Category Archive Mafundisho

UKWELI KUHUSU UISLAMU Sehemu ya kwanza: (Msikiti wa AL-Aqsa).

Je msikiti wa Al-Aqsa ni nini, na unahusikaje katika unabii wa biblia?

Angalizo: Makala hii haina lengo la kushambulia Imani Fulani, wala kushabikia Imani Fulani, pia haina lengo la kumchafua mtu yoyote, wala kumdhalilisha, bali kutoa elimu sahihi kuhusiana na tunayoamini na yanayoaminiwa.

MSIKITI WA Al-Aqsa

Msikiti wa Al-Aqsa ni msikiti uliopo katika mji wa YERUSALEMU, ndani ya Nchi ya Israeli, Msikiti huu unaaminika kuwa ni sehemu ya tatu ya utakatifu kulingana na dini ya kiislamu, Sehemu ya kwanza ikiwa ni Makka (au Mecca), ya pili ni Al-masjid an Nabawi iliyopo Medina (nchini Saudi Arabia), na ya tatu ndio hii Al-Asqa.

Msikiti wa Al-Aqsa umejengwa pembezoni mwa jengo maarufu kama “Kuba ya Mwamba” (au Dome of Rock), tazama picha chini.

kuba ya mwamba

Msikiti huu wa Al-Aqsa unaaminika ulijengwa na mtu aliyeitwa Umayyad caliph Abd al-Malik kati ya Karne ya saba (7) na ya nane (8), baada ya KRISTO. Na kulingana na dini  ya kiislamu, inaaminika kuwa Muhamad ndipo alipopaa mbinguni na kwenda kupewa ufunuo wa kitabu cha Quran (Sasa kujua kama ni kweli au si kweli soma Makala hii mpaka mwisho)..

Mbali na kwamba katika msikiti huu ndio panaaminika kuwa mahali Muhamad alipopaa lakini pia zamani paliaminika na waislamu wa kwanza kuwa ndio maahali pa kutazama wakati wa sala, maarufu kama “kibla”. Hebu tuielezee hii Kibla kidogo..

Kibla ni neno la kiaramu lenye maana ya “Uelekeo”, Waislamu wanaposali kulingana na Imani yao, wanapaswa waelekee upande Fulani, sasa zamani Kibla ilikuwa ni katika huu msikiti wa Al-Aqsa uliopo Yerusalemu Israeli, lakini baadae walikuja kubadilisha kulingana na kuwa mahali pajulikanapo kama Makka (Mecca) huko Saudi Arabia, ambapo ndipo Muhamad alipozaliwa.

Hivyo sasa waslamu wote wanaposali wanaelekea kibla huko Makka Saudi Arabia na si tena Yerusalemu, na pia mtu anapozikwa anaelekezewa huko Makka, na vile vile mnyama anapochinjwa anaelekezewa huko huko Makka (kujua usahihi wa jambo hili na kama wakristo wanaruhusiwa kushiriki vyakula hivyo endelea kufuatilia Makala hizi)..

Sasa swali ni je! Huu msikiti ambao sasahivi upo pale Yerusalemu, unaoaminika na watu Zaidi ya Bilioni 1.9, kuwa ndio sehemu ya Tatu kwa utakatifu, je msikiti huu utaendelewa kuwepo pale milele au utakuja kuondolewa?.

Jibu: Kujua kama utaondolewa au la! Turejee Biblia..

Maandiko yanasema lile Hekalu la Kwanza lililojengwa na Sulemani, lilitengenezwa juu ya Mlima Moria, ambapo ni eneo lile lile Abrahamu alipotaka kwenda kumtoa mwanae Isaka kama sadaka ya kuteketezwa, na sasa ndio eneo hili hili ambalo msikiti wa Al-Aqsa umejengwa.

Na ilikuwaje Hekalu kuondolewa na msikiti kujengwa?..

Sababu iliyofanya Msikiti huo kujengwa mahali pale pale Hekalu lilipokuwepo… ni kuvunjwa kwa hekalu hilo mara ya kwanza na ya pili…na wayahudi (yaani waisraeli), kuondolewa katika nchi yao na kutapanywa katika mataifa yote mwaka ule wa 70 Baada ya Kristo.

Wayahudi walipoondolewa katika nchi yao kutokana na makosa yao kwa Mungu, ndipo Ngome ya kiarabu ikateka na kujenga msikiti huo.

Adhabu ya Mungu kwa Israeli, haikuwa ya milele, kwani aliahidi atawarudia tena, na kuwarudisha katika nchi yao, na tena watalijenga Hekalu. (soma Ezekieli 40-48), na kufikia mwaka 1948, Israeli walirejea nchini kwao na mpaka sasa wapo pale.

Na hatua ya kwanza ya matengenezo ni wao kuirudia torati waliyopewa na Musa, hivyo watalijenga Hekalu kama lile la kwanza na baadaye, watamwagiwa Neema na macho yao kufumbuliwa Zaidi kwa kumwamini Masihi YESU, aliye hekalu halisi, sawasawa na Warumi 11 (kwani kwasasa wengi wao hawaamini hivyo).

Warumi 11:1 “Basi, nauliza, Je! Mungu aliwasukumia mbali watu wake? Hasha! Kwa kuwa mimi nami ni Mwisraeli, mmoja wa wazao wa Ibrahimu, mtu wa kabila ya Benyamini.

2  Mungu hakuwasukumia mbali watu wake aliowajua tokea awali. Au hamjui yale yaliyonenwa na maandiko juu ya Eliya? Jinsi anavyowashitaki Waisraeli mbele za Mungu………………………

25  Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili.

26  Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake”.

Sasa kabla ya huo wakati wa Israeli kufumbuliwa macho,na kumjua Kristo kama Hekalu halisi, watasimamisha kwanza Hekalu la damu na nyama, na mahali litakapojengwa ni palepale lilipojengwa hekalu la kwanza. Na hapo si pengine bali ni eneo lile lile Msikiti wa Al-aqsa ulipo.

Maswali yafuatayo yananyanyuka:

Je! Ni ni kitatokea?..na je huo msikiti utaondolewa kupisha ujenzi wa Hekalu, na kama utaondolewa je utaondolewaje?..na ni lini?.

Jibu ni  kwamba Msikiti ule ni lazima utaondolewa pamoja na ile Kuba ya Mwamba (Dome of Rock)!!, kwasababu Neno la Mungu limeshasema hivyo kwamba Hekalu litajengwa…na Neno la Mungu halijawahi kupita (kilichotabiriwa katika Ezekieli 40-47  kitatimia kama kilivyo), hakuna shaka juu ya hilo, haijalishi ni muda gani utapita!!.. Wakati utakapofika wa unabii huo kutimia msikiti wa Al-Aqsa utaondoka.

Ni kwa njia gani utaondolewa?.. hakuna anayejua kama ni kwa njia ya Amani, au kwa njia nyingine, lakini dunia nzima itatii tu kwasababu ni Bwana ndiye aliyeyasema hayo, na kuyapanga si MTU, wala WATU wala Taifa la Israeli, bali ni MUNGU mwenyewe!!, hivyo hata wakati wa kuondolewa hakuna atakayejisifu kuwa ni nguvu zake, bali Mungu mwenyewe ndiye atakayehusika hapo.

Na dalili zote zinaonyesha kuwa tumekaribia sana hicho kipindi, kwani waisraeli wameshakusanya utajiri mkubwa na utaalamu mwingi, kiasi kwamba endapo ikitokea ukaanza leo, basi hakuna kizuizi chochote cha kifedha wala kiutalaamu.

Na ujenzi huo unauhusiano mkubwa sana na mpinga-Kristo ajaye, ambapo biblia inasema atatafuta kuingia katika hekalu hilo, ili atafute kuabudiwa yeye kama Mungu (2Wathesalonike 2:4), na maandalizi ya mpinga-kristo yapo ukingoni..nafasi yake ipo tayari, kinachongojewa ni parapanda.

HOJA NYINGINE ZISIZO SAHIHI.

  1. Je Muhamad alipaa??..

Je ni kweli Muhamad alipaa, na je ni kweli Qurani ni kitabu cha Mwenyezi Mungu?

Jibu ni la! Hakupaa!!..Kwasababu Biblia inatuambia manabii waliopaa ni wawili tu, Henoko na Eliya.. na BWANA YESU ambaye ndiye Mkuu wa Uzima. Hao ndio waliopaa, na wengine watakaopaa ni watu watakaofufuliwa na kwenda mbinguni siku ya unyakuo, na watakatifu watakaokuwa hai siku ya kurudi kwa Bwana, pamoja na wale manabii wawili waliotajwa katika Ufunuo 11, basi!

Na pia Quran sio kitabu cha mwenyezi Mungu chenye kumfikisha mtu mbinguni. Kinaweza kuwa kitabu chenye baadhi ya maonyo yaliyo sahihi ambayo mtu akiyafuata anaweza kuwa mzuri katika jamii, lakini si kuurithi uzima wa milele…Kwa ujumla kitabu hiko hakina mafundisho ya Uzima wa milele, kwasababu kinamkataa YESU kama NJIA PEKEE ya WOKOVU wa mwadamu.

Na kitabu chochote kisichoelekeza moja kwa moja Uzima wa milele uliopo ndani ya YESU, au  mtu yeyote yule asiyeamini kuwa YESU ndiye BWANA, na Mwokozi, na ndiye njia pekee ya UZIMA, huyo mtu hana uzima wa milele haijalishi atakuwa anafanya mambo mengine yanayoonekana mazuri machoni pa watu, lakini kama hatamwamini Bwana YESU baada ya kumsikia, matendo yake hayo hayatamsaidia chochote, kwasababu hakuna mwanadamu atakayeweza kusimama kwa matendo yake peke yake.

Yohana 3:18 “ Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu”.

Usikose mwendelezo kuhusiana na Kibla ya wanyama na “Kaaba”, na kama wakristo tunaruhusiwa kushiriki vyakula hivyo.. Pia usikose kufuatilia Makala hizi pamoja na nyingine nyingi, juu ya ukweli kuhusiana na Uislamu na Imani nyingine.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Je!Sisi kama wakristo Tunaruhusiwa kuchangia ujenzi wa Imani nyingine?

WEWE NI HEKALU LA MUNGU.

JE! UNA MASIKIO YANAYOSIKIA?

UFUNUO: Mlango wa 11

Je! Wapalestina ni watu gani, na sehemu yao katika biblia ni ipi?

Rudi Nyumbani

Print this post

NIFANYE NINI NIMSHINDE SHETANI?

1) WOKOVU: 

Hilo ndio jambo la kwanza. Kamwe huwezi kumshinda shetani ikiwa upo nje ya Kristo, Ndicho kilichowakuta wale wana wa Skewa, walipotaka kutoa pepo kwa jina la Yesu. Lakini Yule pepo akawaambia Yesu namjua, na Paulo namfahamu, lakini je ninyi ni akina nani?

Matendo 19:13  Baadhi ya Wayahudi wenye kutanga-tanga, nao ni wapunga pepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Nawaapisha kwa Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo.

14  Walikuwako wana saba wa mtu mmoja Skewa, Myahudi, kuhani mkuu, waliofanya hivyo.

15  Yule pepo mchafu akawajibu, akawaambia, Yesu namjua na Paulo namfahamu, lakini ninyi ni nani? 16  Na yule mtu aliyepagawa na pepo mchafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika nyumba ile hali wa uchi na kujeruhiwa.

Wokovu, ni Kristo ndani yako, na kwa huo nguvu za adui zote huyeyuka mara moja. Mtu aliyempokea Yesu, shetani kamwe hamwezi, kwasababu anamwona Kristo ndani yake.

2) MAOMBI: huharibu mipango ya ibilisi.

Unaweza ukawa umeokoka, lakini shetani akapata nguvu za kukusumbua kwa majaribu, kwasababu unashindwa kutumiza baadhi ya wajibu wako kwa mwamini, Yesu alisema..

Mathayo 26:41  Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.

Yesu ijapokuwa alikuwa ni mkamilifu hana dhambi, alijaribiwa na adui, wewe ni nani usikutane na hayo? Usipokuwa mwombaji, uvivu ukakumeza, unaona shida kuomba kila siku, kuhudhuria mikesha ujue tayari upo majaribuni. Hata kama utajiona upo sawa, fahamu tu hapo ulipo kuna eneo Fulani adui anakusumbua, utakuja kugundua pindi utakapoanza kuwa mwombaji. Na ndio maana maisha ya wokovu hayatengwi na maombi. Shetani akimwangalia mwombaji anaona moto umemzunguka mkali, hawezi jiamulia tu kufanya analotaka kwake.

