Tofauti na Ibrahimu, Isaka na Yakobo ambao chimbiko lao linaonekana katika mtiririko wake tokea Adamu mpaka Nuru hadi wao wenyewe..
Ayubu yeye ni tofauti, kwani kitabu kinaanza kwa kumweleza yeye, na mahali tu alipokuwa ambapo ni Usi.
Usi ni nchi ambayo ilikuwa nje ya Israeli, maeneo ya aidha Arabia, Syria au Yordani..lakini eneo sahihi kwa uhakika halijulikani hivyo hakuwa na chimbuko lolote la kiyahudi ndani yake.
Maandiko yanamtaja tu kama “Mtu”, wala sio nabii, au kuhani bali mtu aliyekuwa mkamilifu na mwelekezo aliyemcha Mungu na kuepukana na uovu.
Ayubu 1:1
[1]Palikuwa na mtu katika nchi ya Usi, jina lake alikuwa akiitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mwelekevu, ni mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu.
kwanini Mungu aruhusu, watu kama hawa ambao hawakuwa katika mtiririko wa kifamilia waandikwe kwenye biblia na zaidi hata wawe na sehemu kubwa katika ufalme wa Mungu…
Ni kuonyesha kuwa Mungu hana upendeleo, yeyote yule amchaye yeye hukubaliwa naye..ndicho Petro alichokiona kwa Kornelio akasema..
Matendo ya Mitume 10:34-35 [34]Petro akafumbua kinywa chake, akasema, Hakika natambua ya kuwa Mungu hana upendeleo;
[35]bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye.
Mwanamke Ruthu hakuwa myahudi, lakini Bwana alimkubali.
Hata na wewe kitendo cha kutozaliwa familia ya kikristo au kichungaji haimaanishi kuwa wewe huna neema ya kumtumikia Mungu. Hapana..ukionyesha bidii ile ile wanayoonyesha wengine Mungu hukujalizilisha neema Izidiyo haijalishi ukoo wenu wote ni wa kiganga. Kila mmoja wetu ana nafasi sawa mbele za Mungu, haijalishi kama ni myahudi au mwarabu, kama ni mzungu au mwafika wote kwa Mungu wanayo neema sawa kwasababu yeye haangalii chimbuko wala sura ya mtu.
Je unamcha Mungu?
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Print this post
Je unafahamu kuwa “Hukumu ya ibilisi” ilishapitishwa?.. Ni muhimu kulifahamu hili ili tusipumbazwe na dhambi.
Awali turejee maandiko..
Yohana 16:11 “kwa habari ya hukumu, kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa”.
Haya ni maneno aliyoyasema Bwana YESU kuhusiana na hukumu ya ibilisi kwamba imeshapita, na hana wakati tena wa kusimama mbele ya kiti cha hukumu kuhumiwa tena, tayari kashahukumiwa..
Fahamu kuwa kosa kubwa lililomfanya ibilisi kutupwa katika ziwa la moto si kumdanganya mwanadamu, wala hakuna adhabu yoyote anayojiongezea katika kumdanganya mwanadamu… kwanini?, kwasababu tayari alishahukumiwa na hiko ndicho kinachomfanya afanye kazi yake kwa bidii sana ya kudanganya watu na kuwapoteza..
Kosa kubwa ibilisi alilolifanya ni KUASI HUKO MBINGUNI, na akapimiwa kipimo cha adhabu ya juu kikubwa cha kumstahili ambacho ni ZIWA LA MOTO (yenye makali kuliko jua) yeye pamoja na malaika walioasi pamoja naye, kwa ufupi ni kwamba ziwa la moto lilikwisha kuwepo kabla hata ya mwanadamu kuumbwa, kwasababu biblia inatuambia hilo kuwa lilitengenezwa kwaajili ya shetani na malaika zake na si mwanadamu.
Mathayo 25:41 “Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, ALIOWEKEWA TAYARI IBILISI NA MALAIKA ZAKE”
Umeona?.. moto uliwekwa tayari kwa shetani na malaika zake na si wanadamu, lakini kwasababu wapo wanadamu watakaomfuata ibilisi na kumkataa Mungu, ndipo wataungana na jeshi hilo la ibilisi katika moto huo.
Kwahiyo kamwe tusijidanye kuwa ibilisi ataenda kuulizwa kwanini katupoteza, au kwanini alisababisha wewe uzini, au kwanini alishababisha ajali na watu wakafa, au kwanini aliwatesa watu duniani?..hana hukumu yoyote kwasababu ya kuudanganya ulimwengu, adhabu aliyopewa ni kuasi kule juu, na hiyo adhabu yake ni kubwa sana na ya kutosha..
Siku ile mbele ya kiti cha hukumu ni wanadamu ndio watakaosimamishwa wenyewe kuhukumiwa kwa kadiri ya matendo yao.
Ufunuo 20:11 “Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana. 12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao. 13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. 14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. 15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto”.
Ufunuo 20:11 “Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana.
12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.
13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.
14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. 15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto”.
Kwahiyo dada usimlaumu shetani kana kwamba siku ile ataulizwa kwa kukudanganya wewe, yeye hana maswali tena ya kuulizwa, yeye hana hoja tena za kujibu, yeye tayari adhabu yake imeshapitishwa, na hilo ndilo linalomfanya aendelee kufanya uharibifu kwa kasi sana, kwasababu hakuna anachoongeza wala kupunguza katika adhabu yake.
Hata akiua watu elfu kikatili, hakuna kinachoongezeka kwenye adhabu yake kwasababu amekwisha hukumiwa, ule moto ni mkuu sana ibilisi alioandaliwa.
Kwahiyo dada maisha yako ya uchafu yatafakari sana, kaka maisha yako ya uzinzi yatafakari sana, ndugu maisha yako ya uvuguvugu yatafakari sana, usikae umsingizie shetani kana kwamba shetani ataulizwa siku ile kwaajili yako, siku ile utasimama peke yako, nitasimama peke yangu, futa kale kausemi “shetani kanipitia”
Ni heri ukatubu leo na kumpa Yesu maisha yako kabla hizo siku za hatari hazijafika, kabla siku zako za kuishi hazijafika.
Neno la Mungu linasema, mkumbuke muumba wako kabla roho haijamrudia aliyeitoa (yaani Mungu,
Mhubiri 12:7 “Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, Nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa”.
Bwana atusaidie.
Mafundisho mengine:
Shetani alitoka wapi?
NIFANYE NINI NIMSHINDE SHETANI?
Nimempa Shetani watu hao, ili wafundishwe wasimtukane Mungu.
HIZO NDIZO ROHO ZA MASHETANI.
NI KWA NAMNA GANI SHETANI ANAIZUIA INJILI?
SWALI: Kwanini Anasi na Kayafa walihudumu pamoja? Je Mungu aliruhusu makuhani wakuu wawili kuhudumu kwa wakati mmoja?
Luka 3:2
[2]wakati wa ukuhani mkuu wa Anasi na Kayafa, neno la Mungu lilimfikia Yohana, mwana wa Zakaria, jangwani.
JIBU: Ni kweli kipindi cha Bwana Yesu tunaonyeshwa makuhani wawili walihudumu katika nafasi ya ukuhani mkuu. Jambo ambalo ni kinyume na agizo la Bwana kuhusu nafasi hiyo..Kwani kuhani mkuu alipaswa awe mmoja tu, mpaka atakapokufa ndio asimamishwe mwingine..Lakini kwanini ilikuwa vile.
Uhalisia ni kuwa Ukuhani ulikuwa kwanza kwa Anasi, lakini kwasababu za kisiasa ambazo zilikuwa zikisimamiwa na dola ya Warumi wakati ule.. walimteua ndugu yake ( yaaani mkwe wake) ambaye ni Kayafa asimame kwa awamu nyingine…
Ni kwanini iwe vile..
Kwa warumi nafasi za kikuhani zilikuwa ni moja ya nafasi nyeti, zenye nguvu kubwa ambazo zisipodhibitiwa walihisi uasi unaweza kutokea, na kuhatarisha ufalme, hivyo kupungumza nguvu zao hawakuwa wanawaacha makuhani wamalize muhula wao wote, mpaka kifo.kwasababu sheria ya kikuhani ilikuwa kifo ndio mwisho wa ukuhani, hivyo wenyewe waliwastaafisha makuhani…
Ndicho kilichotokea kwa Anasi, alikatizwa ukuhani wake na warumi akapewa mkwewe Kayafa. Jambo ambalo ni kosa kwa agizo la Mungu.
Yohana 18:13
[13]Wakamchukua kwa Anasi kwanza; maana alikuwa mkwewe Kayafa, yule aliyekuwa Kuhani Mkuu mwaka ule.
Japo kwa wayahudi waliendelea kumheshimu Anasi zaidi ya Kayafa kama ni kuhani sahihi kwa Bwana…lakini Kayafa pia walimpokea maana ndiye aliyekuwa anaendesha shughuli zote za kikuhani.
Ndio maana hata wakati Bwana Yesu anakamatwa, wayahudi walimpeleka kwanza kwa Anasi kabla ya Kayafa. Hiyo kuonyesha walimtambua Anasa hata baada ya kuondolewa ukuhani
Hivyo wote waliheshimika ndio maana wanatajwa kama makuhani.
Ni nini tunafunzwa katika habari zao?
Mkanganyiko.
Si ajabu kwanini nyakati zile mifumo ya kidini haikuweza kumtambua Kristo ijapokuwa alijidhihirisha kwao kwa namna zote..
Wayahudi walivunjika vunjia kwanza kiiamani licha ya kuwepo makuhani wawili…walikuwepo pia mafarisayo na waandishi.. na madhehebu mengine kadha wa kadha.
Mfano tu wasasa uwepo wa madhehebu mengi..ikidhaniwa kuwa Mungu yupo huko.
Leo hii kila mtu ana lake..Lakini je Kristo ni hayo?
Embu tuwazie kwa wakati ule…
Kuhani mkuu halisi (Yesu Kristo), alikuwa akizunguka huku na huko akiwahubiria maskini wa roho habari njema, akiwafanya huru waliosetwa na shetani, akiwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao (Luka 4), sio kuunda dini, au dhehebu au taasisi, fulani, Sio mashindano, n.k.
Sio kwamba taasisi Haziifai, zinafaa sana lakini je, Kazi za msingi za Kristo zinapewa kipaumbele?
Makuhani wakuu wa tatu waliokuwepo.. Kati ya hao Kristo ndiye aliyekubaliwa, hivyo mfuate yeye.
Amen
Jina la Bwana YESU libarikiwe.
Mungu huwa anasema nasi mara nyingi mioyoni mwetu, lakini huwa hatuzingatii na mwisho wake tunaingia katika matatizo.
Matokeo ya kutozingatia sauti ya Mungu ni makubwa, hebu tujifunze kwa mwana mpotevu, aliyeomba urithi kwa Baba yake.
Luka 15:11 “Akasema, Mtu mmoja alikuwa na wana wawili; 12 yule mdogo akamwambia babaye, Baba, nipe sehemu ya mali inayoniangukia. Akawagawia vitu vyake. 13 Hata baada ya siku si nyingi, yule mdogo akakusanya vyote, akasafiri kwenda nchi ya mbali; akatapanya mali zake huko kwa maisha ya uasherati”. 14 Alipokuwa amekwisha tumia vyote, njaa kuu iliingia nchi ile, yeye naye akaanza kuhitaji. 15 Akaenda akashikamana na mwenyeji mmoja wa nchi ile; naye alimpeleka shambani kwake kulisha nguruwe. 16 Akawa akitamani kujishibisha kwa maganda waliyokula nguruwe, wala hapana mtu aliyempa kitu. 17 ALIPOZINGATIA MOYONI MWAKE, alisema, Ni watumishi wangapi wa baba yangu wanaokula chakula na kusaza, na mimi hapa ninakufa kwa njaa. 18 Nitaondoka, nitakwenda kwa baba yangu na kumwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako”
Luka 15:11 “Akasema, Mtu mmoja alikuwa na wana wawili;
12 yule mdogo akamwambia babaye, Baba, nipe sehemu ya mali inayoniangukia. Akawagawia vitu vyake.
13 Hata baada ya siku si nyingi, yule mdogo akakusanya vyote, akasafiri kwenda nchi ya mbali; akatapanya mali zake huko kwa maisha ya uasherati”.
14 Alipokuwa amekwisha tumia vyote, njaa kuu iliingia nchi ile, yeye naye akaanza kuhitaji.
15 Akaenda akashikamana na mwenyeji mmoja wa nchi ile; naye alimpeleka shambani kwake kulisha nguruwe.
16 Akawa akitamani kujishibisha kwa maganda waliyokula nguruwe, wala hapana mtu aliyempa kitu.
17 ALIPOZINGATIA MOYONI MWAKE, alisema, Ni watumishi wangapi wa baba yangu wanaokula chakula na kusaza, na mimi hapa ninakufa kwa njaa.
18 Nitaondoka, nitakwenda kwa baba yangu na kumwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako”
Nataka tuone huo mstari wa 17, unaosema.. “ALIPOZINGATIA MOYONI MWAKE”.
Maana yake tayari sauti ya MUNGU ilikuwa imeshaanza kumsemesha muda mrefu sana moyoni mwake, kwamba njia anayoiendea sio sahihi, mambo anayoyafanya ni mabaya na hivyo ageuke, lakini hakuwa ANAZINGATIA hiyo sauti.
Na kwa kadiri alivyokuwa anaipuuzia ndivyo mambo yalivyozidi kuwa mabaya, mpaka siku alipoamua kuizingatia.
Inawezekana sauti ya MUNGU inasema nawe moyoni mwako muda mrefu (dhamiri inakushuhudia), usiiendee hiyo njia, usiendelee kufanya hayo unayoyafanya, lakini huzingatii, leo anza kuzingatia sauti ya MUNGU, na geuka acha hiyo njia, mrudie Baba yako, mpe Mungu moyo wako…
Mithali 23:26 “Mwanangu, nipe moyo wako; Macho yako yapendezwe na njia zangu”.
Zingatia sauti inayokuambia UOMBE, zingatia sauti inayokuambia ufunge, Zingatia sauti inayokuambia usome Neno, zingatia sauti inayokuambia Usamehe, zingatia sauti inayokuambia mtumikie MUNGU, wakati mwingine zingatia hata sauti unayokuambia uhame hapo ulipo…
Matokeo ya kuikaidi hiyo sauti ni mabaya, ni kama hayo ya Mwana mpotevu na yale ya Yona.
Shalom.. Karibu tujifunze Biblia pamoja.
Zipo nyakati Ngumu ambazo kama mkristo utazipitia, ni nyakati za dhiki, na vilio wakati mwingine…na nyakati hizo haimaanishi kuwa Mungu kakuacha, hapana!, ni iko namna hiyo tu.… maana maandiko yanasema tumewekewa hizo, ingawa ni za kitambo tu.
1Wathesalonike 3:3 “mtu asifadhaishwe na dhiki hizi; maana ninyi wenyewe mnajua ya kuwa twawekewa hizo. 4 Kwa kuwa tulipokuwapo kwenu tulitangulia kuwaambia kwamba tutapata dhiki, kama ilivyotukia, nanyi mwajua”.
1Wathesalonike 3:3 “mtu asifadhaishwe na dhiki hizi; maana ninyi wenyewe mnajua ya kuwa twawekewa hizo.
4 Kwa kuwa tulipokuwapo kwenu tulitangulia kuwaambia kwamba tutapata dhiki, kama ilivyotukia, nanyi mwajua”.
Sasa inapotokea umekutana na dhiki, au majaribu na huku ukijitazama upo sawa kiimani, na wala hujarudi nyuma, ni nini cha kufanya?
Jambo ni moja tu, nalo ni kusimama na kuendelea mbele na si kuendelea kulia (USIKATE TAMAA)…… Machozi yapo kweli, lakini hayawezi kukusaidia sana wakati wa majaribu, bali ujasiri na kusimama ndio kuendelea mbele ndio Nguvu ya kuvuka huo wakati.
Tujifunze kwa habari ya Daudi kabla hajawa mfalme. Maandiko yatuambia, kuna siku alirudi mjini mwake akakuta mji umevamiwa na Waamaleki na wake zake wamechukuliwa mateka pamoja na mali zao, ilikuwa ni kilio kikubwa cha uchungu mkubwa, na Daudi pamoja na wenzake walilia sana..
1Wafalme 30:1 “Ikawa, Daudi na watu wake walipokuwa wamefika Siklagi siku ya tatu, hao Waamaleki walikuwa wameshambulia Negebu, na Siklagi, nao wameupiga Siklagi, na kuuchoma moto; 2 NAO WAMEWACHUKUA MATEKA WANAWAKE WALIOKUWAMO WAKUBWA KWA WADOGO; HAWAKUWAUA WO WOTE, ILA WAKAWACHUKUA, WAKAENDA ZAO. 3 Basi Daudi na watu wake walipoufikilia mji, tazama, ulikuwa umechomwa moto; na wake zao, na watoto wao, waume kwa wake, wamechukuliwa mateka. 4 Ndipo Daudi na watu waliokuwa pamoja naye WAKAINUA SAUTI ZAO NA KULIA, HATA WALIPOKUWA HAWANA NGUVU ZA KULIA TENA 5 Na hao wake wawili wa Daudi walikuwa wamechukuliwa mateka, Ahinoamu wa Yezreeli, na Abigaili, aliyekuwa mkewe Nabali, wa Karmeli ”. Sasa baada ya Daudi na wenzake kulia mpaka machozi yalipoisha ni kitu gani kilitokea….tuendelee… 6 Naye Daudi akafadhaika sana; kwa sababu watu walikuwa wakisema kwamba apigwe kwa mawe, kwa maana nafsi za hao watu wote walisononeka, kila mtu kwa ajili ya wanawe na binti zake; lakini Daudi ALIJITIA NGUVU KATIKA BWANA, MUNGU WAKE. 7 Kisha Daudi akamwambia Abiathari, kuhani, mwana wa Ahimeleki, Tafadhali niletee hapa hiyo naivera. Naye Abiathari akamletea Daudi naivera huko. 8 Daudi akauliza kwa Bwana, akasema, Je! Nikiwafuata jeshi hili, nitawapata? Naye akamjibu, Fuata; kwa kuwa hakika utawapata, nawe hukosi utawapokonya wote…………….. 16 Na hapo alipokuwa amewaongoza chini, tazama, hao walikuwa wametawanyika juu ya nchi yote, wakila na kunywa, na kufanya karamu, kwa sababu ya hizo nyara kubwa walizochukua katika nchi ya Wafilisti, na katika nchi ya Yuda. 17 Naye Daudi akawapiga tangu ukungu wa jioni hata jioni ya siku ya pili; hakuna aliyeokoka, ila vijana mia nne waliopanda ngamia na kukimbia. 18 DAUDI AKAWAPOKONYA WOTE WALIOKUWA WAMECHUKULIWA NA WAAMALEKI; NAYE DAUDI AKAWAOKOA WAKEZE WAWILI. 19 Wala hawakupotewa na kitu, mdogo wala mkubwa, wana wala binti, nyara wala cho chote walichojitwalia hao; Daudi akavirudisha vyote”.
