Biblia inatufundisha kuwa Mazungumzo mabaya ndiyo yanayoharibu tabia njema ya mtu.
1Wakorintho 15:33 “Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema”.
Maandilizi ya dhambi karibia zote yanaanzia katika “mazungumzo”.. wanaopanga kuua wanaanzia na mazungumzo, wanaopanga kuiba wanaanzia katika mazungumzo, hali kadhalika wanaopanga kufanya zinaa na uasherani wanaanza na mazungumzo.
Kwahiyo kama mtu wa Mungu jiangalie sana aina ya mazungumzo yako hali kadhalika na mtu unayezungumza naye.
Yusufu alijua siri ya mazungumzo na hiyo ikamsaidia kushinda dhambi ya “zinaa”. Kwani maandika yanasema Yusufu hakukubali kulala na mke wa Potifa na hata KUZUNGUMZA NAYE!
Mwanzo 39:7 “Ikawa baada ya mambo hayo, mke wa bwana wake akamtamani Yusufu, akamwambia, Lala nami. 8 Lakini akakataa, akamwambia mke wa bwana wake, Tazama, bwana wangu hajui kitu kilichowekwa kwangu nyumbani, na vyote alivyo navyo amevitia mkononi mwangu. 9 Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu cho chote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe. Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu? 10 Akawa akizidi kusema na Yusufu siku baada ya siku, lakini hakumsikia alale naye, WALA AONGEE NAYE”.
Mwanzo 39:7 “Ikawa baada ya mambo hayo, mke wa bwana wake akamtamani Yusufu, akamwambia, Lala nami.
8 Lakini akakataa, akamwambia mke wa bwana wake, Tazama, bwana wangu hajui kitu kilichowekwa kwangu nyumbani, na vyote alivyo navyo amevitia mkononi mwangu.
9 Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu cho chote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe. Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu?
10 Akawa akizidi kusema na Yusufu siku baada ya siku, lakini hakumsikia alale naye, WALA AONGEE NAYE”.
Wengi tunaishia hapo kuwa Yusufu alikataa kulala naye.. lakini biblia inatuonyesha kuwa alikataa pia KUONGEA NAYE..
Huu ni mtego ambao shetani anawanasa wengi katika siku hizi za mwisho, utakuta mtu anajisifia hawezi kuanguka, lakini ni mtu alijaa mazungumzo na jinsia jingine kwa kiwango kikubwa!, ni mtu wa mizaha na utani na wa maneno maneno…hawezi kukaa bila angalau kuanzisha mazungumzo yasiyo na maana na mwingine, hawezi kutulia asipochati na mtu mwingine..
Hapo ni ngumu kushinda dhambi ya zinaa, au dhambi nyingine yeyote… Kwasababu biblia imeshasema kuwa, mazungumzo mabaya ndiyo yanayoharibu tabia ya mtu! (1Wakorintho 15:33), haihitaji maelezo mengi!
Ni lazima tu utaharibikiwa tabia ukiwa ni mtu wa mazungumzo mazungumzo yasiyo na maana… hususani na watu ambao bado hawajamjua Mungu.. na watu wa jinsia nyingine.
Chunga mdomo wako, kama unaipenda tabia yako!
Maran atha
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mada Nyinginezo:
MAZUNGUMZO MABAYA HUHARIBU TABIA NJEMA.
JIHUDHURISHE, ILI AANZISHE MAZUNGUMZO NA WEWE
ALIPO NA ATAKAPOKUWEPO BIBI-ARUSI WA YESU KRISTO.
NDIPO HUENDA AKACHUKUA PEPO WENGINE SABA.
AKAPITA KATIKA LILE SHAMBA AMBALO YAKOBO ALIMPA YUSUFU MWANAWE
Rudi nyumbani
Print this post