SWALI: Yesu kuvishwa taji la miiba kichwani alipokuwa anasulubiwa kulikuwa kuna funua nini rohoni?
JIBU: Kila tendo alilotendewa Yesu katika kipindi cha mateso yake lilikuwa lina ufunuo wake rohoni. Tunajua wale askari waliposikia kuwa yeye ni mfalme, muda ule ule walimvisha vazi la kifalme, kisha wakampa fimbo, na baada ya hapo wakasokota taji la miiba, wakamvisha kichwani, kisha wakaanza kumdhihaki, huku wakimpiga wakisema.. Salamu! Mfalme wa Wayahudi!
Yohana 19:2 “Nao askari wakasokota taji ya miiba, wakamtia kichwani, wakamvika vazi la zambarau. 3 Wakawa wakimwendea, wakisema, Salamu! Mfalme wa Wayahudi! Wakampiga makofi”
Tunajua lengo la wale maaskari kumvisha miiba ni kumfanya aumie zaidi, lakini upo ufunuo mkubwa rohoni, pengine kwanini asingevishwa la matambara mabovu, au taji la udongo, au la vyuma vyenye ncha kali, badala yake wakaona miiba.
Kibiblia, miiba, huwakilisha “mahali palipolaaniwa”.
Adamu alipoasi, Mungu alimwambia ardhi imelaaniwa kwa ajili yako, hivyo itatoa miiba na michongoma. Na matokeo yake ni kwamba italimwa kwa shida
Mwanzo 3:17 Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako; 18 michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni;
Ndio maana shamba ambalo halipaliliwi au halitunzwi, matokeo yake ni kuwa linatoa miiba.
Mithali 24:30 Nalipita karibu na shamba la mvivu, Na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili. 31 Kumbe! Lote pia limemea miiba; Uso wake ulifunikwa kwa viwawi; Na ukuta wake wa mawe umebomoka. 32 Ndipo nilipoangalia na kufikiri sana; Naliona, nikapata mafundisho. 33 Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi! 34 Hivyo, umaskini wako huja kama mnyang’anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha
Na vivyo hivyo rohoni, mioyo yetu inafananishwa na mashamba.
Ukisoma ule mfano wa mpanzi, utaona mbegu(Neno la Mungu), lilipopandwa, zipo ambazo ziliangukia kwenye miiba (yaani mahali ambapo hapajafyekwa na kupapaliwa), ndipo pale kwenye miiba, na mwishowe zikakua na kumea. Lakini zikasongwa na ile miiba hazikashindwa kuzaa.
Yesu akatoa tafsiri yake, akasema, miiba ile ni “anasa, udanganyifu wa mali, na shughuli za ulimwengu huu”.
Luka 8:14 “Na zilizoanguka penye miiba ni wale waliosikia, na katika kuenenda kwao husongwa na shughuli na mali, na anasa za maisha haya, wasiivishe lo lote”.
Sasa Yesu alipokuja kufa msalaba, alishughulika na jambo hilo kubwa, kubeba laana hiyo kubwa kwenye kichwa chake.
Akimaanisha kuwa ile nchi iliyolaaniwa (yaani mioyo wa mtu), kuanzia sasa ni mwisho. Imekwisha.
Miiba iliyokuwa inatoka mimi nimeichukua kichwani mwangu.
Moyo wa mtu kuanzia sasa, utaanza kuzaa matunda, na wala hautasongwa na anasa, wala udanganyifu wa mali, wala shughuli za ulimwengu huu, usiivishe chochote.
Hii ikiwa ni kweli kabisa.
Sisi tunaomwamini Yesu, moja kwa moja tunapewa UWEZO wa kufanyika watoto wa Mungu (Yohana 1:12), na matokeo ya uwezo huo ni kuwa, nguvu ya kusongwa na ulimwengu inakuwa ndogo, kwasababu Roho Mtakatifu aliyemwagwa ndani yetu anatusaidia, Kuukataa ulimwengu, na kuishi maisha ya utauwa. Utakuwa ulimwenguni lakini, hutasongwa na mambo yake. Kwasababu utafundishwa pia “kiasi” na Roho Mtakatifu.
Hivyo uwezo huu utakuja ndani yako, pindi tu unapomgeukia Kristo kwa kumaanisha kabisa, ambapo panaanza na kwa KUTUBU kwanza dhambi zako kwa kumaanisha kabisa kugeuka,na kumfuata Kristo tangu huo wakati, na kisha kubatizwa, na kupokea Roho wake. Lakini nje ya hapo, huwezi kwenda popote.
Je! Umempokea Yesu?
Pasipo yeye huwezi ndugu kuushinda ulimwengu kwa nguvu zako, haiwezekani hata kidogo, hata ufanyeje haiwezekani,miiba itakusonga tu, dunia itakulemea tu, Unahitaji nguvu zake, kwa Roho wake Mtakatifu. Ili kuzipata maanisha tu kumgeukia, na kusudia kutembea naye moyoni mwako.
Utaushinda huu ulimwengu. Wala hakuna mwiba wowote utakaomea kwenye moyo wako. Kwasababu Kristo alishayakomesha yote. Je! upo tayari kuokoka leo? Basi fungua hapa kwa mwongozo wa kimaombi>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini auPiga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
SHAMBA HUWA HALIMTAMBUI WALA KUMSUBIRIA MKULIMA.
Marhamu ni nini? Na Manukato ni nini?
Je vazi alilovikwa Bwana Yesu lilikuwa la Zambarau au Jekundu?
Mbaruti ni mmea gani? (Mathayo 7:16)
Rudi nyumbani
Print this post
Karibu tunayatafakari maandiko…
2Petro 3:3 “Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika siku za mwisho watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe, 4 na kusema, Iko wapi ahadi ile ya kuja kwake? Kwa maana, tangu hapo babu zetu walipolala, vitu vyote vinakaa hali iyo hiyo, tangu mwanzo wa kuumbwa. 5 MAANA HUFUMBA MACHO YAO WASIONE neno hili ya kuwa zilikuwako mbingu tangu zamani, na nchi pia, imefanyizwa kutoka katika maji, na ndani ya maji, kwa neno la Mungu; 6 kwa hayo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji, ikaangamia 7 Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu”.
2Petro 3:3 “Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika siku za mwisho watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe,
4 na kusema, Iko wapi ahadi ile ya kuja kwake? Kwa maana, tangu hapo babu zetu walipolala, vitu vyote vinakaa hali iyo hiyo, tangu mwanzo wa kuumbwa.
5 MAANA HUFUMBA MACHO YAO WASIONE neno hili ya kuwa zilikuwako mbingu tangu zamani, na nchi pia, imefanyizwa kutoka katika maji, na ndani ya maji, kwa neno la Mungu;
6 kwa hayo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji, ikaangamia
7 Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu”.
Maandiko yanatuambia watu wa siku za mwisho watafumba macho yao WASIKUMBUKE KILICHOTOKEA WAKATI WA NUHU. Kwamba Mbingu zilikuwepo na nchi pia ilikuwepo, na watu walikuwa wanaendelea na mambo yao, wakidhihaki mahubiri ya Henoko na Nuhu kuhusiana na hukumu ya Mungu, na wakati ulipotimia wa kikombe cha ghadhabu ya Mungu kujaa, hakuna hata mmoja aliyesalia Zaidi ya Nuhu na wanawe na wake zao, jumla watu 8 kati ya dunia iliyokuwa imejaa mabilioni ya watu.
