Mithali 4:23 “Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako CHEMCHEMI ZA UZIMA”.
Chemchemi kazi yake ni kutoa “maji ya kunywa” lakini pia maji ya “kustawisha mimea”.
Kama chemchemi ikitoa maji ya chumvi au ya magadi, ni wazi kuwa maji yake hayatafaa kwa matumizi yoyote yale, hivyo mahali hapo hapana uhai, watu hawawezi kuishi wala wanyama wala mimea..
Lakini kama chemchemi ikitoa maji safi yasiyo na magadi wala chumvi, na tena masafi, basi mahali pale kila kitu kitasitawi ikiwemo watu, wanyama na mimea, na hata shughuli zote nyingine za kiuchumi.
Mfano wa maji machungu na yasiyofaa ni yale wana wa Israeli waliyokutana nayo kule ‘Mara’
Kutoka 15:22 “Musa akawaongoza Israeli waende mbele kutoka Bahari ya Shamu, nao wakatokea kwa jangwa la Shuri; wakaenda safari ya siku tatu jangwani wasione maji. 23 Walipofika mahali palipoitwa Mara hawakupata kuyanywa yale maji ya Mara, kwa kuwa yalikuwa machungu; kwa ajili ya hayo jina lake likaitwa Mara. 24 Ndipo watu wakamnung’unikia Musa, wakisema, Tunywe nini? 25 Naye akamlilia Bwana; Bwana akamwonyesha mti, naye akautia katika hayo maji, maji yakawa matamu. Basi akawawekea amri na hukumu huko, akawaonja huko”.
Kutoka 15:22 “Musa akawaongoza Israeli waende mbele kutoka Bahari ya Shamu, nao wakatokea kwa jangwa la Shuri; wakaenda safari ya siku tatu jangwani wasione maji.
23 Walipofika mahali palipoitwa Mara hawakupata kuyanywa yale maji ya Mara, kwa kuwa yalikuwa machungu; kwa ajili ya hayo jina lake likaitwa Mara.
24 Ndipo watu wakamnung’unikia Musa, wakisema, Tunywe nini?
25 Naye akamlilia Bwana; Bwana akamwonyesha mti, naye akautia katika hayo maji, maji yakawa matamu. Basi akawawekea amri na hukumu huko, akawaonja huko”.
Sasa Biblia inafananisha “Mioyo yetu na chemchemi zinazotoa maji”… Maana yake yanayotoka mioyoni mwetu yanaweza kukuza, kustawisha au kudhoofisha afya zetu, wanyama wetu, mimea yetu…kwaufupi kila kitu kinachotuzunguka ikiwemo kazi zetu, elimu zetu, nafasi zetu, kibali chetu na mambo mengine yote yanategemea sana yanayotoka mioyoni mwetu.
Sasa najua utauliza haya maji machungu au matamu ni nini?.. Turejee maneno ya Bwana Yesu.
Mathayo 12:34 “Enyi wazao wa nyoka, mwawezaje kunena mema, mkiwa wabaya? Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake. 35 Mtu mwema katika akiba njema hutoa mema; na mtu mbaya katika akiba mbaya hutoa mabaya”.
Mathayo 12:34 “Enyi wazao wa nyoka, mwawezaje kunena mema, mkiwa wabaya? Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake.
35 Mtu mwema katika akiba njema hutoa mema; na mtu mbaya katika akiba mbaya hutoa mabaya”.
Tusome tena Mathayo 15:18-20…
Mathayo 15:18 “Bali vitokavyo kinywani vyatoka moyoni; navyo ndivyo vimtiavyo mtu unajisi. 19 kwa maana MOYONI hutoka MAWAZO MABAYA, UUAJI, UZINZI, UASHERATI; WIVI, USHUHUDA WA UONGO, NA MATUKANO 20 hayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi…….”.
Mathayo 15:18 “Bali vitokavyo kinywani vyatoka moyoni; navyo ndivyo vimtiavyo mtu unajisi.
19 kwa maana MOYONI hutoka MAWAZO MABAYA, UUAJI, UZINZI, UASHERATI; WIVI, USHUHUDA WA UONGO, NA MATUKANO
20 hayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi…….”.
Umeona hapo?.. kumbe moyoni ndiko kunakotoka matukano, uzinzi, wizi, uongo n.k mambo ambayo ndiyo yanayomtia mtu unajisi, na bila shaka hayo ndiyo Maji machungu yatokayo moyoni kupita kinywani, ambayo hayafai kwa kustawisha chochote…
Wengi wamepoteza na kuharibu maisha yao kwasababu ya uzinzi, na wengine kwasababu ya wizi, na wengine kwasababu ya mauaji, wapo waliopoteza kibali kwa Mungu na kwa watu kwasababu ya wizi, au uzinzi, au mauaji..wapo walipoteza kazi zao za mikono na huduma zao zilizokuwa zenye utukufu kwasababu ya uzinzi, au wizi au matukano..
Wapo walioharibu ndoa zao zilizokuwa za heshima na mfano kwasababu ya uzinzi, uongo, na mauaji (utoaji mimba) Kwanini?.. kwasababu chemchemi zao zinatoa maji machungu yanayoua ndoa, kazi, huduma, kibali, heshima na nguvu.
Yakobo 3:8 “Bali ulimi hakuna awezaye kuufuga; ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti. 9 Kwa huo twamhimidi Mungu Baba yetu, na kwa huo twawalaani wanadamu waliofanywa kwa mfano wa Mungu. 10 Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, haifai mambo hayo kuwa hivyo. 11 Je! Chemchemi katika jicho moja hutoa maji matamu na maji machungu? 12 Ndugu zangu, Je! Mtini waweza kuzaa zeituni, au mzabibu kuzaa tini? Kadhalika chemchemi haiwezi kutoa maji ya chumvi na maji matamu”.
Yakobo 3:8 “Bali ulimi hakuna awezaye kuufuga; ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti.
