Kuna hatua za kupitia, ambazo ni lazima kila mkristo azipitie ili aweze kumzalia Bwana matunda, Bwana alizifananisha hatua hizi na ule mfano wa MPANZI;
Tukisoma
Mathayo 13:2-9 ” Wakamkusanyikia makutano mengi, hata akapanda chomboni, akaketi; na ule mkutano wote wakasimama pwani.
3 Akawaambia mambo mengi kwa mifano, akisema, Tazama, mpanzi alitoka kwenda kupanda.
4 Hata alipokuwa akipanda, mbegu nyingine zilianguka karibu na njia, ndege wakaja wakazila;
5 nyingine zikaanguka penye miamba, pasipokuwa na udongo mwingi; mara zikaota, kwa udongo kukosa kina;
6 na jua lilipozuka ziliungua; na kwa kuwa hazina mizizi zikanyauka.
7 Nyingine zikaanguka penye miiba; ile miiba ikamea, ikazisonga;
8 nyingine zikaanguka penye udongo mzuri, zikazaa, moja mia, moja sitini, moja thelathini. 9 Mwenye masikio na asikie. “
Katika mfano huu tunaona huyu mkulima alienda kupanda mbegu, kumbuka hizi hazikuwa mbegu za kuchimbiwa ardhini, bali zilikuwa ni mbegu nyepesi ndogo za kurusha, na alipokuwa akizirusha alizielekeza zote ziende kwenye udongo mzuri, ili zikue na kuzaa matunda, hizi tofauti na mbegu zile za kupanda ambapo mkulima huenda moja kwa moja kwenye udongo mzuri na kuzifukia ardhini, lakini hizi ni tofauti, tunaona zilipewa nguvu ya kutembea kwa kurushwa ili zifike katika eneo lililokusudiwa la udongo mzuri. Lakini kuna nyingine zilikwama kwenye hatua tofauti tofauti katika safari zao kuelekea kwenye udongo mzuri.
Katika mfano huu hapa mbegu zilipitia katika hatua kuu NNE (4), ambazo ni; NJIANI, kwenye MIAMBA, Kwenye MIIBA, na kwenye UDONGO MZURI. Na hizi ndizo hatua NNE za mkristo katika safari ya maisha yake tangu siku ile ya kwanza anayompa Bwana maisha yake. Tuzitazame hatua hizi kwa ufupi;
Unaposikia injili (NENO) kwa mara ya kwanza, wewe unakuwa ni mbegu iliyorushwa na mkulima ambaye ni YESU KRISTO katika shamba lake, Kumbua Bwana alikusudia wewe ufike kwenye udongo mzuri, lakini mbeleni kuna vikwazo sasa hatua ya kwanza ni wewe kurushwa kutokea NJIANI, hapa unajikuta umeshapokea neno la Mungu (yaani kumpokea Kristo) katika namna ya kawaida unajikuta bado haulielewi lile NENO vizuri, ndani yako unasikia kiu ya kutaka kuendelea kumjua Mungu, hivyo unajikuta hauridhiki katika hali uliyopo ndani kunachemka kutaka kuendelea kujua zaidi, unaenda huku na kule kutafuta majibu ya maswali yako ya rohoni, na unakuwa na kiu pia ya kusoma NENO la Mungu.
Ukiona hali kama hiyo ujue ni ile nguvu ya Roho wa Mungu inakusukuma kusonga mbele kuelekea kwenye udongo mzuri ili ukamee. Lakini kwa upande mwingine unakuta mtu amesikia injili na ile nguvu ya kumfanya aendelee kusonga mbele yaani kutaka kumjua Mungu zaidi haipo ndani yake. anaridhika na hali aliyopo, akikuta kitu kwenye NENO la Mungu asichokielewa hajishuhulishi kutafuta jibu la maswali yake , hivyo anatulia njiani, hapo ndipo shetani anapopata nafasi kuchukua kile kilichopo ndani yake, hapo ndipo linakuja lile neno “aliyenacho ataongezewa na asiyenacho hata kile kidogo alichonacho atanyang’anya”.
Hivyo unamkuta mtu anajiita mkristo lakini matendo yake hayaendani na ukristo, hanufaiki na jambo lolote katika NENO la Mungu ,japo anaenda kanisani kila siku, anaimba kwaya, anasema ameokoka pasipo kujua ibilisi ameshamwondolea ile nguvu ya Roho Mtakatifu na kiu ndani yake imekufa, anakuwa hana tofauti na mtu asiyeamini.
Na ndio maana Bwana Yesu alisema
Mathayo 13: 19″ Kila mtu alisikiapo neno la ufalme asielewe nalo, huja yule mwovu, akalinyakua lililopandwa moyoni mwake. Huyo ndiye aliyepandwa karibu na njia.”
Mathayo 13:20-21 “Naye aliyepandwa penye miamba, huyo ndiye alisikiaye lile neno, akalipokea mara kwa furaha; lakini hana mizizi ndani yake, bali hudumu kwa muda; ikitukia dhiki au udhia kwa ajili ya lile neno, mara huchukizwa. “
Kumbuka hii ni hatua ya pili, ambayo inakuja baada ya kushinda ile hatua ya kwanza, shetani akishaona una kiu, hamu, shauku na bidii nyingi ya kutaka kumjua Mungu, na kutafuta kuujua ukweli na hatma ya maisha yako ya milele, na maisha ya kumpendeza Bwana, hapo ndipo majaribu yanapoanza, Kumbuka kila mkristo lazima ajaribiwe imani yake, Mungu mwenyewe ndiye aliyeruhusu iwe hivyo, maana ndivyo wana wa Mungu wote walivyopitia huko nyuma.
Sasa katika hali hii, ile nguvu ya Roho Mtakatifu inakusukuma uikabili hatua inayofuata, hapo ndipo unakutana na majaribu kwa ajili ya NENO la Mungu, pengine utapitia, kuchukiwa na ndugu, kutengwa na marafiki, misiba, magonjwa, kufungwa kwa ajili ya Neno la Mungu, kudharauliwa, kuchukiwa kisa tu umeamua kuifuata hiyo imani, wakati mwingine mambo yako mengine kuharibika kwahiyo hali hii inapotokea usiogope ni IMANI yako inajaribiwa ni uthibitisho kwamba ile mbegu bado ipo safarini kuelekea kwenye udongo mzuri, usichukizwe, shika sana ulichonacho.
Bwana hatakuacha hali hii inaweza ikadumu kwa muda mrefu lakini usikate tamaa Bwana hatakuacha yupo nawe. Kumbuka jambo hili litakuja kwa yule tu mtu ambaye hatua ya kwanza ameivuka kikamilifu. lakini safari bado inaendelea.
Lakini wapo watu wengi wakifika kwenye hii hatua wanaizimisha ile nguvu ya kuendelea mbele kwa kuogopa udhia na dhiki na aibu hivyo wanakwazika na kuiacha imani, hawa ndio wale waliokwama katika miamba natamani ndugu yangu wewe usiwe hivyo. kumbuka Bwana Yesu alisema mtu yeyote akitaka kunifuata ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.
Mathayo 13:22 “Naye aliyepandwa penye miiba, huyo ndiye alisikiaye lile neno; na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno; likawa halizai. “
Shetani akishajua bado unang’ang’ana na NENO na kuzidi kutamaini kufikia utimilifu, na kumtumaini Bwana kuelekea udongo mzuri, japo kuwa unapitia dhiki, udhia, lakini bado upo na Bwana, safari hii hatumii nguvu tena, anakuja na ushawishi, na anafahamu ni mahali gani pa kumkamatia mtu na si pengine zaidi ya Tamaa ya mambo ya ulimwengu huu..hivyo atakuletea nguvu kubwa ya ushawishi ili utamani kuwa kama watu wa ulimwengu huu, kupenda kuwa mali nyingi, kuubadilisha muda wako wa kuwa karibu na Mungu na u-bize, mihangaiko, anasa, Starehe, biashara, ili tu uridhike na hali uliyopo umzimishe Roho, Hali kama hii inapokuja wewe umtazame Bwana na ahadi zake usitamani kufanana na watu wa ulimwengu huu, yeye mwenye alisema “sitakuacha wala kukupungukia kabisa” kumbuka Bwana Yesu alichokisema katika mathayo 6.
Hivyo usipunguze muda wako wa kusoma NENO, kusali, kumtafakari Mungu, kutangaza Neno la Mungu, kisa tu! ya kusongwa na mahangaiko ya maisha, bali kinyume chake uongeze muda wako na Bwana, hayo mengine yaweke kando utafute kwanza ufalme wake na haki yake na hayo mengine yote utazidishiwa.
Lakini katika hatua hii wakristo wengi ndipo waliponasiwa na mwovu, walianza vizuri lakini pesa, shughuli, mahangaiko, yamewasonga wamwache Mungu na kupoa hivyo ile Nguvu ya ROHO wa Mungu ndani yao inapoa, wanaacha kutazamia mambo ya ulimwengu ujao badala yake wanaangalia mambo ya ulimwengu huu, wakidhani katika hali yao ya uvuguvugu ya ukristo waliyopo ndiyo wanamzalia Mungu matunda kumbe bado hawajafika.
Luka 8:15 “Na zile penye udongo mzuri, ndio wale ambao kwa unyofu na wema wa mioyo yao hulisikia neno, na kulishika; kisha huzaa matunda kwa KUVUMILIA. “
Hatua hii ndipo mtu anapokamilishwa kwenye udongo mzuri ili kumzalia Mungu matunda. Kumbuka hatua hii mtu ataifikia kwa KUVUMILIA hari zote tatu zilizopita nyuma, yaani njiani,kwenye miamba, na kwenye miiba, pale mkristo anapolipokea NENO kwa uthabiti wa moyo, kila siku akiendelea kutafuta na kumjua Mungu bila kuchoka japo kuwa adui yupo njiani na majaribu yote, dhiki, udhia, shida, taabu, misiba, kuvunjwa moyo, kukatishwa tamaa, kutengwa, ukame, kufungwa, kuchukiwa kwa ajili ya Kristo, kukana mambo yote ya ulimwengu, naam hata nafsi yake mwenyewe, kwa ajili ya Bwana akizidi kuvumilia hayo yote anakuwa dhahabu iliyosafishwa kwenye moto tayari kwa kusudi na kazi ya Mungu aliyomweka duniani.
Mtu huyu anakuwa ameingia KAANANI yake, Utukufu wa Mungu unafunuliwa juu yake, ili kumzalia Bwana matunda ya haki yaliyokubaliwa. kama alivyosema huyu thelathini, huyu sitini, huyu mia, kulingana na kipimo cha neema alichopimiwa huyo mtu. Wakati huu pia Bwana anambariki kwa vitu vyake vyote alivyovipoteza kwa ajili yake mara mia zaidi kama alivyoahidi katika NENO lake. Na mtu wa namna hii anakuwa na uhusiano wa kipekee na Mungu, na kupewa nafasi za kipekee katika ufalme wa Mungu angalia akiwa hapa hapa duniani.
Kumbuka kuhubiri au kufanya kazi yoyote ya Mungu, kama haujazivuka hizi hatua NNE, hauwezi kumzalia Mungu matunda maana sasa utakuwa umepandwa kwenye udongo gani?. Yatupasa tuyashinde ndipo tumzalie Mungu matunda, kumbuka Yesu alishinda hivyo na sisi pia yatupasa tushinde. BWANA anasema
Ufunuo 3:21 “Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi. “
Hivyo ndugu tujitahidi mimi na wewe, tufikie hapo ili tumzalie Bwana wetu matunda, tujiangalie maisha yetu tujiulize je tupo katika hatua gani?. je ni njiani? au kwenye kwenye miamba,? au kwenye miiba? au kwenye udongo mzuri?. tupige mbio tuufikie utimilifu na jambo lolote lisitusonge au lisitutenge sisi na upendo wa Mungu, iwe ni njaa, dhiki, udhia, taabu, raha, uzima, mauti, lolote lile, TUZIDI KUIITI ILE NGUVU YA ROHO MTAKATIFU ITAKAYOTUFIKISHA KATIKA UDONGO MZURI. Naye Bwana ataturuzukia baraka zake tukishinda.
Mungu akubariki!
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Kwa msaada wa maombi/Ushauri/ubatizo/mafundisho/Whatsapp: Namba zetu ni hizi:
+255693036618/ +255789001312
Mada Nyinginezo:
TOFAUTI KATI YA SHERIA YA ROHO WA UZIMA NA SHERIA YA DHAMBI NA MAUTI!
SHETANI ANATOLEA WAPI FEDHA, ANGALI TUNAJUA FEDHA NA DHAHABU NI MALI YA BWANA?
Waefeso 1:20 “…….akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho; 21 juu sana kuliko UFALME WOTE, na MAMLAKA, na NGUVU, na USULTANI, na KILA JINA LITAJWALO, wala si ulimwenguni humu tu, BALI KATIKA ULE UJAO PIA; 22 AKAVITIA VITU VYOTE CHINI YA MIGUU YAKE, akamweka awe KICHWA juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo 23 ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.
Pia 1Timotheo 6:16″…..yeye aliyehimidiwa, Mwenye uweza peke yake, MFALME WA WAFALME, BWANA WA MABWANA; 16 ambaye yeye peke yake hapatikani na mauti, AMEKAA KATIKA NURU ISIYOWEZA KUKARIBIWA; wala hakuna mwanadamu aliyemwona, wala awezaye kumwona. HESHIMA NA UWEZA UNA YEYE HATA MILELE. Amina. “
Ndugu Bwana YESU KRISTO alivyokuja hapo mwanzo, sio sawa na sasa hivi alivyo, mwanzoni alikuja katika hali ya utumwa akaishi kama sisi tulivyo, lakini alijinyenyekeza akawa mtii kama maandiko yanavyosema, hivyo basi Mungu alimwadhimishia akamweka juu ya vitu vyote, kwahiyo tufahamu tu jambo moja yule sio mtu wa KAWAIDA KABISA, NI MIALE YA MOTO!!!, toa yale mawazo unayodhania kuwa ni mtu fulani wa kuchukuliwa kawaida.
Malaika wenye nguvu na wakuu wa mbingu wanatetemeka mbele yake, ameketi katika mbingu za mbingu asikoweza kufika mtu huko hata malaika!! unaweza ukatengeneza picha ni mtu wa dizaini gani huyo??..Hivyo tuwe makini sana tunapomzungumzia au tunapomtaja huyu MFALME MKUU WA KUTISHA, tuwe MAKINI, tuwe makini!!!.. sio mtu wa kawaida ni MUNGU YULE!
Wafilipi 2:7 “bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu;
8 tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.
9 Kwa hiyo tena MUNGU ALIMWADHIMISHA MNO, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;
10 ILI KWA JINA LA YESU KILA GOTI LIPIGWE, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi;
11 na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba. “
Tunaona maandiko hayo yote yanadhihirisha ukuu alionao Bwana Yesu Kristo sasa hivi, usikae ufikirie kuwa ni mtu wa kawaida kama wengi wao wanavyomwona kwenye maigizo na tamthilia. Kumbuka VITU VYOTE na SHUGHULI ZOTE za MBINGUNI, DUNIANI na KUZIMU zipo chini yake, Hakuna chochote kinachofanyika bila idhini kutoka kwake, liwe ni jambo zuri au baya.
Tena Hakuna malaika yoyote anayeweza akaamua jambo lolote kwa namna yoyote pasipo idhini yake aidha awe mbinguni au duniani, wala hakuna chochote kinachoendelea sasa hivi mbinguni kama hakitoki kwake.
Vivyo hivyo shetani naye hawezi kufanya jambo lolote dunia isipokuwa kwanza amepata idhini kutoka kwake yeye HUYO MKUU WA WAKUU(YESU KRISTO), Kumbuka shetani hajiamulii kufanya jambo lolote jinsi apendavyo, yote uyaonayo anayoyafanya karuhusiwa kuyafanya kwa kibali maalumu kutoka kwa Bwana, Na pia kuzimu hakuna mtu yeyote mwenye uwezo wa kumtoa mtu kuzimu wala kumpeleka.
Ni YESU peke yake ndiye anayewamiliki walio hai na walio kufa. yeye ndiye anayeamua aidha akupandishe juu au akushushe, shetani hana mamlaka yoyote juu ya wafu.(warumi 14:9). Mganga yoyote asikudanganye kwamba anaweza akamleta ndugu yako aliyekufa(mzimu) kuzungumza nawe, huo uwezo hana ukiona mzimu ujue ni pepo hilo limevaa sura ya huyo mtu. Uwezo huo anao MFALME TU (YESU KRISTO).
VIvyo hivyo na wanadamu wote pia hakuna mwanadamu anayeishi kwa nafsi yake mwenyewe, hakuna mamlaka inayojiamulia mambo yake tu yenyewe, kila kitu kipo chini ya utawala wa BWANA YESU KRISTO, hata wafalme waliopo leo duniani hawakuwekwa na watu bali ni MFALME MKUU(yaani YESU KRISTO) ndiye aliyewaweka kwa makusudi yake,Huwezi kufanya jambo lolote liwe baya au zuri kama halikupitishwa kwanza kwenye utawala mkuu wa Bwana YESU,
Mithali 16:3″ Mkabidhi Bwana kazi zako, Na mawazo yako yatathibitika. Bwana amefanya kila kitu kwa kusudi lake; NAAM, HATA WABAYA KWA SIKU YA UBAYA. “ ..soma pia
Maombolezo 3:37 “Ni nani asemaye neno nalo likafanyika, Ikiwa Bwana hakuliagiza? Je! Katika kinywa chake Aliye juu HAYATOKI MAOVU NA MEMA? “.
Hivi ndugu hauogopi unaposikia mambo haya yote halafu hautetemeki mbele ya hili JINA.
Vivyo hivyo hata vitu vya asili kama wanyama, ndege, samaki, milima, mimea, bahari n.k. Hivi vyote vinatetemeka na kungojea maagizo kutoka kwa Bwana YESU, na vyote vinamjua kama vile wewe unavyomjua haviwezi vikajiamulia mambo, mvua haiwezi kunyesha au nchi kuzaa kama hazijapokea amri kutoka kwa BWANA YESU KRISTO.
Na pia katika utawala unaokuja wa miaka 1000 BWANA YESU atakaposhuka kuja kutawala na watu wake hapa duniani, dunia itabadilishwa kuwa kama Edeni bahari itaondolewa, kwahiyo sehemu kubwa ya nchi kavu itaongezeka, kumbuka leo hii robo tatu ya dunia ni maji, kwahiyo bahari ikiondolewa mabara tuliyonayo leo yataongezeka mpaka kufikia 28 au zaidi unaweza ukajenga picha kutakuwaje?,
Hivyo wafalme na watawala watakuwa wengi sana kupita kiasi, dunia itajaa utukufu na ustaarabu wa hali ya juu ambao haujawahi pata kuonekana, matatizo hayatakuwepo huko, njaa, shida, umaskini na magonjwa hayatakuwepo, na YESU KRISTO ndiye atakayekuwa BWANA WA MABWANA, na MFALME WA WAFALME na kiti chake cha enzi kitakuwepo huko Yerusalemu na watu wote wa ulimwengu mzima watakusanyika kwenda kumwabudu huko.
Kama tu huu ulimwengu wa leo wenye dhambi na utawala wake, na wafalme wake unamantiki (unaonekana wa kuvutia) si zaidi huo utakaokuja? huo hauelezeki ni raha zisizo na kifani, kutakuwa na shughuli nyingi na teknolojia kubwa zinazotoka kwa Mungu ambazo kwasasa hazipo, wala haziwezi kufananishwa na hizi, wanyama na wanadamu wataishi kwa amani, watu wa Mungu watajenga na kupanda na hakuna mtu atakayebomoa au kuharibu kwasababu shetani wakati huo atakuwa amefungwa.
Kumbuka ndugu haya mamlaka yote yapo mkononi mwa Bwana YESU KRISTO. Naye aliahidi kumiliki nao wale wote watakaoshinda kama yeye alivyoshinda, soma
Ufunuo 3:20 -21″ Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. Yeye ashindaye, NITAMPA KUKETI PAMOJA NAMI KATIKA KITI CHANGU CHA ENZI, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi. “.
Hatuwezi kumiliki na Bwana haya yote kama hatutapita katika njia aliyopitia yeye. “Yohana 14:6.. Yesu akamwambia, Mimi ndimi NJIA, NA KWELI NA UZIMA; mtu haji kwa Baba, ila kwa NJIA YA MIMI. “. Hapo aliposema NJIA alikuwa anamaanisha MAISHA, na wala sio kumpokea YESU kuwa Bwana na mwokozi wako tu! bali ni maisha yako yanapaswa yapite katika ile ile NJIA ya Yesu Kristo aliyopita.
Je! Njia ya Yesu Kristo ni ipi?
Luka 9:23 “Akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, AJITWIKE MSALABA WAKE KILA SIKU, anifuate.
24 Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha.
25 Kwa kuwa yamfaa nini mtu kuupata ulimwengu wote, kama akijiangamiza, au kujipoteza mwenyewe?
26 Kwa sababu kila atakayenionea haya mimi na maneno yangu, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo, atakapokuja katika utukufu wake na wa Baba na wa malaika watakatifu.
Ishara kuu ya kukutambulisha kwamba unamfuata YESU ni MSALABA WAKO. na msalaba ni nini?. Tunajua YESU alibeba msalaba wake ikiashiria kwenda mautini. Vivyo hivyo na sisi pia tunapaswa kubeba misalaba yetu ikiashiria tunapaswa kufa kila siku kwa mambo ya ulimwengu, na pia tunakuwa tayari kufa katika mwili kwa ushuhuda wa YESU KRISTO. Kumbuka wakati YESU alipobeba msalaba wake, alipitia fedheha, alitemewa mate, aliaibishwa kwa ajili ya ushuhuda wa baba yake. kama yeye alivyopitia hiyo NJIA na sisi tunapaswa tupitie vivyo hivyo kwa ajili ya jina lake, kudharauliwa, kuchekwa, kutukanwa, kufungwa, hata kuuliwa pasipo kuuweka chini msalaba wetu. wafilipi 1:29 “Maana mmepewa kwa ajili ya Kristo, si kumwamini tu, ILA NA KUTESWA KWA AJILI YAKE;”
Kwa yeye kuwa mtii vile katika maisha yake na msalaba wake, ndipo tunaona Mungu akamwadhimisha sana kuwa juu ya vitu vyote vya mbinguni na duniani, Na kama kwa njia hiyo ya kuvumilia Baba alimpa vyote, unadhani ili na wewe uwe kama yeye utapitia NJIA nyingine yoyote tofauti na hiyo ya MSALABA??. Usidanganyike kimbia injili za mafanikio na tamaa za ulimwengu huu tu na za sifa za kutiana moyo na majigambo! yasiyoweza kumzalia mtu matunda ya wokovu, injili zinazokufanya ujione upo sawa na Mungu katika hali yako ya uvuguvugu angali ukijua moyoni mwako hata BWANA akarudi leo utabaki! kimbia ndugu.
Bwana alisema mwenyewe mtumwa sio mkubwa kuliko Bwana wake ikiwa yeye walimuita beelzebuli si zaidi watumwa wake?. Ikiwa yeye alikataliwa na viongozi wakubwa wa dini wakati ule kwa ajili ya ushuhuda wa baba yake, inakuwaje wewe unasifiwa na ulimwengu mzima?.
Jiulize! jiulize! msalaba wako ni upi? mitume wote na manabii walioifuata njia yake waliishia msalabani, au kama sio msalabani maneno yao yalikataliwa na wakuu wa dini wasiompenda Mungu. Jua tu ukienda katika njia iliyosahihi lazima upitie udhia soma..2 Timotheo 3:12 “Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa. “
Unaogopa kumkiri Kristo kwasababu unaogopa utatengwa na dhehebu lako. mwanamke unaogopa kuacha kuvaa suruali na vimini na make-up na fashion kwasababu unaogopa marafiki zako watakuonaje!. Umeujua ukweli kwamba hupaswi kuabudu sanamu, au kusujudia vinyago na dhamiri yako inakushuhudia unachofanya sio sahihi lakini kwasababu unamwogopa mama yako au baba yako au ndugu zako, unaendelea kufanya hivyo, ili usionekane mtu wa ajabu. Bwana Yesu (MFALME WA WAFALME )alisema :
Mathayo 10:32 “Basi, kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni.
33 Bali mtu ye yote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni.
34 Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; la! Sikuja kuleta amani, bali upanga.
35 Kwa maana nalikuja kumfitini mtu na babaye, na binti na mamaye, na mkwe na mkwe mtu;
36 NA ADUI ZA MTU NI WALE WA NYUMBANI MWAKE.
37 APENDAYE BABA AU MAMA KULIKO MIMI , HANISTAHILI; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.
38 WALA MTU ASIYECHUKUA MSALABA WAKE AKANIFUATA, HANISTAHILI.39 Mwenye kuiona nafsi yake ataipoteza; naye mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona. “
Je! msalaba wako ni nini katika ukristo wako??..je! ni Yesu kukufanikisha katika biashara yako au kazi yako huku ukiendelea kuwa vuguvugu? au kuponywa ugonjwa wako huku ukiendelea kuvaa nusu uchi? au kukupa familia nzuri huku ukiendelea kuabudu sanamu?..au kujitoa kikamilifu kwa Bwana na kupita katika njia yeye aliyoipitia bila kujali dunia inasema nini juu yako?. jibu unalo! maombi yangu ni sisi sote tushinde ili siku ikifika tukaketi pamoja naye katika kiti chake cha enzi kama alivyoshinda yeye. (yaani yule MFALME MKUU BWANA WETU NA MWOKOZI WETU YESU KRISTO).
SIFA NA HESHIMA NA UTUKUFU VINA YEYE MILELE NA MILELE. HALELUYA!
Mungu akubariki!.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Kwa msaada wa maombi/Ushauri/ubatizo/mafundisho/Whatsapp: Namba zetu ni hizi:
+255693036618/ +255789001312
Mada Nyinginezo:
DALILI ZIPI ZITAMTAMBULISHA MTU KUWA AMEFANYIKA KIUMBE KIPYA?
TOFAUTI KATI YA NDOTO NA MAONO NI IPI?
TUNAPOSEMA TUISHI KWA NENO, INAMAANISHA TUISHI MAISHA YA NAMNA GANI?
Dhambi ya mauti, ni ipi katika maandiko?
1Yohana 5:16 “Mtu akimwona ndugu yake anatenda dhambi isiyo ya mauti, ataomba, na Mungu atampa uzima kwa ajili ya hao watendao dhambi isiyo ya mauti.
IKO DHAMBI ILIYO YA MAUTI. Sisemi ya kwamba ataomba kwa ajili ya hiyo.Kila lisilo la haki ni dhambi, na dhambi iko isiyo ya mauti.
17 Kila lisilo la haki ni dhambi, na dhambi iko isiyo ya mauti.
Biblia inaeleza wazi kuwa kuna DHAMBI ZA MAUTI na DHAMBI ZISIZO ZA MAUTI:
Hii ni dhambi ambayo mtu akiifanya anaweza akatubu na kusamehewa, na dhambi hii ni ile inayotokana na aidha kutenda pasipo kukusudia, au inatendeka kutokana na uchanga wa kiroho, au kwa kukosa maarifa au jambo lingine lolote linaloweza kutendeka ambalo halijavuka mipaka ya neema.
Dhambi ya namna hii biblia inasema mtu anaweza akatubu au akamuungamania mwenzake na akasamehewa, akaendelea kuishi na asife. Lakini kuna dhambi mtu akiitenda hiyo hata huyo mtu aombeje, anaweza akasamehewa kosa tu lakini adhabu ya mauti ipo pale pale, je! hii dhambi inasababishwa na nini?
Namna hizi mbili tunaweza tukaona zimefananishwa na Musa na wana wa Israeli kule jangwani, Musa akiwa mfano wa “watumishi wa Mungu”, pamoja na kwamba Mungu alitembea nae kwa namna ya tofauti hata kuliko manabii wote, lakini alitenda dhambi kwa kosa kutokutii maagizo ya Mungu na kuchukua utukufu wa Mungu, alifanya vile akijua kabisa kuwa ni kosa ikampelekea kutenda DHAMBI YA MAUTI,
Musa kwa kweli alisamehewa lile kosa lakini adhabu ya mauti ilikuwa pale pale iliyomsababishia apoteze hata zile ahadi zote Mungu alizomuahidia za kuiona nchi ya Ahadi. Hata leo hii wapo watumishi wanatenda hii dhambi, wanachukua utukufu wa Mungu na kutokutii maagizo yake, inapelekea Mungu kuwaadhibu huduma zao zinakatishwa kama ilivyotokea kwa Anania na Safira walipomdanganya Roho Mtakatifu na kupokea adhabu ya kifo pale pale japo walikuwa ni watoto wa Mungu. Hizo zote ni DHAMBI ZA MAUTI.
Vivyo hivyo na wana wa israeli ni mfano kamili wa “wakristo vuguvugu” wa leo kumbuka wana wa israeli ijapokuwa waliuona utukufu wote wa Mungu, na maajabu yote na miujiza yote lakini mioyo yao haikuwa mikamilifu ijapokuwa Mungu aliwavumilia kwa muda mrefu watubu lakini hawakutaka wakaanza kuabudu sanamu, wakafanya uasherati, wakawa wakimnung’unikia Mungu na kumjaribu ikafika wakati neema ya Mungu juu yao ikakoma Mungu akaapa kwamba wote wangekufa nyikani ijapokuwa walitubu kwa kulia na kuomboleza hata hivyo hakuna hata mmoja wao aliyeiona nchi ya ahadi isipokuwa wale wana wao tu!, unaona hiyo ndiyo DHAMBI YA MAUTI.
Unajisikiaje pale ambapo unaona ungestahili kupata baraka fulani halafu unazikosa, hautakaa uzipate tena milele? fikiri juu ya hilo, na ndio maana maandiko yafuatayo yanatuonya yakisema
1 Wakorintho 10:1
Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari;
2 wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari;
3 wote wakala chakula kile kile cha roho;
4 wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo.
5 Lakini wengi sana katika wao, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani.
6 Basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya, kama wale nao walivyotamani.
7 Wala msiwe waabudu sanamu, kama wengine wao walivyokuwa; kama ilivyoandikwa, Watu waliketi kula na kunywa, kisha wakasimama wacheze.
8 Wala msifanye uasherati, kama wengine wao walivyofanya, wakaanguka siku moja watu ishirini na tatu elfu.
9 Wala tusimjaribu Bwana, kama wengine wao walivyomjaribu, wakaharibiwa na nyoka.
10 Wala msinung’unike, kama wengine wao walivyonung’unika, wakaharibiwa na mharabu.
11 Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.
12 Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke.
Mfano kamili wa kanisa la leo lililo vuguvugu kupita kiasi” linaona utukufu wa Mungu karibu kila mtu anafahamu kabisa kuwa KRISTO ni mwokozi, mponyaji, na wengi wao wamebatizwa wanaenda kanisani, wanaujua ukweli wote lakini utakuta bado mtu ni mwasherati, mlevi, mtukanaji, anaenda disco, msengenyaji, anatazama pornography, anavuta sigara, anavaa mavazi ya kiasherati n.k. angali akifahamu Mungu hapendezwi na watu wa namna hiyo. Anaiona neema ya Mungu lakini bado anaidharau mfano ule ule wa wana wa Israeli, Lakini watu kama hawa hawajui kuwa wapo hatarini kutenda DHAMBI YA MAUTI.
kama tu Mungu hakuweza kumwachilia mtumishi wake Musa kwa kosa dogo tu la kutokutii wewe unadhani utaponea wapi ikiendelea na maisha yako ya dhambi?..Ni kweli Musa alisamehema lakini adhabu ya kutokuiona nchi ya ahadi kwa njia ya Mauti ilikuwa pale pale.
Kwa namna hiyo hiyo unahubiriwa injili leo umgeukie Mungu, uache dhambi utubu usamehewe unasema hapana ngoja nile maisha nitakuja kutubu baadaye unaweza usiseme kwa mdomo lakini moyo wako unasema unaendelea kuwa mwasherati pale unapopata ugonjwa usiokuwa na matumaini mfano ukimwi unaona ndio sababu ya kumgeukia Mungu angali wakati ulipokuwa mzima hukufanya hivyo? Ni kweli ukitubu unaweza ukasemehewa lakini adhabu ya mauti ipo pale pale ndio maana utaona watu wa namna hiyo hata waombeweje hawaponi, sababu ni kwamba wameshatenda DHAMBI YA MAUTI.
Sisemi hili kwa kukutisha lakini ndio ukweli, hatuna budi kuyachunguza maisha yetu kila siku.
Mara nyingine sauti ya Mungu inakulilia uache dhambi ya ulevi na uvutaji sigara ili usafishwe maisha yako lakini unaziba masikio yako hutaki kusikia. Mungu anaruhusu pepo la Kansa linakuingia unapata kansa ya koo au mapafu au ini hapo ndipo unapoona sababu ya kumrudia Mungu ni kweli ukitubu Mungu anaweza kukusamehe lakini adhabu ya kifo ipo pale pale Kwasababu apandacho mtu ndicho atakachovuna. Mungu sio wa kumtegea kwamba niache nifanye mambo yangu kisha nikishafika mzee au wakati fulani ndipo nimgeukie, Mungu hadhihakiwi.
Madhara yake makubwa ni kwamba utapoteza thawabu yako katika ule ulimwengu ujao kwasababu umelikatisha kusudi la Mungu juu yako, ndio hapo kama Mungu alikupa huduma au anataka uwe na huduma haiwezekani tena kuendelea nayo kwasababu ulishatenda DHAMBI YA MAUTI, huna budi kuondoka nafasi yako anapewa mtu mwingine kama ilivyomtokea Yuda nafasi yake ilichukuliwa na mtu mwingine. wakati wengine wakipewa mataji yao mbinguni siku ile kwa kazi nzuri walizotaabika nazo duniani wewe utakuwa huna lolote, utabaki mtu wa kawaida milele. Hivyo ndugu, biblia inasema
1Petro 1:10 ” KWAHIYO NDUGU, JITAHIDINI ZAIDI KUFANYA IMARA KUITWA KWENU NA UTEULE WENU; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe. ” .
Itikia wito wa Mungu ulio ndani yako sasa kabla hazijaja siku zilizo mbaya utakazosema ee! Mungu wangu nisamehe nataka kuishi lakini usiweze kusikilizwa dua zako kwa upumbavu wako mwenyewe. Ndugu Tukisikia hili tuogope kwasababu imeandikwa..
Wafilipi 2:12 “Basi, wapendwa wangu, kama vile mlivyotii sikuzote, si wakati mimi nilipokuwapo tu, bali sasa zaidi sana mimi nisipokuwapo, UTIMIZENI WOKOVU WENU WENYEWE KWA KUOGOPA NA KUTETEMEKA.KWA MAANA NDIYE MUNGU ATENDAYE KAZI NDANI YENU, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema. “
AMEN!
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Kwa msaada wa maombi/Ushauri/ubatizo/mafundisho/Whatsapp: Namba zetu ni hizi:
+255693036618/ +255789001312
Mada Nyinginezo:
KUMWAMBIA MTU MWENYE DHAMBI KUWA ATAKWENDA KUZIMU ASIPOTUBU JE! NI KUHUKUMU?
Kuna tofauti kati ya MAMLAKA(CHEO) na UTAJIRI. Unaweza ukawa tajiri lakini usiwe na mamlaka au cheo na pia unaweza ukawa na CHEO na usiwe tajiri au unaweza ukawa na vyote viwili kwa pamoja. Kwamfano viongozi wenye vyeo kama wakuu wa mikoa, madiwani, mawaziri na mameya, wana nguvu na usemi juu ya watu wote pamoja na matajiri huko huko, haijalishi matajiri wana fedha kiasi gani, hiyo haiwapi wao mamlaka ya kuiamrisha nchi. Kiongozi akisema ndiyo ni ndiyo na hapana ni hapana japokuwa hao viongozi wanaweza wasiwe na mali na utajiri wowote wa kuwazidi hao matajiri wa nchi lakini wamepewa mamlaka makuu juu ya wote yaani matajiri na wasio matajiri. Lakini matajiri hawawezi wakawa na mamlaka juu ya wakuu wa nchi (Viongozi).
Vivyo hivyo katika ukristo, kuna UKUU na UTAJIRI. tutazame utajiri ni upi na ukuu ni upi;
UTAJIRI KATIKA UFALME WA MBINGUNI:
Kama tunavyofahamu utajiri unakuja kwa bidii na juhudi za mtu, kwa jinsi unavyofanya kazi sana, na kujiwekea hazina ndivyo utajiri wake unavyokuja. Na ndivyo ilivyo hata kwa Mungu utajiri katika Kristo unakuja unapokuwa mwaminifu katika kazi ya Mungu. bidii yako kuitumia karama uliyopewa katika kuhubiri, kuwavuta watu kwa Kristo, kutumika katika kanisa, kutenda wema na ukarimu, kutoa sadaka, kusaidia yatima na wajane pamoja na maskini n.k, kiufupi kazi zote njema zinazotokana na Mungu. Yote haya ni HAZINA unayojiwekea mbinguni ambao ndio huo UTAJIRI wako,
Luka 12:33 “Viuzeni mlivyo navyo, mtoe sadaka. Jifanyieni mifuko isiyochakaa, akiba isiyopungua katika mbingu, mahali pasipokaribia mwivi, wala nondo haharibu.Kwa kuwa HAZINA YENU ILIPO, ndipo itakapokuwapo na mioyo yenu. “
Unaona jinsi utoavyo sadaka ndivyo utajiri wako unavyoongezeka mbinguni.
Marko 12:41 “Naye akaketi kulielekea sanduku la hazina, akatazama jinsi mkutano watiavyo mapesa katika sanduku. Matajiri wengi wakatia mengi.
42 Akaja mwanamke mmoja, mjane, maskini, akatia senti mbili, kiasi cha nusu pesa.
43 Akawaita wanafunzi wake, akawaambia, Amin, nawaambia, Huyu mjane maskini AMETIA ZAIDI kuliko wote wanaotia katika sanduku la hazina;
44 maana hao wote walitia baadhi ya mali iliyowazidi; bali huyu katika umaskini wake AMETIA VYOTE ALIVYOKUWA NAVYO, ndiyo riziki yake yote pia. ”
Unaona tena hapo kitu cha pekee alichokuwa nacho yule mwanamke ni pale alipotoa vyote alivyo navyo kwa ajili ya BWANA, ikamfanya aonekane mbinguni kuwa mwenye utajiri mkubwa kuliko wote, nasi pia tunafundishwa tufanye hivyo sio tu pale tunapozidiwa na mali tumtolee Mungu, bali hata katika hali ya upungufu tuliyopo tumtolee Mungu vyote ili UTAJIRI wetu mbinguni uwe mkubwa.
UKUU KATIKA UFALME WA MBINGUNI:
Tukisoma..
Mathayo 18:1 “Saa ile wanafunzi wakamwendea Yesu wakisema,
2 Ni nani basi aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni? Akaita mtoto mmoja, akamweka katikati yao,
3 akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa KAMA VITOTO, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.
4 Basi, YE YOTE AJINYENYEKESHAYE MWENYEWE KAMA MTOTO HUYU, huyo ndiye aliye MKUU katika ufalme wa mbinguni.”
Wengi wanadhani unapohubiri injili, au unapotoa sadaka sana, au unapotumika kanisani sana kunakufanya wewe kuwa MKUU mbinguni hapana huko kote ni kukuongezea utajiri(HAZINA) yako mbinguni lakini sio kukupa wewe UKUU au MAMLAKA, Kama tulivyotangulia kusema mtu anaweza akawa na mamlaka na asiwe tajiri, au anaweza akawa na vyote kwa pamoja na ndivyo ilivyo hata kwa Mungu, UKUU au UKUBWA, au MAMLAKA unakuja kwa njia moja tu. Biblia inaiita “KUJINYENYEKEZA NA KUWA MDOGO KULIKO WOTE KATIKA KRISTO” Kwa mfano wa mtoto mdogo Hilo tu!.
Na kujinyenyekeza huku kunakuja kwa namna mbili..
1.Unyenyekevu kwa MUNGU.
Bwana Yesu alituambia tuwatazame watoto wadogo, kwasababu watoto wadogo siku zote wanaweka tegemeo lao lote kwa Baba zao kwa kila kitu kwa chakula,afya,malazi,mavazi n.k., wao ni kama kondoo pasipo wazazi wao hawawezi kufanya lolote, wanapoadhibiwa ni wepesi kubadilika na hawana kinyongo, kichwa cha mtoto mdogo ni chepesi kujifunza kuliko cha mtu mzima kwasababu yupo tayari siku zote kukubali kusikia, mtoto mdogo ni mtii, na anaamini lolote atakaloambiwa na wakubwa zake bila kushukushuku, Na ndivyo Bwana Yesu alivyokuwa kwa BABA yake tunasoma kila mahali alikuwa anamtaja BABA, BABA, BABA,ikiashiria pasipo BABA yake hawezi kufanya lolote soma Yohana 5:19″Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda; kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vile vile. “..Unaona hapo jinsi YESU alivyojinyenyekesha chini ya mapenzi ya baba yake na kuwa mtii hata MUNGU akamfanya kuwa mkubwa kuliko vitu vyote vya mbinguni na duniani.
Wafilipi 2:8 “tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, ALIJINYENYEKEZA AKAWA MTII HATA MAUTI, naam, mauti ya msalaba.
9 Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;
10 ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi;
11 na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba. “
Na sisi vivyo hivyo tunapaswa tujinyenyekeze chini ya BABA yetu wa mbinguni mfano wa MTOTO-na-BABA yake. mapenzi yetu yafe lakini ya Mungu yatimizwe maishani mwetu.Hii ndiyo sadaka ya kwanza mtu anaweza akamtolea Mungu yenye kumpendeza. Kumbuka BWANA YESU alishuhudiwa na BABA kwanza kuwa AMEMPENDEZA kabla hata hajaanza kuhubiri injili au kufanya kazi ya Mungu.(mathayo 4). Hii ni namna ya kwanza na ya pili ni;
2.Kujinyenyekeza chini ya ndugu (wakristo).
Bwana Yesu aliwaeleza wanafunzi wake,atakayetaka kuwa mkubwa kati yenu na awe mdogo kuliko wote, kama yeye alivyokuwa mdogo kuliko wote. YESU alimnyenyekea BABA pamoja na wanadamu Vivyo hivyo na sisi pia sio tu kumtii Mungu halafi tunawadharau ndugu zetu, na kujifanya sisi ni KITU fulani cha kipekee zaidi ya wao. tunapaswa tujishushe tuwatumikie wenzetu mfano ule ule wa YESU KRISTO hata kufikia kiwango cha kuona nafsi ya ndugu yako ni bora kuliko ya kwako. Tusome..
Marko 10:42 “Yesu akawaita, akawaambia, Mwajua ya kuwa wale wanaohesabiwa kuwa wakuu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha.
43 Lakini haitakuwa hivyo kwenu; BALI MTU ATAKAYETAKA KUWA MKUBWA KWENU, ATAKUWA MTUMISHI WENU,
44 NA MTU ANAYETAKA KUWA WA KWANZA WENU, ATAKUWA MTUMWA WA WOTE.45 Kwa maana Mwana wa Adamu naye hakuja kutumikiwa, bali kutumika, NA KUTOA NAFSI YAKE IWE FIDIA YA WENGI.”
Mahali pengine Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake.
Mathayo 11:11 ” Amin, nawaambieni, Hajaondokea mtu katika wazao wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji; walakini ALIYE MDOGO KATIKA UFALME WA MBINGUNI ni MKUU kuliko yeye. “
Hii ikiwa na maana kuwa yule ANAYEJINYENYEKEZA (KWA MUNGU na KWA WANADAMU) na KUWA MDOGO, Huyo ndiye aliye MKUU kuliko Yohana mbatizaji,.Unaweza ukaona ni faida gani aliyonayo mtu yule ajishushaye kama mtoto mdogo halafu anakuwa mkubwa kuliko hata manabii mfano wa Yohana Mbatizaji na wote waliomtangulia kabla yake.
Katika utawala unaokuja huko mbele wa milele, Kristo akiwa kama MFALME WA WAFALME, atatwaa wafalme wengine hao ndio watakaoitawala dunia wakati huo milele, sasa hizi nafasi za wafalme hawatapewa wale MATAJIRI WA ROHO bali wale WAKUU WA ROHO. Hawa wakuu watakuwa na amri, na usemi kwa kila kitu na kila kiumbe duniani kitakuwa chini yao kwasababu watakuwa wamepewa hayo na MKUU WA WAKUU (YESU KRISTO), Biblia inasema wataichunga dunia kwa fimbo ya chuma,(Ufunuo 2:26 Na yeye ashindaye, na kuyatunza matendo yangu hata mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa, naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, kama vyombo vya mfinyanzi vipondwavyo, kama mimi nami nilivyopokea kwa Baba yangu. Nami nitampa ile nyota ya asubuhi. )… watakuwa wenye mataji mengi kama leo hii tu huwezi kuwakaribia hawa wafalme wa dunia ambao sio kitu itakuwaje kwa wale?? watakuwa ni miale ya moto kama BWANA MWENYEWE.
Vivyo hivyo na MATAJIRI watapewa heshima yao, watamiliki hazina nyingi, watakuwa na HESHIMA katika ulimwengu kama tu vile matajiri wa ulimwengu huu wanavyoheshimika sasa, chochote watakachotaka watapata, kwasababu walijiwekea HAZINA nyingi mbinguni, kuna viwango vya umiliki watafikia wewe usiye na kitu hutaweza kufika.
Bwana mwenye haki atamlipa kila mtu kwa kadri ya alichokipanda ulimwenguni. Kumbuka wapo pia watakaokuwa MATAJIRI NA WAKUU kwa pamoja. Hao ndio wale waliojinyenyekeza na kumtumikia Mungu kwa bidii na kwa moyo, waliitangaza injili, walikuwa watumishi kati ya ndugu, watakatifu, waaminifu katika karama walizopewa, walikuwa kama vitoto vidogo mbele za MUNGU, walikuwa na mapenzi yao wenyewe lakini wakayakataa na kuyakubali mapenzi ya MUNGU maishani mwao, katika mapito yao yote hawakumnung’unikia, walitii na kumwamini pasipo majadiliano kama tu mtoto na baba yake mfano wa BWANA WETU YESU KRISTO.
Kwahiyo ndugu tuutafute UKUU na UTAJIRI WA MBINGUNI. lakini zaidi UKUU ambao kwa huo tu ndio utakaokuleta karibu na Mungu.
Ufunuo 3:19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.
20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.
21 Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi. “
Mungu akubariki.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
Neno la Mungu linasema pale tulipo dhaifu ndipo tulipo na nguvu, ikiwa na maana pale tunapokuwa si kitu ndipo tunapoonekana kuwa kitu mbele za Mungu, Bwana Yesu alisema yeye ajishushaye atakwezwa na ajikwezaye atashushwa, pale tunapokataa akili zetu kututawala na kumwachia Mungu azitawale ndipo tutakapofungua mlango na wigo mpana wa kuuona UWEZA wa Mungu zaidi katika maisha yetu.
Na ndio maana mtume Paulo alisema
2Wakoritho 12:9-10″ Naye akaniambia neema yangu yakutosha; maana UWEZA WANGU HUTIMILIKA KATIKA UDHAIFU. Basi najisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili UWEZA WA KRISTO ukae juu yangu.Kwahiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha, na shida kwa ajili ya Kristo. MAANA NIWAPO DHAIFU NDIPO NILIPO NA NGUVU.”
Mungu hawezi akawa ni mponyaji kwetu kama hatujawa na madhaifu (mwenye afya haitaji tabibu),mafarisayo na masadukayo YESU alikuwa hana maana kwao kwasababu wao walijiona kuwa wana afya hivyo hawakufaidiwa chochote na uweza wa Mungu katika Yesu Kristo. Kwa kawaida huwa tunashukuru pale tunapotendewa mahitaji yetu, huwezi ukashukuru au ukaomba kama unayo mahitaji yako yote.
Na pia hauwezi kutegemea kama unao uwezo wa kujitegemea. vivyo hivyo na kwa Mungu wetu ili tuweze kuuona UWEZA WAKE, yatupasa tuwe dhaifu mbele zake kwa namna zote, kiasi cha kwamba tujione pasipo yeye sisi hatuwezi lolote. Kwa jinsi tutakavyojiachia kwake kwa kila kitu ndipo tutakapofungua wigo wa yeye kutuhudumia sisi na kuuona uweza wake,
Watoto wa Mungu wamefananishwa na kondoo na sio mbuzi kwasababu kondoo hawezi akajiongoza mwenyewe huwa anamtegemea mchungaji wake kwa kila kitu tofauti na mbuzi wao wana uwezo wa kwenda kujichunga wenyewe hivyo hawahitaji msaada mkubwa sana kutoka kwa mchungaji. Vivyo hivyo Na mtoto mdogo anahudumiwa kwa kila kitu na wazazi wake ikiwemo malazi, chakula, afya, n.k. kwasababu anaonekana dhaifu kwa wazazi wake pasipo wao hawezi kufanya lolote hivyo uweza mkubwa wa wazazi wake unaonekana juu yake,
Kwa jinsi hiyo hiyo na sisi pia tunapaswa tuwe hivyo kwa Baba yetu wa mbinguni, sisi ni watoto kwake tunapaswa tujinyenyekeze kama vitoto vichanga ili tuone uweza wake katika maisha yetu, kumbuka yule mtoto anapojifanya amekua na kutaka kujiamulia mambo yake mwenyewe ndipo kidogo kidogo anapojiachilia kutoka katika mikono ya wazazi wake na uweza wao unavyozidi kupungua juu yake, mpaka inafikia wakati mzazi hana sehemu yoyote kwa mtoto.
Biblia inasema “Mkaribieni Mungu naye atawakaribia”(Yakobo 4:8). hii ikiwa na maana kwa kiwango kile kile tutakachompa Mungu katika maisha yetu, ndicho atakachokitumia kufanya kazi katika maisha yetu. Kama unampa Mungu Jumapili kwa jumapili na yeye atajifunua kwako hiyo hiyo jumapili kwa jumapili, kama ni mwezi kwa mwezi na ndivyo hivyo atakavyojifunua kwako mwezi kwa mwezi, lakini kama ni siku kwa siku ndivyo utakavyomwona siku kwa siku, kwa kiwango kile kile utakachopima ndicho utakachopimiwa biblia imesema.
Kama umempa Mungu asilimia 20 ya maisha yako ayatawale ataonekana kwako katika hiyo asilimia 20 usitegemee zaidi ya hapo, kama umempa 70% ataonekana katika hiyo 70, kama umempa 100% ataonekana katika hiyo 100% kama Bwana YESU alivyompa Baba yake. Maana uweza wa Mungu unatimilika katika udhaifu na udhaifu huu ni pale unapokataa kuzitegemea akili zako na kuwa kama mtoto mchanga mbele zake.
Nakumbuka kipindi cha nyuma zamani kidogo tulikuwa tumepanga chumba sehemu fulani na kila mwisho wa mwezi tulikuwa na desturi ya kulipia bill ya umeme lakini ilifika wakati fulani hatukupata pesa ya kulipia na hatukuwa na chochote mfukoni lakini tulimwamini Mungu na kumwachia yote, tukasema kama Mungu wetu yupo atatupigania, maana hao wadai pesa za umeme ni watu wakorofi ukipitisha tu siku moja haujalipia ni balaa umelianzisha, lakini ulipofika mwisho wa mwezi hatukuwa na chochote mfukoni,
cha ajabu wale wadai-umeme hawakuja siku hiyo kudai pesa ya umeme na sio desturi yao, vyumba vingine vyote walienda kulipa kilikuwa kimebaki chumba chetu tu! lakini ni kama walipigwa upofu hivi hawakuja, ukaingia mwezi mwingine, tarehe 1,2,3……mpaka tarehe 24 tulikuwa bado hatujalipa deni la mwezi uliopita na kweli hela hatukuwa nayo na umeme tunaendelea kutumia lakini tulimwachia Mungu yote tulisema liwalo na liwe hatutamkopa mtu,
nakumbuka siku hiyo hiyo pia gesi ya kupikia iliisha kwahiyo matatizo yakaongezeka, lakini ilipofika tarehe 25 mida ya jioni huku tukiwa na mawazo tulifungua simu tukakuta sh.48,000 kwenye mpesa hatukujua imetoka wapi, haijatumwa na mtu yoyote, wala hakuna jina wala message ya kuonyesha mtu katuma pesa, ni kama vile iliongezeka katika account ya m-pesa. tukaenda kuitoa jioni ile ile cha ajabu saa hiyo hiyo baada ya kuitoa hiyo pesa wale wadai-umeme wakafika na ghadhabu wanataka pesa yao ya umeme ya mwezi uliopita, tukawapa saa ile ile, sh.15,000 kiasi kilichobaki tulinunua gesi na matumizi mengine.. Bwana amekuwa akituonekania sisi watoto wake kwa namna hii mara nyingi tu na kwa njia nyingi.
Lakini tungesema tujiongeze tukakope pesa hakika uweza wa Mungu tusingeuona maana yeye anasema zaburi 46:1″ Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, MSAADA UTAKAOONEKANA TELE WAKATI WA MATESO.” pale tutapokuwa dhaifu na kumwachia yeye ndipo tutakapouona uweza wa Mungu, wana waisraeli wasiongeweza kuona bahari inagawanyika kama wasingekutana na kizuizi cha bahari, wasingekula mana kama wasingepita jangwani, wasingepasuliwa maji miambani kama wasingekuwa na kiu, Hivyo pale unapomkabidhi Mungu mambo yote atawale katika misukosuko pasipo kutafuta njia mbadala ya akili zako, ndipo uweza wa Mungu utakapoonekana.
Vivyo hivyo unapopitia shida fulani, au unapoumwa, au tatizo fulani haraka haraka usikimbilie kutafuta njia mbadala, usianze kutangatanga jua hiyo ndio fursa ya wewe kuuona uweza wa Mungu na ndio yeye anataka iwe hivyo, ndio ni vizuri kwenda hospitali na sio dhambi kwenda hospitali lakini sio kila ugonjwa kukimbilia hospitali ukifanya hivyo uweza wa Mungu utauonaje?,
Naweza nikakupa mfano ulifikia wakati nilikuwa nikipata ugonjwa kidogo nakimbilia dawa lakini ilifika wakati nikasema nataka nimuone Mungu katika maisha yangu, yeye aniponye pasipo kumtegemea mwanadamu wala dawa, nikasema sitameza kidonge cha aina yoyote wala kwenda hospitali, tangu niseme hivyo hadi sasa ni miaka mingi imepita sijawahi kumeza kidonge wala kwenda hospitali, kila ninaposikia hali ya udhaifu ndani yangu, nasema Bwana ndiye daktari wangu ataniponya na kweli ile hali haidumu baada ya muda mfupi narudia hali yangu ya kawaida, kwa kufanya hivyo uweza wa Mungu nauona ndani ya maisha yangu kila siku.
Na kwako wewe ndugu unaweza ukasema mbona sijawahi kumwona Mungu akinifanyia miujiza katika maisha yangu? ni kwasababu wewe mwenyewe hujaruhusu atende kazi ndani yako. haujataka kuwa dhaifu mbele zake kwa kujishusha kuwa kama mtoto,.jambo fulani limetokea chukua iwe ndio fursa ya wewe kumwona Mungu wako usitegemee akili zako, wala mwanadamu wala kitu chochote,mwachie yeye na utauona utukufu wake kila siku.
Hiyo ndio njia pekee itakayokufanya uone UWEZA WA MUNGU maishani mwako na ndio njia Paulo aliyoinena na kuiishi iliyomfanya amwone Mungu siku baada ya siku katika huduma yake. kwa mfano shedraki, Meshaki na Abednego walipohukumiwa kutupwa katika tanuru la moto hawakusita walimwachia Mungu yote na kwa kufanya hivyo waliweza kukutana na Mungu kule na kupelekea Mungu wao kutukuzwa babeli yote, vivyo hivyo na Danieli pia alipotupwa katika tundu la simba aliuona uweza wa Mungu kule, tukiwaangalia pia akina Paulo na Sila walipotupwa gerezani ndipo walipouona uweza wa Mungu pale malaika wa Mungu alipoitetemesha ardhi na kufungua malango ya gereza. Hawa wote ni kwasababu walikubali kuwa wadhaifu kwa ajili ya Bwana hivyo ikawafanya wauone utukufu mkubwa wa Mungu.
Mithali 3:5-6 ” Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zake mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye naye atanyosha mapito yako.”
Amen!
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Kwa msaada wa maombi/Ushauri/ubatizo/mafundisho/Whatsapp: Namba zetu ni hizi:
+255693036618/ +255789001312
Mada Nyinginezo:
NITASHINDAJE HALI YA KUUMIZWA NA MANENO YA WATU!
MADHARA YA DHAMBI YA UASHERATI
KWANINI MUNGU AWACHOME WATU KWENYE ZIWA LA MOTO NA HALI YEYE NDIYE ALIYEWAUMBA?
Karibu tuongeze maarifa katika Neno la Mungu,
Tukisoma kwenye biblia kitabu cha warumi 4 tunaona mtume Paulo anasisitiza kuwa mtu hahesabiwi haki mbele za Mungu kwa matendo yake bali kwa Imani, lakini tukisoma tena katika kitabu cha Yakobo 2, Yakobo anasisitiza kuwa mtu hahesabiwi haki kwa Imani tu, bali pia na kwa matendo. Tunaona sentensi hizi mbili zinaonekana kama kupingana, Lakini je! Biblia kweli inajipinga au ni sisi uelewa wetu ndio unaojipinga??..tuichambue mistari hii miwili kwa undani kidogo..
“1 Basi, tusemeje juu ya Ibrahimu, baba yetu kwa jinsi ya mwili?
2 KWA MAANA IKIWA IBRAHIMU ALIHESABIWA HAKI KWA AJILI YA MATENDO YAKE, ANALO LA KUJISIFIA, LAKINI SI MBELE ZA MUNGU.3 Maana maandiko yasemaje? Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa haki.
4 Lakini kwa mtu afanyaye kazi, ujira wake hauhesabiwi kuwa ni neema, bali kuwa ni deni.
5 Lakini kwa mtu asiyefanya kazi, bali anamwamini yeye ambaye amhesabia haki asiyekuwa mtauwa, imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki.
6 Kama vile Daudi anenavyo uheri wake mtu yule ambaye Mungu amhesabia kuwa na haki pasipo matendo,.
Ni dhahiri kuwa hapa mtume Paulo alipokuwa anazungumzia MATENDO, alikuwa analenga matendo yatokanayo na sheria ya kwamba hakuna mwanadamu yoyote anaweza akasimama mbele za Mungu kwa matendo yake kuwa ni mema au amestahili kumkaribia Mungu.
Kwa mfano mtu kusema nimestahili kwenda mbinguni kwa matendo yangu mazuri, mimi sio mwasherati, sio mwizi, sio mtukanaji, sio mlevi, sio mwongo, sio mwuuaji n.k. kwa kusimamia vigezo kama hivyo hakuonekana hata mmoja aliyeweza kumpendeza Mungu isipokuwa mmoja tu naye ni BWANA wetu YESU KRISTO! wengine wote kama biblia inavyotaja kuanzia Adamu mpaka mwanadamu wa mwisho atakayekuja duniani Mungu alishawaona wote tangu mwanzo kuwa wamepungukiwa na utukufu wake,
Warumi 3:23″ kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; “
na ukisoma pia Zaburi 14:2-3 inasema
“ Toka mbinguni Bwana aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu.Wote wamepotoka, wameoza wote pamoja, Hakuna atendaye mema, La! Hata mmoja.”
Hivyo hii inadhihirisha kabisa hakuna hata mmoja atapata kibali mbele za Mungu kwa matendo yake mazuri.
Lakini swali ni je! kama sio kwa matendo, basi mtu atapata kibali mbele za Mungu kwa njia gani tena??..
Ukiendelea kusoma mbele tunasoma mtume Paulo anasema ni kwa njia moja tu tunaweza kuhesabiwa haki mbele za Mungu nayo ni njia ya kumwamini BWANA YESU KRISTO tu!. Ndio njia pekee inayotupa sisi kupata kibali mbele za Mungu, kwa namna hiyo basi tunayo haki ya kuwa na uzima wa milele, kwenda mbinguni, kubarikiwa kwasababu tumemwamini mwana wa Mungu YESU KRISTO na sio kwa matendo mema tuyatendayo.
Kumbuka zipo dini nyingi zenye watu ambao wanatenda matendo mema lakini je! wanao uzima wa milele ndani yao? utakuta ni wema kweli wanatoa zaka, wanasaidia maskini, sio waasherati, sio walevi n.k. lakini bado Mungu hawatambui hao. Lakini sababu ni moja tu, hawajamwamini mwana wa Mungu ili aziondoe dhambi zao.
Kwahiyo tunaona hapo jambo kuu Mungu analolitazama ni wewe kumwamini mwana wa Mungu, na ukishamwamini (yaani kumpa maisha yako) ndipo ROHO wake MTAKATIFU anakutakasa na kukufanya uishi maisha matakatifu ya kumpendeza.
“21 JE! BABA YETU IBRAHIMU HAKUHESABIWA KUWA ANA HAKI KWA MATENDO, hapo alipomtoa Isaka mwanawe juu ya madhabahu?
22 Waona kwamba imani ilitenda kazi pamoja na matendo yake, na ya kwamba imani ile ilikamilishwa kwa njia ya matendo yale.
23 Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa ni haki; naye aliitwa rafiki wa Mungu.
24 Mwaona kwamba mwanadamu huhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo yake; si kwa imani peke yake.
25 Vivyo hivyo na Rahabu, yule kahaba naye, je! Hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipowakaribisha wajumbe, akawatoa nje kwa njia nyingine?
26 Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa.
Katika kifungu kile cha kwanza ukiangalia kwa undani utaona kuwa mtume Paulo alikuwa anazungumzia juu ya MATENDO YATOKANAYO NA SHERIA. Lakini hapa Yakobo hazungumzii habari ya matendo yatokanayo na sheria bali ni MATENDO YATOKANAYO NA IMANI.. hivyo ni vitu viwili tofauti.
MFANO WA MATENDO YATOKANAYO NA IMANI:
Kwamfano: Mtu amepimwa na daktari na kuambiwa kuwa anaugonjwa wa kisukari, na hatakiwi kula vyakula vyenye asili ya sukari na wanga. lakini mtu yule akilishikilia lile Neno kwenye biblia Mathayo 8:17 linalosema ” ….Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu. ”
Na kuliamini na kuamua kuchukua hatua na kusema mimi ni mzima na sio mgonjwa kwasababu yeye alishayatwaa madhaifu yetu, na kusimama na kutembea kama mtu mzima asiyeumwa na kula vyakula vyote hata vya sukari na wanga ingawa daktari alimkataza, akiamini kuwa amepona kwa NENO lile atapokea uponyaji wake. sasa kitendo cha yeye kuchukua hatua ya kuishi kama mtu mzima ambaye haumwi japo ni mgonjwa na kula vile vyakula alivyoambiwa asile hicho ndicho kinachoitwa MATENDO YA IMANI Yakobo aliyoyazungumzia..
Unaona hapo haki ya huyo mtu kuponywa haikutokana na matendo ya sheria (yaani utakatifu, kutokuwa mwasherati, au mlevi au mwizi n.k.). bali ni matendo yaliyotakana na kumwamini YESU KRISTO katika NENO lake ndio yaliyomponya. Na ndio jambo hilo hilo lililomtokea Ibrahimu pale alipomwamini Mungu na kumtoa mwanae kuwa dhabihu, kwahiyo kile kitendo cha yeye kumtoa mwanawe hayo ndiyo MATENDO yanayozungumziwa na Yakobo YA IMANI kwasababu hiyo basi ikampelekea yeye kupata haki mbele za Mungu.
