Nanyi mtamweka hata siku ya kumi na nne ya mwezi ule ule(Kutoka 12:4)

Nanyi mtamweka hata siku ya kumi na nne ya mwezi ule ule(Kutoka 12:4)

SWALI: Bwana yesu apewe sifa, Naomba kufahamu, Kwanini Wana wa Israeli walimuhifadhi mwana-kondoo siku nne kabla ya kuchinjwa katika sikukuu ya pasaka.Je Kuna ufunuo gani tunaweza kupata katika Tendo hilo (Kutoka 12:6)


JIBU: Tusome..

Kutoka 12:3-7

[3]Semeni na mkutano wote wa Israeli, mkawaambie, Siku ya kumi ya mwezi huu kila mtu atatwaa mwana-kondoo, kwa hesabu ya nyumba ya baba zao, mwana-kondoo kwa watu wa nyumba moja;

[4]na ikiwa watu wa nyumba ni wachache kwa mwana-kondoo, basi yeye na jirani yake aliye karibu na nyumba yake na watwae mwana-kondoo mmoja, kwa kadiri ya hesabu ya watu; kwa kadiri ya ulaji wa kila mtu, ndivyo mtakavyofanya hesabu yenu kwa yule mwana-kondoo.

[5]Mwana-kondoo wenu atakuwa hana ila, mume wa mwaka mmoja; mtamtwaa katika kondoo au katika mbuzi.

[6]Nanyi mtamweka hata siku ya kumi na nne ya mwezi ule ule; na kusanyiko lote la mkutano wa Israeli watamchinja jioni.

[7]Nao watatwaa baadhi ya damu yake na kuitia katika miimo miwili na katika kizingiti cha juu, katika zile nyumba watakazomla.

Bwana aliwapa agizo la kuwatenga wana-kondoo Kutoka katika kundi siku ya 10, Kisha  siku ya 14 kuchinja.

Maana yake ni kuwa sadaka/dhabihu Yao, ilipaswa itambilike mapema Kisha ikatengwa. Kama wangekaidi agizo hilo na kuchagua mwanakondoo siku Ile Ile ya kuchinja au hata siku moja kabla  ilikuwa ni kosa mbele za Mungu.

Kufunua nini?

Na sisi pia Bwana anapendezwa na dhahibu zenye maandalizi, ambazo zimetengwa mapema…Kwamfano unapokwenda ibadani jijengee desturi ya kumwandalia Mungu sadaka zako mapema..hata ikiwezekena siku kadhaa kabla..Kwa jinsi unavyoandaa mapema ndivyo inavyokuwa na utukufu mwingi zaidi..

Lakini pia Unahakikisha unaitenga kabisa na hesabu zako nyingine..(yaani haiguswi), mpaka siku ya kumtolea. 

Hiyo itaifanya sadaka Yako ipokelewe Kwa furaha na Mungu, kuliko kufikiria kumtolea Mungu muda huo huo wakati ulikuwa na nafasi ya kufanya maandalizi. Ndio ufunuo ulio nyuma ya agizo hilo la Pasaka.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Makerubi wenye sura nne, ni kweli wapo? na je! wanyama wataenda mbinguni?

Kwanini Kristo aitwe Mwana-kondoo. (Yohana 1:29)

Tofauti kati ya zaka na sadaka ni ipi?

TUUTAFUTE USEMI MMOJA. TUUJENGE MNARA WA MUNGU

NI SAA KUMI NA MBILI (12) TU, ZA KRISTO KWAKO.

Bahari mbalimbali zilizoorodheshwa kwenye biblia.

Konzo la Ng’ombe ni nini? (Waamuzi 3:31).

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments