Kitabu hichi kama kinavyojitambulisha katika mwanzo wake ‘Waraka wa kwanza wa Paulo mtume kwa Wathesalonike’.
Paulo ndiye mwandishi wa waraka huu. Aliuandika akiwa Korintho. Tumelijua hilo kufuatana na ujio wa Timotheo kutoka Makedonia na kumpa ripoti nzuri ya maendeleo yao ya kiroho, kuanzia eneo la imani, upendo na tumaini, ambazo tunazisoma katika kitabu cha Matendo ya mitume sura ya 18.
Kwasababu ya ugumu wa kuwafikia uliochangiwa na shetani, Akasukumwa kuandika nyaraka hizi mbili kwa watakatifu hawa, kuwajenga katika maeneo kadha wa kadha, ambazo zilipishana kwa miezi kadhaa tu.
Kitabu hichi kina sura tano (5)
Maudhui kuu ya waraka huu ni matatu(3)
Tuyaangalie hayo maeneo matatu kwa ufupisho;
Paulo anaanza kwa kuwashuhudia kwa maneno mengi dhiki alizozipata katika kuieneza injili kwao, na jinsi alivyoweza kustahimili, Na kwamba wao pia wanapopitia dhiki za namna mbalimbali kutoka kwa watu wa taifa lao, wasivunjike moyo na kuiacha imani. Wajue kuwa dhiki pia wamewekewa watakatifu.
1 Wathesalonike 2:14
[14]Maana ninyi, ndugu, mlikuwa wafuasi wa makanisa ya Mungu yaliyo katika Uyahudi, katika Kristo Yesu; kwa kuwa mlipata mateso yale yale kwa watu wa taifa lenu wenyewe, waliyoyapata na hao kwa Wayahudi;
[15]ambao walimwua Bwana Yesu, na hao manabii, na kutuudhi sisi; wala hawampendezi Mungu, wala hawapatani na watu wo wote;
1 Wathesalonike 3:3
[3]mtu asifadhaishwe na dhiki hizi; maana ninyi wenyewe mnajua ya kuwa twawekewa hizo.
Paulo anagusia maeneo mengi kuanzia upendo hadi utakatifu kwamba wana wajibu wa kuongezeka katika hivyo ili wasionekane katika lawama katika siku ile ya kuja Bwana wetu Yesu Kristo kutoka mbinguni.
1 Wathesalonike 3:12-13
[12]Bwana na awaongeze na kuwazidisha katika upendo, ninyi kwa ninyi, na kwa watu wote, kama vile sisi nasi tulivyo kwenu;
[13]apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote.
> Anagusia pia katika eneo la kudhibiti miili yetu katika utakatifu na heshima na sio katika tamaa mbaya(4:1-5),
> Halikadhalika wakristo kuonyesha mwenendo wa adabu kwa walio nje, kwa kutenda shughuli zetu wenyewe ili tusiwe na uhitaji wa vitu vyao (4:11-12)
> Pia kama watakatifu ni mwiko kulipana baya kwa baya (5:15),
> Tunapaswa sikuzote tudumu katika kuomba, kufurahi, kushukuru kwa kila jambo, tusimzimishe Roho, tusipuuzie unabii, tujitenge na ubaya wa kila namna.(5:16-23)
> Lakini Paulo anahimiza mwenendo wetu unapaswa uende mpaka kwa wale wanaotusimamia na kutuchunga kwamba tuwastahi.
1 Wathesalonike 5:12-13
[12]Lakini, ndugu, tunataka mwatambue wale wanaojitaabisha kwa ajili yenu, na kuwasimamia ninyi katika Bwana, na kuwaonyeni;
[13]mkawastahi sana katika upendo, kwa ajili ya kazi zao. Iweni na amani ninyi kwa ninyi.
> Na katika yote ni wajibu wetu sote kufarijiana na kuonyana na kuvumiliana na kutiana nguvu(5:14-15)
Paulo anawafiriji kwa kuwaambia wafu waliolala katika Kristo, siku ya mwisho wataamshwa wote..wasidhani kuwa hawatawaona wapendwa wao waliotangulia.
1 Wathesalonike 4:13-16
[13]Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini.
[14]Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye.
[15]Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti.
[16]Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.
Sambamba na hilo, anawafumbua macho juu ya nyakati na majira ya kurudi kwa Yesu kwamba hakutakuwa na taarifa zozote au viashiria vyovyote kwa watu wa dunia. Bali itawajilia kwa ghafla tena katika nyakati ambazo wanasema kuna amani na shwari.
Hivyo anawatahadharisha watakatifu nao kuwa macho wakati wote.
1 Wathesalonike 5:1-11
[1]Lakini, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira, hamna haja niwaandikie.
[2]Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.
[3]Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.
[4]Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi.
[5]Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi si wa usiku, wala wa giza.
[6]Basi tusilale usingizi kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi.
[7]Maana walalao usingizi hulala usiku, pia na walewao hulewa usiku.
[8]Lakini sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, hali tukijivika kifuani imani na upendo, na chapeo yetu iwe tumaini la wokovu.
[9]Kwa kuwa Mungu hakutuweka kwa hasira yake, bali tupate wokovu, kwa Bwana wetu Yesu Kristo;
[10]ambaye alikufa kwa ajili yetu, ili tuishi pamoja naye, kwamba twakesha au kwamba twalala.
[11]Basi, farijianeni na kujengana kila mtu na mwenzake, vile vile kama mnavyofanya.
Hivyo kwa ufupi ni kuwa waraka huu. Unawataka wakristo kuthibitika katika imani, haijalishi ni changamoto gani za kimaisha au ugumu gani watakutana nao kwa wapinga-kristo, Wanapaswa waendelee kusimama hivyo hivyo mpaka mwisho katika Kristo Yesu.
Lakini pia wajue Bwana anarudi, na atakuja ghafla, Hivyo yawapasa wawe watu wa mchana sikuzote wasilale usingizi kwa kuhakikisha wanaishi maisha ya utakatifu, na adabu, ili atakaporudi Bwana wasiwe na lawama yoyote.
Bwana akubariki.
Je! Umeokoka? Kama ni la, fungua hapa kwa mwongozo wa sala ya wokovu. >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
SWALI: Nini maana ya 2 Wakorintho 8:9
isemayo alikuwa maskini ili sisi tuwe matajiri kwa umaskini wake.
2 Wakorintho 8:9
[9]Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.
JIBU: Katika sura hii mtume Paulo anawaandikia wakorintho juu ya huduma ya utoaji kwa watakatifu walio maskini katika makanisa mengine, ya mbali
Na hapa anawasisitiza kukubali kutoa kwa kufuata kielelezo cha Kristo katika eneo la neema yake..Jinsi alivyokubali kuwa maskini, kwa kuacha enzi na utukufu na mamlaka juu mbinguni, na kuja duniani, katika hali ya chini sana (ijapokuwa hakuwa duni), ili tu atukomboe sisi tulio katika hali ya ufukara wa roho.
Kwasababu kama asingeweza kujishusha vile, na kukubali kuhesabiwa si kitu (ijapokuwa alikuwa na nguvu), matokeo yake ni kwamba asingekwenda msalabani kusulubiwa kwa ajili yetu tena uchi, na mwisho wake kusingekuwa na msamaha wa dhambi.
Isaya 53:3
[3]Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu.
Lakini sasa tumepokea neema na utajiri wote wa rohoni kupitia yeye kujishusha kwake.
Waefeso 1:3
[3]Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;
Vivyo hivyo Mtume Paulo anawahimiza Wakorintho waige mfano huo huo, katika eneo la kuwahudumia watakatifu wengine. Akitumia mfano wa Wamakedonia ambao walikuwa ni maskini, na wenye dhiki lakini walikuwa tayari kutoa kwa moyo na furaha kwa watakatifu maskini waliokuwa Yerusalemu.
2 Wakorintho 8:1-3
[1]Tena ndugu zetu, twawaarifu habari ya neema ya Mungu, waliyopewa makanisa ya Makedonia;
[2]maana walipokuwa wakijaribiwa kwa dhiki nyingi, wingi wa furaha yao na umaskini wao uliokuwa mwingi uliwaongezea utajiri wa ukarimu wao.
[3]Maana nawashuhudia kwamba, kwa uwezo wao, na zaidi ya uwezo wao, kwa hiari yao wenyewe walitoa vitu vyao;
Halikadhalika Bwana anataka na sisi tuhudumiane katika ufahamu wa Kristo, yaani kuwa tayari kuwasaidia watakatifu wengine hata katika hali zetu za dhiki.
Lakini mtazamo ambao si sahihi kuhusiana na vifungu hivi ni kudhani kwamba andiko hilo moja kwa moja linamaanisha lengo la Bwana Yesu kuwa maskini duniani ni ili sisi tuwe matajiri kifedha. Ni kweli kupitia Yesu, tunabarikiwa mwilini, lakini hicho sio kinachozungumziwa hapo. Bwana Yesu kuwa maskini ni kutupa utajiri wa roho zetu, pamoja na ule wa ulimwengu ujao.
Bwana akubariki.
Shalom
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >>
https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Kama isingekuwa hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi ( 1 Wakorintho 7:14)
Nini maana ya waambatane na Bwana kwa kusudi la moyo? (Matendo 11:23)
Rudi Nyumbani
SWALI: Je! kulingana na mstari huu, watoto wa wapagani hawataokolewa?
1 Wakorintho 7:14
[14]Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa katika mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa katika mumewe; kama isingekuwa hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi; bali sasa ni watakatifu.
JIBU: Ukianzia juu utaona andiko hilo linazungumzia juu ya wandoa wanaoishi pamoja lakini mmojawapo hajaamini. Bwana anatoa agizo kwamba ikiwa bado huyo ambaye hajaamini anaona sawa kuendelea kuishi naye, basi yule aliyeamini asimwache.
Kwasababu kwa kupitia njia hiyo, yule asiyeamini hutakaswa na yule aliyeamini Pamoja na watoto wake pia.
Lakini je mstari huo unamaanisha kuwa mwanandoa mmoja katika familia akiokoka, basi ameiponya familia yote mpaka watoto wake?
Jibu ni la! andiko hilo halikumaanisha hivyo.
Bali linamaanisha kuwa, kwa kupitia yeye, ni rahisi wao kuambukizwa imani na hatimaye kufanya uamuzi wa kuokoka.
Wokovu hauji kwa kurithishana au kwa ‘niaba-ya’ bali kwa mtu mwenyewe kufanya maamuzi binafsi mara baada ya kushawishwa na injili.
Hata sasa tumeona shuhuda nyingi watu wakiwavuta ndugu zao kwa Kristo, aidha kwa injili au mienendo yao, na hatimaye wote kugeuka.
1 Petro 3:1-2
[1]Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno;
[2]wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu.
Hivyo kwa hitimisho, watu wote, haijalishi wakubwa au wadogo, aidha wa waamini au wapagani, wote wanahitaji kumwamini Yesu ndipo waokolewe dhambi zao. Lakini hiyo huja kwa ushawishi wetu, kwa jinsi tunavyosema nao, tunavyoenenda katika mwenendo wetu mzuri, tunapozifanya nyumba zetu kuwa makao ya ibada, ni njia rahisi ya kuwashawishi.
Bwana akubariki.
Washirikishena akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >>
https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Rudi Nyumbani
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine: