Kuota unakojoa kitandani kuna maanisha nini?
Ndio ni kweli zipo ndoto zinazotokana na Mungu, na ni vizuri kuzifahamu hizo, na pia zipo ndoto zinazotokana na shetani pia hizo ni vizuri ukazifahamu.. Kama utahitaji kuzijua kwa undani bofya hapa >> Nitajuaje kama ndoto ni ya Mungu au ya Shetani?
Lakini kuna ndoto pia ambazo hazitokani na Mungu wala shetani bali zinatokana na sisi wenyewe.. Na hizo ndizo tunazoziota katika Maisha yetu kwa sehemu kubwa, naweza kusema hata Zaidi ya asilimia 90.
Tatizo linakuja ni pale watu wanapotaka ndoto zinazotokana na sisi wenyewe basi wapate tafsiri yake ya kiroho. Hilo ndio linalowafanya wengi waangukie katika tafsiri za uongo.
Lakini leo ni vizuri ukaujua ukweli juu ya ndoto za kuota unakojoa kitandani.
Biblia inasema.
Isaya 29:8 “Tena itakuwa kama mtu mwenye njaa aotapo, kumbe, anakula; lakini aamkapo, nafsi yake haina kitu; na kama mtu mwenye kiu aotapo, kumbe, anakunywa; lakini aamkapo, kumbe, anazimia, na nafsi yake inatamani; hivyo ndivyo utakavyokuwa huo wingi wa mataifa waletao vita juu ya mlima Sayuni”.
Umeuelewa mstari huo?
Ndoto kama hizi za ukota unakojoa kitandani ni ndoto zinazotokana na mwili wenyewe. Na hiyo inakuja pale kibofu chako kinapojaa sana mkojo, Na hapo ndipo ubongo wako unatengeneza matukio ambayo yatakufanya ujione kama unajiokojolea ili tu aumke, uende ukakoje.. Na kama mwili utakuwa umezidiwa sana, na ndio hapo unakuta mtu anajikojolea kweli, aidha sana au kidogo.
Mwingine utakuta anaota anakojoa mkojo ambao hauishi, au kila saa anakojoa kojoa, unaona yote hiyo mifumo tu ya mwili.
Kama vile unapolala na njaa, usiku utajiona unatafuta chakula, au unakula haushibi, huo ni mfumo wa ubongo, kukuarifu kuwa mwili unahitaji chakula. Vivyo hivyo unapojikuta katika ndoto ya kuota unakojoa kitandani, hupaswi kuwa na hofu au wasiwasi.
Ipuuzie tu, na kama inakuja mara kwa mara, hakikisha ulalapo hunywi maji mengi, au vitu vyenye maji maji, na kwa kufanya hivyo hutakaa uone tena ikikurudia.
Hivyo kuota unakojoa kitandani ni ndoto ya ubongo wetu wenyewe. Ipuuzie
Shalom.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Mada Nyinginezo:
HAPO NDIPO WATU WALIPOANZA KULIITIA JINA LA BWANA.
KIFO CHA REINHARD BONKEY KINAACHA UJUMBE GANI KWETU?
JISHUSHE ILI MUNGU AKUHUDUMIE.
WACHUNGAJI WA BWANA MAKONDENI.
KILA MMOJA WENU AJUE KUUWEZA MWILI WAKE.
Kwanini Mungu anasema “Afanyaye malaika zake kuwa pepo”?
ZIKIMBIE TAMAA ZA UJANANI! NA MTU YEYOTE ASIUDHARAU UJANA WAKO.
Rudi Nyumbani:
Print this post