Kutoka 21:2-6 ” Ukimnunua MTUMWA wa Kiebrania, atakutumikia muda wa miaka sita; mwaka wa saba atatoka kwako HURU bure.
3 Kwamba aliingia kwako peke yake tu, atatoka hivyo peke yake; kwamba ameoa, mkewe atatoka aende pamoja naye.
4 Kwamba ni bwana wake aliyempa huyo mke, naye amemzalia wana, wa kiume au wa kike; yule mke na wanawe watakuwa ni mali ya bwana wake, naye mume atatoka peke yake.
5 Lakini huyo mtumwa AKISEMA WAZIWAZI, Mimi nampenda bwana wangu, na mke wangu na watoto wangu; SITAKI MIMI KUTOKA NIWE HURU;
6 ndipo hapo huyo bwana wake atamleta mbele ya Mungu na kumleta mlangoni, au penye mwimo wa mlango; na bwana wake ATALITOBOA SIKIO LAKE KWA UMA; ndipo ATAMTUMIKIA SIKU ZOTE. “
Biblia inaeleza wazi kabisa kulingana na maandiko hayo hapo juu, Mtumwa yule aliyetangaziwa uhuru wake baada ya kutumika miaka 6 akakataa (Yaani akaona ni vyema kuendelea katika utumwa wake.). Jambo linalotokea ni hili bwana wake huyo mtumwa atachukua sindano na kutoboa SIKIO lake, kuwa kama MUHURI wa kukataa kuwekwa huru, Hivyo basi huyo mtumwa atamtumikia bwana wake milele, Na kama tunavyofahamu sikio likishatobolewa haliwezi kurejea tena katika hali yake ya kwanza. Na ndio maana ilikuwa inatumika kama ISHARA YA MAPATANO(MUHURI).
Vivyo hivyo kwa wanadamu wa leo, Kristo alikuja kututangazia uhuru wetu kutoka katika UTUMWA WA DHAMBI kulingana na
Mathayo 11:28-29 (Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; “),
Kwasababu Bwana Yesu alisema Yohana 8:34-36″ ….Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.Wala mtumwa hakai nyumbani sikuzote; mwana hukaa sikuzote. Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli. “
Bwana Yesu pia alisema maneno haya luka 4:18-19″ Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma KUWATANGAZIA WAFUNGWA KUFUNGULIWA KWAO, Na vipofu kupata kuona tena, KUWAACHA HURU WALIOSETWA,Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa. “
Kwahiyo injili ililetwa kwetu mahususi kwa kutuweka HURU mbali na dhambi. Hapo anaposema
“kuutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa” akiwa na maana kuwa ndio mwaka wa maachilio, ule mwaka wa saba ( Kwa maana mahali pengine anasema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia; tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa.
2 Wakoritho 6:2). Kwahiyo tunaona MBIU YA MAACHILIO IMESHAPIGWA watu wote wawe HURU kwa YESU KRISTO BWANA. Lakini cha kusikitisha wapo baadhi ya watumwa (watumwa wa dhambi), wanakataa kuupokea uhuru WAO waliotangaziwa na Bwana wanapenda kuendelea kumtumikia bwana wao shetani ambaye hapo mwanzo alikuwa anawatumikisha na kuwatesa. Embu tuitazame hii mihuri inampataje mtu.
Mungu anao MUHURI wake, na shetani pia anao muhuri wake kwa watoto wake. Wale waliokubali kuwekwa huru na BWANA wanatiwa MUHURI WA MUNGU nao ni ROHO MTAKATIFU kulingana na
waefeso 4:30″(Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa MUHURI hata siku ya ukombozi). , na pia biblia inasema katika
2 Wakoritho 3:17 .. walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru. “.
Kwahiyo unaona unapoukubali UHURU Mungu anakupa zawadi ya kupokea Roho Mtakatifu kama Muhuri wa uhuru wako. Lakini kama hauna Roho wa Mungu wewe bado ni mtumwa wa dhambi na UNAJUA MSHAHARA WA DHAMBI NI MAUTI. Warumi 8:9″….Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake. ”
Kwa wale waliokataa uhuru kwa makusudi angali wakijua kabisa wapo kwenye utumwa na wangepaswa wawe huru, lakini wakapenda kumtumikia bwana wao shetani katika dhambi zao kuliko kumtumikia Mungu nao pia wanatiwa MUHURI. Na mihuri hiyo YA SHETANI wanatiwa katika MASIKIO YA MIOYO YAO, maana yake ni hii HAWATAKUWA TENA NA NEEMA YA MUNGU JUU YA MAISHA YAO!,baada ya kuisikia injili na kuikataa Haiwezekani wao kumgeukia Mungu tena, Hata waelezweje injili hawawezi kusikia tena wageuke hao wameshakuwa mali halali ya shetani. Hii ni hatari sana tuwe makini tunaposikia wito wa Mungu.
Na huu muhuri wa shetani mpaka sasa hivi unaendelea kuwapiga watu,
leo hii umeshaisikia injili mara ngapi, umehubiriwa uache uzinzi mara ngapi ewe kijana ewe binti,? umehubiriwa utubu dhambi zako mara ngapi? lakini umekuwa wa kwanza kufanya mizaha? umehubiriwa uache ulevi mara ngapi? unavuta sigara, unaangalia pornoghaphy, unafanya mustarbation, binti unasagana, umekuwa shoga kijana, unaenda kwa waganga, unajifurahisha katika anasa na miziki ya kidunia,
Mwanamke unavaa suruali, vimini, unapaka rangi kucha, kijana unanyoa mitindo isiyofaa na kusuka nywele ,na tatoo kwenye mwili wako, wanawake usengenyaji na umbea, mtukanaji, unajichanganya na watu waovu kwa jinsi isivyopasa, unachati nao mambo maovu, huku ukijua kabisa watu wanaoyafanya hayo wataishia katika jehanum ya moto, JE! UNADHANI NEEMA YA MUNGU ITAENDELEA KUDUMU JUU YAKO MILELE?.
Mungu hadhihakiwi apandacho mtu ndicho atakachokivuna. Tutawezaje kupona tusipouthamini wokovu mkuu namna hii?.
Unashindwa kuona jinsi unavyozidi kutiwa ule MUHURI wa shetani? kwa kuukataa uhuru wako ambao BWANA aliokutangazia pale KALVARI?. Maana kama unasikia sauti ya Mungu kila siku ikisema moyoni mwako UTUBU lakini unaipuuzia nakwambia ukweli utafika wakati HAUTAKAA UISIKIE TENA NDANI YAKO!!,
Na unajua ni kitu gani kitaenda kukutokea? Ni kwamba utafika wakati utaona mambo yote kuwa ni sawa, kuwa ulevi ni sawa,utaona uasherati hauna ubaya wowote, Mungu aliyetuumba hawezi kutuhukumu, hautaamini tena kama kuna jehanamu, utaishia kuwaona watumishi wote wa Mungu ni waongo, utaishia kuukosoa kila siku ukristo na biblia ukisema hayo mambo ni ya kale.
Utaanza kujiona kuwa ni haki yako kuishi unavyotaka hata kujichubua, kubadili maumbile, kuvaa unavyotaka ni sawa, Utajiona kutukana ni sehemu tu ya maisha ya binadamu hakuna kosa lolote kwasababu Roho Wa Mungu hayupo tena ndani yako kwasababu UMESHATIWA MUHURI, utaanza kuona kujipenda mwenyewe ni sawa, Kutazama pornography na kufanya musturabation ni sehemu maisha ya kila mwanadamu ukijidanganya kuwa Mungu hawezi kumuhukumu mtu kwa kufanya hivyo, unajikuta unaanza kupenda kufuatilia mafundisho ya mashetani kuliko mafundisho ya Mungu, Biblia hutaki kusoma kusoma lakini habari za freemasons, na zi kichawi, na filamu pamoja na vitabu kama , harryporter, twightlight, vampires,n.k. ndivyo vinavyokuvutia kusoma na kuangalia, jiulize ni roho gani inakuendesha? n.k.
Ndugu ukishaanza kuona dalili ya mambo kama hayo yanakuja ndani yako, jua kabisa neema ya Mungu ndivyo inavyoondoka kwako kidogo kidogo na ndo unavyoupokea MUHURI wa shetani hivyo, maana jua tu wewe unayeisikia injili kila siku unaambiwa utubu hautaki, neema yako haiwezi kuwa sawa na mtu yule ambaye hajawahi kusikia injili kabisa. soma mstari ufuatao;
2 Wathesalonike 2:10-12 ” na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa.
11 KWAHIYO MUNGU AWALETEA NGUVU YA UPOTEVU, WAUAMINI UONGO;
12 ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu. “
Kwahiyo ndugu maneno hayo hayakuogopeshi?? TUBU! yamkini hii sauti ya upole inayokuambia kila siku utubu bado inaendelea KULIA NDANI YAKO! ..itii na ugeuke maana upo katika HATARI, Maana hiyo sauti haitadumu milele ndani yako. Na ikishaondoka hakutakuwa na njia ya kurudi tena. YAANI MOYO WA KUTUBU hautakuwepo tena ndani yako utafanana na hao watu unaowaona huko ulimwenguni watendao matendo ya giza si kana kwamba hawasikii au hawakusikia injili hapana lakini mioyo yao imeshatiwa MUHURI, hawatakaa wasikie tena na kubadilika, ndugu usifanane nao. Mtii Mungu tubu dhambi zako muda umeenda sana kuliko unavyofikiria.Yesu yupo mlangoni kurudi.
Maana biblia inasema…
Ufunuo 22:10 “Akaniambia, Usiyatie muhuri maneno ya unabii wa kitabu hiki, kwa maana wakati huo umekaribia. MWENYE KUDHULUMU NA AZIDI KUDHULUMU; na MWENYE UCHAFU AZIDI KUWA MCHAFU; na MWENYE HAKI AZIDI KUFANYA HAKI; na MTAKATIFU NA AZIDI KUTAKASWA.Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. “
Naomba umalizie kwa kuyatafakari maneno yafuatayo ujue hatma ya WALIOUKATAA UHURU WAO KUTOKA KWA BWANA;
Warumi 1:24” Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao.
25 Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina.
26 HIVYO MUNGU ALIWAACHA WAFUATE TAMAA ZAO ZA AIBU, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili;
27 wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, WAKAPATA NAFSINI MWAO MALIPO YA UPOTEVU WAO YALIYO HAKI YAO.
28 NA KAMA WALIVYOKATAA KUWA NA MUNGU KATIKA FAHAMU ZAO, MUNGU ALIWAACHA WAFUATE AKILI ZAO ZISIZOFAA, WAYAFANYE YASIYOWAPASA.
29 Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya,
30 wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao,
31 wasio na ufahamu, wenye kuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema;
32 AMBAO WAKIJUA SANA HUKUMU YA HAKI YA MUNGU, YA KWAMBA WAYATENDAYO HAYO, WAMESTAHILI MAUTI, WANATENDA HAYO, WALA SI HIVYO TU, BALI WANAKUBALIANA NAO WAYATENDAYO.Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Kwa mawasiliano/Ushauri/kuokoka/Whatsapp. Namba zetu ni hizi
+255693036618/+255789001312
Mada Nyinginezo:
WAKATI WA JIONI KUTAKUWAKO NA NURU.
NUHU ALIWALETAJE LETAJE WANYAMA KWENYE SAFINA?
NINI TOFAUTI KATI YA 1) KUOKOKA, 2) WOKOVU, 3) KUONGOKA?
UAMSHO MKUU UMEKARIBIA!!
Yoeli 2:28-32″ Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono;
29 tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu.
30 Nami nitaonyesha MAMBO YA AJABU KATIKA MBINGU na KATIKA DUNIA, DAMU, na MOTO, na MINARA YA MOSHI.
31 JUA LITAGEUZWA KUWA GIZA, na MWEZI KUWA DAMU, kabla haijaja hiyo siku ya Bwana iliyo kuu na itishayo.
32 Na itakuwa ya kwamba mtu awaye yote atakayeliita jina la Bwana ataponywa; kwa kuwa katika mlima Sayuni na katika Yerusalemu watakuwako watu watakaookoka, kama Bwana alivyosema; na katika mabaki, hao awaitao Bwana.
Tukisoma mistari hiyo Nabii Yoeli alionyeshwa maono ya uvuvio mkubwa wa Roho ya Mungu ambao ungekuja katika siku za mwisho, Na ni dhahiri kabisa kwa wasomaji wa biblia wanafahamu sehemu ya huo unabii ulitimia wakati wa PENTEKOSTE, pale Roho wa Mungu alipowashukia wale watu 120 kwa mara ya kwanza, na kuwapa vipawa vikubwa na vya ajabu, ishara na miujiza mingi ikifanywa na mitume na wale wote waliojazwa Roho Mtakatifu.
Mvua hii ya Roho Mtakatifu Mungu aliyoiachilia kwa mara ya kwanza pale Pentekoste inajulikana kama “MVUA YA AWALI/MASIKA” ( kwa kiingereza former Rain). Lakini pia Mungu aliahidi kuileta mvua nyingine tena ambayo ni “MVUA YA BAADAYE/ VULI” ( kwa kiingereza Latter Rain). Kwa ufafanuzi wa maelezo haya tusome;
Yoeli 2:23 “Furahini, basi, enyi wana wa Sayuni, mkamfurahie Bwana, Mungu wenu; kwa kuwa yeye huwapa ninyi MVUA YA MASIKA, kwa kipimo cha haki, naye huwanyeshea mvua, MVUA YA MASIKA, na MVUA YA VULI, kama kwanza.”
Kwahiyo hii mvua ya pili (MVUA YA VULI) mbali na ile ya kwanza iliyotokea wakati wa Pentekoste, Tukisoma katika historia ya ukristo Bwana aliishusha tena mwaka 1906, kwenye uamsho uliotokea mtaa wa AZUSA, huko Calfornia Marekani ambapo Bwana alimwaga ROHO wake na kushusha vile vipawa tena vya Roho Mtakatifu kama ilivyokuwa katika Pentekoste ya kwanza baada ya kanisa la Kristo kukaa muda mrefu bila uamsho kwa muda wa karne nyingi, lakini kuanzia huu mwaka 1906 tunaona vipawa vyote vilirejeshwa watu wakaanza kunena kwa lugha, kutabiri, kuponya magonjwa, ishara na miujiza, unabii n.k. vitu ambavyo havikuwahi kutenda tangu wakati wa kanisa la kwanza.
Hivyo basi Mungu alimtuma mjumbe wake William Branham kama mjumbe wa kanisa la mwisho LAODIKIA, ufunuo 3, Mungu alimtumia kwa ishara nyingi na miujiza ya ajabu ambayo haikuwahi kufanyika hapo kabla ikiwemo na utambuzi wa siri za mioyo ya watu, tafsiri za ndoto kama ilivyokuwa kwa Nabii Danieli, na ishara zilizoweza kuonekana wazi na kunaswa katika picha za kimagnetiki, n.k.
Ndipo Mungu akaendeleza kuimwaga hiyo roho kwa watumishi wake wengi waaminifu duniani kote kwa mfano wa William Branham kama oral Robert, Billy Granham, TL Osborn, nk..
( tazama ushuhuda mfupi juu ya huduma na maisha ya William Branham,)
Mvua hii ya mwisho itatimizwa katika huu wakati wa mwisho Bwana aliahidi sehemu hii ya maandiko itaenda kutimia
Yoeli 2:29 “tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu.
30 Nami nitaonyesha mambo ya ajabu katika mbingu na katika dunia, damu, na moto, na minara ya moshi.
31 Jua litageuzwa kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla haijaja hiyo siku ya Bwana iliyo kuu na itishayo.
Kumbuka katika mvua iliyoachiliwa mara ya kwanza, tuliona unabii, lugha, maono, ndoto, ishara, n.k. lakini hatukuona mambo ya ajabu katika dunia na katika mbingu kama jua kutiwa giza, mwezi kuwa damu, moto, minara ya moshi, n.k. tumezoelea kuona unabii na uponyaji, lakini haya mambo mengine yaliyosalia yanaenda kutimilika katika hii mvua ya mwisho na yatakuja na hukumu sio kwa kuwaburudisha watu, Tunaona mfano uliotokea kwa mapigo ya Musa na Eliya. Ni mambo ya kutisha yanakuja. Na ishara ambazo hata hazijawahi kurekodiwa wala kufanywa mahali popote pale katika historia ya dunia.
Kumbuka hakuna ishara isiyokuwa na ujumbe nyuma yake. Hivyo hizi ishara zitakuja na ujumbe, na ujumbe wake utakuwa ni wa kipekee, ukisoma kitabu cha ufunuo 10:4-11″ Inaelezea zile NGURUMO SABA ambazo Yohana aliambiwa asiziandike, ni siri zilizofichwa tangu zamani nazo hazijaandikwa mahali popote katika biblia.
Zipo siri nyingi ambazo hazijulikani kwamfano “Tutakapofika kwenye utawala wa miaka 1000 ni shughuli gani zitakuwa zinaendelea , na tukienda mbinguni tutakuwa tunafanya nini huko, siri za kwenda kwenye unyakuo na siri za kurudi kwa pili kwa Yesu, kuanguka kwa shetani, na mambo yaliyokuwa yanatendeka kabla ya Adamu kuumbwa nk,(huu ni mfano tu, zinaweza zikawa nyingine tofauti ya hizo au zaidi ya hizo ) .Siri hizi zitakuja kufunuliwa katika wakati huu ambao upo karibu katika mvua hii inayokuja kunyesha.
Ndugu William Branham kabla ya kufariki kwake alionyeshwa na Bwana huu uvuvio mkubwa jinsi utakavyokuja kuwa kiasi kilichomfanya yeye mwenyewe atamani kuwepo katika huo uamsho. Katika hilo ono alionyeshwa uponyaji wa kiungu wa ajabu ukitendeka watu wengi walikuwa wakiponywa kabisa kabisa.
lakini tukisoma
Mathayo 24:14″Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.”
Mstari huu unaelezea jambo litakalofanyika kwanza kabla ya Bwana YESU kurudi, Huu uamsho unaokuja ndio utakaokuwa wa mwisho na utapita duniani kote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote, kwasababu mambo dhahiri na ishara za ajabu zitaonekana kwa watu wote na bibi-arusi naye atakusanyika pamoja kwa ajili ya unyakuo na ndipo ule mwisho utakapokuja.
Ndugu hizi siku zipo karibu, wakati huo utakapofika kama leo haujajiweka tayari kule hautaweza kwasababu zitakuja na hukumu kutoka kwa Bwana, utaishia kupinga na kusema ni vya shetani, kwasababu utasikia mambo ambayo pengine hayajarekodiwa mahali popote kwenye biblia, na hautapata uhakiki wa mambo hayo sehemu yeyote kama hauna ROHO MTAKATIFU kwasababu ni mambo mapya kabisa na hautaweza kupambanua utabakia kuwa mtu wa nia mbili kama unyasi utikiswao na upepo hutajua wapi usimame, ikiwa leo tu huwezi kumtambua yupi nabii wa kweli na yupi nabii wa uongo, utawezaje kuelewa yatakayokuja huko mbele ambapo mambo mapya yatakuja kuhubiriwa??.
Tafakari ndugu tunaishi katika siku za mwisho, ijue kalenda ya Mungu katika maisha yako na wakati tuliopo, usije ukafanana na wale wanawali wapumbavu ambao hawakuwa na mafuta ya ziada katika taa zao. Maana ya yale mafuta ya ziada ni roho ya mafunuo ambayo mkristo wa dini tu hawezi kuwa nayo.
Ndugu kaa ukifahamu Huu uamsho utaanza duniani kote hivi karibuni, na mambo ya ajabu yataenda kutendeka na kuhubiriwa, kwa waovu itakuwa ni hukumu bali kwa wenye haki itakuwa ni kwa kuandaliwa kwa ajili ya unyakuo. Maandalizi ni sasa.
“Tumeandika makala hii kuwakumbusha bibi arusi wa Kristo wote popote walipo kuwa kuna uamsho mkuu unakuja mbeleni na kuna baadhi ya watumishi wa Mungu waaminifu wachache wamekwisha anza kuonyeshwa katika maono na Bwana Yesu, jinsi utakavyokuwa. Tazama chini shuhuda chache za watu hawa;”
USHUHUDA WA STEPHEN POWELL’S
Stephen Powell’s ni muhubiri wa kimarekani hivi karibuni tarehe 21 April 2017. Bwana alimwonyesha maono yafutayo na haya ni maneno yake yaliyonukuliwa;
Kulingana na historia, “NEMBO” (Coat of Arms) ni ishara muhimu ya utaratibu wa urithishaji uliotumika katika zama za kati huko Ulaya, Ilitumika mahususi kama utambulisho katika vita, Nembo zilianzishwa kuashiria ukoo wa familia fulani, urithi, umoja, umiliki, na pia katika taaluma fulani .
Bwana kwasasa anaenda kupitisha NEMBO hii ya thamani sana kwa kizazi chenye utukufu anachokinyanyua leo duniani!, Mungu anaenda kuachilia uhalali fulani, ujuzi fulani, na urithishwaji katika roho!. Nisikilize kwa makini kitu ninachokwenda kusema sasa…
Hivi karibuni katika mfululizo wa maono niliyopewa, nilichukuliwa mbinguni nikaonyeshwa vitu vingi. Mara ya mwisho nilijikuta nimerudi katika hali yangu ya kawaida nikiwa na akili zangu juu ya kitanda changu katika hotel moja huko west Virginia. Na nilipokuwa nimelala pale nilisikia BWANA akisema ” NINARUDISHA TENA NEMBO YA VITA ALIYOKUWA AMEIVAA WILLIAM BRANHAM “. Kisha nikaona ono Bwana akishika bega la askari mmoja ambaye kwenye nguo yake kulikuwa na kitu kama NEMBO hivi ingawa sikuweza kuikariri jinsi ilivyokuwa. Kisha Bwana akaniambia ataenda kuachia vipawa vya miujiza katika mikono ya wana wake na binti zake katika hichi kipindi, kama ilivyokuwa kwa William Branham alivyopewa sio tu kuona maono bali pia kipawa katika viganja vyake.
Katika vita askari huwa wanavaa vazi fulani la nje (surcoat) kuzuia dirii isipate kutu. Hichi ndicho nilichokiona usiku ule, na ninaamini NENO la Bwana kuwa ni hili: Bwana anaenda kuendeleza haya katika roho mwaka huu hapa Marekani na itakuwa ni kwa mwendelezo wa William Branham. Dirii ya huyu mtu haitaendelea kushika kutu itatokea tena kwa mara nyingine Marekani katika huu mwaka, wamekwisha vikwa hawa matenda miujiza wapya ambao wataanza kutenda kazi mwaka huu.
Kama vile Mungu alivyoweka fimbo katika mkono wa Musa na kumwambia aende kufanya miujiza kule Misri, vivyo hivyo Mungu ataenda kufanya miujiza kupitia mikono ya hawa mashujaa ambao watatokea katika mwendelezo wa William Branham.
Branham alipewa maagizo mwaka 1946, Mungu alimwambia “miujiza itafanyika kupitia mikono yake”. Moja ya hii miujiza ilifanya kazi katika mkono wake wa kushoto na akapewa uwezo wa kupambanua roho hata kuweza kugundua uwepo wa magonjwa ya kipepo au udhaifu. Ishara ya pili aliyopewa ni kipawa cha ajabu cha maono aliweza kutambua siri za mioyo ya watu kwenye mimbari na kuwasaidia watu kuishinda roho ya kutokuamini (kitu ambacho kinazuia miujiza mingi isitendeke hapa Marekani). Mungu aliyafanya haya yote kupitia maisha ya huyu mtu na huduma yake, Hata hapa Marekani Mungu anaenda tena kufanya haya katika wakati wetu. Anaendeleza Nembo iliyokuwa kwa William Branham.
Bwana alisema msiwe na mitazamo hafifu juu ya uvuvio unaokuja wa Mungu, kwasababu ikiwa haupo katika sehemu ya huo uamsho, ni rahisi wewe kuingia katika hatari ya kumruhusu shetani aufanye moyo wako kuwa mgumu kama hautakuwa makini.
“Kuweni makini sana katika huu wakati mchunge laana mnazotoa katika midomo yenu juu ya huo uamsho unaokuja na kuuita kazi ya Mungu kuwa ni ya shetani. Kwasababu hata mafarisayo walisema maneno hayo hayo japo walikuwa wanauona uwepo dhahiri wa Mungu ukitembea katika dunia. Sio mara zote ni rahisi kufahamu kipi kinatoka kwa Mungu na kipi kinatoka kwa shetani kwahiyo usiwe mwepesi kuhukumu kimakosa huo uvuvi unaokuja. Jinyenyekezeni viongozi wangu, ” Bwana anasema ” Na kwa utulivu hukumuni kazi ya Mungu hichi kipindi kinachokuja, sana sana kama katika kazi za kanisa”
“Kwasababu mimi BWANA nitaijaribu mioyo ya viongozi wangu katika huu uvuvio unaokuja; kwasababu uvivio unaokuja unahitaji kuujaribu uongozi. Mimi BWANA nitafichua siri za mioyo yenu, na kuyakemea mawazo yenu kwa vitu ambavyo hamjawahi kusikia wala msivyovielewa. Lakini kama mkijinyenyekeza na kuwa wavumilivu katika hukumu zenu katika hichi kipindi, Mimi Bwana nitawafunulia kazi zangu ni zipi na za shetani ni zipi.
“Mimi Bwana nitawafanya mtambue tofauti kati ya mwanga na giza. Lakini hawatapewa ujuzi huo viongozi wote wenye majigambo na wenye kujikweza na kujidhani kuwa wana mamlaka yote. Hawatapewa watu wanaojiona wanajua vitu vya Mungu. Siri za Mungu hawatapewa watu wale waliowepesi kuhukumu bali wale wanyenyekevu ndio watakaopewa kuzijua hizi siri.
Katika huu uamsho unaokuja kutafunuliwa vitu vya ajabu, siri zilizojificha, na vitu ambavyo huwezi kuvitegemea, Mimi Bwana nitaleta watenda miujiza na sio tu waponyaji, hawa watafanya miujiza ambayo hamjawahi kusikia wala kuona. Lakini msiogope kwa hivyo vitu msivyovielewa, Kwa kuwa mimi Bwana nitakuwa pamoja nanyi nami nitawapa uwezo wa kutambua. Nitaenda kuwasaidia, viongozi wangu, Mitume wangu, Manabii wangu, Wachungaji wangu, lakini muwe wanyenyekevu na msiwe wepesi kuhukumu. Hili ndilo Neno nalowapeni leo kuwaanda ninyi katika huo uvuvio unaokuja.
Love & Blessings,
Stephen Powell,
Lion of Light Ministries.
Hivi karibuni ndugu Sadhu ambaye ni nabii mwenye asili ya India Bwana amekuwa akimtumia kutoa nabii nyingi na kuja kutimia ikiwemo ushindi wa Obama 2008 na Donald Trump 2016 , mafuriko na matetemeko ya ardhi, mengi pamoja na tetemeko litakalokuja kutokea Calfornia Marekani hivi karibuni, Alionyeshwa na Bwana Yesu Katika maono kwamba nguvu ya uvuvio iliyokuwepo juu ya nabii William Branham itarejeshwa tena ikiwa na nguvu mara saba”, kwa vijana wadogo ambao Mungu ataenda kuwanyanyua. Bwana alimwonyesha katika maono mengine mengi kuwa nguvu ambayo itaenda kuachiliwa katika huu wakati ukifika itakuwa ni kubwa sana na miujiza isiyokuwa ya kawaida itatendeka alisema. bofya hapa kutazama video .
Na kuna manabii wengi wameonyeshwa uamsho huo utakao kuja duniani, baadhi yao ni Rick jonyer, Kenneth Hagin, Neville Johnson, Vincent selvakumar n.k.
Kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno litathibitika. Katika neema tulionayo sasa hivi umejiwekaje tayari umepokea Roho Mtakatifu?. Jitahidi utubu ndugu injili zinazokuja huko mbele sio za kuwafanya watu watubu tena bali ni kwa ajili ya hukumu na ushuhuda kwa watu tu , wakati wa kutubu ndio sasa, wakati wa kupita katika mlango ulio mwembamba ndio sasa, Tafuta mahusiano yako binafsi na Mungu epuka kamba za madhehebu uwe tayari maana Bwana yupo mlangoni kurudi. Ndugu huu ni wakati wa kukaa chini na kumtafuta muumba wako, kalenda ya Mungu isikupite usilemewe na mambo ya ulimwengu huu, Bwana Yesu alisema tukeshe ili siku hiyo isitujie kama mwivi maana ndivyo itakavyoujia ulimwengu mzima. Kukesha sio kujizuia kulala bali ni kuwa macho rohoni, ujumbe wa Mungu unapokushukia uufahamu.
Luka 13:23-28″ Mtu mmoja akamwuliza, Je! Bwana, watu wanaookolewa ni wachache? Akawaambia,
24 Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.
25 Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako;
26 ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu.
27 Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu.
28 Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje”.
Mungu akubariki.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Kwa mawasiliano/Ushauri/kuokoka/Whatsapp. Namba zetu ni hizi
+255693036618/+255789001312
Mada Nyinginezo:
HATUA ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUTUONGOZA
ACHENI MJUE YA KUWA MIMI NI MUNGU.
NINI MAANA YA HUU MSTARI “NIMEVIPIGA VITA VILIVYO VIZURI, MWENDO NIMEUMALIZA, IMANI NIMEILINDA”?
HISTORIA YA WILLIAM BRANHAM
Hii neema tulionayo leo itafika mwisho, kuna baadhi ya misemo imekuwa ikisemwa kuwa Mungu wa agano la kale leo hii hayupo, kama yupo zile ishara alizokuwa anatenda agano la kale ziko wapi leo?. Lakini SIKU YA BWANA inakuja ndugu usitamani uwepo! USITAMANI UWEPO! ni mambo ya kuogopesha ambayo usingetamani hata adui yako yampate, Mungu kuzuia ghadhabu yake ni kwa ajili yetu sisi tutubu lakini tusipotubu hukumu itatukuta.
