Isaya 50:8 “Yeye anipatiaye haki yangu yu karibu; ni nani atakayeshindana nami? Na tusimame pamoja; ni nani aliye HASIMU yangu? Na anikaribie basi”.
“Hasimu” maana yake ni “mpinzani”…Kwahiyo andiko hilo kwa lugha nyingine laweza kusomeka hivi…
Isaya 50:8 “Yeye anipatiaye haki yangu yu karibu; ni nani atakayeshindana nami? Na tusimame pamoja; ni nani aliye MPINZANI WANGU? Na anikaribie basi”.
Andiko hili linaelezea nguvu wanayotembea nayo watu wa MUNGU, kwamba wanao ulinzi mkubwa zaidi ya wote na wanao utetezi mkubwa zaidi ya wenngine wote, kwasababu mbingu inawatetea daima.
Warumi 8:31 “Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu?”.
Je na wewe umezungukwa na Mahasimu? Je mtetezi wako ni nani katikati ya hao?.
Ni heri Mtetezi wako akawa YESU leo, kwasababu wanadamu wala mashetani hayawezi kukutetea wakati wa matatizo bali yatakuwa Mahasimu wako tu siku zote.
Bwana atusaidie.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Print this post
Je Mkristo, anapaswa KULEWA?..
Jibu ni NDIO! Anapaswa alewe lakini si kwa MVINYO (yaani kwa pombe)… bali kwa ROHO MTAKATIFU.
Waefeso 5:18 “Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; BALI MJAZWE ROHO”
Roho Mtakatifu ni Kilevi cha Mkristo, ni lazima sote tujae Roho Mtakatifu katika kiwango cha KULEWA KABISA!!.
Ndio maana ile siku ya Pentekoste watu walipopokea ujazo Roho Mtakatifu na kuanza kunena kwa lugha mpya walisomeka kama “Walevi wa mvinyo mpya” mbele ya waliowasikia.
Matendo 2:12 “Wakashangaa wote wakaingiwa na shaka, wakiambiana, Maana yake nini mambo haya? 13 Wengine walidhihaki, wakisema, WAMELEWA KWA MVINYO MPYA. 14 Lakini Petro akasimama pamoja na wale kumi na mmoja, akapaza sauti yake, akawaambia, Enyi watu wa Uyahudi, na ninyi nyote mkaao Yerusalemu, lijueni jambo hili, mkasikilize maneno yangu. 15 Sivyo mnavyodhani; watu hawa hawakulewa, kwa maana ni saa tatu ya mchana; 16 lakini jambo hili ni lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Yoeli, 17 Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote ROHO YANGU, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto. 18 Naam, na siku zile nitawamwagia watumishi wangu wanaume na wanawake ROHO YANGU, NAO WATATABIRI”.
Matendo 2:12 “Wakashangaa wote wakaingiwa na shaka, wakiambiana, Maana yake nini mambo haya?
13 Wengine walidhihaki, wakisema, WAMELEWA KWA MVINYO MPYA.
14 Lakini Petro akasimama pamoja na wale kumi na mmoja, akapaza sauti yake, akawaambia, Enyi watu wa Uyahudi, na ninyi nyote mkaao Yerusalemu, lijueni jambo hili, mkasikilize maneno yangu.
15 Sivyo mnavyodhani; watu hawa hawakulewa, kwa maana ni saa tatu ya mchana;
16 lakini jambo hili ni lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Yoeli,
17 Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote ROHO YANGU, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto.
18 Naam, na siku zile nitawamwagia watumishi wangu wanaume na wanawake ROHO YANGU, NAO WATATABIRI”.
Umeona?…Mitume walipopokea ujazo wa Roho Mtakatifu walionekana ni walevi.
Ni kweli kabisa walilewa lakini si kwa mvinyo bali Roho Mtakatifu.
Na maandiko yanazidi kutuonyesha kuwa Roho Mtakatifu, TUNAMNYWA!!.. Ni kinywaji tunachokinywa, na kila kilevi lakini si cha kidunia bali cha kimbinguni.
1 Wakorintho 12:13 “Kwa maana katika ROHO MMOJA sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote TULINYWESHWA ROHO MMOJA”.
Sasa sifa za Mlevi ni zipi?
1. UJASIRI.
Mlevi anapolewa huwa kiwango chake cha ujasiri kinapanda..utaona mtu akishakunywa basi atakuwa anaongea neno lolote linakuja kinywani mwake bila haya, hiyo ni sifa mojawapo ya mlevi.
Na halikadhalika mtu aliyejazwa Roho Mtakatifu, huwa anakuwa ana ujasiri mkuu kuzungumza lolote kuhusu ufalme wa MUNGU aoni aibu, ndivyo tunavyosoma pia katika maandiko..
Matendo 4:31 “Hata walipokwisha kumwomba Mungu, mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri”
Hivyo kama umelewa na Roho Mtakatifu basi utaona ujasiri wa kuzungumza habari za Ufalme wa MUNGU pia unaongezeka, ujasiri wa kukemea dhambi unaongezeka, ujasiri wa kusifia mema pia unaongezeka.
2. GANZI
Mtu mlevi, akishalewa anaweza kulala popote hata mtaroni, wala hasikii baridi na wala wadudu kama mbu hawamsogelei, kwanini?..ni kwasababu mwili wake umepata ganzi.
Hali kadhalika mtu aliyejawa na Roho Mtakatifu huwa anapata ganzi katika utumishi, maana yake mazingira yoyote anaweza kwenda katika utumishi wake bali kuona shida mfano wa mtumishi wa Mhngu Mtume Paulo.
2 Wakorintho 11:23 “Wao ni wahudumu wa Kristo? (Nanena kiwazimu), mimi ni zaidi; katika taabu kuzidi sana; katika vifungo kuzidi sana; katika mapigo kupita kiasi; katika mauti mara nyingi. 24 Kwa Wayahudi mara tano nalipata mapigo arobaini kasoro moja. 25 Mara tatu nalipigwa kwa bakora; mara moja nalipigwa kwa mawe; mara tatu nalivunjikiwa jahazi; kuchwa kucha nimepata kukaa kilindini; 26 katika kusafiri mara nyingi; hatari za mito; hatari za wanyang’anyi; hatari kwa taifa langu; hatari kwa mataifa mengine; hatari za mjini; hatari za jangwani; hatari za baharini; hatari kwa ndugu za uongo; 27 katika taabu na masumbufu; katika kukesha mara nyingi; katika njaa na kiu; katika kufunga mara nyingi; katika baridi na kuwa uchi”.
2 Wakorintho 11:23 “Wao ni wahudumu wa Kristo? (Nanena kiwazimu), mimi ni zaidi; katika taabu kuzidi sana; katika vifungo kuzidi sana; katika mapigo kupita kiasi; katika mauti mara nyingi.
24 Kwa Wayahudi mara tano nalipata mapigo arobaini kasoro moja.
25 Mara tatu nalipigwa kwa bakora; mara moja nalipigwa kwa mawe; mara tatu nalivunjikiwa jahazi; kuchwa kucha nimepata kukaa kilindini;
26 katika kusafiri mara nyingi; hatari za mito; hatari za wanyang’anyi; hatari kwa taifa langu; hatari kwa mataifa mengine; hatari za mjini; hatari za jangwani; hatari za baharini; hatari kwa ndugu za uongo;
27 katika taabu na masumbufu; katika kukesha mara nyingi; katika njaa na kiu; katika kufunga mara nyingi; katika baridi na kuwa uchi”.
Nasi ni lazima tufe ganzi katika mwili wakati wa kuhubiri injili.
2 Timotheo 4:2 “lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho”.
3.KUNYWA KILA SIKU.
Mlevi halisi haiwezi kupita wiki bila kulewa, atahisi kuumwa!…ni lazima ajaze tanki lake karibia kila siku ili ajisikie vizuri..
Vile vile Mlevi wa Roho Mtakatifu ni lazima ajazwe Roho Mtakatifu karibu kila siku na Roho Mtakatifu anajaa ndani ya watu kwa njia ya maombi na kumsifu MUNGU.
Luka 11:13 “Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?”
Hivyo maisha ya maombi kwa mtu aliyejaa Roho mtakatifu, yanapaswa yawe sehemu yake daima.
Swali ni je na wewe umeleweshwa na kiti gani??..Ni dhambi? Au Roho Mtakatifu??….Fahamu kuwa ulevi wa pombe matokeo yake ni ufisadi sawasawa na Waefeso 5:18 na hivyo ni upotevu.
Mpokee leo YESU kama bado haujampokea na Ujazwe Roho mtakatifu.
Bwana YESU akubariki sanWashirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Warumi 8:37 “Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda”
Upo ushindi, lakini pia Upo “Ushindi ulio zaidi ya ushindi”
Unaposhindana na Mtu/Watu na kuwashinda hapo unahesabika kuwa ni “Mshindi”.
Hali kadhalika unaposhindana na mashetani/mapepo na kuyashinda hapo unahesabika kuwa ni “Mshindi”.
Lakini unaposhindana na “MUNGU WA MBINGU NA NCHI” na kumshinda huo ni “Zaidi ya ushindi”
Utauliza kivipi?. Je mtu anaweza kushindana na MUNGU aliyemwumba na kumshinda?..jibu ni ndio!.
Yakobo alishindana na watu na MUNGU na kumshinda..
Mwanzo 32:27 “Akamwuliza, Jina lako n’nani? Akasema, Yakobo. 28 Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda”.
Mwanzo 32:27 “Akamwuliza, Jina lako n’nani? Akasema, Yakobo.
28 Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda”.
Tafsiri ya jina “Israeli” ni “Mshindi”..
Yakobo alizishindani baraka za MUNGU na kuziteka, alishavuka viwango vya kupambana na watu, sasa yupo viwango vya kupambana na MUNGU na kushinda…huyo huwezi kumwita tena mshindi, ni zaidi ya Mshindi.
Kadhalika walio ndani ya YESU kikwelikweli ni “Zaidi ya Washindi” Ni Israeli kwelikweli…wamevuka viwango vya kupambana na watu, wapo viwango vya kupambana na MUNGU na kuteka baraka zao.
Waefeso 3:20 “Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu”
Waliookoka kweli kweli hawana muda na wachawi, kwasababu hao tayari wamewashinda..
Hawana muda na wanadamu wabaya, kwasababu tayari wameshawashinda katika ulimwengu wa roho, lakini wenyewe wana muda na MUNGU na baraka zake, wanazishindania hizo, na wanaposhinda hawaitwi tena washindi, bali Zaidi ya washindi! Haleluya.
Na kumbuka ushindi huu usio na maelezo upo ndani ya mmoja tu ambaye ni YESU KRISTO, na si kwa mwingine..
1 Wakorintho 15:57 “Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo”
Hiyo ndio faida ya kuwa ndani ya YESU…
Wachawi hawawezi kukushinda ukiwa ndani ya YESU, Mapepo hayawezi kukushinda ukiwa ndani ya YESU, Watu wanaoshindana nawe hawawezi kukushinda ukiwa ndani ya YESU.
Dhambi haiwezi kukushinda ukiwa ndani ya YESU, Zaidi sana na (mashetani, watu na viumbe vingine vyote), ambavyo vinafanya vita nawe pasipo wewe kujua haviwezi kukushinda, kwasababu wewe ni mshindi na zaidi ya Mshindi.
Unaingiaje katika huu Ushindi?..Kwanza kwa kumwamini Bwana YESU, na kutubu kwa kumaanisha kuacha dhambi, na kubatizwa kisha kupokea ujazo wa Roho Mtakatifu.
Maisha ya mwilini mara nyingi hubeba mafundisho ya rohoni, ndio maana Bwana Yesu alitumia sana mifano ya kidunia kuwafundisha siri za ufalme wa mbinguni.
Katika jamii ili mtu aitwe profesa au daktari(kitaaluma) anapaswa awe ni msomi wa kukaa darasani kwa muda mrefu, awe na ujuzi lakini pia na uzoefu wa tafiti nyingi..yaani kwa ufupi haiwezekani ukaitwa daktari(kitaaluma) halafu usiwe msomi wa elimu za juu.
Lakini kuna udaktari ambao mtu anaweza kupewa kwa kutunikiwa, na mara nyingi huu huja pale mtu anapotoa mchango fulani mkubwa katika jamii…mtu kama huyu anaweza kutunukiwa udaktari hata kama yale mafunzo ya ndani ya kitaaluma hana.
Sasa kiroho ni vivyo hivyo unaweza pia ukawa mkufunzi, mwenye ukomavu mkubwa, zaidi ya mababa zako wa kiroho, hata zaidi ya wachungaji wako, au maaskofu wako, au wazee wako wa kiimani, kwa namna gani?
Mstari ufuatao unatupa jibu;
Zaburi 119:99-100
[99]Ninazo akili kuliko wakufunzi wangu wote, Maana shuhuda zako ndizo nizifikirizo. Ninao ufahamu kuliko wazee, Kwa kuwa nimeyashika mausia yako.
[99]Ninazo akili kuliko wakufunzi wangu wote,
Maana shuhuda zako ndizo nizifikirizo. Ninao ufahamu kuliko wazee, Kwa kuwa nimeyashika mausia yako.
Ukitafakari huo mistari, utaona ni mwanafunzi anayejisifia kuwa ana akili zaidi ya waalimu wake…sio kwamba ameshahitimu, hapana bado yupo chini ya waalimu wake lakini akili zake zimewapita, bado ni kijana lakini ufahamu wake umeshawazidi wazee wake.
Imewezekanikaje?
JE anasoma sana? Au ana kiwapa cha asili tofauti na wengine? Hapana…anasema kwasababu shuhuda za Mungu ndizo anazozitafakari, lakini pia anayashika mahusia ya Mungu .
Hiyo ndio siri yake, usiku na mchana ni kufikiri juu ya “KWELI”, Yaani Neno la Mungu, na na namna ya kulifanya kuwa sehemu ya maisha yake..(kujiepusha na dhambi.)
Hiyo ndio namna inayomkomaza mtu kiroho kwa haraka sana kuliko hata maarifa mengi ambayo wengi hudhani, au mafunuo mengi, au kuhubiri kwingi, au kufundisha kwingi…
Mtu mmoja anaweza akawa na uelewa mkubwa, mwalimu mzuri, mtume mwenye ushawishi mkubwa, lakini bado asimkute mwanafunzi wake ambaye maisha yake anajitahidi kuliishi Neno la Mungu.
Hivyo ndivyo Mungu anavyowatambua wakufunzi wake (kiroho), uwezo wa “kumcha Mungu” haijalishi utapoteza sifa nyingine zote za maarifa,mafunuo, lakini akiwa na hiyo huyo amefika mbali sana.
Kwasababu Biblia inasema hakuna mwisho wa usomi, (kujua maarifa), ila mtu akizingatia kumcha Mungu na kuziishika amri zake, ni zaidi ya usomi wa vitabu vyote.
Mhubiri 12:12-13
[12]Tena, zaidi ya hayo, mwanangu, kubali maonyo; hakuna mwisho wo wote wa kutunga vitabu vingi; na kusoma sana huuchosha mwili. [13]Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.
[12]Tena, zaidi ya hayo, mwanangu, kubali maonyo; hakuna mwisho wo wote wa kutunga vitabu vingi; na kusoma sana huuchosha mwili.
[13]Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa;
Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.
Tuwekeze nguvu zetu zote katika kuliishi Neno na neema ya Mungu itusaidie..
JE! UNATAKA UITWE MSOMI NA MUNGU?
USIKWEPE CHUO CHA UTAKATIFU.
HAWEZI KUWA MWANAFUNZI WANGU.
Nakusalimu katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo, karibu katika kuyatafakari maneno ya uzima
Tengeneza picha Mungu amekutokea amesimama mbele yako, wakati ukiwa na mawazo ya kumwangukia chini umsujudie, unashangaa yeye moja kwa moja anakuwa wa kwanza kuinama na kukusafisha miguu yako…
Hivi utajisikiaje? Ukweli ni kwamba hutajisikia huru hata kidogo, kwa ufupi hutakubali kitendo hicho kifanywe na yeye kutoka na ukuu wake, na heshima yake iliyozidi vyote, ni sawa na uone baba amemnunulia mtoto wake zawadi halafu yeye ndio anayekuwa wa kwanza kumshukuru mtoto, tena kwa kumwinamia..ni wazi kuwa hilo halijakaa sawa, au mtu aliyeibiwa mali zake nyingi, halafu amekutana na aliyemwibia badala ya mwenye mali kungojea kuombwa msamaha, yeye ndio anajionyesha kama ni mkosaji kwake…unaona ni jambo ambalo halina uhalisia, halikubaliki kifikra hata kidogo…
Kwa namna ya kawaida hali kama hizi akitendewa mtu hawezi kuridhia…lakini Mungu anatutendea sisi na anasema kama hutakubali kutendewa naye hivyo kamwe hutuna ushirika naye.
Ndicho kilichotokea kwa mitume na Petro. Wakati ule walipomwona Bwana Yesu, anashika kitambaa na maji kisha akaanza kuwaosha na kuwapangusa miguu yao…Petro hakuweza kuridhia akasema Bwana hutanitawadha miguu kamwe. Lakini Yesu akamwambia usipokubali huna ushirika nami.
Yohana 13:8
[8]Petro akamwambia, Wewe hutanitawadha miguu kamwe. Yesu akamwambia, Kama nisipokutawadha, huna shirika nami.
Hii ni kufunua nini…
Ni lazima tumjue Kristo, ni kweli anasimama kwetu kama mfalme, kama Bwana, kama Mungu…tunamwabudu…lakini pia anasimama kama mtumishi wetu..Ni jambo ambalo hatuwezi kuingia akilini lakini ndivyo alivyo, amependa yeye kuwa hivyo kwetu.
Ni mfalme mwenye taji la kifalme lakini wakati huo huo pia mfalme aliyebeba kitambaa cha kuwasafisha watu miguu.
Hiyo ndio sifa ya ufalme wake. Amesimama kama muumba wetu tumwabuduye, lakini pia anatutumikia, katika kutuponya magonjwa yetu, kutulisha, kutuvisha, kutuombea, kutulinda, kutufuta machozi, na kuchukua mizigo yetu mfano wa punda na hata kufanya mambo ambayo sisi hatuwezi stahimili akitufunulia yote kwa jinsi anavyojishusha na kujishughulisha sana na mambo yetu…. Na mfano tukitataa yeye asituhudumie hivyo anasema wazi kuwa hatuna ushirika naye.
Maana yake ni fahari yake kututendea hayo, wala yeye hayahesabu kuwa ni kitu.
Anatufundisha nini?
Tuwe watumishi pia wa wengine kwa namna hiyo, kama yeye alivyo kwetu…kujitoa kwake sio kutimiza wajibu bali ni fahari yake ambayo isipokubaliwa inaharibu moja kwa moja mahusiano.
Kumsaidia mpendwa mwenzako iwe ni furaha..kujinyenyekeza kwake isiwe ni sababu za umri au cheo bali fahari..Kumwombea iwe ni fahari yako, kumsikiliza iwe ni furaha yako…hivyo ndivyo Bwana anavyotaka.. na ndivyo alivyomwambia Petro.
Yohana 13:12-17
[12]Basi alipokwisha kuwatawadha miguu, na kuyatwaa mavazi yake, na kuketi tena, akawaambia, Je! Mmeelewa na hayo niliyowatendea? [13]Ninyi mwaniita, Mwalimu, na, Bwana; nanyi mwanena vema, maana ndivyo nilivyo. [14]Basi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu, nimewatawadha miguu, imewapasa vivyo kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi. [15]Kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo. [16]Amin, amin, nawaambia ninyi, Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake; wala mtume si mkuu kuliko yeye aliyempeleka. [17]Mkiyajua hayo, heri ninyi mkiyatenda.
[12]Basi alipokwisha kuwatawadha miguu, na kuyatwaa mavazi yake, na kuketi tena, akawaambia, Je! Mmeelewa na hayo niliyowatendea?
[13]Ninyi mwaniita, Mwalimu, na, Bwana; nanyi mwanena vema, maana ndivyo nilivyo.
[14]Basi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu, nimewatawadha miguu, imewapasa vivyo kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi.
[15]Kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo.
[16]Amin, amin, nawaambia ninyi, Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake; wala mtume si mkuu kuliko yeye aliyempeleka.
[17]Mkiyajua hayo, heri ninyi mkiyatenda.
Neema ya Bwana itusaidie.
Shalom.
WEWE NI ZAO LA MAHUSIANO NA USHIRIKA.
USHIRIKA WA ROHO MTAKATIFU UKAE NANYI NYOTE.
WENGINE WANAKESHA KWAAJILI YAKO.
Jibu: Turejee..
Matendo 15:40 “Lakini Paulo akamchagua Sila, akaondoka, akiombewa na wale ndugu apewe neema ya Bwana. 41 Akapita katika Shamu na Kilikia AKIYATHIBITISHA MAKANISA”.
Matendo 15:40 “Lakini Paulo akamchagua Sila, akaondoka, akiombewa na wale ndugu apewe neema ya Bwana.
41 Akapita katika Shamu na Kilikia AKIYATHIBITISHA MAKANISA”.
Tunasoma pia akiwathibitisha Wanafunzi katika Matendo 18:23
Sasa maana ya “kuyathibitisha Makanisa na Wanafunzi” ni Ziara za kuwatembelea wanafunzi/waamini ambao tayari wameshapokea Injili, na kuwatia Nguvu katika Imani, kwa njia ya kuwafundisha na kuwakumbusha kanuni za Imani ya kikristo na kudumu katika misingi huo.
Vile vile katika kutatua changamoto zilizokuwa ngumu kutatulika na pia na kuwateua Maaskofu na Mashemasi katikati ya waamini hao, watakaowachunga na kuliangalia kundi..
Kwa mfano tunasoma katika Matendo 14:21-22, Mtume Paulo na wenzake wakirejea Listra, Ikonio na Antiokia kufanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika ile Imani..
Matendo 14:21 “Hata walipokwisha kuihubiri Injili katika mji ule, na kupata wanafunzi wengi, wakarejea mpaka Listra na Ikonio na Antiokia, 22 wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika ile Imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi. 23 Na walipokwisha kuwachagulia wazee katika kila kanisa, na kuomba pamoja na kufunga, wakawaweka katika mikono ya Bwana waliyemwamini”
Matendo 14:21 “Hata walipokwisha kuihubiri Injili katika mji ule, na kupata wanafunzi wengi, wakarejea mpaka Listra na Ikonio na Antiokia,
22 wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika ile Imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi.
23 Na walipokwisha kuwachagulia wazee katika kila kanisa, na kuomba pamoja na kufunga, wakawaweka katika mikono ya Bwana waliyemwamini”
Utasoma pia katika Matendo Tito 1:5, akiagiza uteuzi wa viongozi watakaoliangalia kundi.
Tito 1:5 “Kwa sababu hii nalikuacha Krete, ili uyatengeneze yaliyopunguka, na kuweka wazee katika kila mji kama vile nilivyokuamuru”
Mambo kama hayo pia tunapaswa kuyafanya sasahivi, Katika siku hizi za mwisho ambapo shetani anafanya kazi kwa nguvu kuyaharibu makanisa, hatuna budi kusimama kwa nguvu na kuyathibitisha makanisa yetu kwa msaada wa MUNGU.
Kwanini Roho Mtakatifu amzuie Paulo kuipeleka injili Asia? (Matendo 16:6-7).
Je Paulo, alihimiza kusikiliza nyimbo za kidunia kulingana na Matendo 17:28
Paulo aliwapaje watu karama ya rohoni?
Uchambuzi wa kitabu cha pili cha Paulo kwa Timotheo (2Timotheo).
WhatsApp
Isaya 1:8 “Na binti Sayuni ameachwa kama kibanda katika shamba la mizabibu, kama KIPENU katika shamba la matango, kama mji uliohusuriwa”.
“Kipenu” ni kijumba kidogo kinachojengwa katikati ya Shamba, kinachomsitiri mlinzi wakati wa kulinda mazao shambani..
Ili kuzuia wezi wa mazao, na wanyama kama nyani, ngedere na wengineo pamoja na ndege inawalazimu wakulima kuweka walinzi mashambani, ili kuyaangalia mazao hayo, sasa kile kijumba cha walinzi, ambacho kinajengwa kwa ubora wa chini kwa kusudi hilo, ndicho kinachoitwa “Kipenu”.
Mara nyingi kijumba hiki, pale ambapo uvunaji umemalizika, huwa kinabaki chenyewe shambani wala hakuna mtu anakithamini tena, wanyama wanaweza kufanya makao huko na hakina thamani tena…… hali hii ya kipenu kusalia chenyewe shambani, na kupoteza uthamani wake ndio Bwana MUNGU anafananisha na jinsi Mji wa Yerusalemu (yaani binti Sayuni) ulivyoachwa..
Kutokana na maovu kuwa mengi Yerusalemu, na Bwana aliwaacha, na mji wao kubaki mpweke kama kipenu, na hivyo hatari yoyote inaweza kuukabili, na ndicho kilichotekea wakati ulipofika Yerusalemu uliachwa kama Kipenu na Nebukadreza, mfalme wa Babeli aliuhusuru na kuuharibu na kuwachukua wenyeji mateka.
Hata sasa tunapomwacha MUNGU, tunakuwa kama Kipenu katikati ya shamba lililokwisha kuvunwa. Nyumba zetu zitakuwa kipenu, roho zetu zitakuwa kama kipenu, biashara zetu zitakuwa kama kipenu na mambo yetu mengine yote yatafananishwa na vipenu.
Hautaweza kuilinda roho yako, wala nyumba yako kama utakuwa nje ya Kristo, ni lazima tu uharibifu wako utafika ghafla siku moja, Mwanadamu ameumbwa kumtegemea MUNGU siku zote, kamwe hawezi kuishi kwa kujitegemea mwenyewe, ni jambo ambalo haliwezekani na gumu sana. Bwana tu ndiye tegemeo letu na ngao yetu.
Zaburi 144:2“Mhisani wangu na boma langu, Ngome yangu na mwokozi wangu, Ngao yangu niliyemkimbilia, Huwatiisha watu wangu chini yangu”.
Bwana atubariki.
AKAPITA KATIKA LILE SHAMBA AMBALO YAKOBO ALIMPA YUSUFU MWANAWE
MAVUNO YAMESHAKWISHA SHAMBANI.
USIWE NA TAMAA YA CHAKULA KINGINE.
KIFO CHA REINHARD BONKEY KINAACHA UJUMBE GANI KWETU?
JE! NINAWEZA KUPOTEZA FURAHA YA WOKOVU?
Karama kibiblia humaanisha uwezo utokao kwa Mungu wa kufanya/ kutenda mambo yaliyo juu ya uwezo wa kibinadamu katika kutimiza kusudi la ki-Mungu. Karama kwa jina lingine huitwa neema za Mungu.
Kwamfano mmoja huwepa uwezo wa kuponya magonjwa, mwingine unabii, mwingine lugha, mwingine kufundisha, mwingine kukirimu, mwingine uinjilisti N.k.
Sasa neema/karama hizi, zipo za aina kuu tatu.
1) Karama zitokazo moja kwa moja kwa Mungu mwenyewe.
Hii ni aina ya karama(neema) ambayo mtu hupewa sio kwa kuomba, au kupanga au kuchagua…hapana bali Mungu humwita mtu mwenyewe na kuweka wito ndani yake, kwamfano kwenye biblia watu kama Yeremia, Isaya, Mitume na Paulo, walichaguliwa na kupewa neema hizi kwa kusudi maalumu na uwezo maalimu ndani yako, wa kufanya kazi.
2) Karama tuzipatazo ndani ya Kristo.
Hizi hupewa kila mwamini, pindi tu anapoamini na kupokea Roho Mtakatifu. Neema hizi, Roho Mtakatifu Humgawia kila mtu kwa jinsi apendavyo yeye. Ndio hizo tuzisomazo katika (1Kor 12:8-10).
3) Karama tuzipatazo kwa msaada wa watu wengi.
Hii ni aina nyingine ya neema ambayo mtu haipokei kwa jinsi ya kivyake, bali huipokea kwa jinsi anavyohudumiwa na watu wengi ndani ya kanisa la Kristo.
Ndio hii tunaisoma katika;
2 Wakorintho 1:11
[11]ninyi nanyi mkisaidiana nasi kwa ajili yetu katika kuomba, ili, kwa sababu ya ile karama tupewayo sisi kwa msaada wa watu wengi, watu wengi watoe shukrani kwa ajili yetu.
Karama hii huja kwa maombi ya watu wengi.
Na hapa ndipo wengi hupapuuzia kwa viongozi wao. Kwasababu maendeleo ya kanisa, huduma, au madhabahu hutegemea sana uimara wa wale wabeba maono/viongozi…ikiwa wabeba maono hawaombewi kuna viwango hawatavuka hata kama watakuwa na juhudi kiasi gani, watakuwa waombaji kiasi gani, watakuwa waaminifu kiasi gani..kama hawataombewa, watabakia kwenye ngazi fulani sikuzote, lakini viwango vya juu hawatafika.
Kufanikiwa kwa Paulo, hakukutegemea tu wito wake, au utendaji kazi wa Roho Mtakatifu Peke yake, bali pamoja na watu wengi waliokuwa wanamwombea.
Kwamfano huduma hii (nuru ya upendo), inategemea maombi mengi ili iinuke. Ikiwa utaguswa kuchukua muda wako kuiombea maana yake ni kuwa unaitia nguvu viongozi na hatimaye injili inahubiriwa kwa uvumilivu na ujasiri zaidi, na watu wanamwamini Mungu na kumshukuru, matokeo yake yanakuwa kupokea thawabu kwa Mungu kwa zile shukrani.
Sisi (wana nuru ya upendo), na watumishi wengine wa Mungu tunahitaji maombi yenu sana, ili tuihubiri injili kwa ujasiri, kama alivyoomba Paulo.
Waefeso 6:18-19
[18]kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote; [19]pia na kwa ajili yangu mimi, nipewe usemi kwa kufumbua kinywa changu, ili niihubiri kwa ujasiri ile siri ya Injili;
[18]kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;
[19]pia na kwa ajili yangu mimi, nipewe usemi kwa kufumbua kinywa changu, ili niihubiri kwa ujasiri ile siri ya Injili;
Mungu awabariki
Wale mbweha wadogo, Waiharibuo mizabibu.
PALE MAOMBI YANAPOGEUKA KUWA MAPAMBANO.
ENYI WAJINGA, ACHENI UJINGA, MKAISHI
Wale mbweha wadogo, Waiharibuo mizabibu
Wimbo ulio bora 2:15
15 : Tukamatie mbweha, Wale mbweha wadogo, Waiharibuo mizabibu, Maana mizabibu yetu yachanua.
Kitabu cha wimbo ulio Bora ni kitabu kinachoeleza asili ya upendo wa Kristo kwetu na jinsi tunavyopaswa kuuitikia.
Kuwa urefu wa masomo yaliyo nyuma ya kitabu hiki fungua hapa >>> NYAKATI TOFAUTI- TOFAUTI ZA UPENDO.
Lakini kwenye mstari huu, tunaona ni kama vile mtu kwa lugha ya picha anaona mbweha “ Wadogo” wamevamia shamba lake la mizabibu inayochanua na hivyo hawapuuzii kwasababu ya udogo wao, bali anatoa tamko la kukamatwa na kuondolewa…ili shamba lake linalochanua liwe salama.
Kimsingi mbweha si mnyama anayekula nyama tu, bali hula pia mizazibu, na mingine kuiharibu.
Hii ni kufunua nini katika hali zetu za rohoni..
Adui akishaona mahusiano Yetu na Kristo yanazaa matunda, huinua vitu Vidogo vidogo ili kuharibu mahusiano wakati mwingine unaweza usione kama vina madhara sana au vina nguvu sana, lakini katika eneo la kiroho kitu kidogo kina nguvu sawa na kitu kikubwa…
Hivi ndio vinavyoitwa mbweha wadogo..
Mambo Kama haya ni kama vile kuendekeza vishawishi vya dhambi kwenye maisha yako.
Kwa mfano wewe ni binti halafu kila siku unaona wanaume wanazungumza na wewe maneno ya mizaha, sasa kama usipokemea tabia hiyo, ukaona ni kawaida, tabia hizo ndogo ndogo ndizo zinazopelekea mtu baadaye kuanguka kwenye dhambi za uzinzi.
Samsoni, alipoona ushawishi wa delila unaendelea, badala aukatishe yeye akapuuzia mwisho wa siku akatekwa..
Hao ni mbweha wadogo wanaoharibu shamba lako, kila kichocheo na kishawishi kiwe kidogo kiasi gani usikipuuzie.
Wakati mwingine kuendekeza uvivu wa kiroho, yaani kupuuzia maombi, kupuuzia ibada, kidogo kidogo hupelekea kupoa kiroho, na hatimaye unajikuta kabisa umerudi duniani..mpaka unajiuliza nimefikaje hapa? Ni kwasababu uliendekeza uvivu wa kiroho..ulisema. nitaomba kesho, nikesha kesho, nitamtumikia Mungu mwezi ujao..mwishowe ukawa hivyo ulivyo leo…
Angalia ni eneo lipi la maisha yako limevamiwa na hawa mbweha wadogo, kisha chukua hatua za haraka kurekebisha.
Shalom
Mwandishi wa kitabu cha wimbo uliobora.
Nini maana ya Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, (Wimbo 2:7)
Pambaja ni nini katika Biblia kama tunavyosoma katika kitabu cha Wimbo ulio bora 1:2?
Kuba ni kitu chenye umbo la duara kinachofunika kwa juu, ni kama paa lililopinda. Lenye mwonekano unaofanana na nusu ya mpira au bakuli lililogeuzwa juu chini.
Mifano ya kuba:
unaweza kuona kwenye ujenzi wa Misikiti mingi na baadhi ya Makanisa na majengo ya kale
Tukirudi kwenye biblia Enzi za kale, ilidhaniwa kuwa dunia ina kuba kwa juu, yaani kifuniko. Ambao ndani yake jua, mwezi na nyota hutembea..
Neno hilo utalisoma katikq vifungu hivi;
Ayubu 22:14
[14]Mawingu mazito ni kifuniko chake, hata asione;
Naye yuatembea juu ya kuba ya mbingu.
Amosi 9:6
[6]Yeye ndiye avijengaye vyumba vyake mbinguni, na kuweka misingi ya kuba yake juu ya nchi; yeye ndiye ayaitaye maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya uso wa nchi; BWANA ndilo jina lake.
Kumbuka, ujumbe unaowasilishwa hapo ni kueleza ukuu uliozidi wa Mungu, katika uumbaji wake na mamlaka yake.
Nini maana ya Israeli?
Binti za Yerusalemu wanaotajwa katika kitabu cha Wimbo ulio Bora 1:5 ni akina nani?
Hiba ni nini? (Wimbo 3:10)
UNAJISIKIAJE, KUTEMBEA NA SANDA?