Somo la nyuma tuliona msingi wa Ukristo ni nini.. kwamba Yesu Kristo Bwana wetu ndiye msingi wenyewe..Yeye huitwa jiwe kuu la pembeni, na mwamba ambao juu yake sisi sote tumewekwa, pasipo Yesu hakuna ukristo. Yeye ndio msingi wa imani yetu.
Lakini pia kikawaida msingi ukishakaa chini, huwa nguzo zinafuata juu yake, kazi ya nguzo ni kulifanya jengo liweze kushikamana na kusimama vema toka juu kwenye paa mpaka chini kwenye msingi wenyewe.
Hivyo wewe kama mkristo ukishaweka msingi chini wa nyumba yako ya kiroho, fahamu pia moja kwa moja utanyanyua na nguzo zake, ili kuliunda jengo. Je nguzo zenye ni zipi?
Hizi ndizo nguzo kuu saba (7), za ukristo .
Ni wajibu wa kila mwamini aliyekombolewa na Kristo, pindi tu alipookoka aanze kukua ki-upendo. Hii ndio nguzo mama, kwasababu Mungu mwenyewe ni upendo (1Yohana 4:8). Zaidi sana anapaswa afahamu kuwa, upendo wa ki-Mungu sio kama ule wa kibinadamu
wa kupenda wanaokupenda, hapana ..huu ni upendo unaozidi usio na sharti wa kujitoa, ambao unapenda mpaka maadui, zaidi na kuwaombea wanaokuudhi.
Mtu asiyejijenga katika huu, haijalishi atajitaabisha vipi kwa Kristo, kazi yake itakuwa ni ya hasara siku ile ya mwisho.
1 Wakorintho 13 : 1-13
1 Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.
2 Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi
cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi.
3 Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama
sina upendo, hainifaidii kitu.
4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;
5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;
6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;
7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.
8 Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha,
zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.
Ili maisha ya mkristo yasimame vema, maombi ni nguzo nyingine inayomkamilisha. Biblia inasema maombi yanapaswa yawe ni jambo la daima.
Wakolosai 4:2 Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani;
Maombi ni sawa na maji mwilini, au mafuta kwenye gari, vikikosekana hivi vitu hakuna utendaji kazi wowote utakaoendelea, vivyo hivyo ukristo wako usipokuwa wa maombi, hautaendelea sana. Utakufa tu siku moja
Ili tujengeke vizuri kiwango cha chini Bwana alichotaka tuombe kwa siku ni saa moja (Mathayo 26:40). Bwana Yesu alikuwa mwombaji, mitume walikuwa waombaji, sisi yatupasaje?
Ukishaokoka, jambo linalofuata ni kuwa karibu na biblia yako. Katika hiyo utapata kuelewa mpango kamili wa Mungu katika maisha yako. Huku ukisaidiwa na waalimu na wakufunzi wako kwenye usomaji wako wa biblia, kama Bwana wetu Yesu alivyokuwa mdogo akifanya bidii kuwasikiliza waalimu wake.
Kujifunza na kusoma kunapaswa kuwe ni tendo la kila siku. Neno ni kama chakula na maombi ni maji. Hivi viwili ndivyo vinakukuza kiroho na kukujenga nafsi. Hupaswi kuacha kusoma.. Mkristo asiyeifungua biblia yake ni rahisi sana kuchukuliwa na upepo wa ibilisi kwa mafundisho potofu. Kwasababu hamjui Mungu.
Hekima, maarifa, imani, ufahamu,na mamkala vinatoka katika kulijua Neno na mafundisho. Hivyo soma hiyo kila siku, pia sikiliza mafundisho kutoka kwa waalimu wako sahihi wa kweli, kwasababu ni muhimu sana kuvipata.
Matendo 2:41 Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu.
42 Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.
1Timotheo 4:13 Hata nitakapokuja, ufanye bidii katika kusoma na kuonya na kufundisha
Ushirika ni kukutana pamoja na wenzako kujengana. Ushirika ni umoja wa Roho katikati yetu.
Waebrania 10:25 wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia.
Kama mtakatifu, hupaswi kujiaminisha utakuwa na utimilifu wote wa ki-Mungu ndani yako kivyako. Utahitaji kukamilishwa na wengine kwa sehemu baadhi, Ndio hapo suala la ushirika linakuja.