Kuna vitu vitatu vinavyokuja huko mbeleni, 1) DHIKI KUU, 2) SIKU YA BWANA, 3) ZIWA LA MOTO. Leo tutaitazama hii SIKU YA BWANA ni ipi, itakuja lini na itakuwa inamuhusu nani.
Kwa ufupi ndugu, DHIKI KUU itakuja na tunafahamu itakuwa kwa wakristo watakaokataa kuipokea ile alama/chapa ya mnyama. Hii itamuhusu mpingakristo akiwatesa wakristo wale waliokataa kuipokea ile chapa ya mnyama wale ambao hawakwenda kwenye unyakuo, Ambapo mwishoni mpinga-kristo atafanikiwa kuwaua kikatili wote wasioipokea chapa. Na hii dhiki itadumu kwa muda wa miaka mitatu na nusu, ni wakati wa kutisha sana unakuja mbeleni. Kwahiyo wakati wakristo wachache wanapitia dhiki kuu, wengine wote waliosalia watakuwa wanaendelea kujifurahisha na mambo yao ya dunia wakimfurahia mpinga kristo na utawala wake.
Sasa SIKU YA BWANA itaanza mara tu baada ya DHIKI KUU kuisha ambapo wale wanawali wapumbavu wote watakuwa wameshaondoka,(wameuliwa na mpingakristo) na unyakuo utakuwa umeshapita wakati huo, lakini hao waliobakia walioipokea chapa ya mnyama itawapasa waingie kwenye adhabu kali sana ya Mungu mwenyewe, Kwasababu wameshirikiana na mpinga kristo kuwaua watu wa Mungu na kwasababu wamekataa kumcha Mungu na kuzishika amri zake, ndugu Hii SIKU YA BWANA usitamani uwepo. Kumbuka haitakuwa jehanamu ya moto, bali itakuwa ni adhabu ya hapa hapa duniani.
maandiko yanasema:
Amosi 5:18 “Ole wenu! Ninyi mnaoitamani SIKU YA BWANA; kwani kuitamani siku ya Bwana? Ni giza, wala si nuru.
19 Ni kama mtu aliyemkimbia simba, akakutana na dubu; au aliingia katika nyumba akauegemeza mkono wake ukutani, nyoka akamwuma.
20 Je! Siku ya Bwana haitakuwa giza, wala si nuru? Naam, yenye giza sana, wala haina mwanga.“
Pia tukisoma…
Isaya 13:6″ Pigeni kelele za hofu; maana SIKU YA BWANA i karibu; itanyesha kama maangamizi yatokayo kwa Mwenyezi Mungu.
7 Kwa sababu hiyo mikono yote italegea, na moyo wa kila mtu utayeyuka.
8 Nao watafadhaika; watashikwa na utungu na maumivu; watakuwa na utungu kama mwanamke aliye karibu na kuzaa; watakodoleana macho; nyuso zao zitakuwa ni nyuso za moto.
9 Tazama, siku ya Bwana inakuja, siku kali, ya hasira na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake.
10 Maana nyota za mbinguni na matangamano havitatoa nuru yake; jua litatiwa giza wakati wa kucha kwake, na mwezi utaacha nuru yake isiangaze.
11 Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayaangusha chini majivuno yao walio wakali;
12 nitafanya wanadamu kuadimika kuliko dhahabu safi, na watu kuliko dhahabu ya Ofiri.”
Maandiko yanaposema SIKU YA BWANA hayamanishi ni siku kama siku moja, bali inamaanisha ni kipindi fulani cha WAKATI ambacho Bwana amekitenga kwa kusudi fulani. Kama maandiko yanavyotueleza ni kipindi ambacho kimetengwa cha GHADHABU NA HASIRA ya Mungu kulipiza kisasi kwa wanadamu wote wasiomcha Mungu.
Kipindi Hichi cha SIKU YA BWANA kitadumu kwa muda wa siku 75, Hizi zimepatikana kutoka katika kitabu cha Nabii Danieli 12:12, ambapo tunaona kipindi cha ile dhiki kuu kitadumu kwa muda wa siku 1260, na hapo zimeongezeka siku nyingine kutoka siku 1260 mpaka kufikia siku 1335, kwahiyo ukichukua hizo siku 1335-1260=75.
Kwahiyo hizi siku 75 zilizoongezwa ni mahususi kwa ajili ya BWANA kujilipizia kisasi kwa wanadamu wote waliosalia juu ya uso wa nchi.
Kabla ya SIKU hiyo ya BWANA kuanza Kutakuwa na baragumu saba zitakazopigwa kuitangulia , Hizi Zitabeba hukumu kwa watu wote, kama onyo watu watubu kumgeukia Mungu, Dunia itapigwa kwa mapigo mengi ya ajabu ukisoma Ufunuo 8 utaona hili, ikiwemo, theluthi moja ya maji kuwa damu, theluthi ya maji duniani kutiwa uchungu,theluthi ya mwezi na jua na nyota kupigwa,hebu tafakari kutakuwaje duniani wakati huo mchana kutakuwa kama jioni, giza litakuwa nene usiku na baridi kali sana, nzige wa ajabu watapandishwa kutoka kuzimu, maumivu yao ni kama ya kung’wata na nge, na meno yao ni kama meno ya simba, n.k.
Biblia inasema watu watakitamani kifo lakini hawatakiona, kumbuka hapo bado SIKU YA BWANA haijaanza huo ni mwanzo wa utungu tu, unatangaza hukumu KUU ya Bwana inayokuja mbeleni kwa urefu soma ufunuo sura ya 8 na ya 9. inaelezea haya mapigo ya baragumu saba za Mungu.
Lakini pamoja na mapigo yote hayo ya baragumu biblia inasema watu watakaokuwa juu ya uso wa nchi hawatatubu maovu yao kwasababu roho ya uovu imeshakaa juu yao kwa kuwa wote wamekwisha ipokea ile chapa ya mnyama neema ya Mungu imeondoka juu yao hawawezi kutubu tena.
Kwahiyo mara baada ya dhiki kuu ya mpinga-Kristo kuisha hapo tayari unyakuo ulishapita siku nyingi na wanawali wapumbavu kuuliwa, Sasa Hawa wanadamu waliobaki ndio watakaoingia katika mapigo ya vitasa Saba vya Mungu , katika hayo ghadhabu ya Mungu imetimia : Hebu tutazame vitasa hivi kimoja baada ya kingine.
Ufunuo 16:1 ” Nikasikia sauti kuu kutoka hekaluni, ikiwaambia wale malaika saba, Enendeni, mkavimimine vile vitasa saba vya ghadhabu ya Mungu juu ya nchi.
2 Akaenda huyo wa kwanza, akakimimina kitasa chake juu ya nchi; pakawa na JIPU BAYA, BOVU, juu ya wale watu wenye chapa ya huyo mnyama, na wale wenye kuisujudia sanamu yake.”
Sasa adhabu hizi zitakuwa ni kwa Dunia nzima na sio theluthi tena ya dunia kama ilivyokuwa kwa zile baragumu saba. Majipu haya tunaona ni mfano wa yale yale waliopigwa wamisri, Kutakuwa na majipu ya ajabu usidhani ni haya ya kuwaida uliyoyazoea, biblia imeyaita ni MAJIPU MABOVU bado hajatokea kabisa duniani, huo ugonjwa bado haujazuka, Tuna magonjwa mengi ya hatari duniani lakini biblia haijayataja yote hayo, lakini ni huu ugonjwa wa MAJIPU tena jipu bovu ndio umetabiriwa utakuja, homa yake itakuwa sio kama hizi za kawaida tulizozizoea. Ndugu usitamani kuwepo huko wewe unayesema Mungu wa agano la kale haishi, siku hiyo utayaona haya wazi wazi.
Ufunuo 16:3 “Na huyo wa pili akakimimina kitasa chake juu ya bahari, ikawa damu kama damu ya mfu, na vitu vyote vyenye roho ya uhai katika bahari vikafa.” .
Duniani kutakuwa na harufu kama ya damu ya mtu aliyekwisha kufa, fikiria jambo hilo dunia nzima kutoa uvundo, hakutakuwa na kiumbe chochote baharini chakula kitapungua duniani, maji yataisha, shughuli za usafirishaji baharini nk. vitakwama, mvua zitaacha kunyesha duniani kutakuwa sio sehemu ya kuishi tena mwanadamu, taabu itaongezeka duniani, hofu kuu itawaingia watu wakitazama ni mambo gani haya yameipata dunia?.. lakini bado mapigo yatakuwa yanaendelea,
Ufunuo 16:4-7 ” Na huyo wa tatu akakimimina kitasa chake juu ya mito na chemchemi za maji; zikawa damu.
5 Nami nikamsikia malaika wa maji akisema, Wewe u mwenye haki, uliyeko na uliyekuwako, Mtakatifu, kwa kuwa umehukumu hivi;
6 kwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu na ya manabii, nawe umewapa damu wainywe; nao wamestahili.
7 Nikaisikia hiyo madhabahu ikisema, Naam, Bwana Mungu Mwenyezi, ni za kweli, na za haki, hukumu zako. “
Baada ya bahari kugeuzwa kuwa damu ya mizoga, watu wote tunajua wangekimbilia kutafuta maji katika mito na kwenye chemchemi za maji, kutokana na kiu kikali, lakini Bwana atayapiga pia maji ya mitoni na chemchemi, wakati huo fedha itakuwa haifanyi kazi tena, Mtu tajiri atakuwa ni mwenye kikombe cha maji safi mkononi mwake na sio fedha, Kwahiyo Bwana atawalazimisha kuyanywa hayo maji ya DAMU kwasababu walishirikiana na yule mnyama kumwaga damu ya watakatifu wa Mungu, hivyo nao Bwana amewapa wainywe. Na kwasababu ya kiu kali watakunywa hiyo damu, na wanadamu wengi wataangamia na kufa kwa pigo hilo.
Ufunuo 16:8-9 “Na huyo wa nne akakimimina kitasa chake juu ya jua, nalo likapewa kuwaunguza wanadamu kwa moto.
9 Wanadamu wakaunguzwa maunguzo makubwa, nao wakalitukana jina la Mungu aliye na mamlaka juu ya mapigo hayo; wala hawakutubu wala kumpa utukufu.”
Baada ya pigo la maji kuwa damu, jua litashushwa chini, maunguzo yatakuwa ni makubwa sana, joto litaongezeka duniani kwa nyuzi joto kubwa kuliko kiwango cha kawaida. Mimea yote itakauka, dunia itafanana na jangwa ndani ya muda mfupi sana, jaribu kutafakari jipu linapigwa na jua kali halafu hakuna maji hata kidogo ya kujipooza,ni dhiki kiasi gani? ni mambo ambayo huwezi dhania yatatokea lakini yapo mbioni kutokea. Lakini pamoja na hayo mapigo yote biblia inasema watu watamtukana Mungu hawatatubu. Mfano tu wa kizazi chetu hichi watu wanapopatwa na majanga badala wageuke na kumuuliza Mungu ni kwanini na kutubu, wao wanalaani.
Ufunuo 16:10-11 “Na huyo wa tano akakimimina kitasa chake juu ya kiti cha enzi cha yule mnyama; ufalme wake ukatiwa giza; wakatafuna ndimi zao kwa sababu ya maumivu,
11 wakamtukana Mungu wa mbingu kwa sababu ya maumivu yao, na kwa sababu ya majipu yao; wala hawakuyatubia matendo yao. “
Sasa pigo hili linamuhusu sana sana yule mnyama aliyewakosesha wanadamu wote kuipokea ile chapa, mahali kiti chake cha enzi kilipo ambapo ni VATICAN, Roma, Mungu ataachilia laana kwa mataifa ya ulaya ambayo ndio zile pembe kumi, zitamchukia na kumwangamiza yule mwanamke kahaba (Kanisa Katholiki) ambalo makao yake makuu ni VATICAN.
Hii ni kutokana na kwamba yale mataifa ambayo yalimtumaini mpinga kristo ayaletee amani duniani, hayajaletewa zaidi ya yote mpingakristo (PAPA) ameiongezea dunia matatizo hivyo basi watamchukia na kumwangamiza, tangu wakati huo utawala wa Roma, pamoja na mpinga kristo (PAPA) na Vatican yake hawatakuwepo tena ufalme wao umekwishatiwa giza.
Soma
ufunuo 17:16″ Na zile pembe kumi ulizoziona, na huyo mnyama, hao watamchukia yule kahaba, nao watamfanya kuwa mkiwa na uchi, watamla nyama yake, watamteketeza kabisa kwa moto. ”
Ufunuo 16:12 “Na huyo wa sita akakimimina kitasa chake juu ya mto ule mkubwa Frati; maji yake yakakauka, ili njia itengenezwe kwa wafalme watokao katika maawio ya jua.
13 Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo.
14 Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.
15 (Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.)
16 Wakawakusanya hata mahali paitwapo kwa Kiebrania, Har-Magedoni.”
Kitasa hichi kunazungumzia ile vita kuu ya HAR MAGEDONI ambayo itakuwa ni vita kati ya Mungu mwenyezi akilipigania taifa la Izraeli dhidi ya wafalme wote wa dunia. karibu kila taifa litaunga mkono vita hii wakiongozwa na mataifa kutoka mawio ya jua. Haya mataifa ya mawio ya jua ni mataifa ya mashariki, nayo ni CHINA,JAPAN, KOREA n,k. Wakati huo Vatican itakuwa haipo, Marekani itakuwa haipo, Urusi itakuwa haipo yatatoweshwa katika vita vilivyoelezwa katika ezekieli 38 & 39,
Kwahiyo zile roho chafu ambazo zilikuwa zinaendesha Vatican na Marekani zitahamia kwenye haya mataifa ya mashariki yaliyosalia kwa ajili ya vita dhidi ya Izraeli. Wakati huo ndio Bwana YESU atakapotokea kuwapigania watu wake Izraeli. Ndugu wakati huo dunia itakuwa mfano wa sayari ya Zebaki, hakutakuwa na maji, chakula, magonjwa, joto litakuwa juu sana,maji yote damu, machafuko pamoja na vita, usitamani ndugu yangu uwepo nakuombea Mungu usiwepo itakuwa ni vilio na kusaga meno, siku hiyo watu watatamani siku hizi za neema tulizonazo leo hawataziona.
Ambacho ndio hasaa kinaizungumzia ile siku ya Bwana..
Ufunuo 16:17-21 ” Na huyo wa saba akakimimina kitasa chake juu ya anga. Sauti kuu ikatoka katika hekalu, katika kile kiti cha enzi, ikisema, Imekwisha kuwa.
18 Pakawa na umeme na sauti na radi; na palikuwa na tetemeko la nchi kubwa, ambalo tangu wanadamu kuwako juu ya nchi hapakuwa namna ile, jinsi lilivyokuwa kubwa tetemeko hilo.
19 Na mji ule mkuu ukagawanyikana mafungu matatu, na miji ya mataifa ikaanguka; na Babeli ule mkuu ukakumbukwa mbele za Mungu, kupewa kikombe cha mvinyo ya ghadhabu ya hasira yake.
20 Kila kisiwa kikakimbia, wala milima haikuonekana tena.
21 Na mvua ya mawe kubwa sana, ya mawe mazito kama talanta, ikashuka kutoka mbinguni juu ya wanadamu. Wanadamu wakamtukana Mungu kwa sababu ya lile pigo la mvua ya mawe; kwa maana pigo lake ni kubwa mno.”
Hili ni pigo la mwisho, na katika hili ghadhabu ya Mungu imetimia tukisoma pale muhuri wa sita ulipofunguliwa ulitoa picha halisi jinsi hii siku itakavyokuwa soma Mathayo 24:30-31 na pia Ufunuo 6:12-17
Ufunuo 6:12-17 ” Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu,
13 na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi.
14 Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake.
15 Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima,
16 wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo.
17 Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?”
Pigo la saba la mwisho kama tunavyosoma ni baya kuliko yote yaliyotangulia maana jua linaondolewa, mwezi utakuwa damu, nyota zitatoweka, unaweza kuona kutakuwa na giza kiasi gani duniani, na baridi kiasi gani,litakuwaa ni giza zito sana, hakutakuwa na chanzo chochote cha umeme, shughuli zote za kimaendeleo zilishamalizwa katika mapigo yaliyotanguliwa, hadi kufikia hapa watu wachache sana watakuwa wamesalia duniani, kumbuka hapo bado ziwa la moto linasubiri watu, Hichi ni kisasi cha hapa hapa duniani.
Mvua ya mawe kubwa sana itanyesha, mawe kama talanta,(talanta 1 ni kama kg 34), Huwezi kujificha kwenye nyumba yako ya bati au ya kigae, kg 34 ni uzani mkubwa sana itaambana na tetemeko ambalo halijawahi kutokea, kiasi cha kwamba visiwa vitahama, kisiwa cha zanzibar kitapotea, Milima itatapika volkano, kumbuka hayo yote yatafanyika katikati ya giza nene, hakuna mawasiliano. hapo hakuna mfalme wala mtumwa, raisi wala mwananchi wote waliosalia watatamani wafe kuliko kuishi, watatamani milima iwaangukie waikwepe ghadhabu ya Mungu, Hapo ndipo itakapoonekana ishara ya mwana wa Adamu mawinguni.
Soma
Mathayo 24:29 “Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika; 30 ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi. “
Rafiki haya mambo ni kweli yatatokea, ndivyo yatakavyokuja kuupata ulimwengu na dalili zote zinaonyesha kuwa yatatokea katika kizazi chetu tunachoishi mimi na wewe, Bwana amekwisha kutuonya mbele, Nia yake ni sisi tuiepuke hiyo ghadhabu na ndio maana kuna mahali alisema alipokuwa katikati ya kitasa cha sita (Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake). Kwahiyo ametuonya tukeshe na kuyatunza mavazi yetu, maana hii siku ya ghadhabu itakuja ghafla.
Ndugu kimbia injili ambazo zinakufanya usifikiri hatma ya maisha yako ya milele badala yake inakupeleka kutazama mambo ya ulimwengu huu. Hii ni roho ya shetani inawapumbaza wengi wafikiri mambo hayo yatakuja kutokea baada ya miaka 2000 mbele, usidanganyike ni uongo wa shetani, ndugu dalili zote zinaonyesha, unabii wote umetimia kwamba tunaishi katika kizazi cha hatari sana.
Chunguza maisha yako angali neema ipo, mambo hayatakuwa hivi siku zote, pale mlango wa neema utakapofungwa kutakuwa hakuna kurudi nyuma itakuwa ni vilio na maombolezo, kimbilia kalvari sasa tubu dhambi zako, uoshwe kwa damu ya Yesu, na Upokee Roho Mtakatifu kabla ya huo wakati kufika. Kumbuka adhabu ya hii SIKU YA BWANA, sio jehanamu ya moto, baada ya mapigo hayo ndipo ziwa la moto ziwa la moto litafuata.
Ikiwa unataka kumpa Bwana Yesu maisha yako na kugeuka leo tubu mwenyewe moyoni mwako au fuatiliza sala hii kwa imani:
Sema:
“Bwana Yesu, Leo hii nasogea mbele zako nikiwa mwenye dhambi, natubu makosa yangu yote niliyokukosea, naomba unisamehe, nimeamua kugeuka leo, nisaidie Bwana Yesu, neema yako iwe juu yangu, nikuishie wewe, siku zote za maisha yangu, asante Bwana Yesu kwa kunisikia na kunisamehe. AMEN! “.
Baada ya kutubu unahitaji kubatizwa, Hivyo basi tafuta kanisa linalobatiza ubatizo sahihi nao ni kwa kuzamishwa kwenye maji mengi na ni kwa jina la YESU KRISTO, Kwa kufanya hivyo Bwana atakupa kipawa cha Roho Mtakatifu na utakuwa umekamilisha wokovu wako.
MUNGU AKUBARIKI.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Kwa msaada zaidi, wa kanisa, au mafundisho, au ushauri, piga namba hizi
+255693036618/ +25578901312
Mada Nyinginezo:
KIKOMBE CHA GHADHABU YA MUNGU KINAJAA…TUBU UMGEUKIE MUNGU
NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE.
JE! SISI NI WAFALME NA MAKUHANI KWA NAMNA GANI?
PETRO ALIAMBIWA NA BWANA YESU UKIONGOKA WAIMARISHE NA NDUGU ZAKO. JE! KUONGOKA MAANA YAKE NINI?
Mpinga-Kristo ni nani?
Vita kubwa inayoendelea duniani leo ni vita kati ya MUNGU na SHETANI. Mungu anatafuta roho za watu vile vile shetani naye anawinda roho za watu. Hizi roho mbili zimekuwa zikipingana siku zote tangu ulimwengu ulipoanza kukaliwa na wanadamu.
Lakini baada ya mwanadamu kuanguka Mungu alitumia njia zote kwa Roho wake kumvuta kwake tena, mwishoni akaona vema kumleta mwanawe mpendwa YESU KRISTO kwa dhumuni moja tu! kutupatanisha sisi na Mungu, ili katika yeye sisi sote tuokolewe.
Vivyo hivyo shetani naye, kwa kuona hivyo kwa roho yake ya uovu, alitumia njia zake zote za kuweza kumtoa mwanadamu katika kusudi la Mungu na kumvuta kwake, jambo hili lilianza tangu Edeni, tunaona shetani jinsi alivyomtumia Nyoka kumdanganya Hawa ili aipate roho yake. Hivyo basi ulipofika wakati alipoona Mungu amemleta mwokozi katika mwili yaani YESU KRISTO na kuwavuta wengi kwa BABA, yeye naye alianza mipango ya kumwandaa mtu mmoja ambaye atakuwa na kazi maalumu ya kuwavuta watu kwake na kwenda kinyume na huyo mmoja Mungu aliyemteua (yaani YESU KRISTO). Sasa mwana huyu wa shetani ndiye anayeitwa MPINGA-KRISTO.
Kumbuka vita vya kwanza kabla ya Kristo kuja vilikuwa ni roho kwa roho (yaani Roho wa Mungu dhidi ya roho ya shetani), lakini vita vya mwisho ni MTU dhidi ya MTU (yaani YESU KRISTO dhidi ya MPINGA-KRISTO).
Wakristo wengi wanapokosa shabaha ni pale wanaposhindwa kumfahamu YESU KRISTO ni nani na MPINGA-KRISTO ni nani?. Ukishindwa kumfahamu YESU KRISTO ni nani huwezi kumfahamu MPINGA-KRISTO ni nani.
Hawa wote wawili waliandikwa kwenye NENO la Mungu katika “SIRI”. Ikiwa na maana utendaji kazi wao ulihitaji “UFUNUO wa ROHO” Kuutambua. Embu kwa ufupi, tutazame siri iliyopo kwa YESU KRISTO ambayo ilikuwa imefichika kwa Muda mrefu na hata sasa baadhi ya watu bado imefichika machoni pao.
1 Timotheo 3:16 ” Na bila shaka SIRI YA UTAUWA NI KUU. Mungu alidhihirishwa katika MWILI, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.”
Ukisoma hapo utaona kuwa jambo hili Mungu aliliweka liwe SIRI,na sio kitu cha wazi ya kwamba Yesu Kristo alikuwa ni MUNGU KATIKA MWILI. Yaani ni Roho ya Mungu ikitenda kazi katika mwili, lakini wengi hawakulijua hilo walimkataa na kumsulubisha,na hata leo wengi hawalifahamu hilo. maana Bwana Yesu alisema “Yohana 5:43 Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, wala ninyi hamnipokei; mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea huyo. “ unaona huyo mwingine BWANA YESU aliyemzungumzia akija kwa jina lake mtampokea ni MPINGA-KRISTO mwenyewe..tusome tena mstari ufuatao
1 Wakoritho 2:6-8″ Walakini iko HEKIMA tusemayo KATI YA WAKAMILIFU; ila si hekima ya dunia hii, wala ya hao wanaoitawala dunia hii, wanaobatilika;
7 bali twanena HEKIMA YA MUNGU KATIKA SIRI, ILE HEKIMA ILIYOFICHWA, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu;
8 ambayo wenye kuitawala dunia hii hawaijui hata mmoja; maana kama wangaliijua, WASINGALIMSULIBISHA BWANA WA UTUKUFU; “.
Kwa maandiko hayo hapo juu, hata leo watu katika mioyo yao wanamchukulia YESU KRISTO kama ni mtu wa kawaida kama walivyofanya watu wa kipindi kile, wanayadharau maneno yake sio kwa mdomo bali kwa matendo, lakini hawajui kuwa wanamkataa na kumsulibisha Mungu mwenyewe ambaye ni BWANA WA UTUKUFU, kwa heshima aliitoa damu yake, imwagike kwa ajili ya dhambi zetu kutupatanisha sisi na yeye lakini bado leo hii unaichezea hii damu ya thamani, itafika wakati hii neema haitakuwepo tena.
2 Wathesalonike 2:3 “Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; AKAFUNULIWA YULE MTU WA KUASI , MWANA WA UHARIBIFU;
4 YULE MPINGAMIZI, AJIINUAYE NAFSI YAKE JUU YA KILA KIITWACHO MUNGU AMA KUABUDIWA; hata yeye mwenyewe kuketi katika HEKALU LA MUNGU, AKIJIONYESHA NAFSI YAKE KANA KWAMBA YEYE NDIYE MUNGU.
5 Je! Hamkumbuki ya kuwa wakati nilipokuwapo pamoja nanyi naliwaambieni hayo?
6 Na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake.
7 Maana “ILE SIRI YA KUASI” HIVI SASA INATENDA KAZI; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa.
8 Hapo ndipo atakapofunuliwa yule ASI, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake;
9 yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo;
10 na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa.”
Ukisoma habari hiyo mstari wa saba inazungumzia SIRI YA KUASI ambayo inatenda kazi duniani, na hii siri ya kuasi inatenda kazi ndani ya yule ASI (ambaye ndio mpinga-kristo mwenyewe) kama maandiko yanavyomtaja kwenye mstari wa 9, kuwa “kutenda kwake kazi ni mfano wa kutenda kwake shetani mwenyewe”. Kama tu vile SIRI YA UTAUWA ilivyokuwa inatenda kazi ndani ya YESU KRISTO, na kutenda kwake kazi Yesu kulikuwa ni mfano wa kutenda kwake Mungu mwenyewe vivyo hivyo na huyu (Mpinga-kristo) siri ya kuasi inatenda kazi ndani yake na kutenda kwake kazi kutakuwa ni mfano wa shetani.
Baada ya shetani kuona kuwa hawezi kuwapata wanadamu wengi kwa kutaka wamwabudu moja kwa moja kama wanadamu wamwabuduvyo Mungu, aliamua kujibadilisha na kujifanya kuwa kama malaika wa Nuru (2Wakoritho 11:14), ili awapate wale wanaoonyesha dalili ya kuipenda Nuru. Kumbuka shetani hafanyi vita na watu wa ulimwengu huu, kwasababu hao alishawapata na siku zote wapo gizani, kwahiyo ili awapate wale wa nuruni ni lazima ajigeuze kuwa mfano wa malaika wa Nuru, vivyo hivyo na watumishi wake nao ni lazima wajigeuze kuwa kama watumishi wa nuru. Hapo ndipo penye vita vikali pale mbwa-mwitu anapokuja kwa vazi la kondoo. Hivyo inahitaji hekima ya Roho Mtakatifu kumtambua mpinga-kristo vinginevyo hawatakaa ufahamu adui yako yupo wapi na anatendaje kazi.
Ndugu kuna vikundi vingi vya kishetani na kichawi, vinavyosifika kama freemason, rotary clubs, iluminati, ku klux klan, brotherhood, n.k. vimekuwa vikiogopeka kana kwamba hivyo ndio makao makuu ya shetani, usidanganyike vikundi hivyo shetani anavitumia kuwadaka watu wasiokuwa wakristo na wakristo wachache wenye imani isiyothabiti kwasababu mkristo wa kweli yoyote hawezi kwenda kwa mganga na shetani analijua hilo, wala hawezi kujiunga kwenye mojawapo ya hivyo vikundi wala kupiga ramli, au kupunga-pepo, shetani anajua kabisa kama angetegemea njia hiyo tu, basi angewakosa wakristo wengi sana duniani. Anafahamu kuwa mkristo mahali pake pekee anajihisi atakutana na Mungu ni kanisani na ndiko huko huko anapowafuata wakristo.
Kumbuka, shetani anatenda kazi katika SIRI, na ndiyo maana ikaitwa “SIRI YA UASI”. na inatenda kazi ndani ya Kanisa la Mungu pale shetani anapovaa mavazi ya kondoo lakini ndani ni MBWA-MWITU(Hii ni SIRI). kuharibu roho za watu(wakristo wa kweli) na kuwapeleka kuzimu. Anatumia hila zake kuwafanya watu waone kama wanamwabudu Mungu, kumbe wanamwabudu yeye.
Anaingia kanisani na kuwafanya watu wajione kuwa wapo katika njia sawa, lakini mwisho wake ni kuzimu,. Na anaowapeleka kuzimu kwa njia hii ni kubwa sana kuliko hata hizo njia nyingine ndogo ndogo kama uchawi, freemason n.k. HAPA NDIPO KRISTO ALIPOTUTILIA MSISITIZO KWAMBA “TUJIHADHARI NA MANABII WA UONGO, WANAOVAA MAVAZI YA KONDOO LAKINI NDANI NI MBWA-MWITU WAKALI”..Ndugu, Bwana hakutuonya tujihadhari na wachawi au wapiga-ramli, au freemason, au wapunga-pepo hilo ni jambo dogo sana ambalo kwa namna ya kawaida mkristo yoyote anaweza kujihadhari nayo.
Baada ya shetani kujiingiza kwa siri kwenye kanisa la Mungu na kukomaa kwa muda mrefu, tunaona alianza kwa kuharibu mafundisho ya Mungu ya kweli na kupachika mafundisho ya kipagani kama ibada za wafu, ibada za miungu mitatu, kuongeza vitabu katika NENO la Mungu, Ibada za sanamu kanisani, kubariki pombe kanisani, na kupindisha maandiko na utaratibu uliokuwepo wa kanisa kwa kupotosha ubatizo sahihi wa maji, na wa Roho Mtakatifu, kwa kuua karama za roho, kuingiza siasa na vyeo katika kanisa visivyotakana na Mungu,kuua mafundisho ya uponyaji wa kiungu, n.k.
Kwa kuendelea hivyo alifanikiwa kutengeneza kanisa lake moja “MFU” lenye jina linalofanana na lile kanisa la mwanzo la kweli lakini sio, watu wakidhani kuwa ndio lile kanisa la kwanza (la Mitume) kumbe wamepotea pasipo wao kujua ROHO MTAKATIFU ameshaondoka muda mrefu imebaki roho ya shetani ikitawala, Kwahiyo shetani akalipa jina hili kanisa lake akaliita UNIVERSAL CHURCH yaani KANISA LA ULIMWENGU (KANISA KATOLIKI).
Na yeye (shetani) akiwa kama mungu wa hilo kanisa aliweka watumishi wake, Na akaweka cheo cha juu zaidi kabisa katika hilo kanisa ambacho ndio cheo kile cha UPAPA (hichi ndicho cheo cha MPINGA-KRISTO mwenyewe) kisimame kwa niaba yake duniani kama Yesu Kristo alivyosimama kwa niaba ya Mungu duniani.
Tunafahamu katika historia chombo chake kiteule alichokitumia shetani kupambana na uzao wa Mungu ni KANISA KATOLIKI,na si kingine, lilifanikiwa kuua zaidi ya wakristo milioni 68, waliojaribu kuenda kinyume na mifumo yake ya kipagani. Na hadi leo kanisa hili linaendelea kuuwa watu wengi kiroho, kwa kudhani wanamwabudu Mungu kumbe wanamwabudu shetani katika hilo kanisa. Na litakuja kuuwa wengi zaidi katika kipindi cha ile dhiki kuu. HAYA NDIYO MALANGO YA KUZIMU.
Hivyo basi roho ya mpinga-kristo inakaa katika cheo cha UPAPA, kwahiyo mtu yeyote atakayekikalia hicho cheo atakuwa amekidhi vigezo vyote kuwa MPINGA-KRISTO.
Injili iliyopo leo hii, kulingana na wakati tunaoishi sio injili tu ya kuwavuta watu kwa Kristo, kwasababu wengi wameshampokea Kristo lakini hawajui kuwa wanamwabudu shetani pasipo wao kujua katika madhehebu yao wakidhani kuwa wapo sawa kumbe hawapo sawa. Ndugu Mungu kashatoa laana juu ya kanisa Katoliki na madhehebu yote yasiyokaa chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu, (maana haya kwa pamoja ndiyo yanayounda ile chapa ya mnyama). Kwa kufahamu zaidi kwa undani juu ya chapa ya mnyama unaweza kusoma soma tuliloliandika linaloitwa “CHAPA YA MNYAMA”.
Haya ndiyo maneno ya Bwana mwenyewe.
Ufunuo 18:4-5″ Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, TOKENI KWAKE, ENYI WATU WANGU, MSISHIRIKI DHAMBI ZAKE, WALA MSIPOKEE MAPIGO YAKE.
5 Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake. “
Bwana anatuonya tutoke (sio kutoka kwa miguu bali kwa roho. Yaani kujihadhari na mafundisho yote yasiotoka na Mungu, ukiri ukristo wa biblia usiukiri udhehebu) Toka katika kamba za madhehebu, umwabudu Mungu katika roho na kweli kwasababu hayo yamefanya uasherati wa kiroho kwa kuchanganya NENO la Mungu na mafundisho ya kipagani hivyo Bwana ameyahukumu na yoyote atakayeshirikiana nayo atashiriki katika mapigo yake yote yaliyoandaliwa kwasababu yameshiriki katika kumwaga damu nyingi za watakatifu wa Mungu.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
Kitabu cha uzima ndio kipi?
Ufunuo 20:11-15
11 Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana.
12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na VITABU VIKAFUNGULIWA; na KITABU KINGINE KIKAFUNGULIWA, AMBACHO NI CHA UZIMA; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa KATIKA VILE VITABU, sawasawa na MATENDO YAO.
13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.
14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto.
15 NA IWAPO MTU YEYOTE HAKUONEKANA AMEANDIKWA, KATIKA KITABU CHA UZIMA, ALITUPWA KATIKA LILE ZIWA LA MOTO.”
Amina! Tukifuatilia mistari hiyo hapo juu tunaona katika ile siku ya mwisho ya Hukumu Bwana Yesu atakapoketi kuwahukumu wanadamu katika kiti chake cheupe cha enzi, kutakuwa na aina kuu mbili za vitabu: KITABU CHA UZIMA na VITABU VINGINE,. Hapo unaona kitabu cha uzima kinaonekana ni kimoja tu!. Lakini pia kuna vitabu vingine, ikiashiria ni vingi, kwa ufupi tuvichunguze hivi vitabu ni vitabu gani;
1) KITABU CHA UZIMA:
Kama kinavyojielezea ni kitabu kinachoelezea UZIMA, kama vile kitabu cha hesabati kinaelezea njia za hesabu, kitabu cha jeografia kinaelezea masuala ya kijeografia vivyo hivyo na vitabu vingine vyote. Na tunafahamu vitabu huwa vinagawanyika katika kurasa mbali mbali. Lakini tunaona vitabu vyote hivi tulivyonavyo duniani vinatueleza tu kanuni na mbinu za mambo mengi yahusuyo ulimwengu huu, na tunaona hakuna kitabu chochote ulimwenguni kilichoweza kuelezea UZIMA wa mwanadamu isipokuwa BIBLIA TU!. Kwahiyo kitabu cha uzima kinachozungumziwa hapo ni BIBLIA ambalo ni NENO LA MUNGU.
2) VITABU VINGINE
Tunaona biblia imevitaja kuwa ni vingi, hivi navyo vinaelezea habari fulani na sio nyingine zaidi ya wanadamu kulingana na biblia inavyosema. Hivi ni VITABU vya wanadamu na kila mwanadamu anacho cha kwake, kikimwelezea maisha yake jinsi alivyoishi hapa duniani kwa muda wote aliopewa hapa duniani kuanzia kuzaliwa kwake mpaka kufa kwake. Na hivi navyo vina ukurasa, ambazo ni hatua unazopitia hapa duniani, Lakini hivi vitabu vyote havina uzima ndani yake, kitabu cha UZIMA ni kimoja tu, na ndio maana hivi vyote vinakitegemea hicho cha UZIMA kutoa hatma ya mwanadamu.
Kwahiyo kile kitabu cha UZIMA kinaelezea kanuni na taratibu za mwadamu anavyopaswa aishi hapa duniani ili aupate huo uzima uliondikwa ndani yake, hivyo basi kama wanadamu tunaoandika vitabu vya maisha yetu tunapaswa tuviandike vifanane na kile cha UZIMA yaani BIBLIA, kuanzia utoto wetu mpaka kuondoka kwetu duniani vitabu vyetu vinatakiwa vifanane na cha UZIMA, na huko ndiko KUONEKANA KWA MAJINA YETU KATIKA KITABU CHA UZIMA.
Hivyo ndugu kitabu chako unakiandikaje? angalia muda unavyokimbia! usiseme nitampokea Kristo au nitaishi maisha matakatifu nifikisha umri fulani au nikishapata kitu fulani. Jua mpaka sasa kitabu chako kinaendelea kuandikwa na ndivyo kurasa zinavyozidi kufunguka na kufunga, muda unavyozidi kwenda ghafla utajikuta kitabu chako kimefungwa kinasubiriwa kufunguliwa kwenye ILE SIKU YA HUKUMU.
Na siku ile ya Hukumu kile cha UZIMA kitafunguliwa na cha kwako pia kitafunguliwa, vitalinganishwa, kama vinafanana au la! ‘”HUKO NDIKO KUHAKIKIWA JINA LAKO”. Kama Jina lako halikuonekana inamaanisha kitabu chako (maisha yako), Hayaendani na kile cha UZIMA (yaani Biblia, NENO LA MUNGU). Hivyo basi kwa kuwa hauna UZIMA ndani yako sehemu yako itakuwa katika lile ziwa liwakalo Moto na kibiriti.
Kama mkristo maisha yetu kila siku tunapaswa tuyalinganishe maisha yetu na biblia, je! tukifanyacho kinaendana na kitabu cha uzima?. unafahamu kabisa waasherati, wazinzi, walevi, watukanaji, waabudu masanamu, waongo, wasengenyaji, mashoga, wasagaji, wavutaji sigara, wafanyaji wa mustarbation, watazamaji wa pornography, waizi, mafisadi,waendaji kwa waganga na wapiga ramli, wala rushwa, wauaji, nk, watu wa dizaini hii maisha yao yapo mbali na kile kitabu cha UZIMA, unategemea vipi uonekane katika kile kitabu, kumbuka majina yanayozungumziwa pale sio John, Yohana au Mary bali ni maisha yako Jihakiki ndugu komboa wakati siku hizi ni za mwisho. soma.
Ufunuo 21:27 ” Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo.”
Siku zote Kitabu hakiandikwi katika siku moja, ili kitabu chako kifanane na kile cha UZIMA Sio hatua ya siku moja bali ya maisha yako ya kila siku, usiishi maisha ya kuidharau injili leo ukasema siku moja nitamgeukia Mungu, usijinganye kile kitabu haukifananishi ndani ya siku moja inahitaji maisha. Bwana YESU alisema
Luka 9:23″ Akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake KILA SIKU, anifuate. ” Unaona sio siku moja.
Maombi yangu ni wewe umgeukie Mungu. Anza kukiandika kitabu chako vizuri katika muda wako wa maisha uliobakiza hapa duniani, kila siku kifananishe kitabu chako na cha UZIMA ili siku ile ikifika JINA LAKO LIONEKANE. UIEPUKE HUKUMU.
Mungu akubariki!
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Kwa mawasiliano/Ushauri/kuokoka/Whatsapp. Namba zetu ni hizi
+255693036618/+255789001312
Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
Mada Nyinginezo:
Yakobo 1:5-8″ Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.
6 Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.
7 MAANA MTU KAMA YULE ASIDHANI,YA KUWA ATAPOKEA KITU KWA BWANA.
8 MTU WA NIA MBILI HUSITA-SITA KATIKA NJIA ZAKE ZOTE.”
Mtu akishakuwa mkristo vita kubwa anayoanza kupitia ni katika AKILI, shetani anahamisha vita vyake kutoka katika mambo ya nje, kwenda katika mambo ya ndani kwa kusudi moja tu, la kumfanya mtu huyo alitilie SHAKA Neno la Mungu!, kwa kumletea mashaka asiuamini wokovu wake jambo linalompelekea mtu kama huyo kuwa katika hali ya KUSITA KWENYE MAWAZO MAWILI.
Shetani anafahamu kuwa mtu atakapoliamini Neno la Mungu kwa asilimia zote pasipo mashaka atapata anachokitafuta, sasa hapo shetani ndipo anapoanza kuwinda imani ya huyo mtu kwa kumletea mashaka moyoni mwake. Tunaona mfano mtu kama Petro alianza kutembea vizuri juu ya maji lakini alipoanza kutia shaka tu akaanza kuzama.
Kwahiyo silaha kubwa shetani anayoitumia kwa mkristo ni kumletea mashaka asiliamini Neno la Mungu aendelee kubaki katika hali ya kusita-sita asipokee kitu chochote kutoka kwa Bwana. Mbinu hii shetani alitoka nayo tangu Edeni pale Hawa aliporuhusu wazo la shetani la kutilia mashaka NENO la Mungu, na kula tunda ikapelekea mauti jambo ambalo linaendelea mpaka sasa. KULITILIA MASHAKA NENO LA MAUNGU!.
Kwamfano Neno la Mungu limeahidi “wakutanikapo wawili au watatu kwa jina lake yeye atakuwepo katikati yao”. Lakini shetani atamletea mtu huyo wazo kwenye akili yake likisema : {…Aah! hilo haliwezekani, Mungu yupo mbinguni hawezi kuwepo hapa katikati yetu,hawezi kuwepo sehemu kama hii, sisi ni wachafu kama sivyo mbona hatumuhisi….}. Sasa mtu huyo akidhani kuwa hilo wazo ni la kwake, kumbe hajui linatoka kwa yule mwovu..kwasababu shetani amemletea hilo wazo likianza na “mimi.. mimi.. mimi”.
Halianzi kama shetani anamwambia mtu huyo bali linakuja kama vile yeye huyo mtu ndio analiwaza hilo wazo. Hivyo inakuwa ni ngumu kwa mtu kama huyo kutambua mawazo ya shetani ni yapi na yake ni yapi. Kwasababu hiyo basi shetani anafanikiwa kumwacha katika hali ya kusita-sita na mwisho wa siku hapokei chochote kutoka kwa Mungu kwasababu Mungu hakai katika mashaka, yeye ni wa kuaminiwa tu!.
Tuchukue mfano mwingine, Neno la Mungu linasema.“Kwa kupigwa kwake sisi tumepona”. Hivyo Mtu akiwa mgonjwa atakapojaribu tu kulitafakari hili NENO limfae kwa ajili ya uponyaji wake, wazo lingine litamjia kwa haraka kichwani mwake,..{….Aaah! Hivi ni kweli inawezakana, hii inahitaji mtu mwenye upako sana, au mtakatifu sana, mimi nimemkosea sana Mungu hawezi kunisamehe wala kunisikia….} .
Kwahiyo mtu huyu anadhani kuwa mawazo hayo ni yeye kayatengeneza kumbe hajui ni shetani ndiye aliyemtengenezea na kuyapandikiza kwenye Akili yake pasipo mtu huyo kujua, Na kama ilivyo ada shetani anamletea hilo wazo lianze na neno “mimi,.. mimi”. Hivyo basi mashaka hayo yakishaingia ndani ya moyo wake yanamsababishia mtu huyo asipokee uponyaji wake. Shetani anakuwa amemshinda.
Mfano mwingine, Bwana Yesu alisema Marko 11:24″ Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu. “. Hapa utamkuta mtu yupo katika kusali na kupeleka mahitaji yake binafsi mbele za Mungu akiwa katikati ya kusali wazo linamjia,{…“Aah! Hivi kweli Mungu atajibu maombi yangu, Mungu lazima atakuwa hapendezwi na mimi!. Ili anisikie ingenipasa nifunge kwanza wiki tatu, Aaah! acha tu niombe anaweza akanijibu”….}..
Unaona hapo hilo neno “anaweza”.tayari ni mashaka hayo hana uhakika na anachokiomba akidhani kuwa hayo ni mawazo aliyoyatengeneza yeye, kumbe ni mawazo ya shetani kayatupa kwenye akili yake, na kumfanya mtu huyo kuwa katika hali ya kusita-sita hivyo hawezi kupokea chochote kutoka kwa Mungu, Kwasababu shetani anajua tu! atakapoliamini hilo NENO kwa asilimia zote, pasipo kutilia shaka kwa namna yoyote, Atapokea chochote anachokiomba.
Tazama hichi kisa hapa chini, jinsi mtu huyu alivyompa Kristo maisha yake, siku ya jumatatu, lakini angalia shetani alivyoanza kuiwinda imani yake, na kumpelekea kuwa MTU WA KUSITA-SITA KATIKA MAWAZO MAWILI.
Siku ya jumanne anaanza kujifunza Neno la Mungu…
..Siku ya jumatano anautilia mashaka wokovu wake…
…Alhamisi anajihisi hajaokoka na kurudia kumpa Kristo tena maisha yake…
NAMNA YA KUSHINDA HALI HIYO:
Wazo lolote linalokuja katika kichwa chako linalokufanya ulitilie shaka NENO la Mungu, lipinge na kulikataa kwa JINA LA YESU kwasababu hayo sio mawazo yako bali ni ya shetani ameyaelekeza kwako ili usipokee kitu kutoka kwa Mungu kwasababu Mungu anasema katika
Yakobo 1:7-8 “Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.
8 Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote.“.
Hivyo basi Rudisha mawazo yako na sema ndani ya moyo wako “maneno ya Mungu, ni kweli na hakika”. yashikile hayo hayo pasipo kujihukumu mwenyewe. Na kwa kufanya hivyo shetani atakukimbia na kukufanya kuwa mshindi siku zote na kupokea Ahadi za Mungu.
Usiruhusu mawazo yoyote ya kulichunguza NENO la Mungu kuwa linafanyaje fanyaje kazi, siku zote njia za Mungu hazichunguziki wewe AMINI tu!. Hayo mengine mwachie yeye, amesema kwa kupigwa kwake tumepona! amini hilo NENO kila siku litamke,sema moyoni mwako Mungu siku zote hawezi kusema uongo! usitafute kujua litafanyaje fanyaje kazi, itaonekana kuwa hakuna matumaini! lakini wewe liamini tu na utashangaa unapokea uponyaji wako. NENO la Mungu linasema “yote yawezekana kwake yeye aaminiye”.
Kwahiyo ukiwa katika sala unaomba jambo lolote amini umelipokea. usianze kusita-sita, au kujiuliza uliza au kutafuta njia mbadala,wewe mwamini Mungu lishikilie hilo neno, nalo litatokea kama lilivyo usitazame muda hata kama litachelewa lakini litakuja tu! wewe liamini tu usiruhusu mawazo mengine yoyote ya shetani ya mashaka kuingia ndani yako.
Pambana shetani hapo ndipo anapofanyia vita na hakuna vita vigumu kama hivyo, Tutamshinda shetani tu pale tutakapokuwa na NENO ndani yetu na kuliamini asilimia mia, lakini tukiwa watu wa mashaka kama maandiko yanavyosema TUSITAZAMIE KUPOKEA KITU CHOCHOTE KUTOKA KWA BWANA.
……Hapa yule mtu anatambua uongo wa shetani na anachukua hatua..
…..mwishoni wokovu wake unakuwa thabiti usiokuwa na mashaka…….
Mungu akubariki!
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Kwa msaada wa maombi/Ushauri/ubatizo/mafundisho/Whatsapp: Namba zetu ni hizi:
+255693036618/ +255789001312
Mada Nyinginezo:
UMEPATA UHAKIKA WA KUTOKUINGIA HUKUMUNI KATIKA SIKU ILE?
JE! NI SAHIHI KWA MKRISTO KUOA/KUOLEWA NA MTU WA IMANI NYINGINE?
Ndoa na talaka, kibiblia ni inakuwaje?
Mathayo 19:3-8″ Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu?
4 Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke,
5 akasema, KWASABABU HIYO, MTU ATAMWACHA,BABAYE NA MAMAYE, ATAAMBATANA NA MKEWE; NA HAO WAWILI WATAKUWA MWILI MMOJA;
6 Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. BASI ALIOWAUNGANISHA MUNGU, MWANADAMU ASIWATENGANISHE.
7 Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha?
8 Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi. “
Hapa tunaona jambo la kuachana kwa mke na mume halimpendezi Mungu hata kidogo, kwasababu biblia inasema alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe. Hivyo ndoa haipaswi kuvunjwa isipokuwa kwa sababu zifuatazo zilizohorodheshwa kwenye biblia;
Biblia inasema kwenye
Mathayo 19:9″ Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, ISIPOKUWA NI KWASABABU YA UASHERATI, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini. “.
Ikiwa mmojawapo kati ya wanandoa amefumaniwa katika uzinzi hapo biblia imeruhusu kumwacha mtu huyo, na kwenda kuoa au kuolewa na mtu mwingine, lakini kama ni kwasababu nyingine yoyote tofauti na uzinzi mfano kugombana, kuudhiana, fitna, matatizo, shida, dhiki,magonjwa n.k. hapo biblia hairuhusu kuachana, na hata kama imetokea wameshindwa kulewana na kupelekea kuachana hairuhusiwi kwenda kuoa au kuolewa tena, Biblia inasema kila mmoja akae kama alivyo, ikiwa kama wakipatana wanaweza wakarudiana kinyume na hapo watakuwa wanafanya uzinzi.(marko 10:11-12) ,
Biblia inasema
1Wakoritho 7:10- 11″ Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe; lakini, ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe”.
Hivyo basi ikiwa jambo kama hili limetokea mmojawapo kukamwatwa katika uzinzi ni vizuri ukajifunza kusamehe ili ndoa isivunjike, Mungu hapendi kuachana, kwasababu hata Bwana Yesu Kristo anatusamehe sisi mara nyingi pale tunapomfanyia uasherati wa kiroho, je! sisi hatupaswi kufanya zaidi? lakini ikiwa huwezi kuvumilia unaweza ukaivunja utakuwa hauna hatia biblia imeruhusu wewe kwenda kuoa au kuolewa na mtu mwingine.
2) IKIWA AMETAKA KUKUACHA KWA SABABU YA IMANI YAKO:
Kama imetokea mlifunga ndoa wakati wote hamjawa waamini, na wewe ukaja kuwa muamini angali ukiwa ndani ya hiyo ndoa, na mkeo/mumeo asitake kukubaliana na imani yako na akaamua kukuacha asiishi tena na wewe, katika hali kama hiyo biblia inaruhusu wewe kwenda kuoa/kuolewa na mtu mwingine lakini iwe katika BWANA TU!. Lakini kama ikitokea yule mtu katika hali yake ya kutokuamini anakubali kuishi na wewe hautakiwi kumuacha ukimuacha na kwenda kuoa/kuolewa na mtu mwingine utakuwa UNAFANYA UZINZI! .
soma…
1Wakoritho 7:12-16 ” Lakini watu wengine nawaambia mimi, wala si Bwana, ya kwamba iwapo ndugu mmoja ana mke asiyeamini, na mke huyo anakubali kukaa naye asimwache.
13 Na mwanamke, ambaye ana mume asiyeamini, na mume huyo anakubali kukaa naye, asimwache mumewe.
14 Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa katika mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa katika mumewe; kama isingekuwa hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi; bali sasa ni watakatifu.
15 Lakini yule asiyeamini akiondoka, na aondoke. Hapo huyo ndugu mume au ndugu mke hafungiki. Lakini Mungu ametuita katika amani.
16 Kwa maana wajuaje, wewe mwanamke, kama utamwokoa mumeo? Au wajuaje, wewe mwanamume, kama utamwokoa mkeo? “.
Kumbuka kuachana huku ni kwa wale tu! walioana kabla ya kuamini! Biblia haitoi ruhusu yoyote kwa wale walioamini kuachana isipokuwa kwa habari ya uasherati tu, na pia biblia hairuhusu mtu mwamini akaoe/kuolewa na mtu asiyeamini! Hilo ni kosa.
Hivyo basi kama maandiko yanavyosema waebrania 13:4″ Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu. “. Ni vizuri mtu unapoingia kwenye ndoa ujue ni jambo la kuheshimika na Mungu hapendezwi na wanandoa kuachana kwasababu yoyote ile! (malaki 2:16 ).
Pale ndoa inapofungwa tu! Mungu anaachilia neema na baraka ya ziada tofauti na mtu ambaye hayupo kwenye ndoa, na pale ndoa inapovunjika kumbuka kuna hasara nyingi, ikiwemo kuzuia baraka za kiroho, watoto unawafanya kuwa kama yatima, unajirudisha nyuma na kuanza safari mwanzo hivyo basi ili kuyaepuka hayo kuwa mwaminifu kwa Bwana na kwa mke/mme wako. Na pia ufanye maamuzi sahihi katika kuchagua mwezi ikiwa kama bado haujaingia kwenye ndoa.
Mungu akubariki!
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Kwa msaada wa maombi/Ushauri/ubatizo/mafundisho/Whatsapp: Namba zetu ni hizi: +255693036618/ +255789001312
Mada Nyinginezo:
JE NI HALALI KUOA WAKE WENGI AU KUTOA TALAKA?
KWANINI NABII ISAYA ALIAGIZWA KUHUBIRI UCHI?
NI KWA JINSI GANI MUNGU ANAPATILIZA MAOVU YA BABA ZETU SAWASAWA NA KUTOKA 20:5-6?
AMPOKEAYE NABII KWA KUWA NI NABII, ATAPATA THAWABU YA NABII; MSTARI HUU UNAMAANA GANI?.
Kuna hatua za kupitia, ambazo ni lazima kila mkristo azipitie ili aweze kumzalia Bwana matunda, Bwana alizifananisha hatua hizi na ule mfano wa MPANZI;
Tukisoma
Mathayo 13:2-9 ” Wakamkusanyikia makutano mengi, hata akapanda chomboni, akaketi; na ule mkutano wote wakasimama pwani.
3 Akawaambia mambo mengi kwa mifano, akisema, Tazama, mpanzi alitoka kwenda kupanda.
4 Hata alipokuwa akipanda, mbegu nyingine zilianguka karibu na njia, ndege wakaja wakazila;
5 nyingine zikaanguka penye miamba, pasipokuwa na udongo mwingi; mara zikaota, kwa udongo kukosa kina;
6 na jua lilipozuka ziliungua; na kwa kuwa hazina mizizi zikanyauka.
7 Nyingine zikaanguka penye miiba; ile miiba ikamea, ikazisonga;
8 nyingine zikaanguka penye udongo mzuri, zikazaa, moja mia, moja sitini, moja thelathini. 9 Mwenye masikio na asikie. “
Katika mfano huu tunaona huyu mkulima alienda kupanda mbegu, kumbuka hizi hazikuwa mbegu za kuchimbiwa ardhini, bali zilikuwa ni mbegu nyepesi ndogo za kurusha, na alipokuwa akizirusha alizielekeza zote ziende kwenye udongo mzuri, ili zikue na kuzaa matunda, hizi tofauti na mbegu zile za kupanda ambapo mkulima huenda moja kwa moja kwenye udongo mzuri na kuzifukia ardhini, lakini hizi ni tofauti, tunaona zilipewa nguvu ya kutembea kwa kurushwa ili zifike katika eneo lililokusudiwa la udongo mzuri. Lakini kuna nyingine zilikwama kwenye hatua tofauti tofauti katika safari zao kuelekea kwenye udongo mzuri.
Katika mfano huu hapa mbegu zilipitia katika hatua kuu NNE (4), ambazo ni; NJIANI, kwenye MIAMBA, Kwenye MIIBA, na kwenye UDONGO MZURI. Na hizi ndizo hatua NNE za mkristo katika safari ya maisha yake tangu siku ile ya kwanza anayompa Bwana maisha yake. Tuzitazame hatua hizi kwa ufupi;
Unaposikia injili (NENO) kwa mara ya kwanza, wewe unakuwa ni mbegu iliyorushwa na mkulima ambaye ni YESU KRISTO katika shamba lake, Kumbua Bwana alikusudia wewe ufike kwenye udongo mzuri, lakini mbeleni kuna vikwazo sasa hatua ya kwanza ni wewe kurushwa kutokea NJIANI, hapa unajikuta umeshapokea neno la Mungu (yaani kumpokea Kristo) katika namna ya kawaida unajikuta bado haulielewi lile NENO vizuri, ndani yako unasikia kiu ya kutaka kuendelea kumjua Mungu, hivyo unajikuta hauridhiki katika hali uliyopo ndani kunachemka kutaka kuendelea kujua zaidi, unaenda huku na kule kutafuta majibu ya maswali yako ya rohoni, na unakuwa na kiu pia ya kusoma NENO la Mungu.
Ukiona hali kama hiyo ujue ni ile nguvu ya Roho wa Mungu inakusukuma kusonga mbele kuelekea kwenye udongo mzuri ili ukamee. Lakini kwa upande mwingine unakuta mtu amesikia injili na ile nguvu ya kumfanya aendelee kusonga mbele yaani kutaka kumjua Mungu zaidi haipo ndani yake. anaridhika na hali aliyopo, akikuta kitu kwenye NENO la Mungu asichokielewa hajishuhulishi kutafuta jibu la maswali yake , hivyo anatulia njiani, hapo ndipo shetani anapopata nafasi kuchukua kile kilichopo ndani yake, hapo ndipo linakuja lile neno “aliyenacho ataongezewa na asiyenacho hata kile kidogo alichonacho atanyang’anya”.
Hivyo unamkuta mtu anajiita mkristo lakini matendo yake hayaendani na ukristo, hanufaiki na jambo lolote katika NENO la Mungu ,japo anaenda kanisani kila siku, anaimba kwaya, anasema ameokoka pasipo kujua ibilisi ameshamwondolea ile nguvu ya Roho Mtakatifu na kiu ndani yake imekufa, anakuwa hana tofauti na mtu asiyeamini.
Na ndio maana Bwana Yesu alisema
Mathayo 13: 19″ Kila mtu alisikiapo neno la ufalme asielewe nalo, huja yule mwovu, akalinyakua lililopandwa moyoni mwake. Huyo ndiye aliyepandwa karibu na njia.”
Mathayo 13:20-21 “Naye aliyepandwa penye miamba, huyo ndiye alisikiaye lile neno, akalipokea mara kwa furaha; lakini hana mizizi ndani yake, bali hudumu kwa muda; ikitukia dhiki au udhia kwa ajili ya lile neno, mara huchukizwa. “
Kumbuka hii ni hatua ya pili, ambayo inakuja baada ya kushinda ile hatua ya kwanza, shetani akishaona una kiu, hamu, shauku na bidii nyingi ya kutaka kumjua Mungu, na kutafuta kuujua ukweli na hatma ya maisha yako ya milele, na maisha ya kumpendeza Bwana, hapo ndipo majaribu yanapoanza, Kumbuka kila mkristo lazima ajaribiwe imani yake, Mungu mwenyewe ndiye aliyeruhusu iwe hivyo, maana ndivyo wana wa Mungu wote walivyopitia huko nyuma.
Sasa katika hali hii, ile nguvu ya Roho Mtakatifu inakusukuma uikabili hatua inayofuata, hapo ndipo unakutana na majaribu kwa ajili ya NENO la Mungu, pengine utapitia, kuchukiwa na ndugu, kutengwa na marafiki, misiba, magonjwa, kufungwa kwa ajili ya Neno la Mungu, kudharauliwa, kuchukiwa kisa tu umeamua kuifuata hiyo imani, wakati mwingine mambo yako mengine kuharibika kwahiyo hali hii inapotokea usiogope ni IMANI yako inajaribiwa ni uthibitisho kwamba ile mbegu bado ipo safarini kuelekea kwenye udongo mzuri, usichukizwe, shika sana ulichonacho.
Bwana hatakuacha hali hii inaweza ikadumu kwa muda mrefu lakini usikate tamaa Bwana hatakuacha yupo nawe. Kumbuka jambo hili litakuja kwa yule tu mtu ambaye hatua ya kwanza ameivuka kikamilifu. lakini safari bado inaendelea.
Lakini wapo watu wengi wakifika kwenye hii hatua wanaizimisha ile nguvu ya kuendelea mbele kwa kuogopa udhia na dhiki na aibu hivyo wanakwazika na kuiacha imani, hawa ndio wale waliokwama katika miamba natamani ndugu yangu wewe usiwe hivyo. kumbuka Bwana Yesu alisema mtu yeyote akitaka kunifuata ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.
Mathayo 13:22 “Naye aliyepandwa penye miiba, huyo ndiye alisikiaye lile neno; na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno; likawa halizai. “
Shetani akishajua bado unang’ang’ana na NENO na kuzidi kutamaini kufikia utimilifu, na kumtumaini Bwana kuelekea udongo mzuri, japo kuwa unapitia dhiki, udhia, lakini bado upo na Bwana, safari hii hatumii nguvu tena, anakuja na ushawishi, na anafahamu ni mahali gani pa kumkamatia mtu na si pengine zaidi ya Tamaa ya mambo ya ulimwengu huu..hivyo atakuletea nguvu kubwa ya ushawishi ili utamani kuwa kama watu wa ulimwengu huu, kupenda kuwa mali nyingi, kuubadilisha muda wako wa kuwa karibu na Mungu na u-bize, mihangaiko, anasa, Starehe, biashara, ili tu uridhike na hali uliyopo umzimishe Roho, Hali kama hii inapokuja wewe umtazame Bwana na ahadi zake usitamani kufanana na watu wa ulimwengu huu, yeye mwenye alisema “sitakuacha wala kukupungukia kabisa” kumbuka Bwana Yesu alichokisema katika mathayo 6.
Hivyo usipunguze muda wako wa kusoma NENO, kusali, kumtafakari Mungu, kutangaza Neno la Mungu, kisa tu! ya kusongwa na mahangaiko ya maisha, bali kinyume chake uongeze muda wako na Bwana, hayo mengine yaweke kando utafute kwanza ufalme wake na haki yake na hayo mengine yote utazidishiwa.
Lakini katika hatua hii wakristo wengi ndipo waliponasiwa na mwovu, walianza vizuri lakini pesa, shughuli, mahangaiko, yamewasonga wamwache Mungu na kupoa hivyo ile Nguvu ya ROHO wa Mungu ndani yao inapoa, wanaacha kutazamia mambo ya ulimwengu ujao badala yake wanaangalia mambo ya ulimwengu huu, wakidhani katika hali yao ya uvuguvugu ya ukristo waliyopo ndiyo wanamzalia Mungu matunda kumbe bado hawajafika.
Luka 8:15 “Na zile penye udongo mzuri, ndio wale ambao kwa unyofu na wema wa mioyo yao hulisikia neno, na kulishika; kisha huzaa matunda kwa KUVUMILIA. “
Hatua hii ndipo mtu anapokamilishwa kwenye udongo mzuri ili kumzalia Mungu matunda. Kumbuka hatua hii mtu ataifikia kwa KUVUMILIA hari zote tatu zilizopita nyuma, yaani njiani,kwenye miamba, na kwenye miiba, pale mkristo anapolipokea NENO kwa uthabiti wa moyo, kila siku akiendelea kutafuta na kumjua Mungu bila kuchoka japo kuwa adui yupo njiani na majaribu yote, dhiki, udhia, shida, taabu, misiba, kuvunjwa moyo, kukatishwa tamaa, kutengwa, ukame, kufungwa, kuchukiwa kwa ajili ya Kristo, kukana mambo yote ya ulimwengu, naam hata nafsi yake mwenyewe, kwa ajili ya Bwana akizidi kuvumilia hayo yote anakuwa dhahabu iliyosafishwa kwenye moto tayari kwa kusudi na kazi ya Mungu aliyomweka duniani.
Mtu huyu anakuwa ameingia KAANANI yake, Utukufu wa Mungu unafunuliwa juu yake, ili kumzalia Bwana matunda ya haki yaliyokubaliwa. kama alivyosema huyu thelathini, huyu sitini, huyu mia, kulingana na kipimo cha neema alichopimiwa huyo mtu. Wakati huu pia Bwana anambariki kwa vitu vyake vyote alivyovipoteza kwa ajili yake mara mia zaidi kama alivyoahidi katika NENO lake. Na mtu wa namna hii anakuwa na uhusiano wa kipekee na Mungu, na kupewa nafasi za kipekee katika ufalme wa Mungu angalia akiwa hapa hapa duniani.
Kumbuka kuhubiri au kufanya kazi yoyote ya Mungu, kama haujazivuka hizi hatua NNE, hauwezi kumzalia Mungu matunda maana sasa utakuwa umepandwa kwenye udongo gani?. Yatupasa tuyashinde ndipo tumzalie Mungu matunda, kumbuka Yesu alishinda hivyo na sisi pia yatupasa tushinde. BWANA anasema
Ufunuo 3:21 “Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi. “
Hivyo ndugu tujitahidi mimi na wewe, tufikie hapo ili tumzalie Bwana wetu matunda, tujiangalie maisha yetu tujiulize je tupo katika hatua gani?. je ni njiani? au kwenye kwenye miamba,? au kwenye miiba? au kwenye udongo mzuri?. tupige mbio tuufikie utimilifu na jambo lolote lisitusonge au lisitutenge sisi na upendo wa Mungu, iwe ni njaa, dhiki, udhia, taabu, raha, uzima, mauti, lolote lile, TUZIDI KUIITI ILE NGUVU YA ROHO MTAKATIFU ITAKAYOTUFIKISHA KATIKA UDONGO MZURI. Naye Bwana ataturuzukia baraka zake tukishinda.
Mungu akubariki!
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Kwa msaada wa maombi/Ushauri/ubatizo/mafundisho/Whatsapp: Namba zetu ni hizi:
+255693036618/ +255789001312
Mada Nyinginezo:
TOFAUTI KATI YA SHERIA YA ROHO WA UZIMA NA SHERIA YA DHAMBI NA MAUTI!
SHETANI ANATOLEA WAPI FEDHA, ANGALI TUNAJUA FEDHA NA DHAHABU NI MALI YA BWANA?
Waefeso 1:20 “…….akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho; 21 juu sana kuliko UFALME WOTE, na MAMLAKA, na NGUVU, na USULTANI, na KILA JINA LITAJWALO, wala si ulimwenguni humu tu, BALI KATIKA ULE UJAO PIA; 22 AKAVITIA VITU VYOTE CHINI YA MIGUU YAKE, akamweka awe KICHWA juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo 23 ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.
Pia 1Timotheo 6:16″…..yeye aliyehimidiwa, Mwenye uweza peke yake, MFALME WA WAFALME, BWANA WA MABWANA; 16 ambaye yeye peke yake hapatikani na mauti, AMEKAA KATIKA NURU ISIYOWEZA KUKARIBIWA; wala hakuna mwanadamu aliyemwona, wala awezaye kumwona. HESHIMA NA UWEZA UNA YEYE HATA MILELE. Amina. “
Ndugu Bwana YESU KRISTO alivyokuja hapo mwanzo, sio sawa na sasa hivi alivyo, mwanzoni alikuja katika hali ya utumwa akaishi kama sisi tulivyo, lakini alijinyenyekeza akawa mtii kama maandiko yanavyosema, hivyo basi Mungu alimwadhimishia akamweka juu ya vitu vyote, kwahiyo tufahamu tu jambo moja yule sio mtu wa KAWAIDA KABISA, NI MIALE YA MOTO!!!, toa yale mawazo unayodhania kuwa ni mtu fulani wa kuchukuliwa kawaida.
Malaika wenye nguvu na wakuu wa mbingu wanatetemeka mbele yake, ameketi katika mbingu za mbingu asikoweza kufika mtu huko hata malaika!! unaweza ukatengeneza picha ni mtu wa dizaini gani huyo??..Hivyo tuwe makini sana tunapomzungumzia au tunapomtaja huyu MFALME MKUU WA KUTISHA, tuwe MAKINI, tuwe makini!!!.. sio mtu wa kawaida ni MUNGU YULE!
Wafilipi 2:7 “bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu;
8 tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.
9 Kwa hiyo tena MUNGU ALIMWADHIMISHA MNO, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;
10 ILI KWA JINA LA YESU KILA GOTI LIPIGWE, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi;
11 na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba. “
Tunaona maandiko hayo yote yanadhihirisha ukuu alionao Bwana Yesu Kristo sasa hivi, usikae ufikirie kuwa ni mtu wa kawaida kama wengi wao wanavyomwona kwenye maigizo na tamthilia. Kumbuka VITU VYOTE na SHUGHULI ZOTE za MBINGUNI, DUNIANI na KUZIMU zipo chini yake, Hakuna chochote kinachofanyika bila idhini kutoka kwake, liwe ni jambo zuri au baya.
Tena Hakuna malaika yoyote anayeweza akaamua jambo lolote kwa namna yoyote pasipo idhini yake aidha awe mbinguni au duniani, wala hakuna chochote kinachoendelea sasa hivi mbinguni kama hakitoki kwake.
Vivyo hivyo shetani naye hawezi kufanya jambo lolote dunia isipokuwa kwanza amepata idhini kutoka kwake yeye HUYO MKUU WA WAKUU(YESU KRISTO), Kumbuka shetani hajiamulii kufanya jambo lolote jinsi apendavyo, yote uyaonayo anayoyafanya karuhusiwa kuyafanya kwa kibali maalumu kutoka kwa Bwana, Na pia kuzimu hakuna mtu yeyote mwenye uwezo wa kumtoa mtu kuzimu wala kumpeleka.
Ni YESU peke yake ndiye anayewamiliki walio hai na walio kufa. yeye ndiye anayeamua aidha akupandishe juu au akushushe, shetani hana mamlaka yoyote juu ya wafu.(warumi 14:9). Mganga yoyote asikudanganye kwamba anaweza akamleta ndugu yako aliyekufa(mzimu) kuzungumza nawe, huo uwezo hana ukiona mzimu ujue ni pepo hilo limevaa sura ya huyo mtu. Uwezo huo anao MFALME TU (YESU KRISTO).
VIvyo hivyo na wanadamu wote pia hakuna mwanadamu anayeishi kwa nafsi yake mwenyewe, hakuna mamlaka inayojiamulia mambo yake tu yenyewe, kila kitu kipo chini ya utawala wa BWANA YESU KRISTO, hata wafalme waliopo leo duniani hawakuwekwa na watu bali ni MFALME MKUU(yaani YESU KRISTO) ndiye aliyewaweka kwa makusudi yake,Huwezi kufanya jambo lolote liwe baya au zuri kama halikupitishwa kwanza kwenye utawala mkuu wa Bwana YESU,
Mithali 16:3″ Mkabidhi Bwana kazi zako, Na mawazo yako yatathibitika. Bwana amefanya kila kitu kwa kusudi lake; NAAM, HATA WABAYA KWA SIKU YA UBAYA. “ ..soma pia
Maombolezo 3:37 “Ni nani asemaye neno nalo likafanyika, Ikiwa Bwana hakuliagiza? Je! Katika kinywa chake Aliye juu HAYATOKI MAOVU NA MEMA? “.
Hivi ndugu hauogopi unaposikia mambo haya yote halafu hautetemeki mbele ya hili JINA.
Vivyo hivyo hata vitu vya asili kama wanyama, ndege, samaki, milima, mimea, bahari n.k. Hivi vyote vinatetemeka na kungojea maagizo kutoka kwa Bwana YESU, na vyote vinamjua kama vile wewe unavyomjua haviwezi vikajiamulia mambo, mvua haiwezi kunyesha au nchi kuzaa kama hazijapokea amri kutoka kwa BWANA YESU KRISTO.
Na pia katika utawala unaokuja wa miaka 1000 BWANA YESU atakaposhuka kuja kutawala na watu wake hapa duniani, dunia itabadilishwa kuwa kama Edeni bahari itaondolewa, kwahiyo sehemu kubwa ya nchi kavu itaongezeka, kumbuka leo hii robo tatu ya dunia ni maji, kwahiyo bahari ikiondolewa mabara tuliyonayo leo yataongezeka mpaka kufikia 28 au zaidi unaweza ukajenga picha kutakuwaje?,
Hivyo wafalme na watawala watakuwa wengi sana kupita kiasi, dunia itajaa utukufu na ustaarabu wa hali ya juu ambao haujawahi pata kuonekana, matatizo hayatakuwepo huko, njaa, shida, umaskini na magonjwa hayatakuwepo, na YESU KRISTO ndiye atakayekuwa BWANA WA MABWANA, na MFALME WA WAFALME na kiti chake cha enzi kitakuwepo huko Yerusalemu na watu wote wa ulimwengu mzima watakusanyika kwenda kumwabudu huko.
Kama tu huu ulimwengu wa leo wenye dhambi na utawala wake, na wafalme wake unamantiki (unaonekana wa kuvutia) si zaidi huo utakaokuja? huo hauelezeki ni raha zisizo na kifani, kutakuwa na shughuli nyingi na teknolojia kubwa zinazotoka kwa Mungu ambazo kwasasa hazipo, wala haziwezi kufananishwa na hizi, wanyama na wanadamu wataishi kwa amani, watu wa Mungu watajenga na kupanda na hakuna mtu atakayebomoa au kuharibu kwasababu shetani wakati huo atakuwa amefungwa.
Kumbuka ndugu haya mamlaka yote yapo mkononi mwa Bwana YESU KRISTO. Naye aliahidi kumiliki nao wale wote watakaoshinda kama yeye alivyoshinda, soma
Ufunuo 3:20 -21″ Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. Yeye ashindaye, NITAMPA KUKETI PAMOJA NAMI KATIKA KITI CHANGU CHA ENZI, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi. “.
Hatuwezi kumiliki na Bwana haya yote kama hatutapita katika njia aliyopitia yeye. “Yohana 14:6.. Yesu akamwambia, Mimi ndimi NJIA, NA KWELI NA UZIMA; mtu haji kwa Baba, ila kwa NJIA YA MIMI. “. Hapo aliposema NJIA alikuwa anamaanisha MAISHA, na wala sio kumpokea YESU kuwa Bwana na mwokozi wako tu! bali ni maisha yako yanapaswa yapite katika ile ile NJIA ya Yesu Kristo aliyopita.
Je! Njia ya Yesu Kristo ni ipi?
Luka 9:23 “Akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, AJITWIKE MSALABA WAKE KILA SIKU, anifuate.
24 Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha.
25 Kwa kuwa yamfaa nini mtu kuupata ulimwengu wote, kama akijiangamiza, au kujipoteza mwenyewe?
26 Kwa sababu kila atakayenionea haya mimi na maneno yangu, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo, atakapokuja katika utukufu wake na wa Baba na wa malaika watakatifu.
Ishara kuu ya kukutambulisha kwamba unamfuata YESU ni MSALABA WAKO. na msalaba ni nini?. Tunajua YESU alibeba msalaba wake ikiashiria kwenda mautini. Vivyo hivyo na sisi pia tunapaswa kubeba misalaba yetu ikiashiria tunapaswa kufa kila siku kwa mambo ya ulimwengu, na pia tunakuwa tayari kufa katika mwili kwa ushuhuda wa YESU KRISTO. Kumbuka wakati YESU alipobeba msalaba wake, alipitia fedheha, alitemewa mate, aliaibishwa kwa ajili ya ushuhuda wa baba yake. kama yeye alivyopitia hiyo NJIA na sisi tunapaswa tupitie vivyo hivyo kwa ajili ya jina lake, kudharauliwa, kuchekwa, kutukanwa, kufungwa, hata kuuliwa pasipo kuuweka chini msalaba wetu. wafilipi 1:29 “Maana mmepewa kwa ajili ya Kristo, si kumwamini tu, ILA NA KUTESWA KWA AJILI YAKE;”
Kwa yeye kuwa mtii vile katika maisha yake na msalaba wake, ndipo tunaona Mungu akamwadhimisha sana kuwa juu ya vitu vyote vya mbinguni na duniani, Na kama kwa njia hiyo ya kuvumilia Baba alimpa vyote, unadhani ili na wewe uwe kama yeye utapitia NJIA nyingine yoyote tofauti na hiyo ya MSALABA??. Usidanganyike kimbia injili za mafanikio na tamaa za ulimwengu huu tu na za sifa za kutiana moyo na majigambo! yasiyoweza kumzalia mtu matunda ya wokovu, injili zinazokufanya ujione upo sawa na Mungu katika hali yako ya uvuguvugu angali ukijua moyoni mwako hata BWANA akarudi leo utabaki! kimbia ndugu.
Bwana alisema mwenyewe mtumwa sio mkubwa kuliko Bwana wake ikiwa yeye walimuita beelzebuli si zaidi watumwa wake?. Ikiwa yeye alikataliwa na viongozi wakubwa wa dini wakati ule kwa ajili ya ushuhuda wa baba yake, inakuwaje wewe unasifiwa na ulimwengu mzima?.
Jiulize! jiulize! msalaba wako ni upi? mitume wote na manabii walioifuata njia yake waliishia msalabani, au kama sio msalabani maneno yao yalikataliwa na wakuu wa dini wasiompenda Mungu. Jua tu ukienda katika njia iliyosahihi lazima upitie udhia soma..2 Timotheo 3:12 “Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa. “
Unaogopa kumkiri Kristo kwasababu unaogopa utatengwa na dhehebu lako. mwanamke unaogopa kuacha kuvaa suruali na vimini na make-up na fashion kwasababu unaogopa marafiki zako watakuonaje!. Umeujua ukweli kwamba hupaswi kuabudu sanamu, au kusujudia vinyago na dhamiri yako inakushuhudia unachofanya sio sahihi lakini kwasababu unamwogopa mama yako au baba yako au ndugu zako, unaendelea kufanya hivyo, ili usionekane mtu wa ajabu. Bwana Yesu (MFALME WA WAFALME )alisema :
Mathayo 10:32 “Basi, kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni.
33 Bali mtu ye yote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni.
34 Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; la! Sikuja kuleta amani, bali upanga.
35 Kwa maana nalikuja kumfitini mtu na babaye, na binti na mamaye, na mkwe na mkwe mtu;
36 NA ADUI ZA MTU NI WALE WA NYUMBANI MWAKE.
37 APENDAYE BABA AU MAMA KULIKO MIMI , HANISTAHILI; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.
38 WALA MTU ASIYECHUKUA MSALABA WAKE AKANIFUATA, HANISTAHILI.39 Mwenye kuiona nafsi yake ataipoteza; naye mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona. “
Je! msalaba wako ni nini katika ukristo wako??..je! ni Yesu kukufanikisha katika biashara yako au kazi yako huku ukiendelea kuwa vuguvugu? au kuponywa ugonjwa wako huku ukiendelea kuvaa nusu uchi? au kukupa familia nzuri huku ukiendelea kuabudu sanamu?..au kujitoa kikamilifu kwa Bwana na kupita katika njia yeye aliyoipitia bila kujali dunia inasema nini juu yako?. jibu unalo! maombi yangu ni sisi sote tushinde ili siku ikifika tukaketi pamoja naye katika kiti chake cha enzi kama alivyoshinda yeye. (yaani yule MFALME MKUU BWANA WETU NA MWOKOZI WETU YESU KRISTO).
SIFA NA HESHIMA NA UTUKUFU VINA YEYE MILELE NA MILELE. HALELUYA!
Mungu akubariki!.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Kwa msaada wa maombi/Ushauri/ubatizo/mafundisho/Whatsapp: Namba zetu ni hizi:
+255693036618/ +255789001312
Mada Nyinginezo:
DALILI ZIPI ZITAMTAMBULISHA MTU KUWA AMEFANYIKA KIUMBE KIPYA?
TOFAUTI KATI YA NDOTO NA MAONO NI IPI?
TUNAPOSEMA TUISHI KWA NENO, INAMAANISHA TUISHI MAISHA YA NAMNA GANI?
Dhambi ya mauti, ni ipi katika maandiko?
1Yohana 5:16 “Mtu akimwona ndugu yake anatenda dhambi isiyo ya mauti, ataomba, na Mungu atampa uzima kwa ajili ya hao watendao dhambi isiyo ya mauti.
IKO DHAMBI ILIYO YA MAUTI. Sisemi ya kwamba ataomba kwa ajili ya hiyo.Kila lisilo la haki ni dhambi, na dhambi iko isiyo ya mauti.
17 Kila lisilo la haki ni dhambi, na dhambi iko isiyo ya mauti.
Biblia inaeleza wazi kuwa kuna DHAMBI ZA MAUTI na DHAMBI ZISIZO ZA MAUTI:
Hii ni dhambi ambayo mtu akiifanya anaweza akatubu na kusamehewa, na dhambi hii ni ile inayotokana na aidha kutenda pasipo kukusudia, au inatendeka kutokana na uchanga wa kiroho, au kwa kukosa maarifa au jambo lingine lolote linaloweza kutendeka ambalo halijavuka mipaka ya neema.
Dhambi ya namna hii biblia inasema mtu anaweza akatubu au akamuungamania mwenzake na akasamehewa, akaendelea kuishi na asife. Lakini kuna dhambi mtu akiitenda hiyo hata huyo mtu aombeje, anaweza akasamehewa kosa tu lakini adhabu ya mauti ipo pale pale, je! hii dhambi inasababishwa na nini?
Namna hizi mbili tunaweza tukaona zimefananishwa na Musa na wana wa Israeli kule jangwani, Musa akiwa mfano wa “watumishi wa Mungu”, pamoja na kwamba Mungu alitembea nae kwa namna ya tofauti hata kuliko manabii wote, lakini alitenda dhambi kwa kosa kutokutii maagizo ya Mungu na kuchukua utukufu wa Mungu, alifanya vile akijua kabisa kuwa ni kosa ikampelekea kutenda DHAMBI YA MAUTI,
Musa kwa kweli alisamehewa lile kosa lakini adhabu ya mauti ilikuwa pale pale iliyomsababishia apoteze hata zile ahadi zote Mungu alizomuahidia za kuiona nchi ya Ahadi. Hata leo hii wapo watumishi wanatenda hii dhambi, wanachukua utukufu wa Mungu na kutokutii maagizo yake, inapelekea Mungu kuwaadhibu huduma zao zinakatishwa kama ilivyotokea kwa Anania na Safira walipomdanganya Roho Mtakatifu na kupokea adhabu ya kifo pale pale japo walikuwa ni watoto wa Mungu. Hizo zote ni DHAMBI ZA MAUTI.
Vivyo hivyo na wana wa israeli ni mfano kamili wa “wakristo vuguvugu” wa leo kumbuka wana wa israeli ijapokuwa waliuona utukufu wote wa Mungu, na maajabu yote na miujiza yote lakini mioyo yao haikuwa mikamilifu ijapokuwa Mungu aliwavumilia kwa muda mrefu watubu lakini hawakutaka wakaanza kuabudu sanamu, wakafanya uasherati, wakawa wakimnung’unikia Mungu na kumjaribu ikafika wakati neema ya Mungu juu yao ikakoma Mungu akaapa kwamba wote wangekufa nyikani ijapokuwa walitubu kwa kulia na kuomboleza hata hivyo hakuna hata mmoja wao aliyeiona nchi ya ahadi isipokuwa wale wana wao tu!, unaona hiyo ndiyo DHAMBI YA MAUTI.
Unajisikiaje pale ambapo unaona ungestahili kupata baraka fulani halafu unazikosa, hautakaa uzipate tena milele? fikiri juu ya hilo, na ndio maana maandiko yafuatayo yanatuonya yakisema
1 Wakorintho 10:1
Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari;
2 wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari;
3 wote wakala chakula kile kile cha roho;
4 wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo.
5 Lakini wengi sana katika wao, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani.
6 Basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya, kama wale nao walivyotamani.
7 Wala msiwe waabudu sanamu, kama wengine wao walivyokuwa; kama ilivyoandikwa, Watu waliketi kula na kunywa, kisha wakasimama wacheze.
8 Wala msifanye uasherati, kama wengine wao walivyofanya, wakaanguka siku moja watu ishirini na tatu elfu.
9 Wala tusimjaribu Bwana, kama wengine wao walivyomjaribu, wakaharibiwa na nyoka.
10 Wala msinung’unike, kama wengine wao walivyonung’unika, wakaharibiwa na mharabu.
11 Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.
12 Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke.
Mfano kamili wa kanisa la leo lililo vuguvugu kupita kiasi” linaona utukufu wa Mungu karibu kila mtu anafahamu kabisa kuwa KRISTO ni mwokozi, mponyaji, na wengi wao wamebatizwa wanaenda kanisani, wanaujua ukweli wote lakini utakuta bado mtu ni mwasherati, mlevi, mtukanaji, anaenda disco, msengenyaji, anatazama pornography, anavuta sigara, anavaa mavazi ya kiasherati n.k. angali akifahamu Mungu hapendezwi na watu wa namna hiyo. Anaiona neema ya Mungu lakini bado anaidharau mfano ule ule wa wana wa Israeli, Lakini watu kama hawa hawajui kuwa wapo hatarini kutenda DHAMBI YA MAUTI.
kama tu Mungu hakuweza kumwachilia mtumishi wake Musa kwa kosa dogo tu la kutokutii wewe unadhani utaponea wapi ikiendelea na maisha yako ya dhambi?..Ni kweli Musa alisamehema lakini adhabu ya kutokuiona nchi ya ahadi kwa njia ya Mauti ilikuwa pale pale.
Kwa namna hiyo hiyo unahubiriwa injili leo umgeukie Mungu, uache dhambi utubu usamehewe unasema hapana ngoja nile maisha nitakuja kutubu baadaye unaweza usiseme kwa mdomo lakini moyo wako unasema unaendelea kuwa mwasherati pale unapopata ugonjwa usiokuwa na matumaini mfano ukimwi unaona ndio sababu ya kumgeukia Mungu angali wakati ulipokuwa mzima hukufanya hivyo? Ni kweli ukitubu unaweza ukasemehewa lakini adhabu ya mauti ipo pale pale ndio maana utaona watu wa namna hiyo hata waombeweje hawaponi, sababu ni kwamba wameshatenda DHAMBI YA MAUTI.
Sisemi hili kwa kukutisha lakini ndio ukweli, hatuna budi kuyachunguza maisha yetu kila siku.
Mara nyingine sauti ya Mungu inakulilia uache dhambi ya ulevi na uvutaji sigara ili usafishwe maisha yako lakini unaziba masikio yako hutaki kusikia. Mungu anaruhusu pepo la Kansa linakuingia unapata kansa ya koo au mapafu au ini hapo ndipo unapoona sababu ya kumrudia Mungu ni kweli ukitubu Mungu anaweza kukusamehe lakini adhabu ya kifo ipo pale pale Kwasababu apandacho mtu ndicho atakachovuna. Mungu sio wa kumtegea kwamba niache nifanye mambo yangu kisha nikishafika mzee au wakati fulani ndipo nimgeukie, Mungu hadhihakiwi.
Madhara yake makubwa ni kwamba utapoteza thawabu yako katika ule ulimwengu ujao kwasababu umelikatisha kusudi la Mungu juu yako, ndio hapo kama Mungu alikupa huduma au anataka uwe na huduma haiwezekani tena kuendelea nayo kwasababu ulishatenda DHAMBI YA MAUTI, huna budi kuondoka nafasi yako anapewa mtu mwingine kama ilivyomtokea Yuda nafasi yake ilichukuliwa na mtu mwingine. wakati wengine wakipewa mataji yao mbinguni siku ile kwa kazi nzuri walizotaabika nazo duniani wewe utakuwa huna lolote, utabaki mtu wa kawaida milele. Hivyo ndugu, biblia inasema
1Petro 1:10 ” KWAHIYO NDUGU, JITAHIDINI ZAIDI KUFANYA IMARA KUITWA KWENU NA UTEULE WENU; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe. ” .
Itikia wito wa Mungu ulio ndani yako sasa kabla hazijaja siku zilizo mbaya utakazosema ee! Mungu wangu nisamehe nataka kuishi lakini usiweze kusikilizwa dua zako kwa upumbavu wako mwenyewe. Ndugu Tukisikia hili tuogope kwasababu imeandikwa..
Wafilipi 2:12 “Basi, wapendwa wangu, kama vile mlivyotii sikuzote, si wakati mimi nilipokuwapo tu, bali sasa zaidi sana mimi nisipokuwapo, UTIMIZENI WOKOVU WENU WENYEWE KWA KUOGOPA NA KUTETEMEKA.KWA MAANA NDIYE MUNGU ATENDAYE KAZI NDANI YENU, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema. “
AMEN!
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Kwa msaada wa maombi/Ushauri/ubatizo/mafundisho/Whatsapp: Namba zetu ni hizi:
+255693036618/ +255789001312
Mada Nyinginezo:
KUMWAMBIA MTU MWENYE DHAMBI KUWA ATAKWENDA KUZIMU ASIPOTUBU JE! NI KUHUKUMU?