Ukikatazwa na Mungu, haimaanishi kuwa umenyimwa unachoomba, kinyume chake amepewa kwa uzuri wa juu zaidi.
Kuna kipindi Daudi aliingiwa na Nia ya kutaka kumjengea Mungu nyumba ..Hivyo akaanda Mali zake nyingi ili aanze ujenzi…lakini alipolileta Hilo wazo kwa Mungu, ilikuwa ni tofauti na alivyotarajia..
Mungu hakumruhusu bali kinyume chake akamwambia wewe hutanijengea mimi nyumba…kwasababu umemwaga damu ya watu wengi, lakini mwanao ndiye atakayenijengea…
1 Mambo ya Nyakati 22:7-8
[7]Daudi akamwambia Sulemani mwanawe, Kwangu mimi nia yangu ilikuwa kujenga nyumba kwa ajili ya jina la BWANA, Mungu wangu. [8]Lakini neno la BWANA likanijia, kusema, Wewe umemwaga damu nyingi, na vita vikubwa umevifanya; wewe hutajenga nyumba kwa ajili ya jina langu, kwa sababu umemwaga damu nyingi juu ya nchi machoni pangu;
[7]Daudi akamwambia Sulemani mwanawe, Kwangu mimi nia yangu ilikuwa kujenga nyumba kwa ajili ya jina la BWANA, Mungu wangu.
[8]Lakini neno la BWANA likanijia, kusema, Wewe umemwaga damu nyingi, na vita vikubwa umevifanya; wewe hutajenga nyumba kwa ajili ya jina langu, kwa sababu umemwaga damu nyingi juu ya nchi machoni pangu;
Jiweke katika hiyo hali unatamani ufanye kitu fulani chema, lakini Mungu anakuambia (aidha kwa maneno au vitendo) hapana wewe hustahili kufanya au kuchukua nafasi hiyo, kwasababu hii na hii na hii, bali ataichukua kijakazi wako, mtumwa wako, rafiki yako, mpendwa mwenzako…Sasa Kibinadamu hilo linaweza likaleta ukakasi lisikuvutie Masikioni mwako…kwasababu unajua litampa cheo mwenzako.
Pengine ndivyo angeweza kufikiri Daudi… Lakini alijifunza kunyenyekea, na kumtii Mungu na kuachilia kijiti kwa mwingine…
matokeo yake ikawa ujenzi ule ukadumishwa na jina lililodumishwa halikuwa lingine bali la Daudi kwa vizazi vyote vijavyo..aliyejenga alikuwa ni Sulemani, lakini utukufu ulikuja kwa jina la Daudi mpaka leo linatajwa.
Hii ni kutufundisha kukubali kunyenyekea Katika mapenzi yote ya Mungu..Zipo nyakati hutafanya wewe, hata kama umeomba na kuitamani hiyo nafasi yakupasa ukubali wengine wafanye, upo wakati hutatukuzwa wewe kubali wengine watukuzwe kupitia wewe, hutaheshimiwa wewe lakini fanya bidii wengine waheshimiwe kupitia wewe…kwasababu hiyo ndio ngazi ya kuinuliwa na Mungu, na matokeo yake utayaona..
Makatazo ya Mungu ni fursa ya mafanikio, unaweza ukawa hujapewa uzao, lakini ukamlea mtoto wa mwingine, Mungu akaja kumfanya raisi wa nchi, ukaitwa mama wa Taifa. Hivyo maadamu unatembea katika njia za Bwana na umeomba, amini kuwa Mungu amekupa zaidi ya kile ukiwazacho.
Kamwe Using’ang’anie jambo, bali jifunze kuachilia neema ya Mungu yenyewe kuamua, kwasababu hutapoteza chochote..
Waefeso 3:20
[20]Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu;
Bwana awe nawe…
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Print this post
SWALI: Kwanini Bwana Yesu alipowatuma wanafunzi wake kuhubiri aliwaambia wasihame- hame nyumba watakazo Karibishwa?
Luka 10:7
[7]Basi, kaeni katika nyumba iyo hiyo, mkila na kunywa vya kwao; maana, mtenda kazi amestahili kupewa ujira wake. Msihame-hame kutoka nyumba hii kwenda nyumba hii.
JIBU: Luka 10, Mathayo 10, Na Marko 6, Kristo inawafundisha mitume wakee nidhamu ya kimisheni. Pale ambapo watu wa Mungu watatoka na kwenda kuhubiri injili kwenye miji, mataifa au nyumba za Watu.
Ukisoma pale utaona Kristo anawapa maagizo kadha wa kadha mfano amri ya kutoa huduma zao bure, anawaagiza wawe wapole kama Hua, na wenye busara kama nyoka, vilevile nyumba watakazokaribishwa kisha chakula kikawekwa mbele yao wale bila kuuliza- uliza…
Lakini agizo lingine lilikuwa ni kutohama-hama nyumba moja kwenda nyingine. Kwamfano wameingia mji fulani halafu ikatokea familia moja ikawaalika kukaa kwao kwa kipindi chote cha huduma, hawapaswi kuhama- hama bali wakae pale mpaka watakapotoka na kwenda mji mwingine ikiwa yule mfadhili hana neno nao. Hata kama wakialikwa nyumba nyingine hawapaswi kuhama- hama..
