Title October 2022

Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na Bwana.

SWALI: Huu mstari una maana gani?

Mithali 19:14 “Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na Bwana”.


JIBU: Mstari huo unatupa picha kuwa, kumbe vipo vitu vya kurithishwa, lakini pia kuna vitu ambavyo hatuvipati kwa kurithishwa..

Kwamfano, hapo anasema mali; kama nyumba, magari, kazi, hivi vitu mtu anaweza kuvipata kutoka kwa wazazi wake,..Lakini linapokuja suala la MKE MWENYE BUSARA.  Sio jambo la kurithishwa, au kutafutiwa na wazazi, au kupatwa kwa njia ya mali, au kwa uzuri, au kwa cheo, au kwa nguvu..Hapana, bali mke mwenye busara anatoka kwa Mungu tu! Na si sehemu nyingine.

Kumbuka hapo anasema ‘mke mwenye busara’..Sio ‘mke’…ikiwa na maana, ‘mke’ anaweza kupatikana popote tu pale, hata bar, kazini, barabarani, disco, vyuoni, mtaani, n.k. utampata.. Lakini mwenye busara, hatoki pengine isipokuwa kwa Bwana tu.

Mke mwenye busara ni yupi?

Ndio kama huyu aliyezungumziwa katika Mithali 31:10-31..Ambaye sifa zake ni; Kumcha Bwana siku zote, kuwahurumia  maskini na wahitaji, Kuishi vyema na watumwa wake, kuwa msaidizi kwa mumewe, asiye mvivu n.k. Biblia pia inasema katika 1Petro 3:1-6 mke mwenye busara ni Ni mtiifu kwa mumewe, mpole, mtulivu, ajisitiriye, aitunzaye nyumba yake.

Hivyo kumpata huyu, wala usijichoshe kwa njia za vitu au mali. Bali nenda mbele za Bwana, mwombe, mshirikishe, mpango wako, kisha yeye mwenyewe atamsogeza kwako, na utamfurahia.

Kumbuka: Kinyume chake pia ni kweli. Mume mwenye busara, hapatikani pengine popote isipokuwa kwa Bwana tu. Mume mwenye busara, ni Yule amchaye Bwana, ampendaye mke wake, kama nafsi yake mwenyewe, ailindaye familia yake, aihudumiaye nyumba yake.(Waefeso 5:25). Hivyo yakupasa umwombe Bwana, kabla ya kuchukua maamuzi ya kutafuta mke/mume.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

TUJIFUNZE JAMBO KWA WANAWAKE HAWA WAWILI.

WANA-NDOA: Baba Mkwe, Na mama Mkwe.

KWANINI NDOA NYINGI ZINAVUNJIKA? (Sehemu ya 1: Upande wa wanaume)

Je! taratibu za kufunga ndoa [yaani harusi] ni agizo la Mungu au ni mapokeo tu ya kibinadamu?

MAFUNDISHO YA NDOA.

Biblia inakataza kuapa kabisa, lakini kwanini watu wanaapa mahakamani na katika vifungo vya ndoa?

MAMBO MANNE,YANAYODHOOFISHA UOMBAJI WAKO.

KUMJUA YESU SI KUPATA UZIMA WA MILELE.

Rudi nyumbani

Print this post

NYAKATI AMBAZO NI LAZIMA TUKUTANE NAZO TU:

Katika maisha bila shaka kuna siku ambazo uliwahi kuamka asubuhi na kuona siku yako inakwenda vizuri sana, una furaha, unafanikiwa, au unautulivu, au unapokea taarifa nzuri mahali Fulani, kazini kwako, kwenye familia n,k. Lakini kuna siku ambazo unaamka huoni uzuri wowote, aidha unaumwa, unaudhiwa na watu, unapata hasara kazini, unapokea taarifa za msiba, unaibiwa, unapigwa, unapata ajali Fulani,  n.k.

Ukiwa kama mwanadamu, nyakati hizi za raha na masumbufu ni lazima ukumbukane nazo, haijalishi utakuwa ni mkamilifu kiasi gani.. Na Mungu ameruhusu iwe hivyo, ili kutaka sisi tukue vema katika hali anayoitaka yeye..

Embu tafakari maandiko haya;

Mhubiri 7:14 “Siku ya kufanikiwa ufurahi, Na siku ya mabaya ufikiri. Mungu ameifanya hiyo moja kwenda sambamba na hiyo ya pili, ili mwanadamu asipate kulijua neno lo lote litakalofuata baada yake”.

Mungu ameyaweka hayo yaende sambamba, kwamba hili lisimuache Yule, wala Yule lisimwache huyu..Haiwezekani kila siku utakayoamka asubuhi tu iwe ya furaha,..au iwe ya huzuni tu..hapana,

Sasa kwanini afanye hivyo?

Sababu zipo tatu (3)

1) Ufurahi:

Mungu anapenda kutupa furaha, hivyo zipo nyakati utaburudishwa tu na Mungu, hata kama sio sasa wakati huo utafika tu katika maisha yako. Atakufajiri tu kwa njia zake mwenyewe anazozijua. Atakatiza furaha katika siku Fulani Fulani, au katika kipindi Fulani cha maisha, Hivyo Jifunze kumfurahia Mungu wako wakati unafanikiwa, kwa kumshukuru sana..(Yakobo 5:13)

2) Ufikiri:

Sikuzote mtu huwa anafikiri vizuri anapokuwa katika shida au mateso Fulani, anapopitia kuumwa kidogo, analazwa, hapo ndipo anapojitambua kuwa yeye sio kitu, hawezi kutenda jambo lolote kwa nguvu zake, au kwa mafanikio yake, hivyo hiyo inamfanya sikuzote tumaini lake alielekeze kwa Mungu. Kwahiyo basi ujifunze kufikiri sana unapokuwa katika matatizo au masumbufu fulani, kwasababu ndicho Mungu anachokitaka hapo, zidi kuwa mwombaji, jifunze Biblia, kaa uweponi, ukishindwa kulielewa hilo utakuwa ni mtu wa kulaumu laumu, kunung’unika nung’unika ovyo sikuzote uingiapo katika vipindi hivi.(Wakorintho 8:1-10 )

3) Uwe mnyenyekevu:

Mungu anataka uhai wetu wote, tuumimine mikononi mwake, anataka kila jambo tunalolifanya tuseme BWANA akipenda, (Yakobo 4:13-16 ), anataka tukiamka asubuhi tumwombe kibali cha siku mpya, tunapomaliza siku tumshukuru..Tunapoanza mwezi mpya tumwombe, tunapomaliza tumshukuru, tunapoongeza umri mwingine wa maisha tupeleke shukrani zetu kwake.

Ndivyo Mungu alivyokusudia tuishi. Ni vizuri tuyatambue haya mapema ili tusiwe watu wa kutokuzielewa njia za Mungu wakati mwingine. Tuendelee kumcha Mungu katika majira tuyapitiayo kwa wakati huo,

Anasema pale mema au mabaya yanapokuja tu ghafla, kwa kutokujua mwenyewe..Hiyo inakupa sababu ya kujinyenyekeza, mbele za Mungu, na kumkabidhi Mungu mambo yako yote. Kwasababu hujui kama kesho utakufa au  utaendelea kuishi..Ndio maana pale anasema “ili mwanadamu asipate kulijua neno lo lote litakalofuata baada yake”

Kwa kumalizia tafakari tena maandiko haya;

Mhubiri 3:1 “Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.

2 Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati wa kung’oa yaliyopandwa;

3 Wakati wa kuua, na wakati wa kupoza; Wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga;

4 Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza;

5 Wakati wa kutupa mawe, na wakati wa kukusanya mawe; Wakati wa kukumbatia, na wakati wa kutokumbatia;

6 Wakati wa kutafuta, na wakati wa kupoteza; Wakati wa kuweka, na wakati wa kutupa;

7 Wakati wa kurarua, na wakati wa kushona; Wakati wa kunyamaza, na wakati wa kunena;

8 Wakati wa kupenda, na wakati wa kuchukia; Wakati wa vita, na wakati wa amani”.

Bwana atusaidie.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Kutazama Nyakati mbaya ni kufanyaje?.

Nyakati za kuburudishwa ni zipi? (Matendo 3:19).

NI WAKATI GANI SHETANI ANAPENDA KUMSHAMBULIA MWAMINI?

Na ulimi laini huvunja mfupa.(Mithali 25:15)

Nini maana ya kilichotarajiwa kikikawia kuja moyo huugua (Mithali 13:12)?.

Mego ni nini kama tunavyosoma katika biblia? (Mithali 17:1)

Rudi nyumbani

Print this post

UTHAMINI WITO WA PILI WA YESU ZAIDI YA ULE WA KWANZA.

Jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo libarikiwe, karibu tujifunze biblia..

Vipo vipindi viwili vya Bwana Yesu kutuita katika maisha yetu. 

Hebu tujifunze namna alivyowaita wanafunzi wake mara ya kwanza na mara ya pili, ili itusaidie na sisi kujua jinsi wito wa Mungu ulivyo..

Mara ya kwanza Bwana Yesu aliwaita wanafunzi wake kipindi wapo katika shughuli zao, ndio hapo utaona anamfuata Petro na Adrea kuwaambia wamfuate (Mathayo 4:19), baadaye tena anamfuata Mathayo katika shughuli yake ya utoza ushuru na kumwambia nifuate (Mathayo 9:9). Lakini katika wito wote wake huo, hakuwapa masharti yoyote magumu wanafunzi wake.. wengi wao aliwapa maneno ya faraja tu kuwa “watakuwa wavuvi wa watu badala ya samaki”.. wengine waliambiwa wataona mbingu zikifunguka na malaika wakishuka na kupanda juu ya Mwana wa Adamu (Yohana 1:51).

Kwahiyo wito wa kwanza kwa ufupi ulikuwa ni wito wa faraja na wa matumaini, haukuwa wito wa Masharti..

Lakini tunapokuja katika wito wa pili, tunaona Bwana Yesu akizungumza maneno mengine ambayo ni magumu kidogo… Tunaona anawaita tena kwa mara ya pili: Na wakati huu hawabagui tena kama alivyofanya hapo kwanza.. kwamba anakwenda mahali Fulani na kumtafuta Petro na Adrea peke yao!, na kuacha watu wengine, au anakwenda Forodhani na kumchagua Mathayo peke yake !, na kuacha watoza ushuru wengine..

Bali tunaona wakati huu wa pili, anawaita watu wote kwa pamoja, bila kubagua yule ni wanafunzi wake au sio wanafunzi wake, na kuwaambia maneno mengine mapya.. Na maneno hayo tunayasoma katika mstari ufuatao…

Marko 8:34  “Akawaita mkutano pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, Mtu ye yote akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe, ajitwike na msalaba wake, anifuate”

Mara ya kwanza Bwana Yesu hakutoa uhuru wa mtu yeyote kumfuata, yeye ndio alikwenda kuwatafuta akina Petro, na kuwachagua watembee naye.. Lakini mara hii ya pili, ANATOA NAFASI KWA WOTE! (wakike au wa kiume, awe mdogo au mkubwa, awe mlemavu au mzima).. na anawaambia wote (Mitume pamoja na Makutano). Kuwa mtu yeyote akitaka kumfuata, “AJIKANE MWENYEWE, AJITWIKE MSALABA WAKE AMFUATE”.

Wito huu wa pili ni kama unaufanya ule wito wa kwanza usiwe na nguvu tena!!.. Kwasababu hapa Bwana Yesu anawaita wote(wanafunzi wake pamoja na watu wa mataifa).. Pengine wakina Petro walingetemea maneno hayo waambiwe wakutano tu!, lakini wanashangaa na wao wanajumuishwa huko huko..

Wote wanapewa agizo moja! Bila upendeleo.. Maana yake ni kwamba pia alitoa mlango wa mtu yeyote kuondoka kama anataka kuondoka, haijalishi tayari alikuwa ameshaitwa hapo kwanza, haijalishi kama alikuwa tayari ameshapewa ahadi na Bwana…

Tunaweza kulithibitisha hilo katika…

Yohana 6:66  “Kwa ajili ya hayo wengi miongoni mwa wanafunzi wake wakarejea nyuma, wasiandamane naye tena.

67  Basi Yesu akawaambia wale Thenashara, JE! NINYI NANYI MWATAKA KUONDOKA?

68  Basi Simoni Petro akamjibu, Bwana! Twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele.

69  Nasi tumesadiki, tena tumejua, ya kuwa wewe ndiwe Mtakatifu wa Mungu”

Umeona hapo?.. Yule Petro ambaye aliitwa hapo kwanza kwa wito wa faraja, safari hii Bwana anamwuliza “JE UNATAKA NA WEWE UNATAKA KUONDOKA??”, anamwuliza pia na Nadhanieli ambaye aliambiwa ataona malaika wakipanda na kushuka juu ya mwana wa Adamu, “JE UNATAKA NA WEWE UNATAKA KUONDOKA??”,   maana yake ni kwamba kama wangetaka kuondoka, basi mlango upo wazi Bwana angewaruhusu wala asingembembeleza… Na ahadi zile alizowaahidiwa Bwana angewapa  wale waliokuwa tayari. (Hii inaogopesha sana!!).

Ndugu inawezekana kipindi unasikia wito wa Mungu kukuita ulikuwa unapokea maneno ya faraja kutoka kwa Bwana Yesu, na kujiona wewe ni wa kipekee sana…huenda Bwana Yesu alikwambia wazi kabisa kuwa utakuwa mtumishi wake na utawavuta wengi kwake na utakuwa Baraka kwa maelfu ya watu..

lakini nataka nikuambia kuwa “usibweteke na wito huo wa kwanza wa faraja”…”utendee kazi wito wa pili”  Kwasababu hata Petro na Yohana waliambiwa hivyo hivyo, hata Nadhanieli mara ya kwanza aliambia maneno ya faraja kama yako!..lakini baadaye Bwana Yesu aliwageukia na kuwaambia kuwa “Mtu ye yote akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe, ajitwike na msalaba wake, anifuate”…Na Bwana Yesu aliwaweka kundi moja na makutano kana kwamba hakuwahi kuwaita huko nyuma.. Kana kwamba siku hiyo ndio aliyokuwa anawaita kwa mara ya kwanza.

Ndugu yangu, huenda ulishausikia wito wa Kwanza, na sasa upo katika wito wa pili,  Amua leo kumfuata YESU upya kwa kujikana nafsi!!.. Wakina Petro, baada ya kusikia hayo maneno ndipo walipojijua kuwa wanapaswa wahakiki wito wao upya!.. Ndipo wakaamua kujikana nafsi kweli kweli na kumfuata Yesu.

Na wewe leo, achana na ukristo vuguvugu wa kujisifia maono au karama, anza kujikana nafsi na kubeba msalaba wako, kaa mbali na dhambi na ulimwengu, kwa kadiri uwezavyo, weka chini fasheni za kidunia ambazo hazimpi Mungu utukufu, acha kuvaa kikahaba, acha kuweka wigi kichwani, acha kuweka hereni na mikufu, na kuvaa nguo za kubana..ni machukizo kwa Mungu (1Timotheo 2:9), acha kuabudu sanamu, acha kufanana na watu wa ulimwengu huu….hata kama dunia nzima itakuona umerukwa na akili, hata kama ndugu na wanadamu watakwona umechanganyikiwa.. wewe mfuate Yesu, na udunia uweke nyuma, na siku ile utapokea Taji ya uzima.

Kumbuka siku zote  kuwa waitwao ni wengi, bali wateule ni wachache”(Mathayo 22:14).

Tujitahidi tuwe wateule wa Bwana Yesu.

Bwana akubariki.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

JINSI MTUME PAULO ALIVYOUTHAMINI WITO WAKE, JUU YA WENYE VYEO.

AMEFANYIKA BORA KUPITA MALAIKA!

NITAUVUTAJE UWEPO WA ROHO MTAKATIFU KARIBU NAMI?

MZAZI, JALI MAISHA YA KIROHO YA MTOTO WAKO.

MAJONZI YA MTUME PAULO KWA NDUGU ZAKE.

Rudi nyumbani

Print this post

Forodhani ni mahali gani?

Swali: Pale Forodhani, Mathayo alipokuwa ameketi ndio mahali gani? (Mathayo 9:9).

Jibu: Tusome,

Mathayo 9:9 “Naye Yesu alipokuwa akipita kutoka huko aliona MTU AMEKETI FORODHANI, aitwaye Mathayo, akamwambia, Nifuate. Akaondoka, akamfuata”

“Forodha” ni  “Nyumba au kijumba kidogo”  kinachotumika kukusanyia mapato.. Kwamfano watu wanaofanya kazi benki, huwa wanaketi ndani ya  madirisha Fulani maalumu ya kupokea au kutoa fedha, sasa vyumba vile walivyopo ndivyo vinavyoitwa “forodha” ( kwa lugha nyingine).

Hali kadhalika watu wanaofanya kazi katika mashirika ya kukusanya mapato, huwa wanaketi katika chumba maalumu chenye dirisha ambapo wanapokea fedha na kutoa risiti. Vyumba hivyo ambavyo vimetengenezwa mahususi kwaajili ya kupokea wateja na kodi zao, au ada zao, au ushuru wao ndivyo vinavyoitwa Forodha.

Katika siku hizi Forodha pia zinatengenezwa na wafanya biashara, kutokana na kutanuka kwa wigo wa kibiashara, kwamfano watu wanaofanya kazi za uwakala wa mitandao ya simu mf. Mpesa n.k huwa wanatengeneza Viforodha vidogo, kwaajili ya shughuli zao hizo za kutoa na kupokea fedha.

Lakini ni funzo gani tunalipata kwa Mathayo aliyeketi Forodhani?.. 

Mathayo alipoitwa na Bwana Yesu, muda ule ule aliitikia wito!, hakungoja kesho, wala baadaye, badala yake muda ule ule alimfuata Bwana YESU.. Ijapokuwa alikuwa yupo katika mazingira magumu ya kumfuata Bwana Yesu, lakini ilimgharimu kuacha vyote na kumfuata Yesu!. Na faida ya kumfuata Yesu, Mathayo pamoja na wenzake waliyoipata, ni kwamba walikuja  kupata mara mia kwa vile vyote walivyovipoteza, na zaidi sana walipata ahadi ya uzima wa milele.

Mathayo 19:27  “Ndipo Petro akajibu, akamwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata; tutapata nini basi?

28  Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli”.

Je ni kazi yako ndio kikwazo cha wewe kumfuata Yesu?, je ni watoto wako au mke wako au wazazi wako ndio kikwazo cha wewe kumfuata Yesu kwa moyo wako wote na nguvu zako zote?.. kama kazi yako ndio kikwazo, basi nataka leo umkumbuke Mathayo, yeye kazi yake aliona si kitu zaidi ya wito wa Mungu!.  Na mwishowe leo hii tunasoma waraka wake huu.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

JE! NI KWELI UMEMFUATA YESU?

Katika (Mathayo 25:8 na Marko 16:8) Wale wanawake walitangaza kufufuka kwa Bwana au walikaa kimya?

REKEBISHA YAFUATAYO ILI UCHUMI WAKO UKAE SAWA.

TOFAUTI YA UBATIZO WA YOHANA NA UBATIZO WA BWANA YESU

JIKANE NAFSI MTEULE WA MUNGU.

Rudi nyumbani

Print this post

HAPAKUWA NA NAFASI YA KUPITA KWA YULE MNYAMA ALIYEKUWA CHINI YANGU.

Nakusalimu katika jina kuu la mwokozi wetu Yesu Kristo. Karibu tujifunze maneno ya uzima.

Nehemia ni mtu  aliyekusudia kutoka katika moyo wake, kwenda kuukarabati ukuta wa Yerusalemu uliokuwa umebomoka, mtu huyu hakuwa nabii, wala kuhani, wala hakujulikana popote, lakini kwa kuguswa kwake moyoni kwa habari alizozisikia kuhusiana na uharibifu ule, aliumia sana, ndipo akajitia nguvu, kumwomba Mungu kibali na baadaye akapewa, na kuweza kwenda Yerusalemu kwa ajili ya kazi hiyo ya kuukarabati. Sasa hatuna muda wa kueleza historia yote, kwa muda wako waweza kusoma habari yake tangu mwanzo hadi mwisho katika kitabu hicho.

Hivyo naamini kwa kuyatazama mapito yake, utapata funzo, hata na wewe ambaye, anataka kuingia katika kazi ya kusimama “mahali palipobomoka” ili upakarabati.

Sasa wakati Nehemia anafika Yerusalemu, ili kuanza operasheni yake ya kuujenga tena ukuta ule, ilimbidi kwanza, atembee, katika malango yote, na sehemu zote za ukuta huo ili atathimini, uharibifu uliotokea, pamoja na nguvu na gharama zitakazotumika kuukarabati tena..

Biblia inatuambia, aliondoka, usiku wakati ambapo watu wamelala, akaanza kuuzunguka ukuta ule wa mji ambao ulikuwa ni mrefu sana, Kuonyesha kuwa mpango bora wa kukarabati kusudi la Mungu, huwa hashirikishwi  kila mtu, bali watu wachache sana tena, waaminifu, ambao wanaweza kuchukua mzigo wako..Tusome

Nehemia 2:11 “Basi nikafika Yerusalemu, nikakaa huko muda wa siku tatu.

12 Kisha nikaondoka usiku, mimi na watu wachache pamoja nami; wala sikumwambia mtu neno hili alilolitia Mungu wangu moyoni mwangu, nilitende kwa ajili ya Yerusalemu; wala hapakuwa na mnyama pamoja nami, ila mnyama yule niliyempanda mwenyewe”.

Anaendelea kusema…

13 Nikatoka nje usiku, kwa njia ya lango la bondeni, nikashika njia iendayo kisima cha joka, na lango la jaa; nikazitazama kuta za Yerusalemu, zilizokuwa zimebomoka; na malango yake yameteketezwa kwa moto. 14 Kisha nikaendelea mpaka lango la chemchemi, na ziwa la mfalme; LAKINI HAPAKUWA NA NAFASI YA KUPITA KWA YULE MNYAMA ALIYEKUWA CHINI YANGU.

15 Kisha nikapanda usiku kando ya kijito, nikautazama ukuta; kisha nikarudi nyuma, nikaingia kwa lango la bondeni, nikarejea hivyo.

16 Wala mashehe hawakujua nilikokwenda, wala nilivyotenda; wala sijawaambia Wayahudi, wala makuhani, wala wakuu, wala mashehe, wala watu wengine waliokuwa wakiifanya kazi hiyo. 17 Kisha nikawaambia, Mnaona hali hii dhaifu tuliyo nayo, jinsi Yerusalemu ulivyo hali ya ukiwa, na malango yake yalivyoteketezwa kwa moto; haya! Na tuujenge tena ukuta wa Yerusalemu, ili tusiwe shutumu tena.

Hapo mwanzo alipoanza safari,alikuwa na mnyama wake, Ambaye ni farasi/punda.. Mnyama Yule alimsaidia sehemu baadhi tu kufika,na kuona uharibifu uliotokea katika kuta, lakini alifika mahali, ambapo mnyama asingeweza kupita katika penyo zile, bali ni mtu tu! Hapo ndipo ikabidi amwache mnyama Yule, atembee yeye kama yeye, mguu kwa mguu, kutazama sehemu za ukuta, ndogo ndogo, za mafichoni, zilizokuwa zimeharibiwa vibaya sana na maadui zao. Asingefanya hivyo, ukarabati wake ungeishia pale pale punda alipoishia, asingekarabati kote.

Ndipo alipomaliza ziara hiyo, akarejea mjini, na kuwaambia makuhani na wahusika wote, hali ilivyokuwa.

Sasa ni nini Bwana anatufundisha katika habari hii?

Bwana anasema..

Ezekieli 22:30 “Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, atakayelitengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka, kwa ajili ya nchi, nisije nikaiharibu, lakini sikuona mtu”.

Sikuzote kusimama mahali palipomoboka si rahisi, Mungu anatafuta watu hao mfano wa Nehemia hawaoni,,ni lazima tufahamu kuwa zipo gharama kubwa sana, za kukarabati, waweza kudhani, utakwenda na taasisi, au utakwenda na ushirika, au utakwenda na kiwango Fulani cha pesa kwenye akaunti yako.. Hapana vyote hivyo vinaweza kukusaidia kwa muda tu, bali utafika wakati hivyo vyote havitakusaidia, bali itakubidi usimame wewe kama wewe, kama ni kuomba, kama ni kuhubiri, kama ni kukemea dhambi, kama ni kuanzisha jambo..

Mnyama aliye chini yako, hataweza kuvuka nawe, ndugu zako hawataweza kutembea na wewe,katika maono hayo Mungu aliyokupa juu ya kusudi lake, .. Bali ni wewe kama wewe.

Ilimpasa Nehemia afanye hivi, japokuwa alipitia changamoto nyingi, mpaka mbeleni wakawa wanamdhihaki na kumwambia, ukuta unaoujenga jinsi ulivyo dhaifu, hata mbweha wakipita juu yake utaanguka.(Nehemia 4:3), Lakini hakuvunjika moyo, yeye aliendelea  kusimama mpaka mwisho ..

Walipokuwa wanaujenga, mkono mmoja ulishika silaha, na mwingine tofali, waliujenga katika hofu, usiku kucha, Lakini mwishoni ulikamilika, katika utukufu mwingi. Na faida yake ni kwamba hadi sasa tunaisoma habari ya Mtu huyu Nehemia, na kumbukumbu lake lipo hadi leo.(Nehemia 4: 17-23)

Ndugu zipo kuta nyingi sana zilizobomolewa na ibilisi, hadi sasa Bwana anatafuta watu watakaosimama, makanisani kujenga nyumba yake, watakaosimama kwa vijana, kuwaweka kwenye misingi ya imani, watakaosimama kwa familia na watoto kuwafundisha kumcha Bwana. Watakaosimama katika Neno la Mungu, kufundisha injili ya kweli isiyoghoshiwa, na kukemea mafundisho potofu..

Swali ni Je! Sisi tutaweza kusimama na kujenga upya?

Kama ni hivyo basi tuwe tayari hata wakati mwingine kusimama peke yetu, kama Nehemia, pale ambapo hatuona sapoti, uwe ndio wakati wa kusonga mbele, na kuitenda kazi ya Mungu, pale ambapo tunaona vita, na dhihaka, tusife moyo bali uwe ndio tuifanye kazi, usivunjike moyo wala usikate tamaa..Kwasababu Kujenga kuna gharama. Lakini faida zake ni kubwa sana mwishoni.

Bwana atusaidie.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Kisima cha joka na lango la jaa ni nini?(Nehemia 2:13)

Wana wa Asafu ni akina nani katika biblia?

Mlango uitwao “Mzuri” Unaozungumziwa katika Matendo 3:2 ndio upi?

TIMAZI NI NINI

UFUNUO: Mlango wa 17

Pango la Makpela ni lipi, je lina umuhimu wowote kwetu?

Neno Buruji lina maana gani katika biblia?

Rudi nyumbani

Print this post