9 Kwa huo twamhimidi Mungu Baba yetu, na kwa huo twawalaani wanadamu waliofanywa kwa mfano wa Mungu.
10 Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, haifai mambo hayo kuwa hivyo.
11 Je! Chemchemi katika jicho moja hutoa maji matamu na maji machungu?
12 Ndugu zangu, Je! Mtini waweza kuzaa zeituni, au mzabibu kuzaa tini? Kadhalika chemchemi haiwezi kutoa maji ya chumvi na maji matamu”.
Lakini kama moyoni kukitoka mambo masafi, ambayo ni upendo, ukweli, utu wema, uvumilivu (kwa ujumla utakatifu)… hakika hiyo ni chemchemi bora inayostawisha kila kitu, maji yake yatastawisha wokovu, kazi ya Mungu, kazi ya mikono, elimu, heshima, ndoa, nafasi na mambo mengine yote mazuri.
Je wewe chemchemi ya moyo wako inatoa maji ya aina gani?.. machungu au matamu?.. Kama inatoa machungu ipo dawa leo?.. dawa hiyo ni Roho Mtakatifu… Mwamini YESU leo kisha ukabatizwe na Roho Mtakatifu ataingia ndani yako na kukutakasa moyo wako Bureeeee kabisa!
Baada ya hapo ndoa yako iliyokufa itafufuka upya, huduma yako, kazi yako, elimu yako au kitu kingine cha thamani ulichopewa na Bwana, kitafufuka kwani tayari maji yatokayo ndani yako ni masafi..
Lakini labda tayari chemchemi yako ni safi, nayo inatoa maji masafi.. bado kuna jambo lingine la ziada la kufanya nalo ni KUILINDA chemchemi yako..
Utaulinda moyo wako kwa MAOMBI, kusoma NENO, kujihadhari na ulimwengu na kushiriki ibada pamoja na watu wenye imani moja na wewe kila mara.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Mafundisho mengine:
Nini maana ya Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu?
Fahamu Maana ya Mithali 15:24 Kwa mtu mwenye akili njia ya uhai huenda juu;
MOYO ULIOELEKEA KWA MUNGU.
JE UPANGA UMEINGIA MOYONI MWAKO?.
JIHADHARI NA MANENO YASIYO NA MAANA
SWALI: Nini maana ya Yeremia 31:30 “Bali kila mtu atakufa kwa sababu ya uovu wake mwenyewe; kila mtu alaye zabibu kali, meno yake yatatiwa ganzi”.
JIBU: Zamani za agano la kale katika taifa la Israeli, kulikuwa na usemi maarufu, unaosema “Baba za watu wamekula zabibu kali, na meno ya watoto wao yametiwa ganzi”.
Kikawaida zabibu au matunda mengine yenye asidi nyingi mtu alapo , huwa meno yanatia ganzi, lakini kamwe haiwezekani mtu mwingine akatiwa ganzi kwa ulaji wa mwingine.
Hapa Waisraeli wakiwa wanamaanisha kuwa adhabu za Mungu huwa zinatembea hata kwa kizazi cha watu, Lakini Mungu kwa kinywa cha Yeremia anawasahihisha kuwa hilo si jambo lake..Anawaambia kila mtu ataadhibiwa sawasawa na uovu wake, wala watoto hawatauchukua uovu wa wazazi wao..Jambo ambalo alilirudia pia kwa kinywa cha Nabii Ezekieli (Ezekieli 18:20).
Lakini pia ukisoma muktadha wa vifungu hivyo, utaona anatoa unabii wa agano jipya ambalo atalifanya na watu wake kupitia Yesu Kristo, akimaanisha kuwa wokovu wake pia , utakuwa ni wa mtu binafsi, mmoja mmoja. Tusome habari yote tokea juu.
Yeremia 31: 27 Tazama, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapoipanda nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda, mbegu ya mwanadamu na mbegu ya mnyama. 28 Tena itakuwa, kwa kadiri nilivyowaangalia, ili kung’oa, na kubomoa, na kuangusha, na kuangamiza, na kutesa; kwa kadiri iyo hiyo nitawaangalia, ili kujenga, na kupanda, asema Bwana. 29 Siku zile, hawatasema tena, Baba za watu wamekula zabibu kali, na meno ya watoto wao yametiwa ganzi. 30 Bali kila mtu atakufa kwa sababu ya uovu wake mwenyewe; kila mtu alaye zabibu kali, meno yake yatatiwa ganzi. 31 Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda. 32 Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa mume kwao, asema Bwana. 33 Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
Hivyo vifungu hivi, vinatupa kutambua kuwa wajibu wa kulitunza agano la Mungu ni la mtu binafsi, sawasawa na alivyokuja kulifunua katika agano jipya kupitia Yesu Kristo, kwamba ijapokuwa wokovu umeachiliwa kwa wote, lakini haupokelewi kijumuiya, kifamilia, au kikabila, bali kibinafsi.
Kila mtu atalibeba furushi lake mwenyewe. (Wagalatia 6:5)
Tafsiri ya Yeremia 29:12 Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza.
Yeremia alikuwa na umri gani alipoitwa?
Mti wa MLOZI alioonyeshwa nabii Yeremia 1:12 tafsiri yake ni nini?
SWALI: Je! Ni sahihi kwa mkristo kujifunza, au kufundishwa na AI (Artificial Inteligence), mfano wa Chatgpt, deepseek n.k.
JIBU: Ili kujibu swali hili ni vema, kutambua mashine hizi za akili bandia (AI), zinafanya kazi gani.
Kwa ufupi ni kuwa AI, inafanya kazi ya kuchakata taarifa nyingi, kutoka katika vyanzo vingi vilivyopo mitandaoni, mfano vitabu, makala, sauti, machapisho n.k, na hivyo inazichanganya taarifa hizo zote kwa kuangalia muktadha unaofanana na kuzifupisha, na kukujibu.
Hivyo kimsingi, ni chombo ambacho kinatoa msaada mkubwa katika ulimwengu wa sasa, na ndio ukweli usiopingika..Kwasababu kinarahisisha utafutaji wa taarifa. Lakini pamoja na hayo haimaanishi kuwa kinatoa kwa ufasaha wote.
Sasa tukija kwenye eneo la kiroho. Je ni vema mkristo kwenda kuuliza AI, au kuandaa maombi au masomo kupitia hiyo, n.k.
Ukweli ni kwamba Imani, sio taarifa, ni zaidi ya taarifa.. Hizi AI, zinatoa tu taarifa lakini hazitoi mafunuo. Hazina pumzi ya Roho Mtakatifu ndani yake.
Ikiwa unataka kuongeza maarifa kwa sehemu fulani zinaweza kukusaidia, lakini sio kukujenga nafsi, kwani inahitaji pumzi ya Mungu na miongozo ya Mungu wewe kujengwa nafsi, na sio taarifa.
Kwamfano ikiwa wewe ni mchungaji halafu, kila inapokaribia jumapili unachowaza ni kwenda chatgpt, kuiambia ikuandalie somo la kufundisha jumapili, ndugu hapo hesabu kuwa umepotea kama sio kukengeuka… Tumia hiyo kwenye biashara zako, masomo yako, projekti zao lakini sio kwenye mambo ya kiroho. Hilo liepuke kabisa.
Kufundisha Neno inahitaji ‘Neno’ mwenyewe (Yesu) akae ndani yako, kwasababu ni UHAI sio taarifa (Waebrania 4:12) ndio hapo itakupasa kupiga magoti kwanza uombe, kwa muda mrefu, utafakari moyoni mwako, ukae kwenye utulivu wa kutosha, ndipo Mungu alipande somo lake moyoni mwako. Ambalo yeye mwenyewe anajua litakuwenda kuwagusa vipi watu wake, wenye changamoto mbalimbali, kwamfano, pengine mtu mmoja alikuwa anakaribia kwenda kujinyonga kwasababu ya ugumu wa maisha na mateso fulani, na Mungu kamwona anataka amsaidie, kwa kuliweka somo linalohusiana na mapito ya Ayubu ili ainuliwe imani. Kinyume chake kwasababu ya uvivu wako wewe unakwenda kuiambia chatgpt (akili bandia), ikuandalie somo. Halafu jumapili utakwenda na taarifa zao sio mafunuo. Badala uokoe roho inayokwenda kujinyonga, unaiambia, “leo tunajifunza kanuni kumi za kudumisha ndoa na mahusiano kibiblia”. Hapo unafanya nini sasa?
Au Neno fulani Bwana anataka kukupa la wakati wako, sasa ikiwa unakimbilia AI ikusaidie, hutaki kuchukua muda wako binafsi kutafakari na kuomba ‘jiandae kukutana na ukame wa kiroho.
Visaidizi hivi, hatupaswi kuvifanya ndio sehemu ya imani yetu, kwamba kila kitu tutegemee kule, hivi ni tone dogo sana kati ya bahari kubwa. Roho Mtakatifu alishatuandalia njia zake, kuu za kujengwa na yeye.
Wekeza zaidi, kuomba msaada kwa wakufunzi wako, viongozi wako, ndugu zako katika Kristo, wekeza katika maombi, mifungo, tafakari, na kujisomea mwenyewe Neno. kwa njia hizi hakika Bwana atasema nawe na kujengwa zaidi kuliko visaidizi. Lakini pia ikiwa pana umuhimu wa kujiongezea taarifa kwa vile unavyovijua, visaidizi hivi vitakufaa (Katika uangalizi maalumu), vinginevyo utajidumaza kiroho.
Karismatiki ni nini?
Uinjilisti kama agizo kuu la Bwana.
Vita vya kiroho, na mwamini Mpya.
WhatsApp
Mathayo 12:36 “Basi, nawaambia, KILA NENO LISILO MAANA, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu. 37 Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa”.
Mathayo 12:36 “Basi, nawaambia, KILA NENO LISILO MAANA, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu.
37 Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa”.
Mfano wa maneno yasiyo na maana ni maneno yote ya kukufuru, kulaani, kutukana, mizaha, mashindano, mazungumzo machafu, nyimbo za kidunia na mengine yanayofanana na hayo.
1. Mizaha
Unapotumia baadhi ya mistari ya kwenye Biblia au matukio kwaajili ya kufanya utani, au mzaha au vichekesho…maneno hayo utayatolea hesabu siku ile. Biblia sio kitabu cha comedy.
Zaburi 1:1 “Heri mtu yule asiyekwenda katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha”.
2. Dhihaka.
Unapotoa dhihaka juu ya Neno la Mungu, au Watumishi wa Mungu ambao unajua kabisa ni wa kweli, siku ya mwisho utatoa hesabu..
3. Mabishano na Mashindano.
Unapobishana na ukweli, kwasababu tu unataka uonekane unajua au unatafuta ushindi wa maneno.. basi fahamu kuwa siku ya mwisho utatoa hesabu ya maneno yako yote… Biblia inasema mashindano ya dini yote ni maneno yasiyo na maana..
1Timotheo 6:20 “Ee Timotheo, ilinde hiyo amana; ujiepushe na maneno yasiyo ya dini, yasiyo na maana, na mashindano ya elimu iitwayo elimu kwa uongo”
4. Kufuru
Unapotoa kufuru na kashfa juu ya kazi ya Mungu, na moyoni unajua kabisa ni kazi kamili ya Mungu, mbeleni kuna kutoa hesabu ya maneno yaliyotoka kinywani.
Mafarisayo walinena maneno ya kumkufuru Roho Mtakatifu katika kitabu hiko cha Mathayo 12, na ndio sababu ya Bwana YESU kusema maneno hayo kuwa “kila neno lisilo maana watu watatoa hesabu yake siku ya mwisho”.
5. Nyimbo za kidunia.
Maneno yaliyopo kwenye nyimbo za kidunia hayana maana na yanamtukuza shetani, na hivyo hata maneno ya nyimbo hizo yatatolewa hesabu.
