Yahu ni nani? (Wimbo 8:6).

Yahu ni nani? (Wimbo 8:6).

Jibu: Turejee,

Wimbo 8:6 “Nitie kama muhuri moyoni mwako, Kama muhuri juu ya mkono wako; Kwa maana upendo una nguvu kama mauti, Na wivu ni mkali kama ahera. Mwako wake ni mwako wa moto, Na miali yake ni MIALI YA YAHU”.

“YAHU” ni jina lingine la “YAHWE” ambalo ndilo “YEHOVA”.

Kutoka 6:2 “Kisha Mungu akasema na Musa, akamwambia, Mimi ni YEHOVA; 

3 nami nilimtokea Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi, bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao”.

Kwahiyo YAHU, YAHWE na YEHOVA ni jina Moja!

Lakini hapo katika Wimbo 8:6 maandiko yanasema kuwa “upendo una nguvu kama mauti”.. maana yake kama vile mauti ilivyo na nguvu kiasi kwamba wanaokufa ni ngumu kurudia uzima! Vile vile Upendo wa Mungu kwetu ni mkuu kiasi kwamba akitupenda ametupenda!, hakuna wakati atatuchukia, anaweza asipendezwe na sisi lakini si kutuchukia!.

Warumi 8:35 “Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?………

38  Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo,

39  wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu”.

Lakini pia anasema wivu ni mkali kuliko Ahera..Ahera ni “Kaburi”, Kwa urefu Zaidi fungua hapa >>>Ahera ni wapi? Kama tunavyosoma katika biblia.

Na miali yake ni miali ya YAHU. Maana yake ni kuwa Mungu ana upendo lakini pia anawivu, huwezi kamwe kutanganisha vitu hivi viwili, UPENDO na WIVU.

Kwahiyo kama Mungu ametupenda, basi hapendi kuona tunaabudu miungu mingine, tukifanya hivyo tunamtia yeye wivu, umbao unaweza kutupeleka kaburini (Ahera).

Kutoka 20:3 “Usiwe na miungu mingine ila mimi.

4 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.

5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, NI MUNGU MWENYE WIVU; NAWAPATILIZA WANA MAOVU YA BABA ZAO, HATA KIZAZI CHA TATU NA CHA NNE CHA WANICHUKIAO, 

6 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu”.

YAHU atusaidie tusimtie Wivu, lakini tumpende, na vile vile upendo wake utubidiishe katika kuyafanya mapenzi yake.

Maran atha.

Mafundisho Mengine:

Wivu ni nini na kuna aina ngapi za Wivu?

UMETEKWA NA UPENDO WA KRISTO?

MWIMBIE BWANA ZABURI KATIKA NYAKATI ZA FURAHA.

IJUE HEKIMA YA MUNGU KATIKA KUKUINUA KIMAISHA.

WEKA KUMBUKUMBU YA MAMBO BWANA ANAYOKUFANYIA KWASABABU YATAKUFAA MBELENI.

Rudi Nyumbani:

 

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments