Kwanini Bwana Yesu ajulikane kama ‘Amina’ (Ufunuo 3:14)

Kwanini Bwana Yesu ajulikane kama ‘Amina’ (Ufunuo 3:14)

Jibu: Turejee,

Ufunuo 3:14 “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye ‘ALIYE AMINA’, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu”

Neno Amina maana yake ni “Na iwe hivyo”.. Neno hili kwa lugha ya kiingereza ni “Amen” Hivyo Popote panapotajwa “Amina” au “Amen” maana yake ni “na iwe hivyo”.

Sasa kwanini Bwana Yesu ajitambulishe kwa neon hilo?..

Ni kuyatofautisha maneno yake na wengine! Kwamba maneno yake ni Thabiti.

Sasa ili tuelewe vizuri, turejee pale Bwana Yesu aliposema kuwa “Mimi ndimi Njia, na Kweli na Uzima, mtu haji kwa Baba ila kwa njia yangu mimi (Yohana 14:6)”.

Tukiunyambua huo mstari vizuri, tunapata sentensi mbili 1. Yeye ndiye Njia, 2. Mtu haji kwa Baba ila kwa njia yake yeye.

Hapo Bwana anajiita kuwa yeye “Njia” anajifananisha yeye na kitu kisicho na uhai..lakini anazidi kufafanua ni kwa jinsi gani yeye ni njia kwa kuendelea kusema… “mtu hafiki kwa Baba isipokuwa kwa njia yake yeye” ikiwa na maana kuwa, kwa maneno ya Yesu na maisha yake, tukiyafuata hayo tutafika mbinguni (hayo ndio njia)… Njia zipo nyingi, lakini zote hizo hazimpeleki mtu mbinguni, isipokuwa njia ya Yesu tu! Ambayo ni Neno lake.

Sasa tukirejea tena hapo Bwana aliposema yeye  ni “Amina” utaona mbele kidogo anaendelea kufafanua ni kwa namna gani yeye ni “Amina”.

Ufunuo 3:14  “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, SHAHIDI ALIYE MWAMINIFU NA WA KWELI, MWANZO WA KUUMBA KWA MUNGU”.

Anasema yeye ni Amina, Shahidi aliye mwaminifu, mwanzo wa kuumbwa kwa Mungu. Maana yake maneno yake ni hakika!, akisema amesema ni lazima iwe hivyo!.. Amina yake ni amina kweli.. wengine wanazo amina lakini zinaweza zisitimie kama walivyoseme. Lakini yeye (Yesu) maneno yake ni hakika!.. akisema basi ni lazima “ITAKUWA HIVYO KAMA ALIVYOSEMA” Ndio maana anaitwa Shahidi mwaminifu.. hajawahi kusema jambo halafu lisitimie..Ni mwaminifu kwa maneno yake siku zote.

Tusome,

Marko 13:31 “Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe”.

2Wakorintho 1:20 “Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni Ndiyo; tena kwa hiyo katika yeye ni Amin; Mungu apate kutukuzwa kwa sisi”.

Je umemtumainia huyu ambaye Maneno yake hayapiti?. Alisema “Aaminiye na kubatizwa ataokoka (Marko 16:16)” je unadhani kutakuwa na kanuni nyingine Zaidi ya hiyo?.. Alisema wadhalimu, na wachawi, na wazinzi, na walevi hawataurithi ufalme wa mbinguni, je unadhani anadanganya??..ni kweli itakuwa hivyo!, maneno yake kamwe hayapiti, Amina yake ni amina kweli..

Je umempokea Yesu?, je umebatizwa kwa maji na kwa Roho Mtakatifu?.. Kama bado basi tafuta kufanya hivyo mapema.

Maran atha?

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

UAMINIFU NI KIGEZO KIKUBWA CHA KUTUMIWA NA MUNGU.

Yeye naye aliye mvivu katika kazi yake, Ni ndugu yake aliye mharabu

Je Henoko aliyeenda na Mungu alikuwa ni mwana wa Kaini? (Mwanzo 4:16)

Vifungu vya biblia kuhusu Uongozi.

HUDUMA YA WALE MASHAHIDI WAWILI.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments