Kanaani ililaaniwa (Mwanzo 9:20-25,) kwanini Mungu awapeleke wana wa Israeli katika nchi iliyolaaniwa?

Kanaani ililaaniwa (Mwanzo 9:20-25,) kwanini Mungu awapeleke wana wa Israeli katika nchi iliyolaaniwa?

Jibu: Turejee,

Mwanzo 9:20 “Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu;

21 akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake.

22 Hamu, BABA WA KANAANI, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje. 

23 Shemu na Yafethi wakatwaa vazi, wakalitanda mabegani mwao wote wawili, wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao; na nyuso zao zilielekea nyuma, wala hawakuuona uchi wa baba yao. 

24 Nuhu akalevuka katika ulevi wake, akajua mwana wake mdogo alivyomtendea.

25 Akasema, NA ALAANIWE KAANANI; Atakuwa mtumwa kabisa kwa ndugu zake”.

Kumbuka hapo kwanza “Kaanani” halikuwa jina la Nchi, bali lilikuwa ni jina la ‘Mtu’. Na mtu huyo alikuwa ni mtoto wa nne (4) wa Hamu..

Mwanzo 10: 6 “Na wana wa Hamu ni Kushi, na Misri, na Putu, na Kanaani”.

Hatujui kwa undani mtoto huyu (Kanaani) alikuwa na tabia gani?..lakini ni wazi kuwa matendo yake yalikuwa kama ya baba yake Hamu, ndio maana akabeba laana ya moja kwa moja ya baba yake.

Sasa huyu Kanaani ndiye aliyelaaniwa na baadaye alikuja kuzaa watoto na uzao wake ukaitwa Uzao wa Kanaani, kufuatia jina la Baba yao, na walipotawanyika usoni pa nchi yote katika ule utawanyiko wa Babeli (Mwanzo 11:8-9) ndipo wakaenda kuishi mahali wana wa Israeli walipowakuta.

Kipindi wanaishi, ardhi ile ilijulikana kama nchi ya Wakanaani. Na kilichokuwa kimelaaniwa na Mungu si ile ardhi/nchi bali ni watu, (ambao ndio hao wakaanani)..ikiwa na maana kuwa hata kama wasingeishi katika ile ardhi na kwenda kuishi katika ardhi nyingine bado wangekuwa chini ya laana.

Kwahiyo wana wa Israeli wakati wanatoka Misri, Mungu aliwatoa Wakanaani kwenye ile ardhi na kuwaweka wana wa Israeli, kwasababu kilicholaaniwa katika Mwanzo 9:5 si ardhi bali ni watu, hivyo watu wanaweza kuondolewa na ardhi ikaendelea kutumika na wengine na ikawa nchi ya Baraka tu, ndio maana baada ya pale haikuitwa tena nchi ya wakanaani bali nchi ya Israeli.

Lakini swali ni je! Hawa Wana wa Hamu mpaka leo wamelaaniwa?.. Maana miongoni mwao kuna Kushi ambaye uzao wake ni watu weusi.

Jibu ni la! Kristo alikuja kuondoa laana zote pale Kalvari, na hivyo hakuna tofauti ya Myahudi na Mmisri, Mkushi na mwisraeli, mbele za Mungu… kama tumeokoka wote tunahesabiwa sawa mbele zake. Lakini kama hatutazaliwa mara ya pili kwa maji na kwa roho wote mbele zake ni kama tuliolaaniwa.

Wakolosai 3:10 “mkivaa utu mpya, unaofanywa upya upate ufahamu sawasawa na mfano wake yeye aliyeuumba.

11  Hapo hapana Myunani wala Myahudi, kutahiriwa wala kutokutahiriwa, mgeni wala mshenzi, mtumwa wala mwungwana, bali Kristo ni yote, na katika yote”.

Waefeso 2:16  “Akawapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa njia ya msalaba, akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba”

Je umezaliwa mara ya pili?..

Yohana 3:3  “Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.

4  Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?

5  Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu”.

Bwana Yesu anarudi!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Wakaanani walikuwa ni watu gani?

TUMEFANYA KAZI YA KUCHOSHA USIKU KUCHA.

NI KWANINI WATU WENGI WANASHINDWA KUMWELEWA MUNGU?

Moabu ni nchi gani kwasasa?

Je ni kweli Isaka alifarijika kwa kifo cha mamaye? (Mwanzo 24:67).

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments

UTAPENDA KUCHANGIA HUDUMA HII?

Tutamshukuru Mungu kwa ajili yako, kwa mchango wako, ili kuifanya injili hii isonge mbele Tuma sadaka yako kwa namba hizi:
Airtel:+255789001312 -Devis Magembe
Mpesa: +255767992434-Denis Magembe