MIRIAMU

MIRIAMU

Miriamu alikuwa ni dada yake Musa na Haruni, wa damu (Hesabu 26:59), Miriamu ndiye aliyekuwa wa mwisho kuzaliwa katika famila ya Yokebedi na Amramu. Biblia inasema naye pia alikuwa ni nabii. Hawa watatu Bwana aliwaita kipekee kuhudumu katika hatua ya kuwaongoza wana wa Israeli. (Mika 6:4)

Huduma ya Miriamu ilikuwa ya kipekee na kielelezo kwa wanawake, kwani baada ya Bwana kulipiga jeshi la Farao kwa kulitosa kwenye Bahari ya Shamu, Miriamu alisimama na jeshi kubwa pamoja na wanawake wenzake, wakamwimbia Bwana kwa MATARI na kucheza! (Kutoka 15:20-21).

Wakiwa jangwani katika safari yao ya kwenda nchi ya Ahadi. Miriamu pamoja na Haruni walianza kumnenea Musa, na kumlaumu, kwasababu ya Mwanamke wa kiKushi aliyemwoa. Jambo hilo likamchukiza sana Bwana na hatimaye Bwana kumpiga Miriamu kwa ukoma. Lakini baadaye alikuja kupona baada ya Musa kumwombea. (Kutoka 12:1-6).

Miriamu alikufa kabla ya kuiona nchi ya Ahadi, alikufa katika Bara la Sini, huko Kadeshi, na huko ndiko alikozikiwa.(Kutoka 20:1).

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

1.Musa ni nani?

2. Haruni ni nani?

3. Fimbo ya Haruni ilikuwaje?

HOME

Print this post

HARUNI

Haruni ni nani

Haruni alizaliwa miaka mitatu kabla ya kuzaliwa Nabii  Musa, alikuwa ni ndugu wa damu kabisa wa Musa. Na walikuwa na dada yao aliyeitwa MIRIAMU. Bwana alimwita Haruni katika huduma baada ya Musa kusita-sita wito wake wa kwenda kwa Farao, na baada ya kutoa vijisababu. Mungu alimwita Haruni ndugu yake awe kama msemaji wake katika safari yao ya kwenda kuwafungua wana wa Israeli dhidi ya mateso ya Farao. (Kutoka 4:10-15).

Haruni pamoja na Musa walikuwa ni wa kabila la LAWI. Bwana aliwapa maagizo kwamba kwa kutumia ile FIMBO wakafanye ajabu zote mbele ya Farao. Fimbo ndiyo iliyokuja kujulikana kama FIMBO YA HARUNI.

Kutokana na utumishi wa Haruni, Bwana alimteua awe KUHANI MKUU, Yeye na wanawe milele. Na kabila la Musa na Haruni, (kabila la Lawi) ndilo lililokabidhiwa shughuli zote za kikuhani, yaani shughuli za kufanya upatanisho kwa ajili ya dhambi zote za wana wa Israeli.

Kutokana na upingamizi mkali wa wana wa Israeli dhidi ya uongozi wa Mtumishi wa Mungu, Haruni mara kadhaa alijaribu kuvutwa na ushawishi wao. Na hivyo wakati Fulani kufikia hatua ya kukubali kuwatengenezea sanamu ya ndama (Kutoka 32:1-5).

Haruni naye hakufika nchi ya Ahadi, kutokana na dhambi waliyoitenda wao na Musa ya kujichukulia utukufu mbele ya Wana wa Israeli.(Hesabu 20:10,24) Hivyo alikufa akiwa jangwani akiwa mzee sana.

Ni nini tunaweza kujifunza kutoka kwa maisha ya Haruni? (Haruni ni nani)

Pamoja na mambo mengi yasiyofaa tusiyoweza kujifunza kutoka kwake, kama kuungana na Wana wa Israeli kutengeneza ile sanamu ya ndama… lakini bado Haruni alikuwa ni mtu mwenye ujasiri mwingi kuliko Musa..Wakati Musa anasita sita kwenda kuzungumza na Farao..yeye alichukua nafasi yake kwa kuuvaa ujasiri uliotoka kwa Mungu..

Na jambo lingine la Muhimu ni nafasi ya ukuhani aliyopewa na Mungu..Musa hakupewa nafasi ya ukuhani isipokuwa Haruni na wanawe..Nafasi ya ukuhani inafananishwa na nafasi ya YESU KRISTO, Kama Kuhani Mkuu…Hivyo alisimama kama Kuhani Mkuu wa Mungu kwaajili ya wana wa Israeli. Na Yesu Kristo kama Kuhani mkuu wa wanadamu wote.

Bwana akubariki. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

1. Fimbo ya Haruni ilikuwaje?

1.Miriamu ni nani?

2. Musa ni nani?

HOME

Print this post

NABII MUSA.

Musa alizaliwa huko Misri, miaka mingi kidogo baada ya Yusufu mwana wa Yakobo kufariki. Wakati wa kuzaliwa kwake, mama yake alimhifadhi mtoni kutokana na hofu ya amri ya Mfalme juu ya kuuawa kwa wazaliwa wote wa jinsia ya kiume.

Jina la Baba yake Musa ni Amramu na Mama yake ni Yokebedi. (Hesabu 26:59).

Musa alikuwa na Kaka yake wa damu aliyeitwa Haruni waliokuwa wamepishana miaka 3, Haruni alikuwa mkubwa kwa Musa, na ndiye yule aliyekuja kuwa Kuhani Mkuu, pia alikuwa na dada yake aliyeitwa Miriamu ambaye naye pia alikuwa ni Nabii wa Bwana.

Bithiani aliyekuwa Binti wa Farao alimwokota akiwa kwenye kijisafina kidogo, pembezoni mwa mto wakati akiwa anaoga. Musa aliishi katika Nyumba ya kifalme mpaka alipofikisha umri wa miaka 40, Baadaye aliasi nyumba ya Farao kutokana na kumsaidia mmoja wa ndugu zake wa Kiebrania, akakimbilia nchi ya Midiani. Huko alipata mke kutoka kwenye nyumba ya kuhani mmoja wa Midiani aliyeitwa Yethro.

Alikaa miaka 40 nyumbani kwa Yethro, akichunga mifugo yake, mpaka siku moja Bwana alipomtokea katika mwali wa moto, ndani ya kile kijiti, alipokuwa anachunga kundi la Yethro, Alipewa maagizo ya kuwaokoa Israeli waliokuwa wanateswa chini ya utawala mkali wa Farao.

Kwa Ishara nyingi na miujiza mingi Musa aliwaongoza wana wa Israeli miaka 40 mingine, na Alifariki akiwa na miaka 120, akiwa na nguvu zake zote. Macho yake hayakupofuka wala mwili haukupungua nguvu (Kumbukumbu 34:7)

Musa pekee ndiye Nabii aliyezungumza na Mungu uso kwa uso, wala baada yake hakuinuka nabii mfano wake yeye (Kumbukumbu 34:10-12)

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

1.Utaji uliokuwepo juu ya uso wa Musa ulikuwa unaashiria nini?

2.Haruni ni nani?

3. Miriamu ni nani?

HOME

Print this post

YEZEBELI ALIKUWA NANI

Yezebeli, alikuwa ni Binti wa Mfalme wa Wasidoni aliyeitwa Ethbaali (1 Wafalme 16:31). Sidoni ilikuwa ni nchi iliyokuwepo Kaskazini mwa Taifa la Israeli, kwasasa nchi hiyo ni nchi ya LEBANONI.

Desturi za Wasidoni zilikuwa ni kuabudu miungu, waliabudu mungu wao maarufu aliyeitwa BAALI.

Mfalme wa Israeli aliyeitwa Ahabu alimwoa Binti huyo wa kifalme na kumleta katika Taifa la Israeli na kuwa Malkia. Na hivyo kuingiza ibada za miungu migeni ndani ya Taifa la Mungu.

Yezebeli licha tu ya kulichafua Taifa la Israeli kwa kumshawishi sana Mumewe Ahabu, alikuwa pia ni mchawi (2 Wafalme 9:22). Aliwaua manabii wengi wa kweli wa Mungu, na aliikosesha Israeli kwa sehemu kubwa sana. Mahali pengine Inamtaja Yezebeli kuwa ni Nabii wa Uongo. (Ufunuo 2:20)

Yezebeli pia ndio mwanamke pekee kwenye Biblia nzima aliyekuwa anapaka WANJA usoni na kupamba uso. Desturi za wanawake makahaba.(2 Wafalme 9:30). Mwanamke huyu ndiye Mwanamke pekee aliyeshindana na maagizo ya Mungu kuliko wanawake wote kwenye Biblia, ndiye aliyemsumbua sana Eliya na hata kufikia hatua Nabii Eliya kumkimbia, kuogopa madhara atakayoyapata kutoka kwake.

