbuke kuomba, Hivyo anza kulirekebisha hilo leo. Na Mungu akubariki sana.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312 Au jiunge na makundi yetu ya mafundisho ya kila siku kwa kwa njia ya Whatsapp kwa kubofya hapa >>>> WHATSAPP GROUP
Mada Nyinginezo:
FAIDA ZA MAOMBI YA USIKU
KUNA MAJIRA MUNGU ATAIVURUGA MIPANGO YETU.
Mruba ni mdudu gani kwenye biblia?(Mithali 30:15)
Ni kwanini mifugo ya Yakobo iliongezeka kwa wingi kiasi kile?
WINGU KUBWA LA MASHAHIDI.
MWANZO WA INJILI YA YESU KRISTO.
Rudi nyumbani
Print this post