Amosi 6:5 “ninyi mnaoimba nyimbo za upuzi pamoja na sauti ya vinanda, na kujifanyizia vinanda vya namna nyingi, kama vile Daudi”.
6. Mazungumzo machafu.
Mazungumzo machafu ni yale yote ya kijiweni au ya mtu na mtu, ambayo ni mazungumzo ya uasherati, ushabiki, uhuni, na mipango mibaya, matusi na mambo mengine yote mabaya.. yote hayo mtu atayatolea hesabu siku ya mwisho.
Sasa nini maana ya kutoa hesabu?
Kutoa hesabu maana yake ni kutoa “maana au tafsiri ya kina ya kile kilichotoka kinywani”. Kwamfano kama mtu umemtukana mtu na kumwita yeye ni Mbwa, basi siku ile utaeleza sababu za kumwita vile, na kama kweli yeye ni mbwa kama ulivyosema… kwaufupi maneno ambayo sisi tuliyatamka kwa utani tu na ufupi, kule yatarefushwa na kuwa mada ndefu mno.
Hivyo hatuna budi kuwa makini na yanayotoka kinywani mwetu.. kwamaana yanarekodiwa yote, na pia ni vizuri kama tumekosea kwa vinywa vyetu kuwahi kurudi kutubu kwa tuliyemtolea maneno mabaya, au tuwahi kurudi kwa Mungu kutubu ili tusiangukie hukumu.
Hukumu inakuja, hukumu inakuja, tumwamini YESU na kutubu na tuyashike sana maungamo yetu.
Ubarikiwe.
KILA MTU ATATOA HABARI ZAKE MWENYEWE.
Je mtu anayeua anabeba dhambi zote za yule aliyemuua?
UTASIMAMA PEKE YAKO SIKU ILE.
USIGEUZE JIWE KUWA MKATE.
USI..USI..USI.
Ikiwa unahitaji Maombezi, wasiliana nasi kwa namba hizi bure. Lakini ikiwa una swali na unahitaji msaada wa kimaandiko andika ujumbe wako katika fomu uionayo chini.
📞 +255 789 001 312
📞 +255 693 036 618
Jina lako
Barua Pepe
Nchi (Lazima)
Namba Ya Simu (Muhimu)
Kichwa cha Ujumbe
Ujumbe Wote
Δ
Jibu: Turejee kuanzia mstari wa 6..
Walawi 17:6 “Naye kuhani atainyunyiza damu yake juu ya madhabahu ya Bwana, mlangoni pa hema ya kukutania, na kuyateketeza mafuta yake, yawe harufu njema mbele za Bwana. 7 WALA HAWATATOA TENA SADAKA ZAO KWA WALE MAJINI, ambao huwafuata ili wafanye uasherati nao. Sheria hii itakuwa sheria ya milele kwao, kizazi baada ya kizazi”.
Walawi 17:6 “Naye kuhani atainyunyiza damu yake juu ya madhabahu ya Bwana, mlangoni pa hema ya kukutania, na kuyateketeza mafuta yake, yawe harufu njema mbele za Bwana.
7 WALA HAWATATOA TENA SADAKA ZAO KWA WALE MAJINI, ambao huwafuata ili wafanye uasherati nao. Sheria hii itakuwa sheria ya milele kwao, kizazi baada ya kizazi”.
“Majini” wanaotajwa hapo ni “mashetani”..
Katika agano la kale sadaka yoyote iliyotolewa nje ya hema ya Mungu (maana yake katika madhabahu nyingine), sadaka hiyo ilihesabika kuwa imetolewa kwa majini/mashetani, na yeyote aliyetoa sadaka yake huko, akabainika sheria ilikuwa ni kutengwa na watu wake.
Walawi 17:8 “Nawe utawaambia, Mtu awaye yote katika nyumba ya Israeli, au miongoni mwa wageni, wanaokaa nao, atoaye sadaka ya kuteketezwa au dhabihu, 9 wala haileti mlangoni pa hema ya kukutania, ili aisongeze kwa Bwana BASI MTU HUYO ATATENGWA NA WATU WAKE”.
Walawi 17:8 “Nawe utawaambia, Mtu awaye yote katika nyumba ya Israeli, au miongoni mwa wageni, wanaokaa nao, atoaye sadaka ya kuteketezwa au dhabihu,
9 wala haileti mlangoni pa hema ya kukutania, ili aisongeze kwa Bwana BASI MTU HUYO ATATENGWA NA WATU WAKE”.
Mahali pekee Bwana Mungu alipopachagua pa kutolea sadaka ni katika “HEMA YA MUNGU”, katika kipindi cha Waamuzi na katika “NYUMBA YA MUNGU” aliyoitengeneza Sulemani katika kipindi cha Wafalme na kuendelea.
Kwahiyo sadaka yoyote inayopelekwa mahali panapoabudiwa ibilisi, basi sadaka hiyo ni imetolewa kwa majini/mashetani..na sadaka inayotolewa kwa mashetani basi mtu huyo au watu hao wanakuwa na ushirika na mashetani, ndivyo Neno la Mungu linavyosema..
1Wakorintho 10:20 “Sivyo, LAKINI VITU VILE WAVITOAVYO SADAKA WAVITOA KWA MASHETANI, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi KUSHIRIKIANA NA MASHETANI. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani”.
Kwahiyo kwa hitimisho ni kwamba “majini” wanaotajwa katika Walawi 17:7 ni mashetani/mapepo ambao pia wanatajwa katika Isaya 13:21 na 2Nyakati 11:15 wakati wa mfalme Yeroboamu.
2Nyakati 11:15 “naye akajiwekea makuhani wa mahali pa juu, na wa WALE MAJINI, na wa zile ndama alizozifanya.”
Na pia zipo sadaka zitolewazo kwa Mungu na pia zitolewazo kwa mashetani, Mtu anayeenda kwa waganga wa kienyeji sadaka yake anaitoa kwa mashetani, na kafara yoyote iwe ya mnyama au kiumbe chochote inayofanyika katika agano jipya ni sadaka kwa mashetani na si kwa Mungu, kwani hatuna tena kafara za wanyama katika agano jipya, wala hakuna kafara za watu kwa Mungu na hazijawahi kuwepo huko kabla, kafara zote za namna hiyo ni za mashetani.
Zaburi 106:37 “Naam, walitoa wana wao na binti zao Kuwa dhabihu kwa mashetani. 38 Wakamwaga damu isiyo na hatia, Damu ya wana wao na binti zao, Waliowatoa dhabihu kwa sanamu”
Zaburi 106:37 “Naam, walitoa wana wao na binti zao Kuwa dhabihu kwa mashetani.
38 Wakamwaga damu isiyo na hatia, Damu ya wana wao na binti zao, Waliowatoa dhabihu kwa sanamu”
Je umempokea YESU?.. fahamu kuwa hakuna wokovu kwa mwingine yoyote isipokuwa kwake!, na tunaishi majira ya kurudi kwa YESU, huu si wakati wa kucheza na dunia, bali kujitoa kwa MUNGU.
1Petro 4:2 “Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika MAPENZI YA MUNGU, WAKATI WENU ULIOBAKI WA KUKAA HAPA DUNIANI. 3 Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali”.
1Petro 4:2 “Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika MAPENZI YA MUNGU, WAKATI WENU ULIOBAKI WA KUKAA HAPA DUNIANI.
3 Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali”.
Bwana atusaidie.
Je mapepo au majini yanaweza kuviingia vitu visivyo na uhai?
MAJINI WAZURI WAPO?
Tunathibitisha vipi kuwa Yule Malaika wa (Yohana 5:4) ni wa MUNGU?
AINA ZA MAJINI, MAJINA YAO, KAZI ZAO, NA TIBA ZAKE.
Ipi tofauti kati ya Uhai na Uzima kibiblia?
Kama mwamini ni lazima ujue kila kitakachotekea siku za mwisho, na kile Mungu alichokiahidi kuhusu maisha yajayo
Siku za mwisho zilianza wakati ule wa pentekoste Roho alipomiminwa duniani, kwa watu wote, na hizo zinaendelea hadi sasa mpaka wakati ambapo Kristo atatokea ulimwengu kwa mara ya pili kuleta hukumu na ufalme wake mpya.
Ni ukweli usiopingika kwamba tupo ukiongoni kabisa mwa siku za mwisho.Ingawa Biblia haitupi tarehe kamili (Mathayo 24:36), inatupa ishara na maagizo ya kuwa macho na wenye tumaini wa siku hiyo kuu.
Hii inaonyesha kwamba historia inaelekea kwenye mwisho ulioamriwa na Mungu.
Yesu aliahidi atarudi tena (Yohana 14:3). Kurudi kwake hakutakuwa kwa siri, bali kutakuwa kwa utukufu, nguvu na hukumu.
[11]Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni. . — Matendo 1:11
Hili si tumaini la kubahatisha — ni matumaini ya hakika yaliyowekwa juu ya ahadi za Mungu.
“Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu.” — Wakolosai 1:27
Kimaandiko, utukufu humaanisha:
Uwepo wa Mungu unaoonekana (Kutoka 33:18-20)
Utakatifu wake ulio mkuu na mkamilifu (Isaya 6:3)
Hali ya mwisho ya waamini — kufanana na Kristo milele (Warumi 8:17; 2 Wakorintho 3:18)
1 Wakorintho 15:52 [52]kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika.
Hakutakuwa na ugonjwa, uchovu, wala mauti tena. Tutakuwa na miili kama wa Yesu baada ya kufufuka kwake (Wafilipi 3:20-21).
ii) Makao ya Milele
Yesu amekwenda kutuandalia makao (Yohana 14:2). Mbingu mpya na dunia mpya hazitakuwa na huzuni, machozi wala laana (Ufunuo 21:1-5).
iv) . Kumwona Mungu Uso kwa Uso
Hatutamtazama tena kwa imani bali tutamwona moja kwa moja (Ufunuo 22:4). Tutamtumikia na kumtukuza milele (Ufunuo 22:5).
🔸Kuwa Macho
Kanisa la kwanza liliishi kwa umakini mkubwa. Wakijua kuwa Yesu anaweza kurudi wakati wowote (Tito 2:13).
→ Usicheleweshe toba wala kuwa mzembe kiroho.
🔸Ishi Maisha Matakatifu
“Kila mwenye tumaini hilo ndani yake hujitakasa, kama Yeye alivyo mtakatifu.” — 1 Yohana 3:3
Ufahamu wa kurudi kwa Kristo unapaswa kutuchochea kuishi maisha ya utakatifu na utii.
🔸 Kuwa na Tumaini
Tufahamu kuwa Majaribu haya ni ya muda. Tumaini letu ni nanga ya roho zetu (Waebrania 6:19).
🔸 Tembea na Ujumbe kwa wengine.
Milele ni halisi. Ndio maana tunahubiri Injili—kwa sababu maisha ya watu yana hatma ya milele.
“Roho na Bibi-arusi wasema, Njoo!” — Ufunuo 22:17
“Amina. Njoo, Bwana Yesu.” — Ufunuo 22:20
Sauti ya kanisa si hofu, bali ni shauku. Nyakati za mwisho si mwisho wa matumaini, bali ni mwanzo wa utukufu wa milele kwa wote waliomo ndani ya Kristo.
Mafundisho ya ziada kuhusu Siku za Mwisho.
KUWA MAKINI, HATUA ZA UNYAKUO ZINAENDELEA.
NYUMBANI MWA BABA YANGU MNA MAKAO MENGI.
SIFA SITA (6), ZINAZOIKAMILISHA ILE SIKU YA BWANA ITISHAYO.
Jehanamu ni nini?
MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 1)
DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.
MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
Biblia unapozungumzia kuhusu kupewa jina jipya inamaanisha nini?
MZEITUNI HALISI UTAKAPOPACHIKWA.
Vita vya kiroho ni mapambano yasiyoonekana kwa macho ya kawaida, yanayofanyika katika ulimwengu wa roho kati ya ufalme wa Mungu na ufalme wa giza (Shetani na mapepo yake).
Ingawa hayaonekani, lakini vita vyao ni vibaya zaidi ya vile vinavyoonekana, kwani vinamuathiri mwanadamu kotekote, mwilini lakini pia rohoni katika mawazo yetu, hisia, tabia, ndoa, huduma, na hata afya.
Biblia inasema:
Waefeso 6:12
Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho
Mfano:
Mtu anayeokoka anaweza ghafla kuanza kupata majaribu makubwa ya kuudhiwa na watenda dhambi, jambo ambalo huko nyuma hakuwahi kuliona, mpaka anawaza kwamba maisha ya wokovu ni magumu. Hili ni shambulio la kiroho, linalolenga kumrudisha nyuma kiroho.
Ulipompokea Yesu, uliingia katika Ufalme wa Mungu. Na moja kwa moja ulifanyika adui wa Shetani.
Shetani alikupoteza na sasa anafanya kila juhudi kukurudisha, kukuzuia usikue kiroho, au kukushawishi uishi maisha yasiyo ya ushindi.
“Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake.” (Wakolosai 1:13)
Maandiko yanatuambia Shetani alikuwa malaika aliyeasi (Isaya 14:12–15).
Anaendesha vita kwa kutumia uongo, hofu, mashaka, tamaa, magonjwa, migawanyiko, na kushambulia akili zetu.
Uongo – Anapandikiza mawazo kama: “Hujasamehewa” au “Mungu hajasikia maombi yako.”
Vishawishi – Hutumia tamaa za mwili, pesa, au kiburi kukushawishi.
Kuchosha kiroho – Anakufanya uchoke au kupoteza hamu ya kusoma Biblia au kuomba.
Kuvuruga mahusiano – Kupitia fitina, chuki, au hasira isiyoisha.
“Yeye ni mwongo na baba wa huo.” (Yohana 8:44)
Waefeso 6:10–18 inatupa silaha saba za kiroho za kujilinda na kushambulia nguvu za giza:
3.1 Kweli kiunoni.
Kuwa na ujuzi wa kweli ya Neno la Mungu na kuiishi.
Hii inasaidia kutambua uongo wa Shetani.
Mfano: Unapofikiri “Mungu hanipendi,” Neno la Mungu linasema “Hakika amekupenda kwa upendo wa milele.” (Yeremia 31:3)
3.2 Dirii ya Haki
Maisha ya uadilifu na kutokubaliana na dhambi.
Haki hii inatoka kwa Yesu, sio kwa matendo yako.
“Yeye asiyemjua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye.” (2 Wakorintho 5:21)
3.3 Viatu vya Injili ya Amani (utayari miguuni)
Kuwa tayari kueneza habari njema na kuishi kwa amani.
Mtu aliye tayari kushuhudia haogopi mapambano.
3.4 Ngao ya Imani
Imani huuzima mishale ya hofu, mashaka, na huzuni.
Unaposema, “Mungu atanitetea,” hata wakati hali ni ngumu, hiyo ni imani.
3.5 Chapeo ya Wokovu
Linda mawazo yako kwa kufikiri mambo yanayohusiana na wokovu wako.
Kukumbuka kwamba umeokolewa hukufanya usiyumbishwe na hila za adui.
3.6 Upanga wa Roho (Neno la Mungu)
Neno la Mungu ni silaha ya kushambulia.
Yesu alilitumia aliposhambuliwa na Shetani (Mathayo 4:1–11).
3.7 Maombi
Maombi ni silaha ya nguvu inayoweza kubadilisha hali yoyote.
Omba kwa ajili yako, familia yako, kanisa, na hata waliopotea.
Waefeso 6:18
[18]kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;
Soma Biblia kila siku – Neno la Mungu hukujenga kiroho.
Omba kila siku – Ushindi unapatikana kwa kusali daima.
Kataa dhambi kimaamuzi – Usingojee hisia, fanya uamuzi wa kiroho.
Tembea na Wakristo wengine – Ushirika hukupa nguvu.
Fanya ibada (Sifu na abudu) – Hukuza uwepo wa Mungu na huvunja vifungo vya giza.
Tubu haraka unapokosea – Usimpe shetani nafasi ya kukushitaki.
5.1 Vita vya Kiroho Sio:
Kila shida ni mapepo – Baadhi ya mambo ni matokeo ya maamuzi au mazingira. Hivyo ni wajibu kuchunguza chanzo cha tatizo ni je Adui kweli au!
Kukemea tu– Mamlaka ya kiroho hutegemea maisha ya utii kwa Kristo. Utiifu wako
Kuwa na hofu – Kwamba tuogope, au tuishi kwa mashaka, kana kwamba tuwekeze nguvu zetu zote kupambana nayo. Hapana Tuna mamlaka kupitia Yesu.
“Nimewapa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge, na kushinda nguvu zote za adui; wala hakuna kitakachowadhuru.” (Luka 10:19)
Ukiwa ndani ya Kristo, huna sababu ya kuogopa. Mapambano yapo, lakini ushindi ni wako kupitia Yesu Kristo.
“Katika mambo haya yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.” (Warumi 8:37)
Waefeso 6:11 – “Vaeni silaha zote za Mungu…”
Yakobo 4:7 – “Mtiini Mungu, mpingeni ibilisi naye atawakimbia.”
2 Wakorintho 10:4 – “Silaha za vita vyetu si za mwili…”
1 Petro 5:8 – “Muwe na kiasi na kukesha… ibilisi yenu… hutafuta mtu wa kummeza.”
Masomo ya ziada kukusaidia kuvishinda vya kiroho
NGUVU YA “KUKATAA” UNAPOPAMBANA VITA VYA KIROHO
Maana ya Mhubiri 9:18 Hekima ndiyo bora kupita silaha za vita;
JINSI YA KUPIGANA MAOMBI YA VITA.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >>
https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
BWANA ni mtu wa vita, BWANA ndilo jina lake.(Kutoka 15:3)
Mishale ya moto ya mwovu inayozungumziwa kwenye Waefeso 6:16 ni ipi?