Swali linakuja kwanini iwe hivyo?
Bwana Yesu alijua kuwa katika ziara mialiko kwa watumishi wa Mungu, huwa ni mingi. Na hivyo ili kuzuia dhamiri mbaya na wengine kuvunjika mioyo, akatoa agizo hilo Kwasababu mfano imetokea mtumishi amealikwa kisha kesho yake akahamia nyumba nyumba nyingine, Yule wa kwanza atajisikiaje? Pengine picha itakayoonekana hapo ni kuwa wanatafuta maisha mazuri, au matajiri wenye hadhi ya kuwatunza..
Lakini wakitulia sehemu moja huleta adabu na kuonyesha tabia ya kuridhika.
Lakini pia Kristo alitaka akili zao zijikite zaidi kwenye huduma.. Kwani kitendo cha kila siku kuhama hapa kwenda kule, hupoteza umakini kihuduma, ni sawasawa na mtu ambaye kila siku anahama nyumba moja ya kupanga kwenda nyingine…unaelewa ni usumbufu gani anaokutana nao.. kuanza tena kuyazoelewa mazingira mapya ni gharama.
Hasa sasa kama watumishi wa Mungu…tunafundishwa utulivu tuwapo ziarani…Mara nyingi ule mlango wa fadhili ambao unafunguliwa wa kwanza, huwa ni wa Mungu…tulia katika huo huo…nyumba ile ya wageni unayoingia ya kwanza…ikiwa amani ya Kristo imekaa ndani yako…tulia hiyo hiyo mpaka utakapomaliza ziara zako…usiwe mtu wa kutafuta makao mazuri, Kwasababu kumbuka upo ziarani… mahali pa muda tu.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >>
https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Huu ni mwongozo wa maombi yetu ya kambi July 30 – Aug 2.
Kanisa la Nuru ya Upendo
Daresalaam Tegeta. Bofya hapa
👇 📥
Miongozo mingine.
MWONGOZO WA MAOMBI YA KUJIKUZA KIROHO.
MWONGOZO WA MAOMBI YA WAHUDUMU/ WASIMAMAO MADHABAHUNI.
MWONGOZO WA MAOMBI YA FAMILIA
Je Mungu anaangalia mwili na kuuhitaji?.. jibu ni Ndio!.. maandiko yanathibitisha hilo wazi kabisa..
1Wakorintho 6:13 “Vyakula ni kwa tumbo, na tumbo ni kwa vyakula; lakini Mungu atavitowesha vyote viwili, tumbo na vyakula. LAKINI MWILI SI kwa zinaa, BALI NI KWA BWANA, NAYE BWANA NI KWA MWILI”.
Nataka uone hayo maneno ya mwisho yanayosema “…mwili si kwa zinaa, BALI NI KWA BWANA, NAYE BWANA NI KWA MWILI”… Kumbe “miili yetu” ipo mahususi kwaajili ya “Bwana” na Bwana yupo mahususi kwaajili ya “miili yetu”.. Si ajabu tunapomwomba mahitaji ya mwilini anatujibu haraka sana kama tu vile ya rohoni.
Si ajabu tunapoteseka katika mwili hapendi, kwasababu miili yetu ni ya thamani sana kwake, kwaufupi ili tuwe wanadamu ni lazima tuwe na miili..
Sasa je! huu usemi ya kwamba Mungu haangalii mwili unatoka wapi?.. bila shaka ni kwa ibilisi!.
Maandiko yanazidi kusema kuwa “sisi si mali yetu wenyewe”
1Wakorintho 6:19 “Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe”.
Tuzidi kusogea mbele katika andiko hilo… tujifunze ni kwa namna gani MWILI ni Kwa BWANA na BWANA ni kwa MWILI.
Muunganiko wa Miili yetu na Kristo ni mpana sana kiasi kwamba Biblia inatafsiri “viungo vyetu vya mwili ni viungo vya Kristo pia”.. maana yake huo mkono unaouona kama ni wako, kibiblia ni mkono wa Kristo, hayo macho si yako bali ni ya Kristo, kwahiyo kama umemwamini Yesu halafu ukaenda kufanya zinaa, maana yake umechukua kiungo cha Kristo na kukifanyisha zinaa..ndivyo Biblia inavyosema..
1Wakorintho 6:15 “Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha!”
Huo mguu unaoona ni wako kiuhalisia kama umeokoka si wako tena bali ni wa Kristo… ndio maana Bwana Yesu alisema mahali watakapowakaribisha basi wamemkaribisha yeye Kristo..na wakiwakataa wamemkataa yeye Kristo… kwanini?.. ni kwasababu miili yetu si mali yetu wenyewe baada ya kuokoka!, bali viungo vyetu vyote vinakuwa ni vya Kristo na vina mhubiri Kristo.
Luka 10:16 “Awasikilizaye ninyi anisikiliza mimi, naye awakataaye ninyi anikataa mimi; naye anikataaye mimi amkataa yeye aliyenituma”.
Umeona??.. maana yake mtu aliyeokoka ni “Kristo anayetembea”.. ukiendelea kujifunza zaidi katika habari ile ya hukumu ya kondoo na mbuzi katika Mathayo 25:31-46… utaona wale watu waliuliza “ni lini Bwana tulipokuona una njaa, upo uchi tukakulisha na kukuvisha” ndipo Yesu atawaambia “kwa kadri mlivyowatendea wadogo wale basi walimtendea yeye”… wadogo wanaozungumziwa pale ni “watu wa Mungu wanaohubiri habari njema”.
Kwahiyo kumbe matumbo yenye njaa ya watu wa kweli wa Mungu ni matumbo ya Kristo, kumbe miguu yenye vumbi ya watu wa Mungu wa kweli ni miguu ya Kristo.. kwaujumla kumbe miili ya watu wa Mungu ni miili ya YESU mwenyewe!… si ajabu pale alisema “…nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha!”
Sasa kama ni hivyo kwanini unauvika mwili wako mavazi ya jinsia nyingine…je ni Kristo yupi unayemhubiri kwa uvaaji wako?..kwanini unafanya zinaa?, kwanini unachora mwili wako?, kwanini unauvutisha sigara na kuunywesha pombe?
Yachukulie haya kwa uzito mtu wa Mungu, wala usipuuzie!, na kusema Mungu haangalii mwili?.. jihadhari na mafundisho ya uongo! Yanayokuambia kuutunza mwili ni mafundisho ya sheria na vifungo!.. Tunapookoka hatujapewa uhuru wa kufanya dhambi!, La! Hatujafunguliwa kufanya dhambi!.
Siku ya mwisho hatutafufuliwa roho bali miili ndio itakayofufuliwa, na Kristo hakutoa roho yake kwa ukombozi wetu, bali mwili wake wenye damu, mifupa, mishipa, nyama, moyo, miguu, mikono, ngozi !.. vyote Kristo alivitoa kwaajili ya ukombozi wetu..
Waebrania 10:5 “Kwa hiyo ajapo ulimwenguni, asema, Dhabihu na toleo hukutaka, Lakini mwili uliniwekea tayari”.
Biblia inazidi kutufundisha kuitoa miili yetu kwa Bwana..
Warumi 12:1 “Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana”..
Mafundisho mengine:
MAAJABU YA AGANO LA UPENDO WA KRISTO.
Tofauti kati ya makuhani na walawi ni ipi?
Je Bwana YESU alimjibu Pilato au hakumjibu? Je biblia inajichanganya?
KILA MMOJA WENU AJUE KUUWEZA MWILI WAKE.
MTUMAINIE YESU ASIYEISHA MATUKIO.
Kutoka 33:17 “Bwana akamwambia Musa, Nitafanya na neno hili ulilolinena, kwa maana umepata neema mbele zangu, NAMI NAKUJUA JINA LAKO
Jina la Mtu limebeba siri kubwa sana, lakini kabla ya kutazama jina la MUNGU.
Kitu pekee kilichomtambulisha na kinachomtambulisha MUNGU kwetu sasahivi ni JINA LAKE!.. Kamwe hajawahi kutuonyesha Sura yake, wala kuitangaza mahali popote pale!, bali jina lake amelitangaza na kulitukuza sana..
Sasa si kwamba anapenda kujificha kwetu!.. La bali ametuchagulia kilicho bora kwake tukijue!.. Kwahiyo kilicho bora kwake kwetu ni jina lake zaidi ya sura yake.
Na kilicho bora kwa MUNGU kwetu kukijua ni MAJINA YETU zaidi ya SURA ZETU… Utauliza kivipi?..
Kitu pekee kilichoko sasa mbinguni kinachotutambulisha sisi sio SURA ZETU bali ni MAJINA YETU.. Mbinguni hakuna picha zetu!, bali majina!..
Ufunuo 13:8 “Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye JINA LAKE HALIKUANDIKWA katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia”.
Soma pia Ufunuo 17:8, Ufunuo 3:5, Wafilipi 4:3 utaona hakuna sura za watu kule mbinguni… hivyo uzuri wako wa sura, weupe wako, weusi wako, urefu wako, ufupi wako, unene wako, ubounsa wako na wangu unaishia hapa!!!..
Hiyo pia ndio sababu ya Bwana YESU kuwaambia wanafunzi wake wasifurahie pepo wanavyowatii bali wafurahie majina yao yameandikwa mbinguni…
Luka 10:20 “Lakini, msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii; bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni”.
Na unajua, Mungu anatujua kwa majina zaidi ya Sura na rangi?…ndivyo alivyomwambia hata nabii Musa.
Kutoka 33:17 “Bwana akamwambia Musa, Nitafanya na neno hili ulilolinena, kwa maana umepata neema mbele zangu, NAMI NAKUJUA JINA LAKO”.
Umeona hapo?.. Mungu anamwambia Musa anamjua jina lake, sio sura yake…. Kwahiyo ni muhimu sana kuangalia MAJINA YETU na kuyatengeneza…. Maandiko yanasema ni heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi..
Mithali 22:1 “Heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi…”
Sasa tunachaguaje majina??.. je tubadilishe majina tuliyonayo?.. jibu ni La!.. tutaendelea kuwa na majina yetu haya haya ikiwa kama yana maana njema.. Lakini majina yetu haya haya yanaweza kubadilika na kuwa BORA..
Kwa jinsi jina lako linavyozidi kuwa Bora mbele za Mungu, ndivyo nafasi yako mbinguni inavyozidi kuwa kubwa, na kwa kadiri linavyozidi kufifia mbele za Mungu ndivyo mbinguni linavyofutika kumbukumbu lako..
Sasa tunafanyaje majina yetu kuwa Bora?.. Si kwa kwenda kuyatolea sadaka ya ukombozi, au kuyaombea kwenye mkesha.. La!.. unaweza kutoa sadaka za aina zote duniani na jina lako lisiwe mbinguni, lakini bado likaendelea kuwa kubwa mbele za watu, na unaweza kuwa na jina la heshima mbele za watu lakini mbele za Mungu ukawa huna jina.
Ifuatayo ni njia pekee ya kulitakasa jina lako, na heshima yako, na hadhi yako.. na njia hiyo si nyingine zaidi ya KUMCHA MUNGU, na KUJITENGA NA DHAMBI.. Utauliza kivipi, tusome maandiko yafuatayo?.
Kutoka 32:31 “Musa akarejea kwa Bwana akasema, Aa! Watu hawa wametenda dhambi kuu wamejifanyia miungu ya dhahabu. 32 Walakini sasa, ikiwa utawasamehe dhambi yao — na kama sivyo, unifute, nakusihi, katika kitabu chako ulichoandika. 33 Bwana akamwambia Musa, MTU YE YOTE ALIYENITENDA DHAMBI NDIYE NITAKAYEMFUTA KATIKA KITABU CHANGU”.
Kutoka 32:31 “Musa akarejea kwa Bwana akasema, Aa! Watu hawa wametenda dhambi kuu wamejifanyia miungu ya dhahabu.
32 Walakini sasa, ikiwa utawasamehe dhambi yao — na kama sivyo, unifute, nakusihi, katika kitabu chako ulichoandika.
33 Bwana akamwambia Musa, MTU YE YOTE ALIYENITENDA DHAMBI NDIYE NITAKAYEMFUTA KATIKA KITABU CHANGU”.
Umeona kitu kinachochafua jina la Mtu?… ni DHAMBI, Hiko ndicho kinachomwondoa mtu kwenye kumbukumbu za MUNGU, na si tu mbinguni na hata duniani pia..
Kumbukumbu 29:20 “Bwana hatamsamehe mtu huyo, lakini wakati huo hasira ya Bwana na wivu wake vitafuka moshi juu ya mtu yule, na laana yote iliyoandikwa katika kitabu hiki itamkalia juu yake, na BWANA ATALIFUTA JINA LAKE CHINI YA MBINGU”.
Huenda dhambi imechafua jina lako!.. suluhisho ni moja tu, kutubu na kuacha dhambi!.. jina lako hilo litasomeka kwenye kitabu cha mwanakondoo mbinguni.
MSINGI WA NYUMBA YA MUNGU, NI JINA LA MUNGU.
KWANINI TUNAOMBA KWA JINA LA YESU?
HAPO NDIPO WATU WALIPOANZA KULIITIA JINA LA BWANA.
FAIDA NYINGINE YA MAOMBI YA KUSHUKURU.
FUNDISHA KILE UNACHOKITENDA NA KUKIISHI
WhatsApp
Ulishawahi kuona mwanamke anajifungua mtoto bila kusikia utungu wowote? Hilo jambo bila shaka Litakuwa ni la ajabu… kwasababu haliendani kabisa na kanuni za asili …
hata maandiko yanasema hivyo..
Isaya 66:7-8
[7]Kabla hajaona utungu alizaa; Kabla maumivu yake hayajampata, Alizaa mtoto mwanamume. [8]Ni nani aliyesikia neno kama hili? Ni nani aliyeona mambo kama haya? Je! Nchi yaweza kuzaliwa siku moja? Taifa laweza kuzaliwa mara?..
[7]Kabla hajaona utungu alizaa; Kabla maumivu yake hayajampata, Alizaa mtoto mwanamume.
[8]Ni nani aliyesikia neno kama hili? Ni nani aliyeona mambo kama haya? Je! Nchi yaweza kuzaliwa siku moja? Taifa laweza kuzaliwa mara?..
Ni kanuni ya asili ili kiumbe kipya kizaliwe, mzaaji ni lazima apate utungu tu kama malipo ya kile akizaacho ..kila mwanadamu unayemwona chini ya jua, kuna mtu alipata maumivu kwa ajili yake..
Kanuni hii ipo rohoni pia…Kila mtakatifu unayemwona (aliyesimama), haikuwa bure bure…au kirahisi rahisi tu kama unavyodhani, kuna Waliopitia utungu juu yao…
Utauliza hili lipo wapi Kwenye maandiko?.
Paulo kwa Wagalatia,aliandika maneno haya;
Wagalatia 4:19
[19]Vitoto vyangu, ambao kwamba nawaonea utungu tena mpaka Kristo aumbike ndani yenu;
Paulo anawalilia wagalatia, kwa jinsi walivyoiacha neema ya Kristo, na kurudia mafundisho ya kiyahudi..anasema nawaonea utungu tena….tafsiri yake ni kuwa hapo nyuma alishawahi kuwaonea utungu…akawazaa…lakini sasa ni kama vile wanahitaji kuzaliwa tena….
Hivyo watu wote waliozaliwa mara ya pili wapo Waliowanea utungu.
1). Hulia na kuugua:
Maana yake hiki ni kipindi cha machozi na kuomba juu ya wale wote unaotamani wampokee Kristo..ndiyo tabia waliokuwa nayo mitume.
Matendo ya Mitume 20:31
[31]Kwa hiyo kesheni, mkikumbuka ya kwamba miaka mitatu, usiku na mchana, sikuacha kumwonya kila mtu kwa machozi.
Watu wengi wanatamani kuona geuko la dhati kwa jamii zao, rafiki zao, waume zao, watoto wao lakini hawana muda wa kuwaombea kwa kuzama sana kwa kipindi kirefu na wakati mwingine kufunga huku wakiwahubiria…wanaikwepa Kanuni hii ya kiumbe kipya kuzaliwa.
Hichi kipindi wanawake wengi huchungulia kifo, kwa sababu ya maumivu, au shinikizo au kutokwa na damu nyingi sana.
Ndivyo ilivyo pale unapojaribu, Kumvuta mwenye dhambi aifikie toba ya kweli, adui huanza kuinua vita, dhidi yako wewe na huyo unayemzaa.. lile joka litataka kufanya vita na wewe.
Ufunuo wa Yohana 12:1-4
[1]Na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili. [2]Naye alikuwa ana mimba, akilia, hali ana utungu na kuumwa katika kuzaa. [3]Ikaonekana ishara nyingine mbinguni; na tazama, joka kubwa jekundu, alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake vilemba saba. [4]Na mkia wake wakokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi. Na yule joka akasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, ili azaapo, amle mtoto wake.
[1]Na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili.
[2]Naye alikuwa ana mimba, akilia, hali ana utungu na kuumwa katika kuzaa.
[3]Ikaonekana ishara nyingine mbinguni; na tazama, joka kubwa jekundu, alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake vilemba saba.
[4]Na mkia wake wakokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi. Na yule joka akasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, ili azaapo, amle mtoto wake.
Ukijikuta katika wakati huu fahamu ni kung’ang’ana kumfuatilia kondoo huyo bila kujali hali au vipingamizi…unaweza kuona visababu sababu visivyoeleweka, mara hataki tena kukusikiliza, mara anaumwa, mara ndugu zake wanampinga, mara anakuwa mzito.hapa hupaswi kukata tamaa..endelea kumfuatilia kwasababu hizo ni hila za adui kumzuia asikate shauri kwa Bwana Yesu..
Fahamu tu kazi yako si bure upo wakati ataamini na kugeuka kabisa kabisa kwasababu Nguvu uliyonayo na kuu kuliko ya ibilisi..na furaha yako itakuwa ni pamoja na malaika mbinguni. (Luka 15:10).
Pia Biblia inasema…
Yohana 16:21
[21]Mwanamke azaapo, yuna huzuni kwa kuwa saa yake imefika; lakini akiisha kuzaa mwana, haikumbuki tena ile dhiki, kwa sababu ya furaha ya kuzaliwa mtu ulimwenguni.
Upo wakati utayafurahia matunda yako. Siku utakapoona kupitia hao makumi, mamia, maelfu ya watu wanaokoka..na siku ile Bwana anakupa thawabu kwa tunda hilo ulilomzalia.
Swali ni je utungu wako upo wapi?.. ni wapi unaweza kusema yule ni mwana wangu nimemzaa mimi katika Kristo?..
Kwenda tu kusema Yesu anakupenda okoka, halafu ukamwongoza Sala ya toba na kumwacha…hili halimaanishi huyo ni mtoto wako. Ndio maana wapo watu wengi wanaosema leo wamemkiri Yesu, lakini ukiwaangalia sio viumbe vipya..kwasababu hawakuzaliwa, bali waliaminishwa tu.
Tukubali kuzaa kwa kuwafundisha, kuwaombea sana, na kuwafuatilia mpaka watakapokata shauri la kweli kumpokea Yesu.
DALILI ZIPI ZITAMTAMBULISHA MTU KUWA AMEFANYIKA KIUMBE KIPYA?
MAFUNDISHO MAALUMU KWA WAONGOFU WAPYA.
MAUMIVU NYUMA-YA-HUDUMA.
SWALI: Sulemani ana maana gani kusema..Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe.?
Wimbo Ulio Bora 2:7
[7]Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe.
[7]Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa paa na kwa ayala wa porini,
Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe.
JIBU: Mwandishi anaeleza hekima ya kweli juu ya mapenzi halisi yanavyoundwa.. na hivyo anawaasa wale wote wanayoyatafuta…wajue kanuni hizo ili wasiingie katika hasara kama sio majuto.
Andiko hilo linalenga nyanja zote mbili;
Anaposema nawasihi enyi binti za Yerusalemu..
Anawakilisha kanisa, au watu wote wanaotaka kuingia katika mahusiano ya kindoa..
Anasema;
Kwa paa na kwa Ayala wa porini… Anaapa Kwa wanyama hawa, lakini tunajua mara nyingi kwenye agano la kale watu walikuwa wanaapa kwa jina la Mungu…lakini hapa anatumia wanyama hawa ambapo ni Paa na Ayala.
Ni aina ya swala, ambao kwa eneo la Mashariki ya kati ilikuwa ni kawaida sana kuwaona kwenye mapori tulivu..
Wanyama hawa wana sifa ya:
Hivyo mwandishi anawasihi watu wanapotaka kuingia katika mapenzi wayaone Kama ni kuwawinda Ayala na Paa… Ambao hawahitaji pupa…
Ndio maana anasema;
“Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe.”
Akiwa na maana kuwa unapochochea mapenzi kwa haraka utayapoteza…mfano tu unapomvamia Ayala kwa pupa, hutampata atapotelea mbali…
Bali unapokuwa mtulivu na kumsogelea kidogo kidogo, ni rahisi kumnasa…
Hivyo Katika mahusiano ya mwilini anatuasa kuwa mahusiano ya kweli, yanajengwa katika muda…sio kwa kuyapaparikia…vijana wengi, wanang’ang’ania kuingia katika mahusiano kabla ya umri sahihi, au nyakati sahihi au wengine wakikutana hata wiki haijakwisha, ndani ya muda mfupi sana, utaona wameshaahidiana kuoana, na hatimaye kujikuta, wapo kwenye mahusiano hayo, kipindi kinapopita na kugundua uhalisia wao, na kasoro nyingi wanaanza kujuta kulitokea nini? Ni kwasababu walikurupukia mapenzi wala hawakuruhusu yaamke yenyewe katika wakati wake.
Lakini katika Roho, Bwana anaeleza mahusiano kati ya yeye na mtakatifu wake..Upendo kwa Kristo thabiti, hujengwa kwa jinsi tunavyokaa na kudumu ndani yake, na kujua sifa zake, tabia zake, na uweza wake, Na hiyo inakuja kwa kusoma Neno, maombi, na ibada…watu wanaotembea katika mambo hayo kwa kipindi kirefu ndio wanaozama katika mapenzi ya kweli na Kristo.
Lakini mtu anayempenda Yesu kwasababu kaponywa ugonjwa, au kwasababu kasaidiwa Biashara yake kustawi, au Bwana amemwonekani mahali fulani kipekee, mwingine anamtumikia Mungu kwasababu ya shinikizo fulani la watu…Hapo ni sawa na kumrukia Ayala kwa pupa…hatimaye utamkosa..
Watu hawa wanakuwa ni upendo wa kitambo tu, mambo yakishabadilika waanza kusema mioyoni mwao, kama Yesu mwenyewe ndio huyu ni heri nirudie tu maisha yangu ya nyuma…
Hiyo yote ni kwasababu alikurupuka…bila kujua sifa na tabia za ampendaye.
Usikubali upendo wako kwa Kristo ujengwe kwa matukio ya ghafla…ujenge upendo katika mahusiano ya muda.. ndipo yatakapokuwa thabiti.
JAWA NA UPENDO UNAOTAFUTA.
USIKAWIE- KAWIE KUUFUNGUA MOYO WAKO
Maombi Maalumu ya Kuombea Ndoa.
SWALI: Naomba kufahamu Tafsiri vifungu hivi Mhubiri 4:13-16, isemayo ‘Kwa maana kutoka gerezani alikuja kumiliki’ Nini maana ya habari ile?
Mhubiri 4:13 Heri kijana maskini mwenye hekima Kuliko mfalme mzee mpumbavu. ambaye hajui tena kupokea maonyo. 14 Kwa maana kutoka gerezani alikuja kumiliki; naam, hata katika ufalme wake alizaliwa hali ya umaskini. 15 Nikawaona wote walio hai waendao chini ya jua, ya kwamba walishikamana na huyo kijana, huyo wa pili aliyesimama badala ya yule. 16 Hawakuwa na kikomo hao watu wote, hao wote ambao alikuwa juu yao; lakini hata hivyo wale wafuatao baada yake hawatamfurahia. Hakika hayo pia ni ubatili, na kujilisha upepo.
JIBU:
Mstari wa 13. Unazungumzia jinsi hekima, ilivyo bora kuliko cheo, au umri wa mtu. Yawezekana mtu akawa na vyote, lakini akipungukiwa na hekima, ni hatari kubwa sana, Na dalili moja wapo ya kupungukiwa hekima kama anavyofafanua mhubiri ni kukataa kupokea maonyo.
Mfano wa viongozi wa namna hii kwenye biblia ni Rehoboamu(mtoto wa Sulemani), Nebukadreza (nyakati za mwanzoni), Belshaza, Ahabu, Herode. Unaweza kuona jinsi utawala wao ulivyokuwa mwiba mkubwa kwa taifa, na wengine hata kwa vizazi vya mbeleni, kwasababu hawakukubali maonyo ya ki-Mungu..
Ni lazima tukubali kufundishika, kwasababu huo ndio msingi wa hekima (Mithali 13:1, 13:18, 15:5)
Lakini mstari wa 14
Anaeleza, jambo lingine, linalohusiana na ubatili… anazungumzia habari ya kijana aliyetoka katika umaskini, mpaka kuwa mfalme, aliyetoka vifungoni mpaka kuwa mfalme..
Kufunua kuwa mafanikio ya mwanadamu hayatabiriki, sio tu walio na cheo, au waliozaliwa katika familia ya kifalme, ndio wanaofanikiwa, Bwana anaweza kumwinua maskini, mtu asife faa, na kumfanya mtawala na mkuu, mfano wa Yusufu, na Daudi.
Pia Mstari 15,
Unaeleza kuinuka kwa mtawala mwingine, baada ya huyo kijana. Halafu watu wakashikamana naye huyo..Kuonyesha kuwa sifa za kibinadamu, huwa hauzidumu, maana yake kuwa hata uweje shujaa, ufanye mambo mazuri kiasi gani, utafurahiwa kwa kitambo tu, baadaye utachokwa, siku atakaponyanyuka mwingine, atapendwa, na kufuatawa..na wewe utasahaulika..
Mstari 16
Unaendelea kusema, bado watu waliendelea kumfauta huyo mfalme mpya, yaani walimfurahia pia sawa tu na walivyofurahiwa wafalme wengine nyuma waliopita, lakini ghafla baada ya muda wakamchoka naye pia..Mzunguko ukawa ni huo huo..
Ndipo mhubiri anahitimisha kwa kusema ni ubatili mtupu..Maana yake heshima, sifa, na mapokeo ya kibinadamu hayana umilele nyuma nyake, ni sawa tu na kufuata, upepo, ambapo unaweza kukupa matumaini ya muda, kukupelekea mbali, lakini katikati ya safari, ukayeyukia mbali na usijue unapokupeleka.
Haya ndio mambo tunayoyaona hata sasa katika ulimwengu, ni rahisi sana kuona watu wakimfurahia kiongozi mpya, tena yule mpambanaji, lakini baada ya muda wanaanza kupoteza furaha naye, na hatimaye kumpinga, wakitaka mwingine, na yule mwingine ajapo, huwa vivyo hivyo, wanamfurahia kwa muda, baadaye wanamchoka, mzunguko huo umekuwepo ulimwenguni wakati wote..
Lengo lao ni wakitumainia, kumpata kiongozi bora, lakini hajawahi kutokea..
Hawajui kuwa yupo kiongozi bora, mwema, asiyechokwa, asiye na hila, asitafuta vya kwake, aliyejitoa nafsi yake yeye mwenyewe, anayedumu milele, ambaye huyo mwanadamu akimkubali basi matarajio yake yanafikiwa, kwasababu ankuwa naye wakati wote moyoni mwake.. Na huyo si mwingine zaidi ya YESU KRISTO.
Amwaminiye, anapokea uzima wa milele. Wengine wote unafuata upepo..
Je! Upo tayari kumpokea leo, Kama ni ndio, basi fungua hapa kwa mwongozo wa sala ya Toba >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Maana ya Mhubiri 9:18 Hekima ndiyo bora kupita silaha za vita;
Nini maana ya hekima ya maskini haisikilizwi? (Mhubiri 9:16)
Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa watoto wake wote.
Ayubu 41:7 Je! Waweza kuijaza ngozi yake na vyuma vyenye ncha, Au kichwa chake kwa vyusa?
Vyusa ni mikuki maalumu iliyoundwa kwa ajili ya kunasia samaki, ambayo wavuvi hutembea nayo, kuvizia samaki, hususani wale waliokaribia na kilele, kisha huwachoma kwa nguvu, na kuwavuta nje ya maji, na kwasababu ya ukali na mvuvi, na wepesi wa ngozi zao, mara nyingi mkuki ule hauwezi kunasuka mwilini mwao.
Sasa katika habari hiyo, ukianzia mistari ya juu hata katika sura nzima na zile zilizotangulia, ni Ni mahojiano kati ya Ayubu na Mungu, ambapo Mungu anamuuliza maswali Ayubu ayajibu, ni maswali ambayo mpaka sasa hayana majibu, mambo makuu ya Mungu na uweza wake usiofafanulika kwa ufahamu wa kibinadamu. Sasa moja ya mambo aliyokuwa anamuuliza Ayubu ni kuhusu, mnyama “Mamba”, kwa jinsi alivyomuumba kwa namna ya kipekee, tofauti na samaki wengine, Anamweleza jinsi alivyo jasiri, asiye na woga, anamuuliza Ayubu je unaweza kutupa ndoano yako ukamvua kama vile ufanyavyo kwa samaki wengine?(Ay 41:1).
Kwa jinsi magamba yake yalivyo magumu, anasema hata upanga ukipita juu yake haumwingii..
41:26 Mtu akimpiga kwa upanga, haumwingii; Wala fumo, wala mshale, wala mkuki wenye ncha.