1Wafalme 30:1 “Ikawa, Daudi na watu wake walipokuwa wamefika Siklagi siku ya tatu, hao Waamaleki walikuwa wameshambulia Negebu, na Siklagi, nao wameupiga Siklagi, na kuuchoma moto;
2 NAO WAMEWACHUKUA MATEKA WANAWAKE WALIOKUWAMO WAKUBWA KWA WADOGO; HAWAKUWAUA WO WOTE, ILA WAKAWACHUKUA, WAKAENDA ZAO.
3 Basi Daudi na watu wake walipoufikilia mji, tazama, ulikuwa umechomwa moto; na wake zao, na watoto wao, waume kwa wake, wamechukuliwa mateka.
4 Ndipo Daudi na watu waliokuwa pamoja naye WAKAINUA SAUTI ZAO NA KULIA, HATA WALIPOKUWA HAWANA NGUVU ZA KULIA TENA
5 Na hao wake wawili wa Daudi walikuwa wamechukuliwa mateka, Ahinoamu wa Yezreeli, na Abigaili, aliyekuwa mkewe Nabali, wa Karmeli ”.
Sasa baada ya Daudi na wenzake kulia mpaka machozi yalipoisha ni kitu gani kilitokea….tuendelee…
6 Naye Daudi akafadhaika sana; kwa sababu watu walikuwa wakisema kwamba apigwe kwa mawe, kwa maana nafsi za hao watu wote walisononeka, kila mtu kwa ajili ya wanawe na binti zake; lakini Daudi ALIJITIA NGUVU KATIKA BWANA, MUNGU WAKE.
7 Kisha Daudi akamwambia Abiathari, kuhani, mwana wa Ahimeleki, Tafadhali niletee hapa hiyo naivera. Naye Abiathari akamletea Daudi naivera huko.
8 Daudi akauliza kwa Bwana, akasema, Je! Nikiwafuata jeshi hili, nitawapata? Naye akamjibu, Fuata; kwa kuwa hakika utawapata, nawe hukosi utawapokonya wote……………..
16 Na hapo alipokuwa amewaongoza chini, tazama, hao walikuwa wametawanyika juu ya nchi yote, wakila na kunywa, na kufanya karamu, kwa sababu ya hizo nyara kubwa walizochukua katika nchi ya Wafilisti, na katika nchi ya Yuda.
17 Naye Daudi akawapiga tangu ukungu wa jioni hata jioni ya siku ya pili; hakuna aliyeokoka, ila vijana mia nne waliopanda ngamia na kukimbia.
18 DAUDI AKAWAPOKONYA WOTE WALIOKUWA WAMECHUKULIWA NA WAAMALEKI; NAYE DAUDI AKAWAOKOA WAKEZE WAWILI.
19 Wala hawakupotewa na kitu, mdogo wala mkubwa, wana wala binti, nyara wala cho chote walichojitwalia hao; Daudi akavirudisha vyote”.
Unapofika wakati umeishiwa nguvu, huo ndio wakati wa KUJITIA NGUVU!.. kwasababu maandiko yanatufundisha kuwa “tulipo dhaifu, ndipo tulipo na nguvu (2Wakorintho 12:10)”
Laiti Daudi angeendelea kulia pale bila kuchukua hatua yoyote, wale watu wangempiga mawe, au hata wasingempiga kwa mawe, bado asingewapata wake zake na mali zake, lakini ALIPOJITIA NGUVU KWA BWANA ndipo nguvu ikaongezeka kwake na Bwana akamsaidia.
Ukipitia majaribu ya afya jitie nguvu endelea mbele na maombi, pia ishi kwa ujasiri kana kwamba huumwi, na utaona maajabu makuwa….
Ukipitia majaribu ya familia jitie nguvu kwa Bwana endelea na maombi na kutafuta masuluhisho Bwana atakuwa nawe,
Ukipitia majaribu ya watoto au ndoa jitie nguvu kwa Bwana,
Ukipitia majaribu ya huduma jitie nguvu kwa Bwana songe mbele,
Ukipitia majaribu ya kipato vile vile jitie nguvu kwa Bwana songe mbele, zidi kumwomba Bwana wala usikate tamaa, njia itaonekana tu na milango itafunguka, haijalishi umeshapita muda gani… na magumu mengine yote fahamu kuwa ni ya kitambo, lakini ujasiri wako kwa Bwana unahusika sana huo wakati.
JIPE MOYO MKUU.
USIKATE TAMAA UNAPOPITIA MAGONJWA.
NI JAMBO GANI LINALOMTAMANISHA SANA BWANA TUMWOMBE BILA KUKATA TAMAA?
Kwanini kuna mrudio wa uumbaji kwenye Mwanzo sura ya pili?
LAKINI NINYI, NDUGU, MSIKATE TAMAA KATIKA KUTENDA MEMA.
Jibu: Turejee…
2Wakorintho 6:15 “Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na BELIARI? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini?”
Neno Beliari ni muunganiko wa maneno mawili ya kiebrania, ambayo ni “Beliy-ya’al” lenye maana ya “Asiyefaa kitu” na Neno lingine la “Baradhuli”
Sasa hapo kwenye 2Wakorintho 6:15 inaweza kusoma hivi kwa Kiswahili kirahisi… “Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na mtu asiye na maana? ”
Kibiblia mtu asiyefaa kitu ni mtu asije mcha Mungu, asiye na hofu ya Mungu, mwenye roho ya ibilisi ndani yake, kwaufupi ni Baradhuli, mfano wa Beliari/baradhuli ni wale tunaowasoma katika 2Nyakati 13:7..
2Nyakati 13:7 “Wakamkusanyikia watu mabaradhuli, WASIOFAA KITU, waliojitia nguvu juu ya Rehoboamu mwana wa Sulemani, Rehoboamu alipokuwa kijana na wa moyo mwororo, asiweze kuwazuia”.
Waamuzi 19:22 “Hapo walipokuwa wakifurahisha mioyo yao, tazama, watu wa mji huo, watu mabaradhuli wakaizingira hiyo nyumba pande zote, wakagonga mlango; wakasema na huyo mwenye nyumba, huyo mzee, na kumwambia, Mlete nje mtu yule aliyefika nyumbani kwako, ili tupate kumjua”.
Soma pia Kumbukumbu 13:13, Waamuzi 11:3, Waamuzi 20:13, 2Samweli 6:20 na Ayubu 11:11.
Na kama maandiko yanavyosema hakuna mapatano au ulinganifu kati ya Kristo na Beliari, maana yake Kristo hawezi kuchanganywa na uchafu, wala hawazi kutembea na Mabeliari au Mabaradhuli, hivyo hatuna budi kujitakasa na uchafu wote wa mwilini na rohoni, ili tutembee na Kristo.
2Wakorintho 7:1 “Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu”.
Baradhuli/Mabaradhuli ni nini au ni nani kwenye biblia?
WATU WASIOJIZUIA.
HII NDIO TABIA YA WATU WA KEILA, USIIGE
Watu wenye kuvunja maagano ndio watu wa namna gani? (Warumi 1:31)
Kwanini Herode aliwakasirikia watu wa Tiro na Sidoni? (Matendo 12:20)
Jibu: Tusome..
Warumi 12:11 “kwa BIDII, si walegevu; mkiwa na JUHUDI katika roho zenu; mkimtumikia Bwana”
“Bidii” ni hamasa/msukumo wa ndani wa kufanya jambo fulani… na mtu anaweza kuwa na bidii lakini asiwe na juhudi.
Kwamfano mtu anaweza kwa na bidii kubwa katika kupanga mambo, lakini katika utekelezaji akashindwa.
Lakini “Juhudi” yenyewe inakwenda mbali zaidi katika utekelezaji kwa vitendo, kwamfano mtu anaweza kuwa na bidii ya kuweka mikakati ya kilimo na mipango, na baadaye akafanya juhudi katika kilimo kwa kuingia shambani na kulima.
Mtu anaweza kuwa na bidii ya kununua vitabu vingi vya imani vya kumsaidia kukua kiroho na akaonyesha “juhudi” ya kuvisoma vile vitabu na akazalisha kitu katika maisha yake ya kiroho… au mtu anaweza kuwa na bidii nyingi kujua mafundisho ya upendo, imani, maombi au wokovu lakini kama hatakuwa na “juhudi” ya kuishi au kukitenda kile anachojifunza au kikosoma “bidii” yake ni bure..
Biblia inatufundisha kuwa na bidii na juhudi pia katika mambo yote..
Usiwe na bidii na kukosa Juhudi kwani Juhudi ni ngazi ya msingi sana kufikia lengo la kiroho..
Tito 2:14 “ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale WALIO NA JUHUDI KATIKA MATENDO MEMA”.
Kwahiyo sio tu BIDII katika kusoma, bali pia na JUHUDI katika kutenda, ndivyo Biblia inavyotufundisha..
1Petro 3:13 “Naye ni nani atakayewadhuru, mkiwa wenye juhudi katika mema?”
1Petro 4:8 “Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi”.
Ipi tofauti ya Kukemea na kukaripia? (2Timotheo 4:2)
Ipi Tofauti ya Agano jipya na Agano la Kale?.
Ipi tofauti ya utakatifu na utukufu?
Ipi tofauti ya Falme, Mamlaka na Wakuu wa giza (Waefeso 6:12)
Ipi tofauti ya Hasira na Ghadhabu ya MUNGU?.
SWALI: Ayubu alipopata yale majaribu, alimwambia mkewe;
Je! Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya? Swali ni je! Mambo mabaya yanatoka pia kwa Mungu?
JIBU:
Ayubu 2:10
[10]Lakini yeye akamwambia, Wewe wanena kama mmoja wa hao wanawake wapumbavu anenavyo. Je! Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya? Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi kwa midomo yake.
Ukweli ni kwamba Mungu hatoi mabaya, bali sikuzote hutoa mema…mabaya huwa yanatoka kwa adui..
Isipokuwa katika kuyapokea mema ya Mungu, yapo mapito ambayo (mbele ya macho yetu), tunayaona kuwa ni mabaya lakini kiuhalisia ni njia tu ya kufikia Mema yetu Mungu aliyotuandalia..wala hakuna lolote linaloharibika..
Angalia mwisho wa Ayubu…kumbe Mungu alitaka kumpatia mara dufu, ya vile alivyokuwa navyo hapo mwanzo, na ndio maana ilinpasa vile vya mwanzo viondoke…
Tengeneza picha miaka mingi baadaye labda tuseme miaka 30 baada ya lile pito, akiwa na watoto wake wapya ambao ni mashuhuri wenye hadhi na nguvu za Mungu..Tena Akiwa Mwenye utajiri mwingi na heshima kuliko mwanzoni..bila shaka huwenda alipokumbuka zile nyakati ambazo alikuwa analia na kusema “ilaaniwe siku ile niliyozaliwa” alikuwa anacheka na kusema Mungu Nisamehe nilikuwa sijui nitendalo!
Yakobo 5:11
[11]Angalieni, twawaita heri wao waliosubiri. Mmesikia habari ya subira yake Ayubu, mmeuona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwingi wa rehema, mwenye huruma.
Mungu hutujenga katika nyakati zote nyakati za furaha lakini pia nyakati za mateso.Ukishalitambua hili kama mwana wa Mungu hutasumbuliwa na tufani..Bali utamtukuza Mungu katika mazingira yote,, ukijua kuwa kusudi la Mungu linatimia katika mazingira yote…Wala hakuna lolote linalo haribika..
Nyakati tuzionazo mbaya huleta baraka..majeshi ya washami yalipowazunguka Israeli, mwisho wake ulikuwa ni kuziachilia nafaka na mali kwao, Samsoni alipokutana na Simba, kumbe ni asali aliletewa..mwanamke apatapo na utungu hawezi kusema ni mabaya anapitia, kwasababu anajua kuwa hiyo ni njia tu ya kupata kiumbe kipya duniani.
Vitu kama Saburi, unyenyekevu, upole Mungu anavijenga ndani ya watoto wake katika nyakati kama hizi (ambazo sisi tunaziita ni mbaya)…
Hivyo jifunze kuliona kusudi la Mungu katika nyakati zako zote.
Kwa hitimishi ni kuwa Ayubu aliposema ‘Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya?’
Alimaanisha nyakati za huzuni..ambazo zinatimiza kusudi la Mungu….lakini sio mabaya mfano wa mabalaa na vifo, ambayo mwisho wake ni uharibifu. Mungu kamwe haleti uharibifu kwa mtoto wake, hawezi kutupatia samaki na wakati huo huo kutupatia nyoka.
Kitabu hicho hakijafunua jina la mwandishi wake moja kwa moja kama baadhi ya vitabu vingine vinavyofunua..Hivyo kwa kuwa hakina uthibitisho wowote wa jina la mwandishi, miongoni mwa wayahudi na wakristo wengi, kumekuwa Na mitazamo tofauti tofauti juu ya muhusika wa uandishi ule.
Baadhi husema ni mordakai, wengine husema ni Ezra, wengine Nehemia na wengine myahudi fulani ambaye alikuwa na uelewa mzuri wa kihistoria katika dola uajemi wakati ule.
Lakini uzito mkubwa umewekwa kwa Mordekai, kutokana na habari zake kuchukua sehemu kubwa katika kitabu hichi.
Lakini pia maneno Yake mwenyewe kunukuliwa katika kitabu hichi; kuonyesha kuwa yamkini ni yeye ndiye mwandishi wa kitabu hichi.
Esta 9:20-21
[20]Basi Mordekai aliyaandika mambo hayo; naye akapeleka barua kwa Wayahudi wote waliokaa katika majimbo yote ya mfalme Ahasuero, waliokuwa karibu na waliokuwa mbali, [21]kuwaonya wazishike siku ya kumi na nne ya mwezi wa Adari, na siku ya kumi na tano yake, mwaka kwa mwaka,
[20]Basi Mordekai aliyaandika mambo hayo; naye akapeleka barua kwa Wayahudi wote waliokaa katika majimbo yote ya mfalme Ahasuero, waliokuwa karibu na waliokuwa mbali,
[21]kuwaonya wazishike siku ya kumi na nne ya mwezi wa Adari, na siku ya kumi na tano yake, mwaka kwa mwaka,
Lakini pia upatikanaji wa taarifa za ndani ya kwenye jumba la kifalme, mfano karamu za kifalme, hukumu zao, sasa taarifa kama hizi ni wazi kuwa hujulikana na watu walio karibu na ikulu za kifalme, mfano wa Mordakai ambaye alikuwa mfungua malango (Esta 2:19,21)
Lakini pia Kuhifadhiwa Kwa kumbukumbu ya sikukuu ya Purimu (Esta 9: 29-32).
Kwani kitabu kinaonyesha kuwa yeye ndiye aliyesambaza habari…hivyo ni sawa kufikiri pia habari hizo angetaka zihifadhiwe Hata katika vizazi vijavyo vya mbeleni, ambazo ndio hizi mpaka sasa tunazisoma.
Esta 9:29-31
[29]Ndipo malkia Esta, binti Abihaili, pamoja na Mordekai Myahudi, alipoandika kwa mamlaka yote kuithibitisha barua hii ya pili ya Purimu. [30]Akapeleka barua kwa Wayahudi wote katika majimbo yote mia na ishirini na saba ya ufalme wake Ahasuero, maneno ya amani na kweli, [31]ili kuzithibitisha siku hizo za Purimu kwa majira yake, kama Mordekai Myahudi na malkia Esta walivyoamuru, na kama walivyojiagizia juu yao wenyewe, na juu ya wazao wao, kwa habari ya kufunga na kilio.
[29]Ndipo malkia Esta, binti Abihaili, pamoja na Mordekai Myahudi, alipoandika kwa mamlaka yote kuithibitisha barua hii ya pili ya Purimu.
[30]Akapeleka barua kwa Wayahudi wote katika majimbo yote mia na ishirini na saba ya ufalme wake Ahasuero, maneno ya amani na kweli,
[31]ili kuzithibitisha siku hizo za Purimu kwa majira yake, kama Mordekai Myahudi na malkia Esta walivyoamuru, na kama walivyojiagizia juu yao wenyewe, na juu ya wazao wao, kwa habari ya kufunga na kilio.
Kwa hitimishi ni kubwa…awe ni Mordekai au mwingine yoyote, Lililo la msingi ni kufahamu agizo la Kristo lililo nyuma ya kitabu hichi.
Hivyo kwa msaada wa uchambuzi wa mafundisho kadha wa kadha yaliyo katika kitabu hichi..basi fungua hapa uweze kujifunza.. >>>
ESTA: Mlango wa 1 & 2
Mabibi wastahiki walikuwa ni watu gani? (Esta 1:18).
Sikukuu ya kutabaruku ni ipi?
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >>https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Zaburi 29:3
[3]Sauti ya BWANA i juu ya maji; Mungu wa utukufu alipiga radi; BWANA yu juu ya maji mengi.
Ulishawahi kujiuliza kwanini ulimwengu ufunikwe kwanza na maji kote, ndipo Mungu atue juu yake lakini pia aseme Neno?(Mwanzo 1:1-2)
Vipi kama maji yasingekuwepo je Mungu asingesema lolote?….ndio ni kweli Neno la Bwana linasimama mahali popote lakini amejiwekea utaratibu wake wa kuzungumza..si kila eneo sauti yake yenye mamlaka ataiachia..
Palipo na maji sauti yake hutokea…
Ndio maana baadaye mwandishi wa zaburi Kwa uvivio wa Roho anasema…
Sasa ni lazima tufahamu kwamba Mungu hakai kwenye maziwa, au bahari au mito…hapana bali Mungu hukaa katika moyo wa Mtu..
Lakini moyo wenye maji mengi… na hapo ndipo Sauti yake yenye nguvu kama radi inaposikika…
Hata mawingi ili yatoe radi huhitaji yajawe kwanza na maji, bila hivyo kamwe huwezi sikia sauti yoyote nyuma yake
Biblia inasema…
Yohana 4:13-14
[13]Yesu akajibu, akamwambia, Kila anywaye maji haya ataona kiu tena; [14]walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele.
[13]Yesu akajibu, akamwambia, Kila anywaye maji haya ataona kiu tena;
[14]walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele.
Na mahali pengine anasema maji hayo ni Roho Mtakatifu. (Yohana 7:39)
Mtu yeyote anayempa nafasi Roho Mtakatifu, ndani yake, kwa kutii, kwa kuwa mwombaji, mwenye ibada nyingi kumtafuta Mungu, kujitenga na dhambi …Huyo Anaongeza wingi wa maji ndani yake na matokeo yake ni kuwa sauti ya Mungu inasikika, na sio tu kisikika lakini pia inakuwa na nguvu kama ngurumo.
Tukiwa wakame, au tuna maji machache, kinyume chake, ni kuwa hatuwezi kumwona Mungu, wala kuisikia sauti yake. Penda kumtii Roho Mtakatifu. Tafuta kwa bidii kumjua Mungu, ongeza maji yako, Bwana aseme.