Category Archive maswali na majibu

Paulo aliwapaje watu karama ya rohoni?

Swali: Hii karama ya rohoni Mtume Paulo aliyowaahidi Warumi kuwa atawapa ni ipi?..na aliwapaje?.


Jibu: Turejee.

Warumi 1:11 “Kwa maana ninatamani sana kuwaona, nipate kuwapa KARAMA YA ROHONI, ili mfanywe imara”

Awali ya yote ni vizuri kuzingatia kuwa hasemi “karama za rohoni” kana kwamba ni nyingi…bali anasema “karama ya rohoni”  ikiwa na maana ni “moja tu”.

Na hiyo si nyingine zaidi ya ile iliyokuwa ndani ya Paulo (Karama aliyokuwa nayo Paulo).

Sasa anaposema “apate kuwapa karama ya rohoni”…hamaanishi kumpa tu mwingine karama kama aliyokuwa nayo yeye, au awawekee mikono wapokee karama za rohoni kama unabii, au lugha, au imani La! Hakumaanisha hivyo, kwasababu vipawa na karama ni Mungu pekee ndiye atoaye na si mwanadamu.

Lakini maana ya “kuwapa karama ya rohoni”…ni kuwanufaisha wale watu kwa karama iliyokuwemo ndani yake Paulo.

Mtu mwenye karama ya unabii na anapompa mwingine unabii kwa uongozo wa Roho Mtakatifu maana yake “amempa mtu huyo karama ya rohoni”..mtu mwenye karama ya uponyaji anaombea wengine na wakapokea uponyaji, maana yake amewapa wale watu karama ya rohoni na ndicho Mtume Paulo alichokimaanisha pale.

Ili tuelewe vizuri tusome tena maandiko yafuatayo..

Warumi 12:6 “Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, TUTOE unabii kwa kadiri ya imani;

7 ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake”.

Umeona hapo?…anasema ikiwa unabii, ualimu, au karama nyingine yoyote basi TUTOE kwa wengine?.

Kwahiyo Mtume Paulo alikuwa amelenga kuwanufaisha watu kwa ile karama Mungu aliyoiweka ndani yake, na si kuwagawia karama za roho mtakatifu zile zinazotajwa katika 1Wakorintho 12.

Na zaidi sana Paulo alikuwa anashauku sana kufanya hivyo kwa makundi yote ya watu (Wayunani na Wayahudi).

Warumi 1:13 “Lakini, ndugu zangu, sipendi msiwe na habari, ya kuwa mara nyingi nalikusudia kuja kwenu, nikazuiliwa hata sasa, ili nipate kuwa na matunda kwenu ninyi pia kama nilivyo nayo katika Mataifa wengine.

14 Nawiwa na Wayunani na wasio Wayunani, nawiwa na wenye hekima na wasio na hekima”.

Je na wewe unaitoa karama yako kwa wengine??..fahamu kuwa kila mtu aliyempokea KRISTO anayo karama ya rohoni, na ni lazima utumike kuwajenga wengine na kuwavuta kwa KRISTO zaidi.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Rudi Nyumbani

Print this post

Je yule mkoma aliyeponywa alifika kwanza kwa makuhani kisha ndio akarudi kumpa Yesu shukrani au alirudi kabla hajafika kwa makuhani?

JIBU: Baada ya Yesu kukutana na wale wenye ukoma kumi, na kuwaagiza waende kujionyesha kwa makuhani

biblia inatuonyesha walipokea uponyaji wote wakiwa bado wapo njiani, lakini tunaona yule mkoma mmoja hakuendelea na safari yake. Palepale ilimbidi ahairishe kwanza safari yake Na kuja kumshukuru Yesu, na ndipo pengine aendelee na safari yake ya kuelekea kwa makuhani.

Luka 17:14-19

[14]Alipowaona aliwaambia, Enendeni, mkajionyeshe kwa makuhani. Ikawa walipokuwa wakienda walitakasika.

[15]Na mmoja wao alipoona kwamba amepona, alirudi, huku akimtukuza Mungu kwa sauti kuu;

[16]akaanguka kifudifudi miguuni pake, akamshukuru; naye alikuwa Msamaria.

[17]Yesu akajibu, akanena, Hawakutakaswa wote kumi? Wale kenda wa wapi?

[18]Je! Hawakuonekana waliorudi kumpa Mungu utukufu ila mgeni huyu?

[19]Akamwambia, Inuka, enenda zako, imani yako imekuokoa.

Kwanini afanye vile ni kwasababu aliona umuhimu wa kumshukuru Yesu Kristo kwanza zaidi ya wahudumu wake.

Jambo lolote Mungu analotaka kututendea kupitia wahudumu wake..Tujue kuwa Shukrani zetu za kwanza zinapaswa zimrudie yeye.

Amina.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Kwanini BWANA awaagize wakoma wakajionyeshe kwa Makuhani?(Luka 17:14

Kwa namna gani tumefanyika Makuhani na Ufalme?.(Ufunuo 1:6)

UKOMA NA UJANE ULIO NDANI YAKO, UMEUPATIA TIBA?

Rudi Nyumbani

Print this post

Kwanini BWANA awaagize wakoma wakajionyeshe kwa Makuhani?(Luka 17:14

Jibu: Turejee kuanzia ule mstari wa 12..

Luka 17:12 “Na alipoingia katika kijiji kimoja, alikutana na watu kumi wenye ukoma; wakasimama mbali,

13 wakapaza sauti wakisema, Ee Yesu, Bwana mkubwa, uturehemu!

14 Alipowaona aliwaambia, Enendeni, MKAJIONYESHE KWA MAKUHANI. Ikawa walipokuwa wakienda walitakasika”.

Sababu kuu ya Bwana YESU kuwaagiza hawa wakome wakajinyeshe kwa Makuhani ni kwasababu Makuhani ndio watu wa mwisho kutangaza kama mtu ni Mkoma au si Mkoma, baada ya uchunguzi.

Kwani zamani mtu akihisiwa au akijihisi mwenyewe kama ni mkoma basi sheria ilikuwa ni kwamba anaenda kwa Kuhani, na kisha kuhani anauchunguza mwili wake na baada ya uchunguzi akibainika kwamba anao Ukoma, basi huyo mtu anakuwa najisi na anatengwa,

Sheria hiyo tunaisoma katika kitabu cha Mambo ya Walawi Mlango wa 13.

Walawi 13:9 “Pigo la ukoma litakapokuwa katika mtu, ndipo ataletwa kwa kuhani;

10 na kuhani ataangalia, na tazama, ikiwa pana kivimbe cheupe katika ngozi yake, na malaika yamegeuzwa kuwa meupe, tena ikiwa pana nyama mbichi iliyomea katika kile kivimbe,

11 ni ukoma wa zamani ulio katika ngozi ya mwili wake, na kuhani atasema kuwa yu najisi; hatamweka mahali, kwa kuwa yeye yuna unajisi”

Kwahiyo endapo wale watu kumi wenye ukoma wangefika kwa Kuhani na baada ya kukaguliwa wakakutwa na madhaifu hayo yaliyotajwa hapo juu, basi wangekuwa NAJISI..maana yake ni wenye ukoma ambao haujatakasika/kupona.

Na kama tayari walishachunguzwa zamani na kubainika wanao ukoma, na sasa wanarudia tena vipimo kwa kuhani ili kubaini kama ukoma wao umepona basi endapo wangekutwa. bado wanao basi wangeendelea kuwa najisi na kutengwa….

Lakini tunaona watu hao kumi (10) wakiwa njiani kuwafuata Makuhani ili waangaliwe, wakiwa njiani walijikuta wametakasika ule ukoma, walijikuta ngozi zao zimerudia hali zao za zamani, kama Naamani alivyoponywa ukoma wake. (2Wafalme 5:14).

Luka 17:14 “Alipowaona aliwaambia, Enendeni, mkajionyeshe kwa makuhani. Ikawa walipokuwa wakienda walitakasika.

15 Na mmoja wao alipoona kwamba amepona, alirudi, huku akimtukuza Mungu kwa sauti kuu;

16 akaanguka kifudifudi miguuni pake, akamshukuru; naye alikuwa Msamaria.

17 Yesu akajibu, akanena, Hawakutakaswa wote kumi? Wale kenda wa wapi?

18 Je! Hawakuonekana waliorudi kumpa Mungu utukufu ila mgeni huyu”

Mambo makuu mawili ya kujifunza kufuatia habari hiyo

   1.Uponyaji wa YESU unahitaji imani yenye Matendo.

Laiti kama  hawa wenye ukoma wangeyadharau maneno ya Bwana YESU  aliyowaambia kuwa wakajionyeshe kwa Makuhani, na wangeenda njia nyingine, hakika wasingepona, wangebaki vile vile.

Lakini walipochukua hatua ya kwenda kwa Makuhani, kumbe maili kadhaa mbele muujiza wao ulikuwa unawangoja, kama tu ilivyokuwa kwa Naamani alipoambiwa akajichovye mara saba Yordani.

Hali kadhalika na wewe, shida au ugonjwa wowote ulio nao, kazi uliyobakiwanayo ni moja tu, kuyaamini maneno ya Bwana YESU na kuendelea mbele katika Neno lake, Muujiza wako utakutana nao mbele, usianze kuutafuta dakika hiyo hiyo.

  2. Kurudi kumpa MUNGU utukufu na kushuhudia.

Hili ni jambo la pili la kujifunza. MUNGU wetu anapendezwa na watu wa Shukrani.

Angalia mtu huyu alirudi kumshukuru MUNGU na kutoa ushuhuda na Bwana YESU akatafsiri tukio hilo ni kama kumpa MUNGU utukufu..

Huwenda MUNGU alishakutendea jambo fulani kubwa je uliwahi kurudi na kumtukuza mbele ya wengi?..Au je una mpango wowote wa kumtukuza katika hilo unalomwomba sasa akutendee?..Jibu unalo wewe.

Je tayari umempokea YESU?..Unao uhakika Bwana akirudi leo unaenda naye?.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Rudi Nyumbani

Print this post

Kufifiliza ni kufanya nini? (Kumbukumbu 32:25).

Jibu: Turejee…

Kumbukumbu 32:25 “Nje upanga UTAWAFILILIZA Na ndani ya vyumba, utisho; Utaangamiza mvulana na msichana,  Anyonyaye pamoja na mwenye mvi”.

Kufifiliza ni “kuangamiza” hivyo neno hilo katika maandiko hayo limesimama badala ya “kuangamiza mtu”..ambapo matokeo yake ni msiba wa mtu muhimu katika nyumba.

Hivyo andiko hilo laweza kueleweka hivi..

Kumbukumbu 32:25 “Nje upanga UTAWAANGAMIZA Na ndani ya vyumba, utisho; Utaangamiza mvulana na msichana,  Anyonyaye pamoja na mwenye mvi”.

Je unaye YESU moyoni?.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Rudi Nyumbani

Print this post

Kuwanda ni kufanya nini?

Jibu: Turejee..

Waamuzi 3:17 “Kisha akamsongezea Egloni, mfalme wa Moabu, hiyo tunu; basi Egloni alikuwa ni mtu AYELIWANDA sana”.

Kuwanda ni kiswahili kingine cha “kunenepa sana”.. Hivyo mtu aliyewanda maana yake ni “mtu aliyenenepa sana”.

Hivyo mstari huo wa Waamuzi 3:17 unaweza kueleweka hivi…

Waamuzi 3:17 “Kisha akamsongezea Egloni, mfalme wa Moabu, hiyo tunu; basi Egloni alikuwa ni mtu ALIYENENEPA sana”.

Neno hilo pia tunaweza kulisoma katika Yeremia 50:11 na katika habari za Yeshuruni katika Kumbukumbu 32:15. 

Kwa habari ndefu kuhusiana na Yeshuruni basi fungua hapa 》》》Yeshuruni ni nani katika biblia?

Je wewe kiroho umewanda/nenepa katika nini?..katika maovu au katika haki?…

Ni hatari kubwa KUWANDA katika mabaya…

Yeremia 5:28 “WAMEWANDA sana, wang’aa; naam, wamepita kiasi KWA MATENDO MAOVU; hawatetei madai ya yatima, ili wapate kufanikiwa; wala hawaamui haki ya mhitaji.

29 Je! Nisiwapatilize kwa mambo hayo? Asema BWANA; na nafsi yangu, je! Nisijilipize kisasi juu ya taifa la namna hii?”

Je unaye Roho Mtakatifu?. Kumbuka Roho Mtakatifu ndiye muhuri wa MUNGU (Waefeso 4:30).

Bwana YESU anarudi (Maran atha).

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Rudi Nyumbani

Print this post

Je Bwana YESU alipanda mlimani na wanafunzi wake baada ya siku sita au nane?

Swali: Je Bwana YESU alipanda mlimani na wanafunzi wake baada ya siku ngapi?..ni Sita au Nane?, Kwa maana katika Mathayo 17:1 na Marko 9:2 panaonyesha ni baada ya siku sita (6) lakini tukisoma Luka 9:28 panaonyesha ni siku ni nane (8) Je ukweli ni upi?.


Jibu: Turejee mistari hiyo..

Mathayo 17:1 “Na baada ya SIKU SITA Yesu akawatwaa Petro, na Yakobo, na Yohana nduguye, akawaleta juu ya mlima mrefu faraghani”

Hapa ni kweli tunasoma “Siku sita” na Marko 9:2 tunasoma vile vile ni siku sita (6).

Tusome tena Luka 9:28..

Luka 9:28  “Baada ya maneno hayo yapata SIKU NANE, aliwatwaa Petro na Yohana na Yakobo, akapanda mlimani ili kuomba”.

Hapa tunasoma ni siku nane (8) na si sita tena, swali ni je! Biblia inajichanganya?, au mwandishi mmoja amekosea?

Jibu ni La! Biblia haijichanganyi na wala hakuna mwandishi aliyekosea, wote wapo sawa na maneno yote ni hakika, kwasababu biblia ni kitabu kilichohakikiwa na Roho Mtakatifu mwenyewe na hakina makossa (Mithali 30:5).

Sasa kama ni hivyo kwanini  panaonekana  kuna tofauti ya siku?..

Mwandishi wa kitabu cha Luka alionyesha jumla ya siku walizokaa mlimani, na Mwandishi wa kitabu cha Mathayo na Marko wakaonyesha siku walizoondoka katika makazi yao na kuelekea mlimani.

Sasa ni kwamba baada ya Bwana kuwaambia wanafunzi wake kuwa wapo ambao hawataonja mauti hata watakapoona ufalme wa Mungu ukija kwa nguvu, zilipita siku sita akawachukua wanafunzi wake baadhi (ambao ni Petro, Yohana na Yakobo) akapanda nao mlimani.

Na biblia haijaeleza katika hizo siku sita kabla ya kupanda mlimani walikuwa wanafanya nini au walikuwa wapi, pengine waliachana kidogo, au walikuwa katika huduma zilizowatenga kwa muda siku sita, mpaka ilipofika siku hiyo ya kupanda mlimani….hiyo yote haijaeleza lakini inasema tu baada ya siku sita alipanda nao mlimani, na ndicho Mwandishi Mathayo na Marko walichokieleza.

Lakini sasa Luka yeye hakulenga kuelezea siku waliyopanda mlimani, kwamba ni baada ya siku sita za yale maneno, bali yeye alisema “YAPATA SIKU NANE”… Hilo Neno “Yapata” ni neno la ujumla, likielezea Muda wa safari Nzima, kuwa ni SIKU NANE (8), Maana yake baada ya siku sita walipanda mlimani sawasawa na Mwandishi Mathayo na Marko na kule mlimani walikaa siku mbili (2), na kufanya jumla ya siku kuwa nane, ndicho mwandishi alichokilenga. (kwahiyo muda waliokaa mlimani ni siku mbili, lakini walipanda baada ya siku sita).

Kwahiyo biblia haijajichanganya hapo, bali ni uelewa wetu ndio unaojichanganya.

Je umempokea BWANA YESU?.. Na je unajua kuwa dalili zote zinaonyesha kuwa kizazi tulichopo ni cha mwisho?..Je umejiandaaje? Taa yako inawaka?

Luka 12:35  “Viuno vyenu na viwe vimefungwa, na taa zenu ziwe zinawaka;

36  nanyi iweni kama watu wanaomngojea bwana wao, atakaporudi kutoka arusini, ili atakapokuja na

Je bado unaendelea na maisha ya dhambi?, bado unakunywa pombe?, bado unazini, bado unajichua, bado unavaa kidunia?

Muda umeisha, msikilize Roho Mtakatifu, na usizisikilize roho zidanganyazo.

1Timotheo 4:1“Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani”

Maran tha!

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

TABIA SITA (6) ZA WANAFUNZI WA YESU.

KWANINI MTINI KATIKATI YA MIZABIBU?

MPENDEZE MUNGU ZAIDI.

Je maombi ya mlimani yana ulazima wowote kwa mkristo?

USIISHIE KUTAZAMA JUU, ENDELEA MBELE.

Rudi Nyumbani

Print this post

Kwanini Mungu azungumze na Ayubu kupitia upepo wa kisulisuli (Ayubu 38:1)

Ayubu 38:1

[1]Ndipo BWANA akamjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli, na kusema,


JIBU: Tukumbuke kuwa Mungu ana njia nyingi za kuzungumza na watu. Na kila njia huwa na maana fulani nyuma yake.

Utakumbuka Alipokutana na Musa alizungumza naye katika kijiti kinachoungua lakini hakiteketei..Kuwafundisha wana wa Israeli kuwa atakuwa pamoja nao hata katika moto wa majaribu lakini hawatateketea kabisa.. 

Kwamfano akina Shedraki, Meshaki na Abednego, walipojaribiwa kwa kutupwa tanuruni, hawakuungua au Danieli kwenye tundu la simba, hakupatwa na dhara lolote kwasababu walimtumaini Mungu. 

Kutufundisha kuwa hata  sasa, na sisi tuliomwamini Kristo, hakuna jaribu la aina yoyote linaloweza kutufanya sisi tuangamie na kupotea mbali na uso wa Mungu. Kwasababu yeye yupo nasi sikuzote.

Halikadhalika tunaona na hapa pia anamtokea Ayubu katika upepo wa kisulisuli..

Kisulisuli hutafsirika kama aina nyingine ya janga, mfano tu wa gharika au tetemeko. Kazi ya kisulisuli huwa ni kuzomba vitu  dhaifu labda makapi, au vitu ambavyo havina msingi imara…

Isaya 40:24

[24]Naam, hawakupandwa; hawakutiwa katika ardhi kama mbegu; naam, shina lao halikutia mizizi katika ardhi; tena awapuzia tu, wakanyauka, upepo wa kisulisuli wawaondoa kama mabua makavu. 

Hivyo Mungu kutumia njia hii, ni kumwonyesha Ayubu kwamba hata katika zomba-zomba za kiroho yeye yupo huko na watu wake.

Vitu vyote vya Ayubu vilizombwa, Kuanzia mali, watoto,.mifugo, hadi mke wake kwasababu ya udhaifu wa imani akazombwa na hila za shetani. Wao wakidhani kuwa Mungu amewaacha kumbe alikuwa nao daima. Tufahamu kuwa dhoruba, tufani, giza, au mwanga..vyote kwake ni sawasawa.

Lakini pia kuna wakati Mungu anazungumza katika utulivu. Utakumbuka tena habari ya Eliya wakati ule anamfuata Mungu kule mlima Horebu, akitarajia Mungu aseme naye katika fujo. Lakini hakumwona Mungu, katika matetemeko wala moto, bali katika sauti ndogo ya utulivu.

Kuonyesha kuwa Mungu husema nasi pia katika utulivu.

1 Wafalme 19:11-12

[11]Akasema, Toka, usimame mlimani mbele za BWANA. Na tazama, BWANA akapita; upepo mwingi wa nguvu ukaipasua milima, ukaivunja-vunja miamba mbele za BWANA; lakini BWANA hakuwamo katika upepo ule; na baada ya upepo, tetemeko la nchi; lakini BWANA hakuwamo katika lile tetemeko la nchi; 

[12]na baada ya tetemeko la nchi kukawa na moto; lakini BWANA hakuwamo katika moto ule; na baada ya moto sauti ndogo, ya utulivu. 

Hivyo ikiwa umeokoka na umesimama imara na Bwana ni vizuri kufahamu kuwa nyakati zote, Mungu yupo nasi. Ni kawaida watu wakishapitia changamoto fulani hufikiri kuwa Mungu hayupo nao, kumbe sivyo nyakati zote nm ziwe za majaribu, za visulisuli, za mafuriko n.k. Tunapaswa tumwone yeye,.kwasababu yupo pamoja na sisi.

Kwasababu ndiye msaada wetu.

Shalom

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >>

https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

JINSI YA KUSHINDA VISULISULI(Mithali 10:25)

UPEPO WA KUSI HULETA MVUA;

NITAUVUTAJE UWEPO WA ROHO MTAKATIFU KARIBU NAMI?

Rudi Nyumbani

Print this post

Masheki ni akina nani? (Ayubu 29:10).

Swali: Masheki ni watu gani kama tusomavyo katika Ayubu 29:10?

Jibu: Turejee..

Ayubu 29:10 “Sauti yao masheki ilinyamaa, Na ndimi zao zilishikamana na makaakaa yao”.

Masheki ni jina lingine la “Wana wa wafalme”

Hivyo hapo aliposema.. “Sauti yao masheki ilinyamaa..”  ni sawa na kusema “sauti zao wana wa wafalme zilinyamaa”.

Neno hili pia tunalisoma katika..Zaburi 68:31, Zaburi 83:11 na Zaburi 105:22, na zote zina maana ile ile moja (wana wa wafalme ambao ni wakuu wa nchi).

Zaburi 68:31 “]Masheki watakuja kutoka Misri, Kushi itamnyoshea Mungu mikono yake mara”.

Je umempokea YESU Mwokozi?. na kukamilisha haki yote kwa ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Bwana YESU? (sawasawa na Matendo 2:38)?

Kama bado basi tengeneza mambo yako hayo kabla ule mwisho haujafika.

Bwana akubariki.

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Rudi Nyumbani

Print this post

Shetani alitoka wapi?

Swali: Je shetani yule audanganyaye ulimwengu alitoka wapi?


Jibu: shetani kwa asili aliumbwa na Mungu, na kabla ya kuwa shetani alikuwa akiitwa “Kerubi afunikaye”

Ezekieli 28:14 ” Wewe ulikuwa KERUBI MWENYE KUTIWA MAFUTA AFUNIKAYE; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto”.

Na MUNGU alimwumba akiwa mkamilifu (asiye na dosari) kama tu MAKERUBI wengine, lakini baadaye moyo wake uliinuka akajidanganya mwenyewe kuwa anaweza kuwa kama MUNGU (aabudiwe kama MUNGU) Na ndipo Uovu huo ukaonekana ndani yake, na hakutaka kubadilika.

Ezekieli 28:15 “Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako”

Na baadaye alipoasi ndipo akawa shetani, na maana ya shetani ni Mshitaki/Mchongezi, maana yake anawashitaki wanadamu mbele za MUNGU mchana na usiku.

Ufunuo 12:9 “Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.

10  Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana AMETUPWA CHINI MSHITAKI WA NDUGU ZETU, YEYE AWASHITAKIYE MBELE ZA MUNGU WETU, MCHANA NA USIKU”.

Kwahiyo shetani aliumbwa na MUNGU, na akaasi na  ataharibiwa na MUNGU katika ziwa la MOTO baada ya hukumu ya kile kiti cheupe.

Ufunuo 20:10 “Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele”.

Bwana atuepushe na ibilisi.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

NAO WAKAMSHINDA KWA DAMU YA MWANA-KONDOO.

JINSI YA KUPIGANA MAOMBI YA VITA.

NYOTA YA ASUBUHI.

ZIFAHAMU KAZI TATU ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA ULIMWENGU.

FAHAMU JINSI MUNGU NA SHETANI WANAVYOZUNGUMZA NA WATU.

Rudi Nyumbani

Print this post

Ufidhuli ni nini (2Wakorintho 12:10).

Swali: Ufidhuli ni nini kama tunavyosoma katika 2Wakorintho 12:10?


Jibu: Turejee..

2 Wakorintho 12:10 “Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na UFIDHULI, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu”

Maana ya “Ufidhuli” kama ilivyotumika hapo ni “Matukano”

Hivyo Mtume Paulo kwa ujasiri katika Roho Mtakatifu alidiriki kusema kuwa “anapendezwa na madhaifu”  katika Kristo maana yake ni kwamba pale anapojiona kuwa ni mdhaifu basi alijiona mwenye heri.

Lakini pia anapendezwa na UFIDHULI (Matukano). Yaani pale anapotukanwa kwaajili ya Kristo basi jambo hilo kwake alilipenda zaidi.

Sasa kujua kwa marefu kama ni sahihi kwa Mtume Paulo kujisifia udhaifu fungua hapa >>> Je ni sawa kuukubali udhaifu kama mtume Paulo alivyojisifia kwa huo? (2Wakorintho 12:9-10)

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Rudi Nyumbani

Print this post