Shalom mtu wa Mungu, karibu tena tuyatafakari maandiko, leo tutaona dalili nyingine kubwa inayoutambulisha UZAO WA NYOKA..kama biblia inavyosema ulimwenguni kuna watu ambao wanafanya dhambi kwa makusudi huku wakijua kabisa watu wanaofanya hivyo wanastahili hukumu ya mauti lakini wao wanaendelea kufanya hivyo kwasababu ile hali ya kujali au kuchukua tahadhari haipo ndani yao(ukisoma Warumi 1:32 utaona jambo hilo), hao watu sio wachache ni wengi sana..Embu tuitazame hii habari fupi itatukumbusha kitu kingine cha msingi.
Mathayo 28:1 “Hata sabato ilipokwisha, ikipambazuka siku ya kwanza ya juma, Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, walikwenda kulitazama kaburi. 2 Na tazama, palikuwa na tetemeko kubwa la nchi; kwa sababu malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni, akaja akalivingirisha lile jiwe akalikalia. 3 Na sura yake ilikuwa kama umeme, na mavazi yake meupe kama theluji. 4 Na kwa kumwogopa, wale walinzi WAKATETEMEKA, WAKAWA KAMA WAFU. 5 Malaika akajibu, akawaambia wale wanawake, Msiogope ninyi; kwa maana najua ya kuwa mnamtafuta Yesu aliyesulibiwa”……… 11 Nao wale walipokuwa wakienda, tazama, baadhi ya askari waliingia mjini, wakawapasha wakuu wa makuhani habari za mambo yote yaliyotendeka. 12 Wakakusanyika pamoja na wazee, wakafanya shauri, wakawapa askari fedha nyingi, 13 wakisema, Semeni, ya kwamba wanafunzi wake walikuja usiku, wakamwiba, sisi tulipokuwa tumelala. 14 Na neno hili likisikilikana kwa liwali, sisi tutasema naye, nanyi tutawaondolea wasiwasi. 15 Basi wakazitwaa zile fedha, wakafanya kama walivyofundishwa. Na neno hilo likaenea kati ya Wayahudi hata leo.”
Mathayo 28:1 “Hata sabato ilipokwisha, ikipambazuka siku ya kwanza ya juma, Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, walikwenda kulitazama kaburi.
2 Na tazama, palikuwa na tetemeko kubwa la nchi; kwa sababu malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni, akaja akalivingirisha lile jiwe akalikalia.
3 Na sura yake ilikuwa kama umeme, na mavazi yake meupe kama theluji.
4 Na kwa kumwogopa, wale walinzi WAKATETEMEKA, WAKAWA KAMA WAFU.
5 Malaika akajibu, akawaambia wale wanawake, Msiogope ninyi; kwa maana najua ya kuwa mnamtafuta Yesu aliyesulibiwa”………
11 Nao wale walipokuwa wakienda, tazama, baadhi ya askari waliingia mjini, wakawapasha wakuu wa makuhani habari za mambo yote yaliyotendeka.
12 Wakakusanyika pamoja na wazee, wakafanya shauri, wakawapa askari fedha nyingi,
13 wakisema, Semeni, ya kwamba wanafunzi wake walikuja usiku, wakamwiba, sisi tulipokuwa tumelala. 14 Na neno hili likisikilikana kwa liwali, sisi tutasema naye, nanyi tutawaondolea wasiwasi.
15 Basi wakazitwaa zile fedha, wakafanya kama walivyofundishwa. Na neno hilo likaenea kati ya Wayahudi hata leo.”
Sasa kama tukiwatazama hawa askari ambao walikuwa wanalilinda kaburi la Bwana Yesu, pindi tu walipomwona Yule malaika kashuka pale, walitetemeka kwa hofu kubwa wakawa kama wafu, Na unajua mfu tabia yake ikoje?, Mfu huwa hawezi kufanya lolote anakuwa ameganda tu hapo chini, ndivyo ilivyowatokea hawa, ile hofu iliwafanya washindwe hata kukimbia au kufanya kitendo kingine chochote isipokuwa kungojea tu lolote litakalotokea, ni wazi maono yale ya wazi yaliwaingia sana moyoni, walitamani ingekuwa ni ndoto lakini haikuwa hivyo lilikuwa ni jambo la wazi kabisa mbele ya macho yao..
Waliona walichokiona, walisikia walichokisia, kulikuwa hakuna namna yoyote ungewashawishi kuwa Bwana Yesu hajafufuka kwa tukio lile, lakini kwa kuwa walipenda pesa kama Yuda, wakajiamulia tu kuudanganya uma kwamba hakuna kitu kama hicho, japo ukweli wote ulikuwa ndani yao..Hiyo ni mbaya sana. Ndugu Uzao wa Nyoka sikuzote huwa na tabii hii, hata kama ukizungumza na Mungu uso kwa uso, hata kama ukaona uweza wake wote na ukuu wake wote ni rahisi kuchukuliwa na jambo dogo sana, na hata kukana alichokiona dakika chache tu hapo nyuma.
Walichokiona askari hawa hakina tofauti na alichokiona Sauli wakati anaelekea Dameski kuwaua watakatifu, tofauti yao ni kwamba Sauli alitubu na kugeuka kwa mono yale, kuonesha kuwa yeye ni uzao wa Mungu, lakini hawa wengine walikwenda kusambaza uzushi pamoja na kwamba wameona maono makubwa kama yale… kuonesha kuwa wao sio uzao wa Mungu, ni uzao mwingine wa nyoka.
Wapo watu wengi leo Mungu kajidhihirisha kwao kwa namna nyingi sana, wengine Mungu kasema nao kwenye ndoto wazi wazi, wengine wametokewa na malaika, wengine wameonyeshwa maono mengi,wengine wameuona mkono wa Mungu waziwazi katika mambo yao, wengine wameepushwa na hatari nyingi na kusema kabisa hakika huyu ni Mungu wala hakuna pingamizi, wengine hata walimwomba Mungu awafanikishe katika vitu vyao akawafanikisha sawasawa na walivyomwomba kwa wakati waliomwomba, wakatetemeka na kusema kweli Mungu yupo… wakaogopa kweli kweli wakalia, wakazimia, wakawa kama wafu wakasema Mungu wangu kuanzia leo nitakutumikia, wengine wakasema ukinipa nafasi ya pili basi mimi nitakutumikia milele, mimi sitatenda dhambi tena kuanzia leo, lakini cha kushangaza akitoka hapo siku chache baadaye, au miezi michache mbeleni, pengine kakutana tu na vitu vidogo vidogo visivyokuwa na maana vya ulimwengu huu vinavyopita, utamwona karudi nyuma kwa kasi kubwa kana kwamba hajawahi kukutana na Mungu hapo nyuma hata siku moja…
Tena anaweza akawa ndio wa kwanza kuzungumza maneno ya mzaha kuhusu kazi ya Mungu au watumishi wake, lakini ndani ya moyo wake anajua kabisa Mungu alishawahi kumtembelea na kumwambia atubu. Watu kama hao wapo wengi sana inawezekana mmojawapo ni wewe unayesoma habari hii… Fanya utafiti uangalie utaona wale ambao hawajawahi kuuona uweza wa Mungu mwingi wale ambao Mungu anajihirisha kwao mara chache sana hao ndio wanaodumu na wanaomtumikia Mungu kwa moyo thabiti kuliko hawa wengine….na ndio maana Bwana Yesu alimwambia Tomaso heri wale ambao wameamini bila kuona..kwasababu alijua ugumu wa hawa wengine..
Ndugu unaendelea bado kumtumikia shetani na umesahau Mungu aliyokutendea hapo nyuma..Usidhani yataendelea kujirudia rudia hivyo kila siku, wakati utafika Roho wa Mungu ataondoka moja kwa moja ndani yako, utakachokuwa unangojea ni adhabu kubwa kuliko hata ile ya watu wa Sodoma na Gomora, Bwana Yesu ndio alisema hivyo kama wale wangeona Ishara na maajabu Mungu anayowatendea watu leo hii, miji ile ingekuwepo hadi leo, hivyo basi akasema itakuwa rahisi kwa watu wale kustahimili adhabu kuliko sisi tuliyoyaona na kuyakataa.
Ndugu salimisha maisha yako kwa Bwana kithabiti..Anapokuita sio kana kwamba anataka kukunyima haki yako ya kuchagua unayoyataka hapana, lakini anakupenda UPEO hataki upotee hata unywele wako, hataki uende kuzimu hilo tu!…Tubu sasa ukabatizwe katika ubatizo sahihi, uanze kuuishia wokovu katika hichi kipindi kifupi tulichobakiwa nacho duniani. Usikubali uwe sehemu ya UZAO wa nyoka ambao hata uhubiriweje injili na kuona maajabu yote hauwezi kugeuka..Naamini wewe sio mmojawapo na kwamba utapoisikia leo hii utageuka na kumwishia Kristo.
Ubarikiwe sana. Tafadhali “Share” Ujumbe huu kwa wengine. Na Bwana atakubariki.
Mada zinazoendana:
UZAO WA NYOKA.
WATU WASIOJIZUIA.
UZAO WAKO UTAMILIKI MALANGO YA KUZIMU
MTI WA UZIMA NA MTI WA MAARIFA.
Rudi Nyumbani:
JIUNGE NA GROUP LETU LA WHATSAPP HAPA >> WHATSAPP GROUP….
Shalom, Mtu wa Mungu, karibu tulitafakari kwa pamoja Neno la Mungu, biblia inasema Neno la Mungu ni Taa iongozayo miguu yetu na mwanga wa njia zetu (Zab.119:105), hivyo ni vyema tukalitafakari hilo kila kukicha ili njia yetu iwe safi na salama..(Zab.119:9 “Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako”).
Kama tunavyojua wengi wetu kwamba tunaishi katika siku za mwisho, na sio siku za mwisho tu! Bali ukingoni mwa siku za mwisho…Kwasababu siku za mwisho zilianza tangu zamani, sasa tupo ukingoni mwa hizo siku..Na kama tunavyojua ishara kubwa ya kututambulisha kuwa tupo ukingoni ni KUNYANYUKA KWA TAIFA LA ISRAELI. Ukienda kila mahali utasikia Israeli, Israeli..dunia ina mataifa mengi lakini ki-nchi kidogo kama kile kinavumisha upepo wa dunia na kuwa mada ya kuzungumziwa katika siasa yote ya dunia? Kuna nini pale?…Ni wazi kuwa kuna jambo la kiroho linaendelea kwenye Taifa hilo…Ndugu yangu hebu kama hujafuatilia ni nini kinaendelea kwenye Taifa hilo hebu tenga angalau wiki moja usiingie hata kwenye mitandao kuchat, tenga muda ulifuatilie kwa makini, soma historia ya Taifa hilo kwenye Biblia na kwenye historia…Ndio utajua tunaishi kipindi gani.
Wengi wetu tumezaliwa kipindi ambacho tunaambiwa kuna Taifa la Israeli, lakini wengi wetu hatujui kuwa Waisraeli wenyewe halisi, hawakukaa kwenye taifa lao, na kuwa na Mfalme wao wenyewe kwa takribani miaka 2,500 mpaka ilipofikia juzi tu mwaka 1948 ndipo wakarudi kuwa Taifa huru na kuwa na Raisi wao wenyewe…Kabla ya hapo walikuwa wametawanyishwa kwenye mataifa yote.
Sasa kama tunavyojua Kuwa Hawa Waisraeli tunaowaona, hawakua hivi, kwenye karne kadhaa huko nyuma… walikuwa wametawanyishwa katika Mataifa yote duniani, maandiko yanasema hivyo….Sasa kwanini Mungu aliwatawanyisha kwenye mataifa yote?..Jibu ni ili sisi watu wa mataifa tupate Neema, kwani Baada ya wayahudi (yaani waisraeli) kumkataa Masia wao Yesu Kristo, Bwana aliwaambia maneno haya…
Luka 21:20 “Lakini, hapo mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, ndipo jueni ya kwamba uharibifu wake umekaribia. 21 Ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani, na walio katikati yake wakimbilie nje, na walio katika mashamba wasiuingie. 22 Kwa kuwa siku hizo ndizo za mapatilizo, ili yatimizwe yote yaliyoandikwa. 23 Ole wao wenye mimba na wanaonyonyesha katika siku hizo! Kwa kuwa kutakuwa na shida nyingi katika nchi, na hasira juu ya taifa hili. 24 Wataanguka kwa ukali wa upanga, nao watatekwa nyara NA KUCHUKULIWA KATIKA MATAIFA YOTE; na Yerusalemu utakanyagwa na Mataifa, hata majira ya Mataifa yatakapotimia”
Luka 21:20 “Lakini, hapo mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, ndipo jueni ya kwamba uharibifu wake umekaribia.
21 Ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani, na walio katikati yake wakimbilie nje, na walio katika mashamba wasiuingie.
22 Kwa kuwa siku hizo ndizo za mapatilizo, ili yatimizwe yote yaliyoandikwa.
23 Ole wao wenye mimba na wanaonyonyesha katika siku hizo! Kwa kuwa kutakuwa na shida nyingi katika nchi, na hasira juu ya taifa hili.
24 Wataanguka kwa ukali wa upanga, nao watatekwa nyara NA KUCHUKULIWA KATIKA MATAIFA YOTE; na Yerusalemu utakanyagwa na Mataifa, hata majira ya Mataifa yatakapotimia”
Sasa Swali lingine linakuja…Wayahudi/Waisraeli kutawanywa kwenye mataifa yote ina uhusiano gani na sisi watu wa mataifa kupata Neema?…Yaani wengine waumie ili sisi tupate Neema?..Wengine wachukuliwe mateka ndipo sisi tupate Neema?..Kwani Mungu hawezi kuwaacha tu wawe salama, na kutupa Neema wote sisi na wao?.
Ni swali zuri lakini ni vizuri pia kujua kuwa ili kimoja kipate uzima ni lazima kingine kife! Kwamfano ili ule tunda na kupata virutubisho vilivyomo ndani yake ni lazima ulichume kutoka kwenye mti, ulitafune na kulisagasaga…hapo ni sawa na umeliua…ili ule nyama ikusaidie kwa protini ni lazima mnyama Fulani auawe, huwezi kula kitu kizima…kadhalika ili upate kitu Fulani ni lazima hicho kitu kiwe kimepunguka kutoka sehemu Fulani, hata fedha mtu anazozotafuta ni kwamba zimepunguka sehemu Fulani zikaenda kwa huyo mtu, ikiwa na maana kuwa endapo ukifanikiwa kuzikusanya zote basi kwingine kutakuwa kumepunguka pia pakubwa, kwahiyo hakuna kuongezekewa kama hakuna kupunguka sehemu Fulani nyingine…wala hakuna kupata heshima Fulani kama mwingine hajapata dharau, hata cheo, au nafasi,ni lazima mmoja aondoke mwingine aingie…. Mambo ndivyo yanavyokwenda hivyo…Kwahiyo ili sisi watu wa Mataifa tupate heshima mbele za Mungu ni lazima wawepo wengine walioharibu mahali Fulani.
Kwahiyo Waisraeli walipomkataa Yesu na injili yake, wakawa wamejiharibia wenyewe hivyo hiyo ikawa faida kwetu sisi watu wa mataifa ndio maana Mtume Paulo aliwaambia..
Matendo 13:44 “Hata sabato ya pili, watu wengi, karibu mji wote, wakakusanyika walisikie neno la Mungu. 45 Bali Wayahudi, walipowaona makutano, wakajaa wivu, wakayakanusha maneno yaliyonenwa na Paulo, wakibisha na kutukana. 46 Paulo na Barnaba wakanena kwa ushujaa wakasema, Ilikuwa lazima neno la Mungu linenwe kwenu kwanza; lakini kwa kuwa mnalisukumia mbali, na kujiona nafsi zenu kuwa hamkustahili uzima wa milele, angalieni, twawageukia Mataifa. 47 Kwa sababu ndivyo tulivyoamriwa na Bwana, Nimekuweka uwe nuru ya Mataifa, Upate kuwa wokovu hata mwisho wa dunia. 48 Mataifa waliposikia hayo wakafurahi, wakalitukuza neno la Bwana, nao waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini. 49 Neno la Bwana likaenea katika nchi ile yote”.
Matendo 13:44 “Hata sabato ya pili, watu wengi, karibu mji wote, wakakusanyika walisikie neno la Mungu.
45 Bali Wayahudi, walipowaona makutano, wakajaa wivu, wakayakanusha maneno yaliyonenwa na Paulo, wakibisha na kutukana.
46 Paulo na Barnaba wakanena kwa ushujaa wakasema, Ilikuwa lazima neno la Mungu linenwe kwenu kwanza; lakini kwa kuwa mnalisukumia mbali, na kujiona nafsi zenu kuwa hamkustahili uzima wa milele, angalieni, twawageukia Mataifa.
47 Kwa sababu ndivyo tulivyoamriwa na Bwana, Nimekuweka uwe nuru ya Mataifa, Upate kuwa wokovu hata mwisho wa dunia.
48 Mataifa waliposikia hayo wakafurahi, wakalitukuza neno la Bwana, nao waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini.
49 Neno la Bwana likaenea katika nchi ile yote”.
Kwa dhambi hiyo walioifanya Mungu hakuishia tu kuwapokonya injili bali pia aliwatawanya kwenye mataifa yote, na hiyo pia ikawa ni faida ya PILI kwetu.
Kumbuka popote wayahudi wanapopelekwa, mahali pale lazima pabarikiwe hata kama wamepelekwa kwa makosa yao…mfano utaona Yusufu alipoingia Misri pamoja na wana wa Israeli wote, Taifa la Misri lilibarikiwa sana…Farao hakufa na njaa, na zaidi ya yote Farao aliyekuwa mtu wa Mataifa alipata nafasi hata ya kuoneshwa maono na Mungu mwenyewe, jambo ambalo si la kawaida Mungu kuzungumza na watu wamataifa.
Kadhalika utaona wakati Wana wa Israeli tena wamepelekwa Babeli utumwani, Mungu aliibariki Babeli kwa ajili ya wana wa Israeli waliomo mule, Babeli ilizidi kustawi, na pia Mfalme Nebukadneza alipata hadi Neema ya kuoneshwa maono na Mungu ya wakati ujao, jambo ambalo sio la kawaida Mungu kuzungumza na watu wa Mataifa, hiyo ni kutokana na waisraeli waliokuwepo kwenye hiyo nchi, ijapokuwa walipelekwa kule kwa dhambi zao lakini bado kulikuwa na Baraka Fulani za kimwili na kiroho zilizokuwa zinaambatana nao.
Kadhalika kipindi cha Esta, Mfalme Ahasuero alifanikiwa katika enzi yake kwasababu ya Esta, Mordekai pamoja na Wayahudi waliokuwepo kwenye ufalme wake..
Na sehemu zote ndio hivyo hivyo, popote Wayahudi walipokwenda kulibarikiwa mwilini na rohoni.
Vivyo hivyo katika siku zile baada ya kumkataa Yesu Kristo, walipotawanyishwa tena kwenye mataifa yote ulimwenguni, popote walipokaribishwa sehemu zile zilibarikiwa kimwili na kiroho, Ukiangalia mataifa mengi ya Ulaya, mafanikio yao yametokana na Wayahudi waliokuwemo kule kipindi kile, kadhalika na Marekani, na nchi nyingine zote…baraka zao ni kwasababu ya waisraeli waliowakaribisha kipindi wanatawanywa.. na Mungu kayabariki mataifa yote kwasababu ya Israeli na Baraka kubwa aliyowabaikia ya rohoni, ni KUWAPA MATAIFA ZAWADI YA YESU KRISTO. Hiyo ndio zawadi kubwa Mungu anayoweza kumpa mwanadamu…Kwahiyo sisi kuzawadiwa Yesu Kristo yaani kuzawadiwa hii Neema ya kumkubali Yesu Kristo ni kutokana na Wayahudi kuwemo humu mataifani, tulimo sisi.
Lakini cha kuogopesha ni kwamba wayahudi sasa wameshaanza kurudi nchini kwao, kidogo kidogo wameshaanza kuhisi makosa yao waliyoyafanya miaka 2000 iliyopia, mioyo ya kutubu kidogo kidogo imeanza kurudi ndani mwao, mamia kila siku wanamiminika kurudi kwao, hiyo ni ishara ya nini?..Ni ishara kuwa Neema inaondoka huku…Zile Baraka zinaondoka huku, baraka za rohoni na za mwilini…Kumbuka Baada ya majeshi ya Israeli kutoka Misri nini kilitokea huko nyuma?, jibu ni mapigo! ..hakuna Neema tena! Hujasikia tena tangu hapo na kuendelea Mfalme yeyote wa Misri anaota zile ndoto za kiMungu tena! Wala hujasikia chochote cha maana kilichokuwa kinaendelea Misri…Hiyo yote ni kwasababu Uzao wa Mungu umerudi kwao, na Bwana amewarudia watu wake.
Kadhalika wana wa Israeli waliporudi nchini kwao, baada ya kuchukuliwa Babeli, hutaona Mungu akishughulika tena na Babeli, au Umedi au Uajemi…Habari zao ndio zilikuwa zimeishia pale, sasa Mungu anarudi kushughulika na watu wake Israeli.
Ndugu, Hii Neema ipo ukingoni, hivi karibuni! Wayahudi wanakwenda kutubu kabisa kabisa! Na Bwana atawasamehe, na atawamwagia kipawa chake cha Roho, na wakati huo huo Roho Mtakatifu atakuwa ameshaondoka huku kwetu mataifani, yaani unyakuo utakuwa umeshapita! Kitakachokuwa kumesalia ni dhiki kuu na siku ya Bwana inayotisha!, Bwana akirudi leo hatutasema hatukusikia wala hatukuona, vyombo vya habari vinatuhubiria injili kila mahali, mtu asipotaka kuyatilia maanani basi ni kwa uzembe wake mwenyewe, mwenye macho haambiwi tazama, mwenye masikio haambiwi sikia
Ikiwa hii neema ambayo inafifia unaichezea, moja ya hizi siku itazima kabisa..Jitathimini wewe mwenyewe umesimama upande upi.
Maran Atha!
Tafadhali share na kwa wengine, Mungu akubariki.
Mada Zinazoendana:
MAMBO YATAKAYOTOKEA ISRAELI SIKU ZA HIVI KARIBUNI.
MZEITUNI HALISI UTAKAPOPACHIKWA.
SIKU YA TAABU YA YAKOBO.
HATA ILIPOTIMIA SIKU YA PENTEKOSTE.
NJIA SAHIHI YA KUFUNGA.
Rudi Nyumbani
Biblia inatuambia moja ya kazi ya malaika ni kuwahudumia watakatifu, (Waebrania 1:14) na tunajua siku zote kama mtu ni muhudumu ni lazima akae eneo husika la wale anawahudumia, kwamfano Daktari anafanya kazi ya kuwahudumia wagonjwa, japokuwa anao kwake mwenyewe lakini huwezi kumkuta masaa yote yupo nyumbani bali muda wake mwingi utakumkuta anakesha mahospitalini, kwasababu huko ndipo wagonjwa walipo. Vivyo hivyo na malaika wa Bwana, wamepewa jukumu la kuwahudumia watakatifu, sasa japo makazi yao ni mbinguni lakini muda wao mwingi wapo duniani wanazunguka huko na huko kuhakikisha yale yote yaliyokusudiwa na Mungu juu ya watakatifu yanatimia.
Hivyo tusichokujua tu ni kuwa hata sasa tunapozungumza kuna mamilioni ya malaika wanaozunguza duniani kila siku, na kazi yao ni moja kuhakikisha kusudi la Mungu linatimia kwa namna zote. Na malaika kama biblia inavyotuambia ni viumbe wa rohoni hivyo Mungu amewapa uwezo wa kuchukua maumbile tofauti tofauti, wanaweza wakatembea kama nguzo ya moto, au wingu, au taswira za mnyama, au taswira ya mwanadamu. Kwahiyo katika sikuzote za maisha yako, kwa namna moja au nyingine ulishawahi kukutana au kupishana na malaika wa Mungu wengi pasipo hata wewe kujijua, Na ndio maana Mtume Paulo anasema:
Waebrania 13:1 “Upendano wa ndugu na udumu. 2 Msisahau kuwafadhili wageni; maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua.”
Waebrania 13:1 “Upendano wa ndugu na udumu.
2 Msisahau kuwafadhili wageni; maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua.”
Tukimwangalia Ibrahimu siku moja wakati amekaa nyumbani kwake ghafla aliona watu watatu wamesimama nyumbani kwake, Lakini Ibrahimu hakuwafukuza au kuwaita wapepelezi badala yake yeye ndiye aliyewashurutisha waangie nyumbani mwake wale na wanywe, na kumbe walikuwa ni malaika wa Bwana pamoja na Bwana mwenyewe wakiwa katika safari yao ya kwenda kuupeleleza mji..
Vivyo hivyo hao hao waliposhuka Sodoma, Lutu alipowaona kuwa ni wageni sio wenyeji wa pale hakusubiri wafike nyumbani kwake bali yeye ndiye aliyewakimbilia na kuwaambia waingie kwake! Wale na wanywe na walale, lakini wale watu walikataa kata kata, lakini Lutu hakuacha kuwashurutisha sana, na walipokubali baadaye ndipo Lutu alipojua kuwa wale hawakuwa watu wa kawaida.. Na Kuwafadhili wageni
Sio lazima tu iwe wale wanaotaka kuja kulala nyumbani kwetu, lakini pia kuwatendea ukarimu wale ambao wanaonekana wanahitaji msaada kwa wakati huo, hususani wale tusiowajua….na ukarimu huo unaweza ukawa chakula, fedha, ushauri, n.k.
Biblia inatukumbusha tuwe wakarimu, ni wazi kuwa dunia ya sasa upendo umepoa kila mtu anajipenda nafsi yake, zamani ilikuwa mwenyeji ndio anamshurutisha mgeni aje kwake, lakini sikuhizi mwenye hitaji ndio anamshurutisha mwenye nacho amsaidie, na bado anaweza asiambulie chochote, utakuta muda mwingine unapishana na mtu barabarani anakuambia ninasikia njaa sijala, na hakuombi hata pesa anakuomba tu ukamnunulie muhogo mmoja pale apooze njaa! Utasikia huyo mtu anasema, mimi sina kitu na ukiangalia mfukoni ana kiasi tu kikubwa cha fedha ambayo haina matumizi imekaa tu kwenye pochi.. mwingine atakuambia naomba unilipie nauli, utaona mtu anasema sina pesa, lakini ukweli ni kuwa anayo lakini hataki kumpa, Ndugu kama unacho chochote wewe mpe tu! Sio lazima kiwe kingi, hata kama kakudanganya usijali chochote, kwa maana hujui huyo aliyekuomba ni nani?.
Mwingine hataonyesha dalili ya kukuomba chochote, lakini wewe ukimtazama utaona anao uhitaji Fulani, na huku ukiangalia una vichenchi chenchi vimebaki mfukoni wewe mpe tu, kwasababu hujui huyo unayempa ni nani…Lakini simaanishi kwamba uumpe tu kila mtu, hata kama mtu anahitaji pesa ya sigara au pombe au madawa ya kulevya uumpe hapana!..Mtu wa namna hiyo hapaswi kupewa chochote kwasababu mtu mwenye shida kweli ya msingi hawezi kuomba vitu kama hivyo, vilevile hata malaika wa Bwana hawawezi kufanya hivyo. Ukimkuta Mtu kalewa halafu anakuomba kitu usimpe chochote, ukimkuta mtu kashika sigara halafu anakuomba usimpe! Mpe kwanza injili n.k
Lakini mbali na hao asilimia kubwa ya wengi wanaotuomba wanao matatizo..pengine hata wewe ilishakukuta ulifika wakati ulitamani mtu akusaidie kitu Fulani, pengine hata sio chakula, bali kitu Fulani kingine cha muhimu sana ambacho unahitaji tu kwa muda huo na hauna….sasa watu wa namna hiyo wapo mamia kwa mamia… tuwasaidie kwa vidogo tulivyo navyo. Utajisikiaje siku ile umefika mbinguni halafu malaika kama 100 wanatokea kila mmoja anakuambia ulishawahi kunisaidia mara 2 nilipokuwa duniani. Ni furaha kiasi gani unadhani Bwana Yesu ataona fahari juu yako kiasi, lakini siku ile mfano unafika na unaona malaika hawana habari na wewe, wakati unashangaa hilo wanakuambia ulishawahi kutufukuza, au ulishawahi kutunyima kitu Fulani tulichowahi kukuomba tukiwa duniani. Na wakati haukutani na malaika bali na MKUU mwenyewe Bwana Yesu, sasa tukiwa wabinafsi kila wakati kuna hatari kubwa sana ya kukosa mema Mungu aliyotuandalia..
Mathayo 25:31 “Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake; 32 na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi; 33 atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto. 34 Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu; 35 kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha; 36 nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia. 37 Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha? 38 Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika? 39 Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia? 40 Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi. 41 Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake; 42 kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe; 43 nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama. 44 Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie? 45 Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi. 46 Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.”
Mathayo 25:31 “Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake;
32 na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi;
33 atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto.
34 Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu;
35 kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha;
36 nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia.
37 Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha?
38 Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika?
39 Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia?
40 Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.
41 Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;
42 kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe;
43 nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama.
44 Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie?
45 Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi.
46 Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.”
Bwana akubariki. Tafadhali “Share” Ujumbe huu kwa wengine.
HUDUMU YA MALAIKA WATAKATIFU.
JE! BAADA YA ULIMWENGU HUU KUISHA MALAIKA WATAKUWA NA KAZI GANI TENA?
JE! MBINGUNI KUNA MALAIKA WA KIKE?. NA JE! TUKIFIKA MBINGUNI TUTAFANANA WOTE?
KUNDI LA MALAIKA WALETAO MABAYA.
MALAIKA WA MAJI NI NANI? (UFUNUO 16:5)
Yohana 5:24 “Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani.”
Warumi 8:1 “Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu”.
KUNA HUKUMU ZA AINA NGAPI?
UFUFUO WA UZIMA NA WA HUKUMU.
UTALIPWA KATIKA UFUFUO WA WENYE HAKI.
KAMA MHUBIRI NI WOKOVU UPI UNAUPELEKA KWA WATU?
WhatsApp
1Samweli 2 :6 “Bwana huua, naye hufanya kuwa hai; Hushusha hata kuzimu, tena huleta juu. 7 Bwana hufukarisha mtu, naye hutajirisha; Hushusha chini, tena huinua juu.
8 Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Humpandisha mhitaji kutoka jaani, Ili awaketishe pamoja na wakuu, Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu; Kwa maana nguzo za dunia zina Bwana, Naye ameuweka ulimwengu juu yake”.
Mhubiri 7:21 “Tena, usitie moyoni mwako maneno yote yaliyosemwa; usije ukamsikia mtumwa wako mwenyewe ali anakutukana.
22 Kwa kuwa mara nyingi moyo wako pia unajua ya kwamba wewe mwenyewe umewatukana watu wengine”.
SAMEHE KUTOKA NDANI YA MOYO WAKO.
TOBA IGUSAYO MOYO WA BWANA.
KWANINI PALE BWANA YESU ALICHUKUA HATUA YA KUMSAMEHE DHAMBI KWANZA KABLA YA KUMPONYA YULE MTU MWENYE KUPOOZA?(MARKO 2).
KISASI NI JUU YA BWANA.
EPUKA MUHURI WA SHETANI
1Wakorintho 1:25 “Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu’’.
1Wakoritho 1:22 “Kwa sababu Wayahudi wanataka ishara, na Wayunani wanatafuta hekima;
23 bali sisi tunamhubiri Kristo, aliyesulibiwa; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wayunani ni upuzi; 24 bali kwao waitwao, Wayahudi kwa Wayunani, ni Kristo, nguvu ya Mungu, na hekima ya Mungu.
25 Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu.”
1Wakorintho 2:7 “bali twanena hekima ya Mungu katika siri, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu;
8 ambayo wenye kuitawala dunia hii hawaijui hata mmoja; maana kama wangaliijua, wasingalimsulibisha Bwana wa utukufu;”
Zaburi 37:25 “Nalikuwa kijana nami sasa ni mzee, Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa Wala mzao wake akiomba chakula.”
UWEZA WA MUNGU UNAONEKANA WAPI?
BASI MUNGU AKAMUADHIMISHA SANA..
NJIA YA MSALABA
NI KWASABABU YA YESU KRISTO.
2 Timotheo 4:1 “Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, atakayewahukumu walio hai na waliokufa; kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake;
2 lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho. 3 Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti;
4 nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo”
Wagalatia 5:19 “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, 20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu”.
Biblia inasema ” HAMJUI YA KUWA MTAWAHUKUMU MALAIKA? (1Wakorintho 6:2-3) ”. je! sisi tutawahukumuje Malaika?.
NI UTHIBITISHO UPI UNAOONYESHA KUWA KUNA MBINGUNI NA KUZIMU?
KUZIMU NI MAHALI PA NAMNA GANI ,JE! HUKO WANAISHI WATU WAKIFA NA KWENDA KUPATA MATESO AU NI VINGINEVYO?
NI HALALI KUBATIZA WATOTO WADOGO?
USHUHUDA WA RICKY:
Ufunuo 16:12 “Na huyo wa sita akakimimina kitasa chake juu ya mto ule mkubwa Frati; maji yake yakakauka, ili njia itengenezwe kwa wafalme watokao katika maawio ya jua.
13 Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo. 14 Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi. 15 (Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.)
16 Wakawakusanya hata mahali paitwapo kwa Kiebrania, Har-Magedoni”
UFUNUO: Mlango wa 16.
SIKU YA BWANA INAYOTISHA YAJA!
Naomba kuuliza kati ya Unyakuo wa kanisa, Dhiki kuu, Vita vya har-magedoni, Utawala wa miaka 1000, Vita ya gogu na magogu, hukumu ya kiti cha enzi cheupe. Je, ni nini kinaanza na kingine kufuata kwa mpangilio wa matukio hayo?
UNYAKUO.
Inadhaniwa na wengi ili kwamba mtu asemehewe dhambi zake na Mungu ni lazima aongozwe sala Fulani ijulikanayo kama sala ya Toba, na kwamba mtu asipoongozwa sala hiyo basi huwezi kusamehewa dhambi zake, Na hiyo imewafanya watu wengi hata wale wasio wakristo kusema wameokoka, kisa tu huko nyuma walishawahi kuongozwa Sala ya Toba. Lakini biblia inatufundisha nini juu ya toba halisi inayopelekea kusamehewa dhambi?. Embu tufuatilie kwa pamoja tukio hili alilokutana nalo Bwana wetu Yesu na mwitikio wake jinsi ulivyokuwa, kuna jambo la Fulani nataka ulione pengine hata na wewe hujawahi kulijua japo ni habari tunayoisoma kila siku, Tusome:
Luka 7:37 “Na tazama, mwanamke mmoja wa mji ule, aliyekuwa mwenye dhambi, alipopata habari ya kuwa ameketi chakulani katika nyumba ya yule Farisayo, alileta chupa ya marimari yenye marhamu. 38 Akasimama nyuma karibu na miguu yake, akilia, akaanza kumdondoshea miguu machozi yake, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake, akiibusu-busu miguu yake na kuipaka yale marhamu. 39 Basi, yule Farisayo aliyemwalika alipoona vile, alisema moyoni mwake, Mtu huyu kama angekuwa nabii, angemtambua mwanamke huyu amgusaye, ni nani, naye ni wa namna gani, ya kwamba ni mwenye dhambi. 40 Yesu akajibu akamwambia, Simoni, nina neno nitakalo kukuambia. Akasema, Mwalimu, nena. 41 Akasema, Mtu mmoja mkopeshaji alikuwa na wadeni wawili; mmoja amwia dinari mia tano, na wa pili hamsini. 42 Nao walipokuwa hawana cha kumlipa, aliwasamehe wote wawili. Katika hao wawili ni yupi atakayempenda zaidi? 43 Simoni akajibu akasema, Nadhani ni yule ambaye alimsamehe nyingi. Akamwambia, Umeamua haki. 44 Akamgeukia yule mwanamke, akamwambia Simoni, Wamwona mwanamke huyu? Niliingia nyumbani kwako, hukunipa maji kwa miguu yangu; bali huyu amenidondoshea machozi miguu yangu, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake. 45 Wewe hukunibusu; lakini huyu tangu nilipoingia hakuacha kunibusu sana miguu yangu. 46 Hukunipaka kichwa changu mafuta; bali huyu amenipaka miguu yangu marhamu. 47 Kwa ajili ya hayo nakuambia, Amesamehewa dhambi zake ambazo ni nyingi, kwa kuwa amependa sana; lakini asamehewaye kidogo, huyo hupenda kidogo. 48 Kisha alimwambia mwanamke, UMESAMEHEWA DHAMBI ZAKO. 49 Ndipo wale walioketi chakulani pamoja naye walianza kusema mioyoni mwao, Ni nani huyu hata asamehe dhambi?”.
Luka 7:37 “Na tazama, mwanamke mmoja wa mji ule, aliyekuwa mwenye dhambi, alipopata habari ya kuwa ameketi chakulani katika nyumba ya yule Farisayo, alileta chupa ya marimari yenye marhamu.
38 Akasimama nyuma karibu na miguu yake, akilia, akaanza kumdondoshea miguu machozi yake, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake, akiibusu-busu miguu yake na kuipaka yale marhamu.
39 Basi, yule Farisayo aliyemwalika alipoona vile, alisema moyoni mwake, Mtu huyu kama angekuwa nabii, angemtambua mwanamke huyu amgusaye, ni nani, naye ni wa namna gani, ya kwamba ni mwenye dhambi.
40 Yesu akajibu akamwambia, Simoni, nina neno nitakalo kukuambia. Akasema, Mwalimu, nena.
41 Akasema, Mtu mmoja mkopeshaji alikuwa na wadeni wawili; mmoja amwia dinari mia tano, na wa pili hamsini.
42 Nao walipokuwa hawana cha kumlipa, aliwasamehe wote wawili. Katika hao wawili ni yupi atakayempenda zaidi?
43 Simoni akajibu akasema, Nadhani ni yule ambaye alimsamehe nyingi. Akamwambia, Umeamua haki.
44 Akamgeukia yule mwanamke, akamwambia Simoni, Wamwona mwanamke huyu? Niliingia nyumbani kwako, hukunipa maji kwa miguu yangu; bali huyu amenidondoshea machozi miguu yangu, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake.
45 Wewe hukunibusu; lakini huyu tangu nilipoingia hakuacha kunibusu sana miguu yangu.
46 Hukunipaka kichwa changu mafuta; bali huyu amenipaka miguu yangu marhamu.
47 Kwa ajili ya hayo nakuambia, Amesamehewa dhambi zake ambazo ni nyingi, kwa kuwa amependa sana; lakini asamehewaye kidogo, huyo hupenda kidogo.
48 Kisha alimwambia mwanamke, UMESAMEHEWA DHAMBI ZAKO.
49 Ndipo wale walioketi chakulani pamoja naye walianza kusema mioyoni mwao, Ni nani huyu hata asamehe dhambi?”.
Utaona pia sehemu nyingi ambazo Bwana Yesu anatamka hili Neno “UMESAMEHEWA DHAMBI ZAKO.” Watu wanachukizwa na kumwona kama ni mkufuruji, kujiamulia kumtolea mtu tu hukumu kana kwamba yeye ni Mungu, utasoma hilo pia katika (Marko 2:112) pale alipomwona Yule mtu aliyepooza na kumwambia umesamehewa dhambi zako, watu walikasirika sana na kusema huyu anakufuru..Lakini hawakuona kitu ambacho Kristo alikuwa anakiona, wao walidhani anajiamulia tu kutamka maneno yale kwa kila mtu, hata kwa Yule ambaye hana mpango na Mungu kumwambia “Umesamehewa dhambi” hapana Bali Kristo alikuwa anaona ndani kabisa kwenye vyumba vya ndani vya mioyo ya watu wale
Alikuwa anaona mioyo ya Toba, mioyo inayojutia dhambi zao, mioyo inayosema laiti Mungu angenisikia akanisamehe wingi wa dhambi zangu hizi, nitamtumikia milele, mioyo inayosema sitakaa nirudie tena dhambi hizi natuja ni kwanini nilijihusisha katika dhambi hizi,..Ndicho Bwana Yesu alichokiona ndani ya yule mwanamke na Yule mtu aliyepooza..Sasa japo kwa nje! Hawakuzungumza na Bwana lolote, lakini ndani walikuwa wanamlilia Bwana.. Na pale pale utaona Yesu anawatamkia hadharani “UMESAMEHEWA DHAMBI ZAKO”, Sasa wale watu ambao hawajui chochote na huku wakimwona yule kahaba asemi chochote, na kumsikia Bwana Yesu anazungumza maneno kama yale wanasema anakufuru. Na kumbuka Bwana hakusema “nimekusamehe dhambi” hapana! Bali alisema “umesamehewa” ikiwa na maana kuwa alikuwa ni kama anatoa taarifa ya kitu ambacho kimefanyika tayari huko mbinguni…ni sawa na wewe umwambie mtu Fulani “umesamehewa riba” hiyo haimaanishi ni wewe ndio umemsamehe, bali wewe unasimama kama mwakilishi wa kitu ambacho kimefanyika sehemu nyingine. Na ndio Mamlaka Kristo aliyokuwa nayo ya kusamehe dhambi duniani. Alikuwa hafanyi chochote isipokuwa ameona kwanza kwa Baba yake.
Yohana 5: 19 “Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda; kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vile vile”.
Lakini endapo Bwana angemwona yule mwanamke amekuja na marhamu na kulia chini ya miguu yake, na kuanza kumpangusa miguu yake kwa machozi yake, na ndani ya moyo wake hana moyo wa Toba, ni Dhahiri kuwa asingemwambia yale maneno, labda angemwambia maneno mengine ya kumjenga lakini sio kumwambia amesamehewa dhambi zake.
Ndugu Mungu hategemei Sala 100 za toba unazoongozwa kila siku, hategemei unafungua kinywa chako kumkiri yeye mbele zake mara ngapi na kulia kwa kupaza sauti ya kuomba msamaha mara ngapi..Ikiwa ndani yako hakuna moyo wa kudhamiria kabisa kugeuka moja wa moja kuacha dhambi na kumfuata Kristo,..Toba yako ni batili.
Mtu mmoja anaweza akawa ni muuaji, jambazi na gaidi lakini siku moja akajutia makosa yake na kusema kuanzia leo Mungu wangu ninakugeukia na haya mambo siyataki tena, na akayaacha kweli akaanza kumtafuta Mungu, lakini wewe unayekwenda kila siku madhahabuni pa Mungu na kulia daima na kumwambia Mungu nisamehe, unaongozwa kila siku sala ya Toba lakini bado huku nyuma unazini kisiri siri, unatazama picha chafu za ngono kisirisiri, unakunywa pombe kisirisiri unajiita ni mshirika wa siku nyingi kanisani nataka nikuambie ukweli ni kwamba Mungu “HAKUWAHI KUKUSAMEHE DHAMBI ZAKO”.