Sasa mambo hayo yalishawahi kutokea katika rekodi za wanadamu.. lakini watu WANAFUMBA MACHO YAO!, Wasione hilo, wala kulitafakari.. na hatimaye wanadhihaki wakisema mbona Yesu harudi!.. mbona tumesubiri na kusubiri!..
Lakini hao hao wanaelewa kilichotokea wakati wa Nuhu kuwa dunia iligharikishwa yote..na wanajua kabisa kuwa walikuwepo watu wenye dhihaka kama za kwao, wakisema hakuna Mungu, na hakuna mtakatifu duniani.. Lakini siku ilipofika ya kuokoka Nuhu peke yake na familia yako, ndipo walipoelewa kuwa walikuwepo wacha Mungu duniani, na tena Mungu haangalii wingi.
Ndugu usidanganyike!. KRISTO ANARUDI! Na wala hatakawia..
Waebrania 10:37 “Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, Yeye ajaye atakuja, wala hatakawia”.
Baada ya Kristo kuwachukua watu wake, kitakachofuata duniani ni gharika ya Moto wa ghadhabu ya MUNGU juu ya wote wasiomcha Mungu, kama tu ilivyokuwa nyakati za Nuhu.
2Petro 3:7 “Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu.
Hivyo kamwe usifikiri wala kuwaza, wala kutia wasiwasi juu ya ujio wa BWANA YESU KRISTO.. Kama ulishawahi kudanganywa, au kulaghaiwa basi ni wanadamu ndio waliokudanganya na kukulaghai, lakini MUNGU muumba wa mbingu na nchi, kamwe hajawahi kusema uongo, na hatakaa aseme uwongo..
Kizazi chetu kitahukumiwa zaidi kuliko kile cha Nuhu kwasababu laiti watu wa kipindi cha Nuhu, wangepata mfano wa wengine waligharikishwa kabla yao, huenda wangeyatii mahubiri ya Nuhu lakini hawakuwa na mifano kabla yao, lakini sisi tunao mfano, wa watu hao.. ni kitu gani kinatutia kiburi!.
Ni nini kinachotufumba macho, na kinachowafumba watu macho????
Unadhani ni shetani????... nataka nikuambie shetani anahusika kwa sehemu ndogo sana, (Na adui anapenda kila kitu asingiziwe yeye ili watu waendelee kujifariji namna hiyo)…..kinachowafanya watu KUFUMBA MACHO YAO, wasitafakari yaliyotokea nyakati za Nuhu na Sodoma na Ghomora ni KIBURI CHA UZIMA, na watu kwa mioyo yao wenyewe KUCHAGUA GIZA na KUIKATAA NURU.
Yohana 3:19 “Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu”.
Siku hizi za Mwisho watu wameyafumba macho yao, wasione na wanajiaminisha ni shetani, kumbe si shetani bali ni wao…tupo! kizazi cha hatari sana..
Mathayo 13:15 “Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya”
Kwa hitimisho usilisahau andiko lifuatalo…
2Petro 3:8 “Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja. 9 Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba”.
2Petro 3:8 “Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja.
9 Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba”.
Ikiwa bado hujampokea BWANA YESU, bali mlango wa wokovu sasa upo wazi, na tunaishi ukingoni kabisa mwa wakati. Hatuna muda mwingi KRISTO anarudi!. Ni wakati wa kutubu na kuishi maisha masafi yanayoendana na toba yetu.
Ufunuo 22:12 “Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. 13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho. 14 Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake”
Ufunuo 22:12 “Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.
13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.
14 Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake”
Maran atha!
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
NUHU WA SASA.
UMEFUNULIWA AKILI?
KWANINI NI NUHU, AYUBU NA DANIELI?
Kuna tofauti gani kati ya uso wa Bwana na macho ya Bwana?
NI WAKATI UPI UTAUONA USO WA KRISTO?
WhatsApp
Nakusalimu katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo. Karibu tujifunze maneno ya uzima ya mwokozi.
Watu waliomwamini Yesu Kristo, yaani waliopokea ondoleo la dhambi zao. Hutambulika kama NGANO, lakini watu ambao bado wapo kwenye dhambi, hujulikana kama MAKAPI.
Sasa kazi ya kwanza ambayo Yesu anaifanya kwa mwamini, ni kumtenganisha yeye na makapi, kisha humweka katika ghala lake.
Mathayo 3:12 Ambaye pepeto lake li mkononi mwake, naye atausafisha sana uwanda wake; na kuikusanya ngano yake ghalani, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.
Ghalani ni uweponi mwa Mungu, yaani kutengwa na udunia.
Soma pia..Mathayo 13:29-30.
Sasa kama wewe unafahamu ukulima, unajua kabisa si mbegu zote zinawekwa ghalani kwa matumizi ya chakula, zipo nyingine, zinachukuliwa na kurudishwa shambani ili kwenda kuzalisha nyingine. Na baadaye huongeza ghala la mkulima.
Tofauti kabisa na ile inayobakia pale ghalani, itaendelea kubakia vilevile hata miaka 10, lakini ile inayokwenda shambani, ndani ya hicho kipindi cha miaka 10, yaweza kuongeza magunia mengi sana ya ngano nyingine.
Ndio maana Bwana Yesu alisema maneno haya;
Yohana 12:24 Amin, amin, nawaambia, CHEMBE YA NGANO ISIPOANGUKA KATIKA NCHI, IKAFA, HUKAA HALI IYO HIYO PEKE YAKE; BALI IKIFA, HUTOA MAZAO MENGI. 25 Yeye aipendaye nafsi yake ataiangamiza; naye aichukiaye nafsi yake katika ulimwengu huu ataisalimisha hata uzima wa milele. 26 Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.
Umeona hapo? Kumbe isipoanguka na kuoza basi itaendelea kubakia katika hali ile ile. Lakini ikikubali kuanguka na kuoza, ardhini, basi itachipuka kama shina, na mwisho wa siku itazaa sana.
Na hapa ndipo waamini wengi, hawataki kuingia gharama. Wanatamani wamzalie Mungu matunda, lakini hawawezi, kwasababu hawajakubali “kufa na kuoza” kwa habari ya huu ulimwengu.
Hawajakubali kuziangamiza nafsi zao kwa ajili ya Kristo. Sasa hiyo ndio inayopelekea wabakie tu kama wakristo wa ghalani,wasioweza kuzalisha chochote.
Yesu alitoa sifa za mbegu yenye kuzaa katika ule mfano wa mpanzi, akasema nyingine ziliangukia njiani, nyingine kwenye miamba, nyingine kwenye miiba, na nyingine kwenye udongo mzuri. Akasema vilizoangukia kwenye udongo mzuri ziliweza kuzaa kwa tendo moja tu la “kuvumilia”
Kuvumilia nini?
Kuvumilia dhiki, na udhia kwasababu ya Kristo, kuvumilia vishawishi vya anasa, udanganyifu wa mali, na shughuli za ulimwengu huu zilizopitiliza, lakini pia kwa unyofu wa moyo walikuwa wanalitendea kazi Neno ili walilolisikia lisiwe bure adui akaliiba ndani yao. (Luka 8:11-15). Hao ndio wakristo wasio wa ghalani, ni wakristo waliokubali kutoka nje, kumletea Bwana matunda.
Je! Na sisi tunaweza kupiga hatua nyingine? Umeokoka ndio, lakini ni lazima wokovu wako uwe na matokeo kwa wengine, uwavute na wengine kwa Kristo, kama wewe ulivyovutwa. Hivyo kubali kumaanisha kumfuata Yesu na kukaa mbali na udunia kwa kadiri uwezavyo.
Jitoe pia kwa Bwana, mali zako, zitumike kuhubiri injili, tenga fungu lako kwa Bwana, penda kusapoti kazi za Mungu, usiwe msomaji tu na kusema Amen!. Onyesha kuwa na wewe ni mtendaji kazi ili thawabu yenu iwe ni moja, na yule mtendaji kazi mwingine.
Bwana atusaidie, tutoke ghalani.
Shalom.
NI YESU YUPI UMEMPOKEA?, NI ROHO IPI UMEIPOKEA? NA INJILI IPI UMEIPOKEA?
ANGALIA JINSI USIKIAVYO:
SEMA KWA LUGHA NYINGINE.
Je Mungu ana njia ngapi za kuzungumza?
SWALI: Je kulikuwa na umuhimu wowote wa ile merikebu ya Iskanderia walioipanda Paulo na wafungwa wengine kutajwa jina lake ‘ndugu Pacha’,?
Matendo 28:11 Baada ya miezi mitatu tukasafiri katika merikebu ya Iskanderia iliyokuwa imekaa pale kisiwani wakati wa baridi; na alama yake ni Ndugu Pacha. 12 Tukafika Sirakusa, tukakaa siku tatu. 13 Kutoka huko tukazunguka tukafikia Regio; baada ya siku moja upepo wa kusi ukavuma, na siku ya pili tukawasili Puteoli. 14 Huko tukakuta ndugu, wakatusihi tukae nao siku saba; na hivi tukafika Rumi.
JIBU: Safari ya mtume Paulo kama mfungwa, kutoka Kaisaria kwenda Rumi kuhukumiwa, haikuwa rahisi, iligubikwa na misuko suko mikubwa ambayo ilihatarisha maisha yao ukisoma Matendo 27, utaona mtume Paulo alionywa na Roho Mtakatifu kuhusu hatari hiyo lakini alipomwambia akida na manahodha, walipuuzia agizo lake, kwasababu watu wale hawakuamini habari za “miungu kabisa”. Maandiko yanasema walipoona upepo wa kusi umevuma kidogo tu, unaoruhusu kusafiri, wakadhani itakuwa hivyo mbeleni.
Lakini tunaona walipofika katikati, ghafla ile bahari iliwachafukia sana, upepo wa nguvu ukavuma merikebu yao ikawa karibu na kuzama, baadaye ilivunjika kabisa, na wakaokoka kwa shida kwasababu Mungu alimuhakikishia Mtume Paulo kuwa hakuna hata mmoja wao atakayeangamia.
Walipookoka na kufika kisiwa kile kilichoitwa Melita, walikaa miezi mitatu pale, kuruhusu hali ya hewa kutulia, kabla ya kuondoka. Lakini tunaona walipotaka kuondoka, safari hii wale mabaharia pamoja na maakida, hawakuichukulia safari yao kirahisi rahisi, yaani hivi hivi tu bila uongozo wowote. Ndipo walipojifunza kuchagua merikebu yenye “ulinzi wa kiroho”. Wakaipata hiyo ya Iskanderia iliyokuwa na nembo ya “Ndugu Pacha” kwa mbele.
Ndugu Pacha ni miungu ya kipagani ya kiyunani, ukisoma tafsiri nyingine za biblia imewataja moja kwa moja miungu hiyo kama Castor na Pollux. Ni miungu ambayo waliamini inahusika na ulinzi wa safari za majini. Hivyo kwa imani yao ya kipagani, wakachukua nembo yao kuonyesha tunaiabudu na kuiheshimu hii miungu, na kutaka iwaongoze salama katika safari yao, hawategemei tena elimu zao na nadharia zao.
Sasa tukirudi kwenye swali, linalouliza, kulikuwa ni umuhimu gani, hiyo merikebu ya Iskanderia kutajwa hadi nembo yake ya ndugu Pacha. Sababu ndio hiyo, Sio kwamba biblia inatufundisha, na sisi tukaweke miungu ya kipagani, kwenye vyombo vyetu vya usafiri kutuhakikishia ulinzi, hapana!
Bali inatufundisha Safari ya maisha hapa duniani. Kila mwanadamu anasafiri, lakini Je! Katika safari yako ni kitu gani kinakuongoza na kukulinda ili kukufikia ng’ambo yako salama?
Hakuna mwanadamu ambaye anaweza kujiongoza mwenyewe. Na ndio maana utaona hawa kwasababu hawakumjua Mungu wa kweli iliwabidi wakatafuta vinyago visivyoweza kuwasaidia kitu viwaongoze, na kama sio mtume Paulo kuwepo ndani ya Merikebu ile, safari yao ndio ingekuwa mbaya mara mbili zaidi. Hawakujua tu waliongozwa na Kristo Yesu pasipo wao kujua kwa neema tu!. Kwasababu watumishi wa Mungu walikuwa ndani.
Na sisi, hapa tulipo, fahamu kuwa maisha yako, bila KRISTO ni mauti mbele. Shetani hakuwazii mema, wala akili zako mwenyewe hazikusaidii ndugu, hiyo elimu ni kazi bure, huo uzoefu na ujuzi ulionao ni bure rafiki. Unamuhitaji Kristo, yeye ndio awe nembo ya maisha yako. Mwamini leo akupe msamaha wa dhambi, mwamini leo akuokoe, safari yako iwe salama hapa duniani. Ukifa leo katika hali hiyo, fahamu ni jehanamu moja kwa moja. Umesikia injili ikihubiriwa mara ngapi, kwamba Yesu ni mwokozi lakini unapuuzia? Walio kuzimu wanatamani hata dakika moja, watubu hawawezi kwasababu kule hakuna maisha ya kuishi. Lakini wewe unaishi.
Usikiapo maneno haya, ugeuze moyo wako, umruhusu Kristo leo akuokoe, ikiwa upo tayari kumgeukia Bwana Yesu , na unatamani upate mwongozo wa kimaombi kwa ajili ya wokovu wako. Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo mwisho wa makala hii, bure.
Bwana akubariki.
NA UPEPO WA KUSI ULIPOANZA KUVUMA KIDOGO,
MAJARIBU MATANO (5) YA MKRISTO.
Kalafati ni nini? (Ezekieli 27:9)
KWANINI DANI ALIKAA KATIKA MERIKEBU.
1Wafalme 4:32 Naye akanena mifano elfu tatu, na nyimbo zake zilikuwa elfu moja na tano. 33 Akanena habari za miti tangu mwerezi ulioko Lebanoni hata HISOPO UMEAO UKUTANI; pia akanena habari za wanyama, na za ndege, na vitambaavyo, na samaki.
