Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe daima. Karibu tujifunze Maneno ya uzima.
Siku zote tunavyolijua Neno la Mungu ndivyo tunavyozidi kuwa na amani na ujasiri zaidi wa kusonga mbele kwasababu biblia inasema.. Neno lake ni taa ya miguu yetu, Na mwanga wa njia zetu (Zab 119:105).
Leo kwa neema za Bwana tutajifunza tena kisa cha Yohana Mbatizaji,. Kama tunavyoijua habari yake Yohana alikuwa ni mkuu zaidi ya nabii yeyote aliyewahi kutokea kulingana na maneno ya Bwana wetu Yesu, na kwamba tangu wakati wake, kurudi nyuma hakuna nabii yote aliyemzidi kwa ukuu mbinguni, si Eliya, si Isaya, si Yeremia, si Musa wala si mwingine yeyote yule.
Lakini pamoja na ukuu wake wote, kuna wakati alimtilia shaka Bwana Yesu..Japokuwa aliisikia kabisa sauti kutoka mbinguni ikimshuhudia kuwa Yesu ndiye mwana pekee wa Mungu, aliyependezwa naye..Japokuwa alimwona Roho Mtakatifu akishuka juu yake kama hua, kumtia mafuta..Lakini kuna wakati alifikia kumtilia shaka..
Japokuwa aliwashuhudia wanafunzi wake, na watu wengine kuwa Yule kweli ni mwana wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu, mpaka baadhi ya waliokuwa wanafunzi wake wakamwacha, wakafuatana na Yesu, lakini alikuja kumtilia shaka wakati fulani.
Hiyo ilitokea siku moja akiwa gerezani akawatuma wanafunzi wake, kumfuata Yesu ili kumuuliza, je! yeye kweli ni Yule mwokozi wa ulimwengu waliyekuwa wanamsubiria au wamtazamie mwingine..?
Jaribu kutafakari maneno hayo, mtu ambaye maisha yake yote amekuwa akimshuhudia, na ambaye ndiye aliyetiwa mafuta na Mungu kumtengenezea njia leo hii, anauliza tena kana kwamba alikuwa hana uhakika kuwa yeye ndiye..
Mathayo 11:1 “Ikawa Yesu alipokwisha kuwaagiza wanafunzi wake kumi na wawili, alitoka huko kwenda kufundisha na kuhubiri katika miji yao.
2 Naye Yohana aliposikia huko gerezani matendo yake Kristo, alituma wanafunzi wake, kumwuliza,
3 Wewe ndiwe yule ajaye, au tumtazamie mwingine?
4 Yesu akajibu akawaambia, Nendeni mkamweleze Yohana mnayoyasikia na kuyaona;
5 vipofu wanapata kuona, viwete wanakwenda, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa habari njema.
6 NAYE HERI AWAYE YOTE ASIYECHUKIZWA NAMI.
Unadhani ni kwanini Yohana alisema vile? Alisema vile kwasababu “alimtazamia zaidi ya matazamio yenyewe kwa wakati ule”, Pengine alitazamia Bwana Yesu atakwenda kukaa kama mfalme awaokoe Israeli na maadui zao, kama maandiko yanavyosema, lakini akashangaa, mbona havutiwi hata na mambo ya ufalme wa duniani hii!!..Alitazamia atakaa kuwahukumu Israeli kwa mkono wa Mungu kama maandiko yanavyosema!, lakini yeye anamwona ndio kwanza anawahubiria wenye dhambi na maskini habari njema..Alitazamia atakuwa tajiri kwasababu ya ufalme wake, lakini anamsikia analala kwenye milima, hana hata kibanda n.k..
Unaona? Si kwamba matazamio yake yalikuwa ni uongo hapana, yalikuwa ni kweli lakini si katika wakati husika.
Ndipo Yesu aliposikia hivyo, akawatuma wale watu kumrudishia ujumbe juu ya kazi alizokuwa anazifanya..Na mwisho kabisa akamalizia na kuwaambia “Heri awaye yote asiyechukizwa nami”
Au kwa namna nyingine heri mtu Yule asiyekwazwa na haya niyafanyayo sasa..
Ndivyo ilivyo hata leo, mawazo kama hayo yapo miongoni mwetu kanisa la leo, si watumishi, si washirika.. wote.
Tunasema Yesu wewe ni mkuu, ni tajiri, nimempokea siku nyingi, nimesoma shuhuda zake, na mambo yake makuu aliyoyafanya kwenye biblia, na aliyowafanyia watu wengine, lakini mbona sioni akinibadilisha maisha yangu, na uchumi wangu.? Huyu ni Yule kweli wa kwenye biblia, au nimtazamie mwingine?
Bwana anasema.. Heri awaye yote asiyechukizwa nami.
Ndugu yangu, usivunjwe moyo ukamwacha Yesu, kisa tu hajakuponya ugonjwa wako ulionao kwa muda mrefu..
Usichukizwe na Yesu kisa tu hajayajibu maombi yako uliyokuwa unamwomba kwa muda mrefu.. Si kila jambo ni lazima ujue sababu yake leo, wewe endelea kumwamini tu..Anasema heri mtu Yule asiyechukizwa nami.
Hujui kesho kakupangiaje.. Wale walioweza kumvumilia Bwana Yesu mpaka dakika za mwisho ndio waliokuja kumjua yeye vizuri alikuwa ni nani, walijua kuwa kumbe itampasa aje mara mbili, kumbe mara ya kwanza ilikuwa ni kwa lengo la kuwaokoa watu dhambi zao, na mara ya pili ndio itakuwa ni ya kuketi kama Mfalme wa Wafalme na kuwahukumu mataifa, na kutawala pamoja na watakatifu wake..Na kwamba yeye ndiye atakayeshika utajiri wote wa mataifa. Lakini wao waliokuwa wanataka yatokee yote kwa wakati mmoja, hapo ndipo walipokosa shabaha.
Kumbuka upo ufalme Bwana Yesu alikwenda kutuandalia mbinguni, ambapo sisi tutakaoshinda, sisi ambao hatukuchukizwa na yeye tukiwa hapa duniani, tutaurithi huo, nasi tutawala naye kama wafalme na makuhani, wakati huo, ndio tutajua kuwa Mungu alikuwa anatuwazia mawazo mazuri.
Kwahiyo ukiona mambo hayaendi kama ulivyoyatazamia leo, ndio kwanza zidi kumpenda Yesu. Usimtilie shaka, Yesu ni Mungu. Siku zote anatuwazia mawazo mazuri, Na kesho yetu ipo mikononi mwake, tusichukizwe naye hata kidogo, pale ambapo hajibu maombi yetu kama tulivyotazamia..Kila jambo lina majira yake na wakati wake.
Mhubiri 3:1 “Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.
2 Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati wa kung’oa yaliyopandwa;
3 Wakati wa kuua, na wakati wa kupoza; Wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga;
4 Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza;
5 Wakati wa kutupa mawe, na wakati wa kukusanya mawe; Wakati wa kukumbatia, na wakati wa kutokumbatia;
6 Wakati wa kutafuta, na wakati wa kupoteza; Wakati wa kuweka, na wakati wa kutupa;
7 Wakati wa kurarua, na wakati wa kushona; Wakati wa kunyamaza, na wakati wa kunena;
8 Wakati wa kupenda, na wakati wa kuchukia; Wakati wa vita, na wakati wa amani”.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
JIBU: Nyamafu ni nyama ya mnyama aliyekufa (kibudu) bila kuuliwa kwa asili (yaani kuchinjwa). Mungu aliwakataza wana wa Israeli katika agano la kale wasile nyama ya mnyama yoyote aliyekufa bila kuchinjwa..
Walawi 17: 15 “Tena kila mtu atakayekula NYAMAFU, au nyama aliyeraruliwa na wanyama, kama ni mzalia, kama ni mgeni, atafua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hata jioni; ndipo atakapokuwa safi.
16 Lakini kwamba hazifui, wala haogi mwili, ndipo atakapochukua uovu wake”.
Mistari mingine ya biblia inayozungumzia maagizo kama hayo ni kama ifuatavyo (Kumbukumbu 14:21, Walawi 22:8, Ezekieli 4:14, Ezekieli 44:31)..Unaweza ukaipitia binafsi upatapo muda.
Lakini Mungu aliwakataza wasile nyamafu kwasababu ni nyama ambayo ina damu ndani yake..
Utauliza kwani kuna nyama isiyo na damu na ambayo ina damu?
Jibu ni ndio!..Ipo tofauti kati ya nyama ya mnyama aliyechinjwa na damu yake kutoka na ile ya Mnyama ambaye hajachinjwa na wala damu yake haijatoka..wanjichaji wanajua zaidi. Sasa sio kwamba nyama ya mnyama aliyechinjwa itakosa damu kabisa, itakuwa na damu lakini sio kiwango cha kama ile ambayo haijachinjwa.
Sasa Bwana Mungu aliwakataza wana wa Israeli wasile nyama na damu yake, ndio maana akawapa maagizo ya kuwachinja Wanyama na damu yao waimwage juu ya nchi..
Mwanzo 9: 3 “Kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu, kama nilivyowapa mboga za majani, kadhalika nawapeni hivi vyote. 4 Bali nyama pamoja na uhai, yaani, damu yake, msile”
Ezekieli 33:25 “Basi, waambie, Bwana MUNGU asema hivi; MNAKULA NYAMA PAMOJA NA DAMU YAKE, na kuviinulia vinyago vyenu macho yenu, na kumwaga damu; je, mtaimiliki nchi hii”
Na pia sio usafi kumla mnyama ambaye kafa mwenyewe!.. hata katika hali ya kawaida Mwili unakataa wenyewe! Hata hamu haipo!, hiyo ni kuonyesha kwamba sio kitu cha kufaa kula, kwasababu hujui mnyama kafaje kafaje, pengine kwa kula sumu au.
Hivyo hiyo ndio maana ya nyamafu (Ni nyama ya mnyama aliyejifia mwenyewe bila kuchinjwa).
Lakini katika kumnjicha mnyama ni kitu gani cha rohoni tunajifunza?
Ilikuwa ili mwili wa Bwana wetu Yesu Kristo uweze kukubalika na kuleta matokeo makubwa ya ukombozi, ilipaswa naye pia auawe, na damu yake imwagike!, ndipo ilete uhai kwetu sisi.. Hivyo mwili wa Kristo ni chakula cha ulimwengu, ambaye ni mfano wa kondoo aliyechinjwa na kuandaliwa vyema na si nyamafu. Kwa kupigwa kwake sisi tumepona.
Yohana 6:31 “Baba zetu waliila mana jangwani kama vile ilivyoandikwa, Aliwapa chakula cha mbinguni ili wale.
32 Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Siye Musa aliyewapa chakula kile cha mbinguni, bali Baba yangu anawapa ninyi chakula cha kweli kitokacho mbinguni
33 Kwa maana chakula cha Mungu ni kile kishukacho kutoka mbinguni na kuupa ulimwengu uzima.
34 Basi wakamwambia, Bwana, sikuzote utupe chakula hiki.
35 Yesu akawaambia, Mimi ndimi chakula cha uzima; yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe.”
Je na wewe leo umekipata hichi chakula halali kilichoshushwa kutoka mbinguni? Au unakula nyamafu?..Nyamafu ni kitu chochote ambacho hakikufa kwa kumwaga damu yake kwa ajili yako, hakijachinjwa kwaajili yako.
Kuutumainia ulimwengu ni kujilisha nyamafu, kuzitumainia fedha zako, au umaarufu wako, au kumtumainia mwanadamu yoyote ambaye hajui hata mapigo ya moyo wako yanadundaje ni kujilisha nyamafu na hivyo ni machukizo kwa Mungu.
Mtegemee Yesu, Mwamini Yesu, HUYO PEKE YAKE NDIYE CHAKULA KILICHOSHUSHWA KUTOKA MBINGUNI, Mwanakondoo halisi aliyechinjwa Kalvari kwaajili yetu, (na si kibudu), huyo pekee ndiye anayeweza kutupa uzima.
Kama hujampokea, Leo anakuita, unachotakiwa kufanya ni kukiri tu wewe ni mwenye dhambi, hicho tu! (Anahitaji rehema na si sadaka)..ndicho anachokitafuta kutoka kwetu..Baada ya kukiri na kukubali, basi unaomba msaada kutoka kwake, kwamba akurehemu na kukusaidia, na ukiisha kumwomba rehema..thibitisha ulichokiomba kwa kuyaacha mabaya yote uliyokuwa unayafanya yasiyompendeza yeye..kama ulikuwa mlevi, mwizi, mzinzi n.k yaache yote.
Na yeye ni mwaminifu, kwasababu kabla hata hujamaliza kusema Amen, katika sala yako hiyo ya toba tayari atakuwa ameshakusamehe na kuingia moyoni mwako, kwasababu anakupenda upeo, na anatupenda wote. Na atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu ambaye atakusaidia kukuongoza katika kuijua kweli yote ya biblia. Pia unahitaji kubatizwa katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo sawasawa na Matendo 2:38, Kama utakuwa tayari kufanya hivyo, basi wasiliana na sisi Inbox, tutakuongoza ni wapi utabatiziwa.
Usikubali kula au kulishwa nyamafu wakati chakula halisi kipo!
Bwana atubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618/ +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Herode aliliwa na chango, Je, chango ni nini kibiblia?
Kula uzao wa tumbo lako maana yake nini? (Kumbukumbu 28:53)
Huyu Azazeli ni nani tunayemsoma katika(Walawi 16:8)
Kwanini Bwana aliwalenga mbwa na nguruwe tu katika Mathayo 7:6?
Orodha ya wafalme wa Israeli.
Kabla ya Israeli kugawanyika sehemu mbili kulikuwa na wafalme wakuu watatu waliotawala Israeli
Baada ya kugawanyika. Na kuwa mataifa mawili,.. lile kubwa lilichukua makabila 10 hivyo likaendelea kuitwa jina hilo hilo Israeli, na lile dogo lilibakiwa na kabila moja tu,la Yuda, na lenyewe pia likaendelea kuchukua jina la kabila hilo hilo Yuda (1Wafalme 11:35-36). Ikumbukwe kuwa kabila la 12 la Lawi lenyewe halikuwa na urithi, walitawanywa katikati ya makabila 11 yote ya Israeli.
Jumla ya wafalme wote waliotawala upande wa Israeli (iliyogawanyika) walikuwa ni 19.
Jumla ya wafalme wote waliotawala Yuda ilikuwa ni wafalme 19, malkia 1.
Shalom.
Tazama mada nyingine chini.
Pia Kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Israeli ipo bara gani?
MTO YORDANI UKO NCHI GANI KWA SASA?
Mto Frati upo nchi gani, Umuhimu wake katika biblia ni upi?
DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.
CHAPA YA MNYAMA
MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
MKUMBUKE MKE WA LUTU.
SWALI: Yakobo 5:14 inasema, wazee wa kanisa wakitaka kumwombea mgonjwa wampake mafuta, je! yale ni mafuta ya upako au?. Na kama sio, ni mafuta gani yanayozungumziwa pale?.
Yakobo 5:14 “Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana”.
JIBU: Kabla hutujaona ni mafuta gani yanayozungumziwa pale..Tuutazame kwanza kwa ukaribu mstari huo, ukiungalia vizuri utaona umegawanyika katika vipengele viwili.. utaona baada ya hao wazee wa kanisa kuitwa, hatua ya kwanza ni wanamuombea, (hicho ni kipengele cha kwanza kilichotenganishwa na alama ya mkato), na hatua ya pili inayofuata sasa baada ya hapo ni kumpaka mafuta kwa jina la Bwana.
Watu wengi hawalioni hilo, wanayaunganisha hayo maneno mawili pamoja, na ndio hapo wanadhani, mafuta Fulani ya chupa ndio maombezi yenyewe, .. Jambo ambalo si sahihi?. Kilichomaanishwa pale ni kuwa maombi yakishakwisha, kinachofuata ni kupakwa mafuta…Ukisoma biblia kwa haraka haraka ni rahisi kupoteza shabaha ya maandiko mengi.
Sasa tukirudi kwenye swali ni mafuta gani yale yaliyomaanishwa?..
Biblia inasema..
1Yohana 2:20 “Nanyi mmepakwa mafuta na Yeye aliye Mtakatifu nanyi mnajua nyote”.
Roho Mtakatifu ndiye anayepaka watu mafuta, na mafuta yenyewe ni Neno lake (Yohana 16:13). Hivyo mtu aliye na Neno la Mungu kwa wingi ndani yake, mtu huyo ana mafuta mengi sana ya kumsaidia.
2Wakorintho 1:21 “Basi Yeye atufanyaye imara pamoja nanyi katika Kristo, na kututia mafuta, ni Mungu.
22 naye ndiye aliyetutia muhuri akatupa arabuni ya Roho mioyoni mwetu.”
Sasa mitume na wazee wa kanisa kwa kujua mafuta hasaa na halisi ni yapi, ilikuwa ni desturi yao mara baada ya kuwaombea wagonjwa, jambo linalofuata na kuwaimarisha kwa Neno, ,Kwasababu walijua hicho ndicho kinachoweza kumfanya mtu asimame na kuweza kufanya mambo yote mwenyewe, hata baada ya kutoka pale.
1Yohana 2:27 “Nanyi, mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli wala si uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake”.
Vivyo hivyo, na sasa, tunapaswa tuendeleze desturi hiyo, si kuwaombea tu wagonjwa matatizo yao, sio kufanyia tu kuwafanyia maombi ya ukombozi peke yake halafu hakuna cha ziada baada ya hapo, bali pia, tuwapake mafuta ya Roho wa Bwana..Tuwape chakula cha uzima..ambacho hata wakitoka pale, wanaweza kusimama wao wenyewe, pindi wanapokumbana na matatizo kama hayo na hata kumshinda shetani.
Huo ndio uponyaji hasaa, Lakini kama mtu atatolewa mapepo kwa kuombewa, halafu hatiwi mafuta,(Yaani hufundishwi au ajifunzi maneno ya uzima), akitoka pale, ataendelea na dhambi zake, na yale mapepo yatamrudia baada ya kipindi kifupi, tena yenye nguvu mara saba zaidi, na hali yake ya mwisho itakuwa mbaya kuliko ile ya kwanza kama biblia inavyosema. Na kazi inakuwa ni bure, Hivyo jitathmini na wewe kama mhubiri je unafanya hivyo?.
Kwahiyo mafuta yanayozungumziwa pale, sio mafuta ya chupa, bali ni Neno la Mungu, linalomiminwa na Roho Mtakatifu mwenyewe ndani ya mtu..
Shalom.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Kwanini Mungu alisema hakuna mtu awazaye kuuona uso wake akaishi?
Mistari ya biblia kuhusu kifo.
Kifo ni jambo lisilozoeleka kwa mtu yeyote, Lakini pamoja na hayo lipo tumaini la uzima tena, kwa wale waliomwamini Bwana Yesu Kristo. Na ndio maana mtume Petro aliwatia moyo waaminio wote wa wakati ule, akiwaambia wasistaajabie sana, msiba huo utakapowapata kwa ghafla kama jaribu la moto, kinyume chake wafurahie kwasababu lipo tumaini tena la uzima siku ile ya ufufuo..Kwasababu watafufuliwa tena, na kuwaona wapendwa wao.
1Petro 4:12 “Wapenzi, msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho.
13 Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe”.
Hivyo na wewe unapoipitia mistari hii naomba uitafakari kwa utulivu, itakuponya sehemu Fulani.
Kwababu biblia inasema tena..
Mhubiri 7:2 “Heri kuiendea nyumba ya matanga, Kuliko kuiendea nyumba ya karamu. Kwa maana huo ndio mwisho wa wanadamu wote, naye aliye hai atautia moyoni mwake.
3 Huzuni ni afadhali kuliko kicheko, Maana simanzi ya uso ni faida ya moyo”.
Na pia Bwana Yesu alisema…
Mathayo 5:4 “Heri wenye huzuni; Maana hao watafarijika”.
Na bado biblia inaendelea kusisitiza na kusema..
Mhubiri 7: 1 “Heri sifa njema kuliko marhamu nzuri; Na siku ya kufa kuliko siku ya kuzaliwa”.
1Wathesalonike 4:13 “Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini.
14 Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye.
15 Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti.
16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.
17 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.
18 Basi, farijianeni kwa maneno hayo.”.
Zaburi 23:4 “Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji”.
Warumi 14:8 “Kwa maana kama tukiishi, twaishi kwa Bwana, au kama tukifa, twafa kwa Bwana. Basi kama tukiishi au kama tukifa, tu mali ya Bwana”.
Luka 23:43 “Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi”.
Yohana 11:26 “naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo”?
Yohana 14:1 “Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi.
2 Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.
3 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.
4 Nami niendako mwaijua njia”.
Zaburi 116:15 “Ina thamani machoni pa Bwana Mauti ya wacha Mungu wake”.
Ufunuo 14:13 “Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao”.
Mhubiri 3:1 “Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.
2 Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati wa kung’oa yaliyopandwa;
3 Wakati wa kuua, na wakati wa kupoza; Wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga;
4 Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza”;
1Wakorintho 15:26 “Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti”.
Ufunuo 21:4 “Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita”.
2Wakorintho 5:1 “Kwa maana twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia hii ikiharibiwa, tunalo jengo litokalo kwa Mungu, nyumba isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele mbinguni”.
Wafilipi 3:20 “Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo;
21 atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake.
2Wakorintho 12:9 “Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.
10 Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu”.
Warumi 5:12 “Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi”
Lakini tukishafahamu hayo, tukishafahamu kuwa haya maisha ni ya kitambo tu, yanayeyuka kama mvuke, swali linakuja je! Wewe umejiwekaje kipindi hichi kifupi ulichobakiwa nacho duniani?
Yakobo 4:14 “walakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutoweka”.
Jiulize ukifa na wewe leo ghafla, utakuwa upande gani?.Ukiona moyoni mwako huna jibu la uhakika ni wazi kuwa ukifa huwezi kwenda mbinguni..Kwasababu wanaokwenda mbinguni Yesu Kristo anauweka uhakika huo moyoni mwao. Lakini kama wewe ni mwenye dhambi, biblia inasema, mauti ya pili inakuongojea huko mbeleni, hata baada ya kifo hichi cha kawaida.
Warumi 6:23 “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu”
Embu yatafakari vizuri maisha yako, hata ukipata kila kitu, na pesa zote duniani ujue ipo siku isiyokuwa na jina utakuwa ni vumbi tu..
Mhubiri 12:7 “Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, Nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa”.
Mhubiri 9: 5 “kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa”.
Zaburi 146: 4 “Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake, Siku hiyo mawazo yake yapotea”.
Ndio kifo kitakukuta, lakini Bwana hapendi ufe katika hali ya dhambi, kwasababu hutakuwa na tumaini tena la maisha baada ya hapo.
Ezekieli 18:32 “Maana mimi sikufurahii kufa kwake afaye, asema Bwana MUNGU; basi ghairini, mkaishi”.
Inawezekana upo katika msiba wa mtu wako wa karabu, fahamu kuwa wakati mwingine Bwana anaruhusu uyapitie hayo, au uyaone hayo ili kukumbusha jambo la muhimu unalotakiwa kulifikiria kwanza.
Mhubiri 7: 14 “Siku ya kufanikiwa ufurahi, Na siku ya mabaya ufikiri. Mungu ameifanya hiyo moja kwenda sambamba na hiyo ya pili, ili mwanadamu asipate kulijua neno lo lote litakalofuata baada yake”.
Unaona?
Lakini ukimpa leo Yesu maisha yako, atakupa tumaini la kweli, atakuondolea hofu la mauti, atakuponya roho yako na wewe utakuwa na amani wakati wote, hata ikitokea umekufa leo, unaouhakika wa kwenda mbinguni.. anasema..
Mathayo 11:28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha”.
Wokovu ni bure, kwa wakati wote, na unapatikana wakati wowote mtu anapoufungua moyo wake. Kwanini usimkaribishe Yesu mwokozi maishani mwako?
Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele”.
Hivyo ikiwa leo umeguswa ndani yako na unasema sitaki tena kuishi maisha ya kubahatisha, sitaki kuishi maisha ya mguu mmoja ndani mwingine nje, nataka kuwa upande wa Yesu moja kwa moja. Basi uamuzi huo ni wa busara sana kwako, Kwasababu yeye anasema wote wajao kwangu sitawatupa nje kamwe.. Hivyo fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba na Bwana akubariki. >>>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Maran Atha.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
NINI KINATOKEA BAADA YA KIFO?
USIUZE URITHI WAKO.
VIFUNGO VYA GIZA VYA MILELE.
UNYAKUO.
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!
MIHURI SABA
Naomba kufahamu Nyama zilizosongolewa ni zipi?Je kunywa damu ni dhambi kwa Mkristo?
Nyama zilizosongolewa ni nyama za wanyama ambao hawajachinjwa, na damu yao kumwagika chini.
Kipindi kabla hata ya agano la kwanza(Kale) , Mungu tayari alikuwa ameshampa Nuhu maagizo kuwa asile nyama ya mnyama yoyote pamoja na damu yake ndani yake.
Mwanzo 9:4 “Bali nyama pamoja na uhai, yaani, damu yake, msile”.
Tunaona miaka mingi baadaye Mungu anakuja kumwambia tena Musa jangwani maneno hayo hayo:
Kumbukumbu 12:23 “Ila ujihadhari kwamba usile damu, kwani ile damu ndiyo uhai; na uhai usile pamoja na nyama. 24 Usiile; imwage juu ya nchi kama maji”.
Walawi 17:10 “Kisha mtu awaye yote wa nyumba ya Israeli, au miongoni mwa hao wageni wakaao kati yao, atakayekula damu, ya aina yo yote, nitakunja uso wangu juu ya mtu huyo alaye damu, nami nitamkatilia mbali na watu wake.
11 Kwa kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu; nami nimewapa ninyi hiyo damu juu ya madhabahu, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu; kwani ni hiyo damu ifanyayo upatanisho kwa sababu ya nafsi.
12 Kwa hiyo naliwaambia wana wa Israeli, Hapana mtu miongoni mwenu aliye na ruhusa kula damu, wala mgeni aketiye kati yenu asile damu”.
Lakini tukirudi tena katika agano letu jipya, tunaona moja ya maagizo ambayo mitume wanalipa kanisa la mataifa(yaani sisi) Ni kutokula nyama zilizongolewa( yaani nyama ambazo hazijachinjwa na damu kumwagika)..
Matendo 15:19 “Kwa sababu hiyo mimi naamua hivi; Tusiwataabishe wale waliomgeukia Mungu katika Mataifa;
20 bali tuwaandikie kwamba wajiepushe na unajisi wa sanamu, na uasherati, na nyama zilizosongolewa, na damu.
21 Kwa maana tangu zamani za kale Musa anao watu wahubirio mambo yake; katika kila mji husomwa kila sabato katika masinagogi”.
Sasa swali linakuja Je kwa mantiki hiyo wakristo haturuhusiwi kabisa kula nyama zilizongolewa au kunywa damu?
Ukweli ni kwamba kulingana na mazingira ya wakati ule kwa watu wa mataifa, na ya sasa, ni ngumu kuishi bila kukutana na nyama za namna hiyo.. Kwasababu nyama nyingi siku hizi, hazichinjiwi nyumbani, unazikuta mabuchani, au supermarket, na kule hujui zimechinjwaje chinjwaje.. Hivyo huwezi kuuliza hii nyama iliandiliwaje, vinginevyo hutakaa ule nyama kabisa…Sasa Bwana Yesu kwa kulijua hilo akawaagiza mitume wake, kuwa watakachokutana nacho mbele yao kila mahali mnapokaribishwa wale (Luka 10:8),
Mtume Paulo naye aliliweka wazi hilo kwa wakorintho na kuwaambia..
1Wakorintho 10:25 “Kila kitu kiuzwacho sokoni kuleni, bila kuuliza-uliza, kwa ajili ya dhamiri;
26 maana, Dunia ni mali ya Bwana na vyote viijazavyo”.
Kwamfano Soseji nyingine zinatengenezwa na damu ndani yake, na nyingine hazitengenezwi na damu, Hivyo ukipewa kula bila kuuliza uliza, ukikuta zinauzwa dukani nunua ule bila kuuliza uliza.
Kwasababu sisi agano letu halipo katika vyakula, bali lipo rohoni..vyakula havitubadilishi kitu. Lakini pale inapotokea unachinja mbuzi wako, au kuku wako, au ng’ombe wako nyumbani ni vema ukaimwaga damu ya mnyama huyo chini, usinywe kisusio..Si vema kufanya hivyo, kwasababu tumeshapewa maagizo hayo.
Zaidi ya yote amani ya Kristo iamue ndani yako.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
DAMU YA YESU INANENAJE MEMA KULIKO YA HABILI?
MUNGU AKIKUPITA LEO, HAIMAANISHI KUWA HAJAKUCHAGUA.
USITAFUTE FAIDA YAKO MWENYEWE BALI YA WENGINE.
MAJONZI YA MTUME PAULO KWA NDUGU ZAKE.
HUDUMA YA WALE MASHAHIDI WAWILI.
UNYAKUO.
SWALI: Je tunaruhusiwa kujipaka mafuta au kujipulizia marashi/manukato (perfumes)?
JIBU: Sio vibaya kujipaka mafuta usoni au mwilini, ili kuondoa ule mpauko wa asili, mafuta hususani yale ya asili ni mazuri kwa ngozi, lakini pia sio amri kwamba lazima tujipake mafuta, hata hivyo ngozi zetu huwa zinatoa zenyewe mafuta yake ya asili.
Lakini yapo mafuta ya kuchubua ngozi, na yenye marashi makali, hayo ni kinyume na maandiko kuyatumia kwasababu lengo lake ni kubadilisha maumbile, ambayo maudhui yake ni Udunia!..Biblia inasema miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu na pia miili yetu sio mali yetu wenyewe, ni mali ya Mungu, hivyo hatupaswi kuibadilisha kutoka katika hali yake ya asili na kuifanya tutakavyo sisi (1Wakorintho 6:19).
Sasa unaweza kuuliza ni wapi katika agano jipya tumepewa ruhusa ya kutumia mafuta?
Mathayo 6: 16 “Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao.
17 Bali wewe ufungapo, JİPAKE MAFUTA KİCHWANİ, UNAWE USO;
18 ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi”
Hayo ni maneno yaliyozungumzwa na Bwana Yesu mwenyewe.
Swali lingine ni je! Ni mafuta gani yanayofaa?..Hakuna orodha maalum ya mafuta yanayofaa, kikubwa mafuta yoyote yale yawe ya kiwandani au ya asili ambayo hayana kemikali nyingi na hayana marashi makali yanafaa kutumika.
Na Marashi ni hivyo hivyo, yapo marashi ya nguo..ambayo lengo lake ni kudhibiti nguo isitoe harufu mbaya aidha ya jasho au ya kitu kingine kisichofaa. (Katika mazingira fulani)
Nayo pia sio vibaya kuyatumia, ilimradi tu yasiwe na maudhui ya kishetani. Marashi yanayotumika mengi siku hizi yana maudhui ya kidunia, marashi mtu anayotumia ambapo mtu aliyesimama mita 2 mbele yake au nyuma yake anasikia harufu yake, tayari lengo la marashi hayo sio kudhibiti harufu bali kuvuta hisia kutoka kwa mwingine…jambo ambalo sio sawa.
Kiwango cha marashi kinapaswa kiwe kidogo sana)..kiasi kwamba mpaka pua ifike karibu na nguo ndipo isikike..(na hiyo ni kama kuna ulazima wa kuyatumia kutokana na mazingira, lakini kama hakuna ulazim hayapaswi kutumika kabisa).
Na zaidi sana, mafuta mengi tunayotumia au sabuni zina kiwango tosha cha marashi ambayo hatuhitaji kuongeza mengine juu yake.
Katika biblia marashi yametafsiriwa sehemu kadha wa kadha kama “Marhamu” au “Manukato”. Unaweza kupitia mistari ifuatayo binafsi (Mathayo 26:7-13, Marko 14:3, Marko 16:1).
Lakini zaidi sana Marashi yetu yanayompendeza Mungu ni Maombi yetu kwake, na utakatifu wetu.
Ufunuo 5:8 “Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele za Mwana-Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa MANUKATO, AMBAYO Nİ MAOMBİ YA WATAKATİFU”.
2Wakorintho 2:14 “Ila Mungu ashukuriwe, anayetushangiliza daima katika Kristo, na kuidhihirisha harufu ya kumjua yeye kila mahali kwa kazi yetu.
15 Kwa maana sisi tu manukato ya Kristo, mbele za Mungu, katika wao wanaookolewa, na katika wao wanaopotea;
16 katika hao wa pili harufu ya mauti iletayo mauti; katika hao wa kwanza harufu ya uzima iletayo uzima. Naye ni nani atoshaye kwa mambo hayo”
Hivyo tukiwa maridadi wa mwilini, tukanukia vizuri na huku rohoni tunatoa harufu mbaya, hatusali, hatufungi, hatuombi, hatuishi maisha ya kumpendeza yeye..basi mbele za Mungu tunapeleka harufu mbaya.
Lakini tukiwa waombaji, tukimwomba Mungu rehema, na neema..pamoja na tukiwaombea na wengine na kuliombea kanisa, na tukiishi maisha masafi, basi tutakuwa ni lulu mbele za Mungu.
Mungu atasaidie katika hilo.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
SWALI: Ni jeshi gani la Mbinguni ambalo Mungu aliwaacha wana wa Israeli waliabudu katika Matendo 7:42? Je ni Malaika au?
JIBU: Matendo 7: 41 “Wakafanya ndama siku zile, wakaleta dhabihu kwa sanamu ile, wakafurahia kazi za mikono yao.
42 Basi Mungu akaghairi, akawaacha ili waliabudu jeshi la mbinguni, kama ilivyoandikwa katika chuo cha manabii, Je! Mlinitolea mimi dhabihu na sadaka Miaka arobaini katika jangwa, enyi nyumba ya Israeli?”
Habari hii inawazungumzia wana wa Israeli wakati wanatoka Misri. Wakiwa jangwani biblia inasema walikuwa wakikengeuka mara kadhaa, walikuwa wakimwacha Mungu na kugeukia kuchonga sanamu, na wakati mwingine kumjaribu Mungu (Kutoka 17:2).
Lakini kuna jambo lingine tunaliona walilokuwa wanalifanya ambalo lilikuwa ni machukizo kwa Mungu, na hilo si lingine zaidi ya KULIABUDU JESHI LA MBINGUNI.
Sasa swali la msingi hapo ni je! Hilo jeshi ni lipi?, ni malaika au ni nini?.
Jibu ni kwamba si Malaika, bali ni miungu ya kipagani.
Si kila mahali kwenye biblia palipoandikwa neno “mungu” panamaanisha “Mungu wa mbingu na nchi”, vivyo hivyo sio kila mahali katika biblia palipoandikwa neno “bwana” panamaanisha “Bwana Mungu wa mbingu na nchi”…hali kadhalika sio kila mahali katika biblia palipoandikwa neno “mbingu” au “mbinguni”, panamaanisha “Mbinguni malaika watakatifu walipo”..
Dini karibia zote zinaamini kwamba kuna mbingu..kwamba kuna mahali huko juu ambapo kuna viumbe watakatifu wanaishi,..Na nyingine zinaamini huko mbinguni kuna miungu mingi, kuna jeshi kubwa la miungu, ambayo yote inastahili kuabudiwa. Kwamfano dini ya kihindu tu peke yake ina zaidi ya miungu milioni 330.
Sasa ikatokea kwa mtu ambaye ni mkristo, ambaye ameshajua ukweli wote kwamba Mungu ni mmoja tu aliyeko mbinguni ambaye anaabudiwa katika roho na kweli.. akaiacha hiyo imani na kisha akaenda kujiunga na imani nyingine(kama hiyo ya kihundu) inayoamini kwamba mbinguni kuna miungu mingi, na akaenda kuiabudu hiyo miungu yao. Hapo ni sawa na kusema “AMEKWENDA KULİSUJUDİA JESHİ LA MBİNGUNİ”..na si mbingu ile ambayo malaika watakatifu wapo bali ni mbingu ya kihindu, ambayo kiuhalisia haipo! ni uongo uliotengenezwa na shetani tu kuwadanganya watu kuwa kuna mbingu yenye miungu mingi!,
Ni agenda ya shetani na mapepo yake Kutafuta kuabudiwa na kuwapotosha watu wa Mungu. Hiyo idadi yote ya miungu wanayoiabudu ni mapepo yanayojiguza na kuchukua sura ya hivyo wanavyoviabudu. (zingatia: wengi wanaoabudu hiyo miungu, sio watu wabaya na wala si maadui zetu, wengi wao ni watu wazuri, wanafanya hayo kwasababu bado hawajaujua ukweli, au macho ya mioyo yao bado hayajafumbuliwa, kwahiyo wanaabudu vitu wasivyovijua, hivyo ni jukumu letu wewe na mimi kuwapelekea injili na kuwaombea!, ili macho yao yafumbuliwe wapate kuona na kuokolewa Matendo 17:29-31).
Kwahiyo Jeshi la mbinguni linalozungumziwa hapo sio Malaika waliopo mbinguni, bali ni miungu iliyopo mbinguni huko angani, ambayo kiuhalisia ni shetani na mapepo yake.
Na malkia wa mbinguni aliyezungumziwa pia katika Yeremia 7:18, 44:17-25 sio Bikira Mariamu wala sio Malaika fulani wa kike aliyeko mbinguni bali ni mungu fulani wa kipagani, wanayedai kwamba yupo mbinguni (kwa maelezo marefu utatutumia ujumbe inbox), ambaye ni Pepo!.
Mwisho ni muhimu kuchukua tahadhari!.. pale tunapoonywa mara nyingi!…Hapo kwenye matendo 7:42, biblia inasema “ Basi MUNGU AKAGHAİRİ, AKAWAACHA ili waliabudu jeshi la mbinguni,”.
Litazame hilo neno kwa makini!..Mungu akaghairi!, akawaacha!! İli waliabudu jeshi la mbinguni…Ni jambo la kuogopesha sana pale Mungu anapoghairi juu yako, na kukuacha uendelee kufanya unayoyafanya!…hilo ni jambo la kuogopesha sana!..Anaabudu masanamu unayodhani ni watakatifu Fulani wa mbinguni, na umeonywa mara nyingi husikii, hapo unamfanya Mungu aghairi juu yako.
Warumi 1:28 “Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa”
2Wathesalonike 2:10 “na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa. Kwa hiyo Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo”.
Jiupeshe na ibada za sanamu ni dhambi, jiepushe na mambo yote maovu na mwisho soma neno kwa bidii..
Bwana atubariki.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
AINA YA MAADUI UTAKAOKUTANA NAO KATIKA SAFARI YAKO YA WOKOVU.
AINA YA MAADUI UTAKAOKUTANA NAO KATIKA SAFARI YAKO YA WOKOVU.
CHUKIZO LA UHARIBIFU
MUNGU WANGU,MBONA UMENIACHA?.
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!
2Wakorintho 13:14 “Neema ya Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote”.
Hii ni salamu ya kumalizia ambayo mtume Paulo aliwaandikia wakorintho, na watu wote watakaousoma waraka huo (ikiwemo mimi na wewe).
Maneno haya, yamegusa Nyanja zote tatu za Kusudi la Mungu kwetu sisi wanadamu.
> Paulo anaanza kwa kusema, Neema ya Bwana Yesu Kristo, ikae nasi; Akiwa na maana kuwa mpaka sisi tukamilike, mpaka sisi tushinde, tunaihitaji hii neema ya Yesu Kristo wakati wote itembee na sisi, tukipungukiwa neema, basi ni ngumu kuweza kuushinda ulimwengu. Na neema hii inaanza kutembea juu ya mtu kwa mara ya kwanza pale anapookoka.
> Anasema tena, Pendo la Mungu likae nasi: Ni kwa njia ya upendo Mungu alitukuomboa (Yohana 3:16). Hivyo na sisi tukiukosa Upendo, haijalishi tutakuwa washirika wazuri kiasi gani, haijalishi tutafanya miujiza mingi kiasi gani, tutanena kwa lugha za malaika nyingi kiasi gani, bado sisi tutabakia kuwa si kitu. Hivyo Pendo la Mungu linapokaa ndani yetu basi Mungu anakuwa karibu na sisi. Na pendo la Mungu ndio lile linalozungumziwa katika 1Wakorintho 11:1-8
Na ndio huo Paulo alikuwa analiombea kanisa ukae ndani yao.
> Anamalizia na kusema pia Ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote; Hii ikiwa na maana palipo na Roho Mtakatifu pana ushirika.. Sisi kama wakristo tuliookoka ni jukumu letu kuutunza ushirika wa Roho tukinia mamoja, tukiifanya kazi ya Mungu..
Waefeso 4:3 “na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani.
4 Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu.
5 Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja.
6 Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote”.
Mambo haya matatu yakienda pamoja na sisi, basi Mungu naye ataenda pamoja na sisi, lakini tukipungukiwa kimoja wapo, aidha neema, au Upendo, au Ushirika, ni ngumu kusimama kama Kanisa.
Hivyo mimi na wewe tujitathmini ni wapi, hatujakamilisha, kisha tukamilishe, Na Bwana atusaidie.
Shalom.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
UNYAKUO.
KWANINI MUNGU ALIMTUMIA MUSA KWA VIWANGO VILE?
UPONYAJI WA ASILI
JE UDHAIFU WANGU UNAWEZA KUZUIA INJILI?
ADAM NA EVA.
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!
Kibanzi Na Boriti, kwenye biblia vinamaanisha nini?
Boriti ni kipande kikubwa sana cha mbao, kinaweza kikawa ni ki-gogo, au nguzo, au mbao yoyote pana..
Lakini kibanzi, ni kichembe kidogo sana cha mbao, kama mchanga, hata wakati mwingine kufikia kuwa kama vumbi la mbao ambalo ni ngumu sana kuliona. Hicho ndicho kibanzi.
Sasa Bwana Yesu alitoa mfano huo, wa picha ili kuweka msisitizo kile alichotaka kukisema, yaani katika hali ya kawaida, kama wewe huwezi kuona nguzo iliyosimama mbele ya macho yako inayokuzuia usione kabisa, utaona vipi vumbi la mbao lililo katika jicho la mwenzako?..Umeona moja kwa moja huo ni unafki..
Vivyo hivyo na sisi kabla hatujawahukumu watu, tuyachunguze maisha yetu Je! hayo wanayoyafanya Je, hayapo ndani yetu na sisi? Kabla hujamwambia Fulani acha usengenyaji, Je! na wewe si msengenyaji? Kama sivyo basi ni heri ukae tu kimya, kwasababu mistari ya juu yake inasema, kipimo kile kile tuhukumucho ndicho tutakachokuhumiwa na sisi.
Mathayo 7:1 “Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi.
2 Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa.
3 Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii?
4 Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe?
5 Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako.
Bwana atusaidie sote tuyashinde hayo.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
https://wingulamashahidi.org/ikabodi-maana-yake-ni-nini/
KAMA MMOJA TU NDIO HIVI! SI ZAIDI 153?
UNYAKUO.
MKUMBUKE MKE WA LUTU.
CHUKIZO LA UHARIBIFU
Israeli ipo bara gani?
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!