Tusome,
2Petro 3:8 “Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja”.
Kama ukiendelea mbele kidogo kusoma mstari wa 9, utaona Mtume Petro anajaribu kumwelezea Mungu kwamba huwa hakawii kuzitimiza ahadi zake kwetu sisi wanadamu.
2Petro 3:8 “Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja.
9 Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba”.
Aliona kuna watu wengi wanaona kama Mungu huwa anachelewa sana kutimiza aliyoyasema.. Alisema atarudi, mbona harudi na imeshapita miaka mingi? N.k
Ndipo akazungumza maneno hayo, ambayo pia yalizungumzwa kwa sehemu na Mfalme Daudi katika Zaburi..
Zaburi 90:4 “Maana miaka elfu machoni pako Ni kama siku ya jana ikiisha kupita, Na kama kesha la usiku”.
Maana yake ni kwamba tunapodhania kwamba Miaka elfu ni kipindi kirefu sana, kwa Mungu kwake ni kama siku moja tu ya jana iliyoisha. Na kwanini Kristo hajarudi mpaka miaka hii, sababu imeshatolewa hapo juu, kwamba “hapendi mtu yoyote apotee, bali wote waifikilie toba”. Hivyo anatuvumilia ili watu wote tuingie katika neema ya wokovu, kabla ya ule mwisho kufika, maana ule mwisho ukifika kama hatutakuwa ndani ya wokovu, hakutakuwa na nafasi ya pili.
Lakini pia kama tukifikiri Mungu kawahi sana, basi tusisahau kuwa siku moja kwa Mungu ni sawa na miaka elfu, maana yake, tunaishi nje ya muda, (muda umeenda sana), na ule mwisho upo karibu sana. Kristo yupo mlangoni..
Na ndio maana biblia inasema “saa ya wokovu ni sasa”.
2Wakorintho 6.2 “Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia;tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa”
Kadhalika katika mambo mengine ya kimaisha, tunapoona siku moja ni fupi sana kwetu Mungu kufanya jambo, tujue kuwa kwa Mungu ni kama miaka elfu, maana yake ahadi zake alizotuahidi anaweza kuzitimiza ndani ya siku moja… Kwahiyo hatupaswi kumkosea Mungu Imani, hata kama tumeona siku inakaribia kuisha na hatujapata kile tunachokitafuta, tufahamu kuwa Mungu anaweza kufanya jambo kubwa ndani ya siku hiyo hiyo moja kabla haijaisha yote, kwasababu kwake yeye ni kama miaka elfu.
Bwana atubariki
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Nini maana ya “Siku moja nyuani mwa Bwana ni bora kuliko siku elfu”?
IMESALIA RAHA YA SABATO KWA WATU WA MUNGU.
Bwana Yesu alikufa akiwa na umri gani?
Je! Kuna malaika wangapi mbinguni?
LAKINI NINYI, NDUGU, MSIKATE TAMAA KATIKA KUTENDA MEMA.
WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.
About the author