Nini maana ya huu mstari ” Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda;”?(2Timotheo 4:7)
Kila mwamini ameitwa kuieneza injili ya Yesu Kristo. Ambayo huitwa habari njema.
Mathayo 28:19-20
[19]Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; [20]na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
[19]Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
[20]na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
Habari njema ni nini? Ni habari za wokovu kwa mwanadamu, ulioletwa na kupitia mtu mmoja Yesu Kristo kwa tendo la kufa na kufufuka kwake kaburini.
Kama tulivyotangulia kuona hapo juu, kuwa siku Yesu alipoondoka hakutuacha bila wajibu, bali kila mmoja wetu alipewa sehemu ya huduma katika shamba lake. Ya kuenenda ulimwenguni kote kuwafanya watu kuwa wanafunzi wake.
Kazi hii sehemu nyingine anaifananisha na talanta, ambayo amempa kila mwamini na anataka kila mmoja aizalishe (Mathayo 25:14-30), sehemu nyingine anaifananisha na matunda, anasema sisi ni matawi na yeye ni mzabibu kwamba tumzalie matunda, (Yohana 15:1-7),sehemu nyingine nyingine anaiita posho, huku yeye akijiita bwana, na sisi mawakili wake, akitutaka tutoe posho kwa wakati kwa watu wake, (Luka 12:42-48)
Sasa ukiangalia utaona sehemu zote hizo tunazofananishwa nazo, kama mtu hajafanya chochote au hajazalisha chochote, haachwi hivi hivi, bali kuna aidha kuondolewa sehemu ya thawabu yake, au kukataliwa kabisa.
Ndio maana ni lazima tujue mwamini yoyote yule, ni lazima aishi maisha ya kuwashuhudia wengine injili.
Warumi 10:14 Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri?
Ni lazima ujue kuwa hukumu ipo na kuzimu pia ipo, na inawameza wengi, Na watu hawawezi kuokoka tu wenyewe hivi hivi bila kusikia injili kama wewe ulivyosikia. Tengeneza picha unamwona baba yako, au mama yako kwenye ziwa la moto, halafu anakuambia laiti ningelijua ukweli nisingekuwa huku, utajisikiaje? Ukilijua hili basi huruma ya ki-Mungu itakujaa tu ndani yako, na utasukumwa kujitoa kuwaendea wenye dhambi, kama Kristo alivyotujia sisi, kutoka mbinguni, na kama mitume walivyowaendea watu, ili kuhakikisha wanaokoka.
Luka 15:7 Nawaambia, Vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa ajili ya wenye haki tisini na kenda ambao hawana haja ya kutubu
Mungu hufurahi malaika pia hufurahi, wanapoona roho za watu zinaokoka,duniani, Hivyo sisi kama wana wa Mungu ni wajibu wetu kuyatenda yale tu ambayo yanamfanya Baba yetu afurahi, na hilo si lingine zaidi ya kutoka na kwenda kuwashuhudia watu injili.Hapo tunaufanya moyo wa Mungu hufurahi sana.
Ni ukweli usiopingika kuwa kila mmoja wetu kuna mahali Mungu amemtoa mpaka hapo alipomfikisha, anayo mengi ya kushuhudia kuhusu uzuri wa Kristo.
Wazia yule kichaa ambaye alikuwa katika hali mbaya kule makaburini, uchi, usiku na mchana, ameshindikana kwa vifungo vyote. Lakini Yesu alipokutana naye saa ile ile alipona, akataka kuambatana na Yesu, lakini Yesu akamwambia nenda nyumbani kwa watu wako uwasimulie matendo makuu ambayo Mungu amekutendea, Na tunaona alikwenda kusimulia yote mji ule, na watu wengi wakamwamini Kristo, kwa ushuhuda wake tu.
Marko 5:20 Akaenda zake, akaanza kuhubiri katika Dekapoli, ni mambo gani makuu Yesu aliyomtendea; watu wote wakastaajabu
Hata wewe, wazia uzuri ulioupata pindi ulipompokea Kristo, utamani pia mwingine aupate, na huo ndio upendo, umeonja uzuri wa Kristo unakwenda kuwaambia na wengine mfano tu wa yule mwanamke pale kisimani.
Sawasawa na agizo ambalo Yesu alimwagiza yule mtu ambaye aliteswa Na mapepo akamfungua. (Marko 5:19-20)
Hii ni njia bora, ambayo utapata nguvu ya kikanisa, kwasababu mule akutanapo na vipawa mbalimbali vya Mungu, hurahisisha zaidi moyo wake, kuamini ujumbe uliompelekea.
Ishi maisha yanayomuhakisi Kristo. Kwasababu matendo yako ni injili kuwa wengine kumgeukia Kristo. (1Petro 3: 1-2)
Hivi Ni kama vitabu, kanda, luninga, na kwa dunia ya sasa, Vitu kama whatsapp, websites, panaweza pakawa mahali Ambapo injili yetu kupaa sana na kuwavuta wengi ndani ya ufalme. Ulimwengu wa sasa, upo mtandaoni, hivyo tumia fursa hiyo, kushea mafundisho, mahubiri sahihi ya Neno la Mungu kwa marafiki zako, familia, ndugu, majirani, huko huko Mungu ataanza kazi ya wokovu ndani yao.
Haya ni mambo ya kukumbuka kila uendapo kushuhudia, ili usishindwe na hofu.
Usiwe na hofu ikiwa huoni mwitikio wowote, kwa yule unayemweleza habari ya wokovu, fahamu kuwa ipo mbegu imemwingia ambayo itakuja kumea tu kwa wakati wake.