Unaona hapo haikuwa sababu ya yeye kutokuwa mwongo, au mlevi, au muuaji n.k. ndio kulimpa haki yeye ya kubarikiwa hapana bali ni kumwamini Mungu na kuiweka ile imani katika matendo. Kwasababu kama ingekuwa kwa usafi wake Mtume Paulo asingesema Ibrahimu hana la kujisifu mbele za Mungu.
Vivyo hivyo kwa mambo mengine yote kwamfano haki ya kuzungumza na Mungu, haki ya kuponywa magonjwa, haki ya kubarikiwa, haki ya kwenda mbinguni, haki ya karama za rohoni, haki ya kuwa mrithi, n.k. havitokani na MATENDO YA SHERIA bali MATENDO YA IMANI. Kwa sisi kumwamini YESU KRISTO katika Neno lake ndipo tunapopata vyote.
Kwahiyo matendo yote mema ya sheria yanakuja baada ya kuwa ndani ya Kristo na hayo ndiyo yanayokupa uhakika kama upo ndani ya Kristo, ni kweli huwezi ukawa ni mkristo halafu bado ni mlevi, mwasherati, mwongo, mwizi n.k.. lakini jua katika hayo mtu hahesabiwi haki mbele za Mungu kama tukitaka tuhesabiwe katika hayo hakuna mtu atakayesimama mbele za Mungu.
Kumbuka Ibilisi anawinda IMANI yetu kwa Bwana pale tunapoiweka katika matendo na sio kingine, tunasamehewa dhambi kwa imani, tunaponywa kwa imani, maombi yetu yanajibiwa kwa imani, kila jambo tunapokea kwa Mungu kwa IMANI IPATIKANAYO KATIKA NENO LAKE.
Lakini shetani anaenda kinyume kukufanya udhani utasamehewa dhambi kwasababu unashika amri kumi, au kwa kufunga na kuomba sana ndio utapata haki ya kuponywa, n.k. Bwana amesema Waebrania 10:38 ” Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye. “
Wagalatia 2:16 ” hali tukijua ya kuwa mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria, bali kwa imani ya Kristo Yesu; sisi tulimwamini Kristo Yesu ili tuhesabiwe haki kwa imani ya Kristo, wala si kwa matendo ya sheria; maana kwa matendo ya sheria hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki. “
Waefeso 2:8-9 “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. “
Bwana akubariki.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
+255693036618/ +255789001312
Mada Nyinginezo:
TOFAUTI KATI YA SHERIA YA ROHO WA UZIMA NA SHERIA YA DHAMBI NA MAUTI!
KUWAHUDUMIA MALAIKA PASIPO KUJUA
KUNA TOFAUTI GANI KATI YA SALA NA DUA?
Kumbukumbu 22:5″ Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako”.
Na bado Isitoshe BWANA anawapelekea watu wake kuwaonya lakini bado wanadhihaki na kuziba masikio yako wasisikie
Warumi 1:18-28″ Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu.
Kwa kuwa mambo ya Mungu yanayojulikana yamekuwa dhahiri ndani yao, kwa maana Mungu aliwadhihirishia.
Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake; hata wasiwe na udhuru; kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza.
Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika;…….Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao. Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo,………………
Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili;
wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao. Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.
Tunahitaji uthibitisho gani tena kuwa tunaishi katika siku za mwisho nyakati za hatari kama hizi?? JE! umeokolewa,..umempa KRISTO maisha yako? umeoupokea ujumbe wa wakati huu aliouleta Mungu kupitia mjumbe wake ndugu William Marrion Branham wa kanisa la saba na la mwisho ?.
Kama hujafanya hivyo ndugu ni vema ukamgeukia BWANA kabla mlango haujafungwa…
Mungu akubariki.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Kwa msaada wa maombi/Ushauri/ubatizo/mafundisho/Whatsapp: Namba zetu ni hizi:
+255693036618/ +255789001312
Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
Mada Nyinginezo:
JE! KUFANYA MASTURBATION (PUNYETO) NI DHAMBI?
Pale Edeni Mungu alimweka Adamu na Hawa, Na kwa muda wote waliokuwepo bustanini Biblia inatuambia walikuwa UCHI na hawakujitambua kuwa wako vile, lakini baada ya dhambi kuingia ndipo walipojijua kuwa wapo uchi. Hii ina maana gani?.
Hapo mwanzo Mungu alipowaumba Mungu aliwawekea “UTAJI MTAKATIFU” katika macho yao ambao ungewafanya wasijue dhambi na ule utaji ulikuwa si kingine bali ni ROHO MTAKATIFU. Lakini tunajua walipoasi ule utaji ukaondoka hivyo Mungu akaamua kuwafanyia mavazi ya ngozi ili kuwasitiri.
Lakini Shetani naye tangu ule wakati alianza kutengeneza EDENI yake kidogo kidogo, awarudishe watu katika kuwa UCHI tena na kuwavua mavazi ambayo Mungu aliwavisha.
Takribani Miaka elfu sita sasa tangu Adamu kuumbwa imepita na shetani amekuwa akiimarisha hii edeni yake kwa kuwatia watu “UTAJI WAKE MCHAFU” wa kuwafanya watu waishi na wasijione kuwa wako uchi na wenye dhambi. Hii ni hatari sana.
Miaka ya zamani kwa kweli mwanamke kutembea amevaa suruali barabarani alikuwa anajulikana kama KAHABA, Lakini sasa hivi zimekuwa ni nguo rasmi kuendea kila mahali mpaka kwenye nyumba za ibada, na sasa imevuka zaidi ya hapo vimini na nguo zinazoonyesha maungo yote wazi ni jambo la kawaida kuliona na hata haliwashangazi watu tena..Huoni kama ni “UTAJI” wa shetani huo umewavaa watu hata pasipo wao kujua??. na wanaume pia wanaonyesha maumbile yao wakiwa na nguo za ndani tu!. Leo hii wanaume na wanawake wanatembea uchi wa mnyama barabarani pasipo aibu yoyote.
Edeni hii ya shetani inaanzia katika roho. Tunaona kanisa la kwanza lililoanza na Mitume lilikuwa na ule UTAJI wa ROHO MTAKATIFU, Ikiwa na maana kazi zake zote zilitendeka katika uvuvio wa Roho wa Mungu na usafi lakini sasa hivi katika kanisa hili la mwisho tunaloishi ule utaji wote umeondoka kilichobakia ni utaji wa shetani unaomfanya mtu awe VUGUVUGU na asijijue,
Utakuta mwanamke anaingia kanisani nusu uchi na asijione kuwa yupo uchi, mwanamume ni mzinzi lakini anajiona yeye yupo sawa tu mbele za Mungu, mtu ni mlevi na anajiona yeye ni mkristo aliyesafi, mwanaume anafuga rasta na kujiona hana hatia, utakuta mkristo anaabudu sanamu na asione shida yoyote angali biblia inasema usijifanyie sanamu ya kuchonga usiisujudie wala kuiabudu, mtu kaokoka ni msengenyaji na hata hasikii kuhukumiwa nafsini mwake juu ya hilo analolifanya.n.k.
Ni dhahiri kabisa tunaishi katika kanisa la mwisho linaloitwa, LAODIKIA na ujumbe wetu tuliopewa na BWANA ni huu..
Ufunuo 3:14 “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.
15 Nayajua matendo yako, YA KUWA HU BARIDI WALA HU MOTO; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.
16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.
17 KWA KUWA WASEMA, MIMI NI TAJIRI, NIMEJITAJIRISHA, WALA SINA HAJA YA KITU; NAWE HUJUI YA KUWA WEWE U MNYONGE, MWENYE MASHAKA, NA MASKINI, NA KIPOFU NA UCHI.
18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.
19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.
20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.
21 Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.
22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. “
Kama unavyoona sisi tunaambiwa tunajiona kuwa ni matajiri kumbe ni maskini na tu “UCHI”
Ni uthibitisho kabisa kuwa huu ni UTAJI WA SHETANI umelifunika kanisa hili la mwisho. Tunaishi nyakati za hatari tubu. mpokee ROHO MTAKATIFU huo ndio muhuri wa Mungu utakaotuokoa sisi katika kizazi hichi cha mwisho. kumbuka pasipo Roho Mtakatifu hakuna unyakuo, Umeamua kumfuata Bwana mfuate kweli kweli na kama umeamua kumfuata shetani mfuate kweli kweli usiwe vuguvugu.
Tazama video chini, ujionee mwenyewe ulimwengu tunaoishi ulipofikia na jinsi Edeni hi ya shetani ilipofikia ili ujue tunaishi katika nyakati za hatari watu kutembea uchi barabarani si ajabu tena..Na kama vile shetani alivyoiharibu Edeni ya Mungu vivyo hivyo na ya kwake imeandaliwa kwa ajili ya uharibifu ambao upo karibu kutokea.
Mungu akubariki.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
Kwa msaada wa maombi/Ushauri/ubatizo/mafundisho/Whatsapp: Namba zetu ni hizi:
+255693036618/ +255789001312
Mada Nyinginezo:
AGENDA KUBWA YA SHETANI KWA KANISA HILI LA LAODIKIA.
NAMNA YA KUITAMBUA SAUTI YA MUNGU
BWANA YESU ALIMAANISHA NINI PALE ALIPOSEMA “MKONO WAKO UKIKUKOSESHA UKATE?
Siku zote roho ya mwanadamu imejawa na KIU ya mambo mengi yahusuyo mema, kwa mfano KIU ya kupata FURAHA, kiu ya kuwa na AMANI, kiu ya UZIMA USIOKOMA,kiu ya kuwa na UPENDO kiu ya KUTENDA MEMA, kiu ya kutaka UTAKATIFU, kiu ya kuwa MNYENYEKEVU na MVUMILIVU, kiu ya KUWA NA RAHA, kiu ya KUWA KARIBU NA MUNGU ..n.k..
Lakini wengi wanatafuta njia za kuzikata kiu hizi kwa njia nyingi tofauti tofauti za kibinadamu. wengine wanatafuta RAHA kwa kufanya anasa, wengine wanatafuta AMANI kwa kunywa pombe, wengine wanatafuta FURAHA kwa kupata mali, wengine wanatafuta UZIMA WA MILELE kwa waganga na wapiga ramli, wengine wanatafuta UPENDO kwa kulaghai, wengine wanatafuta UHURU kwa kuua n.k..
Lakini ni dhahiri kuwa njia zote hizo ni batili, yaani aidha hazikati kabisa au zinakata kiu kwa muda tu! baada ya hapo tatizo linarudi palepale..Lakini kuna habari njema, ya mmoja tu anayeweza kuikata kiu yako moja kwa moja isikuwepo tena naye si mwingine zaidi ya BWANA YESU.
