Mwanzo 1:26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi
JIBU: Mara nyingi Mungu alikuwa anatumia neno “sisi” kama wingi kuashiria kuwa hakufanya mambo yote peke yake, bali alikuwa na wengine aliowashirikisha mawazo yake, Kumbuka kuumba aliumba yeye peke yake lakini mawazo yake ya kufanya baadhi ya mambo aliwashirikisha wengine, hivyo hapo aliposema na tumfanye mtu kwa mfano wetu alikuwa anaongea na malaika zake, na hakuwa anazungumza na nafsi ya tatu katika uungu wake, kama wengi tunavyodhani Mungu ni mmoja tu na hana nafsi tatu, neno “TUMFANYE” halimaanishi ni watatu tu! bali linaweza likamaanisha wawili, au watano, au mia au milioni n.k.
Hivyo tukisema Mungu ana nafsi tatu kwa kuusimamia mstari huu sio kweli, pale Bwana alikuwa anazungumza na malaika zake ambao walikuwa wameshaumbwa kabla yetu sisi, Tunaona pia jambo hili linajirudia sehemu nyingine nyingi katika biblia Bwana akizungumza na malaika zake, Ukisoma
Mwanzo 3:22″Bwana Mungu akasema basi huyu mtu amekuwa kama MMOJA WETU, kwa kujua mema na mabaya”…,
pia,
Mwanzo 11:6 “Bwana akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya. 7 Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao. 8 Basi Bwana akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote; wakaacha kuujenga ule mji.”
Unaona hapo sehemu zote hizi mbili Bwana alionekana akijadiliana na malaika zake. Mungu huwa anatenda kazi na malaika zake. Tukisoma pia
Isaya 6:8 Kisha nikasikia sauti ya Bwana ikisema, nimtume nani? naye ni nani atakayekwenda KWA AJILI YETU? Ndipo niliposema mimi hapa nitume mimi. Naye akaniambia enenda ukawaambie watu hawa fulizeni kusikia lakini msifahamu; fulizeni kutazama lakini msione…”
Unaona tena hapo Bwana alimuuliza nabii Isaya ni nani atakayekwenda kwa ajili yetu (yaani Mungu na jeshi lake la mbinguni)?. Kwahiyo Mungu kujadiliana na malaika zake sio jambo jipya tunaweza tukaliona pia kwenye ile habari ya mfalme Ahabu na nabii Mikaya ukisoma
2 nyakati 18:15-22” utaona jinsi Bwana alivyokuwa anashauriana na malaika zake juu ya hatma ya mfalme Ahabu.
Kwahiyo pale katika mwanzo 1:26 aliposema Na tumfanye mtu kwa mfano wetu Mungu alikuwa hazungumzi na YESU wala Roho Mtakatifu bali na malaika zake waliokuwepo kabla yetu sisi. (Lakini kumbuka sio kwamba malaika ndio waliokuwa wanaumba, hapana Mungu peke yake ndiye aliyekuwa muumbaji.)
Ubarikiwe sana.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada zinazoendana:
MTI WA UZIMA NA MTI WA MAARIFA.
JIBU: Biblia inasema kuna ufufuo wa aina mbili,
Ufufuo wa kwanza, umejumuisha wale watakatifu waliofufuka na Bwana Yesu ukisoma (Mathayo 27:52) utaona..,pamoja na watakatifu watakao fufuka katika unyakuo, na watakao fufuliwa wakati wa kuingia kwenye ule utawala wa miaka 1000 (Ufunuo 20:4) haya ni makundi matatu yanayotengeneza aina ya kwanza ya ufufuo.
Ufunuo 20:6 “….Heri na mtakatifu ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza, juu ya hao mauti ya pili haina nguvu…”
Na ufufuo wa pili utakuja mara tu baada ya utawala wa miaka 1000 kuisha..ambapo wafu wote ambao hawakuwepo katika ufufuo wa kwanza watafufuliwa na kuhukumiwa na Kristo mwenyewe katika hukumu ya kile kiti cheupe cha Enzi cha Yesu Kristo tukisoma
Ufunuo 20:11 “Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana.
12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.
13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.
14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto.
15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.”
Kwahiyo ndugu biblia inasema wana heri wale watakaokuwepo katika ule ufufuo wa kwanza. kwasababu mauti ya pili haitakuwa na nguvu juu yao. Na mauti ya pili ni ziwa la moto. Hivyo tujitahidi hata kama Bwana atakupokuja akatukuta tumelala(tumekufa), basi tuwe na nafasi katika ule ufufuo wa kwanza.
Ubarikiwe sana.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada zinazoendana:
Miriamu alikuwa ni dada yake Musa na Haruni, wa damu (Hesabu 26:59), Miriamu ndiye aliyekuwa wa mwisho kuzaliwa katika famila ya Yokebedi na Amramu. Biblia inasema naye pia alikuwa ni nabii. Hawa watatu Bwana aliwaita kipekee kuhudumu katika hatua ya kuwaongoza wana wa Israeli. (Mika 6:4)
Huduma ya Miriamu ilikuwa ya kipekee na kielelezo kwa wanawake, kwani baada ya Bwana kulipiga jeshi la Farao kwa kulitosa kwenye Bahari ya Shamu, Miriamu alisimama na jeshi kubwa pamoja na wanawake wenzake, wakamwimbia Bwana kwa MATARI na kucheza! (Kutoka 15:20-21).
Wakiwa jangwani katika safari yao ya kwenda nchi ya Ahadi. Miriamu pamoja na Haruni walianza kumnenea Musa, na kumlaumu, kwasababu ya Mwanamke wa kiKushi aliyemwoa. Jambo hilo likamchukiza sana Bwana na hatimaye Bwana kumpiga Miriamu kwa ukoma. Lakini baadaye alikuja kupona baada ya Musa kumwombea. (Kutoka 12:1-6).
Miriamu alikufa kabla ya kuiona nchi ya Ahadi, alikufa katika Bara la Sini, huko Kadeshi, na huko ndiko alikozikiwa.(Kutoka 20:1).
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Haruni alizaliwa miaka mitatu kabla ya kuzaliwa Nabii Musa, alikuwa ni ndugu wa damu kabisa wa Musa. Na walikuwa na dada yao aliyeitwa MIRIAMU. Bwana alimwita Haruni katika huduma baada ya Musa kusita-sita wito wake wa kwenda kwa Farao, na baada ya kutoa vijisababu. Mungu alimwita Haruni ndugu yake awe kama msemaji wake katika safari yao ya kwenda kuwafungua wana wa Israeli dhidi ya mateso ya Farao. (Kutoka 4:10-15).
Haruni pamoja na Musa walikuwa ni wa kabila la LAWI. Bwana aliwapa maagizo kwamba kwa kutumia ile FIMBO wakafanye ajabu zote mbele ya Farao. Fimbo ndiyo iliyokuja kujulikana kama FIMBO YA HARUNI.
Kutokana na utumishi wa Haruni, Bwana alimteua awe KUHANI MKUU, Yeye na wanawe milele. Na kabila la Musa na Haruni, (kabila la Lawi) ndilo lililokabidhiwa shughuli zote za kikuhani, yaani shughuli za kufanya upatanisho kwa ajili ya dhambi zote za wana wa Israeli.
Kutokana na upingamizi mkali wa wana wa Israeli dhidi ya uongozi wa Mtumishi wa Mungu, Haruni mara kadhaa alijaribu kuvutwa na ushawishi wao. Na hivyo wakati Fulani kufikia hatua ya kukubali kuwatengenezea sanamu ya ndama (Kutoka 32:1-5).
Haruni naye hakufika nchi ya Ahadi, kutokana na dhambi waliyoitenda wao na Musa ya kujichukulia utukufu mbele ya Wana wa Israeli.(Hesabu 20:10,24) Hivyo alikufa akiwa jangwani akiwa mzee sana.
Pamoja na mambo mengi yasiyofaa tusiyoweza kujifunza kutoka kwake, kama kuungana na Wana wa Israeli kutengeneza ile sanamu ya ndama… lakini bado Haruni alikuwa ni mtu mwenye ujasiri mwingi kuliko Musa..Wakati Musa anasita sita kwenda kuzungumza na Farao..yeye alichukua nafasi yake kwa kuuvaa ujasiri uliotoka kwa Mungu..
