IFAHAMU KANUNI YA KUTAKA NA KUPATA.

IFAHAMU KANUNI YA KUTAKA NA KUPATA.

Warumi 7:18  “Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa KUTAKA NATAKA, bali KUTENDA LILILO JEMA SIPATI.

19  Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo”.

Je na wewe ni miongoni mwa watu wanaosumbuliwa na utumwa wa namna hiyo?.. UNATAKA na kutamani lakini unajikuta HUPATI au HUWEZI au HUFANYI au HUPOKEI?.

> Unataka kumtumikia Mungu lakini unajikuta huwezi..

> Unataka kuwa msomaji wa Neno lakini unajikuta hufanikiwi.

> Unataka na kutamani kufanya mema na mazuri kwaajili ya Mungu wako lakini hufanikiwi n.k

Kama UMETAKA mambo mengi na huoni uelekeo wa kulipata, basi huwenda NJIA unayoitumia kutaka na kutafuta hayo mambo ina kasoro..

Hebu jaribu njia hii, ya kutaka mambo halafu uone kama hutapata uyatakayo,

Na njia hii si nyingine Zaidi ya ile aliyoitumia Danieli.

Danieli 9:3 “Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ILI KUTAKA kwa MAOMBI, NA DUA, PAMOJA NA KUFUNGA, NA KUVAA NGUO ZA MAGUNIA NA MAJIVU. 

4 Nikamwomba Bwana, Mungu wangu, nikaungama, nikasema, Ee Bwana, Mungu mkuu, mwenye kutisha, ashikaye maagano na rehema kwao wampendao, na kuzishika amri zake”

Umeona kanuni Danieli aliyoitumia??… HAKUTAKA mambo kwa kupiga ramli, au kwenda kwa waganga wa kienyeji, wala kwa kwenda Kuwadhulumu watu au kukorofishana na watu au kula rushwa, au kujipendekeza kwa watu bali KWA MAOMBI, NA DUA NA KUFUNGA NA KUVAA NGUO ZA MAGUNIA NA MAJIVU, na matokeo yake alipata alichokuwa anakitafuta..

Na sisi tunajifunza mambo hayo hayo…

> Tukitaka Amani nyumbani.. kanuni ni hiyo > Kufunga na Kuomba.

> Tukitaka Amani katika ndoa.. Kanuni ni hiyo > Kufunga na Kuomba.

> Tukitaka Amani kazini.. Kanuni ni hiyo > Kufunga na Kuomba.

> Tukitaka Akili darasani.. Kanuni ni hiyo > Kufunga na Kuomba.

> Tukitaka Ulinzi na afya.. Kanuni ni hiyo > Kufunga na Kuomba.

> Tukitaka Ujazo wa Roho Mtakatifu.. Kanuni ni hiyo > Kufunga na Kuomba.

Luka 11:13 “Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?”

Kama Bwana YESU alivyosema kuwa “kuna mambo hayawezekaniki, isipokuwa kwa kufunga na kuomba”

Wafilipi 2:13 “Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, KUTAKA KWENU na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.

14  Yatendeni mambo yote pasipo manung’uniko wala mashindano”

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

KANUNI JUU YA KANUNI.

NJIA SAHIHI YA KUFUNGA.

MAMBO MENGINE HAYATOKI ISIPOKUWA KWA KUFUNGA.

Nini maana ya “Heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi”?

HIZI NI NYAKATI ZA KUFUNGA NA KUOMBA.

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments