Title June 2019

MFALME ANAKUJA.

Watu wengi wanadhani makao ya watakatifu yatakuwa ni mbinguni milele, yani siku ile ya mwisho dunia itakunjwa kunjwa na kutupwa motoni, halafu sisi tutakwenda kuishi na Mungu mbinguni milele, Ni wazi kuwa jambo hilo sio la kimaandiko kabisa, Biblia inatufundisha kuwa tutakaa mbinguni miaka saba tu! Kisha tutarudi kutawala na KRISTO hapa duniani Milele.

Mungu alivyotuumba sisi wanadamu ni tofauti kabisa na alivyowaumba malaika, Utukufu Mungu aliouweka kwetu sisi, haufanani na ule wa malaika zake, Sisi tumeumbiwa miili, sisi tumeumbiwa kumiliki, sisi tumeumbiwa kutawala, na hivyo tutamwabudu Mungu katika njia hiyo hiyo. tofauti na malaika, Ndio maana Adamu mtu wa kwanza alishushwa hapa duniani, ili kutimiliza hayo makusudi. Alishushiwa mbingu yake hapa chini.

Lakini alipoasi ndipo alipofanya dunia ionekane kuwa sio sehemu ya kutamaniwa tena kuishi kwa watu, lakini ashukuriwe Mungu, vitu vyote vitakuja kurejeshwa katika uhalisia wake moja ya hizi siku.

Biblia inaposema Dunia inapita na tamaa zake zote (1Yohana 2:17), Haimaanishi kuwa Dunia itateketezwa na kuondolewa kabisa hapana bali Inaamisha kuwa Ulimwengu huu uliopo ndio unaopita na ndio utakaoteketezwa, mambo yote tunayoyaona, falme zote unazoziona, shughuli zote unazoziona na tunazozifanya, ustaarabu wote uliopo duniani leo hii, serikali zote na mamlaka yote hakuna hata mmoja kitakachosalia, vyote hivi vitaondoshwa kupisha majira mengine kuanza. Na ndio maana tunaambiwa tuishi kama wapitaji, kwasababu vitu tunavyovisumbukia havituwekei kumbukumbu la milele.

Leo hii unaipenda dunia, unapenda kuwa na maisha mazuri, unapenda kufanikiwa na kuwa tajiri na ndio maana unatafuta mali kwa nguvu zote, Unafanya hivyo ni ili uishi maisha mazuri na ya raha hapa duniani. Ni wazi kuwa hakuna mtu ambaye anaufurahia umaskini, kila mmoja anatamani awe na mafanikio makubwa, na hiyo ndiyo inayombidiisha afanye kazi kwa bidii. Lakini jifunze pia kukaa chini kutafakari nini kusudi la maisha, usiishi tu kama mnyama, hutaki kujua umetokea wapi na unakwenda wapi, badala yake unajitaabisha sana kujitashirisha.. mwisho wa siku unakuwa kama Yule mtu Bwana aliyemtolea mfano baada ya kufanikiwa sana kwa shughuli zake, sasa anatulia ili aiburudishe nafsi yake, lakini usiku ule ule waliitaka nafsi yake.

Ndipo Bwana akasema na zile mali alizozisumbukia zitakuwa za nani?(Luka 12:16) Unaona, ni muhimu kujua maisha unayopitia leo iwe ni katika vingi au katika vichache je! inafunua nini katika ulimwengu wa roho?.

Sasa Mungu karuhusu tuyaonje hayo, kama kivuli cha huo ufalme mwingine mkuu sana utakaokuja huko mbeleni. Kwamba watu hawatakuwa sawasawa kutakuwa na matajiri sana na vilevile kutakuwa na watu wa kawaida sana. Ufalme huo ambao utashuka hapa mara baada ya siku ile kuu ya Bwana kupita duniani, Yesu atakapotokea katika mawingu pamoja na watakatifu wake aliokuwa amewanyakua zamani, sasa wakati huo dunia itakuwa imeshasafishwa, na shetani ameshafungwa kwenye lile shimo la kuzimu kwa muda wa miaka 1000, dunia kuanzia huo wakati itakuwa Paradiso kama hapo mwanzo, Ustaarabu mpya wa kimbinguni utaanza kutenda kazi duniani, YESU KRISTO akiwa kama Mfalme wa wafalme, na Bwana wa Mabwana, ikimaanisha kuwa atakuwa na wafalme wengi sana chini yake na mabwana wengi sana chini yake, na makuhani wengi sana chini yake, ili kutumiza pamoja nao kazi ya ufalme wa Mungu Baba.(Ufunuo 1:6)

Nafasi hizo hazitakuwa za kila mtakatifu, hapana bali kila mmoja atalipiwa kulingana na matendo yake na taabu yake hapa duniani, kama wewe maisha yako yote yalikuwa ni ya ulevi, mpaka uzee wako ndio unamrudia Bwana, ukifika kule hutakuwa sawa na Mtume Paulo. Maisha tunayoishi sasa kwa Kristo ndio yanayotuleza kule tutakuwa nani.

Wakati huo ukifika kutakuwa na majuto mengi sio tu kwa watu waliokufa katika dhambi, hapana bali pia kwa watakatifu wakijutia kwanini hawakufanya zaidi kwa kujiwekea hazina katika huo ufalme wa milele wa Yesu Kristo utakaoshuka duniani.

Sasa kutakuwa na shughuli nyingi sana, na mambo mengi sana yatakayokuwa yanaendelea kule, na tunasoma baadaye hizi bahari zote zitakuja kuondolewa, leo hii ni 21% tu ya dunia inakaliwa na wanadamu sehemu nyingine zote ni maji na pamoja na hayo bado haijajazwa, sasa wakati huo habari hazitakuwepo Eneo la makazi ya watu litaongeza na haya mabara basi yatakuwa si chini ya 30, leo hii yapo 7 tu,na kote huko kutakuwa ni miji mikubwa, na makazi yaliyobuniwa mbinguni. kutakuwa hakuna magonjwa wala laana, wala wachawi, wala ajali, tutumwabudu Mungu katika makazi hayo milele na milele.

Kwa mambo makuu yote hayo utajisikiaje unakuwa mtu wa kawaida kule milele?, Ukitaka kufahamu vizuri utakuwa katika hali gani jijengee picha sasahivi, katika hali uliyopo, ujifananishe labda na Raisi, au Waziri, au mtu Fulani aliye na mali nyingi, uone tofauti yake na yako jinsi ilivyo kubwa, mambo mengi unavyoyakosa ndivyo itakavyokuwa kule, tofauti tu ya huku na kule, ni kwamba huku unaishi bado katikati ya hatari na shida na bado ni kwa kipindi kifupi tu, lakini kule Ukiwa umepewa mamlaka na YESU ni mamlaka ya milele na milele isiyokuwa na mwisho, hakutakuwa na kupandishwa cheo wala kushushwa cheo,Karama za Mungu hazina majuto…Ni afadhali tukose kila kitu hapa, lakini kule tukapate kila kitu.

Na ndio maana tunashauriwa tukiwa hapa duniani tuukomboe wakati, kwa kutafuta kujua mapenzi ya Mungu hasa ni nini kwetu. kwa jinsi ile ile tunavyohangaika kutafuta mambo ya ulimwengu huu, ni wakati sasa wa kupeleka nguvu zetu nyingi zaidi kutafuta mambo ya ufalme wa mbinguni unaokuja wa milele wa Yesu Kristo Bwana wetu …Kwasababu huko ndiko ndio kuna maisha. Haleluya.

Kumpa Yesu maisha yetu tu haitoshi, ni lazima tufanye na kitu cha ziada, safari ndio inaanza…tujiwekee hazina kule, kwa kufanya mapenzi ya Mungu na kuitenda kazi yake kwa uaminifu. Bwana anasema hivi.

Ufunuo 22:10 “Akaniambia, Usiyatie muhuri maneno ya unabii wa kitabu hiki, kwa maana wakati huo umekaribia.

11 Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa.

12 TAZAMA, NAJA UPESI, NA UJIRA WANGU U PAMOJA NAMI, KUMLIPA KILA MTU KAMA KAZI YAKE ILIVYO.

13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.”

Napenda umalizie kwa kusoma habari hii, kisha sasa uanze kuchukua hatua kuanzia leo….

Luka 19:12 “Basi akasema, Mtu mmoja, kabaila, alisafiri kwenda nchi ya mbali, ili ajipatie ufalme na kurudi.

13 Akaita watu kumi katika watumwa wake, akawapa mafungu kumi ya fedha, akawaambia, Fanyeni biashara hata nitakapokuja.

14 Lakini watu wa mji wake walimchukia, wakatuma wajumbe kumfuata na kusema, Hatumtaki huyu atutawale.

15 Ikawa aliporudi, ameupata ufalme wake, aliamuru waitwe wale watumwa aliowapa fedha, ili ajue faida aliyopata kila mtu kwa biashara yake.

16 Akaja wa kwanza, akasema, Bwana, fungu lako limeleta faida ya mafungu kumi zaidi.

17 Akamwambia, Vema, mtumwa mwema; kwa vile ulivyokuwa mwaminifu katika neno lililo dogo, uwe na mamlaka juu ya miji kumi.

18 Akaja wa pili, akasema, Bwana, fungu lako limeleta mafungu matano faida.

19 Akamwambia huyu naye, Wewe uwe juu ya miji mitano.

20 Akaja mwingine akasema, Bwana, hili ndilo fungu lako, ambalo nililiweka akiba katika leso.

21 Kwa maana nilikuogopa kwa kuwa u mtu mgumu; waondoa usichoweka, wavuna usichopanda.

22 Akamwambia, Nitakuhukumu kwa kinywa chako, mtumwa mwovu wewe. Ulinijua kuwa ni mtu mgumu, niondoaye nisichoweka, na kuvuna nisichopanda;

23 basi, mbona hukuiweka fedha yangu kwa watoao riba, ili nijapo niipate pamoja na faida yake?

24 Akawaambia waliosimama karibu, Mnyang’anyeni hilo fungu, mkampe yule mwenye mafungu kumi.

25 Wakamwambia, Bwana, anayo mafungu kumi.

26 Nawaambia, Kila aliye na kitu atapewa, bali yule asiye na kitu atanyang’anywa hata alicho nacho.”

Mfalme anakuja.

Ubarikiwe sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

SIKU ZA MAPATILIZO.

MFANO ULE YESU ALIOUTOA WA KABAILA ALIYESAFIRI KATIKA NCHI YA MBALI, UNA MAANA GANI (LUKA 19:12-27)?

UTAWALA WA MIAKA 1000.

NI KWELI MTU ANAWEZA AKAFA LAKINI ROHO YAKE IKAWA INATUMIKA KAMA MSUKULE (KUMILIKIWA NA MTU FULANI KWA WAKATI) MAHALI PENGINE?


Rudi Nyumbani

Print this post

MFALME ANAKUJA.


Watu wengi wanadhani makao ya watakatifu yatakuwa ni mbinguni milele, yani siku ile ya mwisho dunia itakunjwa kunjwa na kutupwa motoni, halafu sisi tutakwenda kuishi na Mungu mbinguni milele, Ni wazi kuwa jambo hilo sio la kimaandiko kabisa, Biblia inatufundisha kuwa tutakaa mbinguni miaka saba tu! Kisha tutarudi kutawala na KRISTO hapa duniani Milele.

Mungu alivyotuumba sisi wanadamu ni tofauti kabisa na alivyowaumba malaika, Utukufu Mungu aliouweka kwetu sisi, haufanani na ule wa malaika zake, Sisi tumeumbiwa miili, sisi tumeumbiwa kumiliki, sisi tumeumbiwa kutawala, na hivyo tutamwabudu Mungu katika njia hiyo hiyo. tofauti na malaika, Ndio maana Adamu mtu wa kwanza alishushwa hapa duniani, ili kutimiliza hayo makusudi. Alishushiwa mbingu yake hapa chini.

Lakini alipoasi ndipo alipofanya dunia ionekane kuwa sio sehemu ya kutamaniwa tena kuishi kwa watu, lakini ashukuriwe Mungu, vitu vyote vitakuja kurejeshwa katika uhalisia wake moja ya hizi siku.

Biblia inaposema Dunia inapita na tamaa zake zote (1Yohana 2:17), Haimaanishi kuwa Dunia itateketezwa na kuondolewa kabisa hapana bali Inaamisha kuwa Ulimwengu huu uliopo ndio unaopita na ndio utakaoteketezwa, mambo yote tunayoyaona, falme zote unazoziona, shughuli zote unazoziona na tunazozifanya, ustaarabu wote uliopo duniani leo hii, serikali zote na mamlaka yote hakuna hata mmoja kitakachosalia, vyote hivi vitaondoshwa kupisha majira mengine kuanza. Na ndio maana tunaambiwa tuishi kama wapitaji, kwasababu vitu tunavyovisumbukia havituwekei kumbukumbu la milele.

Leo hii unaipenda dunia, unapenda kuwa na maisha mazuri, unapenda kufanikiwa na kuwa tajiri na ndio maana unatafuta mali kwa nguvu zote, Unafanya hivyo ni ili uishi maisha mazuri na ya raha hapa duniani. Ni wazi kuwa hakuna mtu ambaye anaufurahia umaskini, kila mmoja anatamani awe na mafanikio makubwa, na hiyo ndiyo inayombidiisha afanye kazi kwa bidii. Lakini jifunze pia kukaa chini kutafakari nini kusudi la maisha, usiishi tu kama mnyama, hutaki kujua umetokea wapi na unakwenda wapi, badala yake unajitaabisha sana kujitashirisha.. mwisho wa siku unakuwa kama Yule mtu Bwana aliyemtolea mfano baada ya kufanikiwa sana kwa shughuli zake, sasa anatulia ili aiburudishe nafsi yake, lakini usiku ule ule waliitaka nafsi yake.

Ndipo Bwana akasema na zile mali alizozisumbukia zitakuwa za nani?(Luka 12:16) Unaona, ni muhimu kujua maisha unayopitia leo iwe ni katika vingi au katika vichache je! inafunua nini katika ulimwengu wa roho?.

Sasa Mungu karuhusu tuyaonje hayo, kama kivuli cha huo ufalme mwingine mkuu sana utakaokuja huko mbeleni. Kwamba watu hawatakuwa sawasawa kutakuwa na matajiri sana na vilevile kutakuwa na watu wa kawaida sana. Ufalme huo ambao utashuka hapa mara baada ya siku ile kuu ya Bwana kupita duniani, Yesu atakapotokea katika mawingu pamoja na watakatifu wake aliokuwa amewanyakua zamani, sasa wakati huo dunia itakuwa imeshasafishwa, na shetani ameshafungwa kwenye lile shimo la kuzimu kwa muda wa miaka 1000, dunia kuanzia huo wakati itakuwa Paradiso kama hapo mwanzo, Ustaarabu mpya wa kimbinguni utaanza kutenda kazi duniani, YESU KRISTO akiwa kama Mfalme wa wafalme, na Bwana wa Mabwana, ikimaanisha kuwa atakuwa na wafalme wengi sana chini yake na mabwana wengi sana chini yake, na makuhani wengi sana chini yake, ili kutumiza pamoja nao kazi ya ufalme wa Mungu Baba.(Ufunuo 1:6)

Nafasi hizo hazitakuwa za kila mtakatifu, hapana bali kila mmoja atalipiwa kulingana na matendo yake na taabu yake hapa duniani, kama wewe maisha yako yote yalikuwa ni ya ulevi, mpaka uzee wako ndio unamrudia Bwana, ukifika kule hutakuwa sawa na Mtume Paulo. Maisha tunayoishi sasa kwa Kristo ndio yanayotuleza kule tutakuwa nani.

Wakati huo ukifika kutakuwa na majuto mengi sio tu kwa watu waliokufa katika dhambi, hapana bali pia kwa watakatifu wakijutia kwanini hawakufanya zaidi kwa kujiwekea hazina katika huo ufalme wa milele wa Yesu Kristo utakaoshuka duniani.

Sasa kutakuwa na shughuli nyingi sana, na mambo mengi sana yatakayokuwa yanaendelea kule, na tunasoma baadaye hizi bahari zote zitakuja kuondolewa, leo hii ni 21% tu ya dunia inakaliwa na wanadamu sehemu nyingine zote ni maji na pamoja na hayo bado haijajazwa, sasa wakati huo habari hazitakuwepo Eneo la makazi ya watu litaongeza na haya mabara basi yatakuwa si chini ya 30, leo hii yapo 7 tu,na kote huko kutakuwa ni miji mikubwa, na makazi yaliyobuniwa mbinguni. kutakuwa hakuna magonjwa wala laana, wala wachawi, wala ajali, tutumwabudu Mungu katika makazi hayo milele na milele.

Kwa mambo makuu yote hayo utajisikiaje unakuwa mtu wa kawaida kule milele?, Ukitaka kufahamu vizuri utakuwa katika hali gani jijengee picha sasahivi, katika hali uliyopo, ujifananishe labda na Raisi, au Waziri, au mtu Fulani aliye na mali nyingi, uone tofauti yake na yako jinsi ilivyo kubwa, mambo mengi unavyoyakosa ndivyo itakavyokuwa kule, tofauti tu ya huku na kule, ni kwamba huku unaishi bado katikati ya hatari na shida na bado ni kwa kipindi kifupi tu, lakini kule Ukiwa umepewa mamlaka na YESU ni mamlaka ya milele na milele isiyokuwa na mwisho, hakutakuwa na kupandishwa cheo wala kushushwa cheo,Karama za Mungu hazina majuto…Ni afadhali tukose kila kitu hapa, lakini kule tukapate kila kitu.

Na ndio maana tunashauriwa tukiwa hapa duniani tuukomboe wakati, kwa kutafuta kujua mapenzi ya Mungu hasa ni nini kwetu. kwa jinsi ile ile tunavyohangaika kutafuta mambo ya ulimwengu huu, ni wakati sasa wa kupeleka nguvu zetu nyingi zaidi kutafuta mambo ya ufalme wa mbinguni unaokuja wa milele wa Yesu Kristo Bwana wetu …Kwasababu huko ndiko ndio kuna maisha. Haleluya.

Kumpa Yesu maisha yetu tu haitoshi, ni lazima tufanye na kitu cha ziada, safari ndio inaanza…tujiwekee hazina kule, kwa kufanya mapenzi ya Mungu na kuitenda kazi yake kwa uaminifu. Bwana anasema hivi.

Ufunuo 22:10 “Akaniambia, Usiyatie muhuri maneno ya unabii wa kitabu hiki, kwa maana wakati huo umekaribia.

11 Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa.

12 TAZAMA, NAJA UPESI, NA UJIRA WANGU U PAMOJA NAMI, KUMLIPA KILA MTU KAMA KAZI YAKE ILIVYO.

13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.”

Napenda umalizie kwa kusoma habari hii, kisha sasa uanze kuchukua hatua kuanzia leo….

Luka 19:12 “Basi akasema, Mtu mmoja, kabaila, alisafiri kwenda nchi ya mbali, ili ajipatie ufalme na kurudi.

13 Akaita watu kumi katika watumwa wake, akawapa mafungu kumi ya fedha, akawaambia, Fanyeni biashara hata nitakapokuja.

14 Lakini watu wa mji wake walimchukia, wakatuma wajumbe kumfuata na kusema, Hatumtaki huyu atutawale.

15 Ikawa aliporudi, ameupata ufalme wake, aliamuru waitwe wale watumwa aliowapa fedha, ili ajue faida aliyopata kila mtu kwa biashara yake.

16 Akaja wa kwanza, akasema, Bwana, fungu lako limeleta faida ya mafungu kumi zaidi.

17 Akamwambia, Vema, mtumwa mwema; kwa vile ulivyokuwa mwaminifu katika neno lililo dogo, uwe na mamlaka juu ya miji kumi.

18 Akaja wa pili, akasema, Bwana, fungu lako limeleta mafungu matano faida.

19 Akamwambia huyu naye, Wewe uwe juu ya miji mitano.

20 Akaja mwingine akasema, Bwana, hili ndilo fungu lako, ambalo nililiweka akiba katika leso.

21 Kwa maana nilikuogopa kwa kuwa u mtu mgumu; waondoa usichoweka, wavuna usichopanda.

22 Akamwambia, Nitakuhukumu kwa kinywa chako, mtumwa mwovu wewe. Ulinijua kuwa ni mtu mgumu, niondoaye nisichoweka, na kuvuna nisichopanda;

23 basi, mbona hukuiweka fedha yangu kwa watoao riba, ili nijapo niipate pamoja na faida yake?

24 Akawaambia waliosimama karibu, Mnyang’anyeni hilo fungu, mkampe yule mwenye mafungu kumi.

25 Wakamwambia, Bwana, anayo mafungu kumi.

26 Nawaambia, Kila aliye na kitu atapewa, bali yule asiye na kitu atanyang’anywa hata alicho nacho.”

Mfalme anakuja.

Ubarikiwe sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Print this post

SHUKURU KWA KILA JAMBO.

Shalom, mtu wa Mungu karibu tujifunze Neno la Mungu, Taa iongozayo miguu yetu..na mwangaza wa njia zetu…

Leo tutajifunza juu ya Kumshukuru Mungu kwa kila jambo…

Kwanini tunapaswa tumshukuru Mungu kwa kila jambo? Jibu ni rahisi kwasababu hatukukaa naye kikao cha yeye kutuumba sisi…tumejikuta tumetokea tu ulimwenguni, kwahiyo lolote lijalo mbele yetu sio sisi tulilolitengeneza bali ni yeye, na hatukumpa yeye kitu hata atakapokitwaa tumwulize kwanini anafanya hivyo (Ayubu 41:11)…kwahiyo tuna sababu zote za kumshukuru kwa mambo yoyote yatakayotokea mbele yetu yawe ni mazuri au mabaya…

Wakati mwingine Mungu anaruhusu maovu yaje juu yetu kama gharika… kama ilivyokuwa kwa Ayubu, wakati mwingine Mungu anaruhusu mambo hayo kwasababu zake yeye ambazo sio lazima wakati mwingine akuambie ni kwanini…Lakini unapaswa ushukuru.

Kama Biblia inavyotuambia katika 1 Wathesalonike 5:16 “ Furahini siku zote; ombeni bila kukoma; SHUKURUNI KWA KILA JAMBO; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu”.

Hata tukipitia misiba tushukuru? ndio..hata tukifilisika tushukuru? jibu ni NDIO?..Hata tukiwa katika magonjwa tushukuru? jibu ni NDIO…Kwasababu hayo ndio mapenzi ya Mungu.

Kitu ambacho wengi wetu hatujui ni kuwa…Mungu anaweza kuleta pia UOVU au UBAYA juu ya watu wake…haijalishi huo ubaya utatekelezwa na shetani, au malaika au mwanadamu…lakini Ana uwezo wa kuleta Ubaya juu ya mtu ambaye hata anayeupendeza moyo wake kabisa kwa kusudi Fulani…

Biblia inasema katika…Maombolezo 3:37 “Ni nani asemaye neno nalo likafanyika, Ikiwa Bwana hakuliagiza? 38 Je! Katika kinywa chake Aliye juu Hayatoki MAOVU NA MEMA?”

Unaona? Sio mema tu yanatoka kwake hata maovu…lakini Maovu anayoyaleta juu ya watu wake sio ya kuwaangusha bali kuwapa tumaini katika siku zao za mwisho(Yeremia 29:11)..Haleluya!..Bwana atajeruhi lakini ataponya! Ataangusha chini lakini atanyanyua! Ataua lakini atahuisha, Atafukarisha lakini atatajirisha N.k

1 Samweli 2:6 “Bwana huua, naye hufanya kuwa hai; Hushusha hata kuzimu, tena huleta juu. Bwana hufukarisha mtu, naye hutajirisha; Hushusha chini, tena huinua juu.”

Hosea 6:1 “Njoni, tumrudie Bwana; maana yeye amerarua, na yeye atatuponya; yeye amepiga, na yeye atatufunga jeraha zetu.