Ndio sababu Mungu ameweka karama tofauti tofauti ili tujengane. Katika ushirika mtaombeana, kushiriki meza ya Bwana pamoja, mtafarijiana, mtasaidiana n.k.
Na pia biblia inasema wawili walalapo watapata joto.
Mhubiri 4:9 Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; Maana wapata ijara njema kwa kazi yao.
10 Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua!
11 Tena, wawili wakilala pamoja, hapo watapata moto; lakini mmoja aliye peke yake tu awezaje kuona
moto?
12 Hata ikiwa mtu aweza kumshinda yule aliye peke yake, wawili watampinga; wala kamba ya nyuzi tatuhaikatiki upesi.
Muwapo pamoja kuna ulinzi wa kipekee unaongezeka juu yenu. Hivyo kamwe usijaribu ule ukristo wa kivyako-vyako. Ni lazima tuwe washirika wa kanisa. Kama kanisa la kwanza lilivyoweza kusimama kwa kanuni hiyo.
Utakatifu ni utambulisho wa ukristo. Huwezi kuwa mkristo, halafu ukawa mwovu, huwezi kupokea Roho Mtakatifu halafu sifa za utakatifu usizionyeshe ndani yako. Kwasababu maandiko yanasema Mungu tunayemtumikia ni Mtakatifu hivyo na sisi pia hatuna budi kuenenda katika utakatifu. Bwana Yesu pamoja na watakatifu wa kwanza walizingatia viwango vyote vya usafi na ukamilifu. Vivyo hivyo na sisi
1Petro 1:16 kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.
Ushuhudiaji unaanza pindi tu unapookoka. Kila mkristo ameitwa kuitenda kazi ya Bwana. Na ni lazima afanye hivyo kama sehemu ya maisha yake, ili safari yake ya wokovu hapa duniani iwe imara ni lazima azae matunda. Uwakili ni kazi yetu ya daima. Ukristo bila uinjilisti hauwezi kuwa imara. Kanisa la kwanza lilikuwa la kiinjilisti. Kila mmoja alitambua wajibu wake wa kuisambaza injili kila mahali walipokuwa wakilizingatia lile agizo la Bwana.
Matendo 8:4 Lakini wale waliotawanyika wakaenda huko na huko wakilihubiri neno.
.
Sifa ya Mungu ni utoaji, ndio maana mpaka leo tunanufanika na mengi katika ulimwengu wake. Hata tulipopotea katika dhambi alijitoa kwa ajili yetu kwa kumtoa mwanawe awe fidia.
Na sisi kujitoa kihali na kifedha kwa ajili ya injili na kanisa la Kristo, ni nguzo muhimu sana. Unawajibu wa kuisapoti huduma inayokukuza kiroho, kwa zaka na changizo zako, pamoja na kuwasaidia ndugu (maskini). Kwasababu, Bwana Yesu na kanisa la kwanza lilikuwa na desturi hiyo.
1 Wakorintho
16:1 Kwa habari ya ile changizo kwa ajili ya watakatifu, kama vile nilivyoamuru makanisa ya Galatia, nanyi fanyeni vivyo
Hivyo sisi sote tukizitendea kazi nguzo hizo muhimu, basi tuwe na uhakika jengo letu la Imani litakuwa imara sana, linaloweza kustahili tufani na majaribu yote, lililoundwa vyema, kwa utukufu wa Mungu, hata siku ile ya kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Rudi Nyumbani
Mtakatifu Rita, ambaye kwa kanisa katoliki anajulikana pia kama ‘mwombezi wa mambo yasiyowezekana’, na ‘mfanya miujiza’.
Ni mama aliyezaliwa mwaka 1381, katika mji unaitwa Kashia, taifa la Italy. Aliolewa akiwa na umri mdogo lakini baada ya mume wake na watoto wake wawili kufa aliamua kujiunga na utawa, ijapokuwa alipitia changamoto, kujiunga na jamii hiyo kwasababu tayari alikuwa ameshaolewa(sio bikira), lakini mwishoni alifanikiwa.
kulingana na kanisa katoliki maombi ya Rita yaliwaletea wengi majibu, lakini pia alitambulika kwa jeraha dogo kwenye kipaji cha uso wake, wakiamini kuwa ni alama ya ukristo, kufuatana na mateso ya Yesu msalabani, mahali alipowekewa taji ya miiba. Alikufa kati ya umri wa miaka 75-76.
Na ilipofika tarehe 24 May 1900, papa Leo XIII, Alimtangaza kuwa mtakatifu. Yaani ukitangazwa kuwa mtakatifu, unakidhi vigezo vya kuwa mwombezi wa walio hai.
Tangu huo wakati wakatoliki wengi duniani wamekuwa wakimfanyia novena, na litania. Na wengi wakishuhudia kuwa matatizo yao sugu, yakitatuliwa, hivyo imemfanya kuwa maarufu sana.
Lakini Je! Jambo hili ni kweli? Ni vema kufahamu kuwa katika maandiko matakatifu (BIBLIA), Hakuna mahali popote, tunafundishwa kuwa watakatifu waliokufa zamani au sasa wanaweza kutuombea. Zaidi sana wanakuwa hawaelewi neno lolote linaloendelea duniani, biblia inasema hivyo katika;
Mhubiri 9:5 kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.
Umeona? Kwahiyo desturi hii, ya kupeleka maombi yetu kwa watakatifu watuombee, ni ya kipagani, Ni ibada za sanamu, ambayo asili yake ilianzia kwenye dini zinazoamini mizimu inaweza kuwasiliana nasi. Kusema hivi haimaanishi tunawapinga wakatoliki, au tunatangaza chuki hapana, bali tunasemezana ukweli ili tupone, kwasababu safari yetu ni moja sote tuurithi uzima wa milele, sisi tunasema ni wakristo.
Haijalishi utakuwa ulifanya novena ya Rita ikakuletea majibu kiasi gani, bado ni ibada ya sanamu, kumbuka pia shetani analeta majibu, si ajabu mambo hayo kutendeka, ili watu wapumbazike katika hayo.
2Wakorintho 11:14 Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.
Mwombezi wetu ni mmoja tu naye ndiye YESU KRISTO (1Yohana 2:1). Lakini sio pamoja na Petro, au Paulo, au Eliya, au Mariamu, au Yusufu. Hao wote ni watakatifu ambao walihitaji ukombozi tu kama sisi, na wenyewe walituelekeza kumtazama Yesu Kristo, na sio wao.
Mtume Paulo alisema maneno haya;
1Wakorintho 1:13 Je! Kristo amegawanyika? Je! Paulo alisulibiwa kwa ajili yenu? Au je! Mlibatizwa kwa jina la Paulo?
Hivyo hakuna haja ya kupeleka maombi yako kwa mtakatifu yoyote, na vilevile wale walio kule hawawezi kutuombea sisi pia. Halikadhalika wewe huwezi kumwombea mwenye dhambi aliyekufa, kwamba Bwana amtoe matesoni. Imani hiyo haipo pia katika biblia. Soma (Waebrania 9:27). Mafundisho ya watu kupitia toharani hayapo katika biblia.
Tujifunze kusoma biblia tutafunguka kwa mengi, mapokeo ya kidini sio Neno la Mungu. Hao wanaoabudu miti na mawe twaweza kuwacheka, lakini tukawa kama wale tu isipokuwa katika mfumo mwingine, tusipopenda kusoma biblia. Tukikataa kuwa wafuasi tu wa kidini tukapenda Neno la Mungu, Roho Mtakatifu atatusaidia kufunguka kwa mengi.
Hivyo ikiwa wewe ulikuwa ni mmojawapo wa wanaopeleka maombi kwa Rita wa kashia, au kwa mtakatifu mwingine yoyote acha sasa kufanya hivyo. Tubu dhambi ukabatizwe, upokee Roho Mtatakatifu ambaye atakuongoza na kukutia katika kweli yake yote(Yohana 16:13).
Ikiwa upo tayari leo kuokoka, basi waweza fungua hapa kwa ajili ya mwongozo wa sala ya Toba >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
Mada Nyinginezo:
Novena ni nini? Na je ipo kibiblia?
LITANIA YA BIKIRA MARIA JE! NI SALA YA KIMAANDIKO?