Uinjilisti wa wawili huwa mrahisi zaidi ya ule wa mmoja (isipokuwa unao uzoefu). Yesu aliwatuma wanafunzi wake wawili wawili, alijua ujasiri utaongezeka lakini wangeweza kufanya zaidi, pale mmoja anapochoka anamtia nguvu mwenzake. Vivyo hivyo na wewe katika hatua za awali ongozana na kiongozi wako, au mshirika mwenza katika kazi ya injili.
Yohana 3:16
Warumi 3:23
Warumi 6:23
Warumi 10:9–10
2 Wakorintho 5:17
Kwa mwongozo wa namna ya kutembea katika baadhi ya vifungu hivyo, pitia hili fundisho >>> NJIA/BARABARA YA WOKOVU NDANI YA KITABU CHA WARUMI.
Mafundisho ya ziada
KWANINI TUNAPASWA KWENDA KUIHUBIRI INJILI KWA UJASIRI WOTE?
IHUBIRI INJILI, KILA MAHALI KWASABABU AKUZAYE NI MUNGU.
HEKIMA NANE(8) ZA KIUINJILISTI, KATIKA KUWAVUA WATU KWA KRISTO.
JE UDHAIFU WANGU UNAWEZA KUZUIA INJILI?
KUTOKUIHUBIRI INJILI,KUNA MADHARA GANI?
KWANINI KILA MWAMINI ANAPASWA AWE MHUBIRI WA INJILI
Baraka yaweza kutokana na matendo mtu aliyoyatenda au maombi aliyoyaomba.
Kwamfano utamwona mtu anayeitwa Yabesi alimwomba Mungu ambariki na Mungu akasikia na kumbariki.
1Nyakati 4:10 “Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibarikia kweli kweli, na kunizidishia hozi yangu, na mkono wako ungekuwa pamoja nami, nawe ungenilinda na uovu, ili usiwe kwa huzuni yangu! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba”
Baraka za MUNGU zimegawanyika katika makundi makuu mawili;
1. BARAKA ZA ROHONI.
Hizi ni baraka zinazoinufaisha roho ya mtu na ndizo zenye umuhimu sana kuliko zile nyingine.
Baraka ya kwanza ya rohoni ni “WOKOVU”. Mtu aliyepata Neema ya kumwamini YESU na kuoshwa dhambi zake huyo amebarikiwa, kwasababu anao uzima wa milele.
Waefeso 1:3 “Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa BARAKA ZOTE ZA ROHONI, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo”.
Baraka ya rohoni inazaa Furaha, amani, utulivu na utakatifu kwa ujumla.
Watu waliobarikiwa rohoni hata wakose vyote vya mwilini bado wanaishi maisha ya raha, kwasababu roho zao zimebarikiwa kuwa ndani ya YESU ambaye ni kila kitu.
2. BARAKA ZA MWILINI.
Baraka za mwilini ni vyote ambavyo mtu anavipokea kutoka kwa MUNGU vyenye manufaa ya mwili, ikiwemo afya, cheo, uzao au mali.
Mfano wa watu waliobarikiwa kwa baraka za mwilini ni Sulemani, alipewa utajiri mkubwa hata baada yake hakukuwa na mtu kama yeye,
Na wengine kwenye Biblia agano la kale ni Abramu na Ayubu hawa walibarikiwa vingi na MUNGU.
Lea naye alibarikiwa kuwa na watoto wengi, Samsoni alibarikiwa nguvu za mwilini n.k
Katika Agano jipya walikuwepo akina Yusufu wa Arimathaya, (Mathayo 27:57), na wanawake si haba, akina Yoana, Suzana na wengine wengi (Luka 8:3).
Na waliobarikiwa kwa vyeo, waliomwamini Bwana YESU walikuwa wengi sana wanaume na wanawake (soma Matendo 17:12-14).
Na kubarikiwa mwilini kunaweza kuwa ishara ya kubarikiwa pia rohoni, lakini sio ishara pekee kwasababu wapo matajiri wasiomwamini YESU na walikuwepo matajiri kabla ya Bwana YESU,
Na watakuwepo matajiri wengi katika ziwa la moto (Soma Luka 16:20-34).
Na tena Bwana Yesu alisema itamfaidia nini mtu apate kila kitu halafu apate hasara ya nafsi yake (Marko 8:34).
Na pia wapo maskini ambao hawajabarikiwa baraka za mwilini lakini wamebarikiwa mambo ya rohoni..
Yakobo 2:5 “Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni, Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao?”.
Kwahiyo tukiwa wote ndani ya Kristo, hatupaswi kudharauliana kwa hali zetu, bali tunapaswa tuhudumiane kwa viwango vya baraka tulivyobarikiwa..
kwasababu yule unayemwona ni maskini wa vya mwilini huenda ni tajiri wa vya rohoni sana, ndivyo Neno la Mungu linavyosema..
Ufunuo 2:9 “Naijua dhiki yako na umaskini wako, (lakini u tajiri)…”
Na yule unayemwona hana vya rohoni kama ulivyo navyo wewe basi amebarikiwa vya mwilini, ambavyo kupitia hivyo vinahitajika kwaajili ya injili, ili mambo yote yakae katika uwiano na wote tuheshimiane.
Na pia inawezekana mtu akabarikiwa kwa vyote vya rohoni na mwilini, kwa mapenzi ya MUNGU, lakini haiwezekani mtu aliyemwamini YESU akakosa vyote..
Ikitokea dalili ya kukosa vyote basi kuna kasoro katika imani, hivyo mtu huyo anapaswa aangalie jinsi alivyosikia na anavyoenenda.
Je umempokea YESU?..huo uchungu na hofu na wasiwasi ni ishara ya kupungukiwa baraka za rohoni.
Leo hii mpokee YESU ili uanze kula matunda ya baraka za rohoni.
MAOMBI YA YABESI.
Fahamu maana ya Mithali 28:20 Mtu mwaminifu atakuwa na baraka tele;
KILA MTU NA AMCHE BABA YAKE NA MAMA YAKE.
MUNGU HANA MBARAKA MMOJA TU!..MWAMINI.
TAFUTA UZIMA WA MILELE NA SI UZIMA TU!.