Ndio hapo sasa mbeleni anasema tena, je! Je unaweza kukitoba kichwa chake kwa vyusa, kama vile ufanyavyo kwa sangara, na perege? Si itakuwa sawa na unautoboa ukuta na chelewa.
Mungu kwa urefu ameeleza sifa zake mnyama huyu katika sura yote ya 41 (japo kimsingi alikuwa anamwelezea Kristo Yesu, kwa mfano wa wanyama), akimfananisha na mnyama huyu jinsi alivyokuwa thabiti kiasi kwamba hakukuwa silaha yoyote ya adui iliyompata, na jinsi alivyotisha na kuwa na nguvu za kushinda hata mauti..
Kwa uerfu wa habari hiyo fungua hapa usome>>>> SIFA ZA MAMBA YULE MKUBWA WA AYUBU.
Je! Umempokea mfalme huyu moyoni, mwenye nguvu za kutisha, asiyetikiswa na kitu chochote?. Kumbuka wokovu ni kwa faida yako mwenyewe, hakuna njia unaweza ukamshinda adui, kama Kristo hajakuficha ndani yake. Utavuliwa tu na adui kama samaki dhaifu, lakini uwapo ndani ya Kristo hakuna awezaye kukuvua. Ikiwa upo tayari kuyasalimisha maisha yako kwa Bwana Yesu..wasiliana na sisi kwa namba uzionazo mwisho wa makala hii.
Pia kwa maana za maneno mengine ya kwenye biblia fungua hapa >>>> Maana ya Maneno Kwenye Biblia
Madongoa ni nini? (Ayubu 7:5)
Nini maana ya Selahamalekothi?
Ayubu alimaanisha nini kusema ‘nami nitarudi tena huko uchi vilevile;?
Wimbo Ulio Bora 2:10-13
[10]Mpendwa wangu alinena, akaniambia, Ondoka, mpenzi wangu, mzuri wangu, uje zako, [11]Maana tazama, kaskazi imepita, Masika imekwisha, imekwenda zake; [12]Maua yatokea katika nchi, Wakati wa kupelea umefika, Na sauti ya mwigo husikiwa kwetu. [13]Mtini wapevusha tini zake, Na mizabibu inachanua, Inatoa harufu yake nzuri; Ondoka, mpenzi wangu, mzuri wangu, uje zako.
[10]Mpendwa wangu alinena, akaniambia, Ondoka, mpenzi wangu, mzuri wangu, uje zako,
[11]Maana tazama, kaskazi imepita, Masika imekwisha, imekwenda zake;
[12]Maua yatokea katika nchi, Wakati wa kupelea umefika, Na sauti ya mwigo husikiwa kwetu.
[13]Mtini wapevusha tini zake, Na mizabibu inachanua, Inatoa harufu yake nzuri; Ondoka, mpenzi wangu, mzuri wangu, uje zako.
Mahusiano yoyote yale hukumbwa na vipindi tofauti tofauti.ni sawa na dunia na misimu yake, kuna vipindi Vya kiangazi, vipindi vya masika, vipindi vya joto, na vipindi vya baridi…
Vivyo hivyo pia mahusiano yoyote hukumbwa na nyakati kama Hizi..
Watu wa agano la kale walikuwa katika nyakati ngumu za upendo na Mungu, nyakati zao zilijawa na misuko-suko, ukame na kutaabika, nyakati za jasho na damu…Kwasababu shetani alikuwa na nafasi kubwa katika maisha ya wanadamu, lakini walikuwa hawajamjua bado Mungu vizuri.
Lakini mwokozi alipokuja, alituliza dhoruba zote, mawimbi yote, jua lote, mizigo yote, na taabu zote ..alilitimiza hilo kwa kujitoa kwake pale msalabani. Ndio maana akasema yeye ni Bwana wa sabato, ( pumziko). Kwasababu Alikuja kuleta pumziko haswaa la pendo lake, ili mtu asikae katika masumbufu ya aina yoyote rohoni.
Hivyo leo hii anasema nasi kama mtu amwambiaye mpenzi wake habari za faraja..
10]Mpendwa wangu alinena, akaniambia, Ondoka, mpenzi wangu, mzuri wangu, uje zako, [11]Maana tazama, kaskazi imepita, Masika imekwisha, imekwenda zake; [12]Maua yatokea katika nchi, Wakati wa kupelea umefika,
10]Mpendwa wangu alinena, akaniambia, Ondoka, mpenzi wangu, mzuri wangu, uje zako,
[11]Maana tazama, kaskazi imepita, Masika imekwisha, imekwenda zake; [12]Maua yatokea katika nchi, Wakati wa kupelea umefika,
Huu ni wakati wa kuitikia wito wake mkuu wa upendo usio na usumbufu.. mpokee sasa ukuburudishe maishani. Akupe uzima wa milele, akupe faraja na tumaini uone maana ya maisha. Nyakati hizi ni za hatari, ulimwengu hauwezi kukupeleka popote, kinyume chake utaishia jehanamu tu ukiufuata, lakini ukimgeukia mwokozi na kumfuata utapata uzima wa milele.
SHALOM.
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 11 (Mithali, Wimbo ulio bora, Mhubiri)