Title December 2025

Wale mbweha wadogo, Waiharibuo mizabibu.

Wale mbweha wadogo, Waiharibuo mizabibu

Wimbo ulio bora 2:15

15 : Tukamatie mbweha, Wale mbweha wadogo, Waiharibuo mizabibu, Maana mizabibu yetu yachanua.

Kitabu cha wimbo ulio Bora ni kitabu kinachoeleza asili ya upendo wa Kristo kwetu na jinsi tunavyopaswa kuuitikia.

Kuwa urefu wa masomo yaliyo nyuma ya kitabu hiki fungua hapa >>> NYAKATI TOFAUTI- TOFAUTI ZA UPENDO.

Lakini kwenye mstari huu, tunaona ni kama vile mtu kwa lugha ya picha anaona mbweha “ Wadogo” wamevamia shamba lake la mizabibu inayochanua na hivyo hawapuuzii kwasababu ya udogo wao, bali anatoa tamko la kukamatwa na kuondolewa…ili shamba lake linalochanua liwe salama.

Kimsingi mbweha si mnyama anayekula nyama tu, bali hula pia mizazibu, na mingine kuiharibu.

Hii ni kufunua nini katika hali zetu za rohoni.. 

Adui akishaona mahusiano Yetu na Kristo yanazaa matunda, huinua vitu Vidogo vidogo ili kuharibu mahusiano wakati mwingine unaweza usione kama vina madhara sana au vina nguvu sana, lakini katika eneo la kiroho kitu kidogo kina nguvu sawa na kitu kikubwa…

Hivi ndio vinavyoitwa mbweha wadogo..

Mambo Kama haya ni kama vile kuendekeza vishawishi vya dhambi kwenye maisha yako.

Kwa mfano wewe ni binti halafu kila siku unaona wanaume wanazungumza na wewe maneno ya mizaha, sasa kama usipokemea tabia hiyo, ukaona ni kawaida, tabia hizo ndogo ndogo ndizo zinazopelekea mtu baadaye kuanguka kwenye dhambi za uzinzi.

Samsoni, alipoona ushawishi wa delila unaendelea, badala aukatishe yeye akapuuzia mwisho wa siku akatekwa..

Hao ni mbweha wadogo wanaoharibu shamba lako, kila kichocheo na kishawishi kiwe kidogo kiasi gani usikipuuzie.

Wakati mwingine kuendekeza uvivu wa kiroho, yaani kupuuzia maombi, kupuuzia ibada, kidogo kidogo hupelekea kupoa kiroho, na hatimaye unajikuta kabisa umerudi duniani..mpaka unajiuliza nimefikaje hapa? Ni kwasababu uliendekeza uvivu wa kiroho..ulisema. nitaomba kesho, nikesha kesho, nitamtumikia Mungu mwezi ujao..mwishowe ukawa hivyo ulivyo leo…

Angalia ni eneo lipi la maisha yako limevamiwa na hawa mbweha wadogo, kisha chukua hatua za haraka kurekebisha.

Shalom

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Mwandishi wa kitabu cha wimbo uliobora.

Nini maana ya Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, (Wimbo 2:7)

Pambaja ni nini katika Biblia kama tunavyosoma katika kitabu cha Wimbo ulio bora 1:2?


 

Print this post

Kuba ni nini kibiblia?

Kuba ni kitu chenye umbo la duara kinachofunika kwa juu, ni kama paa lililopinda. Lenye mwonekano unaofanana na nusu ya mpira au bakuli lililogeuzwa juu chini.

Mifano ya kuba:

unaweza kuona kwenye ujenzi wa Misikiti mingi na baadhi ya Makanisa na majengo ya kale

Tukirudi kwenye biblia Enzi za kale, ilidhaniwa kuwa dunia ina kuba kwa juu, yaani kifuniko. Ambao ndani yake jua, mwezi na nyota hutembea..

Neno hilo utalisoma katikq vifungu hivi; 

Ayubu 22:14

[14]Mawingu mazito ni kifuniko chake, hata asione; 

Naye yuatembea juu ya kuba ya mbingu. 

Amosi 9:6

[6]Yeye ndiye avijengaye vyumba vyake mbinguni, na kuweka misingi ya kuba yake juu ya nchi; yeye ndiye ayaitaye maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya uso wa nchi; BWANA ndilo jina lake. 

Kumbuka, ujumbe unaowasilishwa hapo ni kueleza ukuu uliozidi wa Mungu, katika uumbaji wake na mamlaka yake.

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Nini maana ya Israeli?

Binti za Yerusalemu wanaotajwa katika kitabu cha Wimbo ulio Bora 1:5 ni akina nani?

Hiba ni nini? (Wimbo 3:10)

UNAJISIKIAJE, KUTEMBEA NA SANDA?

Print this post

Nini maana ya Israeli?

JIBU: Maana yake ni “yeye ashindanaye na Bwana”

Siku ile Yakobo alipotokwa na Mungu, kisha akashindana naye usiku kucha bila kumwacha, ndipo yule mtu akamuuliza jina lako nani, akasema Yakobo, akaambiwa hutaitwa tena hilo jina Yakobo, bali Israeli.

Mwanzo 32:28

[28]Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda.

Au kwa namna nyingine tafsiri yake ni

“mtu anayeng’ang’ana na Mungu mpaka kuona matokeo”

Ndio jina ambalo kabila zake zote ziliitwa. Leo hii tunaposema taifa la Israeli, tunamaanisha taifa la washindanaji.

Lakini Israeli kwa agano jipya si hii ya mwilini tu.. bali ile ya rohoni ambayo imeundwa na Yesu Kristo mwenyewe..

Warumi 2:28-29

[28]Maana yeye si Myahudi aliye Myahudi kwa nje tu, wala tohara siyo ile ya nje tu katika mwili;

[29]bali yeye ni Myahudi aliye Myahudi kwa ndani, na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko; ambaye sifa yake haitoki kwa wanadamu bali kwa Mungu.

Maana yake ikiwa umempokea Kristo, wewe tayari ni mwisraeli/myahudi.

Na kama ni mwisraeli, jua asili ya jina lako..kuwa wewe ni mtu wa kung’ng’ana na Mungu…sio mtu mwepesi mwepesi…

Usimrajie Mungu katika vitu virahisi rahisi, huyo ndio sababu kwanini tunakuwa na mifungo na mikesha, kudumu uweponi mwa Bwana wakati mwingi, kumtafuta Bwana, sio kwamba yeye ni mgumu kupatikana hapana, bali kwa asili hataki wana walioitwa kwa jina hilo wawe walegevu,

Wengi hulalamika, mbona sioni uwepo wa Mungu, mbona sioni amani ya kutosha ndani, siono furaha ya wokovu, ukiwauliza vipi juhudi yako rohoni…mmoja atasema ratiba yangu huwa ni maombi ya dk 10 kwa siku, kusoma Neno dk 10.. Sasa mtu kama huyu hawezi kuhudumiwa vema na Mungu ikiwa ameokoka…

Ndugu jitambue wewe ni nani! Ikiwa ni mwisraeli, simama kama mtu shupavu kung’ang’ana na Mungu wako, nje ya hapo, tafuta jina lingine na mungu mwingine mwenye vigezo vyake vya kukuhudumia, lakini kama ni waisraeli wa Kristo, basi ni watu wa kuliitia jina la Bwana bila kukoma (Luka 18)

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

NINI MAANA YA UKOMBOZI?

Urujuani ni nini? (Wimbo 3:10)?

PALE MAOMBI YANAPOGEUKA KUWA MAPAMBANO.

Print this post

Mtakatifu wa Israeli ni nani?

Swali: Mtakatifu wa Israeli anayetajwa katika Isaya 30:9-12 ni nani hasa? Na anakomeshwaje?


Jibu: Turejee..

Isaya 30:9 “Kwa maana watu hawa ni watu waasi, watoto wasemao uongo, watoto wasiotaka kuisikia sheria ya Bwana;

10 wawaambiao waonaji, Msione; na manabii, Msitoe unabii wa mambo ya haki, tuambieni maneno laini, hubirini maneno yadanganyayo;

11 tokeni katika njia, geukeni mtoke katika mapito; MKOMESHENI MTAKATIFU WA ISRAELI MBELE YETU”.

“Mtakatifu wa Israeli” anayezungumziwa katika maandiko hayo na mengine mengi, si mwingine zaidi ya MUNGU MWENYEZI, ALIYEUMBA MBINGU NA NCHI, Huyo ndiye aliye Mtakatifu ambaye alifanya Agano na Israeli, Tunalithibitisha hilo zaidi katika maandiko yafuatayo..

Sasa tukirejea hayo maandiko hapo anaposema “…MKOMESHENI MTAKATIFU WA ISRAELI MBELE YETU”.. kukomesha kunakozungumziwa hapo sio “kule kutoa adhabu” tunakokuelewa, bali ni kitendo cha “Kuzuia jambo lisiendelee kufanyika(kufikisha jambo kikomo)”.. Hivyo andiko hilo lilihusu watu waasi ambao hawapendi sheria za MUNGU, na hivyo wanataka kuambiwa tu maneno laini na manabii, maneno ya faraja si ya kukemewa makosa yao, na lengo la kutaka kusikia hivyo ni ili WAKOME (Yaani wasiendelee) kumwangalia MUNGU, na MUNGU pia aache kuwaangalia.

Kwahiyo Mtakatifu wa Israeli ni MUNGU MWENYEZI, na ndiye pekee anayestahili kuabudiwa na kutukuzwa, na mtu anayejitenga naye ni kwa hasara yake mwenyewe.

Isaya 48: 17 “Bwana, mkombozi wako, MTAKATIFU WA ISRAELI, asema hivi; Mimi ni Bwana, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata”.

Mistari mingine inayomtaja Mungu kama Mtakatifu wa Israeli ni pamoja na Isaya 12:6, Isaya 47:4, Isaya 17:7, Isaya 30:12,  Isaya 47:4, Isaya 48:2 na mingine mingi..

Je umemwamini YESU?.. Fahamu ya kuwa hakuna njia nyingine yoyote ya kumfikia MUNGU isipokuwa kwa kupitia yeye.

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

VILIO VINAVYOUFIKIA MOYO WANGU.

MWONGOZO WA MAOMBI YA WAHUDUMU/ WASIMAMAO MADHABAHUNI.

PALE MAOMBI YANAPOGEUKA KUWA MAPAMBANO.

HAKUNA MTU ANIONDOLEAYE, BALI MIMI NAUTOA MWENYEWE

HATARI YA KUTOKUITAFAKARI BIBLIA VIZURI?

Print this post

NINI MAANA YA UKOMBOZI?

Wakolosai 1:13 “Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake; 

14 ambaye katika yeye TUNA UKOMBOZI yaani, MSAMAHA WA DHAMBI”.

Tusome tena Waefeso 1:7..

Waefeso 1:7 “Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao UKOMBOZI WETU, MASAMAHA YA DHAMBI, sawasawa na wingi wa neema yake”. 

Kumbe! Maana ya “Ukombozi” ni “MSAMAHA WA DHAMBI”.

Kwamba Tunapopata Msamaha wa dhambi zetu, tunakuwa tumekombolewa na tena tumeokolewa na Nguvu za giza, na kuingizwa katika ufalme wa Mwana wa Pendo lake?.

Hivyo maombi makuu ya Ukombozi ni maombi ya Toba!, kwasababu tunapoomba Toba na kusamehewa katika roho tumepata ukombozi, jambo ambalo ni kuu sana.

Je umemwamini Bwana YESU na kutubu dhambi zako ili upate msamaha wa dhambi??..

Fahamu kuwa hakuna maombi yoyote ya ukombozi zaidi ya yale ya KUTUBU DHAMBI kwa kumaanisha kuziacha kwasababu adui wa kwanza wa mtu ni dhambi ikaayo ndani yake.

Hiyo ndio inayomfunga mtu, na kumharibia njia yake duniani, na njia pekee ya mtu kukombolewa na laana, vifungo, mikosi na kila aina ya vifungo ni kwa njia ya kutubu dhambi.

Ukitaka ndoa yako ikombolewe, tubu na acha uzinzi unaoufanya nje ya ndoa, kama unafanya hayo, hapo ukombozi wa ndoa utazalika wenyewe.

Ukitaka ukombozi wa kazi yako, watoto wako, na mambo yako yote suluhisho ni kutubu na kupata msamaha wa dhambi!.

Lakini tukiikwepa toba na kujitumainisha katika maombi ya kuombewa na kuvunjiwa laana, hakuna ukombozi wowote tutakaopata na hiyo ni Biblia sio theolojia wala mapokeo..

Tubu dhambi leo upate ukombozi, na ufurahie wema wa MUNGU.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Print this post

Njumu ni nini? (Wimbo 3:10)

Wimbo 3:10 “Nguzo zake alizifanyiza za fedha, Na mgongo wake wa dhahabu, Kiti chake kimepambwa urujuani, GARI LAKE LIMENAKISHIWA NJUMU, Hiba ya binti za Yerusalemu”.

Neno hili pia tunalisoma katika 1Nyakati 29:2..

1Nyakati 29:2 “Basi kwa uwezo wangu wote nimeiwekea akiba nyumba ya Mungu wangu, dhahabu kwa vitu vya dhahabu, na fedha kwa vitu vya fedha, na shaba kwa vitu vya shaba, na chuma kwa vitu vya chuma, na miti kwa vitu vya miti; vito vya shohamu, na vya kujazia, VITO VYA NJUMU, na vya rangi mbalimbali, na mawe ya thamani ya kila namna, na marimari tele.

“Njumu” ni malighafi za “kung’ara ng’ara/ kuwaka-waka” Tazama picha juu, mfano wa vazi lililonakshiwa na Njumu..

Na gari la Mfalme Sulemani kulingana na maandiko hayo ya Wimbo 3:10, lilikuwa limenakshiwa na malighafi hizo za kung’ara ng’ara, hivyo lilikuwa linavutia sana, lakini pamoja na kunakshiwa kwa vito hivo vyote vya thamani lakini bado sifa za binti Yerusalemu zilikuwa bora zaidi.

Kufahamu kwa kina Gari/Machela ya Sulemani jinsi ilivyokuwa na rangi ya Urujuani ilikuwaje fungua masomo chini ya somo hili, Bwana akubariki..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea.

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Machela ni nini (Wimbo ulio bora 3:7)

Urujuani ni nini? (Wimbo 3:10)?

Hiba ni nini? (Wimbo 3:10)

MAANA YA KUISHI NA MKE KWA AKILI.

MAUTI NA UZIMA HUWA KATIKA UWEZO WA ULIMI.

Print this post

Urujuani ni nini? (Wimbo 3:10)?

Jibu: Turejee..

Wimbo 3:10 “Nguzo zake alizifanyiza za fedha, Na mgongo wake wa dhahabu, Kiti chake kimepambwa URUJUANI, Gari lake limenakishiwa njumu, Hiba ya binti za Yerusalemu”.

“Urujuani” ni neno lingine la rangi ya “Zambarau”..

Neno hilo pia tunalisoma katika kile kitabu cha 2Nyakati 2:7..

2Nyakati 2:7 “Unipelekee basi mtu mstadi wa kazi ya dhahabu, na ya fedha, na ya shaba, na ya chuma, NA YA URUJUANI, na nyekundu, na samawi, mwenye kujua kuchora machoro, pamoja na wastadi walioko Yuda na Yerusalemu pamoja nami, aliowaweka baba yangu Daudi”.

Rangi ya Urujuani/Zambarau kibiblia iliwakilisha Enzi/Ufalme… Hivyo mtu aliyevaa Mavazi yenye rangi hiyo ya Urujuani/zambarau alifahamika kama mtu mkuu, aidha mfalme, Malkia au jemedari.

Ufunuo 7:3 “Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi.

4 Na mwanamke yule alikuwa AMEVIKWA NGUO YA RANGI YA ZAMBARAU, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake”.

Utasoma tena juu ya rangi hiyo katika.. Mithali 31:22, Yeremia 10:9, Ezekieli 27:7, na Ezekieli 27:16.

Bwana atubariki.

Mafundisho Mengine

Hiba ni nini? (Wimbo 3:10)

Kimiami ni nini? (Wimbo ulio bora 2:9).

Machela ni nini (Wimbo ulio bora 3:7)

Pambaja ni nini katika Biblia kama tunavyosoma katika kitabu cha Wimbo ulio bora 1:2?

Namna sahihi ya kusoma Neno (biblia).

Print this post

Binti za Yerusalemu wanaotajwa katika kitabu cha Wimbo ulio Bora 1:5 ni akina nani?

Swali: Katika kitabu karibia chote cha Wimbo uliobora tunaona wakitajwa sana Binti za Yerusalemu je, hawa walikuwa ni mabinti wa aina gani?..au ni wa mji wa Yerusalemu kama Biblia inavyosema hapo?

Jibu: Turejee..

Wimbo 1:5 “Mimi ni mweusi-mweusi, lakini ninao uzuri, ENYI BINTI ZA YERUSALEMU, Mfano wa hema za Kedari, Kama mapazia yake Sulemani.”

Sehemu nyingine Biblia inawaasa hawa Binti za Yerusalemu kutoyachochea mapenzi ..

Wimbo 2:7 “Nawasihi, enyi BINTI ZA YERUSALEMU, Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe”.

Sasa swali hawa Binti za Yerusalemu ni akina nani?

“Binti za Yerusalemu” au kwa lugha nyingine “Binti Sayuni” ni lugha ya mithali inayowakilisha “Jamii nzima ya watu wa Israeli”… na si Mabinti waliopo Yerusalemu tu peke yao..la! bali jamii yote ya wana wa Israeli.

Turejee maandiko yafuatayo ili tuweze kulielewa hili vizuri…

Zekaria 9:9 “Furahi sana, EE BINTI SAYUNI; piga kelele, EE BINTI YERUSALEMU; Tazama, mfalme wako anakuja kwako; Ni mwenye haki, naye ana wokovu; Ni mnyenyekevu, amepanda punda, Naam, mwana-punda, mtoto wa punda.”

Unabii huu ulimuhusu Bwana YESU kipindi anaingia Yerusalemu, ambapo jamii ya watu wote walipomwona walikata majani ya mitende na kutandaza njiani ili apite..

Yohana 12:15 “Nayo siku ya pili yake watu wengi walioijia sikukuu walisikia ya kwamba Yesu anakuja Yerusalemu;

13 wakatwaa matawi ya mitende, wakatoka nje kwenda kumlaki, wakapiga makelele, HOSANA! NDIYE MBARIKIWA AJAYE KWA JINA LA BWANA, MFALME WA ISRAELI!

14 Naye Yesu alikuwa amepata mwana-punda, akampanda, kama vile iliyoandikwa,

15 Usiogope, binti Sayuni; tazama, Mfalme wako anakuja, amepanda mwana-punda.

16 Mambo hayo wanafunzi wake hawakuyafahamu hapo kwanza; lakini Yesu alipotukuzwa, ndipo walipokumbuka ya kwamba ameandikiwa hayo, na ya kwamba walimtendea hayo”.

Umeona hapo?.. waliooimba Hosana! Hosana! si tu mabinti waliokuwepo Yerusalemu bali “ni jamii yote na marika yote!”.. ikifunua kuwa Binti za Yerusalemu ni jamii nzima wa Israeli, kuzidi kulithibitisha hilo soma pia Mika 4:8, 2Wafalme 19:20-21, Isaya 37:22, na Isaya 62:1.

Na sisi kama wakristo (wakike na kiume) tunahesabika kama Israeli ya Rohoni, hivyo sisi sote pasipo kujalisha jinsia zetu, marika yetu wala nafasi zetu, maadamu tu tumempokea YESU tunafahamika kama Binti Sayuni, au Binti za Yerusalemu.

Na Biblia inatuonya Binti za Yerusalemu, mji wa Mungu tujiepushe na dhambi, hususani Uasherati wa rohoni na mwilini.

Uasherati wa rohoni ni ibada zote za sanamu.. Je umempokea BWANA YESU KRISTO?.

Fahamu kuwa hizi ni siku za Mwisho na YESU amekaribia sana kurudi.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

DANIELI: Mlango wa 2

Machela ni nini (Wimbo ulio bora 3:7)

Pambaja ni nini katika Biblia kama tunavyosoma katika kitabu cha Wimbo ulio bora 1:2?

MAAJABU YA AGANO LA UPENDO WA KRISTO.

JE UMEJIFUNZA ULE WIMBO MPYA?

Print this post

WEWE NI NANI PALE AMBAPO WATU HAWAKUONI?

Tunasahau sana maisha yetu ya sirini, na kuweka nguvu kubwa, katika kuonekana kwetu kwa  nje mbele za watu, hatujui kuwa Darasa kubwa la Mungu kwa mwanadamu lipo katika maisha yake ya sirini.  Na Mungu humlipa mtu kwa hayo na si mengine.

Mathayo 6:4….na Baba yako aonaye sirini atakujazi.

Kujazi maana yake ni kulipa.

Ikiwa na maana, unayoyatenda sasa iwe ni mema au mabaya kwa siri, malipo yake utayaona baadaye kwa wazi.

Yusufu, kabla ya kuwekwa kuwa msimamizi wa mali yote ya Farao, alitumika kama wakili mwaminifu katika nyumba ya potifa, kwa muda mrefu. Baadaye Mungu akamlipa kwa kumpa Misri yote.

Yuda mpaka kuingiwa na shetani, hadi kumuuza Bwana wake, ni matokeo ya wizi aliokuwa anaufanya kwa siri kwa muda mrefu.

Daudi kabla ya kujazwa mafuta ya kumwangusha Goliathi, ni maisha ya sirini ya Imani aliyokuwa anayadhihirisha kule maporini kwa Mungu wake, mbele ya simba na dubu walipokuwa wanakuja kulishambulia Kundi. 1 Samweli 17:34-37)

Vilevile, kwa mtu yeyote yule, kupata kibali, kutumiwa na Mungu, kuinuliwa viwango vya kiroho..hutegemea sana hali zetu za sirini zinazoendelea sasa, Kwamfano utakuta labda huyu ni mwanakwaya, au mtumishi wa Mungu, lakini katika maisha yake ya sirini, anajichua, ni mzinzi, anakunywa pombe, Lakini kwa nje, anajionyesha kuwa ni mwema, anautunza ushuhuda wake, anavaa mavazi ya kujisitiri, anaongea kwa staha, ana juhudi katika utumishi, akidhani kuwa hilo ndio litamshawishi Mungu kumwongezea neema.

Ukweli ni kwamba hapo anapoteza nguvu, kwasababu tusipokuwa waaminifu katika madogo ya sirini, Bwana Yesu hawezi kutuaminisha katika makubwa.. Tabia mbaya za sirini, zinaharibu huduma zetu, utumishi wetu wa baadaye.

Mtu anataka apandishwe labda cheo kazini, lakini katika nafasi hiyo hiyo ya chini, anaiba,  mwingine anataka apewe cheo lakini pale pale alipo hawajali watu walio chini yake, ni mwenye wivu, . Unategemea vipi Mungu amlipe mtu kama huyu?

Kabla hujalipwa na Mungu, unakuguliwa kwanza na Mungu.

Shughulika na maisha yako ya binafsi ya sirini, kwasababu hayo ndiyo yanayokueleza utakuwa nani mbele za watu baadaye.

Nini cha kufanya..

Mwalike Bwana, akuchunguze, sirini mwako, Mawazo yako, tabia zako, matendo yako. Kisha mwombe akuponye, na baada ya hapo anza kutendea kazi uliyoyaomba.

Simamia andiko hili;

Zaburi 139:23-24

23 Ee Mungu, unichunguze, uujue moyo wangu, Unijaribu, uyajue mawazo yangu;
24 Uone kama iko njia iletayo majuto ndani yangu, Ukaniongoze katika njia ya milele

Mungu akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

USIIHARIBU TABIA YAKO KWA MAZUNGUMZO YAKO.

NIONYESHE MARAFIKI ZAKO, NIKUAMBIE TABIA ZAKO.

HII NDIO TABIA YA WATU WA KEILA, USIIGE

Print this post

PALE MAOMBI YANAPOGEUKA KUWA MAPAMBANO.

Si kila wakati maombi yatakuwa ni mazungumzo ya utulivu na amani, wakati mwingine maombi hugeuka kuwa mapambano, na ung’ang’anizi, na usumbufu. Kuna nyakati Mungu anabadilika tabia, kuonyesha kama hakujali hivi, hakusikii hivi, Sio kwamba anakuonea, au anafurahia wewe kuendelea kuteseka katika hali hiyo, hapana bali anafanya hivyo ili kukutengeneza wewe, kwa namna usiyoijua.