2 Baada ya siku mbili atatufufua; siku ya tatu atatuinua, nasi tutaishi mbele zake.”

Kwahiyo kuna umuhimu mkubwa sana wa kutomnung’unikia Mungu pale jambo Fulani baya linapokuja juu yako…kinyume chake mshukuru kwasababu anakuwazia yaliyo mema katika siku zako za mwisho..Na pia kumbuka kuwa hakuna mwanadamu awezaye kumwuliza Mungu kwanini unafanya hivi au kwanini unafanya vile, au kwanini unaruhusu hili, au kwanini unaruhusu lile,…Kila kitu anafanya kama apendavyo. Na pia hatukuja na chochote hivyo hata vikichukuliwa vyote hatuna sababu ya kulaumu kwasababu hatukuja na kitu duniani..

Ayubu alizungumza sentensi moja ambayo ni muhimu sana kwetu sisi kuielewa…alisema …Ayubu 1:21 “ akasema, Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu nili uchi, nami nitarudi tena huko uchi vilevile; Bwana alitoa, na Bwana ametwaa; jina la Bwana na libarikiwe”.

Maana ya kutoka kwa mama yake uchi, alimaanisha hakuja na kitu duniani, hata nguo, wala watoto, wala mashamba, wala wale ng’ombe aliowapoteza, wala wale mbuzi na ngamia…bali alikuja bila chochote…kwahiyo hata siku atakapokufa atarudi huko alikotokea bila kitu…kwa ufunuo huo basi akahitimisha kwa kusema Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake libarikiwe!!.

Ni ufunuo mkubwa sana aliupata…na sisi tunapaswa tuwe hivyo..tulikuja duniani bila ya kitu chochote na hivyo tutaondoka bila chochote…kwahiyo tukipata misiba,misiba, tukifilisika, tukipungukiwa tujue kuwa hatukuja na kitu..tukiyajua hayo tutaishi kwa Amani na kama wapitaji tu hapa duniani. Na hiyo itatufanya kuweka tumaini letu lote kwake, wakati Fulani mtume Paulo na wenzake walisongwa na taabu nzito mpaka wakakata tamaa ya kuishi..Lakini hiyo iliwafanya wazidi kumtumainie Mungu awaokoaye watu wote.

2Wakorintho1:8 “Maana ndugu, hatupendi, msijue habari ya dhiki ile iliyotupata katika Asia, ya kwamba tulilemewa mno kuliko nguvu zetu, hata tukakata tamaa ya kuishi.

9 Naam, sisi wenyewe tulikuwa na hukumu ya mauti katika nafsi zetu ili tusijitumainie nafsi zetu, bali tumtumaini Mungu, awafufuaye wafu,

10 aliyetuokoa sisi katika mauti kuu namna ile; tena atatuokoa; ambaye tumemtumaini kwamba atazidi kutuokoa;”

Kwahiyo tunapaswa tushukuru kwa kila jambo, na kuridhika kwa vile Mungu alivyotukiria, kwasababu hatukuja na kitu vile vile tutaona bila kitu chochote.

1 Timotheo 6:6 “Walakini utauwa pamoja na kuridhika ni faida kubwa. Kwa maana hatukuja na kitu duniani, tena hatuwezi kutoka na kitu.”

Bwana akubariki sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

SWALI LA KUJIULIZA!

KUNA TOFAUTI GANI KATI YA SALA NA DUA?

FAIDA ZA MAOMBI.


Rudi Nyumbani

Print this post

DHAMBI ZINAZOTANGULIA NA ZINAZOFUATA.

Biblia inatueleza kuwa kuna aina mbili za dhambi, zipo dhambi zinazomtangulia mtu kwenda hukumuni na zipo dhambi zinazomfuata mtu hukumuni. Na leo tutaona hizi dhambi ni zipi:

1Timotheo 5:24 ‘Dhambi za watu wengine zi dhahiri, zatangulia kwenda hukumuni; wengine dhambi zao zawafuata’.

Unajua ni heri kitu kinachokutangulia kuliko kile kinachokufuata, kwasababu kinachokutangulia siku zote kipo mbele yako unakiona, na hivyo kuona madhara yake na kutafuta njia ya kukikwepa ni rahisi, lakini kile kinachokufuata kipo nyuma yako, na wakati mwingine unaweza hata usijue kama kuna hatari nyuma yako mpaka pale kitakapokuletea madhara ndipo utakapojua. Mfano leo hii ukaenda porini kwa bahati mbaya ukakutana na mnyama DUBU, ikatokea ukafanikiwa kumponyoka na kukimbia mbali kidogo kwenda kupumzika labda tuseme umbali wa kilometa moja, Ni rahisi kudhani kuwa umempoteza, ni kweli kwa wakati huo utakuwa umempoteza hayupo pamoja na wewe, lakini Dubu ni mnyama mwenye uwezo mkubwa wa kunusa kuliko wanyama wote porini, anao uwezo wa kunusa chakula chake mahali kilipo zaidi ya kilometa 30 na kukifuata. Huo ni umbali kutoka Daresalaam mpaka Kibaha.. Hivyo haijalishi atachukua siku ngapi kukufikia, atakuwa anakufuatilia taratibu mpaka mwisho wa siku atafika pale ulipo na madhara yatakukuta.

Ndivyo ilivyo asili ya dhambi, zipo dhambi ambazo ni dhahiri kabisa zipo mbele ya mtu zinaonekana, hizo tayari zimeshafika hukumuni na kumurudishia majibu yake kuwa anastahili jehanamu. Kwamfano mtu anapokuwa msagaji au shoga, hana haja ya kujihakiki mara mbili kama yeye ataenda motoni au la! Ni dhahiri kuwa anachofanya si Mungu tu kakitaa bali hata jamii imekikataa, vivyo hivyo na anayezini, anayeua, anayefanya kazi ya ujambazi,anayetoa mimba, mchawi, mshirikina, n.k. hizi ni dhambi zilizodhahiri kabisa haihitaji mtu kusubiri kupandishwa kizimbani achunguzwe ndio ahukumiwe, akiwa hapa hapa duniani ameshajua yeye ni wa motoni tu moja kwa moja. Na hizi ni rahisi kuziepuka ikiwa unafanya mfano wa vitu kama hivyo, nakushauri utubu haraka sana ndugu umgeukie Mungu.

Lakini zile zinazomfauta mtu, ni dhambi za siri, ambazo kwa macho ya kawaida ni ngumu kuziona na dhambi hizi huwa mtu ni rahisi sana kuzifanya na rahisi pia kuzisahau, kwamfano mtu anapozungumza maneno yasiyokuwa na maana, mizaha kumuhusu Mungu, kama vile Yesu alivyosema katika Mathayo 12:36 “Basi, nawaambia, Kila neno lisilo maana, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu. 37 Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa.”

Sasa Siku ile ya hukumu anaweza kudhani atahukumiwa kwa mambo yaliyodhahiri tu, lakini mazungumzo yote yatawekwa wazi Hizo ndio dhambi zinazokufuata.. Vitu vingine ni kama vinyongo, kutokusamehe, visasi, usengenyaji,uzishi, n.k.Yote haya mtu anaweza akawa navyo watu wasijue, au pengine yeye mwenyewe asijue kuwa ni makosa, siku ile ya hukumu ndipo atakaposhangaa ni nini hiki.?..Mfano dhambi ya kutokusamehe hii ndio itakayowashitusha wengi sana siku ile…watasema mbona mimi niliomba toba zote kwa Mungu, iweje Mungu hakunisamehe dhambi zangu..Lakini hakujua kuwa Bwana alisema ‘msipowasamehe watu makossa yao na Baba yenu wa mbinguni hatawasamehe nyinyi makosa yenu’.

Lakini vile vile Kumbuka “kifungu hicho hicho” kinatuambia yapo MATENDO MEMA yanayomtangulia mtu hukumu na yale yatakayomfuata.

1Timotheo 5:24 ‘Dhambi za watu wengine zi dhahiri, zatangulia kwenda hukumuni; wengine dhambi zao zawafuata.

25 VIVYO HIVYO MATENDO YALIYO MAZURI YA DHAHIRI; WALA YALE YASIYO DHAHIRI HAYAWEZI KUSITIRIKA’.

Unaona, mtu pia akitenda matendo mema iwe ni kwa siri au kwa dhahiri hakuna lolote litakalosahaulika, kama tu vile dhambi ya siri na isiyo ya siri isivyosahaulika.

Mhubiri 12:14 “Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, LIKIWA JEMA AU LIKIWA BAYA.”

Sasa Matendo yaliyo dhahiri ni kama yapi?, mfano kama kufanya kazi ya Mungu, kusaidia ndugu,na kusaidia yatima, kuwa mtetezi wa watu, kupatanisha, n.k…

Lakini pia yapo matendo mema yaliyositirika, ambayo kwa macho ya kawaida mtu yeyote hawezi kuyaona, na rahisi pia kuyatenda na kuyasahau, mfano wa hayo ni kama vile kuombea wengine na kubariki, kuwaombea watakatifu na kanisa la Mungu kwa ujumla, kumtetea mtu Fulani aliyeonewa, kumsamehe mtu Fulani n.k..

Hivi ni vitu ambavyo siku ile ya hukumu huyu mtu aliyekuwa anavitenda atasimama akidhani hakuna lolote alilolifanya kwa Mungu..Lakini atashangaa siku hiyo thawabu zake zinakuja mahali asipojua atauliza hizi zinatoka wapi? ndio hapo Bwana atamkumbusha, kwa yale maombi yako ya kila siku aliyokuwa analiombea kanisa na watakatifu wote, Fulani na Fulani aliokoka kwa hayo…Fulani na Fulani alisimama kwa kupitia hayo..Fulani na Fulani aliponywa kupitia hayo.(Yakobo 5:16). Ipo faida kubwa sana kutenda mema bila kutarajia malipo au kuonekana na watu kwasababu siku ile matendo yako mema yatakufuata.

Ufunuo 14.13 ‘Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao’.

Hivyo ndugu kila mmoja wetu atasimama hukumuni, lakini lipo tumaini zuri kwa wewe ambaye bado upo kwenye dhambi, njia pekee ya kufutiwa hilo deni la mzizi wa dhambi zako, iwe ni zile zilizokutangulia au zinazokufuata dawa ni moja tu, Ni kumkabidhi leo Bwana YESU maisha yako. Huo ndio mwanzo wa Uzima.

Yeye atakusamehe kabisa, na siku ile, hakutakuwa na shitaka lolote juu yako. Wala hakutakuwa na harufu yoyote ya dhambi itakayokufuata, kwasababu sasahivi jambo atakalolifanya ikiwa utamruhusu aje ndani ya maisha yako ni kuhakikisha anaweka dhambi zako zote mbali na wewe kama vile Mashariki ilivyo mbali na Magharibi. Kwasababu anakuhurumia na kukupenda. Hapo ndipo tunaopoona faida ya DAMU ya YESU isiyoweza kuharibika.Haleluya!!

Zaburi 103: 11 “Maana mbingu zilivyoinuka juu ya nchi, Kadiri ile ile rehema zake ni kuu kwa wamchao.

12 Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi.

13 Kama vile baba awahurumiavyo watoto wake, Ndivyo Bwana anavyowahurumia wamchao.

14 Kwa maana Yeye anatujua umbo letu, Na kukumbuka ya kuwa sisi tu mavumbi”.

Hiyo yote ni ukiwa tayari kutii.

Ubarikiwe sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

DHAMBI YA MAUTI

MADHARA YA DHAMBI YA UASHERATI.

JE! KUBET NI DHAMBI?

MSHAHARA WA DHAMBI:

DHAMBI YA ULIMWENGU.

NGUVU YA UPOTEVU.

Rudi Nyumbani

Print this post

LILE TUMAINI LILILO NDANI YETU LINAPOULIZIWA.

Jina la mwokozi wetu YESU KRISTO lisifiwe daima, Nakukaribisha ndugu mpendwa tujifunze maandiko, Leo tutangazia kwa sehemu kitabu cha waraka wa kwanza wa Petro tutaona Neno kuu la msingi ambalo mtume Petro aliwasihi ndugu wote katika Bwana ambao walikuwa wanaishi kama wageni katika mataifa mengi, Ikumbukwe kuwa wakati ule dhiki kuu ilipotokea Yerusalemu, wakristo wakiyahudi walipokuwa wakitafutwa wafungwe na kuuawa, wengi wao waliondoka Yerusalemu, na kukimbilia katika mataifa mengine ya mbali, vile vile na kule katika mataifa wale wakristo waliopokea injili nao pia hawakuwa katika hali ya usalama, nao pia shetani alikuwa anawawinda na hivyo walikuwa wanahama hama. Na ndio maana ukisoma nyaraka zote za mitume utaona wakristo wote walikuwa wanajulikana kama wasafiri, wageni na wapitaji katika dunia.

Na ndio maana tunaona waraka huu wa kwanza wa Petro, anauandika kwa watu wote (wakristo wa-kimataifa na wa-kiyahudi). Walio katika UTAWANYIKO, yaani kwenye mataifa mengine ya kigeni, Tunasoma hayo katika :

1Petro 1:1 “Petro, mtume wa Yesu Kristo, kwa wateule wa Utawanyiko, wakaao hali ya ugeni katika Ponto, na Galatia, na Kapadokia, na Asia, na Bithinia;

2 kama vile Mungu Baba alivyotangulia kuwajua katika kutakaswa na Roho, hata mkapata kutii na kununyiziwa damu ya Yesu Kristo. Neema na amani na ziongezwe kwenu.”

Unaona sasa ukisoma waraka huu utaona Petro akiwasihi wawaheshimu watu wote, wawe na mwenendo mzuri, watii mamlaka, waheshimiane wao kwa wao, wasaidiane, wapendane, na wasishitakiwe kwa jambo lolote ovu, ili kusudi kwamba watu wa mataifa wasiomjua Mungu wao wasipate Neno la kuwashitaki. Aliwasihi pia wakristo wote waliopo huko wavumilie, na zaidi ya yote wafurahie pale wanapoteswa kwa ajili ya Kristo.

1Petro 4:13 “Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe.

14 Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni heri yenu; kwa kuwa Roho wa utukufu na wa Mungu anawakalia.

15 Maana mtu wa kwenu asiteswe kama mwuaji, au mwivi, au mtenda mabaya, au kama mtu ajishughulishaye na mambo ya watu wengine.

16 Lakini ikiwa kwa sababu ni Mkristo asione haya, bali amtukuze Mungu katika jina hilo.”

Unaona?, Huko katika mataifa ya ugenini, walikuwa ni kama kioo, na matamasha,watu wote wanawaangalia..Lakini mwisho wa siku Mtume Petro akawaambia maneno haya:

“Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu.” (1Petro 3:15)

Hii ikiwa na maana kuwa itafika wakati wale watu wanaowazunguka watavutiwa kujua nini hasa sababu ya wao kuwa hivyo.Japo kuwa ni wageni, japokuwa wanapitia dhiki na mateso na shida lakini bado wapo na msimamo wao..Nini hasaa hawa watu wanakitazamia?.. Ndio hapo mtume Petro anawaasa sasa wawe tayari kuwaeleza habari za TUMAINI lililo ndani yao..

Kwamba ule uzuri waliowekewa mbele yao, na ufalme ambao upo karibuni kufunuliwa na wao wakiwa kama wafalme na makuhani,Taifa takatifu la Mungu pamoja na kiongozi wao mkuu Yesu KRISTO,kama MFALME wa Wafalme, ndio sababu inayowafanya waishi kama walivyo, wakae mbali na dhambi na matendo yote ya giza, wasione kama hizo dhiki na mateso ni kitu kikubwa katika maisha yao kulinganisha na tumaini lilipo mbele yao.(1Petro 2:9)

Embu jaribu kufikiria huyo mtu akisikia hivyo ataachaje kubadilika. Na sisi vivyo hivyo tunapaswa tuishi kama wapitaji, kama wageni wasafiriji, huku tukiwa na TUMAINI la amani na furaha, ili siku moja nasi tuulizwe na watu wasiomjua Mungu, watu wenye mahangaiko, wenye hofu ya maisha na mizigo ya dhambih watuulize je! Mbona nyinyi mpo hivi na bado maisha yenu ni ya amani.. Nasi ndipo tuwaeleze TUMAINI lililo ndani yetu habari za YESU KRISTO…kwa upole na hofu, sio kwa kuwatisha hapana bali kwa upole na hofu biblia inatuambia hivyo. Na mwisho tutajikuta wengi wanavutiwa na TUMAINI hilo..Lililo la kweli.

Wafilipi 3:1 “Hatimaye, ndugu zangu, furahini katika Bwana….”

4 Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini.

5 Upole wenu na ujulikane na watu wote. BWANA YU KARIBU.

6 Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.

7 Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.(Wafilipi 4:4-7)

Amen. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

TUTAWEZAJE KUMZALIA MUNGU MATUNDA?

BABA YANGU ANATENDA KAZI HATA SASA!

UPUMBAVU WA MUNGU.

MUNGU NDIYE ANAYEISHAWISHI MIOYO.

Rudi Nyumbani

Print this post

MPENDE JIRANI YAKO KAMA NAFSI YAKO.

Luka 10: 25 “Na tazama, mwana-sheria mmoja alisimama amjaribu; akisema, Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?

26 Akamwambia, Imeandikwa nini katika torati? Wasomaje?

27 Akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako.

28 Akamwambia, Umejibu vema; fanya hivi nawe utaishi. 

29 Naye akitaka kujidai haki, alimwuliza Yesu, Na jirani yangu ni nani?

30 Yesu akajibu akasema, Mtu mmoja alishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko, akaangukia kati ya wanyang’anyi; wakamvua nguo, wakamtia jeraha, wakaenda zao, wakimwacha karibu ya kufa.

31 Kwa nasibu kuhani mmoja alishuka kwa njia ile; na alipomwona alipita kando.

32 Na Mlawi vivyo hivyo, alipofika pale akamwona, akapita kando.

33 Lakini, Msamaria mmoja katika kusafiri kwake alifika hapo alipo; na alipomwona alimhurumia,

34 akakaribia, akamfunga jeraha zake, akizitia mafuta na divai; akampandisha juu ya mnyama wake, akampeleka mpaka nyumba ya wageni, akamtunza.

35 Hata siku ya pili akatoa dinari mbili, akampa mwenye nyumba ya wageni, akisema, Mtunze huyu, na cho chote utakachogharimiwa zaidi, mimi nitakaporudi nitakulipa.

