Jibu: Turejee..
Isaya 1:8 “Na binti Sayuni ameachwa kama kibanda katika shamba la mizabibu, kama KIPENU katika shamba la matango, kama mji uliohusuriwa”.
“Kipenu” ni kijumba kidogo kinachojengwa katikati ya Shamba, kinachomsitiri mlinzi wakati wa kulinda mazao shambani..
Ili kuzuia wezi wa mazao, na wanyama kama nyani, ngedere na wengineo pamoja na ndege inawalazimu wakulima kuweka walinzi mashambani, ili kuyaangalia mazao hayo, sasa kile kijumba cha walinzi, ambacho kinajengwa kwa ubora wa chini kwa kusudi hilo, ndicho kinachoitwa “Kipenu”.
Mara nyingi kijumba hiki, pale ambapo uvunaji umemalizika, huwa kinabaki chenyewe shambani wala hakuna mtu anakithamini tena, wanyama wanaweza kufanya makao huko na hakina thamani tena…… hali hii ya kipenu kusalia chenyewe shambani, na kupoteza uthamani wake ndio Bwana MUNGU anafananisha na jinsi Mji wa Yerusalemu (yaani binti Sayuni) ulivyoachwa..
Kutokana na maovu kuwa mengi Yerusalemu, na Bwana aliwaacha, na mji wao kubaki mpweke kama kipenu, na hivyo hatari yoyote inaweza kuukabili, na ndicho kilichotekea wakati ulipofika Yerusalemu uliachwa kama Kipenu na Nebukadreza, mfalme wa Babeli aliuhusuru na kuuharibu na kuwachukua wenyeji mateka.
Hata sasa tunapomwacha MUNGU, tunakuwa kama Kipenu katikati ya shamba lililokwisha kuvunwa. Nyumba zetu zitakuwa kipenu, roho zetu zitakuwa kama kipenu, biashara zetu zitakuwa kama kipenu na mambo yetu mengine yote yatafananishwa na vipenu.
Hautaweza kuilinda roho yako, wala nyumba yako kama utakuwa nje ya Kristo, ni lazima tu uharibifu wako utafika ghafla siku moja, Mwanadamu ameumbwa kumtegemea MUNGU siku zote, kamwe hawezi kuishi kwa kujitegemea mwenyewe, ni jambo ambalo haliwezekani na gumu sana. Bwana tu ndiye tegemeo letu na ngao yetu.
Zaburi 144:2“Mhisani wangu na boma langu, Ngome yangu na mwokozi wangu, Ngao yangu niliyemkimbilia, Huwatiisha watu wangu chini yangu”.
Bwana atubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
AKAPITA KATIKA LILE SHAMBA AMBALO YAKOBO ALIMPA YUSUFU MWANAWE
MAVUNO YAMESHAKWISHA SHAMBANI.
USIWE NA TAMAA YA CHAKULA KINGINE.
KIFO CHA REINHARD BONKEY KINAACHA UJUMBE GANI KWETU?
JE! NINAWEZA KUPOTEZA FURAHA YA WOKOVU?
Print this post
Karama kibiblia humaanisha uwezo utokao kwa Mungu wa kufanya/ kutenda mambo yaliyo juu ya uwezo wa kibinadamu katika kutimiza kusudi la ki-Mungu. Karama kwa jina lingine huitwa neema za Mungu.
Kwamfano mmoja huwepa uwezo wa kuponya magonjwa, mwingine unabii, mwingine lugha, mwingine kufundisha, mwingine kukirimu, mwingine uinjilisti N.k.
Sasa neema/karama hizi, zipo za aina kuu tatu.
1) Karama zitokazo moja kwa moja kwa Mungu mwenyewe.
Hii ni aina ya karama(neema) ambayo mtu hupewa sio kwa kuomba, au kupanga au kuchagua…hapana bali Mungu humwita mtu mwenyewe na kuweka wito ndani yake, kwamfano kwenye biblia watu kama Yeremia, Isaya, Mitume na Paulo, walichaguliwa na kupewa neema hizi kwa kusudi maalumu na uwezo maalimu ndani yako, wa kufanya kazi.
2) Karama tuzipatazo ndani ya Kristo.
Hizi hupewa kila mwamini, pindi tu anapoamini na kupokea Roho Mtakatifu. Neema hizi, Roho Mtakatifu Humgawia kila mtu kwa jinsi apendavyo yeye. Ndio hizo tuzisomazo katika (1Kor 12:8-10).
3) Karama tuzipatazo kwa msaada wa watu wengi.
Hii ni aina nyingine ya neema ambayo mtu haipokei kwa jinsi ya kivyake, bali huipokea kwa jinsi anavyohudumiwa na watu wengi ndani ya kanisa la Kristo.
Ndio hii tunaisoma katika;
2 Wakorintho 1:11
[11]ninyi nanyi mkisaidiana nasi kwa ajili yetu katika kuomba, ili, kwa sababu ya ile karama tupewayo sisi kwa msaada wa watu wengi, watu wengi watoe shukrani kwa ajili yetu.
Karama hii huja kwa maombi ya watu wengi.
Na hapa ndipo wengi hupapuuzia kwa viongozi wao. Kwasababu maendeleo ya kanisa, huduma, au madhabahu hutegemea sana uimara wa wale wabeba maono/viongozi…ikiwa wabeba maono hawaombewi kuna viwango hawatavuka hata kama watakuwa na juhudi kiasi gani, watakuwa waombaji kiasi gani, watakuwa waaminifu kiasi gani..kama hawataombewa, watabakia kwenye ngazi fulani sikuzote, lakini viwango vya juu hawatafika.
Kufanikiwa kwa Paulo, hakukutegemea tu wito wake, au utendaji kazi wa Roho Mtakatifu Peke yake, bali pamoja na watu wengi waliokuwa wanamwombea.
Kwamfano huduma hii (nuru ya upendo), inategemea maombi mengi ili iinuke. Ikiwa utaguswa kuchukua muda wako kuiombea maana yake ni kuwa unaitia nguvu viongozi na hatimaye injili inahubiriwa kwa uvumilivu na ujasiri zaidi, na watu wanamwamini Mungu na kumshukuru, matokeo yake yanakuwa kupokea thawabu kwa Mungu kwa zile shukrani.
Sisi (wana nuru ya upendo), na watumishi wengine wa Mungu tunahitaji maombi yenu sana, ili tuihubiri injili kwa ujasiri, kama alivyoomba Paulo.
Waefeso 6:18-19
[18]kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote; [19]pia na kwa ajili yangu mimi, nipewe usemi kwa kufumbua kinywa changu, ili niihubiri kwa ujasiri ile siri ya Injili;
[18]kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;
[19]pia na kwa ajili yangu mimi, nipewe usemi kwa kufumbua kinywa changu, ili niihubiri kwa ujasiri ile siri ya Injili;
Mungu awabariki
Wale mbweha wadogo, Waiharibuo mizabibu.
PALE MAOMBI YANAPOGEUKA KUWA MAPAMBANO.
ENYI WAJINGA, ACHENI UJINGA, MKAISHI