Kuomba katika roho ni kupi? na je nifanye nini ili niweze kuomba hivyo?
Upo umuhimu wa kufanya ushirika.
Ushirika unatokana na neno kushiriki. Na matokeo ya kushiriki ni kuambukizwa sifa au tabia ya kile kitu unachoshirikiana nacho.
Watu wengi hatujui hata Neno USHIRIKINA limetokana na neno kushiriki. Washirikina wanashiriki mambo ya kipepo, ili wapate sifa za kipepo, au waambukizwe tabia zao ndani yao na ndio maana wanaitwa washirikina. Ndio hapo utaona mtu anakwenda kwa mganga, kisha anapewa dawa Fulani anaambiwa anywe au aweke chini ya biashara yake, halafu itamfanya wateja wavutiwe na biashara yake. Mtu huyo analivuta pepo la mauti ndani yake, kwa ushirika anaoufanya kisa lile pepo linasimama pale na kushawishi watu waovu , kisha Yule mtu anapata anachokitafuta kwa muda, halafu mwisho wa siku pepo lile linageuka na kumuua,.kwasababu hatma ya shetani sikuzote ni kuchinja na kuiba. Lakini ikiwa mtu huyo hatofanya ushirikina wowote, hawezi kuwa na uwezo huo wa kipepo.
Sasa na katika Mungu ni vivyo hivyo. Unapokuwa nyumbani mwa Mungu Usiwe ni mtu wa kwenda na kutoka tu, kama mtembeleaji. Huna ushirika wowote na watakatifu wengine, huna ushirika wowote na Mungu,. Ukifanya hivyo hutakuwa na nguvu zozote au sifa au tabia zozote za ki-Mungu ndani yako.
Ushirika wa Kikristo Ni upi?
Kwamfano Unapohudumu, yaani unapojishughulisha na jambo Fulani ndani ya Kanisa labda kufundisha, kujitoa kwa ajili ya maendeleo ya kanisa kama kuchangia, kufagia, kujenga, kupiga deki, na vyovyote vile. Hapo ni sawa unafanya ushirika na watakatifu wengine katika kuujenga mwili wa Kristo. Na hivyo rohoni, unapokea uwezo au sifa nyingine ya ziada ambayo hapo kwanza ulikuwa huna. Na moja ya uwezo huo ni nguvu ya kuendelea mbele katika imani.
Na pia Meza ya Bwana. Huna budi kushiriki. Kwasababu hiyo inakuunganisha na Mungu moja kwa moja. Embu soma maandiko haya upate kuelewa vema;.
1Wakorintho 10:14 “Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya sanamu. 15 Nasema kama na watu wenye akili; lifikirini ninyi ninenalo.
16 Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, JE! SI USHIRIKA wa damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao, SI USHIRIKA wa mwili wa Kristo? 17 Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja.
18 Waangalieni hao Waisraeli walivyokuwa kwa jinsi ya mwili; wale wazilao dhabihu, je! Hawana shirika na madhabahu? 19 Basi niseme nini? Ya kwamba kile kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu? Au ya kwamba sanamu ni kitu?
20 Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani”.
Umeona? Kumbe kikombe na mkate ule ni USHIRIKA.. ambao sisi tunafanya na Mungu. Na hivyo una matokeo yake makubwa rohoni. Yesu alisema mtu asipoula mwili wangu, na kuinywa damu yangu hana uzima ndani yake. (Yohana 6:53)
Vivyo hivyo na kutawadhana miguu watakatifu. Unapomwosha mwenzako miguu, maana yake ni kuwa unajishusha na kujinyenyekeza kwake, hivyo unapokea neema ya Upendano wa ndugu ndani yako.
Hivyo kwa ufupi ili utake kupokea tabia zote za Ki-Mungu ndani yako, kama Upendo, utu wema, furaha, amani, Uvumilivu, huna budi kuwa katika ushirika wake. Nje ya hapo, huwezi.
Matendo 2:41 “Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu. 42 Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali”
Usiukwepe ushirika wa Bwana.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
Mada Nyinginezo:
MEZA YA BWANA, NA KUTAWADHANA MIGUU.
KANUNI RAHISI YA KUPOKEA BARAKA MARA DUFU.
HISTORIA YA BIBLIA YA KING JAMES, INA FUNZO GANI KWETU?
Ni lini na wapi Ibrahimu aliioona siku ya Bwana akashangilia?
Mwanamke wa adabu huheshimiwa daima; (Mithali 11:16)
Nakusalimu katika jina tukufu sana la mwokozi wetu Yesu Kristo, Nakualika katika kuyatafakari maneno ya uzima.
Leo tutajifunza siri mojawapo iliyokuwa nyuma ya watu wa zamani, ambayo tukiitumia na sisi italeta mageuzi makubwa sana katika ulimwengu huu tunaoishi. Wengi wetu tunadhani watu wa leo wanayoakili zaidi ya kuwashinda wale, lakini ukweli ni kwamba yapo mambo mengi yalifanywa na watu wa kale, ambayo mpaka leo hatuwezi kuyafanya. Mfano mmojawapo ni yale mapiramidi yaliyopo Misri (ambayo yapo katika maajabu saba ya dunia), teknolojia iliyotumika pale, hadi sasa hakuna ujenzi unaoweza kuwa kama ule, ijapokuwa tunazo teknolojia kubwa na za kisasa.
Tukisoma katika maandiko tunaona, Jinsi Babeli ilivyoanza kujengwa na kusitawi. Lakini hilo halikuwa jambo zito, kwasababu miji mingi pia ilikuwa inajengwa. Jambo lililoipelekea Babeli kuwa tofauti na miji mingine ni pale watu walipotaka kuunda Mnara, ndani ya mji ule, lengo lao likuwa ni kufika MBINGUNI, ili wajipatie jina. Sasa wengi wetu tunaona kama walikuwa ni wajinga kuunda hiyo Projekti yao. Tunadhani walikuwa wanafanya jambo la masiara au walikuwa hawaelewi kitu wanachokifanya. Ni sawa na leo mtu akumbie ninaunda ndege, ambayo itanifikisha mbinguni, ni rahisi kusema amerukwa na akili. Lakini maandiko yanatuonyesha watu hawa, walikuwa wanajua wanachokifanya mpango huo wangeweza kufanikiwa kama Mungu asingeingilia kati. Embu tusome habari hiyo tuombe jambo hilo;
Mwanzo 11:1 “Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja. 2 Ikawa watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi tambarare katika nchi ya Shinari; wakakaa huko.
3 Wakaambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome moto. Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa. 4 Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote.
5 Bwana akashuka ili auone mji na mnara waliokuwa wakiujenga wanadamu. 6 Bwana akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, WALA SASA HAWATAZUILIWA NENO WANALOKUSUDIA KULIFANYA.
7 Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao. 8 Basi Bwana akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote; wakaacha kuujenga ule mji. 9 Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo Bwana alipoichafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko Bwana akawatawanya waende usoni pa nchi yote”.
Umeona hapo? Mungu hakusema hawa watu wamerukwa na akili, wanafanya kazi isiyokuwa na faida, bali alisema hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya. Maana yake ni kuwa watafanikiwa, Hivyo Mungu akaangalia NGUVU yao ya kufikia adhma yao ipo wapi? Akaona kuwa sio katika ile teknolojia, bali katika ule USEMI MMOJA waliokuwa nao.
Usemi maana yake ni NIA. Hawa watu waliingia maagano,wakapatana kwa moyo mmoja, kwamba kila mmoja atajitoa kwa akili, hali na mali, kuhakikisha Mnara huo unajengeka na kilele chake kinafika mbinguni, hata kama itawagharimu miaka 1000, lakini mwisho wa siku ni lazima wafike mbinguni. Lakini Mungu akaenda kuuchafua usemi wao wakawa hawaelewani baada ya pale, kwasababu walichokuwa wanakijenga ni kwa ajili ya JINA LAO na sio jina la MUNGU. Hivyo Usemi wao ukachafuliwa wakawa hawaelewani, mpaka na lugha zao zikageuzwa pia.
Ni nini Bwana anataka tuone hapo,
Ni nguvu ya USEMI MMOJA.
Na sisi kama kanisa la Kristo lililo hai. Nafasi yetu ya kuufikia utukufu WOTE wa Mungu ulio mbinguni tunao.
