NYAKATI AMBAZO NI LAZIMA TUKUTANE NAZO TU:

NYAKATI AMBAZO NI LAZIMA TUKUTANE NAZO TU:

Katika maisha bila shaka kuna siku ambazo uliwahi kuamka asubuhi na kuona siku yako inakwenda vizuri sana, una furaha, unafanikiwa, au unautulivu, au unapokea taarifa nzuri mahali Fulani, kazini kwako, kwenye familia n,k. Lakini kuna siku ambazo unaamka huoni uzuri wowote, aidha unaumwa, unaudhiwa na watu, unapata hasara kazini, unapokea taarifa za msiba, unaibiwa, unapigwa, unapata ajali Fulani,  n.k.

Ukiwa kama mwanadamu, nyakati hizi za raha na masumbufu ni lazima ukumbukane nazo, haijalishi utakuwa ni mkamilifu kiasi gani.. Na Mungu ameruhusu iwe hivyo, ili kutaka sisi tukue vema katika hali anayoitaka yeye..

Embu tafakari maandiko haya;

Mhubiri 7:14 “Siku ya kufanikiwa ufurahi, Na siku ya mabaya ufikiri. Mungu ameifanya hiyo moja kwenda sambamba na hiyo ya pili, ili mwanadamu asipate kulijua neno lo lote litakalofuata baada yake”.

Mungu ameyaweka hayo yaende sambamba, kwamba hili lisimuache Yule, wala Yule lisimwache huyu..Haiwezekani kila siku utakayoamka asubuhi tu iwe ya furaha,..au iwe ya huzuni tu..hapana,

Sasa kwanini afanye hivyo?

Sababu zipo tatu (3)

1) Ufurahi:

Mungu anapenda kutupa furaha, hivyo zipo nyakati utaburudishwa tu na Mungu, hata kama sio sasa wakati huo utafika tu katika maisha yako. Atakufajiri tu kwa njia zake mwenyewe anazozijua. Atakatiza furaha katika siku Fulani Fulani, au katika kipindi Fulani cha maisha, Hivyo Jifunze kumfurahia Mungu wako wakati unafanikiwa, kwa kumshukuru sana..(Yakobo 5:13)

2) Ufikiri:

Sikuzote mtu huwa anafikiri vizuri anapokuwa katika shida au mateso Fulani, anapopitia kuumwa kidogo, analazwa, hapo ndipo anapojitambua kuwa yeye sio kitu, hawezi kutenda jambo lolote kwa nguvu zake, au kwa mafanikio yake, hivyo hiyo inamfanya sikuzote tumaini lake alielekeze kwa Mungu. Kwahiyo basi ujifunze kufikiri sana unapokuwa katika matatizo au masumbufu fulani, kwasababu ndicho Mungu anachokitaka hapo, zidi kuwa mwombaji, jifunze Biblia, kaa uweponi, ukishindwa kulielewa hilo utakuwa ni mtu wa kulaumu laumu, kunung’unika nung’unika ovyo sikuzote uingiapo katika vipindi hivi.(Wakorintho 8:1-10 )

3) Uwe mnyenyekevu:

Mungu anataka uhai wetu wote, tuumimine mikononi mwake, anataka kila jambo tunalolifanya tuseme BWANA akipenda, (Yakobo 4:13-16 ), anataka tukiamka asubuhi tumwombe kibali cha siku mpya, tunapomaliza siku tumshukuru..Tunapoanza mwezi mpya tumwombe, tunapomaliza tumshukuru, tunapoongeza umri mwingine wa maisha tupeleke shukrani zetu kwake.

Ndivyo Mungu alivyokusudia tuishi. Ni vizuri tuyatambue haya mapema ili tusiwe watu wa kutokuzielewa njia za Mungu wakati mwingine. Tuendelee kumcha Mungu katika majira tuyapitiayo kwa wakati huo,

Anasema pale mema au mabaya yanapokuja tu ghafla, kwa kutokujua mwenyewe..Hiyo inakupa sababu ya kujinyenyekeza, mbele za Mungu, na kumkabidhi Mungu mambo yako yote. Kwasababu hujui kama kesho utakufa au  utaendelea kuishi..Ndio maana pale anasema “ili mwanadamu asipate kulijua neno lo lote litakalofuata baada yake”

Kwa kumalizia tafakari tena maandiko haya;

Mhubiri 3:1 “Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.

2 Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati wa kung’oa yaliyopandwa;

3 Wakati wa kuua, na wakati wa kupoza; Wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga;

4 Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza;

5 Wakati wa kutupa mawe, na wakati wa kukusanya mawe; Wakati wa kukumbatia, na wakati wa kutokumbatia;

6 Wakati wa kutafuta, na wakati wa kupoteza; Wakati wa kuweka, na wakati wa kutupa;

7 Wakati wa kurarua, na wakati wa kushona; Wakati wa kunyamaza, na wakati wa kunena;

8 Wakati wa kupenda, na wakati wa kuchukia; Wakati wa vita, na wakati wa amani”.

Bwana atusaidie.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Kutazama Nyakati mbaya ni kufanyaje?.

Nyakati za kuburudishwa ni zipi? (Matendo 3:19).

NI WAKATI GANI SHETANI ANAPENDA KUMSHAMBULIA MWAMINI?

Na ulimi laini huvunja mfupa.(Mithali 25:15)

Nini maana ya kilichotarajiwa kikikawia kuja moyo huugua (Mithali 13:12)?.

Mego ni nini kama tunavyosoma katika biblia? (Mithali 17:1)

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments