Title 2019

TABIA YA WAZI INAYOWATOFAUTISHA MANABII WA UONGO NA WALE WA UKWELI.

Mathayo 24: 24 “Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule”.

Manabii wa uongo wa agano la kale ni kivuli cha manabii wa uongo katika agano jipya. Mfano wa yale yaliyokuwa wanayafanya agano lake ndio hayo hayo wanayoyafanya sasa katika agano jipya.

Waliwapoteza wale waliokuwa wachanga kiimani kadhalika walifanikiwa pia kuwapoteza hata baadhi ya wale waliokuwa wamesimama kiimani. Mfano wa manabii hao tunamwona mtu kama Hanania aliyetokea kipindi cha wafalme, wakati ambapo Mungu alisema Yerusalemu utateketezwa na watu wake kupelekwa utumwani Babeli, yeye alisimama kwa ujasiri mkubwa mbele ya mfalme na mbele ya makuhani wa Bwana na mbele ya watu wote na kusema Bwana anasema hivi haitatimia miaka miwili mpaka vile vyombo na vitu vyote Nebukadreza alivyovichukua kwenye ile awamu ya kwanza na kuvipeleka Babeli kurudishwa tena Israeli,.. Lakini kama tunavyosoma kumbe Mungu hakumtuma na unajua kwa namna ya kawaida mtu akitoa maneno ya faraja hata kama yawe ni ya uongo kiasi gani atapendwa tu!. Na ndio maana tunakuja kuona nabii kama Yeremia alipokuja kusema kuwa Yerusalemu utateketezwa na watu wake kuchukuliwa mateka alionekana kama ni mpinga-kristo, asiyeutakia mema Yerusalemu mji wa Mungu, hivyo mfalme na wale watu wakaamuru kwamba afungwe, katika vifungo vya mateso. Habari hizo tunazisoma katika kitabu cha Yeremia 28.

Kadhalika Walikuwepo na manabii wengine 400 enzi hizo hizo za wafalme wa Israeli waliokuwa wakimtabiria mfalme Ahabu siku zote, lakini ilipofika wakati ambapo Mungu amekusudia kuleta jambo baya juu ya mfalme Ahabu kutokana na maovu yake, ndipo likazuka jopo kubwa la manabii wa uongo wakaanza kumtabiria mfalme habari za kufanikiwa kwake atakapokwenda vitani. Lakini kulikuwa na nabii mmoja aliyeitwa Mikaya yeye hakupenda kusimamia upande wowote, lakini yeye kwa uaminifu kabisa alimwomba Mungu na kuuliza habari za mfalme Ahabu na ndipo Mungu akamwambia ni lazima Ahabu afe atakapokwenda vitani, lakini kwa kuwa mfalme aliona ni manabii wengi wanaomtabiria mafanikio yake zaidi ya uharibifu wake, na kwasababu yeye mwenyewe siku zote anapenda mambo ya faraja tu! hivyo akaamua kuwasikiliza wale wengi na kwenda vitani na kama tunavyosoma alipokwenda tu alikufa.(2Nyakati 18).

Sasa hawa wote ni mifano wa manabii wachache ambao hata sasa wapo kwenye agano jipya. Kadhalika lipo kundi lingine la manabii wa uongo lilikuwa kwenye agano la kale, Na hilo ndilo libaya zaidi kwasababu linatumika mahususi kuwaangusha wale wanaoonekana kusimama katika imani, hilo linaweza kuwaangusha hata walio manabii wa ukweli, na mfano wa kundi hilo tunaweza kulisoma habari yake katika kitabu cha 1Wafalme 13

Embu tusome pamoja na Bwana atatusaidia kupata kitu hapo:

1Wafalme 13:1-32

1 Na tazama, akatoka mtu wa Mungu katika Yuda kwa neno la Bwana, akafika Betheli. Naye Yeroboamu alikuwa akisimama penye madhabahu, afukize uvumba.

2 Basi mtu huyo akapiga kelele juu ya madhabahu, kwa neno la Bwana akasema, Ee madhabahu, madhabahu, Bwana asema hivi, Angalia, mtoto atazaliwa katika nyumba ya Daudi, jina lake Yosia; na juu yako atawachinja makuhani wa mahali pa juu, wanaofukiza uvumba juu yako, na mifupa ya watu itateketezwa juu yako.

3 Akatoa ishara siku ile ile, akasema, Hii ndiyo ishara aliyoinena Bwana, Tazama, madhabahu itapasuka, na majivu yaliyo juu yake yatamwagika.

4 Ikawa, mfalme Yeroboamu alipoyasikia maneno ya yule mtu wa Mungu, alipopiga kelele juu ya madhabahu huko Betheli, alinyosha mkono wake pale madhabahuni, akasema, Mkamateni. Basi ule mkono wake aliounyosha ukakatika, wala hakuweza kuurudisha kwake tena.

5 Madhabahu ikapasuka, majivu ya madhabahuni yakamwagika, sawasawa na ishara aliyoitoa mtu wa Mungu kwa neno la Bwana.

6 Mfalme akajibu, akamwambia yule mtu wa Mungu, Umsihi sasa Bwana, Mungu wako, ukaniombee, ili nirudishiwe mkono wangu tena. Yule mtu wa Mungu akamwomba Bwana mkono wa mfalme ukarudishwa tena, ukawa kama ulivyokuwa kwanza.

7 Mfalme akamwambia mtu wa Mungu, Karibu nyumbani kwangu ujiburudishe, nami nitakupa thawabu.

8 Mtu wa Mungu akamwambia mfalme, Ujaponipa nusu ya nyumba yako, sitaingia pamoja nawe, wala sitakula chakula, wala sitakunywa maji mahali hapa;

9 maana ndivyo nilivyoagizwa kwa neno la Bwana, kusema, Usile chakula cho chote wala usinywe maji, wala usirudi kwa njia ile uliyoijia.

10 Basi akaenda zake kwa njia nyingine, wala hakurudi kwa njia ile aliyoijia Betheli.

11 Basi nabii mmoja mzee alikuwa akikaa katika Betheli; na wanawe wakamwendea wakamwambia kila neno alilolitenda yule mtu wa Mungu siku ile katika Betheli; na maneno aliyomwambia mfalme, hayo nayo walimwambia baba yao.

12 Baba yao akawaambia, Amekwenda zake kwa njia ipi? Kwa maana wanawe walikuwa wameiona njia ile aliyoiendea yule mtu wa Mungu aliyetoka katika Yuda.

13 Akawaambia wanawe, Nitandikieni punda. Wakamtandikia punda, naye akampanda.

14 Akamfuata mtu wa Mungu, akamkuta ameketi chini ya mwaloni, akamwambia, Je! Wewe ndiwe yule mtu wa Mungu aliyetoka katika Yuda? Akamwambia, Mimi ndiye.

15 Akamwambia, Karibu kwangu nyumbani, ule chakula.

16 Naye akamwambia, Siwezi kurudi pamoja nawe, wala kuingia pamoja nawe; wala sili chakula wala sinywi maji pamoja nawe hapa;

17 kwani nimeambiwa kwa neno la Bwana, Usile chakula wala usinywe maji huko, wala usirudi kwa njia ile uliyoijia.

18 Akamwambia, Mimi nami ni nabii kama wewe, na malaika akaniambia kwa neno la Bwana, kusema, Mrudishe pamoja nawe nyumbani kwako, ale chakula, akanywe maji. Lakini alisema uongo.

19 Basi mtu yule akarudi pamoja naye, akala chakula, akanywa maji nyumbani mwake.

20 Hata ikawa, walipokuwa wameketi mezani, neno la Bwana likamjia nabii yule aliyemrudisha;

21 akamlilia yule mtu wa Mungu aliyetoka katika Yuda, akinena, Bwana asema hivi, Kwa sababu umeiasi kauli ya Bwana, wala hukuishika amri ile aliyokuamuru Bwana, Mungu wako,

22 bali umerudi, ukala chakula ukanywa maji, hapo alipokuambia, Usile chakula, wala usinywe maji; maiti yako haitaliingia kaburi la baba zako.

23 Basi ikawa, alipokwisha kula chakula na kunywa maji, yule nabii aliyemrudisha akamtandikia punda.

24 Na alipokuwa amekwenda zake, simba alimkuta njiani, akamwua. Maiti yake ikatupwa njiani, na yule punda akasimama karibu naye; na yule simba naye akasimama karibu na maiti.

25 Na tazama, watu wakapita, wakauona mzoga umetupwa njiani, na yule simba akisimama karibu na mzoga, wakaenda, wakatoa habari katika mji ule alimokaa yule nabii mzee.

26 Na yule nabii aliyemrudisha njiani alipopata habari, akasema; Ndiye yule mtu wa Mungu, aliyeiasi kauli ya Bwana; kwa hiyo Bwana amempambanisha na simba, simba akamrarua, akamwua, sawasawa na neno la Bwana alilomwambia.

27 Akawaambia wanawe, akasema, Nitandikieni punda. Wakamtandikia.

28 Akaenda, akamwona yule maiti ametupwa njiani, na punda na simba wamesimama karibu na maiti; yule simba alikuwa hakumla maiti, wala hakumrarua punda.

29 Nabii yule akamtwaa maiti wa yule mtu wa Mungu, akamweka juu ya punda wake, akamrudisha; yule nabii mzee akaenda mjini mwake, kukaa matanga, na kumzika.

30 Akamweka maiti katika kaburi lake mwenyewe; wakamlilia, wakisema, Aa! Ndugu yangu!

31 Hata ikawa, alipokwisha kumzika, akawaambia wanawe, akasema, Nikifa mimi, nizikeni katika kaburi hili alimozikwa yule mtu wa Mungu; iwekeni mifupa yangu kando ya mifupa yake.

32 Kwa maana neno hilo alilolia juu ya madhabahu katika Betheli, kwa neno la Bwana, na juu ya nyumba zote za mahali pa juu zilizo katika miji ya Samaria, hakika litatimizwa.

Amen.

Ukifuatilia utaona huyu mtu wa Mungu, alikuwa amethibitika kabisa katika Imani kiasi kwamba hata mfalme Yerobohamu mwenyewe licha ya utajiri wake na fahari yake kuwa nyingi hakuweza kumshawishi kukaa na kuyaasi maagizo ya Mungu. Wala hakukuwa na mtu yeyote njiani aliyeweza kumshawishi ayatupilie mbali maagizo ya Mungu aliyompa. Lakini alipofika mbali kidogo na kukaribia kuimaliza safari yake, ndipo akazuka mmoja wa wale manabii wa uongo wale ambao kazi yao siku zote ni KUTAMKA MANENO YA FARAJA kinyume na maagizo ya Mungu.

Embu fikiria huyu mtu wa Mungu katika safari yake yote ya kuukatiza mji, bila kula wala kunywa, jua kali, uchovu mwingi, ni kweli angetamani hata apate mahali pa kustarehe kwa muda mfupi ili ale na kunywa apate nguvu kisha baada hata ya siku moja au mbili aende zake nyumbani, lakini Mungu hakuwambia afanye hivyo, Mungu hakutaka mtumishi wake aliyemtia mafuta mwaminifu akae au ashirikiane na watu waovu wanaoishi kwenye mji uliojaa sanamu uliojaa sanamu na machukizo. Mji uliojaa manabii vuguvugu, wanaopenda kutabiri mambo ya amani tu, siku zote, wanaopenda kutabiri mambo ya kuwafurahisha watu, yale mengine ya hukumu hawataki kuyazungumza. Lakini huyu mtu wa Mungu hakuisikia sauti ya Bwana ndipo nabii huyu mzee wa uongo ambaye kazi yake ni kutabiri mambo ya faraja akaja kumletea habari kwamba Bwana amemwambia arudi kwake ale, anywe..Kumbe hajui kuwa anakwenda kuiponza roho yake mwenyewe. Na mwisho wa siku kama tunavyosoma hakufika mbali simba akamuua.

Ndugu Hizi ni nyakati mbaya zile zilizobiriwa kuwa watatokea manabii wa uongo wapate kuwapoteza hata yamkini walio wateule. Inawezakana ikawa wewe ni mteule wa Mungu, inaweza ikawa hata wewe ni mtumishi mwaminifu wa Mungu na unatembea katika njia zilizonyooka za Yesu Kristo, mfano wa huyu mtu wa Mungu tuliyesoma habari zake. Lakini kumbuka dunia ya sasa inapumbaza sana, na wanaoipumbaza ni manabii wa uongo, hao ambao kazi yao kubwa ni kutabiri mambo ya Baraka tu, mambo malaini tu, mambo ya matumaini tu, kana kwamba Mungu wakati wote anapendezwa na dunia hii ya sasa iliyojaa dhuluma na uchafu kuliko hata ile ya sodoma na Gomora.

Hivyo kwa kuwa husikii tena ukikemewa dhambi au husikii tena habari za dhiki kuu ambayo inakaribia kuikumba hii dunia siku sio nyingi, kama ulivyokuwa unasikia hapo zamani, wewe unastarehe na kulegeza kamba zako za wokovu, na kuwa vuguvugu. Kwa kuwa husikii tena manabii hao wakizungumzia juu ya siku za mwisho wewe unaona kumbe mwisho bado sana, na wala uharibifu hautaikumba dunia leo wala kesho. Kwa kuwa hawagusii tena uvaaji wako, angali wewe hapo mwanzo ulikuwa ni mwanamke mtakatifu vimini huvai wala suruali, lakini sasa unaona watiwa mafuta wa Bwana hawakemei tena hivyo vitu wanakwambia vyote ni sawa na wewe unasikiliza uongo wao unaanza kuvaa vuguvugu tu kama wanawake wa kidunia. Hujui kuwa unachukuliwa na wimbi hilo la manabii wa uongo kukupoteza wewe. Uende kuzimu.

Ndugu usitazame ni jinsi gani wanaona maono ambayo ni sahihi kabisa, ni kweli hata wale wa agano la kale walikuwa vivyo hivyo, walikuwa wanaona maono ya ukweli na ndio maaana waliaminiwa na watu pamoja na wafalme kirahisi, lakini linapokuja suala la kutabiri juu ya uharibifu na hukumu za Mungu, na kiama hapo ndipo utakapoweza kuyatenga magugu na ngano. Kwasababu hilo kundi lingine halipendi kutabiri juu ya hayo, lenyewe ni maneno ya faraja tu siku zote, Unamwona huyu Nabii, aliyempotosha Nabii mwenzake aliwe na Simba alichofanya?? Baada ya kumfariji na kumdanganya kwamba Bwana kamwambia arudi ale pamoja na yeye, alijua kabisa Bwana hakumwambia lakini kamdanganya makusudi…

Yeremia 14: 14 “Ndipo Bwana akaniambia, Hao manabii wanatabiri uongo kwa jina langu mimi; mimi sikuwatuma, wala sikuwaamuru, wala sikusema nao; wanawapeni unabii wa maono ya uongo, na uaguzi, na neno la ubatili,” na hadaa ya mioyo yao. 15 Basi, kwa hiyo Bwana asema hivi, Kwa habari za manabii wanaotabiri kwa jina langu, wala mimi sikuwatuma, LAKINI HUSEMA, UPANGA NA NJAA HAVITAINGIA KATIKA NCHI HII; Kwa upanga na njaa manabii hao wataangamizwa. 16 Na watu hao, waliopewa unabii na wao, watatupwa nje katika njia kuu za Yerusalemu kwa sababu ya upanga na njaa; wala hawatakuwa na mtu wa kuwazika, wao na wake zao, na wana wao, na binti zao; maana nitamwaga uovu wao wenyewe juu yao”.

Unaona?. Huu si wakati wa kuziamini kila roho zinazokutakia mafanikio tu, na wala hazijali hatma ya maisha yako baada ya kifo, zichunguze sana, leo zitakutabiria utajifungua mapacha, kesho zitakutabiria utajenga jumba, mwezi ujao zitakutabiria faraja za ajabu, lakini hazitakutabiria madhara ya dhambi baada ya kifo, hazitakutabiria madhara ya sanamu ndani ya moyo wako, hazitakutabiria Neno la Yesu linalosema “ukiwa vuguvugu nitakutapika” Biblia inasema mbingu na nchi zitapita lakini maneno ya Mungu hayatapita kamwe, Bwana alisema dunia itaangamizwa, ni kweli itaangamizwa, alisema ufalme wa mbinguni umekaribia ni kweli umekaribia, alisema kutakuwa na dhiki kuu, ni kweli dhiki kuu lazima ije, alisema yupo mlangoni kurudi, ni kweli yupo mlangoni, alisema tujiepushe na hichi kizazi cha ukaidi kilichopotoka, na alisea pia “hakuna mtu atakayemwona yeye asipokuwa mtakatifu Waebrabia 12:14” Je! wewe leo umejiwekaje?. Ni matumaini yangu utaanza kuufanya wito wako na uteule wako imara kuanzia sasa, na kuacha kujitumainisha na mafundisho ya faraja ya hao wanabii wa uongo ambao wapo wengi duniani. Na kuanza pia kutazama siku za vilio ambazo nazo zinakuja mbeleni.

Bwana akubariki sana.

Tafadhali “Share” ujumbe huu kwa wengine na Bwana atakubariki.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Print this post

DAMU YA YESU INANENAJE MEMA KULIKO YA HABILI?

Je Damu ya yesu inanenaje mema kuliko ya habili?..Nini madhara ya kuidharau sauti ya Damu ya thamani ya Yesu Kristo?

Shalom! karibu tujifunze Neno la Mungu kwa pamoja, Leo tutajifunza juu ya damu ya YESU kwa ufupi. Naamini utaongeza kitu juu ya vile ulivyojaliwa kuvijua na Bwana..

Tukisoma katika kile kitabu cha Mwanzo, tunamsoma Kaini aliyemwua ndugu yake Habili, kwasababu sadaka yake haikukubaliwa na Mungu, na ya ndugu yake kukubaliwa..Habari hiyo tunaisoma katika kitabu cha…

Mwanzo 4: 8 “Kaini akamwambia Habili nduguye, [Twende uwandani]Ikawa walipokuwapo uwandani,Kaini akamwinukia Habili nduguye,akamwua.

9 Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?

10 Akasema, Umefanya nini? SAUTI YA DAMU YA NDUGU YAKO INANILILIA KUTOKA KATIKA ARDHI.

11 Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako;

12 utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao”.

Tunaona hapo Bwana alimwambia Kaini “sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.”..kumbuka haikusema “sauti ya roho ya ndugu yako”, hapana bali ilisema “sauti ya damu”..ikiwa na maana kuwa damu ina sauti na inanena.

Pia haikusema “sauti ya damu inanililia kutoka mbinguni”..bali ilisema “sauti inanililia kutoka katika ardhi”..kwahiyo kuna uhusiano pia wa damu na ardhi..tutakuja kuiona huko mbeleni..

Lakini pia tukisoma kitabu cha Waebrani Mlango 12: 24 inasema “Na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, INENAYO MEMA kuliko ile ya Habili”.

Hapa tunaona kuna damu mbili ya Kwanza ni ya Habili na ya pili ni ya Bwana Yesu…Lakini tunasoma damu ya YESU KRISTO inanena mema kuliko ile ya Habili.

SASA DAMU YA YESU INANENAJE MEMA KULIKO YA HABILI?
Habili tunamsoma alikuwa ni mtu wa Haki, na alienda katika ukamilifu, hata akapata ufunuo bora wa kumtolea Mungu sadaka, na zaidi ya yote alimtolea katika sehemu zilizonona na katika wazaliwa wa kwanza wa wanyama wake…Ikionyesha kabisa kuwa alikuwa ni mtu wa Haki aliyemjali Mungu, na kumfanya Mungu kuwa wa kwanza katika maisha yake..Na pia alikuwa anakwenda katika maagizo yake na sheria zake…Na hivyo mpaka kufikia wakati anauawa na ndugu yake, hakuwa na hatia yoyote na hivyo damu yake ikawa ni kama damu ya mtu asiyekuwa na hatia..Na ilipofika ardhini ikaanza kutoa sauti ikimlilia Mungu..

Na kadhalika Bwana Yesu Kristo, aliuawa pasipo hatia yoyote, yeye hakuwa na kosa lolote hata kuuawa pale Kalvari,

Matendo 4: 25 “Nawe ulinena kwa Roho Mtakatifu kwa kinywa cha babaetu Daudi, mtumishi wako, Mbona mataifa wamefanya ghasia, Na makabila wametafakari ubatili?
26 Wafalme wa dunia wamejipanga, Na wakuu wamefanya shauri pamoja Juu ya Bwana na juu ya Kristo wake.
27 Maana ni kweli, Herode na Pontio Pilato pamoja na Mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika katika mji huu juu ya Mtumishi wako mtakatifu YESU, ULIYEMTIA MAFUTA,”

damu ya Yesu

 Lakini Tunaona matokeo ya damu ya Habili kumlilia Mungu kutoka katika ardhi ni ndugu yake Kaini kulaaniwa juu ya ardhi na kuwa mtu mtoro asiyekuwa na kikao….Kwahiyo kwa ufupi damu ya Habili ilinena hukumu juu ya Kaini juu ya nchi.

Lakini tukirudi kwa upande wa Yesu Kristo, tunaona matokeo ya Damu ya Yesu Kristo hayakuwa hukumu kwa wale waliomwua..Bali yalikuwa ni rehema na msamaha, na kuhesabiwa haki bure kwa Neema..Na ndio maana Bwana kabla hajakata roho alimaliza na Kusema “Baba wasamehe” kwakuwa hawajui watendalo…lakini Habili hakusema hivyo, na zaidi ya yote Bwana Yesu alisema “Imekwisha” lakini Habili hakusema hivyo…Kwahiyo damu ya Yesu ni Bora kuliko ya Habili, Damu ya Yesu imetuletea msamaha wa dhambi badala ya hukumu, Damu ya Yesu imetuletea Baraka badala ya Laana..Kwahiyo Inanena mema sana..

Kwa ufupi wale wote waliomsulibisha Bwana Yesu Kristo pale msalabani, pamoja na sisi sote tunaomsulibisha sasa Yesu Kristo kwa matendo yetu, tulistahili kulaaniwa juu ya ardhi kama alivyolaaniwa Kaini na hata zaidi ya pale, kwasababu tulimwua Mwana wa Mungu asiyekuwa na hatia…Lakini kwasababu Damu yake inanena mema kuliko ya Habili..tumepata rehema badala ya Hukumu, ardhi imebarikiwa kwa ajili yetu badala ya kulaaniwa..zaidi sana tumepewa tumaini la uzima wa milele Haleluya!.

Huo ni msamaha wa kipekee sana, Hakuna mwanadamu yoyote duniani leo ambaye mwanawe mpendwa auawe kikatili tena pasipo hatia, halafu badala ya kuwalipizia kisasi wale wauaji,na kuwalaani anawabariki kupitia mauti ya mwanae..Huo ni upendo usio kuwa na kipimo.

Damu ya Yesu ilimwagwa juu ya ardhi hapa duniani, miaka 2,000 iliyopita na si mbinguni..ili inene mema kwa wanadamu wa vizazi vyote vya duniani. Kwa kupitia damu ya Bwana isiyoharibika, mambo yote yanafanyika kuwa mapya, na kwa kupitia damu ya Bwana tunakikaribia kiti cha Neema kwa ujasiri.

Tukiyajua hayo, ni wakati wa kujichunguza na kuogopa, na kutetemeka kwasababu kama tulistahili kulaaniwa kama Kaini lakini Bwana hajatulaani, sio wakati tena wa kuidharau hii DAMU YA THAMANI YA YESU KRISTO, sio wakati wa kujisifu kuwa tunajua..Jambo ambalo watu wengi hawalifahamu ni kwamba Neema yote tunayoiona leo hii duniani ni kwasababu damu ya YESU bado inafanya kazi juu ya NCHI. Mvua tunazozipata kwa wakati ni kwasababu ya Damu ya thamani ya Yesu bado inafanya kazi, majanga tunayoepushwa nayo duniani ni kwasababu Damu ya Yesu bado inafanya kazi licha ya kwamba maasi ya sasa yamezidi yale ya Sodoma na Gomora lakini bado tunafaidika na neema hii kwa kitambo.,

tunavipindi vizuri vya usiku na mchana, na hewa safi ni kwasababu damu ya thamani ya Yesu ipo inayonena Mema.Unafuu wowote tunaouona duniani ni kwasababu ya Damu ya Yesu. Utafika wakati Hii damu itafikia mwisho wa kufanya kazi yake ya kunena na mambo mengine yatafunguliwa, kwasababu kumbuka sio wakati wote Mungu atakuwa anafanya kazi ya kuokoa, upo wakati wa mambo mengine kufunguliwa..hapo ndipo ile dhiki kuu itakapoanza…wakati huo hakuna mtu atakayeweza kununua wala kuuza pasipokuwa na chapa ya mnyama…wakati huo maji ya dunia nzima, na chemichemi zote zitakapogeuzwa kuwa damu, wakati huo ambao Jua litatiwa giza na nyota za mbinguni zitakapoanguka, wakati huo ambao gonjwa zito ya ajabu yataikumba dunia nzima,

Kipindi hicho sio cha kutamani kufika, ni kheri ujisalimishe Kwa Yesu Kristo leo kama hujafanya hivyo, kabla ya nyakati hizo, ukatubu na kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na Kwa jina la Yesu Kristo, upate ondoleo la dhambi zako, usiidharau hii Neema iliyopo leo na kufanya dhambi kwa makusudi, na kama ulikuwa hujasimama imara katika wokovu wako huu ni wakati wa kuweka mambo yako sawa..Biblia inasema katika..

Waebrania 10: 26 “Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, HAIBAKI TENA DHABIHU KWA AJILI YA DHAMBI;

27 bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao.

28 Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu.

29 MWAONAJE? HAIKUMPASA ADHABU ILIYO KUBWA ZAIDI MTU YULE ALIYEMKANYAGA MWANA WA MUNGU, NA KUIHESABU DAMU YA AGANO ALIYOTAKASWA KWAYO KUWA NI KITU OVYO, NA KUMFANYIA JEURI ROHO WA NEEMA?

30 Maana twamjua yeye aliyesema, Kupatiliza kisasi ni juu yangu, mimi nitalipa. Na tena, Bwana atawahukumu watu wake.
31 NI JAMBO LA KUTISHA KUANGUKA KATIKA MIKONO YA MUNGU ALIYE HAI.”

Ndugu yangu/kaka yangu unayesoma haya ambaye ni mlevi, ni mwasherati, unafanya anasa, unakula rushwa, unatazama pornography, n.k mambo hayo yote ni njia panda ya kuelekea kuzimu,Dada unayesoma haya..unayevaa vimini na suruali, unayepaka lipstick na wanja, unayevaa hereni na wigi na unayesokota dread, unayesikiliza na kushabikia miziki na fashion za kidunia..mambo yote hayo kama hautaamua kuyaacha yatakupeleka kuzimu.

Mkabidhi Bwana leo maisha yako kikamilifu, pasipo kuwa vuguvugu..ili damu ile izidi kunena Mema juu yako.

Print this post

UMEFUNULIWA AKILI?

Je! Umefunuliwa akili?..Baada ya Bwana Yesu kufufuka, tunasoma habari ya vijana wawili waliokuwa wanaenda kijiji kimoja kilichopo mbali kidogo na mji wa Yerusalemu, na walipokuwa njiani wakizungumza habari za kufufuka kwa Bwana biblia inatuambia Bwana wenyewe aliungana nao pasipo hata wao kujua, kwani  macho yao yalifumbwa wasimtambue lakini  baadaye mwisho wa safari yao walikuja  kumtambua..tunasoma habari hiyo katika..

Luka 24.13 “Na tazama, siku ile ile watu wawili miongoni mwao walikuwa wakienda kijiji kimoja, jina lake Emau, kilichokuwa mbali na Yerusalemu kama mwendo wa saa mbili.

14 Nao walikuwa wakizungumza wao kwa wao habari za mambo hayo yote yaliyotukia.

15 IKAWA KATIKA KUZUNGUMZA NA KUULIZANA KWAO, YESU MWENYEWE ALIKARIBIA, AKAANDAMANA NAO.

16 Macho yao yakafumbwa wasimtambue.

17 Akawaambia, Ni maneno gani haya mnayosemezana hivi mnapotembea? Wakasimama wamekunja nyuso zao.

18 Akajibu mmoja wao, jina lake Kleopa, akamwambia, Je! Wewe peke yako u mgeni katika Yerusalemu, hata huyajui yaliyotukia humo siku hizi?

19 Akawauliza, Mambo gani? Wakamwambia, Mambo ya Yesu wa Nazareti, aliyekuwa mtu nabii, mwenye uwezo katika kutenda na kunena mbele za Mungu na watu wote;

20 tena jinsi wakuu wa makuhani na wakubwa wetu walivyomtia katika hukumu ya kufa, wakamsulibisha.

21 Nasi tulikuwa tukitumaini ya kuwa yeye ndiye atakayewakomboa Israeli. Zaidi ya hayo yote, leo ni siku ya tatu tangu yalipotendeka mambo hayo;

22 tena, wanawake kadha wa kadha wa kwetu walitushitusha, waliokwenda kaburini asubuhi na mapema,

23 wasiuone mwili wake; wakaja wakasema ya kwamba wametokewa na malaika waliosema kwamba yu hai.

24 Na wengine waliokuwa pamoja nasi walikwenda kaburini wakaona vivyo hivyo kama wale wanawake walivyosema, ila yeye hawakumwona.

25 Akawaambia, Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii!

26 Je! Haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia katika utukufu wake?

27 Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe.

28 Wakakikaribia kile kijiji walichokuwa wakienda, NAYE ALIFANYA KAMA ANATAKA KUENDELEA MBELE.

29 Wakamshawishi wakisema, Kaa pamoja nasi, kwa kuwa kumekuchwa, na mchana unakwisha. Akaingia ndani kukaa nao.

30 Ikawa alipokuwa ameketi nao chakulani, alitwaa mkate, akaubariki, akaumega, akawapa.

31 Yakafumbuliwa macho yao, wakamtambua; kisha akatoweka mbele yao.

32 Wakaambiana, Je! Mioyo yetu haikuwaka ndani yetu hapo alipokuwa akisema nasi njiani, na kutufunulia maandiko?”.

Wengi tunatamani Kristo atutokee siku moja, na kuanza kutembea nasi, ndipo tuamini Yupo na sisi, lakini hatujui kwamba Kristo yupo pamoja na sisi kila siku, akitufundisha na kutufunulia maandiko…kama Neno lake linavyosema “walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.”…Unaona hapo kwa wakati huo Macho yetu ya mwilini yanakuwa yamefumbwa yasimwone lakini macho yetu ya rohoni yanamwona.

Ndicho kilichowatokea hawa watu wawili waliokuwa wanaenda Emau..Bwana alipojiunga katikati yao Macho yao ya mwilini yalifumbwa wasimtambue lakini macho yao ya rohoni yalikuwa yanamwona Bwana, alipokuwa anawafunulia maandiko kumhusu yeye.

Ni kwanini Bwana alijiunga nao? Ni kwasababu “tayari walikuwa wameshakusanyika wawili kwa jina lake, wakizungumza habari zake” ..hivyo Kristo lazima atimize Neno lake “la kuwepo katikati yao”.

Sasa maana ya kuwepo katikati yao sio kumwona sura yake hapana! Bali kumwona yeye katika  Neno lake. Ndio maana wale watu wawili Bwana hakuwafumbua macho yao wamwone sura yake, bali alianza kwanza kuwafunulia maandiko wamwone yeye katika Neno lake.

Kwahiyo unaweza kuona Bwana havutiwi sana, na sisi kumwona yeye uso wake, bali anavutiwa sana na sisi kumwona yeye katika Neno lake. Ndio maana leo hatokei wengi, kwasababu anataka tumjue katika Neno lake, zaidi ya uso wake.

Ukiendelea kusoma habari za hawa vijana wawili, utagundua hata baada ya Bwana kumaliza kuwafunulia maandiko, hakutaka kuwafumbua macho ya mwili wamwone, badala yake utaona alitaka kuondoka kuwaacha katika hali ile ile ya kutomtambua, alitaka kuendelea mbele na safari yake, Ni kwanini alifanya vile? Ni kwasababu lengo lake halikuwa kuwaonyesha uso wake, bali lengo lake lilikuwa wamwelewe katika maandiko..Na baada ya kutimiza kusudi lake la kuwafunulia maandiko kazi ilikuwa imeshakwisha, alitaka kutengana nao… Lakini walipomshawishi sana ndipo akaamu kwenda  kula nao, na huko ndio akawafumbua macho yao ya mwilini wamwone.

28 Wakakikaribia kile kijiji walichokuwa wakienda, NAYE ALIFANYA KAMA ANATAKA KUENDELEA MBELE.

29 Wakamshawishi wakisema, Kaa pamoja nasi, kwa kuwa kumekuchwa, na mchana unakwisha. Akaingia ndani kukaa nao”.

Na ndio maana tunakuja kusoma pia Bwana alimkemea Tomaso kwa kutokumwamini…yeye alitaka auone uso wa Bwana na majeraha yake ndipo aamini, lakini Bwana hakutaka amwamini kwa njia hiyo..alitaka Tomaso amwamini kwa njia ya maandiko?..alitaka Tomaso amwamini kwa ufunuo wa maandiko, sio kwa kumwona uso..alitaka Tomaso amtambue yeye kwa kuyajua yaliyotabiriwa kumhusu yeye kuanzia kwa Musa, zaburi na kwa manabii wote, na hayo mengine yawe baadaye sana kama yana umuhimu.

Ndugu sura ya Yesu haiwezi kutufanya tumwamini yeye hata kidogo, kitakachotufanya tumwamini Bwana Yesu ni ufunuo katika Neno lake, ni kumtambua kupitia Neno lake, kumwona ametabiriwa wapi katika maandiko, na nafasi yake ni ipi katika Roho sasa.

Wanafunzi hata baada ya kumwona Bwana YESU uso wake,akiwa amefufuka hawakumwamini, walimtilia mashaka, walidhani wanaona mizimu..Na hata kama Bwana angewatokea mara 100 kama asingewafunulia akili zao wayaelewe maandiko wasingemwamini…wangeendelea kumtilia mashaka tu!..Tunaona mtu kama  Yuda yeye sio kutokewa tu dakika chache halafu basi, hapana bali yeye aliishi, alikula, alilala na Yesu lakini mwisho wa siku akaja kumsaliti.

Luka 24.36 “Na walipokuwa katika kusema habari hiyo, yeye mwenyewe alisimama katikati yao, akawaambia, Amani iwe kwenu.

37 Wakashituka, wakaogopa sana, wakidhani ya kwamba wanaona roho.

38 Akawaambia, Mbona mnafadhaika? Na kwa nini mnaona shaka mioyoni mwenu?

39 Tazameni mikono yangu na miguu yangu, ya kuwa ni mimi mwenyewe. Nishikenishikeni, mwone; kwa kuwa roho haina mwili na mifupa kama mnavyoniona mimi kuwa nayo.

40 Na baada ya kusema hayo aliwaonyesha mikono yake na miguu yake.

41 Basi walipokuwa hawajaamini kwa furaha, huku wakistaajabu, aliwaambia, Mna chakula cho chote hapa?

42 Wakampa kipande cha samaki wa kuokwa.

43 Akakitwaa, akala mbele yao.

44 Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii na Zaburi.

45 NDIPO AKAWAFUNULIA AKILI ZAO WAPATE KUELEWA NA MAANDIKO.

46 Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu;

47 na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu”.

Je! na wewe leo amefunua akili zako, ili upate kuyaelewa maandiko??..ukiona huna hamu ndani yako ya kuyasoma maandiko, na hakuna msukumo wowote ndani yako wa kupenda kusoma Neno, mwombe Bwana leo hii akupe Neema…akupe hiyo nguvu, maana hawezi kukufunulia macho yako ya rohoni uyaelewe maandiko kama maandiko huyasomi… kuna hatari kubwa sana ya kukosa kulijua Neno la Mungu.. Kumbuka Kristo hakufungui macho uuone uso wake yeye, wala halitamani hilo…ingekuwa anataka tuuone uso wake, angeruhusu wakati ule picha yake ichorwe na iifadhiwe kwa vizazi vyetu hivi, kama neno lake limeweza kuhifadhiwa kwa vizazi vyote hivyo si zaidi picha? Ni kitu kidogo sana kuifanya picha yake ihifadhiwe kwa vizazi vyote lakini hakutaka… au angekuja kipindi hichi cha teknolojia ambapo kila mtu angeweza kumpiga picha na kuweka katika chumba chake cha ndani…Lakini hiyo sio njia anayoitumia ili sisi tumwamini yeye…yeye anataka tumwamini yeye, na tumjue, na tumfahamu sana kwa ufunuo wa Neno lake, biblia takatifu. Tukimtafuta katika nyuso tutamkosa hayupo huko…alimwambia Tomaso wana heri wale wasioona wakasadiki.

Je! na wewe ndugu unamtafuta Bwana leo kwa njia ipi? Kwa njia ya uso au maandiko?…Je Bwana amefunua akili zako uweze kumwona? Unasema unampenda Yesu wa kwenye picha au Yesu wa kwenye maandiko?..Na kama ni wa kwenye maandiko je! unayapenda maagizo yake yote aliyoyatoa?. Je! unajumuika na wengine wenye imani moja na wewe kwa maana alisema “wakusanyikapo wawili watatu kwa jina lake atakuwepo katikati yao”. Ni lazima tukusanyike kuanzia wawili na kuendelea ili Kristo, ajumuike pamoja nasi kutufunulia maandiko. Ni muhimu sana kuhudhuria bible study, au kukusanyika na mwenzetu kujifunza biblia kila iitwapo leo maadamu siku ile inakaribia, ndipo tutakapomwona Yesu.

Bwana akubariki sana.

Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine, Bwana akubariki.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

SAA YA KIAMA.

BIBLIA INAPOSEMA “HERI WALIO MASKINI WA ROHO MAANA UFALME WA MBINGUNI NI WAO”JE HATUNA RUHUSA YA KUWA MATAJIRI KATIKA ROHO?.

JE! NI KWELI KUNA VIUMBE VINAVYOISHI SAYARI NYINGINE (ALIENS)?

Mstari huu una maana gani? “Tupa chakula chako usoni pa maji; Maana utakiona baada ya siku nyingi”. (Mhubiri 11:1)


Rudi Nyumbani

Print this post

VIFUNGO VYA GIZA VYA MILELE.

Luka 8: 30 “Yesu akamwuliza, Jina lako nani? Akasema, Jina langu ni Jeshi; kwa sababu pepo wengi wamemwingia.

31 Wakamsihi asiwaamuru WATOKE KWENDA SHIMONI.

32 Basi, hapo palikuwa na kundi la nguruwe wengi wakilisha mlimani; wakamsihi awape ruhusa kuwaingia wale. Akawapa ruhusa.

33 Pepo wakamtoka mtu yule wakawaingia nguruwe, nalo kundi lilitelemka gengeni kwa kasi, wakaingia ziwani, wakafa maji”.

Shalom! Mtu wa Mungu, ni siku nyingine Bwana ametupa neema ya kuliona jua lake, sifa na utukufu ni vyake milele, karibu tujifunze pamoja maneno ya uzima ya Yesu Kristo Bwana wetu, leo tukilitazama kwa undani tukio hilo walilokutana nalo Yesu na wanafunzi wake, mara baada ya kuvuka bahari ya Galilaya pale walipokutana na Yule mtu mwenye jeshi la mapepo waliomsumbua sana kwa muda mrefu, lakini tunaona jambo la kwanza kabisa kama tunavyosoma wale mapepo walichofanya, ni kumsihi Bwana kwa nguvu asiwapeleke SHIMONI..Swali la kujiuliza hapo ni kwanini shimoni na sio sehemu nyingine, na huko shimoni ni wapi?.

Ni wazi kabisa kama tukichunguza mawazo ya hayo mapepo tunaona kuwa yalikuwa yanafahamu kabisa hilo eneo, lakini hayakuwepo kwa wakati huo , na ndio maana jambo la kwanza walipokutana tu na mtu anayewatambua vizuri na makao yao wastahiliyo kuwepo kwa wakati huo moja kwa moja waliona ni heri wajisalimishe na kuomba sharti ya amani mapema, kabla ya mambo mabaya kutokea ya kuamriwa kurudi Shimoni, waliona ni heri wapitie nusu shari kuliko shari kamili.

Mfano leo hii ukiona mtu mwenye akili timamu anachagua kwenda kuishi porini sehemu isiyo na huduma zozote za kijamii kuliko kuishi Mogadishu Somalia, utajua kuwa anazosababu zake za msingi kuchagua hivyo. Jambo la kwanza utajua aidha alishawahi kuishi katika mazingira yote mawili na kuona kule porini ni bora zaidi ya Mogadishu, au alishawahi kusikia habari za kule Mogadishu kwamba sio sehemu salama ya kuweka makazi ya kudumu kwa mtu yeyote kutokana na vita au vitendo vya kigaidi vinavyoendelea kutokea huko mara kwa mara, hivyo akaona bora achague mahali penye unafuu zaidi..

Hali Kadhalika na haya mapepo vivyo hivyo, yalifahamu kabisa hali halisi ya huko shimoni jinsi kulivyo, na ubaya wake, na shida zake na mateso yake, kutokana na kwamba aidha walishawahi kuwepo huko kwa kipindi Fulani au waliwaona wenzao wakiteseka katika makao hayo ya shida, na hivyo wao nao hawataki kwenda huko.

Biblia inasema.

2Petro 2: 4 “Kwa maana ikiwa Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, BALI ALIWATUPA SHIMONI, akawatia katika vifungo vya giza, walindwe hata ije hukumu”;

Unaona? Kama tunavyosoma hapo, makao ya malaika wote ambao hawakuilinda enzi yao, malaika wote ambao hawakuisimamia kweli, malaika wote ambao hawakudumu katika mipaka ya msingi waliyowekewa na Mungu, malaika wote waliokaidi kanuni za Mungu walizopewa waziendee walikuja kutupwa wote shimoni baadaye, katika vifungo vya giza wakae huko mpaka siku ile ya mwisho ya hukumu.

Kama tunavyofahamu mtu akitumbukia katika Shimo refu basi mtu huyo anakuwa katika hali ya mashaka na ya kukosa matumaini, kwasababu makao yake yatakuwa ni pale pale daima isipokuwa labda mtu amekuja kumtoa. Hivyo malaika wote walioasi makao yao yanapaswa yawe ni shimoni kwa sasa, kwenye vifungo vya milele wakingojea hukumu ya mwisho. Lakini pia si wote walio humo kwasasa biblia inasema hivyo, wapo baadhi wanaozunguka zunguka duniani pamoja na mfalme wao ibilisi, Sababu za Mungu kuwaruhusu wao wawe hivyo hatujui Bwana anazijua, lakini wakati utafika Shetani naye atatupwa katika shimo hilo kwa muda wa miaka 1000 akiungana na wale waliokuwa wamefungwa tangu zamani, kisha baadaye ataachiliwa kwa muda mfupi kwa kutimiza kusudi Fulani duniani. Na baada ya hapo ndipo kwa pamoja watatupwa wote kwenye lile ziwa la moto.

Ufunuo 20:1” Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake.

2 Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu;

3 akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache”.

KAMA KUNA BAADHI YA MAPEPO AMBAYO HAYAPO SHIMONI KWA SASA, BASI MAKAO YAO YAKO NI WAPI ?

Hakuna pepo lolote lenye makao ya kustarehe duniani, hakuna mahali popote pepo anapata unafuu isipokuwa ndani ya mtu tu! basi. Nje ya hapo, ni dhiki kubwa na mateso. Na ndio maana wanafanya bidii sana kila mmoja walau apate mahali pa kujiegesha ndani ya mtu duniani. Sasa mara baada ya pepo kumtoka mtu baada ya kuombewa au baada ya mtu kumpa Kristo maisha yake haliendi kustarehe mahali Fulani tu, hapana linakwenda mahali pa jangwa, mahali penye ukame. Bwana Yesu alisema hivi.

Mathayo 12:.43 “Pepo mchafu, amtokapo mtu, HUPITIA MAHALI PASIPO MAJI, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate.

44 Halafu husema, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija, aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa.

45 Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya”.

Unaona hapo linakwenda mahali pasipo maji ni sawa na kusema linakwenda mahali pa jangwa pasipo na uhai, mahali pa shida na dhiki pasipo kuwa na kiburudisho chochote. Sasa pepo linapomtoka mtu ndipo katika roho linakuwa katika hali kama hiyo ya mtu aliyeachwa jangwani mwenyewe pasipo na msaada wowote. Kumbuka Hapo ni tofauti na shimoni, na kwa jinsi atakavyoendelea kukosa mahali pa kutulia ndivyo hali yake itakavyozidi kuwa mbaya zaidi, sawasawa tu na wale walioko shimoni. Ataendelea hivyo hivyo mpaka siku ile ya mwisho ya Hukumu ambayo wote kwa pamoja na wale walio vifungoni kwenye mashimo sasahivi watakapotupwa kwenye lile ziwa la moto.

Hivyo unaweza ukuona ni shida nyingi kiasi gani hivi viumbe vilivyolaaniwa vinapitia vinapokosa mahali pa kustarehe, lakini sasa pale mtu anapovipa makao katika mwili wake, mtu huyo naye anafanyika kuwa mwana wa laana, Mungu anamwona mtu kama huyo naye anastahili kutupwa shimoni. Naye pia anashiriki laana zile zile walizowekewa hayo mapepo tangu zamani.

Na ndio hapo sasa mtu mwovu akifa, pindi tu anapokata roho moja kwa moja anajikuta anashuka kwenye shimo refu la giza, kwenye vifungo vya milele sasa huko chini kuna taabu na mateso yasiyoneneka Mahali ambapo baadhi ya hayo mapepo yalipo sasahivi, mateso ya huko ni makubwa jaribu kifikiria hata mapepo yaliyopo duniani hayataki kupelekwa huko, ni mahali pabaya kiasi gani.

Sasa wote kwa pamoja wataendelea kukaa huko wakisubiria hukumu ya siku ile ya mwisho kisha watupwe kwenye lile ziwa la moto. Hayo ndio mambo yaliyowakuta hata watu wa kipindi cha Nuhu na watu wa kipindi cha Sodoma na Gomora biblia inasema sasahivi wapo katika vifungo hivyo vya milele, wapo shimoni wakingojea hukumu ya mwisho na ndipo wahukumiwe na kutupwa kwenye lile ziwa la moto.

Yuda 1:6 “Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu.

7 Kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kando-kando, waliofuata uasherati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele”.

2Petro 2: 4 “Kwa maana ikiwa Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika vifungo vya giza, walindwe hata ije hukumu;

5 wala hakuuachilia ulimwengu wa kale, bali alimhifadhi Nuhu, mjumbe wa haki, na watu wengine saba, hapo alipoleta Gharika juu ya ulimwengu wa wasiomcha Mungu;

6 tena akaihukumu miji ya Sodoma na Gomora, akiipindua na kuifanya majivu, akaifanya iwe ishara kwa watu watakaokuwa hawamchi Mungu baada ya haya;”

Unaona hapo? Kuna hatari nyingi sana leo hii tukiifanya miili yetu kuwa makao ya mashetani, mtu yeyote ambaye bado hajasafishwa kwa damu ya YESU KRISTO na kupata ondoleo la dhambi zake na kubatizwa ipasavyo na kupokea Roho Mtakatifu, basi mtu huyo yeye ni makao na kimbilio la roho chafu za mashetani zilizoasi.. Mtu yeyote ambaye ni mwasherati na mzinzi basi yeye ni hifadhi wa makao ya mapepo, mtu yeyote ambaye ni mwabudu sanamu, kadhalika yeye naye ni makao ya mapepo, mtu yoyote aliye mshirikiana na mchawi, na anayejihusisha na masuala ya waganga wa kienyeji, mwili wake ni makao ya mapepo wachafu..mwanamke yeyote ambaye anavaa nguo za uchi, na vimini na suruali basi huyo ni makao ya mapepo. Na akiendelea hivyo hivyo mpaka siku atakapokufa naye moja kwa moja atajikuta kwenye vifungo vya shimo hilo la kuzimu pamoja na watu wa sodoma na gomora na watu wa kipindi cha Nuhu pamoja na yale mapepo wakisubiria hukumu ya siku ya mwisho. Kisha wakatupwe kwenye lile ziwa la moto.

Zamani katika agano la kale mtu mwenye pepo hukumu yake ilikuwa ni kifo.

Walawi 20: 26 “Nanyi mtakuwa watakatifu kwangu mimi; kwa kuwa mimi Bwana ni mtakatifu nami nimewatenga ninyi na mataifa, ili kwamba mwe wangu.

27 TENA MTU MUME AU MTU MKE ALIYE NA PEPO, au aliye mchawi, hakika atauawa; watawapiga kwa mawe; damu yao itakuwa juu yao”.

Tukiyajua hayo, na tukifahamu kuwa shetani na mapepo yake yanazunguka kila siku duniani yakitafuta hifadhi ndani ya wanadamu. Basi tutaishi maisha ya kujichunga kila siku. Tutazijaribu hizi roho zote zinazokuja mbele yetu na mafundisho yake ya uongo. Tutaishi maisha ya uangalifu huku tukimruhusu Roho Mtakatifu achukue sehemu yote ya maisha yetu. 

Print this post

TUSIFUNGWE NIRA PAMOJA NA WASIOAMINI.

2 Wakorintho 6:14 “Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, KWA JINSI ISIVYO SAWASAWA; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?”

Biblia inasema tusifungiwe Nira pamoja na wasioamini..NIRA ni KIFAA kinachowekwa katikati ya wanyama wawili wa jamii moja, kinachowafunga pamoja…ili kutimiza kusudi la kazi Fulani, kama vile kulima, kusafirisha mizigo n.k mfano ng’ombe wawili wanaweza kufungwa nira pamoja kwa kazi ya kilimo, na kulivuta lile jembe nyuma yao…kadhalika farasi wawili wanaweza kufungwa nira moja ili kulivuta gari la kubebea watu au vitu nyuma yao..Punda nao wanaweza kufungwa nira pamoja ili kusaidia kuvuta mzigo Fulani nyuma yao…

Tukirudi katika maandiko biblia inatuonya tusifungwe nira pamoja na wasioamini, Kumbuka haikumaanisha tukae mbali kabisa na wasioamini, au tusizungumze nao, au tusifanye nao kazi, au tusiishi nao, au tusisome nao au tusile nao, au tusisalimiane nao…hapana haikumaanisha hivyo… ukisoma kwa makini huo mstari unasema “msifungiwe nira pamoja na wasioamini kwa jinsi isivyo sawasawa”..Sasa zingatia hilo neno “kwa jinsi isivyo sawasawa”… Ikiwa na maana kuwa kumbe kuna jinsi iliyo sawasawa ambayo tunaweza tukafungwa nao nira, unaweza ukafanya kazi ofisi moja na mtu asiyeamini, unaweza ukasoma darasa moja na mtu asiyeamini, unaweza ukala sahani moja ya chakula na mtu asiyeamini kama Bwana alivyofanya n.k…Lakini kuna mipaka ambayo hatupaswi kufungiwa nao Nira.

Kwa mfano, mtu asiyeamini anaweza akawa ni mwizi, au mwasherati, au mtukanaji sasa kama ni shuleni tunaweza tukawa naye darasa moja, tukazungumza naye kwa upendo na kujaribu kumvuta kwa KRISTO lakini, kukaa naye katika mazingira yake ya utukanaji, au ya uasherati, au ya wizi au ya usengenyaji hayo tumeonywa tujiepushe nao…kushirikiana naye katika anasa, au ulevi hivyo vyote tumeonywa tukae mbali navyo..tukiwa shuleni tutashirikiana nao katika masuala ya shuleni tu basi, lakini masuala ya kwenda disko, au kwenye starehe za kidunia, au kutazama picha chafu, au kufanya nao mustarbation hayo tumeonywa..vivyo hivyo kazini tutashikamana nao kwa masuala ya kazini tu basi..lakini katika eneo la maisha ya rohoni hilo tumeonya tujiepushe nao.

Sasa kwanini Bwana alituonya tusijifunge Nira nao kwa jinsi isivyopaswa?.

Kwani tukiishi nao hivyo hivyo kuna shida gani??..si tutajiepusha nao tu!!

Hekima ya Mungu ni kuu kuliko hekima ya mwanadamu… Umewahi kujiuliza kwanini watu wa ukanda Fulani wana lafudhi zinazofanana? Au wana tabia zinazofanana?..Unadhani wote walipenda wawe wanalafudhi zinazofanana? Au walishauriana wawe vile?..Utakuja kugundua kwamba ni “kule kukaa pamoja kwa muda mrefu” ndiko kuliko wafanya wote wafanane tabia na lafudhi bila hata wenyewe kujijua kuwa wapo hivyo.

Kwahiyo unaweza ukaona kuwa kuna nguvu Fulani ya kumbadilisha mtu ipo katika ya jamii anayojiunganisha nayo..hata kama yeye hataki lakini kwa jinsi anavyokaa na ile jamii atajikuta tu kwa muda Fulani ameshafanana na jamii ya wale watu kiusemi, na kifikra.

Ndio maana katika agano la kale Bwana alitoa maagizo punda na ng’ombe wasifungwe nira pamoja…punda afungwe na punda mwenzake na ng’ombe afungwe na ng’ombe mwenzake… Kumbukumbu 22: 10 “Usilime kwa ng’ombe na punda wakikokota jembe pamoja”.

Unajua ni kwasababu gani?

Sababu ni kwamba watakapofungwa nira pamoja punda na ng’ombe..kuna tabia ng’ombe alizo nazo punda atakazoanza kuziiga na kadhalika kuna baadhi ya tabia za punda ng’ombe ataziiiga hivyo itazaliwa tabia moja ambayo haifai katika shughuli zozote za kazi..

Fuatilia utaona kuwa mahali palipo na mchanganyiko wa kuku na bata, utaona bata kuna wakati wanaonyesha tabia Fulani kama za kuku na kuku vivyo hivyo kuna wakati wanaonyesha tabia kama za Bata..Mimi nimewahi kushuhudia hilo na pia kitafiti limethibitishwa…Pia kwa wanyama wengine wote ndio hivyo hivyo, wakichanganyikana pamoja wanakuwa wanaingiliana tabia…

Hivyo ndivyo Bwana alivyoviumba viumbe vyake vyote ikiwemo wanadamu kwamba…tabia ya mmoja inaweza kumuathiri na kumgeuza mwingine endapo wakikaa pamoja kwa muda mrefu.

Ndio maana maandiko yanazidi kusema katika ..

Mithali 22: 24 “Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira nyingi; Wala usiende na mtu wa ghadhabu nyingi; .. USIJE UKAJIFUNZA NJIA ZAKE; NA KUJIPATIA NAFSI YAKO MTEGO”.

Unaona hapo?..inasema usije ukajifunza njia zake? HIYO KUJIFUNZA sio kujifunza kwa kutaka hapana! Hakuna mtu yoyote anapenda kujifunza njia mbaya…hiyo kujifunza ni tabia ambayo inaingia ndani ya mtu pasipo hata yeye kujijua, kama alikuwa sio msengenyaji na akakaa na mtu ambaye ana tabia ya kuzungumzia habari za watu wengine kila wakati..na yeye baada ya muda Fulani atajikuta tu anaanza anazungumzia habari za wengine kila mahali…

Kama alikuwa hana hasira nyingi lakini akajiunganisha na mtu wa hasira nyingi na anaye kufoka foka..mara ya kwanza ataishangaa ile tabia lakini baada ya muda Fulani, ataona ile hali ni ya kawaida tu! Kutukana na kukasirika ni kawaida…hivyo na yeye atakapoudhiwa kidogo tu hasira zitamjia na kuanza kufoka na kutukana kama mwenzake anavyofanya, kwasababu moyo wake ulishakufa ganzi siku nyingi..Hata mara ya kwanza ukipita mahali penye kelele nyingi na harufu nyingi tofauti tofauti siku ya kwanza utaona kuna usumbufu mkubwa na harufu nyingi lakini kwa jinsi utakavyoendelea kupita hapo kila siku, unakuja kuona ile sehemu ni ya kawaida tu! Unapazoea!! Harufu zinapotea na kelee huzioni tena kuwa ni nyingi..Watu wanaoishi machinjioni ukiwauliza hivi huwa hamwisikii hiyo harufu mbaya ya damu, watakujibu hawasikii kitu wanaona kawaida tu! Ni kwasababu gani ni kwasababu wameshakufa ganzi katika yale mazingira.

Kwahiyo ni kujihadhari kama Bwana anavyotuonya..Yeye ndiye aliyetuumba sisi, ana hekima kuliko sisi, unajua madhaifu yetu yapo wapi, na ndio anatuambia “tusifungwe nira pamoja nao kwa jinsi isivyopaswa” Kinyume chake tujifunge nira na wanaoamini, maana hao nao watatuambukiza tabia zao njema zinazompendeza Mungu..ndio maana Bwana alipowatuma wanafunzi wake aliwatuma wawili wawili..kuonyesha kwamba Bwana anatufunga nira yake kuanzia wawili na kuendelea? Kwasababu na yeye Bwana anayo Nira yake, anayotufunga sisi watoto wake pamoja, lakini anasema Nira yake ni laini na mzigo wake ni mwepesi..Maagizo yake sio mazito tunapokuwa wawili au watatu kwa jina lake, tunakuwa tuna uwezo wa kushinda kwasababu tumefungwa nira yake pamoja.

Ni matumaini yangu, kuanzia leo utaangalia mazingira yanayokuzunguka, na watu unaojishughulisha nao, je! ni kwa mambo ya maana tu, au wanaingilia mpaka utaratibu wako wako Imani. TUJILINDE!

Bwana akubariki.

Tafadhali tangaza habari njema za ufalme popote ulipo, kama umeshampa Bwana maisha yako, na pia kama hujamkabidhi Bwana maisha yako, ni vyema ukafanya hivyo leo kabla nyakati za hatari hazijaanza, maana tunaishi katika kipindi cha siku za mwisho, ambacho Bwana yupo karibu sana kurudi.


Mada Nyinginezo:

JE! TUNARUHUSIWA KUMUOMBEA MTU AMBAYE HAWEKI BAYANA KILE ANACHOHITAJI KUOMBEWA?

KUWAHUDUMIA MALAIKA PASIPO KUJUA.

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 6


Rudi Nyumbani

Print this post

KWANINI TUWE WENYE BUSARA KAMA NYOKA?

Mathayo 10:16 “Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.”

Sentensi hiyo imekuwa ikiwatatiza wengi, wakijiuliza ni kwanini Bwana YESU alisema maneno kama hayo: IWENI NA BUSARA KAMA NYOKA. Kwani nyoka anayobusara gani, kwanini hapo asingesema iweni na busara kama simba au mnyama mwingine wa mwituni na sio nyoka?. Tunafahamu katika biblia nyoka ni mnyama aliyepoteza sifa kuliko wanyama wote aliowaumba Mungu, kadhalika ni mnyama aliyelaaniwa kuliko wanyama wote, katika biblia mnyama anayefananishwa na shetani ni nyoka peke yake, tofauti na wanyama wengine kama njiwa ambaye anaonekana akimwakilisha Roho Mtakatifu na wanyama wengine kama kondoo, ng’ombe, na simba lakini nyoka hastahili hata kutamkwa kwenye vinywa vya wakristo kwa sifa njema lakini hapa Bwana kamtaja.

Na zaidi ya yote Bwana wetu YESU anatuonya na kutumbia; basi iweni na busara kama nyoka, Leo hii tutafunza ni busara gani nyoka aliyokuwa nayo.

Awali ya yote ukisoma kuanzia ule mstari wa 1 utaona kuwa maneno hayo Bwana Yesu alikuwa anawaambia wale wanafunzi wake 12. Muda huo alikuwa anawapa maagizo ya msingi ya kuzingatia katika kwenda kufanya kazi ya utumishi. Ni mahusia ya msingi kabisa ambayo walipaswa wazingatie na sio tu katika kile kipindi walichokuwa na Bwana Yesu pindi walipotumwa bali pia hata baada ya kuondoka kwake. Na ndio hapo tunakuja kusoma huo mstari wa 16, akiwaambia maneno hayo akisema: “Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu;”.. Umeona hapo? Mpaka hapo tumeshafahamu kuwa maneno hayo yanawahusu wale tu WANAOTUMWA!, na si watu wengine.

Sasa hao ndio walioambiwa katika kutumwa kwao wanapaswa wawe na tabia kama kondoo katikati ya mbwa-mwitu, na sio kama simba katikati ya mbwa-mwitu, hii ikiwa na maana kuwa watakapotendewa mabaya au watakapopigwa au watakapoudhiwa wasirudishe baya kwa baya, bali wajifanye kama kondoo wasioweza kufanya lolote. Bwana alikuwa anayomaana ya msingi kabisa kuwaambia hivyo, kwasababu alijua umuhimu wake katika kuziokoa roho za watu. na ndio tabia tuliokuja kuiona kwanza kwa Bwana wetu YESU Kristo kisha kwa mitume wake baadaye..Sasa baada ya hapo, ndipo akawapa maagizo haya kwamba huko mtakapokwenda IWENI NA BUSARA KAMA NYOKA. NA KUWA WATU WAPOLE KAMA HUA.

Ni busara gani aliyonayo NYOKA?

Nyoka anavyozungumziwa hapa ni nyoka jinsi alivyokuwa katika asili yake pale Edeni.Embu jaribu kifikira Adamu na Hawa watu ambao Mungu alikuwa anazungumza nao uso kwa uso wakiisikia sauti yake kila siku kwa kipindi cha muda kirefu sana, wakiyatimiza maagizo yake yote aliyowapa kwa muda mrefu kwamba wasile matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, halafu kirahisi rahisi tu ndani ya siku moja wakate shauri waache kuyatii maagizo ya Mungu na kuasi..Usidhani ni jambo jepesi jepesi kufikia hatua ya kula lile tunda, ushawishi wa namna hiyo unahitaji maarifa na busara ya hali ya juu sana..

Nyoka alijua kabisa ili kuwapata wale watu sipaswi kutumia nguvu ya aina yoyote, kama angejaribu kufanya hivyo basi yeye mwenyewe angejikuta kwenye hali mbaya sana kwasababu Adamu asingemvumilia. Alijua kabisa hapaswi kutumia maneno ya kufuru kwa Mungu wao, kama angefanya hivyo basi Adamu asingemvumilia pia kwa hilo, alijua kabisa kuzungumza na Adamu ni ngumu hivyo akatafuta njia mbadala mahali palipo dhaifu ili afanikishe mpango wake wa kuwadondosha. Alitumia busara nyingi kuupindua mpango wa Mungu uliokuwa ndani ya wanadamu. Hivyo japo aliruhusu busara yake itumiwe vibaya na shetani lakini bado mbele za Mungu alionekana kuwa ni mnyama mwenye busara nyingi..

Hata baada ya kulaaniwa, unamwona katika mawindo yake, hatumii papara, huwa unatulia sana, na kukamata mawindo yake kwa ghafla, hana mikono, hana miguu, lakini anamkamata panya mwenye uwezo mkubwa wa kusikia, na kuponyoka.

Unaukumbuka ule mfano Bwana alioutoa katika Luka 16:1-9, wa Yule wakili aliyekuwa mwizi, lakini katika wizi wake alikuwa na busara?…Kama hukuwahi kuupitia basi kaupitie tena, naamini utajifunza kitu.

Vivyo hivyo na wale wanaotumwa na Bwana kupeleka injili, Bwana YESU anawaambia IWENI NA BUSARA KAMA NYOKA. Alimaanisha kuwa huko waendako watakutana na watu waliojikita katika misingi ya imani zao potofu, hata ufanyeje huwezi kuwang’oa mahali walipo..Shetani ameshawahubiria kwa miaka mingi, kwamba akitokea mtu mwingine anawaletea habari za Imani nyingine zaidi ya hiyo waliyofundishwa hawawezi kuwaamini wala kuwapokea. Hivyo kama huyo anayetumwa kupeleka Injili hataweza kutumia busara kuwahubiria habari mpya ya wokovu katika Kristo Yesu basi anaweza kujikuta anampoteza kondoo Yule au anajitafutia matatizo yeye mwenyewe yasiyo ya lazima.

Leo inasikitisha kuona mtu anasema ni mtumishi wa Kristo na ni mhubiri lakini mambo anayoyafundisha kwa watu ambao wapo katika misingi ya imani nyingine mbali na Kristo, haina busara kabisa..Utamkuta anakutana na mtu labda pengine haamini katika kula nyama ya nguruwe. Lakini yeye kwasababu anajua kuwa nguruwe si kitu mbele za Mungu, badala ya kumfundisha mambo ya msingi, halafu kwa jinsi atakavyoendelea kukua kiiamini baadaye ndipo amwambie na habari hizo pia, jambo la kwanza ataanza kwa kumwambia nguruwe si dhambi!, ataanza kuwaambia dini yenu ni ya kigaidi, ataanza kuwaambia mnaabudu majini n.k. Unadhani itakuwa ni rahisi kumvuta huyo mtu kwa Kristo? Jibu ni hapana Kinyume chake utazua migongano na malumbano na kusababisha jina la Mungu kutukanwa.

Mtume Paulo katika safari yake ya kutangaza injili alikutana na watu wengi tofauti tofauti, lakini alifanikiwa kuwageuza wengi wao kwa busara ya Roho iliyokuwa ndani yake. Tunasoma hayo katika

1Wakorintho 9: 20 “Nalikuwa kama Myahudi kwa Wayahudi, ili niwapate Wayahudi; kwa wale walio chini ya sheria, nalikuwa kama chini ya sheria, (ingawa mimi mwenyewe si chini ya sheria), ili niwapate walio chini ya sheria.

21 Kwa wale wasio na sheria nalikuwa kama sina sheria, (si kwamba sina sheria mbele za Mungu, bali mwenye sheria mbele za Kristo), ili niwapate hao wasio na sheria.

22 Kwa wanyonge nalikuwa mnyonge, ili niwapate wanyonge. Nimekuwa hali zote kwa watu wote, ili kwa njia zote nipate kuwaokoa watu.

23 Nami nafanya mambo yote kwa ajili ya Injili ili kuishiriki pamoja na wengine”.

Wakolosai 4:5 “Enendeni kwa hekima mbele yao walio nje, mkiukomboa wakati.

6 Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea munyu, mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu.

Unaona hapo?. Tukikosa busara, tutazua mashindano ya dini badala ya wokovu kwa watu. wengine wanapotukanwa tu kidogo wao nao wanarudisha matusi, hawajui kuwa wale ni mbwa-mwitu ni kawaida yao kutukana, sasa na wao kwa kukosa busara wanarudisha na wao dhihaka, sasa hapo ni mtu gani unatazamia aupokee wokovu?. Matokeo yake badala ulete faida katika ufalme wa mbinguni unaleta hasara kwa jambo dogo tu la kukosa busara.

Upo mitandaoni, badala ya kuwavutia watu Kristo wampokee ndani yao, unakwenda kutafuta sehemu za madhaifu yao na kuanza kuwakasirisha kwa maneno ya hasira, hujui kuwa ipo siku utaulizwa na Bwana kwa hiyo huduma unayoifanya: Sisemi kuwa hupaswi kukosoa mabaya, lakini katika ukosoaji wako tumia busara. Angalia mwisho wa siku unamshawishi nani?. Au malengo yako ni nini? kukoa au kuonyesha kuwa wale hawako sahihi na wewe upo sahihi?. Jichunguze lengo lako ni nini? kujenga au kutaka kuonyesha kuwa una ujuzi mwingi?..Biblia inasema upendo hujenga, bali ujuzi huleta majivuno (1 Wakoritho 8:1)

Luka 12:42 “Bwana akasema, Ni nani, basi, aliye wakili mwaminifu, MWENYE BUSARA, ambaye bwana wake atamweka juu ya utumishi wake wote, awape watu posho kwa wakati wake?

43 Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta anafanya hivyo.

44 Kweli nawaambia, atamweka juu ya vitu vyake vyote.

45 Lakini, mtumwa yule akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia kuja, akaanza kuwapiga wajoli wake, wanaume kwa wanawake, akila na kunywa na kulewa;

46 bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani na saa asiyojua, atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wasioamini.”

Unaona?. Ni maombi yangu kwa kusoma haya sisi sote hatutaanza kuwa mawakili wenye busara wa Kristo, ambao tutawapa posho wale walio nje kwa wakati, na sio kuwapiga, na kuwaudhi, na kuwadharau ili Bwana atakapokuja atupe thawabu iliyostahili, na tufanikiwe kuleta matunda mengi kwa Bwana.

Ubarikiwe sana.

Print this post

DHAMBI YA ULIMWENGU.

Dhambi ipo moja tu! nayo ni kutomwamini BWANA YESU KRISTO, hayo mengine ni matokeo ya dhambi, uwizi, usengenyaji, rushwa, uasherati, utukanaji, uuaji n.k si dhambi bali ni matokeo ya dhambi iliyo moja tu! nayo ni KUTOKUMWAMINI BWANA YESU KRISTO.

Na kumbuka kumwamini Yesu Kristo, sio kumsoma na kuamua kumwamini, hapana! Bali ni kupata ufunuo wa yeye ni nani, alitoka wapi, alikuja kufanya nini, na umuhimu wake kwa ulimwengu ni upi?.…ukishamwelewa kwa namna hiyo, basi ndani yako kutawaka shauku ya kutaka kujishughulisha na mambo yake (hapo utakuwa tayari umeshamwamini).

Kwahiyo kama dhambi ni moja tu! ambayo ni kutokumwamini Kristo Yesu Kristo, hayo mengine ni matokeo ya hiyo dhambi, Hivyo siku ya hukumu Bwana hatamuhukumu mtu kwasababu alikuwa mvuta bangi, au kwasababu alikuwa mwasherati, au kwa sababu alikuwa mwongo…hapana atamuhukumu mtu kwanza kwa sababu hakumwamini YESU KRISTO, MWANA WA MUNGU. Hiyo ndiyo dhambi ya msingi kabisa..

Yohana 3: 17 “Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.

18 Amwaminiye yeye hahukumiwi; ASIYEAMINI AMEKWISHA KUHUKUMIWA; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu”.

Tuchukue mfano mwepesi, kuna kichaa mahali Fulani, kaonekana akivunja vioo vya magari ya watu, na kupiga watu barabarani, na kaharibu mali, na kisha wakamkamata na kumfunga kamba! Je! wale waliomfunga kamba watamhukumu kwanza kwa kuanza kumuuliza kwanini amevunja vioo vya magari?, au kwanini anapiga watu, au kwanini ni mwaribifu…utagundua kwamba! Hawataweza kufanya hivyo…watajua tatizo halipo katika matendo anayoyafanya, bali tatizo lipo katika akili zake nalo ni ile hali ya ukichaa iliyondani yake!!…Hivyo wakitaka wapate ufumbuzi wa tatizo lao, watashughulika kwanza na tiba ya akili yake, zaidi ya tiba ya mambo anayoyafanya, hawawezi kumshauri aache uaribifu, au aache kupiga watu katika hali yake ya ukichaa aliyokuwepo, ni sawa na kupaka rangi upepo.. sharti wamtibu kwanza tatizo lake hilo moja!..Na mengine yatatibika yenyewe.

Ndivyo ilivyo kwa mtenda dhambi yoyote yule aliye mwasherati, mwizi, muuaji, mla rushwa, msengenyaji n.k….tatizo lake ni moja tu HAJAMWAMINI YESU KRISTO. Hajapata ufunuo utakaoweza kumfanya aache vitendo viovu. Na njia pekee ya kuviacha hivyo haitaokani na bidii au nguvu za mtu binafsi, anaweza akajitahidi kufanya hivyo leo na kesho lakini kesho kutwa akarudia uchafu wake ule ule wa kale, bali hiyo inakuja kwa kumwamini yule awezaye kuondoa mambo hayo ndani ya mtu. Na huyo si mwingine zaidi ya YESU KRISTO.

Biblia inasema “ Yohana 1:29 “Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, AICHUKUAYE DHAMBI YA ULIMWENGU!”

Ukisoma hapo kwa makini utaona hakusema “AZICHUKUAYE DHAMBI ZA ULIMWENGU” bali imesema “AICHUKUAYE DHAMBI YA ULIMWENGU”..ikimaanisha kuwa hiyo dhambi NI MOJA TU! sio nyingi nayo ni KUTOKUAMINI. Ndugu Yesu pekee ndiye anayeweza kuwa tiba ya hofu unayopitia sasa hivi, yeye pekee ndiye anayeweza kuwa kimbilio lako yeye pekee ndiye nguvu zako na faraja yako, yeye pekee ndiye kila kitu kwako, wewe peke yako hutaweza kuondoa dhambi yoyote ndani yako, kadhalika mwingine yoyote hakuna. Hivyo Ndivyo ilivyo, na ndivyo itakavyokuwa daima. Na huo ndio ukweli. Hakuna mwingine, na mtu akimpinga huyo basi amethibitisha kwamba yeye mwenyewe anaweza kujiokoa na kusimama kwa nguvu zake kumshinda shetani na dhambi…Lakini fahamu kuwa hakuna ambaye alishawahi kuwa mkamilifu kwa nguvu zake mwenyewe tangu dunia kuumbwa isipokuwa YESU pekee.

Kwa yeyote atakayemwamini na kumpokea HATI hiyo ya dhambi itaondolewa juu yake. Na kutakaswa kila siku wa Roho wake. Lakini kwa atakapuuzia hukumu hatoikwepa kwa namna yoyote.

Bwana alisema sharti injili ikahubiriwe kwa kila kiumbe, ndipo ule mwisho uje!! Na ni kwasababu Neno lake huwa halipiti! Ni lazima kila mtu atasikia habari za Yesu Kristo, wengine mara moja tu! wengine mara mbili mbili, wengine mara tatu tatu..Lakini mwisho injili itasikika kwa kila mtu, Roho Mtakatifu atanyanyua watu wake popote pale, iwe mijini, iwe vijijini, iwe shuleni, iwe mtaani, iwe gerezani iwe ikulu..Injili itafika..Na wewe unayesoma ujumbe huu, leo imekufikia kwa njia hii, sijui kwako hii ni mara ya ngapi?..labda ni mara ya kwanza, au mara ya 20..jibu unalo wewe… Lakini umesikia habari za Huyu Yesu Mkombozi wa ulimwengu na Madhara ya kutomwamini. Ni heri ukamtafuta leo kabla nyakati za hatari hazijafika…Ukimpokea na kumwamini atausafisha uovu wako wote, na kukufanya wewe kiumbe kipya.

1 Yohana 5.3 “Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito.

4 Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu.

5 Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, ISIPOKUWA NI YEYE AAMINIYE YA KWAMBA YESU NI MWANA WA MUNGU?

6 Huyu ndiye aliyekuja kwa maji na damu, Yesu Kristo; si katika maji tu, bali katika maji na katika damu.

7 Naye Roho ndiye ashuhudiaye, kwa sababu Roho ndiye kweli”.

Tafadhali “share” na pia wahubirie wengine habari njema za msalaba kwa kadri uwezavyo popote ulipo.Na pia tembelea website yetu /www wingulamashahidi org/ kwa mafundisho ya ziada.

Bwana akubariki.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

JE! SISI NI WAFALME NA MAKUHANI KWA NAMNA GANI?

BIBLIA INASEMA “HAMJUI YA KUWA MTAWAHUKUMU MALAIKA? (1WAKORINTHO 6:2-3) ” TUTAWAHUKUMUJE?.

NADHIRI.

MANA ILIYOSHUSHWA KUTOKA MBINGUNI.


Rudi Nyumbani

Print this post

NADHIRI.

Kumbukumbu 23: 21 “Utakapoweka nadhiri kwa Bwana, Mungu wako, usiwe mlegevu katika kuiondoa; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, hataacha kuitaka kwako; nayo hivi itakuwa dhambi kwako.

22 Lakini ukijizuia usiweke nadhiri, haitakuwa dhambi kwako.

23 Yaliyotoka midomoni mwako yashike kuyafanya; kwa mfano wa ulivyomwekea nadhiri Bwana, Mungu wako, ni sadaka ya hiari uliyoahidi kwa kinywa chako”.

Nadhiri, ni kitu chochote unachoweza kukiahidi kumtolea Mungu kwa ihari yako mwenyewe. Na kitu hicho kinaweza kuwa sadaka mfano mali, fedha, shamba n.k..Lakini pia nadhiri ni ahadi mtu anayoweza kuiahidi ya maisha Fulani mbele za Bwana mfano mtu anaweza akaahidi mbele za Bwana kumtumikia yeye endapo atafanyiwa kitu Fulani na Mungu..Mfano tunamwona Yakobo wa kwenye maandiko.. wakati ambapo anamkimbia Esau Ndugu yake kwasababu aliuchukua mbaraka wake maana Esau alimkasirikia kwa hilo…Hivyo ikamlazimu Yakobo aende nchi ya mbali katika ukoo wa baba yake na mama yake huku akiwa mikono mitupu hana kitu kabisa… Na wakati akiwa njiani akamwekea Mungu nadhiri kwamba endapo Mungu atamlinda njia aiendayo na kumfanikisha katika chakula na mavazi ndipo Yehova atakuwa Mungu wake na atamtolea yeye fungu la kumi la kwa kila alichopewa.. Tunasoma hayo katika..

Mwanzo 28: 18 “Yakobo akaondoka asubuhi na mapema, akalitwaa lile jiwe aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha kama nguzo, na kumimina mafuta juu yake.

19 Akaita jina la mahali pale Betheli; lakini jina la mji ule hapo kwanza uliitwa Luzu.

20 Yakobo akaweka nadhiri akisema, Mungu akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae;

21 nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo Bwana atakuwa Mungu wangu. 22 Na jiwe hili nililolisimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi”.

Na tunaona baada ya kumwekea Mungu hiyo nadhiri, Bwana Mungu kweli alimfanikisha Yakobo alimpa utajiri mwingi katika mifugo na mali na wakati anamrudia ndugu yake Esau kutoka kwa Labani mjomba yake, aliikuwa amepata mali nyingi sana na utajiri , na ndipo Yakobo akaitoa nadhiri ile, akamtumikia Mungu siku zake zote na kumtolea fungu la kumi.

Mwanzo 31: 13 “Mimi ni Mungu wa Betheli, huko ulikotia mafuta nguzo, na kuniwekea nadhiri. Sasa ondoka, toka katika nchi hii, urudi mpaka nchi ile uliyozaliwa”.

Kwahiyo hiyo ni moja wapo ya nadhiri, nadhiri ya kumtumikia Mungu, endapo atakufanyia kitu Fulani. Na kama tunavyoona hapo Mungu anakumbuka kila nadhiri mtu anayoiweka mbele zake, alikumbuka ya Yakobo siku aliyomwekea na mahali alipomwekea..hivyo anamkumbusha.

Kuna usemi unaosema kwamba AHADI ni DENI, lakini NADHIRI ni ZAIDI YA DENI..ni kifungo, biblia inatuonya kabla hatujaweka nadhiri, tujitafakari kwanza mara mbili mbili mbele za Mungu kabla ya kuchukua uamuzi huo.. Inasema

Hesabu 30: 1 “Kisha Musa akanena na wale vichwa vya kabila za wana wa Israeli, na kuwaambia, Neno hili ndilo aliloliagiza Bwana.

2 Mtu atakapomwekea Bwana NADHIRI, au, atakapoapa kiapo ili kufunga nafsi yake kwa kifungo, asilitangue neno lake; atafanya sawasawa na hayo yote yamtokayo kinywani mwake”.

Na pia inarudia kusema kitu hicho hicho katika kitabu cha… 

Mhubiri 5:4 “Wewe ukimwekea Mungu NADHIRI, usikawie kuiondoa; KWA KUWA YEYE HAWI RADHI NA WAPUMBAVU; basi, uiondoe hiyo uliyoiweka nadhiri.

5 Ni afadhali usiweke nadhiri, Kuliko kuiweka usiiondoe”.

Mistari yote hiyo inaonyesha jinsi gani Mungu anafuatiliza kila Neno linalotoka katika kinywa cha mtu, Neno lolote linalotoka vinywani mwetu mbele za Bwana.

Kitu kimoja wengi wasichojua ni kwamba, NDOA NI NADHIRI. Na kwanini Mungu anachukia kuachana sio kwasababu tu Mungu anachukia uasherati! Hapana zaidi ya hilo anachukia sana mtu anapoivunja nadhiri aliyoitoa kwa kinywa chake. Wakati wa ndoa kufungwa mtu anaahidi mbele za Mungu kuishi kwa upendo, na mwenzake na kwa uvumilivu, kutoachana katika hali yoyote ile watakayoipitia katika maisha, aidha katika umaskini au katika utajiri, katika uzima au ulemavu, katika huzuni au furaha n.k..Na wanaahidi kuwa Kifo ndicho kitakachowatenganisha…

Sasa kwa wanandoa kama hawa pasipo kufikiri wanaweza wakadhani kuwa wameahidiana wao hizo ahadi, kumbe hawajui na nadhiri wamemwekea Mungu..kwasababu wamekwenda kuziweka mbele zake..Na endapo ikitokea wameachana kwasababu yoyote mojawapo ya hizo hapo juu, Biblia inasema “Bwana hawi radhi na wapumbavu”..inasema ni afadhali mtu kutokuiweka kabisa kuliko kuiweka asiiondoe..Hicho ni kifungo cha maisha.

Kumuacha mke wako au mume wako kwasababu tu amekuwa maskini, au mlemavu…ni tiketi kamili ya kwenda katika lile ziwa la moto hakuna msamaha juu ya hiyo dhambi, ukimwacha mume wako au mke wako kwasababu tu mmegombana siku moja au kwasababu amekuwa mnene, au kwasababu amekuwa mzee au havutii tena..hakuna neema juu ya hilo, suluhisho pekee ni kumrudia tu!!.

Bwana anasema katika

Hesabu 30:2 “ Mtu atakapomwekea Bwana NADHIRI, au, ATAKAPOAPA KIAPO ILI KUFUNGA NAFSI YAKE KWA KIFUNGO, ASILITANGUE NENO LAKE; ATAFANYA SAWASAWA NA HAYO YOTE YAMTOKAYO KINYWANI MWAKE”.

Hii ina maana kuwa kabla ya kuamua kuoa, au kuolewa..yatafakari hayo yote kwanza na upige gharama kabisa..endapo ikitokea atakayekuja kuwa mume wako/ mke wako kafilisika utaendelea kumpenda na kuishi naye…endapo ikatokea kawa mlemavu utaendelea kumheshimu na kumpenda,..endapo mmegombana utakuwa tayari kumsamehe n.k, utakuwa tayari kumtunza kama mwili wako mwenyewe?? Kama hayo yatakushinda ni afadhali USIWEKE HIYO NADHIRI KABISA. Ni afadhali usioe wala kuolewa kabisa.

Mhubiri mmoja wa kimarekani anaitwa William Branham, wakati Fulani Alienda kumwombea mtu mmoja aliyekuwa anaumwa sana karibia na kufa…na kwasababu Bwana amemkirimia karama ya kinabii, wakati akiwa katika hatua ya kumwekea mikono Yule mgonjwa ili amwombee…Ono likamjia kutoka kwa Mungu, akamwona Yule mtu akiwa katika hali ya Kuzama maji, na wakati akiwa katika kuzama…akamlilia Mungu amwokoe asife maji, akiwa katika ile hali akamwekea Mungu nadhiri na kumwambia endapo, atamwokoa na MAUTI ILE YA KUZAMA MAJI basi atamtumikia yeye siku zote za maisha yake..na Bwana akamsikia akamwokoa na mauti ile ya kufa maji..Lakini Yule mtu alipotoka pale akaisahau ile nadhiri aliyomwekea Mungu..akaendelea na maisha yake ya kawaida…Na Bwana akamwambia katika ono ndugu William Branham kwamba huyo mtu hatapona ugonjwa uliompata bali atakufa..kwasababu alimwekea Mungu nadhiri na hakuitimiza…Na alipomwambia Yule mtu, mambo hayo Bwana aliyomwonyesha Yule akakiri ni kweli alimwekea Mungu nadhiri wakati anakaribia kuzama maji..Lakini alilolisema Bwana amelisema, baada ya siku kadhaa Yule mtu alifariki.

Ipo mifano kadha kadha katika maandiko, ambayo watu walifanya mchezo na nadhiri, Mmojawapo wa watu hao tunamwona ni Anania na Safira mkewe. Hawa wakiwa katika vyumba vyao vya siri waliahidi kuuza shamba lao na kiasi chote cha fedha kitakachopatikana basi watakipeleka madhabahuni kwa Bwana…ndivyo walivyoahidi mbele za Bwana na Bwana akasikia, akawajalia kufanikisha haja ya mioyo yao, lakini walipoona Bwana amewafanikisha na wameuza lile shamba kwa kiwango kizuri walichokitarajia tamaa ikawaingia wakasahau kuwa walimwahidi Mungu kiasi chote, lakini wao wakaficha sehemu ya fedha, na kumpelekea Mungu kiasi kidogo…Biblia inasema kwa kosa hilo hawakudanganyana wao bali walimdanganya Mungu mwenyewe na walikufa wote wawili ndani ya siku moja.

 Matendo ya Mitume 5 : 1-42

“1 Lakini mtu mmoja jina lake Anania, pamoja na Safira mkewe, aliuza mali,

2 akazuia kwa siri sehemu ya thamani yake, mkewe naye akijua haya, akaleta fungu moja akaliweka miguuni pa mitume.

3 Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja?

4 Kilipokuwa kwako, hakikuwa mali yako? Na kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani yake haikuwa katika uwezo wako? Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu.

5 Anania aliposikia maneno haya akaanguka, akafa. Hofu nyingi ikawapata watu wote walioyasikia haya.

6 Vijana wakaondoka, wakamtia katika sanda, wakamchukua nje, wakamzika.

7 Hata muda wa saa tatu baadaye mkewe akaingia, naye hana habari ya hayo yaliyotokea.

8 Petro akamjibu, Niambie, Mlikiuza kiwanja kwa thamani hiyo? Akasema, Ndiyo, kwa thamani hiyo.

9 Petro akamwambia, Imekuwaje hata mkapatana kumjaribu Roho wa Bwana? Angalia, miguu yao waliomzika mumeo ipo mlangoni, nao watakuchukua nje wewe nawe.

10 Mara akaanguka miguuni pake akafa; wale vijana wakaingia wakamkuta amekufa, wakamchukua nje, wakamzika pamoja na mumewe.

11 Hofu nyingi ikawapata kanisa lote na watu wote walioyasikia haya”.

Ndio maana Zamani katika agano la kale, Bwana aliwakataza kabisa watu waliomwekea Mungu nadhiri, wasinywe mvinyo wa aina yoyote, wala divai,wala hata mzao wa mzabibu usifike vinywani mwao, unajua ni kwasababu gani?..Ni kwasababu mtu aliyemwekea Mungu nadhiri kila wakati anapaswa awe katika akili yake timamu, ili asiisahau ile nadhiri aliyomwekea Mungu…Mvinyo unamfanya mtu ajisahau, unamfanya mtu atoke katika akili yake ya kawaida.. Na pia Bwana alitoa maagizo mtu yoyote aliyejiweka kuwa mnadhiri wa Bwana asikate nywele zake sharti ataziacha ziwe ndefu mpaka siku atakapoitimiza nadhiri yake? Unajua ni kwasababu gani?..Ni kwasababu kila atakapoziona nywele zake kichwani nyingi akumbuke kuwa alimwekea Mungu nadhiri, inakuwa ni kama kitu cha kumkumbusha kuwa ana deni sehemu Fulani katika maisha yake. Ndio maana Samsoni alionywa asikate nywele zake,wala wazazi wake wakati wa ujauzito wake alionywa asinywe divai. Kwasababu yeye alikuwa ni mnadhiri wa Bwana biblia inasema hivyo.

Hesabu 6: 1 “Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia,

2 Nena na watu wa Israeli, uwaambie, Mtu mume au mtu mke atakapoweka nadhiri kubwa, nadhiri ya Mnadhiri, ili ajiweke wakfu kwa Bwana;

3 ATAJITENGA NA DIVAI NA VILEO; hatakunywa siki ya divai, wala siki ya kileo, wala asinywe maji yo yote ya zabibu, wala asile zabibu, mbichi wala zilizokauka.

4 Siku zote za kujitenga kwake asile kitu cho chote kilichoandaliwa kwa mzabibu, tangu kokwa hata maganda.

5 Siku zote za nadhiri yake ya kujitenga, wembe usimfikilie kichwani mwake; hata hizo siku zitakapotimia, ambazo alijiweka wakfu kwa Bwana, atakuwa mtakatifu, ataziacha nywele za kichwani mwake zikue ziwe ndefu”.

Ni hatari sana kuweka nadhiri na kutoitimiza..Katika maandiko matakatifu nyakati za Waamuzi kulikuwa na mwamuzi mmoja anayeitwa YEFTHA, huyu alimwekea Mungu nadhiri kwamba endapo ataenda vitani na kushinda, basi Yule atakayetokea wa kwanza mbele yake kumpokea basi atamfanya sadaka ya kuteketezwa, lakini kwa bahati mbaya alitegemea kije kitu kingine, pengine ng’ombe zake lakini alikuja binti wake wa pekee na alikuwa hana mwingine…lakini kwasababu anajua madhara ya kuahidi nadhiri na kutoitimiliza, akamteketeza binti wake kwa moto, ili kuiondoa ile nadhiri, na Mungu hakumhesabia makosa.

Waamuzi 11: 29 “Ndipo roho ya Bwana ikamjilia juu yake Yeftha, naye akapita katika Gileadi na Manase, akapita na katika Mispa ya Gileadi, na kutoka hapo Mispa ya Gileadi akapita kuwaendea wana wa Amoni.

30 Naye Yeftha akamwekea Bwana nadhiri, akasema, Kwamba wewe utawatia wana wa Amoni mkononi mwangu kweli,

31 ndipo itakuwa ya kwamba, kile kitakachotoka katika milango ya nyumba yangu kunilaki, hapo nitakaporudi na amani kutoka kwa hao wana wa Amoni, kitu hicho kitakuwa ni cha Bwana, nami nitakisongeza kiwe sadaka ya kuteketezwa.

32 Basi Yeftha akavuka kuwaendea wana wa Amoni ili kupigana nao; naye Bwana akawaua mkononi mwake.

33 Akawapiga kutoka Aroeri hata kufikilia Minithi, miji ishirini, na mpaka Abel-keramimu, akawapiga kwa machinjo makuu mno. Basi hivyo wana wa Amoni walishindwa mbele ya wana wa Israeli.

34 Kisha Yeftha akafika Mispa nyumbani kwake, na tazama, binti yake akamtokea kumlaki, na matari na machezo; naye alikuwa ni mwanawe pekee; hakuwa na mwingine, mwana wala binti, ila yeye.

35 Ikawa alipomwona akayararua mavazi yake, akasema, Ole wangu! Mwanangu, umenitweza sana, nawe u mmoja miongoni mwahao wanisumbuao; KWA KUWA MIMI NIMEMFUNULIA BWANA KINYWA CHANGU, NAMI SIWEZI KUREJEA NYUMA”.

Kumbuka Bwana hajawahi kuagiza watu wamtolee yeye sadaka ya kuteketezwa, na yeyote afanyaye hayo alikuwa anakwenda kinyume na maagizo yake, lakini kwasababu ya NADHIRI Bwana hakumhesabia YEFTHA makosa. Na Yefha alitambua kabisa endapo asingetimiza maneno aliyoyazungumza kwa kinywa chake basi yangeweza kumtokea mambo mabaya sana..mfano wa Anania na Safira.

Ndugu unayesoma haya, ulimwahidi Mungu nini alipokuponya? Ulimwahidi Mungu nini alipokufanikisha katika mambo yako? Ulimwahidi nini siku alipokuokoa?…Ulimwekea Nadhiri gani, kama ipo je! Unaikumbuka bado? Au umeisahau? Kama wewe umeisahau kumbuka Mungu hajaisahau?..uliahidi kumtolea fungu la kumi je unafanya hivyo?..uliahidi kutoa kitu Fulani kwa ajili yake..je! ulifanya hivyo?? Uliahidi endapo akikuponya, au akikufanikisha, au akikufaulisha au akikufikisha salama utamtumikia? Je! Umefanya hivyo?..Wakati mwingine upo katika hatari nyingi na unapitia mambo magumu ni kwasababu uliweka nadhiri na haukuitoa.

Bwana akujalie kuyaona hayo!. Ili uukwepe mkono wa Mungu.

Tafadhali “share” kwa wengine na Bwana akubariki.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

MSHIKE SANA ELIMU.

HISIA YA MUNGU ILIYO MBAYA KULIKO ZOTE.

JINA LAKO NI LA NANI?

IKO NJIA IONEKANAYO KUWA SAWA MACHONI PA MTU.


Rudi Nyumbani

Print this post

MCHE MWORORO.


Kuja kwa Bwana duniani kulikuwa kwa kitofauti sana, wakati ambapo Israeli ilimtazamia aje kipindi ambacho uzao wa Daudi unaonekana wazi kwa wafalme waliokuwa wanatawala Yuda zamani za wafalme. Lakini yeye hakutokea hicho kipindi, walipotazamia labda pengine angetokea wakati ambapo wamerudishwa kutoka Babeli lakini hakuonekana hata katika hicho kipindi, wengine walizani utawala wa Umedi hautaisha hata ajapo lakini hakutokea pia ndani ya utawala ule mpaka ulipoisha, Wengine walitazamia labda ingekuwa ni katika utawala wa Uyunani, lakini hata huo nao hakutokea, mpaka ulipoanza utawala mwingine mpya uliojulikana kama Rumi ya kipagani, na ndipo akaja kuzaliwa mwokozi wa ulimwengu Bwana Yesu Kristo, Ni siku ambazo Israeli tayari imeshapoa sana, siku ambazo Israeli tayari imeathiriwa na tamaduni za kigeni za kipagani , siku ambazo Israeli imeshasahau hata kama kuna masihi mkombozi wao anayetakiwa kuja isipokuwa kwa wayahudi wachache tu ndio waliokuwa wanamtazamani, lakini taifa lote lilishalala na ndio maana hata siku ile Mamajusi kutoka mashariki walipoleta taarifa za kuzaliwa mfalme wa wayahudi, biblia inasema habari zile sio tu zilimfadhaisha Herode peke yake bali na Yerusalemu yote pia. Alishuka wakati viwango vya maovu katika Israeli na dunia nzima vipo juu, Bwana alikiita kizazi kile, kizazi cha zinaa na uzinzi , Lakini huo ndio wakati Mungu aliouchagua kumleta mwanae duniani.

Biblia inasema alikuwa kama mche mwororo kwenye nchi kavu, alikuwa kama mzizi mbichi katika nchi kame, siku ambazo watu hawakuwa na habari na Mungu, siku ambazo viongozi wa kidini walikuwa ni wapenda fedha kupindukia, kuliko kumpenda Mungu (Luka 16:14) tofauti na ilivyokuwa hapo zamani, ambapo walawi waliokuwa wanahudumu katika nyumba ya Bwana, hawakujiuhusisha na mambo ya kidunia, bali fungu lao lilitengwa kwa ajili yao, lakini wahudumu wa kipindi cha Yesu, sio tu walikuwa ni wapenda fedha, bali pia walikuwa wafanyaji wa biashara katika sehemu takatifu hekaluni mwa Mungu. alikuja kipindi ambacho unafki umejaa katikati ya viongozi wa kidini (Mathayo 23:13-15), kipindi ambacho viongozi wa kidini wamejaa kutokuwa na kiasi na dhihaka biblia inasema hivyo (Mathayyo 23:25). kipindi ambacho watu wote wenye haki na manabii pindi walipojaribu kusema ukweli walikuwa wanapigwa hadharani kwenye masinagogi yao na kuuliwa na hao hao viongozi wa kidini. Na tunaona ndivyo walivyokuja kufanya hata kwa Bwana(Mathayo 23:33).

Lakini huo ndio uliokuwa wakati wa Mungu aliouchagua kuleta wokovu duniani. Bwana Yesu Alikuwa kama jani bichi jangwani, alikuwa kama mizizi mibichi kwenye ardhi ya ukame, alikuja wakati usiostahili wa yeye kuja, kipindi ambacho Israeli haijawahi kuona nabii kwa muda wa miaka 300 kwa maana nabii wa mwisho alikuwa ni Malaki…Kipindi ambacho watu wa mataifa wanalimiliki taifa la Israeli, wakiamrishwa kana kwamba wapo nchi ya ugenini. Kipindi ambacho kila mtu anajiamulia mambo yake. Lakini ndio wakati wa Masihi kutokea, kutengeneza tena upya mambo yote.

Isaya 53: 1 “Ni nani aliyesadiki habari tuliyoileta? Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani?

2 Maana alikua mbele zake kama MCHE MWORORO, NA KAMA MZIZI KATIKA NCHI KAVU; Yeye hana umbo wala uzuri; Na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani.

3 Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu.

4 Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa.

5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, NA KWA KUPIGWA KWAKE SISI TUMEPONA“.

Maandiko yanasema ni nani aliyesadiki habari tuliyoileta?. Inaamanisha kuwa kuzaliwa kwa Kristo duniani lilikuwa ni jambo lisilosadika kwa yeyote Yule aliyelisikia, eti katikati ya ouvu atokee masihi?..afadhali ingekuwa wakati wa kipindi cha waamuzi au kipindi cha wafalme wa Israeli. Lakini sio kwa wakati ule aliokuja..

Hivyo pamoja na ukame wote huo wa kiroho uliokuwa Israeli kwa wakati ule. Hapo ndipo Kristo alipotokea, Hapo ndipo wale wenye nguvu wachache ambao hawakukata tamaa walitambuka kuja kwa Kristo, walisadiki habari za kuja kwake, Mkono wa Mungu ulifunuliwa kwao..Mfano wa hao kwenye biblia tunamwona HANA, mwanamke aliyekuwa amejitoka kikamilifu kwa Mungu, Licha ya kufiwa na mume wake katika siku za ujana wake, lakini hakuona sababu ya kwenda kuolewa tena bali alichagua kudumu hekaluni usiku na mchana akimwomba Mungu, auharakishe wokovu aliowaahidia wayahudi tangu zamani, wakati wayahudi wengine wameshakata tamaa na kuendelea na mambo yao, na kusahau kitu kinachoitwa mwokozi duniani, lakini Hana hakuwa hivyo yeye alidumu hekuluni kwa miaka 84. usiku na mchana akimtafakari Mungu na wokovu uliokuwa unatarajiwa Israeli tangu zamani. Mpaka siku moja wakati Yesu anaenda kuwekwa wakfu Hekaluni na wazazi wake ndipo Mungu akamwonyesha huyu ndiye aliyekuwa anamtazamia…

Kadhalika alikuwepo mzee mwingine naye vivyo hivyo alikuwa anatazamia faraja ya Israeli yaani kuja kwa mwokozi kwa muda mrefu, mpaka ikafikia wakati Mungu akamshuhudia kwamba hatakufa mpaka atakapomwona mwokozi duniani.

Habari hizo tunazisoma katika Luka 2:25-38

“25 Na tazama, pale Yerusalemu palikuwa na mtu, jina lake Simeoni, naye ni mtu mwenye haki, mcha Mungu, akiitarajia faraja ya Israeli; na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake.

26 Naye alikuwa ameonywa na Roho Mtakatifu ya kwamba hataona mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana.

27 Basi akaja hekaluni ameongozwa na Roho; na wale wazazi walipomleta mtoto Yesu ndani, ili wamfanyie kama ilivyokuwa desturi ya sheria,

28 yeye mwenyewe alimpokea mikononi mwake, akamshukuru Mungu, akisema,

29 Sasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako, Kwa amani, kama ulivyosema;

30 Kwa kuwa macho yangu yameuona wokovu wako,

31 Uliouweka tayari machoni pa watu wote;

32 Nuru ya kuwa mwangaza wa Mataifa, Na kuwa utukufu wa watu wako Israeli.

33 Na babaye na mamaye walikuwa wakiyastaajabia hayo yaliyonenwa juu yake.

34 Simeoni akawabariki, akamwambia Mariamu mama yake, Tazama, huyu amewekwa kwa kuanguka na kuinuka wengi walio katika Israeli, na kuwa ishara itakayonenewa.

35 Nawe mwenyewe, upanga utaingia moyoni mwako, ili yafunuliwe mawazo ya mioyo mingi.

36 Palikuwa na nabii mke, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila ya Asheri, na umri wake ulikuwa miaka mingi, alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya uanawali wake.

37 Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba.

38 Huyu alitokea saa ile ile akamshukuru Mungu, NA WOTE WALIOKUWA WAKIUTARAJIA UKOMBOZI KATIKA YERUSALEMU AKAWATOLEA HABARI ZAKE”.

Embu leo hii jaribu kufikiria ungekuwa na wewe upo katika kipindi kile je! Ungeweza kutambua kuzaliwa kwa Bwana duniani? Je! Hata ungehadhithiwa ungeweza kusadiki habari hizo?, kati ya mamilioni waliokuwa Yerusalemu ni watu wachache sana walioweza kufunuliwa tukio hilo la kuja kwa mwokozi duniani. Alikuja kama MWIVI, hakuja kwa kujionyesha onyesha, au kwa kupigwa parapanda angani ili dunia nzima itazame, bali alikuja kama mwivi. Alizaliwa zizini.

Na ndivyo itakavyokuwa kuja kwake mara ya pili. Kama ilivyokuwa katika kuja mara ya kwanza, wakati ambao watu wameshakata tamaa ya kuja Masihi duniani ndipo alipokuja na kujifunua kwa wale wachache ambao hawakuzimia mioyo yao katika kumsubiria mfano wa ANA na SIMEONI. Wakati ambao unafki mwingi na upendaji fedha umekithiri katika kanisa la Kristo na kwa watu wanaojiita watumishi wake,kama ilivyokuwa kipindi kile, ndipo Kristo atakaposhuka. Wakati ambapo manabii wengi wa uongo wamezagaa kila mahali na wale wa ukweli wanatengwa na kanisa ndipo Kristo anaposhuka 

Hivyo ndugu mambo tunayoyaona sasahivi ni dalili madhubuti inayotutambulisha kuwa tunaishi katika majira ya kuja kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Siku hiyo itakapofika siku ile ya UNYAKUO, dunia haitajua chochote, wakristo vuguvugu wanaodai wanamngojea Bwana na huku mguu mmoja upo nje, mambo ya kidunia yakiwasonga siku hiyo hawatajua chochote, bali atakuja kwa watu wachache sana, mfano wa Ana na Simeoni watu waliojazwa Roho Mtakatifu, watu ambao usiku na mchana wanautazamia wokovu na macho yao yapo mbinguni siku zote ndio watakajua, watu ambao ni wacha Mungu kama Simeoni, watu ambao wanadumu madhabahuni pa Mungu, hawataki kutoka katika mstari wa Neno ndio watakaojua lakini wengine wote watabaki wakisubiria hukumu ya Mungu mwenyezi.

Bwana atatokea kwao kama mche mwororo, kama jani bichi katika dunia chafu, katika jamii ya watu wenye dhihaka wanaosema huyo Yesu mnayengojea kwa miaka 2000 sasa yuko wapi, tulidhani angekuja wakati wa mitume hakutokea, tulidhani angekuja wakati wa kipindi cha matengenezo ya kanisa mbona hakutokea, wakati wa kipindi cha upentekoste hakutokea mpaka millennium mpya imeanza hajaja bado, huyo sio wa kuja leo wala kesho. Nyie mnapoteza mida yenu, badala ya kufikiria mambo ya muhimu mnawaza juu ya kuja kwa YESU hichi ni kizazi kipya…

Unaona? Hao watu wa kudhihaki biblia inasema watatokea katika siku za mwisho. Lakini wewe kaka/dada, unayemngojea Bwana sasa. Usikatishwe tamaa, siku ya wokovu wetu ipo karibu kushinda hata sisi tunavyodhani. Usiache kumtazama Kristo, majira haya dunia inayoona kuwa hakuna uwezekano wa kuja kwa Bwana, lakini ndio haya haya atakayokujia kama mwivi. Ndio haya Mungu aliyoyachagua. Siku yoyote hatutakuwepo hapa duniani.

Ni matumaini yangu utaufanya uteule wako na wito wako imara sasa kabla siku ile haijafika.

Amen.

Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine. Na Mungu akubariki!

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

MWAMBA WETU.

IELEWE SAUTI YA MUNGU.

ROHO ZILIZO CHINI YA MADHABAHU:

NI JAMBO LINALOMTAMANISHA SANA BWANA TUMWOMBE BILA KUKATA TAMAA?


Rudi Nyumbani

Print this post

TUKAZE MWENDO KWA TULIYOANDALIWA.

Luka 10:22 “Akasema, NIMEKABIDHIWA VYOTE NA BABA YANGU, wala hakuna amjuaye Mwana ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia.”


Yohana 13:3 “Yesu, hali akijua ya kuwa Baba amempa vyote mikononi mwake, na ya kuwa alitoka kwa Mungu naye anakwenda kwa Mungu”


Ufunuo wa Yohana 5 : 1-14 

1 Kisha nikaona katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi kitabu kilichoandikwa ndani na nyuma, kimetiwa muhuri saba. 

2 Nikaona malaika mwenye nguvu akihubiri kwa sauti kuu, N’nani astahiliye kukifungua kitabu, na kuzivunja muhuri zake? 

3 Wala hapakuwa na mtu mbinguni, wala juu ya nchi, wala chini ya nchi, aliyeweza kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama. 

4 Nami nikalia sana kwa kuwa hapakuonekana mtu astahiliye kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama. 

5 Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila ya Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na zile muhuri zake saba. 

6 Nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na wale wenye uhai wanne, na katikati ya wale wazee, Mwana-Kondoo amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote. 

7 Akaja, akakitwaa kile kitabu katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi. 

8 Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele za Mwana-Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni maombi ya watakatifu. 

9 Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa, 

10 ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi. 

11 Nikaona nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale wenye uhai, na za wale wazee, na hesabu yao ilikuwa elfu kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu, 

12 wakisema kwa sauti kuu, Astahili Mwana-Kondoo aliyechinjwa, kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na baraka.”

Shalom! Umewahi kujiuliza wafu leo wapo wapi?, je! mtu akifa leo katika dhambi au katika haki anakwenda wapi?…Ni wazi kuwa mtu akifa katika haki, roho yake inakwenda mahali panapojulikana kama Paradiso au peponi, ni mahali pa zuri na pa raha, ambapo roho ya mtu huyo itapumzishwa huko kwa kitambo kidogo pamoja na wenzake wa imani moja naye ambao nao walikufa katika haki..Huko wanakusanyika pamoja, mpaka siku Kristo atakapokuja mawinguni ambapo wataamshwa(au kufufuliwa) na kuvaa miili ya utukufu, na kisha kwenda mbinguni kwa Baba.


Kumbuka mbinguni Bwana Yesu alipo hakuna mtu aliyefika sasa, ni mahali pa zuri ambapo hapana mfano huko hata Eliya hayupo, wala Musa, wala Henoko, wala Ibrahimu, huko ni sehemu mpya kabisa ambayo jicho halijawahi kuona wala sikio kusikia mambo yaliyopo kule…Eliya na Henoko ambao hawakuonja mauti hawakupelekwa huko mbinguni Bwana aliko sasa,bali walipelekwa Paradiso.


Yohana 3: 13 WALA HAKUNA MTU ALIYEPAA MBINGUNI, ila yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, yaani, Mwana wa Adamu”.


Bwana Yesu alisema “Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo. Yohana (14:2-3)


Umeona Bwana anasema anakweda kutuandalia makao, ikiwa na maana kuwa, ni mahali kupya kabisa panapokwenda kuandaliwa…na akishamaliza atatukaribisha kwake, ili alipo nasi tuwepo.


Kwahiyo kwa muhtasari huo unaweza ukaona kwamba Kristo Yesu pekee ndiye aliyeko mbinguni sasa, akituandalia sisi makao, na Makao hayo si mengine zaidi ya nafasi zetu sisi tutakazukuwa nazo kule, pamoja na miili yetu ya utukufu tutakayoivaa siku atakayokuja kutuchukua.


Sasa unaweza ukauliza mbona kuna watu wengi wanasema wamepelekwa mbinguni wakaona hiki na kile?..Jibu rahisi ya swali hilo ni kwamba hawakupelekwa mbinguni bali walionyeshwa maono ya mbinguni..Na kumbuka maono ni lugha ya picha…Mtu anaweza akapewa maono ya mbinguni, katika maono yale akaona barabara za dhahabu, akaona na milima na mabonde mazuri, akaona na maua mazuri na chemchemi nzuri, lakini mtu huyo hajapelekwa mbinguni…bali amepewa tu maono ya mahali ambapo pangeweza pakafananishwa na Mbinguni…Ni sawa leo, mtu aoneshwe clip ya Taifa la Urusi akiwa hapa Tanzania, je! mtu huyo atakuwa amefika Urusi? Ni dhahiri kuwa bado hajafika, ni kaonyeshwa tu kipande cha video ya Urusi, Ndivyo ilivyo kwa watu wengi wanaopewa maono ya Mbinguni, wanakuwa tu wanapewa vipengele vidogo vidogo vya jinsi mbingu ilivyo uzuri wake kwa lugha ya kibinadamu. Lakini kiuhalisia kabisa ni mambo ambayo hayatamkiki kibinadamu.


mbinguni Bwana Yesu alipo hakuna mtu yoyote anayejua yanayoendelea huko..Ni siri, mpaka siku Kanisa litakaponyakuliwa ndipo watakatifu watakapoenda kuona mambo mazuri na mapya walioandaliwa. Ni mambo ambayo jicho halijawahi kuona wala sikio kusikia.


Biblia inasema..

Waebrania 11: 36 “wengine walijaribiwa kwa dhihaka na mapigo, naam, kwa mafungo, na kwa kutiwa gerezani;  

37 walipigwa kwa mawe, walikatwa kwa misumeno, walijaribiwa, waliuawa kwa upanga; walizunguka-zunguka wakivaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi; walikuwa wahitaji, wakiteswa, wakitendwa mabaya;  

38 (watu ambao ulimwengu haukustahili kuwa nao), walikuwa wakizunguka-zunguka katika nyika na katika milima na katika mapango na katika mashimo ya nchi.  

39 Na watu hao wote wakiisha kushuhudiwa kwa sababu ya imani yao, hawakuipokea ahadi;  

40 kwa kuwa Mungu alikuwa ametangulia kutuwekea sisi kitu kilicho bora, ILI WAO WASIKAMILISHWE PASIPO SISI.


Unaona hapo, watakatifu wote waliotutangulia, ukisoma Waebrania 11&12 yote utaona wingu kubwa la mashahidi linazungumziwa pale, utaona akina Ibrahimu, Henoko, Musa, Gideoni, n.k. fahamu tu wote hao mpaka sasa hawajaipokea ile ahadi walioahidiwa kwasababu yetu sisi, na ndio maana hapo biblia inasema ILI WAO WASIKAMILISHWE PASIPO SISI. Hii ikiwa na maana wingu hilo la mashahidi waaminifu wa Kristo waliojitoa maisha yao kikamilifu kwa ajili ya Bwana wote bado hawajakamilishwa wote wapo mahali wamehifadhiwa wakitusubiria sisi nasi tukamilishe ili kwa pamoja siku ile ya Bwana wote tuende mbinguni YESU wetu alipo kwenye makao aliyokwenda kutuandalia.


Ni raha iliyoje tukifahamu hilo. Hivyo mimi na wewe tukazane tufike sehemu hiyo, ambayo imeandaliwa kwa ajili yetu. Kwasababu itakuwa ni majuto makubwa sana na vilio kwa wale ambao watakosa unyakuo,.Wakati huo ukifiria wenzako wapo mbinguni wanang’aa kama jua na wewe unasubiria ziwa la moto, itakuwa ni majuto kiasi gani, kibaya zaidi ukijua kabisa ulikuwa na muda wa kutubu lakini uliupuuzia..Fanya uamuzi leo, yatengeneze maisha yako upya tena, naye Bwana atakurehemu.


Ubarikiwe sana.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Print this post