3) KUBALI KUWA MJINGA: Utamweka chini shetani.

Warumi 16:19  Maana utii wenu umewafikilia watu wote; basi nafurahi kwa ajili yenu, lakini nataka ninyi kuwa wenye hekima katika mambo mema, na wajinga katika mambo mabaya. 20  Naye Mungu wa amani atamseta Shetani chini ya miguu yenu upesi. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi. [Amina.]

Hapo anasema tuwe wajinga katika mambo mabaya. Ni nafasi kubwa kwa Mungu kumweka shetani chini ya miguu yetu. Kwamfano, unapokuwa hujui kuhusu mitindo mipya ya kidunia, sio mfuatiliaji wa miziki ya kidunia, muvi mpya mpya zilizotoka duniani, yaani kwa ufupi unapitwa na mambo ya kidunia yasiyokuwa na maana kwako, kinyume chake, unakuwa na ujuzi na hekima katika mambo ya rohoni jua hapo umemshinda shetani kwa sehemu kubwa. Hana kitu kwako, kwasababu bidhaa zake, huna mpango nazo, hununui chochote kwake.  Kuipenda dunia ni kuwa adui wa Mungu, na rafiki wa shetani.

4) WEKA NENO LA MUNGU NDANI: Utamfukuza shetani.

Kuweka Neno sio, kukariri vifungu vingi vya biblia, hapana, bali ni kufahamu “ukweli” (ufunuo)  wa kila Neno unaloliweka moyoni mwako. Pale jangwani, Yesu alipokutana na shetani, alimjaribu kwa Neno hilo hilo,lakini Yesu akamwambia kweli yote ipoje.

Mathayo 4:6  akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; Na mikononi mwao watakuchukua; Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe. 7  Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako.

Ni muhimu ukalifahamu Neno la Mungu katika kweli yake, na hiyo huchangiwa na kufundishwa kwa ufasaha Neno la Mungu na waalimu, kwasababu Roho Mtakatifu atasema na wewe kupitia wao. Lakini pia kumpa Roho Mtakatifu nafasi ya moja kwa moja kukufundisha. Vinginevyo adui atakudanganya sana, hususani kupitia manabii wa uongo, kwasababu hulijui Neno vema.

 5) LITII NENO: Utaweza yastamili majaribu yake yote.

Kulifahamu Neno, na kuijua kweli, ni jambo muhimu lakini bado shetani anaweza pata mianya ya kukunasa endapo hutaweza kulitii Neno. Penda utakatifu, penda kutendea kazi kile unachofundishwa. Yesu alisema, wapo watu wasikiao tu, lakini wapo wasikiao na kuyatendea kazi. Wote hujaribiwa kwa pepo, mafuriko na mvua za shetani. Sasa Yule aliyejijenga  juu ya fundisho tu, na sio kutendea kazi fundisho, ndio huyo anayechukuliwa na mafuriko.

Mathayo 7:26  Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga;

27  mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa.

Mateso mengine huwapata watu kwasababu ya dhambi. Kuishi maisha matakatifu, humnyima adui mlango wa kukushambulia kwa namna yoyote. Liishi Neno.

6) HUBIRI NENO: Utamwangusha adui kutoka juu.

Watu wengi hudharau ushuhudiaji. Tunapokuwa na moyo mmoja wa kuitenda kazi ya Mungu, adui hawezi kukaa juu ya anga hili, kutupinga. Tunalisoma wapi hilo? Utakumbuka wakati ule Bwana alipowatuma wanafunzi  wake wawili wawili kuhubiri, waliporudi kwa furaha, huku wakimwambia Bwana  hata mapepo yanawatii. Yesu akawaambia nalimwona shetani akianguka kutoka juu kama umeme. Kuonyesha kuwa kitendo cha wao kuhubiri adui alikuwa anaporomoka kwa kasi sana.

Mathayo 10:17  Ndipo wale sabini waliporudi kwa furaha, wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako. 18  Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme.

Hivyo ukizingatia mambo  hayo sita (6), Utakuwa sio tu umemdhibiti adui kila Nyanja, bali pia umemteka. Ni wajibu wako mimi na wewe kuboresha mahali ambapo hapako sawa, ili kwa pamoja tukaujenge ufalme wa Mungu na kuziangusha kazi za shetani.

Yakobo 4:7  Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

ZIFAHAMU KAZI KUU (10) ZA SHETANI DUNIANI.

YAFUATAYO NI MAWAZO YA ADUI HIVYO USIYASIKILIZE.

USIWE ADUI WA BWANA

Rudi Nyumbani

Print this post

Ijapokuwa amekufa, angali akinena(Waebrania 11:4)

SWALI: Maandiko yanaposema Habili ijapokuwa amekufa angali akinena, je! Ananenaje, wakati yeye ni marehemu. Je! Hiyo inamaana wazee wetu wa zamani wanaweza kunena na sisi?

Waebrani 11:4  Kwa imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini; kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo, ijapokuwa amekufa, angali akinena


JIBU: Kibiblia ni kweli kabisa watakatifu waliokufa kale hunena nasi. Lakini kunena kwao ni tofauti na huku kunakodhaniwa, kwamba mzimu unakutokea kwenye ndoto, au unasikia sauti ya petro makaburini ikizungumza na wewe,  Hapana, ukiona hivyo ujue huzungumzi na huyo mtu, bali ni pepo.

Sasa watakatifu waliokufa wanazungumzaje na sisi?

Ni kwa ushuhuda waliouacha. Maisha yao na maagizo yao, ndio huzungumza nasi, sikuzote, kana kwamba tupo nao sasa, kwa mafundisho yao yaliyopo  mpaka sasa kana kwamba tunawaona wenyewe kumbe wamekufa.

Ndio maana ile habari ya Yule tajiri wa Lazaro, tunaambiwa alipofika kule kuzimu akaomba mtu atolewe kwa wafu awahubirie injili, akakataliwa, kuonyesha kuwa hakuna mtu aliyekufa mwenye uwezo wa  kuja tena kuzungumza na sisi, nafasi hiyo haipo kwao. Lakini waliambiwa WANAO MUSA NA MANABII, WAWASIKILIZE.

Luka 16:29  Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.

Maana yake ni kuwa sio kwamba Musa kweli alikuwepo duniani, au manabii wa kale kama Isaya walikuwa duniani kwa wakati huo, anaambiwa hayo maneno. Lakini shuhuda zao na mahubiri yao, huwawakilisha wao. Tunaweza kusema “ijapokuwa wamekufa wangali wakinena”

Ndivyo ilivyo kwa Habili, ijapokuwa aliuliwa na ndugu yake, lakini IMANI yake inasema nasi mpaka leo. Mitume wa Kristo ijapokuwa hawapo duniani lakini sauti zao tunazisikia hadi sasa.

Lakini pia kuna mahali pengine biblia inasema damu ya Yesu hunena mema kuliko ya Habili (Waebrania 12:24). Kufahamu kwa kina damu ya mtakatifu  hunenaje? Pitia somo hili. >>> DAMU YA ZAKARI BIN BARAKIA.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

JE! Kaini alimpatia mke wake wapi?

KUOTA MTU AMEKUFA/NDUGU AMEKUFA.

ALIPOKUWA ANGALI MBALI, BABA YAKE ALIMWONA.

Rudi Nyumbani

Print this post

TABIA SITA (6) ZA WANAFUNZI WA YESU.

Zifuatazo ni baadhi ya tabia za kuigwa walizokuwa nazo wanafunzi wa Bwana YESU ambazo nasi tunapaswa tuzionyeshe.

1. WALIJIKANA NAFSI ZAO.

Hii ni sifa ya kwanza waliyokuwa nayo wanafunzi wa YESU, Kwani mtu aliyekosa hii sifa hakuweza kuwa mwanafunzi wake.

Luka 14:27 “Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu”.

Halikadhalika na sisi kama wanafunzi wa Bwana ni sharti tujikane nafsi kila siku, na kubeba msalaba. (Zingatia hilo neno, “Kila siku”), na si siku moja tu..

Luka 9:23 “Akawaambia wote, Mtu yeyote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate”.

2. WALIKAA KUFUNDISHWA NA BWANA.

Maana ya kuwa mwanafunzi ni kuketi na kufundishwa mpaka kuhitimu. Na wanafunzi wa Bwana YESU walilijua hilo, hivyo walikuwa walijiunga na chuo hicho cha Bwana ili kupokea mafunzo.

Na leo ni hivyo hivyo, Mwalimu wetu ni ROHO MTAKATIFU na chuo chetu ni Biblia. Na kila mtu ni lazima apite chini ya chuo hicho, ili aweze kuwa mwanafunzi wa Bwana.

3. WALIMFUATA BWANA KILA ALIKOKWENDA.

Maisha ya Bwana YESU hayakuhusisha kukaa mahali pamoja, bali kuzunguka huku na kule, katika miji na vijiji kuhubiri injili.

Mathayo 9:35 “Naye Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina”.

Hata wanafunzi wasomao chuo, upo wakati wanaenda katika mafunzo kwa njia ya vitendo kabla ya kuhitimu (maarufu kama mafunzo ya field).

Na vivyo hivyo na sisi kama wanafunzi  ni lazima tuifanye kazi ya Bwana kwa yale tuliyoyapokea hata kama hatubobea katika hayo..

Lakini utaona leo, mtu hataki kuwahubiria wengine kwa hofu ya kwamba yeye hajui….Ni kweli usifundishe usichokijua lakini kile kidogo ambacho umeshakijua, usikifukie chini bali kawape wengine wasiokijua kabisa.

4. WALIMTII BWANA.

Tabia nyingine ya mwanafunzi Halisi ni UTII na NIDHAMU.

Wanafunzi wa Bwana YESU wale 11 walimtii Bwana kwakila jambo, kuanzia maagizo ya ubatizo, kuhubiri, meza ya Bwana na mengineyo.

Na wote walimwogopa Bwana (hakuna aliyedhubutu kuhojiana naye wala kushindana naye) Luka 9:45.

5. WALIMWAMINI BWANA.

Wanafunzi halisi wa Bwana YESU hawakuwa na mashaka mashaka na Bwana YESU…walimwamini moja kwa moja…

Yohana 2:11 “Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko Kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini”

6. WALIMVUMILIA BWANA

Hata kama yalikuwepo mambo ambayo yalikuwa ni magumu kueleweka kwa katika hali yao.ya uchanga…lakini walivumilia wakiamini siku moja watakuja kuelewa vizuri..

Yohana 6:67 “Basi Yesu akawaambia wale Thenashara, Je! Ninyi nanyi mwataka kuondoka?

68 Basi Simoni Petro akamjibu, Bwana! Twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele.”

Na sisi kama wanafunzi wa YESU hatupaswi kurudi nyuma,  tunapokutana na mambo tusiyoyaelewa katika imani au maandiko..badala yake tunapaswa kuwa wavumilivu kwa matumaini mazuri yajayo.

Na kumbuka maana ya kuwa MRISTO ni kuwa MWANAFUNZI…Huwezi kusema ni mkristo na sio mwanafunzi.

Matendo ya Mitume 11:26 “hata alipokwisha kumwona akamleta Antiokia. Ikawa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. Na wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza hapo ANTIOKIA”.

BWANA ATUSAIDIE.

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

NINI MAANA YA KUWA MKRISTO?

Chuo cha vita vya Bwana ni kipi?(Hesabu 21:14)

HAWEZI KUWA MWANAFUNZI WANGU.

MPENDEZE MUNGU ZAIDI.

USIISHIE KUTAZAMA JUU, ENDELEA MBELE.

Rudi Nyumbani

Print this post

NDOA TAKATIFU NI MKE MMOJA/MUME MMOJA.

Ndoa za wake wengi ni za ibilisi!..ndoa za wake wengi ni za ibilisi!!… ndoa za wake wengi ni za ibilisi!!!. Hali kadhalika ndoa za waume wengi ni za ibilisi, kama tu zilivyo za jinsi moja (zote ni zao la ibilisi).

Zipo hoja kuwa kwasababu Daudi, Sulemani na manabii wengine wakale walioa wake wengi, basi hata leo ni halali kuoa wake wengi.. tena zipo hoja zifananishazo wanyama wa porini na wa kufungwa na uhalali wa kuoa wake wengi.

Hoja zote hizi ni za ibilisi… Ndugu, usiongeze wake, wala wala usiongezee waume.

Bwana YESU alipokutana na yule mwanamke Msamaria kisimani hakumwambia akawalete WAUME ZAKE!.. Ingawa alikuwa ana wanaume wengi (na Bwana alilijua hilo), lakini alimwambia nenda “kamlete mumeo”… ikimaanisha kuwa ndoa halali na takatifu ni ya mume mmoja na mke mmoja.

Sasa Kristo alikuwa anamjua Sulemani, na Daudi..

Yohana 4:15 “Yule mwanamke akamwambia, Bwana, unipe maji hayo, nisione kiu, wala nisije hapa kuteka.

16  Yesu akamwambia, NENDA KAMWITE MUMEO, uje naye hapa.

17  Yule mwanamke akajibu, akasema, Sina mume. Yesu akamwambia, Umesema vema, Sina mume;

18  kwa maana umekuwa na waume watano, naye uliye naye sasa siye mume wako; hapo umesema kweli”.

Bwana YESU kabla ya kukutana na huyu mama, alikuwa anamjua Daudi pamoja na Sulemani na idadi ya wake wake waliooa!.. Lakini tunaona hakumwambia huyu mwanamke Msamaria, kwamba akawalete waume zake!!.. Bali alimwambia kamlete mumeo! (maana yake mmoja tu).. bado huoni tu, kuwa ndoa za mitara ni batili na za ibilisi!.

Na tena biblia inasema hapo Mwanzo Mungu alimwumba mwanaume na mwanamke, na si mwanaume na wanawake, au mwanamke na wanaume (soma Mwanzo 1:27 na Mathayo 19:4).

Huoni kuwa ndoa hizo za wake wengi zitakukosesha maji ya uzima!.. Na pia fahamu kuwa ndoa za wake wengi sio zile tu zinazohusisha mtu kuwa na wake wengi katika boma moja kwa wakati mmoja…la! Hata zile za kuacha na kuoa mwingine ilihali yule wa kwanza bado yupo hai.. hiyo ni mitara! Ndicho kilichokuwa kwa huyu mwanamke Msamaria.

Huyu mwanamke msamaria alikuwa na wanaume watano kulingana na darubini ya kimbingu! Ingawa haishi nao, lakini alikuwa nao watano, na anayeishi naye ni wa 6, vile vile kuna watu leo hii wamecha wake zao na kuoa wengine, na kuacha tena na kuoa wengine, (hawa hawana tofauti na wale waliooa wake wawili na kuishi nao wote kwa pamoja).

Na madhara ya ndoa za mitara ni “KUKOSA MAJI YA UZIMA”..

Yapo maji ya Uzima tuyanywayo hapa Duniani, na yapo yale tutakayoyanywa katika mbingu mpya na nchi mpya.

Maji ya Uzima duniani ni YESU KRISTO, tumpatapo yeye tunapata uzima wa milele (Yohana 4:14), lakini ukijiunganisha na hizi ndoa za mitara hawezi kuingia ndani yako!.. vile vile maji ya uzima baada ya maisha haya tutayanywa kutoka katika ule mto wa maji ya Uzima katika mbingu mpya na nchi mpya.

Ufunuo 22:1 “Kisha akanionyesha mto wa maji ya uzima, wenye kung’aa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana-Kondoo,

2  katikati ya njia kuu yake. Na upande huu na upande huu wa ule mto, ulikuwapo mti wa uzima, uzaao matunda, aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa.

3  Wala hapatakuwa na laana yo yote tena. Na kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-Kondoo kitakuwamo ndani yake. Na watumwa wake watamtumikia;

4  nao watamwona uso wake, na jina lake litakuwa katika vipaji vya nyuso zao.

5  Wala hapatakuwa na usiku tena; wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu huwatia nuru, nao watatawala hata milele na milele”.

Neema ya Bwana YESU itufunike.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

MAFUNDISHO YA NDOA.

MISTARI YA BIBLIA KUHUSU NDOA.

VIGEZO VYA KUWA KARIBU NA YESU KRISTO KATIKA ULIMWENGU UJAO.

NDOA NI NINI?

KUWA NA  MAFUTA YOTE YA ROHO MTAKATIFU NDANI YAKO.

Rudi Nyumbani

Print this post

FUNDISHO LA BWANA JUU YA KUZALIWA MARA YA PILI.

Jina la BWANA wetu YESU KRISTO libarikiwe, karibu tujifunze biblia neno la Mungu wetu ambalo ni Taa na Mwanga wa njia yetu (Zab.119:105).

Hebu tuangalie uzito wa kuzaliwa mara ya pili kupitia maneno ya BWANA WETU YESU KRISTO.

Yohana 3:1 “Basi palikuwa na mtu mmoja wa Mafarisayo, jina lake Nikodemo, mkuu wa Wayahudi.

2  Huyo alimjia usiku, akamwambia, RABI, TWAJUA YA KUWA U MWALIMU, UMETOKA KWA MUNGU; KWA MAANA HAKUNA MTU AWEZAYE KUZIFANYA ISHARA HIZI UZIFANYAZO WEWE, ISIPOKUWA MUNGU YU PAMOJA NAYE.

3  Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.

4  Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?

5  Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, MTU ASIPOZALIWA KWA MAJI NA KWA ROHO, HAWEZI KUUINGIA UFALME WA MUNGU”.

Hapa Nekodemo anataja vigezo vya Mtu kuwa na MUNGU kuwa ni “Ishara azifanyazo”…na anamthibitisha Bwana kwa ishara hizo, lakini Bwana anamrekebisha, kuwa “MTU asipozaliwa mara ya pili hawezi kuurithi ufalme wa Mungu (maana yake hawezi kuwa na MUNGU)”… Je! na sisi leo tunalijua hilo??????….Je unalijua hilo??? .

Nikodemo anaona ISHARA ni tiketi ya kuwa na MUNGU,… Bwana YESU anataja KUZALIWA MARA YA PILI ndio TIKETI.. Sasa tuchukue ya nani tuache ya nani?.. Bila Shaka maneno ya BWANA YESU ni hakika, na tena ndio uzima.

Ndugu haijalishi tutakuwa na uwezo wa kufanya miujiza mingi na mikubwa kiasi gani, kama HATUJAZALIWA MARA YA PILI (Maana yake kwa maji na kwa Roho) hatuwezi kuwa na Mungu, kutembea naye wala hatutamwona siku ile.

Mtu anapozaliwa mara ya pili anakuwa kiumbe kipya, maana yake yale maisha ya kwanza ya dhambi yanakuwa hayapo tena maishani mwake.

Kuzaliwa kwa maji ni Ubatizo wa Maji mengi na kwa jina la Bwana YESU na kuzaliwa kwa Roho ni ubatizo wa Roho Mtakatifu (Matendo 2:37-38), mambo haya ndiyo yanamkamilisha mtu baada ya kutubu.