Kwa yeye utapata Raha nafsini mwako, furaha isiyokoma, amani, upendo, unyenyekevu, upole, utakatifu, kujua kumcha Mungu, na uzima wa milele n.k..Hivyo nakushauri Mkaribishe moyoni mwako na hakika ataikata KIU yako, usiipuuzie sauti yake ikuitapo . kwa maana maandiko yanasema:
Yohana 7:37-38 “Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, YESU akasimama, akapaza sauti yake akisema, MTU AKIONA KIU, NA AJE KWANGU ANYWE. Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake”.
Yohana 4:13-14 “Yesu akajibu, akamwambia, Kila anywaye maji haya ataona kiu tena; walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele.
Mungu akubariki.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Kwa msaada wa maombi/Ushauri/ubatizo/mafundisho/Whatsapp: Namba zetu ni hizi:
+255693036618/ +255789001312
Mada Nyinginezo:
MANENO YA MUNGU YANAPINDULIWAJE?
NI RAHISI KWA NGAMIA KUPENYA KATIKA TUNDU LA SINDANO, JE! NI SINDANO IPI HIYO INAYOZUNGUMZIWA?
JE! MABALASI BWANA ALIYOYATUMIA KUGEUZIA MAJI KUWA DIVAI, YALITUMIKA TU KWA KAZI HIYO?
Tangu kipindi cha Bwana Wetu Yesu Kristo kuondoka duniani mpaka sasa imepita miaka takribani elfu mbili na katika hichi kipindi cha miaka hii elfu mbili kanisa limekuwa likipitia katika vipindi tofauti tofauti saba vinavyoitwa NYAKATI SABA ZA KANISA, kulingana na kitabu cha..
Ufunuo 1:12-20″ Nikageuka niione ile sauti iliyosema nami. Na nilipogeuka, niliona vinara vya taa saba vya dhahabu;
13 na katikati ya vile vinara nikaona mtu mfano wa Mwanadamu, amevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa mshipi wa dhahabu matitini.
14 Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe, kama theluji; na macho yake kama mwali wa moto;
15 na miguu yake kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti yake kama sauti ya maji mengi.
16 Naye alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kuume; na upanga mkali, wenye makali kuwili, ukitoka katika kinywa chake; na uso wake kama jua liking’aa kwa nguvu zake.
17 Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,
18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.
19 Basi, uyaandike mambo hayo uliyoyaona, nayo yaliyopo, na yale yatakayokuwa baada ya hayo.
20 Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na ya vile vinara saba vya dhahabu. Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba; na vile vinara saba ni makanisa saba.
Ufunuo huu alipewa Yohana na Bwana Yesu alipokuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, akionyeshwa jinsi kanisa litakavyokuja kupitia katika siku za mwisho. Leo hii si rahisi sana kuona kitabu cha ufunuo kikiguswa au kuelezewa katika kanisa, na shetani hataki watu wafahamu siri zilizoandikwa katika hiki kitabu maana ndio kinaelezea hatma ya mambo yote ikiwemo na shetani mwenyewe. Kwahiyo ndugu fungua moyo wako ujifunze na Mungu akusaidie unapoenda kusoma ujue ni wakati gani tunaishi na jinsi Bwana Yesu alivyo mlangoni kurudi kuliko hata unavyoweza kufikiri. Tafadhali pitia taratibu mpaka mwisho ili uelewe.
Kanisa: Efeso
Malaika/Mjumbe: MTUME PAULO
kipindi cha kanisa: 53AD -170AD
Tabia ya kanisa: limeacha upendo wake wa kwanza,tangu wakati wa mauaji ya wakristo yaliyoongozwa na Nero mtawala wa Rumi hadi kifo cha mtume Yohana. Na kipindi hiki ndipo matendo ya wanikolai yalianza kuingia katika kanisa (mafundisho ya kipagani). kuanza kujichanga na ukristo. ufunuo 2:1-7
onyo kwa kanisa- litubu lirudi katika upendo wake wa kwanza, lililopoteza.
Thawabu: Yeye ashindaye atapewa kula matunda ya mti wa uzima ulio katika bustani ya Mungu.
Kanisa; Smirna
Malaika/Mjumbe;IRENIUS
kipindi cha kanisa: 170AD -312 AD
Tabia ya kanisa; Ni kanisa lilopitia dhiki nyingi kutoka katika utawala mkali wa Diocletian wa Rumi , watakatifu wengi waliuawa katika hichi kipindi kuliko kipindi chochote katika historia ya kanisa.walichinjwa wengi, na wengine kutupwa kwenye matundu ya simba na wanawake kukatwa matiti na kuachwa mbwa walambe damu zao, na ukatili mwingi sana wakristo walitendewa katika hichi kipindi lakini walistahimili dhiki zote hizi soma kitabu cha (Foxe’s book of Martyr- kwenye archives zetu kinaelezea vizuri mauaji ya wakristo). Japo wakristo walikuwa maskini sana Lakini Kristo aliwafariji kuwa wao ni Matajiri. ufunuo 2:8-11
Thawabu; Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.
Kanisa ; Pergamo
Malaika/Mjumbe; MARTIN
Kipindi; 312AD -606AD
Tabia ya kanisa; Kanisa laingiliwa na mafundisho ya uongo zaidi, ambayo ndio yale matendo ya wanikolai sasa wakati huu yamegeuka kuwa mafundisho ya kidini. Ukristo ukaoana na upagani ukazaa Kanisa mama mfu Katoliki, katika baraza la Nikea AD 325 siasa na mafundisho ya miungu mitatu,ibada za sanamu na za wafu,sherehe na sikukuu za kipagani, ubatizo wa Jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, vyeo vya upapa n.k ndipo vilipochipukia. kwa mambo haya basi ikasababisha kanisa kuingia katika kipindi kirefu cha giza (Dark age). Ufunuo 2:12-17
Onyo kwa kanisa: litubu lirudi katika imani iliyoanzishwa na mitume wa Kristo
Thawabu; Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu, ila yeye anayelipokea.
Kanisa; Thiatira
Malaika/Mjumbe;COLUMBA
Kipindi; 606AD -1520AD
Tabia ya kanisa; Japo kanisa lilikuwa na juhudi na bidii katika kumtafuta Mungu, lakini bado lilikuwa na mafundisho ya yule mwanamke kahaba Yezebeli yaani mafundisho ya Kanisa Katoliki.
Onyo; Litubu litoke katika mafundisho ya wanikolai. Ufunuo 2:18-29
Thawabu;Yeye ashindaye na kuyatunza matendo yangu hata mwisho nitampa mamlaka juu ya mataifa, naye atawachunga kwa fimbo ya chuma.
Kanisa; Sardi
Malaika/Mjumbe; MARTIN LUTHER
kipindi; 1520AD -1750AD
Tabia; Ni kanisa lililokuwa linarudi katika matengenezo kutoka katika mafundisho ya yule kahaba mkuu kanisa katoliki. lakini lilikuwa bado na Jina lililokufa, wakishikilia baadhi ya mafundisho ya kanisa mama katoliki, huku ndiko chimbuko la walutheri lilipoanzia.Ufunuo 3:1-6
Onyo: litubu, lirejee kwenye mafundisho ya mitume.
Thawabu; Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri Jina lake mbele za baba yangu na mbele ya malaika zake.
Kanisa;Filadelfia
Malaika/Mjumbe; JOHN WESLEY
Kipindi; 1750AD -1906AD
Tabia; Ni kanisa lililosifiwa kwa matendo yake mema, lilifanikiwa kujua na kuyarekebisha mafundisho ya uongo Kristo alisema ”tazama nakupa walio wa sinagogi la shetani wasemao kwamba ni wayahudi nao sio, bali wasema uongo, tazama nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda”.ufunuo 3:7-13
Thawabu;Yeye ashindaye nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu, huo Yesalemu mpya ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe lile jipya.
Kanisa; Laodikia
Mjumbe;WILLIAM BRANHAM
Kipindi;1906- Unyakuo
Tabia; Ni kanisa ambalo sio baridi wala moto, bali ni vuguvugu, Kristo anasema ni heri lingekuwa moto au baridi, hii ndiyo hali ya kanisa tunaloishi sasa mimi na wewe, uvuguvugu mbaya umeingia katika kanisa, watu wanajiona kuwa wanamwabudu Mungu katika uzuri wao wa majengo ya kanisa, kwaya na injili ya mafanikio, wakidhani kuwa hivyo yatosha tu kumjua Mungu kumbe hawajui wameshaingia katika udanganyifu wa shetani pasipo wao kujua, watu wanasema kuwa wanampenda Mungu na bado wanapenda mambo ya ulimwengu huu kama fashion za mitindo ya kisasa wanawake kuvalia mavazi ya nusu uchi, michezo, miziki, muvi, ponography, ulevi. anasa,uasherati,na shughuli za ulimwengu huu ambazo zinawasonga wengi hususani kwa kizazi hichi cha ubize, watu wanapata muda wa kufanya kazi sana, lakini muda wa kumtolea Mungu hawana na bado ni wakristo., huu ndio uvuguvugu Kristo anaouzungumzia kwa kanisa letu la Laodikia.Hapa Kristo anasema unajiona kuwa tajiri kumbe ni maskini na mnyonge na uchi na unamashaka na kipofu, jiulize ni hali gani ya kanisa tulilopo sasa.
Na hakutakuwa na kanisa lingine baada ya hili, na ndio linakaribia kuisha. jiulize umejiwekaje tayari kumpokea Bwana Yesu akirudi mara ya pili?. Mungu alimtuma mjumbe wake ndugu William Branham kulionya kanisa letu lirudi katika NENO na imani iliyohubiriwa na mitume pamoja na utakatifu.
Onyo; Kristo anasema kanisa liwe na bidii likatubu na kumgeukia Mungu.
Thawabu;Yeye ashindaye nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na baba yangu katika kiti chake cha enzi. ufunuo 3:14-22
Watu wa Mungu hili ndilo kanisa la mwisho tunaloishi hakutakuwa na kanisa lingine baada ya hapa, tunaishi katika wakati ambao Kristo yupo mlangoni kulichukua kanisa lake teule, JIULIZE! UMEKWISHA KUJIWEKA TAYARI KUMLAKI BWANA, TAA YAKO INAWAKA??UMEMPOKEA ROHO MTAKATIFU??YEYE ALIYE NA SIKIO, NA ALISIKIE NENO HILI AMBALO ROHO AYAAMBIA MAKANISA.
Mungu akubariki
MARAN ATHA!
Kwa msaada wa maombi/Ushauri/ubatizo/mafundisho/Whatsapp: Namba zetu ni hizi:
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
+255693036618/ +255789001312
Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
Mada Nyinginezo
VIPINDI VINNE VYA MAISHA VILIVYO VIGUMU MTU KUMKUMBUKA MUUMBA WAKE.