Kwasababu Tayari siku ile ya Pentekoste, Roho Mtakatifu alirudisha USEMI HUU mmoja katikati yetu. Na ndio maana siku ile utaona watu walianza kunena kwa lugha za mataifa mengine magheni, kuonyesha kuwa Sasa Mungu anataka mataifa yote wakaribie waliunde taifa la Mungu haijalishi lugha zao, jinsia zao, rangi zao. Alikuwambusha tukio lile la Babeli, kwamba sasa lianze kufanyika tena kwa jina la Bwana.Watu wale wakatii na siku ile ile kanisa likaanza. Mnara wa Mungu ukaanza kujengwa duniani.
Matendo 2:1 “Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja.
2 Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. 3 Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao.
4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka. 5 Na walikuwako Yerusalemu Wayahudi wakikaa, watu watauwa, watu wa kila taifa chini ya mbingu. 6 Basi sauti hii iliposikiwa makutano walikutanika, wakashikwa na fadhaa, kwa kuwa kila mmoja aliwasikia wakisema kwa lugha yake mwenyewe.
7 Wakashangaa wote, wakastaajabu wakiambiana, Tazama, hawa wote wasemao si Wagalilaya? 8 Imekuwaje basi sisi kusikia kila mtu lugha yetu tuliyozaliwa nayo? 9 Warparthi na Wamedi na Waelami, nao wakaao Mesopotamia, Uyahudi na Kapadokia, Ponto na Asia.
10 Frigia na Pamfilia, Misri na pande za Libia karibu na Kirene, na wageni watokao Rumi, Wayahudi na waongofu,.11 Wakrete na Waarabu; tunawasikia hawa wakisema kwa lugha zetu matendo makuu ya Mungu.
12 Wakashangaa wote wakaingiwa na shaka, wakiambiana, Maana yake nini mambo haya?
Na ndio maana hatushangai kwanini Kanisa la kwanza lilikuwa na mapinduzi makubwa sana. Kwa kipindi kifupi sana injili ilinea duniani kote, na walikuwa hawana vyuo vya biblia. Ni kwasababu walikuwa na USEMI mmoja.
Lakini leo kanisa limevunjika vunjika, shetani kalisambaratisha, kachafua lugha yetu. Hata ndani ya kanisa moja kila mmoja anao usemi wake. Ijapokuwa wote mnaliamini Neno hilo hilo moja. Kwasababu gani, ni kwasababu tunatafuta utukufu wetu wenyewe na sio ule wa Mungu.
Ni kweli tutaunganishwa na Neno lakini tusipotaka kujishusha na kutii, ili tumwinue Kristo na sio sisi wenyewe, kamwe hatutaona utukufu wa Mungu kama vile inavyopaswa. Hatutaufikia moyo wa Mungu mbinguni, hatutaona udhihirisho wa wazi wa Miujiza mikubwa ya Mungu katika kanisa. Ni sharti tujikane nafsi zetu kila mmoja tumfuate Yesu , ili tuujenge mnara huu wa Bwana.
Luka 14:27 “Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. 28 Maana ni nani katika ninyi, KAMA AKITAKA KUJENGA MNARA, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia? 29 Asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi, watu wote waonao wakaanza kumdhihaki”.
Tufahamu kuwa kanisa sio shirika la kijamii, sio huduma, wala sio chuo Fulani, bali ni udhihirisho wa Mungu duniani kupitia watu wake aliowakomboa. Hivyo ni lazima sisi kama viungo vya Kristo tujishikamanishe tuwe mwili mmoja Ili Kristo atende kazi zake duniani kama alivyokuwa anatenda zamani. Na hii inaanza na mtu mmoja mmoja, pale tunapodhamiria kuyatii maneno ya Kristo.
Bwana atujalie kuliona hilo.
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
Mada Nyinginezo:
NITAUVUTAJE UWEPO WA ROHO MTAKATIFU KARIBU NAMI?
Je kunena kwa Lugha mpya kukoje?
NI NINI TUNAJIFUNZA KWA YOANA NA MANAENI?
USIIKARIBIE DHAMBI, KAA NAYO MBALI.
Kibiriti ni kitu gani? kama kinavyozungumziwa kwenye maandiko?