Yezebeli alikuwa na mtoto wa kike, aliyeitwa ATHALIA ambaye naye alirithi tabia zote za mama yake ambaye naye pia alikuwa anaabudu Baali, Athalia alikuwa muuaji na aliutwaa umalkia kwa nguvu ndani ya kabila la YUDA.

Yezebeli hakudumu muda mrefu kwani alikufa sawasawa na unabii uliotolewa juu yake, kwamba atakufa na mbwa watalamba damu yake. Siku ya kufa Yezebeli aliangushwa kutoka juu ya ghorofa refu na kuchuruza damu ukutani mwote, na alipofika chini farasi alimkanyaga kanyaga..na Mbwa walikumla na kubakisha viganja tu vya mikono na kifuvu (2 Wafalme 9:35)

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

NABII ELIYA NI NANI?

Rudi Nyumbani

Print this post

Shetani ni nani?

Shetani ni nani?…Tafsiri ya Jina shetani ni ‘mshitaki’ au ‘mchongezi’.  Kazi yake ni kuwashitaki watakatifu mbele za Mungu.

Jina lingine la shetani ni “LUSIFA” Maana yake ‘NYOTA YA ALFAJIRI’. (Isaya 14:12) Jina  hili Lusifa aliitwa kabla hajaasi, baada ya kuasi ndio akawa shetani.

Alikuwa ni Malaika wa Sifa (Kerubi) huko mbinguni, alikuwa ni Mzuri kwa mwonekano na mkamilifu katika njia zake zote, aliishi katika taratibu za Mungu, na katika njia za Mungu,  na hivyo akapata heshima kubwa mbinguni zaidi ya Malaika wengi (Ezekieli 28:14).. Alikuwa mkamilifu mpaka siku uovu ulipoonekana ndani yake (Ezekieli 28:15).

Kwasababu ya uzuri wake Moyo wake ukainuka, akataka kujiinua awe kama Mungu, aabudiwe kama Mungu na kwa ujuzi wake mwingi akawashawishi theluthi ya Malaika mbinguni (1/3) waambatane naye.

Vita, vikali vikatokea Mbinguni kati ya Malaika waliokataa kuungana na Lusifa na malaika waliokubali kuungana naye. Biblia haisema vita hivyo vilipiganwa kwa muda gani, lakini inasema mwisho wa siku lusifa pamoja na malaika wake walishindwa vita vile, na kutupwa chini duniani (Ufunuo 12:7).

Na vita hivyo bado havijaisha, vita vya kwanza vilipiganwa mbunguni, kati ya Malaika walio upande wa shetani na wale walio upande wa Mungu na Malaika waliokuwepo Upande wa Mungu wakavishinda, lakini vita vya pili na vya mwisho vinapiganwa hapa duniani na hata sasa bado vinaendelea..Na vitaisha mwisho wa dunia. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

1. Je! Ni nani aliyemdanganya shetani?

2. Huduma 10 za shetani sasahivi duniani ni zipi?

3. Mpango wa shetani kwa watoto katika siku hizi za mwisho.

4. Agenda kubwa ya shetani kwa kanisa hili la siku za mwisho

5. Mafundisho ya Mashetani ni yapi katika siku hizi za mwisho?

6. Kazi ya Malaika watakatifu sasa ni nini?

HOME

Print this post

Yohana Mbatizaji anaigeuzaje mioyo ya mababa iwaelekee watoto?

Malaki 4:5 kama inasema  angalieni nitawapelekea Eliya Nabii, kabla haijaja siku ile ya BWANA, iliyo kuu na ya kuogfya. Naye ataigeuza mioyo ya Baba iwaelekee watoto wao na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana.”

Kama Mungu alivyoahidi angemtua Eliya nabii. ambaye kulingana na maandiko tunafahamu Yohana mbatizaji aliyatimiza hayo maandiko ( Yaani kuja kabla ya ile siku KUU YA BWANA) ambaye yeye alitangulia kuja kwake Kristo kwa mara ya kwanza kwa kusudi la kuigeuza Mioyo ya Baba iwaelekee Watoto.

Hii inamaanisha kwamba Yohana alihubiri injili ya kuwarejeza waalimu wa sheria na marabi wa torati pamoja na wote wanaoujia torati na kuifuatilia (ambao ndio mababa wa Torati) ili waiamini injili ya Kristo.

Na tonaona…Baadhi ya wanafunzi wake mwenyewe Yohana, waliiamini Injili yake na baadaye hao hao wakaja kuwa wanafunzi wa Yesu Kristo, (mfano Andrea na Yohana) ambao walikuwa hapo kwanza wanafunzi wa Yohana Mbatizaji lakini wakaja kuwa wanafunzi wa Bwana Yesu..na ndio sasa mababa wetu wa Imani ya Kikristo leo.

Hivyo Yohana mbatizaji kazi aliyoifanya ni kuwageuza Mababa wa Torati kuwa Mababa wa Imani ya Kristo na mioyo ya watoto iwaelekee mababa.

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

HOME

Print this post

YOHANA MBATIZAJI

Yohana Mbatizaji alizaliwa huko Uyahudi miezi michache kabla ya kuzaliwa Mwokozi wa Ulimwengu Yesu Kristo, Baba yake mzazi aliitwa Zekaria aliyekuwa Mlawi, ambaye alikuwa ni kuhani, akihudumu katika Nyumba ya Mungu illiyokuwepo huko Yerusalemu…Mama yake aliitwa Elizabeth ambaye alikuwa ana undugu wa karibu na Bikira Mariamu mama yake Yesu.

Habari za kuzaliwa kwake kimiujiza,  zinapatikana kwa urefu katika kitabu cha (Luka 1:1-60).

Maandiko yanasema Yohana Mbatizaji alijazwa Roho Mtakatifu tangu akiwa tumboni mwa mama yake (Luka 1:15). Na inasadikiwa kuwa miaka michache sana baada ya kuzaliwa kwake wazazi wake wote wawili walifariki. Na hivyo akaondoka na kwenda kukaa majangwani, mpaka siku alipotokea tena hadharani kuhubiri habari za msamaha na toba.

Aliitwa Yohana Mbatizaji kutokana na ufunuo alioupata wa ubatizo. Hapo kabla kulikuwa hakuna mwingine aliyekuwa anafanya ubatizo Zaidi yake, ndio maana alijulikana kama Yohana Mbatizaji, kumtofautisha na wakina Yohana wengine.

Yohana Mbatizaji sio Yohana yule aliyeandika kitabu cha Ufunuo, aliyeandika kitabu cha Ufunuo ni Yohana aliyekuwa mwanafunzi wake Yesu. Yohana Mbatizaji hakuandika kitabu chochote katika Biblia

Yohana Mbatizaji, maandiko yanasema alikuwa ndiye Eliya aliyetabiriwa atakayekuja kumtengenezea Bwana Njia (Luka 1:17). Atakayeigeuza mioyo ya baba iwaelekee Watoto.

1. Yohana Mbatizaji anaigeuzaje mioyo ya mababa iwaelekee watoto?

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

HOME

Print this post

Je! Ni Eliya mwenyewe atarudi au ni roho yake?

Tofauti na inavyodhaniwa na wengi kuwa Nabii Eliya mwenyewe ndiye atakayerudi.

Ili kuelewa vizuri juu ya jambo hilo hebu tafakari mfano ufuatao.

Ametokea kiongozi mmoja mashuhuri sana wa mambo ya kisiasa na akaleta mabadiliko makubwa sana katika taifa hilo, tuchukulie mfano Aliyekuwa Raisi wa Taifa la Tanzania, Hayati J. K. Nyerere baada ya kufa kwake, mwananchi mmoja akatabiri, Miaka ya huko mbeleni watazaliwa wakina Nyerere wengi ambao watafanya kama alivyofanya Baba wa Taifa.

Je! kwa sentensi hiyo ni sawa na kusema, Nyerere atazaliwa tena yule yule aliyefariki na kuishi na kuja kuwa Raisi tena?..Ni wazi kuwa hiyo siyo tafsiri yake, tafsiri yake ni kwamba atazaliwa au watazaliwa watu ambao watakuja kuwa mashujaa kama Nyerere

Na ndivyo ilivyo kwa unabii wa ujio wa Eliya, sio kwamba ni Eliya yule yule atazaliwa tena hapana bali atakuja mtu au watu watakaobeba huduma inayofanana na ya Eliya.

Na mtu wa Kwanza aliyeibeba huduma hiyo baada ya Eliya mwenyewe alikuwa ni Nabii Elisha na baada ya Elisha alifuata Yohana Mbatizaji..

1.Yohana Mbatizaji ni nani?

HOME

Print this post

NABII ELIYA

Historia inaonesha Nabii Eliya aliishi karne ya 9 kabla ya Kristo,  Ni Nabii aliyeshindana sana na Utawala wa kipagani wa Mfalme Ahabu wa Israeli na mkewe Yezebeli.

kadhalika Biblia hairekodi kama alikuwa na mke wala Watoto. Wala haielezi huduma yake aliifanya kwa miaka mingapi.

Miujiza mingi iliambatana na Nabii huyu, Miujiza maarufu iliyoambatana na Nabii huyu ni ule wa  KUSHUSHA MOTO na ule wa KUCHUKULIWA JUU NA MAJESHI YA FARASI.

Katika kitabu cha Malaki 4:5, biblia imeahidi kurudi tena kwa Nabii huyu.

1.Je! Ni Eliya mwenyewe atarudi au ni roho yake?

2.Je! Kazi ya Eliya atakaporudi itakuwa ni ipi?

3. Yezebeli ni nani?

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

HOME

Print this post

MANENO YA MUNGU YANAPINDULIWAJE?


Siku moja nilikuwa ninamsikiliza Mh.Raisi akizungumza na wafanyabiashara Ikulu, nikapata kitu ambacho kiuhalisi ndio kinachoendelea katika Ukristo isipokuwa tu ni katika upande mwingine wa shilingi. Kwa kawaida mimi sio mfuatiliaji wa mambo ya siasa, lakini siku hiyo nilijikuta ninasikiliza mahojiano kati ya Raisi na wafanyabiashara ikulu ni hotuba wakipeleka changamoto zao na malalamiko yao wanayokumbana nayo katika taasisi cha kiserikali hususani TRA….Wengi wao walipewa nafasi ya kutoa kilicho moyoni mwao..Na baadaye Raisi akasema hawa watu wa taasisi za umma, wanatumia kauli mbiu yake ya kuchapa kazi, ili kuwakandamiza wafanyabiashara na wananchi kwa kuwapa makadirio makubwa kushinda uwezo wao wa kulipa..Na wakishamaliza kuwakandamiza wanatumia kauli ya HAPA KAZI TU!, yaani kwa lugha nyepesi tunaweza kusema wanaongezea makali kile Raisi anachokiamini kwa kutimiza matakwa yao binafsi, ambayo hayalengi kujenga bali kubomoa ..Hilo ni jambo ambalo lilimuhuzunisha sana Mh Raisi.

Sasa ukiangalia, ni kweli kauli mbiu ya Raisi ni kuwa kila mtu achape kazi, lakini hakuwa na lengo la kumaanisha kuzidi mipaka hadi kuwakandamiza watu wenye nia njema ya kulijenga Taifa..Bali kanuni hiyo ilikuwa inalengo la kuwahamasisha wananchi wafanya kazi kwa bidii..

Leo hii ukirudi katika ukristo utakutana pia na hili neno maarufu, “Hatuishi chini ya Sheria, bali tupo chini ya neema”(Warumi 6:14)..Na hivyo Mungu haangalii matendo yetu bali Roho zetu…Ukiangalia ni kweli kabisa biblia inatuambia hivyo, lakini tunashindwa kufahamu Neno hilo lilikuwa linawahusu watu wa namna gani..

Neno hilo lilikuwa linawahusu watu waliokuwa ndani ya Kristo na wala sio walio nje ya Kristo, ikiwa na maana kuwa katika bidii yako ya kuishi maisha ya kumpendeza Mungu ndani ya Kristo, Usihesabu kuwa hicho ndicho kinachokupa uhalali kwa kukubaliwa na Mungu au kwenda mbinguni..,Hapana, mbinguni ni mahali patakatifu sana, hakuna kinyonge kitakawezakuingia na kama hivyo hakuna mtakatifu yoyote ambaye angestahili kwenda mbinguni isipokuwa YESU KRISTO tu peke yake kwasababu yeye ndiye hakuwahi kutenda dhambi yoyote tangu kuzaliwa kwake hadi kufa kwake..

Hivyo ili na sisi tuhesabiwe kama watakatifu basi neema lazima ichukue nafasi yake, lakini huku tukiwa bado ndani ya Kristo, na tukijitahidi kuishi maisha makamilifu na matakatifu kwa kadiri tuwezavyo..Lakini leo hii utakuta, mtu anatembea uchi barabarani, anavaa vimini na suruali kama soksi, na bado anajiita mkristo, ukimuuliza kwanini unafanya hivi . Anakwambia Biblia inatuambia hatuishi chini ya sheria bali chini ya neema, Mungu haangalii vya nje bali vya ndani.

Hata mtu aliye nje ya wokovu utamsikia akizungumza maneno hayo hayo, hatupo chini ya sheria bali chini ya neema. Nataka nikuambie, biblia inasema katika siku za mwisho maneno haya ..“lakini watu wabaya na wadanganyaji wataendelea, na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika. (2Timotheo 3:13)..

Usikubali kudanganyika, Maovu yanavyozidi kuongezeka shetani ndivyo anavyotumia silaha ile ile ya maandiko kudanganya watu wengi. Kama vile tu alivyojaribu kutumia silaha hiyo kumdanganya Bwana Yesu kule jangwani…Ukiendelea na mtazamo huo kuwa tunaokolewa kwa neema na sio kwa matendo na huku unafanya mambo maovu kwa makusudi, unawasababishia wengine watende dhambi ya kutamani kwa ajili yako, kuwa na uhakika tu siku ile utahukumiwa na Mungu kwa kushindwa kulipambanua Neno la Mungu ipasavyo.

Warumi 6:15 “Ni nini basi? Tufanye dhambi kwa sababu hatuwi chini ya sheria bali chini ya neema? Hasha!

16 Hamjui ya kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake katika kumtii, mmekuwa watumwa wake yule mnayemtii, kwamba ni utumishi wa dhambi uletao mauti, au kwamba ni utumishi wa utii uletao haki.”

Na Neno lingine lililo maarufu leo hii, utalisikia kila mahali ni hili ‘Usihukumu usije ukahukumiwa’..Na kwamba ikitokea mtu anahubiri kuwa walevi wote na waasherati wataenda motoni, kama biblia inavyosema anaambiwa kuwa anahukumu…Lakini mtu huyo huyo yupo tayari kumweleza kwa uwazi wote mtoto wake ikiwa anapotea mwisho wake utakavyokuwa, utasikia anamwambia usiposoma mwanangu, utaishia kuwa teja, au kuwa kibaka, au kuwa maskini…hilo kwake haoni kama ni hukumu, lakini yeye akihubiriwa kwamba endepo akiendelea kuwa mlevi ataishia jehanamu ya moto utasikia anakumbia unahukumu, mwenye uwezo wa kuhukumu ni Mungu tu!…Hiyo yote ni kutokana na kushindwa kulichambua vizuri neno la Mungu. Utakapokwenda mahali popote ukaanza kuwafundisha tu watu wadhara ya dhambi na mwisho wake ni upi, utasikia wakisema unawahukumu..

Na mambo mengine mengi tu, ya namna hiyo. Hivyo tunapaswa tukae mbali na misemo hiyo, ambayo inatumia kivuli cha maandiko kusitiri maovu na mabaya. Kwasababu siku ile Mungu hatakuwa radhi na sisi.

Kama bado haujafahamu thamani ya kuwa ndani ya Kristo, ni vema ufanya hivyo sasa kabla ya mlango wa neema haujafungwa..Unachopaswa kufanya ni kutubu kwa kumaanisha kabisa kuacha kufanya dhambi, kisha tafuta mahali wanapobatiza ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi, na kwa Jina la BWANA YESU KRISTO, upate ondoleo la dhambi zako kama bado hujafanya hivyo..kisha Uukulie wokovu mpaka siku ya kunyakuliwa..

Ubarikiwe sana. Tafadhali “Share” Ujumbe huu kwa wengine. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

1.Angalieni Jinsi Msikiavyo

2. Umesikia inavyopaswa?

3. Je! Una masikio yanayosikia?

.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Print this post