Na anayetuzaa mara ya si mtu bali ni Mungu mwenyewe, na Mungu ni Roho (sawasawa na Yohana 4:24), na tunapozaliwa na Roho, basi tunakuwa watu wa rohoni.

Yohana 3:6 “Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho”

Na kuwa mtu wa rohoni, si kuona maono, au mapepo, bali ni kuzaliwa katika Roho, na Maji. Na sifa kuu ya mtu wa rohoni ni kuushinda ulimwengu (dhambi na mambo mengine ya kidunia).

1Yohana 5:4  “Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu”.

Soma pia 1Yohana 3:9 na 1Yohana 5:18.

Hivyo ukiona tamaa za kidunia bado zinakusumbua kuna uwezekano kuwa bado hujazaliwa mara ya pili, kwasababu wote waliozaliwa mara ya pili wanayo nguvu ndani yao ya kuushinda ulimwengu na ndio watu wa rohoni.

Je ishara ni uthibitisho wa mtu kuwa na Mungu??..jibu ni ndio!, lakini si uthibitisho wa kwanza… bali uthibithsho wa kwanza wa mtu kuwa na Mungu ni KUZALIWA MARA YA PILI. Kwasababu wapo watakaotenda miujiza na kufanya ishara nyingi lakini wasimwone Bwana siku ile sawasawa na Mathayo 7:22.

Kwahiyo kilicho cha msingi kuliko vyote ni “KUZALIWA MARA YA PILI (kuwa kiumbe kipya)”  na mengine ndio yafuate.

Wagalatia 6:15 “Kwa sababu kutahiriwa si kitu, wala kutokutahiriwa, bali kiumbe kipya“.

1Petro 1:23 “Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele”.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

FUNDISHO KUU LA NEEMA YA MUNGU KWETU.

JE! SISI KAMA WAKRISTO NI DHAMBI KUSHEHEREKEA KRISMASI?.

UMUHIMU WA KUZALIWA MARA YA PILI.

VITA VYA KIFIKRA BAADA YA KUZALIWA MARA YA PILI

KWANINI YESU NI ADAMU WA PILI?

Rudi Nyumbani

Print this post

Matangamano ni nini? (Isaya 13:10)

Jibu: Turejee…

Isaya 13:10 “Maana nyota za mbinguni na MATANGAMANO havitatoa nuru yake; jua litatiwa giza wakati wa kucha kwake, na mwezi utaacha nuru yake isiangaze

 “Matangamano” ni “Mkusanyiko wa nyota” unaoonekana na kutengeneza umbile Fulani. Wanajimu baadhi wameyataja matangamano hayo kwa maumbile ya wanyama mbali mbali, kwamfano lipo kundi moja wamelitaja kuwa na umbile kama la N’ge, lingine kama Dubu, lingine kama Simba, lingine mapacha n.k

Kwamfano kundi la nyota lenye umbile kama la Ng’e jinsi linavyoonekana mbinguni kwa macho ya damu na nyama ni kama linavyoonekana kwenye picha hapo juu.. Lakini kwa jinsi lilivyounganishwa na wanajibu mpaka kuleta umbo kama la Ng’e ni kama inavyoonekana hapa chini..

Matangamano ni nini?

Na makundi haya ya nyota, sasa yanatumika kwa unajibu (ambayo ni elimu ya shetani asilimia mia) kwaajili ya utambuzi wa majira na nyakati za watu, Elimu hii kwa jina lingine inaitwa FALAKI, Fungua hapa kwa maelezo Zaidi >>>Falaki ni elimu gani? (Isaya 47:13).

Elimu hii wanajimu wanaitumia kutabiri mambo yajayo juu ya mtu, ndio hapo mtu anaenda kusomewa nyota yake na kufanyiwa utabiri, jambo ambalo kiuhalisia ni elimu ya giza, mtu yule anakuwa haambiwi mambo yajayo bali anapangiwa mambo yajayo na ibilisi, akidhani ndio katabiriwa.

Sasa Elimu hizi za Falaki pamoja na ibada zote za jua na mwezi na sayari, Bwana Mungu kazilaani, na siku za mwisho Jua, na mwezi vitatiwa giza, na Nyota zote za mbinguni zitaanguka na Matangamano yote yatazima.. kuonyesha kuwa mambo hayo yaliyotukuka kwa wanadamu si kitu mbele za Mungu, na Bwana atawaadhibu waovu pamoja na ulimwengu, ndivyo maandiko yasemavyo.

Isaya 13:9 “Tazama, siku ya Bwana inakuja, siku kali, ya hasira na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake.

10 Maana nyota za mbinguni na MATANGAMANO havitatoa nuru yake; jua litatiwa giza wakati wa kucha kwake, na mwezi utaacha nuru yake isiangaze.

11 Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayaangusha chini majivuno yao walio wakali”.

Kuhusiana na unabii wa kufutwa kwa Mwezi, nyota na sayari zote siku za mwisho pitia maandiko haya Yoeli 3:15, Marko 13:24,  Mathayo 24:29, na Ufunuo 6:12.

Kwahiyo ndugu usiende kusoma gazeti kwa lengo la kutafuta utabiri wa nyota, ni machukizo kwa Bwana, usiende kwa waganga ili wakakusafishie nyota, kinyume chake ndio unaenda kuharibu maisha yako, badala yake mfuate Bwana YESU naye atayasafisha maisha yako.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

MKUU WA GIZA.

UMEFUNGWA KATIKA GIZA NA UVULI WA MAUTI?

MKUU WA GIZA.

Kwanini Mungu aliupenda ulimwengu?

AGIZO LA UTUME.

Rudi Nyumbani

Print this post

FAHAMU KANUNI ZA KUZISUBIRIA AHADI ZA MUNGU?

Mungu anaweza kuahidi, lakini kama hujui kanuni za kusubiria ahadi za Mungu unaweza usipokee lolote. Kila mmoja wetu amestahili kupokea lolote analo mwomba Mungu endapo ameomba sawasawa na mapenzi yake (yaani sio kwa matumizi mabaya). Yawezekana wewe umeomba Bwana akupe kazi, akupe mke/mume bora, akuponye ugonjwa wako, aikuze  karama yako n.k.