Ni lazima ufahamu, Mafanikio ya maombi si lazima yawe majibu, bali mafanikio ya maombi ni mabadiliko yako.  Mungu akitaka kukutengeneza, ili tegeo lako lote liwe kwake, hukawia kutimiza ombi Fulani, ili uongeze tegemeo lako lote kwake.

Imani, tumaini, ukomavu, na Upendo wa ki-Mungu, mara nyingi hujengwa katika namna hiyo ya maombi ambayo yanakugharimu kumtaabisha Mungu.

Yakobo alipomtaka Mungu ulinzi, Mungu hakuonyesha kujali hata kidogo, Hivyo mazungumzo yao, yakabadilika kutoka kuwa ya amani, hadi mapambano, wakapigana mweleka usiku kucha mpaka akajeruhiwa uvungu wa paja, ijapokuwa maombi yalikuwa ni ya ung’ang’anizi sana, ya kuumwa, ya kudhoofika, ya kuchakaa, ya kukonda, ya njaa, lakini hakujua anakwenda kubadilisha hali yake ya ndani,  alikuwa anaandiliwa kuwa ISRAELI, na sio Yakobo tena mdhaifu.(Mwanzo 32:24-28)

Fahamu kuwa maombi hufanya jambo la ziada juu ya majibu. Wakati mwingine unaweza usijibiwe kabisa hata hilo ombi unaloliomba lakini fahamu kuwa hutabaki kuwa yule yule.. Mtume Paulo, alimlilia sana Mungu (maombi ya ung’ang’anizi), kuhusu mwiba uliokuwa ubavuni mwake uondolewe, ukweli ni kwamba haukuondolewa, lakini alitoka na ufunuo mpya wa “Neema ya Mungu” ukambadilisha mtazamo wa maisha yake moja kwa moja kuhusu Mungu, Maana yake ni kuwa kama mwiba ule usingemtesa na kumlilia sana Mungu asingeielewa neema ya Mungu, ambayo mpaka leo hii tunajifunza kupitia masumbufu yake.

2Wakorintho 12:7-10

Na makusudi nisipate kujivuna kupita kiasi, kwa wingi wa mafunuo hayo nalipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani ili anipige, nisije nikajivuna kupita kiasi.
Kwa ajili ya kitu hicho nalimsihi Bwana mara tatu kwamba kinitoke.
Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.
10 Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu.

Hii ni siri ambayo wengi hawaijui, Uonapo upo kwenye Wakati mgumu na umeomba kwa namna ya kawaida huoni dalili yoyote ya kujibiwa, anza maombi ya kung’ang’ana, funga zaidi, lia zaidi, kemea zaidi, zama zaidi …Fanya hivyo kwasababu ipo kazi ya ziada Mungu anataka kuitenda ndani yako zaidi ya  majibu unayoyataka,. Usiridhike tu na maombi ya utulivu, shindana na Mungu wako, ng’ang’ana sana, ikiwa hujajibiwa jana, endelea leo, tena kwa nguvu zaidi, ukiona hali imekuwa mbaya, usipoe, shughulika na Mungu zaidi na zaidi, hakuna kukata tamaa, hakuna kurudi nyuma, kwasababu Maombi hufanya kazi nyingine ya ndani zaidi ya majibu tu..

Mwisho utauna uzuri wa Mungu, jinsi atakavyokuleta  katika matokeo bora zaidi, ambayo utamshukuru Mungu maisha yako milele. Hivyo fahamu kukawia kwake ni kwa faida yako.

Maombolezo 3:31-33

31 Kwa kuwa Bwana hatamtupa mtu Hata milele.
32 Maana ajapomhuzunisha atamrehemu, Kwa kadiri ya wingi wa huruma zake.
33 Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu. Wala kuwahuzunisha

Mungu akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

NGUVU YA MAOMBI

MWONGOZO WA MAOMBI YA FAMILIA

MWONGOZO WA MAOMBI YA KUJIKUZA KIROHO.

Print this post