Salaam! karibu tujifunze na kutafakari bahari za mwokozi wetu Yesu Kristo na uzuri wake maishani mwetu.
Habari yetu itaanzia kwa mfalme Sulemani ambaye Mungu alimjalia hekima nyingi zaidi ya wanadamu wote waliokuwa duniani kwa wakati ule. Na moja ya mambo ambayo, aliyatafakari sana, hayawakuwa tu yanayowahusu wanyama na viumbe hai, lakini ni pamoja na mimea mbalimbali.
Hivyo kama tunavyosoma katika vifungu hivyo, aliweza kutambua hekima iliyokuwa imejificha nyuma ya miti mikubwa na yenye umaarifu kama mierezi, lakini, kilichomtafakarisha pia sio katika mimea mikubwa, lakini pia midogo mfano wa Hisopo, na jinsi inavyomea. Na hapo tunaona anaeleza sifa yake, kwamba ni mmea unaomea ukutani.
Ikiwa na maana, mahali palipo na ardhi ngumu, au mwamba au jiwe, wenyewe unamea, na kukua na kuzaa bila shida yoyote. Tofauti na mimea mingine mingi yenye nguvu, itahitaji udogo mlaini mwingi, tena tifutifu, lakini huu wa hisopo ni wa kipekee unahitaji mahali pagumu.
Mmea huu unamfunua Bwana wetu Yesu Kristo,yeye Hakuhitaji mahali palipoandaliwa pa kitajiri, ili kulitimiza kusudi la kifalme duniani, hakuhitaji familia ya kidini maarufu, au kabila la kikuhani, ili aishi maisha makamilifu, hakuhitaji kuishi mji mtakatifu Yerusalemu ili ampendeze Mungu. Bali alitokea mahali ambapo ni vijijini (Nazareti), familia maskini, tena nyakati za kipagani, ambazo imani ilikuwa imekongoroka sana, pia, kabila lisilojiuhusisha na mambo yoyote ya kikuhani kabisa. Hivyo Yesu aliishi katika jamii ya wapagani.
Wakati sisi katikati ya dhiki nyingi (yaani penye mwamba mgumu) tunanyauka. Yeye ndio alikuwa anasitawi. Aliweza kustahimili mapingamizi ya kila namna zaidi ya mwanadamu yoyote aliyewahi kutokea hapa duniani. Alichukiwa na ulimwengu, alisalitiwa, alikanwa, aliachwa peke yake, aliaibishwa, alipigwa mpaka kuuawa. Lakini hakuwahi kuanguka au kutenda dhambi yoyote. Haleluya! Anastahili hakika mwokozi wetu Yesu Kristo.
Ni hisopo umeao ukutani. Mahali ambapo mimea mingine imeshindwa, yeye ameweza.
Na ndio maana Neno linasema;
Waebrania 12:2 tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu. 3 MAANA MTAFAKARINI SANA YEYE ALIYEYASTAHIMILI MAPINGAMIZI MAKUU NAMNA HII YA WATENDAO DHAMBI JUU YA NAFSI ZAO, msije mkachoka, mkizimia mioyoni mwenu. 4 Hamjafanya vita hata kumwagika damu, mkishindana na dhambi;
Waebrania 12:2 tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.
3 MAANA MTAFAKARINI SANA YEYE ALIYEYASTAHIMILI MAPINGAMIZI MAKUU NAMNA HII YA WATENDAO DHAMBI JUU YA NAFSI ZAO, msije mkachoka, mkizimia mioyoni mwenu.
4 Hamjafanya vita hata kumwagika damu, mkishindana na dhambi;
Umeona ni kwa namna gani Yesu alivyokuwa mwamba imara wa kutegemea sana?
Na ndio maana maandiko sasa yanasema, kwa kuwa alijaribiwa kama sisi, basi anaweza kuchukuliana na sisi pia katika mambo yetu ya udhaifu.
Waebrania 4:14 Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu. 15 Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi. 16 Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.
Waebrania 4:14 Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu.
15 Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi.
16 Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.
Hivyo ndugu, ni nini unachongoja, usiokoke leo?. Wewe peke yako hutaweza, kuushinda huu ulimwengu, unaihitaji neema ya Yesu Kristo ikusaidie. Mpokee leo, upate ondoleo la dhambi zako, Akupe na Roho wake mtakatifu ili kukusaidia sasa kuishi maisha ya ushindi kama yeye alivyoishi.
Ukipita katika miamba lakini unaendelea kumea. Hivyo chukua uamuzi huo leo. Ikiwa upo tayari kuokoka basi fungua hapa kwa mwongozo wa sala ya Toba. >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
ALIFANYIKA SADAKA KWA AJILI YETU!
VITA BADO VINAENDELEA.
TUKAZE MWENDO KWA TULIYOANDALIWA.
TUNAHESABIWA HAKI BURE KWA NJIA YA IMANI.
Swali: roho za Malipizi ni nini na mtu anawezaje kuzifunga?
Jibu: roho ya Malipizi au roho za malipizi ni roho zinazojilipiza kisasi baada ya kushindwa vita.
Maandiko yanasema vita vyetu sisi si juu ya damu na nyama, bali juu ya falme na mamlaka za giza katika ulimwengu wa roho.
Waefeso 6:12 “Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho”.
Sasa hizi roho za mapepo na za wakuu wa giza, zinaposhindwa vita dhidi ya mtu, au watu, au kanisa basi, huwa zina tabia ya kukimbilia kutafuta sehemu nyingine iliyo dhaifu ya huyo mtu, au watu au kanisa na kushambulia ili kumwumiza yule aliyekuwa anashindana nazo.
Tuchukue mfano, mtu mmoja aliyeokoka ameomba kwaajili ya familia yake (Labda kwajili ya Mke wake au Mume au watoto), na katika kuomba kwake, ameomba ulinzi, na neema ya kumjua Mungu, na Zaidi sana amezikemea roho zote zinazopambana na familia yake, (roho za kurudi nyuma, roho za magonjwa na matatizo mengine) na amezishinda kwa maombi na kuziadhibu sawasawa na 2Wakorintho 10:6.
Sasa roho hizo (za mapepo na wakuu wa giza) zinapoanguka na kushindwa namna hiyo, huwa zina tabia ya kulipiza kisasi…kwa wakati huo zinaondoka na kwenda kutafuta sehemu nyingine ya maisha ya huyo mtu zilizo dhaifu na kuzivamia au kufanya nazo vita kutokana na uchungu na hasira za kushindwa..
Ndio hapo zitaacha kushughulika na familia ya huyo mtu kwa muda, na kwenda kupiga marafiki wa karibu wa huyo mtu, au wazazi, au watu wengine wowote walio wa muhimu katika maisha ya huyo mtu, lengo ni ili kumwumiza huyo mtu au kumsumbua na zinaweza kwenda kupiga kwa magonjwa, hasara au hata mauti kabisa..
Hivyo ni muhimu sana kumalizia maombi kwa kuomba ulinzi kwa watu wote walio karibu nawe ili wazidhurike na ghadhabu za hizo roho.
Hiyo siku zote ndio tabia ya shetani na majeshi yake, “kujilipiza kisasi”…
Sasa pengine utauliza ni wapi katika biblia jambo kama hilo limetokea?..tusome maandiko yafuatayo..
Ufunuo 12:7 “Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; 8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. 9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.
Ufunuo 12:7 “Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;
8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.
9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.
10 Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.
11 Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa. 12 Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! KWA MAANA YULE IBILISI AMESHUKA KWENU MWENYE GHADHABU NYINGI, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu”.
11 Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.
12 Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! KWA MAANA YULE IBILISI AMESHUKA KWENU MWENYE GHADHABU NYINGI, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu”.
Umeona hapo mstari wa 12, maandiko yanasema yule ibilisi aliposhindwa alitupwa chini mwenye ghadhabu nyingi, na anashuka kujilipiza kisasi kwa kufanya vita na hao wakaao juu ya nchi na bahari kutokana na kushindwa kwake vita mbinguni. Na hapa tumeshapata jibu kwanini shetani anafanya vita na sisi wanadamu?.. sababu si nyingine Zaidi ya kisasi alichonacho, lakini ashukuriwe Kristo YESU Bwana wetu yupo katika mkono wa kuume akituombea (Warumi 8:34) .
Lakini tukizidi kusoma maandiko hayo mpaka ule mstari wa 17 bado tunaendelea kuona kisasi cha shetani baada ya kushidwa tena vita dhidi ya yule ya yule mtoto (YESU KRISTO) na dhidi ya yule mwanamke (Israeli).
Ufunuo 12:13 “Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika nchi, alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa mtoto mwanamume. 14 Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo. 15 Nyoka akatoa katika kinywa chake, nyuma ya huyo mwanamke, maji kama mto, amfanye kuchukuliwa na mto ule. 16 Nchi ikamsaidia mwanamke; nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake. 17 Joka akamkasirikia yule mwanamke, AKAENDA ZAKE AFANYE VITA JUU YA WAZAO WAKE WALIOSALIA, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari”.
Ufunuo 12:13 “Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika nchi, alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa mtoto mwanamume.
14 Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo.
15 Nyoka akatoa katika kinywa chake, nyuma ya huyo mwanamke, maji kama mto, amfanye kuchukuliwa na mto ule.
16 Nchi ikamsaidia mwanamke; nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake.
17 Joka akamkasirikia yule mwanamke, AKAENDA ZAKE AFANYE VITA JUU YA WAZAO WAKE WALIOSALIA, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari”.
Umeona tena hapo?.. baada ya Ibilisi kumshindwa “mtoto na yule mwanamke” anapanga tena malipizi juu ya uzao wake, hiyo yote ni kuonyesha roho mbaya ya kisasi aliyonayo adui.
Vivyo hivyo, mpaka leo hiyo roho anayo pamoja na mapepo yake, yakishindwa vita yanaenda kutafuta wengine kumalizia hasira zao, kwahiyo ni muhimu sana pia kuomba maombi ya kufunga na kuzuia hizo roho zisiende kuleta madhara sehemu nyingine ya maisha ya watu unaohusiana nao!.
Na huu ndio umuhimu wa kuwaombea wengine, na pia ndio umuhimu wa kuomba.. Usipokuwa mwombaji na kusubiri kuombewa tu mara kwa mara, upo katika hatari ya kuvamiwa na maroho ya malipizi kutoka katika kila kona (kutokana na maombi ya wengine) endapo hawatafunga hizo roho. Kwahiyo ni muhimu sana kuomba na kuwaombea wengine.
2Wakorintho 10:4 “(maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;) 5 tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo; 6 tena tukiwa tayari kupatiliza maasi yote, kutii kwenu kutakapotimia”
2Wakorintho 10:4 “(maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)
5 tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;
6 tena tukiwa tayari kupatiliza maasi yote, kutii kwenu kutakapotimia”
Maran atha.
HIZO NDIZO ROHO ZA MASHETANI.
USILIPIZE KISASI.
UFUNUO: Mlango wa 12
JINSI YA KUPIGANA MAOMBI YA VITA.
Nini maana ya Dirii, Chapeo na Utayari?
Kama mwamini hizi si nyakati za kuishi kilegevu, unapoona, watu wanakufa katika dhambi na kwenda jehanamu bila kumjua Kristo, unajisikiaje, unapoona kazi za shetani zinasitawi, na kuwaharibu watu unawezaje kutujulia moyoni mwako?
Ni Funzo gani unalipata nyuma ya hasira ya Samsoni? Alipoona mke wake ameuzwa kwa wageni na baba-mkwe wake, je alitulia, na kusema basi tu hii siyo bahati yangu? Kinyume chake Alinyanyuka kwa hasira akasema ninakwenda kulipiza kisasi, kwa hawa wafilisti.
Alikwenda kuwachukua mbweha mia tatu (300), Akawafunga wawili wawili mikia yao, kisha, akawafungia mienge ya moto, na kuwaachia waingie kwenye mashamba ya ngano ya wafilisti. Baada ya hapo ni jambo gani akawa analifanya? Ni kuwaangalia tu wale mbweha walivyokuwa wanayateketeza mashamba ya ngano hekari kwa mahekari. Jambo lililowafanya wafilisti waamke wote kwenye majumba yao wamtafute huyu Samsoni ni nani?
Waamuzi 15:3 “Samsoni akasema, Safari hii nitakuwa sina hatia katika habari za hawa Wafilisti, hapo nitakapowadhuru. 4 Samsoni akaenda akakamata mbweha mia tatu; kisha akatwaa vienge vya moto akawafunga mbweha mkia kwa mkia, akatia kienge kati ya kila mikia miwili. 5 Alipokwisha kuviwasha moto vile vienge, akawaachia mbweha kati ya ngano ya Wafilisti, akayateketeza matita, na ngano, hata na mashamba ya mizeituni”
Ni Yesu Kristo,
Bwana alipoona kazi za adui zinapaswa ziharibiwe pale Israeli. Alichofanya ni kuwachukua wanafunzi wake pia, akawatuma wawili-wawili akawaambia waende mahali alipotaka yeye kwenda, akawapa amri ya kutoa pepo, kupooza magonjwa na kuhubiri habari njema. Na unajua ni nini kilitokea baada ya pale, ndani ya kipindi kifupi, waliporudi?
Yesu alikuwa akiwaangalia “MBWEHA WAKE” katika roho wakiziharibu kazi za shetani, akasema, nalimwona shetani akianguka kutoka mbinguni kama umeme.. Ha! ha! ha! ha! Mbweha wamfanya kazi.
Luka 10:17 “Ndipo wale sabini waliporudi kwa furaha, wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako. 18 Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme. 19 Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru”.
Na sisi (yaani mimi na wewe), tuliookoka, Ikiwa umeshajazwa “Roho Mtakatifu” wewe tayari ni mbweha, Sijui unasubiri nini kwenda kuziharibu kazi za shetani, kwa kumuhubiri Kristo, na wokovu wake? Unasubiri nini mpendwa?
Angalia Yesu alichokisema..
Luka 12:49 “Nimekuja kutupa moto duniani; na ukiwa umekwisha washwa, ni nini nitakalo zaidi?
Moto umekwisha kuwekwa kwenye mkia wako, angalia usije ukazima kabla haujafanya kazi yake. Ndio huo moto wa Roho Mtakatifu unaochoma ndani yako, kukuagiza uhihubiri neema ya Kristo kwa ndugu zako na watu wengine ili waokoke.
Kwa pamoja tunaweza upindua ulimwengu. Tumuhubiri Kristo, hilo ndilo agizo kuu kwa wanadamu wote. Kila mmoja wetu ni mbweha wa Kristo. Simama sasa, pokea ujasiri, kamuhubiri Kristo, watu waokoke.
KWANINI KILA MWAMINI ANAPASWA AWE MHUBIRI WA INJILI
JE! NYWELE ZAKO ZINAOTA AU ZIMESIMAMA?
KITENDAWILI CHA SAMSONI
HUDUMA YA MALAIKA WAWILI.
Hizi ni sababu kuu nne (4), ambazo zinampa sababu mwaminio yoyote kuihubiri injili kwa nia yote kutoka moyoni.
Marko 16:15 “Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. 16 Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa”
Bwana wetu alituagiza, na kutupa jukumu la kufanya sisi kama wakristo. Sio tu kusema sisi tumeokoka halafu basi, hapana bali ni pamoja na kuwafanya wengine kuwa kama sisi, kuwafanya kuwa wanafunzi wa Kristo.
Mitume walikuwa na ujasiri wa kumuhubiri Kristo, kwasababu ya ushuhuda wao wenyewe kwa mambo waliyoyaona kwa Bwana Yesu akiwatendea.
Matendo 4:18 Wakawaita, wakawaamuru wasiseme kabisa wala kufundisha kwa jina la Yesu. 19 Petro na Yohana wakawajibu wakawaambia, Kwamba ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza ninyi kuliko Mungu, hukumuni ninyi wenyewe; 20 maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo tuliyoyaona na kuyasikia.
Matendo 4:18 Wakawaita, wakawaamuru wasiseme kabisa wala kufundisha kwa jina la Yesu.
19 Petro na Yohana wakawajibu wakawaambia, Kwamba ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza ninyi kuliko Mungu, hukumuni ninyi wenyewe;
20 maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo tuliyoyaona na kuyasikia.
Ukisoma pia 1Yohana 1:1-3 Mtume Yohana anasema..
1Yohana 1:1 Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya Neno la uzima; 2 (na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu); 3 HILO TULILOLIONA NA KULISIKIA, TWAWAHUBIRI NA NINYI; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo.
1Yohana 1:1 Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya Neno la uzima;
2 (na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu);
3 HILO TULILOLIONA NA KULISIKIA, TWAWAHUBIRI NA NINYI; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo.
Hii ikiwa na maana, kuwa kila mkristo aliyekombolewa, anaoushuhuda wa mambo makuu aliyotendewa na Yesu tangu siku alipookoka, Tofauti kubwa aliyoipata katika maisha yake mpya ukilinganisha na yale ya zamani, jinsi mizigo yake ilivyotuliwa, hofu kuondolewa, magonjwa yake kuponywa, kufunguliwa, kupokea furaha ya wokovu isiyo na kiasi, amani, utulivu. N.k.
Yote haya kwa mkristo anayethamini wema wa Mungu hataona aibu kutamani na wengine wauonje uzuri huo ulio katika Kristo Yesu. Na hivyo atatoka nje! na kwenda kuwahubiria wengine Injili ya Yesu Kristo,kama mitume walivyofanya.
Hili lilimkuta mtume Paulo, Hapo mwanzoni alidhani yeye ndio anayekwenda kuwashawishi watu kuhusu Yesu, lakini siku moja aliona maono, watu wa mbali Makedonia wakiwa na uhitaji mkubwa sana wa kumjua Mungu. Hivyo akalitii ono lile akaenda.
Matendo 16:9 Paulo akatokewa na maono usiku; alimwona mtu wa Makedonia amesimama, akimsihi, na kumwambia, Vuka, uje Makedonia utusaidie. 10 Basi alipokwisha kuyaona yale maono, mara tukataka kutoka kwenda Makedonia, kwa kuwa tuliona hakika ya kwamba Mungu ametuita tuwahubiri Habari Njema.
Matendo 16:9 Paulo akatokewa na maono usiku; alimwona mtu wa Makedonia amesimama, akimsihi, na kumwambia, Vuka, uje Makedonia utusaidie.
10 Basi alipokwisha kuyaona yale maono, mara tukataka kutoka kwenda Makedonia, kwa kuwa tuliona hakika ya kwamba Mungu ametuita tuwahubiri Habari Njema.
Hata sasa, wapo watu wengi wana kiu ya kuijua njia ya kweli, mioyoni mwao wakiwa na shauku ya kuifahamu hiyo NJIA. Lakini sisi tukikaa na kusema hakuna mwenye haja, twajidanganya. Hatupaswi kuona watu kwa nje wanatuchekea, wanafurahi, wana raha, tukadhani hali zao rohoni ndio hivyo zilivyo, tukapuuzia kuwahubiria injili. Wengi wapo kwenye vifungo na wanatamani wapate msaada wa kutoka huko, hawasemi tu. Na anayeweza kuwatoa hapo ni Kristo tu peke yake. Siku ukizungumza nao ndio utajua kweli walikuwa na haja na Kristo. Hivyo usichague wa kumshuhudia. Fahamu tu watu wana haja na kuujua ukweli. Hubiri injili ya Kristo.
Tunajua mtu akifa nje ya Kristo, hakuta tumaini, ni moja kwa moja jehanamu. Tengeneza picha ndugu zako uwapendao, rafiki zako, wazazi wako, na wanadamu wenzako wanakwenda kwenye moto wa milele. Wewe una raha gani leo hii usiwashuhudie habari za Yesu Kristo?.Embu tengeneza picha habari ya Yule tajiri na Lazaro, (Luka 16:19-30) alitamani, mtu atoke kuzimu akawahubirie watu injili ili wasifike mahali pale pa mateso, lakini akaambiwa wapo Musa na manabii huko duniani (ambao ndio sisi), tuwahubirie.
Hivyo kwa sababu hizo kuu nne (4), wewe kama mwaminio uliyeokoka, huna budi kuwashuhudia wengine habari za Kristo. Utasema mimi sina uzoefu, Kumbuka Yesu haitaji uzoefu wako, kuwaokoa watu, kwasababu hata wewe hukuupokea kwa uzoefu wowote, anahitaji kuwaambia Yesu anasemehe dhambi, anaokoa wanadamu, anatoa uzima wa milele bure, anatuepusha na hukumu ya milele, anatua mizigo ya watu, anafariji, anaponya roho, anatupa nguvu ya kuushinda ulimwengu na dhambi. Njoo kwake, akufanye kiumbe kipya upokee uzima wa milele. Hivyo tu. Na hayo mengine mwachie yeye, usifikiri fikiri atakuongoza kwa jinsi utakavyokuwa unasema.
Mathayo 10:20 “ Kwa kuwa si ninyi msemao, bali ni Roho wa Baba yenu asemaye ndani yenu”.
Anza sasa.
NI INJILI GANI UNAHUBIRI?
INJILI YA MILELE NI IPI KATIKA BIBLIA?
BIBLIA INAITAJA NJIA KUU YA MFALME, NJIA HII NI IPI?
NJIA KUU YA KUINGIA KATIKA ULE MJI.
JE KANISA LITAPITIA DHIKI KUU?
Kawaida MUNGU huwa anajibu maombi, isipokuwa Majira yake mara nyingi ni tofauti na Majira yetu.. Sisi uwa tunapenda tujibiwe maombi muda ule ule tunapoomba!.. Hiyo inaweza kutokea ikiwa ombi uliloomba linastahili kujibiwa wakati huohuo..
Lakini ikiwa si mapenzi ya Mungu upate hiko ulichokiomba kwa wakati huo, basi itakupasa usubiri mpaka wakati wa Bwana, na hiyo haimaanishi kuwa Mungu hajakujibu!.. Ameshakujibu isipokuwa jibu lako hajaliweka leo, bali kaliweka kesho, au mwezi ujao au mwaka ujao, au miaka kadhaa ijayo..Kwasababu majibu mengine yanahitaji kwanza mtu aandaliwe ndipo apokee alichokiomba.
Haiwezekanani mtoto ambaye hajaanza hata shule amwombe baba yake amnunulie gari ili aendeshe kwasababu tu baba yake ana uwezo, halafu yule mzazi amjibu kwa kumnunulia hilo gari na kumpa aendeshe siku ile ile alipoomba..Ni kitu ambacho hakiwezekani! Kwa mzazi mwenye akili timamu.
Badala yake mzazi atalichukua lile ombi la mwanae na kuliweka akiba, mpaka atakapokuwa mtu mzima, amekomaa kiakili na kielimu ndipo ampe zawadi ile ya gari, ambayo aliomba miaka kadhaa nyuma…kwasababu wakati huo atakuwa anajua jinsi ya kuliendesha na amekomaa kiakili. Lakini mtoto huyo huyo akiomba peremende kutoka kwa baba yake ni rahisi kupewa wakati ule ule alioomba, kwasababu ombi lake ni dogo, na halihitaji maandalizi yoyote.
Vile vile na kwa upande wa Mungu wetu (ambaye tunamwita BABA)..yapo maombi ambayo anayajibu papo kwa hapo na mengine yatachukua muda, mpaka mtu ajibiwe…
Ndio maana baada ya kuomba ni vizuri kuruhusu mapenzi ya MUNGU yatimie kama Daudi alivyosema katika..
Zaburi 69:13 “Nami maombi yangu nakuomba Wewe, Bwana, Wakati ukupendezao; Ee Mungu, Kwa wingi wa fadhili zako unijibu, Katika kweli ya wokovu wako. 14 Uniponye kwa kunitoa matopeni, Wala usiniache nikazama. Na niponywe nao wanaonichukia, Na katika vilindi vya maji”.
Zaburi 69:13 “Nami maombi yangu nakuomba Wewe, Bwana, Wakati ukupendezao; Ee Mungu, Kwa wingi wa fadhili zako unijibu, Katika kweli ya wokovu wako.
14 Uniponye kwa kunitoa matopeni, Wala usiniache nikazama. Na niponywe nao wanaonichukia, Na katika vilindi vya maji”.
LAKINI PAMOJA NA HAYO YAPO MAOMBI AMBAYO MUNGU HAJIBU KABISA!!. NA MAOMBI HAYO NI KAMA YAFUATAYO.
1. MAOMBI YA TAMAA.
Mfano wa maombi ya tamaa ni yale mtu anaomba kitu si kwasababu ana haja na hiko kitu, bali kwasababu anataka kukitumia kwa anasa, au kwa mashindano, au kwa maonesho.
Mfano mtu ataomba Mungu ampe pesa, si kwasababu anataka atokane na changamoto Fulani za msingi, bali lengo lake ni ili awe nazo ili awaoneshe watu, au ajivune mbele za watu, au azitumie kwa anasa.. Mtu huyu anaweza asiseme kwa kinywa lakini moyo wake ndivyo vitu unavyovitamani.. Sasa maombi ya mtu wa namna hiyo biblia imesema huwa hayajibiwi.
Yakobo 4:3 “Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu”. Kwahiyo ni muhimu sana, kuzichunguza NIA zetu, (kwamba kwanini tunaomba)..tuhakikishe nia zetu ni safi, na kweli tuna haja na hiko kitu tukiombacho kwa NIA njema.
Yakobo 4:3 “Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu”.
Kwahiyo ni muhimu sana, kuzichunguza NIA zetu, (kwamba kwanini tunaomba)..tuhakikishe nia zetu ni safi, na kweli tuna haja na hiko kitu tukiombacho kwa NIA njema.
2. MAOMBI YA MTU MWOVU.
Mtu ambaye hamtaki Mungu moyoni mwake, lakini anataka vya Mungu (anataka kupokea kutoka kwa Mungu), maombi yake mtu huyo hayajibiwi!.
Ni muuaji na hataki wala hana mpango wa kuacha uuaji wake, ni mwizi wala hana mpango wa kuacha wizi wake, ni mzinzi na mwasherati wala hana mpango wa kuacha uasherati wake ijapokuwa anasikia mahubiri yahusuyo hayo kila siku, maombi yake mtu huyu hayajibiwi kulingana na biblia.
Isaya 1:15 “Nanyi mkunjuapo mikono yenu, nitaficha macho yangu nisiwaone; naam, mwombapo maombi mengi, sitasikia; mikono yenu imejaa damu. 16 Jiosheni, jitakaseni; ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu; acheni kutenda mabaya; 17 jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane”.
Isaya 1:15 “Nanyi mkunjuapo mikono yenu, nitaficha macho yangu nisiwaone; naam, mwombapo maombi mengi, sitasikia; mikono yenu imejaa damu.
16 Jiosheni, jitakaseni; ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu; acheni kutenda mabaya;
17 jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane”.
3. MAOMBI YA MANUNG’UNIKO NA MALALAMIKO.
Maombi ya Manung’uniko na malalamiko ni yale mtu anaomba kwa kulaumu, na kunung’unika kana kwamba kaonewa au kadhulumiwa, maombi kama haya majibu yake mara nyingi ni kinyume.. badala ya mtu kupokea anachokinung’unikia kinyume chake anaweza kupoteza hata kile kidogo alicho nacho.
1Wakorintho 10:10 “Wala msinung’unike, kama wengine wao walivyonung’unika, wakaharibiwa na mharabu. 11 Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani”.
1Wakorintho 10:10 “Wala msinung’unike, kama wengine wao walivyonung’unika, wakaharibiwa na mharabu.
11 Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani”.
Epuka manung’uniko wakati wa maombi.. badala yake kuwa mtu wa shukrani, na mtu wa kumsihi Mungu kwa unyenyekevu na heshima.
4. MAOMBI YA KUMJARIBU MUNGU.
Mfano wa maombi haya ni yale, shetani aliyompelekea Bwana YESU kule jangwani.
Luka 4:9 “Akamwongoza mpaka Yerusalemu, akamweka juu ya kinara cha hekalu, akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini; 10 kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake wakulinde; 11 na ya kwamba,mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe. 12 Yesu akajibu akamwambia, Imenenwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako”.
Luka 4:9 “Akamwongoza mpaka Yerusalemu, akamweka juu ya kinara cha hekalu, akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini;
10 kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake wakulinde;
11 na ya kwamba,mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
12 Yesu akajibu akamwambia, Imenenwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako”.
Usiombe maombi ya kumwangalia BWANA atafanya nini… maombi ya nama hiyo hayana majibu, na zaidi wakati mwingine yanaishi kupokea adhabu badala ya Baraka.
1Wakorintho 10:9 “Wala tusimjaribu Bwana, kama wengine wao walivyomjaribu, wakaharibiwa na nyoka”
Jihadhari na aina hizo nne (4) za Maombi ili upokee majibu ya Maombi yako.
FAIDA ZA MAOMBI.
Kuomba katika roho ni kupi? na je nifanye nini ili niweze kuomba hivyo?
NDUGU,TUOMBEENI.
KUNA AINA NGAPI ZA MAOMBI?
Si kila mtu anayesema “amemwamini” Yesu ni kweli, ameokoka, au amepokea msamaha wa dhambi zake. Ukweli ni kwamba kuupokea msamaha wa dhambi kwa kuiamini kazi aliyoimaliza Yesu Kristo pale msalabani ya ukombozi wa wanadamu si kugumu, Lakini haiji kwa kusema “naamini tu” halafu basi ndio uwe tayari umetiwa muhuri na Mungu kwamba ni wake milele.
Imani ya namna hiyo inatiwa imani ya” bure” (1Wakorintho 15:2).
Na sehemu nyingine inajulikana kama “imani ya wote” ambayo hata mashetani wanayo. Wanamwamini Yesu kuwa ni mwokozi, lakini pia wanaiamini vizuri sana kazi ya msalaba (Yakobo 2:19). Lakini je! Wamesamehewa dhambi zao?
Zipo injili zinazowafundisha watu, “kuamini tu” au “kukubali tu msamaha” inatosha. Hakuna la ziada baada ya hapo. Ndugu hizo sio sifa za mwaminio yoyote.
Neno “kuamini” kwa kigiriki ni PISTIS, lenye maana ya sio tu kuwa na ujasiri na Mungu wako kwa kile anachokupa au kukuelekeza,lakini pia kuwa ‘mwaminifu”.
Maana yake ni kuwa ili tuseme tumeamini ni lazima pia tuwe waaminifu kwa Yule tuliyemwamini.
Sasa mtu yeyote aliyemwamini Kristo. viashiria hivi vitatu(3) utaviona ndani yake
Yohana 10:2 Aingiaye mlangoni ni mchungaji wa kondoo. 3 Bawabu humfungulia huyo, na kondoo humsikia sauti yake; naye huwaita kondoo wake kwa majina yao, na kuwapeleka nje. 4 Naye awatoapo nje kondoo wake wote, huwatangulia; na wale kondoo humfuata, kwa maana waijua sauti yake. 5 Mgeni hawatamfuata kabisa, bali watamkimbia; kwa maana hawazijui sauti za wageni… 27 Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata. 28 Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu. 29 Baba yangu aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote; wala hakuna mtu awezaye kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu.
Yohana 10:2 Aingiaye mlangoni ni mchungaji wa kondoo. 3 Bawabu humfungulia huyo, na kondoo humsikia sauti yake; naye huwaita kondoo wake kwa majina yao, na kuwapeleka nje. 4 Naye awatoapo nje kondoo wake wote, huwatangulia; na wale kondoo humfuata, kwa maana waijua sauti yake. 5 Mgeni hawatamfuata kabisa, bali watamkimbia; kwa maana hawazijui sauti za wageni…
27 Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata. 28 Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu. 29 Baba yangu aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote; wala hakuna mtu awezaye kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu.
Umeona, ni kondoo tu, ndio hawawezi kupokonywa katika mikono ya mchungaji wake. Lakini mbuzi wanaweza, kwasababu hawategemei sana sauti ya mchungaji, wanaweza kujichunga wenyewe. Ukiona mtu anasema ameokoka, halafu, maisha yake ni kama ya mbuzi, ujue huyo si wa Kristo. Haisikii sauti ya Kristo ikimwelekeza aache maisha ya kiulimwengu, ajitofautishe na watu wa kidunia, . Ujue huyo bado hajapokea kweli msamaha wa dhambi, kwasababu hajaamini. Anapaswa ashuhudiwe mpaka aamini. Na aseme kuanzia leo, Kristo ndio kiongozi wa maisha yangu na sio dunia tena. Akubali TOBA ya kweli.
2. Atakuwa Ni kiumbe kipya.
Yesu alisema..
Yohana 1:12 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake. 13 waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu
Yohana 1:12 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake.
13 waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu
Wenye sifa ya kwamba wamemwamini Yesu ni lazima pia wawe wamegeuzwa kuwa watoto wa Mungu, yaani wamezaliwa mara ya pili kwa mbegu isiyo ya kibinadamu, bali ya Mungu mwenyewe.
Na kama tunavyofahamu mtoto hubeba tabia za Baba. Vivyo hivyo mwaminio ni lazima moyoni mwake kuwake, tamaa za Baba yake. Maandiko yanasema Baba ni Mtakatifu, vivyo hivyo tamaa ya mwaminio huyo mpya itakuwa ni kupenda utakatifu, na kuutafuta huo kwa bidii.
Haiwezekani mtu aliyemwamini Yesu, awe na raha tena katika maisha ya kidunia ya dhambi. Au asipige hatua yoyote ya kuutafuta ukamilifu. Halafu tuseme ni mwaminio si kweli.
1Yohana 3:9 Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu
3) Atakuwa ni mwanafunzi
Mwaminio mpya amefananishwa na mwanafunzi, na mwanafunzi sikuzote huwa yupo tayari kujifunza, na kukua kiufahamu.
Matendo 2:41 Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu. 42 Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.
Hivyo mtu yoyote anayesema amemwamini Yesu, na hapendi fundisho, hapendi kuchungwa, hapendi kufuatiliwa maendeleo yake ya kiroho, anapinga ubatizo, na wakati mwingine kufanya ushirika, huyo mtu bado hajaamini.
Lakini akiwa na sifa zote hizo tatu, ni uthibitisho kuwa amemwamini Yesu, na hivyo kaupokea pia msamaha wa dhambi. Mtu wa namna hiyo wokovu kwake ni uhakika. Kwasababu Yesu ameumbika ndani yake. Kazi ya Mungu kamilifu imetimilika ndani ya mwanadamu.
Je! Na wewe Umepokea ondoleo la dhambi zako? Je! Ni mwanafunzi, ni kondoo, ni mwana wa Mungu?. Kama bado basi fahamu unamwihitaji Kristo, fungua moyo wako mkaribishe ndani yako akuokoe. Sasa, Maanisha tu tangu sasa kuwa na badiliko na yeye mwenyewe atakuokoa.
JE! UNAMPENDA BWANA?
NAMNA YA KUITAMBUA SAUTI YA MUNGU INAPOZUNGUMZA NA WEWE
LISHA KONDOO WANGU, LISHA WANA-KONDOO WANGU.