Sasa mahitaji kama hayo na mengine yoyote. Mungu alisema kwenye Neno lake, atatupatia (1Yohana 5:14). Na hivyo inakuwa kwake ni ahadi ambayo lazima aitimize. Kwahiyo wewe unachopaswa kufanya ni kusubiri tu. Kuzingojea hizo ahadi za Mungu kwasababu ni lazima zije. Jifunze tu kungojea.

Maombolezo 3:25 Bwana ni mwema kwa hao wamngojeao, Kwa hiyo nafsi imtafutayo.  26 Ni vema mtu autarajie wokovu wa Bwana Na kumngojea kwa utulivu

Sasa unazingojea katika mazingira gani?. Hapo ndipo unapopaswa ujue.

Embu tuangalie kwa mtu mmoja ambaye aliahidiwa jambo na Mungu. Na hivyo alikuwa katika mazingira gani, mpaka akalipokea. Mtu mwenyewe si mwingine zaidi ya Simeoni.

Tusome.

Luka 2:25  Na tazama, pale Yerusalemu palikuwa na mtu, jina lake Simeoni, NAYE NI MTU MWENYE HAKI, MCHA MUNGU, AKIITARAJIA FARAJA YA ISRAELI; na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake.

26  Naye alikuwa ameonywa na Roho Mtakatifu ya kwamba hataona mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana.

27  Basi akaja hekaluni ameongozwa na Roho; na wale wazazi walipomleta mtoto Yesu ndani, ili wamfanyie kama ilivyokuwa desturi ya sheria,

28  yeye mwenyewe alimpokea mikononi mwake, akamshukuru Mungu, akisema,

29  Sasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako, Kwa amani, kama ulivyosema;

30  Kwa kuwa macho yangu yameuona wokovu wako,

31  Uliouweka tayari machoni pa watu wote;

Wengi wetu tukimtafakari Simeoni, tunatengeneza picha ya mtu Fulani, mzee aliyekuwa anamngoja Mungu tangu ujana wake hadi uzee atimiziwe ahadi yake. Lakini biblia haituelezi katika picha hiyo, inatueleza alikuwa ni “mtu mwenye haki mcha Mungu”. Na tazamio lake lilikuwa ni kuona mkombozi anakuja duniani, Mungu akasikia kiu yake, ndipo akamwambia utamwona.

Ni jambo gani unapaswa ujue?

Kungojea ahadi za Mungu sio tu kusema  ‘Bwana naomba hiki au kile’. Hapana, ni pamoja na kutembea katika haki na kumcha Mungu. Simoni alikuwa hivyo, hakuwa mtu anayetarajia jibu lake, huku anaendelea na udunia kama wengine, huku anaendelea ni anasa kama wanadamu  wengine, huku anaendelea ni uzinzi kama wapagani.

Alidumu muda wote, kuyalea maono aliyoonyeshwa na Mungu, katika hofu ya Kristo. Ndipo wakati ulipofika akaona alichokuwa akikitarajia.

Palilia maono yako uliyomwomba Mungu akutimizie/ au aliyokuonyesha, kwa kutembea ndani ya Kristo. Mche Mungu, kuwa mtu wa rohoni uliyejazwa Roho kama Simoni, tembea katika usafi wa Kristo, kataa udunia, na maisha ya kipagani, kuwa mwombaji.

Ni hakika hilo ulilomwomba Bwana utaliona tu, baada ya wakati Fulani, haijalishi ni gumu/zito kiasi gani, au limepitiliza muda kiasi gani. Utalipokea tu, katika ubora ambao hukuutegemea.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

PALE AHADI ZA MUNGU ZINAPOKUJARIBU.

ZIJUE TABIA ZA AHADI ZA MUNGU KWA MWAMINIO.

KANUNI JUU YA KANUNI.

Rudi Nyumbani

Print this post

USIPENDE USINGIZI USIJE UKAWA  MASKINI.

Mithali 20:13 “Usipende usingizi usije ukawa maskini; Fumbua macho yako nawe utashiba chakula”.

Usingizi unaozidi unachelewesha utekelezaji wa majukumu ya muhimu. Kwamfano Mwanafunzi anayelala kupita kiasi ni lazima atakuwa mchelewaji wa shule, vilevile mfanyakazi alalaye kupita kiasi ni lazima atakuwa mchelewaji wa kazini, mfanya biashara anayealala kupita kiasi ni lazima atachelewa kuanza biashara  yake.

Upo usemi usemao “biashara ni asubuhi” maana yake kwa mtu anayefanya biashara labda ya kuuza duka, asubuhi ndio wakati wa kufungua bishara maana watu wengi wanawahi kutafuta bidhaa asubuhi Zaidi ya mchana, hivyo alalapo sana hatapata zile faida za asubuhi, na hivyo yupo hatarini kufilisika.

Atapanga kweli kuwahi kuamka mapema kesho, lakini ifikapo asubuhi kitanda kinakuwa na nguvu kuliko maamuzi yake, atajiongezea muda wa kulala, na mwisho wa siku atashtukia kumeshapambazuka na jua linawaka..na hayo ni matokeo ya kusema “bado kulala kidogo”.

Mithali 6: 9 “Ewe mvivu, utalala hata lini? Utaondoka lini katika usingizi wako?

10 Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi!

11 Hivyo umaskini wako huja kama mnyang’anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha”.

Sasa biblia ni kitabu kilichojaa hekima ya kumwongoza mtu hata katika maisha ya kawaida Zaidi yay ale ya rohoni…. ni kitabu kilichojaa mafunzo mengi mema yahusuyo kanuni za kimaisha na kitabu cha Mithali kimejaa mafunzo hayo.

Hivyo biblia inatufundisha wakristo tuwe na kiasi katika kulala, kwani usingizi unaozidi una matokeo mabaya.. Si kila changamoto inasababishwa na “wachawi”….. nyingine zinatokana na tabia zetu wenyewe.., na hivyo biblia inatufundisha jinsi ya kuepukana nazo, kwamba ni kubadili tu mienendo.

Maana yake ni kwamba, tukitaka kuepukana na “umasikini”  kanuni sio tu “kufunga na kuomba” bali pia ni KUTOUPENDA USINGIZI!. Ukifunga na kuomba na huku unaendekeza usingizi kupita kiasi hakuna matokeo yoyote utakayoyaona.

Maana yake kama ni mfanyakazi basi usiwe mtu wa kupenda kulala mno..Ni kweli hatuwezi kuacha kulala kabisa, lakini kusizidi mipaka, kwani usingizi uliozidi ni zao la ibilisi.