Bwana anaisamehe mioyo ya Toba, sio midomo ya toba.
Hivyo hatupaswi kujidanganya kwa namna yoyote ile. Toba ya kweli haipo midomoni bali moyoni, Iwe ni kwa sala au sio kwa sala kinachojalisha ni kugeuka kwa dhati ndani ya moyo, na kujutia kile kitu na kusema sifanyi tena kwa vitendo..Je! wewe umegeuka? kama bado basi wakati ndio huu, fanya uamuzi wa busara usio na majuto, mguekie yeye ili upokee msamaha halisi na wa kweli kutoka Mbinguni kwa Mungu Baba..
Ubarikiwe sana.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
MATUNDA YAPATANAYO NA TOBA!
JIBU: Tukisoma Yohana 10:16 Inasema…
“Na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta; na sauti yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja”.
Katika Mstari huo tunaona imeweka wazi kabisa kuwa Mchungaji ni Bwana Yesu mwenyewe…na Bila shaka kondoo ni watu wake…..Na kama kondoo ni watu wake ni Dhahiri kuwa ni lazima Mahali wanapoishi ndipo patakuwa zizi lao. Sasa katika Biblia Nchi ya Israeli inafananishwa na zizi la Mungu, ikiwa na maana kuwa wayahudi ni kondoo wa Mungu waliopo katika zizi linaloitwa Israeli. Tunalithibitisha hilo katika..
Ezekieli 34:13 “Nami nitawatoa katika watu wa mataifa, na kuwakusanya katika nchi zote, nami nitawarudisha katika nchi yao wenyewe; nami nitawalisha juu ya milima ya Israeli, kando ya mifereji ya maji; na katika mahali pote pa nchi panapokaliwa na watu. 14 Nami nitawalisha malisho mema, pa juu ya milima ya mahali PALIPOINUKA PA ISRAELI LITAKUWA ZIZI LAO; huko watalala katika zizi jema; nao watakula malisho mema, juu ya milima ya Israeli. 15 Mimi mwenyewe nitawalisha kondoo zangu, nami nitawalaza, asema Bwana MUNGU”.
Ezekieli 34:13 “Nami nitawatoa katika watu wa mataifa, na kuwakusanya katika nchi zote, nami nitawarudisha katika nchi yao wenyewe; nami nitawalisha juu ya milima ya Israeli, kando ya mifereji ya maji; na katika mahali pote pa nchi panapokaliwa na watu.
14 Nami nitawalisha malisho mema, pa juu ya milima ya mahali PALIPOINUKA PA ISRAELI LITAKUWA ZIZI LAO; huko watalala katika zizi jema; nao watakula malisho mema, juu ya milima ya Israeli.
15 Mimi mwenyewe nitawalisha kondoo zangu, nami nitawalaza, asema Bwana MUNGU”.
Vivyo hivyo kinyume chake, watu wote ambao si wa Israeli ndio wapo zizi lingine ambalo Bwana alilolizungumzia pale, Yaani sisi watu wa Mataifa ndio Bwana aliokuwa ana maanisha kondoo wa Zizi lingine, ambao nasi pia ulifika wakati, tuliingizwa na kuwa miongoni mwa kondoo wake Bwana, kwasababu injili ilianza kwanza kwa wayahudi ndipo ikaja kwetu…..na kwa kupitia msalaba sisi pamoja na wayahudi wote tumekuwa kundi moja, na Bwana wetu amekuwa ni mmoja (Yesu Kristo).
Waefeso 2:11 “Kwa ajili ya hayo kumbukeni ya kwamba zamani ninyi, mlio watu wa Mataifa kwa jinsi ya mwili, mnaoitwa Wasiotahiriwa na wale wanaoitwa Waliotahiriwa, yaani, tohara ya mwilini iliyofanyika kwa mikono; 12 kwamba zamani zile mlikuwa hamna Kristo, mmefarakana na jamii ya Israeli, wageni wasio wa maagano ya ahadi ile. Mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu duniani.13 Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa damu yake Kristo. 14 Kwa maana yeye ndiye amani yetu, ALIYETUFANYA SISI SOTE TULIOKUWA WAWILI KUWA MMOJA; akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga”
Waefeso 2:11 “Kwa ajili ya hayo kumbukeni ya kwamba zamani ninyi, mlio watu wa Mataifa kwa jinsi ya mwili, mnaoitwa Wasiotahiriwa na wale wanaoitwa Waliotahiriwa, yaani, tohara ya mwilini iliyofanyika kwa mikono;
12 kwamba zamani zile mlikuwa hamna Kristo, mmefarakana na jamii ya Israeli, wageni wasio wa maagano ya ahadi ile. Mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu duniani.
13 Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa damu yake Kristo.
14 Kwa maana yeye ndiye amani yetu, ALIYETUFANYA SISI SOTE TULIOKUWA WAWILI KUWA MMOJA; akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga”
Unaona hapo? Alitufanya sisi wawili (yaani sisi watu wa mataifa na wayahudi) kuwa mmoja…yaani kwa kundi moja.
Wagalatia 3:27 “Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo. 28 Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu”.
Wagalatia 3:27 “Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo.
28 Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu”.
Je! Na wewe ni miongoni mwa kondoo wake?..Umeingizwa ndani ya kundi la Kristo, Kumbuka hatufanyiki kondoo wa Kristo kwa kujiunga na Kanisa bali kwa kutubu na kubatizwa na kupokea Roho? Na kuishi Maisha matakatifu?.
Ubarikiwe.
MAANA YA HUU MSTARI NI IPI? MITHALI 14:4 ‘ZIZI NI SAFI AMBAPO HAPANA NGOMBE;BALI NGUVU ZA NGOMBE ZALETA FAIDA NYINGI’.
AMIN! NAWAAMBIA KIZAZI HIKI HAKITAPITA!
CHUKIZO LA UHARIBIFU
JE! MABALASI BWANA YESU ALIYOYATUMIA KUGEUZIA MAJI KUWA DIVAI, YALITUMIKA TU KWA KAZI HIYO?
WAFALME WATOKAO MAWIO YA JUA.