Na jambo lingine la Muhimu ni nafasi ya ukuhani aliyopewa na Mungu..Musa hakupewa nafasi ya ukuhani isipokuwa Haruni na wanawe..Nafasi ya ukuhani inafananishwa na nafasi ya YESU KRISTO, Kama Kuhani Mkuu…Hivyo alisimama kama Kuhani Mkuu wa Mungu kwaajili ya wana wa Israeli. Na Yesu Kristo kama Kuhani mkuu wa wanadamu wote.
Bwana akubariki. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Musa alizaliwa huko Misri, miaka mingi kidogo baada ya Yusufu mwana wa Yakobo kufariki. Wakati wa kuzaliwa kwake, mama yake alimhifadhi mtoni kutokana na hofu ya amri ya Mfalme juu ya kuuawa kwa wazaliwa wote wa jinsia ya kiume.
Jina la Baba yake Musa ni Amramu na Mama yake ni Yokebedi. (Hesabu 26:59).
Musa alikuwa na Kaka yake wa damu aliyeitwa Haruni waliokuwa wamepishana miaka 3, Haruni alikuwa mkubwa kwa Musa, na ndiye yule aliyekuja kuwa Kuhani Mkuu, pia alikuwa na dada yake aliyeitwa Miriamu ambaye naye pia alikuwa ni Nabii wa Bwana.
Bithiani aliyekuwa Binti wa Farao alimwokota akiwa kwenye kijisafina kidogo, pembezoni mwa mto wakati akiwa anaoga. Musa aliishi katika Nyumba ya kifalme mpaka alipofikisha umri wa miaka 40, Baadaye aliasi nyumba ya Farao kutokana na kumsaidia mmoja wa ndugu zake wa Kiebrania, akakimbilia nchi ya Midiani. Huko alipata mke kutoka kwenye nyumba ya kuhani mmoja wa Midiani aliyeitwa Yethro.
Alikaa miaka 40 nyumbani kwa Yethro, akichunga mifugo yake, mpaka siku moja Bwana alipomtokea katika mwali wa moto, ndani ya kile kijiti, alipokuwa anachunga kundi la Yethro, Alipewa maagizo ya kuwaokoa Israeli waliokuwa wanateswa chini ya utawala mkali wa Farao.
Kwa Ishara nyingi na miujiza mingi Musa aliwaongoza wana wa Israeli miaka 40 mingine, na Alifariki akiwa na miaka 120, akiwa na nguvu zake zote. Macho yake hayakupofuka wala mwili haukupungua nguvu (Kumbukumbu 34:7)
Musa pekee ndiye Nabii aliyezungumza na Mungu uso kwa uso, wala baada yake hakuinuka nabii mfano wake yeye (Kumbukumbu 34:10-12)
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
1.Utaji uliokuwepo juu ya uso wa Musa ulikuwa unaashiria nini?
Yezebeli, alikuwa ni Binti wa Mfalme wa Wasidoni aliyeitwa Ethbaali (1 Wafalme 16:31). Sidoni ilikuwa ni nchi iliyokuwepo Kaskazini mwa Taifa la Israeli, kwasasa nchi hiyo ni nchi ya LEBANONI.
Desturi za Wasidoni zilikuwa ni kuabudu miungu, waliabudu mungu wao maarufu aliyeitwa BAALI.
Mfalme wa Israeli aliyeitwa Ahabu alimwoa Binti huyo wa kifalme na kumleta katika Taifa la Israeli na kuwa Malkia. Na hivyo kuingiza ibada za miungu migeni ndani ya Taifa la Mungu.
Yezebeli licha tu ya kulichafua Taifa la Israeli kwa kumshawishi sana Mumewe Ahabu, alikuwa pia ni mchawi (2 Wafalme 9:22). Aliwaua manabii wengi wa kweli wa Mungu, na aliikosesha Israeli kwa sehemu kubwa sana. Mahali pengine Inamtaja Yezebeli kuwa ni Nabii wa Uongo. (Ufunuo 2:20)
Yezebeli pia ndio mwanamke pekee kwenye Biblia nzima aliyekuwa anapaka WANJA usoni na kupamba uso. Desturi za wanawake makahaba.(2 Wafalme 9:30). Mwanamke huyu ndiye Mwanamke pekee aliyeshindana na maagizo ya Mungu kuliko wanawake wote kwenye Biblia, ndiye aliyemsumbua sana Eliya na hata kufikia hatua Nabii Eliya kumkimbia, kuogopa madhara atakayoyapata kutoka kwake.
Yezebeli alikuwa na mtoto wa kike, aliyeitwa ATHALIA ambaye naye alirithi tabia zote za mama yake ambaye naye pia alikuwa anaabudu Baali, Athalia alikuwa muuaji na aliutwaa umalkia kwa nguvu ndani ya kabila la YUDA.
Yezebeli hakudumu muda mrefu kwani alikufa sawasawa na unabii uliotolewa juu yake, kwamba atakufa na mbwa watalamba damu yake. Siku ya kufa Yezebeli aliangushwa kutoka juu ya ghorofa refu na kuchuruza damu ukutani mwote, na alipofika chini farasi alimkanyaga kanyaga..na Mbwa walikumla na kubakisha viganja tu vya mikono na kifuvu (2 Wafalme 9:35)
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Shetani ni nani?…Tafsiri ya Jina shetani ni ‘mshitaki’ au ‘mchongezi’. Kazi yake ni kuwashitaki watakatifu mbele za Mungu.
Jina lingine la shetani ni “LUSIFA” Maana yake ‘NYOTA YA ALFAJIRI’. (Isaya 14:12) Jina hili Lusifa aliitwa kabla hajaasi, baada ya kuasi ndio akawa shetani.
Alikuwa ni Malaika wa Sifa (Kerubi) huko mbinguni, alikuwa ni Mzuri kwa mwonekano na mkamilifu katika njia zake zote, aliishi katika taratibu za Mungu, na katika njia za Mungu, na hivyo akapata heshima kubwa mbinguni zaidi ya Malaika wengi (Ezekieli 28:14).. Alikuwa mkamilifu mpaka siku uovu ulipoonekana ndani yake (Ezekieli 28:15).
Kwasababu ya uzuri wake Moyo wake ukainuka, akataka kujiinua awe kama Mungu, aabudiwe kama Mungu na kwa ujuzi wake mwingi akawashawishi theluthi ya Malaika mbinguni (1/3) waambatane naye.
Vita, vikali vikatokea Mbinguni kati ya Malaika waliokataa kuungana na Lusifa na malaika waliokubali kuungana naye. Biblia haisema vita hivyo vilipiganwa kwa muda gani, lakini inasema mwisho wa siku lusifa pamoja na malaika wake walishindwa vita vile, na kutupwa chini duniani (Ufunuo 12:7).
Na vita hivyo bado havijaisha, vita vya kwanza vilipiganwa mbunguni, kati ya Malaika walio upande wa shetani na wale walio upande wa Mungu na Malaika waliokuwepo Upande wa Mungu wakavishinda, lakini vita vya pili na vya mwisho vinapiganwa hapa duniani na hata sasa bado vinaendelea..Na vitaisha mwisho wa dunia. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
1. Je! Ni nani aliyemdanganya shetani?
2. Huduma 10 za shetani sasahivi duniani ni zipi?
3. Mpango wa shetani kwa watoto katika siku hizi za mwisho.
4. Agenda kubwa ya shetani kwa kanisa hili la siku za mwisho
5. Mafundisho ya Mashetani ni yapi katika siku hizi za mwisho?
Malaki 4:5 kama inasema “ angalieni nitawapelekea Eliya Nabii, kabla haijaja siku ile ya BWANA, iliyo kuu na ya kuogfya. Naye ataigeuza mioyo ya Baba iwaelekee watoto wao na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana.”
Kama Mungu alivyoahidi angemtua Eliya nabii. ambaye kulingana na maandiko tunafahamu Yohana mbatizaji aliyatimiza hayo maandiko ( Yaani kuja kabla ya ile siku KUU YA BWANA) ambaye yeye alitangulia kuja kwake Kristo kwa mara ya kwanza kwa kusudi la kuigeuza Mioyo ya Baba iwaelekee Watoto.
Hii inamaanisha kwamba Yohana alihubiri injili ya kuwarejeza waalimu wa sheria na marabi wa torati pamoja na wote wanaoujia torati na kuifuatilia (ambao ndio mababa wa Torati) ili waiamini injili ya Kristo.
Na tonaona…Baadhi ya wanafunzi wake mwenyewe Yohana, waliiamini Injili yake na baadaye hao hao wakaja kuwa wanafunzi wa Yesu Kristo, (mfano Andrea na Yohana) ambao walikuwa hapo kwanza wanafunzi wa Yohana Mbatizaji lakini wakaja kuwa wanafunzi wa Bwana Yesu..na ndio sasa mababa wetu wa Imani ya Kikristo leo.
Hivyo Yohana mbatizaji kazi aliyoifanya ni kuwageuza Mababa wa Torati kuwa Mababa wa Imani ya Kristo na mioyo ya watoto iwaelekee mababa.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Yohana Mbatizaji alizaliwa huko Uyahudi miezi michache kabla ya kuzaliwa Mwokozi wa Ulimwengu Yesu Kristo, Baba yake mzazi aliitwa Zekaria aliyekuwa Mlawi, ambaye alikuwa ni kuhani, akihudumu katika Nyumba ya Mungu illiyokuwepo huko Yerusalemu…Mama yake aliitwa Elizabeth ambaye alikuwa ana undugu wa karibu na Bikira Mariamu mama yake Yesu.
Habari za kuzaliwa kwake kimiujiza, zinapatikana kwa urefu katika kitabu cha (Luka 1:1-60).
Maandiko yanasema Yohana Mbatizaji alijazwa Roho Mtakatifu tangu akiwa tumboni mwa mama yake (Luka 1:15). Na inasadikiwa kuwa miaka michache sana baada ya kuzaliwa kwake wazazi wake wote wawili walifariki. Na hivyo akaondoka na kwenda kukaa majangwani, mpaka siku alipotokea tena hadharani kuhubiri habari za msamaha na toba.
Aliitwa Yohana Mbatizaji kutokana na ufunuo alioupata wa ubatizo. Hapo kabla kulikuwa hakuna mwingine aliyekuwa anafanya ubatizo Zaidi yake, ndio maana alijulikana kama Yohana Mbatizaji, kumtofautisha na wakina Yohana wengine.
Yohana Mbatizaji sio Yohana yule aliyeandika kitabu cha Ufunuo, aliyeandika kitabu cha Ufunuo ni Yohana aliyekuwa mwanafunzi wake Yesu. Yohana Mbatizaji hakuandika kitabu chochote katika Biblia
Yohana Mbatizaji, maandiko yanasema alikuwa ndiye Eliya aliyetabiriwa atakayekuja kumtengenezea Bwana Njia (Luka 1:17). Atakayeigeuza mioyo ya baba iwaelekee Watoto.
1. Yohana Mbatizaji anaigeuzaje mioyo ya mababa iwaelekee watoto?
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Tofauti na inavyodhaniwa na wengi kuwa Nabii Eliya mwenyewe ndiye atakayerudi.
Ili kuelewa vizuri juu ya jambo hilo hebu tafakari mfano ufuatao.
Ametokea kiongozi mmoja mashuhuri sana wa mambo ya kisiasa na akaleta mabadiliko makubwa sana katika taifa hilo, tuchukulie mfano Aliyekuwa Raisi wa Taifa la Tanzania, Hayati J. K. Nyerere baada ya kufa kwake, mwananchi mmoja akatabiri, Miaka ya huko mbeleni watazaliwa wakina Nyerere wengi ambao watafanya kama alivyofanya Baba wa Taifa.
Je! kwa sentensi hiyo ni sawa na kusema, Nyerere atazaliwa tena yule yule aliyefariki na kuishi na kuja kuwa Raisi tena?..Ni wazi kuwa hiyo siyo tafsiri yake, tafsiri yake ni kwamba atazaliwa au watazaliwa watu ambao watakuja kuwa mashujaa kama Nyerere
Na ndivyo ilivyo kwa unabii wa ujio wa Eliya, sio kwamba ni Eliya yule yule atazaliwa tena hapana bali atakuja mtu au watu watakaobeba huduma inayofanana na ya Eliya.
Na mtu wa Kwanza aliyeibeba huduma hiyo baada ya Eliya mwenyewe alikuwa ni Nabii Elisha na baada ya Elisha alifuata Yohana Mbatizaji..