Mithali 19:15 “Uvivu humtia mtu katika usingizi mzito; Na nafsi yake mvivu itaona njaa”

Lakini pia kiroho hatupaswi kulala kabisa, kwani usingizi wa kiroho matokeo yake ni mabaya kuliko ule wa kimwili.. Matendo yote ya giza mtu ayafanyayo ni matokeo ya usingizi wa kiroho..

Mtu anayefanya uzinzi, uasherati, anayelewa pombe, anayeiba, anayetukana, anayesengenya…huyo macho yake yamefumba kwa usingizi mzito.

Je na wewe umo miongoni mwa waliolala kiroho? Basi huu si wakati wa kuendelea kulala, bali wa kuamka na kuyaacha matendo ya giza.

Warumi 13:11 “Naam, tukiujua wakati, kwamba SAA YA KUAMKA KATIKA USINGIZI imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini

12  USIKU UMEENDELEA SANA, mchana umekaribia, basi na tuyavue matendo ya giza, na kuzivaa silaha za nuru.

13  Kama ilivyohusika na mchana na tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu”

Waefeso 5:14 “ Hivyo husema, Amka, wewe usinziaye, Ufufuke katika wafu, Na Kristo atakuangaza

15 Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima;

16  mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu”.

Bwana atubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.

SABATO ILIFANYIKA KWAAJILI YA MWANADAMU NA SI MWANADAMU KWAAJILI YA SABATO!

ROHO I RADHI, LAKINI MWILI NI DHAIFU.

NYOTA YA ASUBUHI.

Nini maana ya usijiongezee hekima mno? (Mhubiri 7:16b)

Rudi Nyumbani

Print this post

USIPINDUE MAMBO

Masomo maalumu kwa wahubiri.

Isaya 29:16 “NINYI MNAPINDUA MAMBO; Je! Mfinyanzi ahesabiwe kuwa kama udongo; kitu kilichofinyangwa kimnene yeye aliyekifinyanga, Hakunifinyanga huyu; au kitu kilichoumbwa kimnene yeye aliyekiumba, Yeye hana ufahamu?”

Kama Mtumishi/Mhubiri jihadhari na MAPINDUZI yasiyo na msingi!.

USIIPINDUE INJILI YA KRISTO KWASABABU YA TAMAA YA FEDHA.

Unapoanza kuwadanganya watu wa wenye nia ya kumtafuta Mungu, ili tu upate fedha kutoka kwao!.. unapoanza kuwatumainisha watu wa Mungu mambo ya uongo ili tu uwatoe fedha!.. Hiyo ni ishara mbaya na hatari kubwa sana kwako!. Bwana ataenda kukupindua nawe pia!.

Tito 1:11 “Hao WANAPINDUA watu wa nyumba nzima, wakifundisha yasiyowapasa kwa ajili ya mapato ya aibu”.

Ukilipindua Neno la Mungu na kuanza kufanya biashara katika nyumba ya Mungu (ambayo ni wewe mwili wako sawasawa na 1Wakorintho 3:16) kwa kuanza kufanya uasherati na uzinzi na ukahaba fahamu kuwa Bwana naye atakupindua (Soma 1Wakoritho 6:19).

Ukilipindua Neno la Mungu kwa kuiharibu nyumba yake (kama jengo) kwa kuanza kufanya biashara ndani yake na kufanya yasiyofaa Bwana YESU atazipindua meza zako (soma Mathayo 21:12)

Ukilipindua Neno la Mungu juu ya utakatifu wa mwilini na rohoni (sawasawa na 1Wathesalonike 5:23) na kuanza kufundisha/ kuhubiri kuwa Mungu haangalii mwili bali anaangalia roho tu peke yake ni kupindua maandiko ambako matokeo yake ni Mungu kuyapindua maneno yako na wewe kwa ujumla.

Mithali 22: 12 “Macho ya Bwana humhifadhi mwenye maarifa; Bali HUYAPINDUA MANENO YA MTU HAINI”

Ukilipindua Neno la Mungu na kuanza kuhubiri kuwa  YESU KRISTO bado sana arudi, au kwamba hakuna mwisho wa dunia, huko ni kupindua mambo ambako matokeo yake ni mabaya kama ya Fileto na Himenayo.

2Timotheo 2:17 “na neno lao litaenea kama donda-ndugu. Miongoni mwa hao wamo Himenayo na Fileto,

18  walioikosa ile kweli, wakisema ya kwamba kiyama imekwisha kuwapo, hata KUIPINDUA imani ya watu kadha wa kadha”.

Kama Mhubiri Ni heri KUPINDUA ulimwengu kwa mambo ya kweli ya INJILI kama walivyofanya Mitume wa kanisa la kwanza  kuliko kuigeuza/kuipindua injili kwa faida zetu wenyewe.

Matendo 17:6 “na walipowakosa, wakamkokota Yasoni na baadhi ya ndugu mbele ya wakubwa wa mji, wakipiga kelele, wakisema, Watu hawa WALIOUPINDUA ULIMWENGU WAMEFIKA huku nako”

Siku ya Mapinduzi makuu inakuja, ambapo Bwana ataipindua dunia yote kama alivyoipindua miji ya Sodoma na Gomora (soma Kumbukumbu 29:23) na kipindi cha gharika ya Nuhu (Soma Ayubu 12:15).

Ezekieli 21:27 “NITAKIPINDUA, NITAKIPINDUA, NITAKIPINDUA; hiki nacho hakitakuwa tena, hata atakapokuja yeye ambaye ni haki yake; nami nitampa”

Hegai 2:22 “nami nitakipindua kiti cha enzi cha falme, nami nitaziharibu nguvu za falme za mataifa; nami nitayapindua magari, na hao wapandao ndani yake; farasi na hao wawapandao wataanguka chini; kila mtu kwa upanga wa ndugu yake”.

Usipindue Mambo yaliyonyooka, bali pindua yale yaliyopotoka.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

VIJANA NA MAHUSIANO.

MWISHO WA HAO WAMSAHAUO MUNGU.

IMANI “MAMA” NI IPI?

NJIA KUU YA KUINGIA KATIKA ULE MJI.

JINSI YA KUPOKEA UPONYAJI, TUNAPOMWOMBA BWANA ATUGUSE MARA YA PILI.

Rudi Nyumbani

Print this post