36 Waonaje wewe, katika hao watatu, ni yupi aliyekuwa jirani yake yule aliyeangukia kati ya wanyang’anyi?

37 Akasema, Ni huyo aliyemwonea huruma. Yesu akamwambia, Enenda zako, nawe ukafanye vivyo hivyo”.

Kuna kitu kidogo cha kujifunza katika hichi kisa…Mwanasheria mmoja alisimama kumwuliza swali la kumjaribu Bwana Yesu…kumwangalia atajibuje! Lakini Bwana alimjibu kwa kumrudisha kwenye Torati na kumwuliza imeandikwaje! Akamjibu “mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako”.

Bwana akampongeza akamwambia afanye hivyo naye utaupata huo uzima wa milele. Lakini Yule mwanasheria hakuishia hapo…akataka kuendelea kumpima ufahamu Bwana Yesu kwa kumwuliza jirani yake ni nani??.

Sasa kumbuka huyu mtu hakuwa na lengo la kutaka kujifunza bali kwa lugha ya sasa hivi tunaweza kusema ni mtu aliyekuwa anajifanya mjuaji…Kwasababu alikuwa anajua kabisa vigezo vya kuupata uzima wa milele ni kumpenda Mungu kwa moyo wote na akili zote na pia kumpenda jirani kama nafsi yake, lakini bado alikuwa anamwuliza Bwana kwa kumjaribu…Na hapa anamwuliza tena Bwana jirani yangu ni nani…Na wakati Bwana ameshamjibu kuwa anapaswa ampende jirani yake kama nafsi yake..Kwahiyo alikuwa anajua kabisa jirani yake ni nani lakini alitaka kumwonyesha Bwana yeye ni mjuaji zaidi….

Na hicho kiburi alikipata kutokana na kusoma kwingi, alifahamu mambo mengi ya torati na dini yake kwasababu hapo juu biblia inasema alikuwa ni mwanasheria…Sasa hakuwa mwanasheria kama hawa wanasheria tunaowajua sasahivi wanaotumia katika ya nchi kuhukumu…Hapana bali yeye alikuwa ni mwanasheria aliyesoma sheria zote za Mungu kupitia Torati za Musa…Kwahiyo alikuwa anajua kufumbua maswali yote yanayohusiana na torati…kukitokea jambo Fulani anaweza kukupatia ufumbuzi kamili kwa kurejea kwenye Torati…atakwambia Aya Fulani ya torati, kipengele Fulani kinasema hivi na hivi…Kwahiyo ni watu ambao ulikuwa huwezi kuwadanganya kitu chochote kinachotoka kwenye Torati, walikuwa wanaijua yote.

Ndio maana alikuja kwa ujasiri kumjaribu Bwana akiwa tayari na majibu sahihi ya maswali yake kichwani.

Wakati yeye anadhani anajua kumbe mbele za Mungu alikuwa anaonekana hajui chochote.

Sasa katika mfano huo hapo juu Bwana Yesu alioutoa, alikuwa anataka kumwonyesha Yule mwanasheria kuwa “dhana ya kufikiri kuwa wayahudi ndio majirani zao pekee ni uongo”..Kama Torati ilivyowafundisha kuwa… “jirani yako ni Mwisraeli mwenzako”..Mtu mwingine tofauti na mwisraeli (Myahudi) sio jirani yako. Hivyo mtu unayepaswa kumpenda kama nafsi yako ni mwisraeli mwenzako tu!…Ndivyo huyu mwanasheria alivyokuwa anajua kichwani mwake na ndivyo torati ilivyokuwa inasema. Lakini ashukuriwe Mungu Bwana Yesu ndiye ukamilifu wa Torati Haleluya!!. Ndio maana Biblia inatuonya tutoke katika kamba za madhehebu kwasababu zinatufungia mlango wa kumjua Mungu…kamba za madhehebu zinatufanya tusimwelewe Mungu wala tusimsikie Mungu kwa kisingizio tu! Dini yetu inasema hivi, dhehebu letu linasema hivi. Zinatufanya tujione tunajua kila kitu kumbe hatujui chochote kama huyu mwanasheria hapa!.

Sasa tukirudi kwenye Torati ya Musa, Baada ya Mungu kuwatoa wana wa Israeli Misri na kuwaingiza nchi ya Kaanani aliwaambia…wapendane wao kwa wao, yaani wayahudi kwa wayahudi kama nafsi zao, pia walionywa wasichangamane na watu wa mataifa, hata wasioe watu wa mataifa. Na waliambiwa pia wasitozane riba wao kwa wao, wanaweza kuwatoza riba watu wa mataifa lakini sio wao kwa wao. Hivyo ilikuwa inaaminika na kufahamika kuwa sheria hiyo Musa aliyoitoa ya kumpenda jirani yako kama nafsi yako, inawahusu tu wayahudi kwa wayahudi, kwamba wao tu watapendana kama nafsi zao, kwamba mtu mwingine tofauti na Taifa lao ni ruksa kutokumjali..ni ruksa kutojishughulisha naye. Lakini mwisraeli mwenzako ndio unapaswa umpende kama nafsi yako. Ukisoma kitabu cha Mambo ya Walawi utaweza kuelewa jambo hilo vizuri kwa undani, lakini moja ya mstari unaozungumzia upendo kwa wayahudi tu ni huu..

Walawi 19:18 “Usifanye kisasi, WALA KUWA NA KINYONGO JUU YA WANA WA WATU WAKO; bali umpende jirani yako kama nafsi yako; Mimi ndimi Bwana”.

Umeona?..Biblia inasema hapo “juu ya watu wako”..ikiwa na maana watu wengine (yaani watu wa mataifa) ni ruksa kuwawekea kinyongo endapo wamefanya jambo la kukwaza.

Kwahiyo ndivyo ilivyokuwa inaeleweka miaka na miaka…Na huyu mwanasheria ndivyo alivyokuwa anajua…Lakini tunaona Bwana alimwambia kitu kipya..kuhusu JIRANI YAKE KUWA NI NANI?…Alitegemea aambiwe kuwa jirani yake ni myahudi mwenzake, (aidha mlawi au kuhani au mwisraeli wa kawaida tu)..lakini Bwana alimwonyesha Msamaria ndiye ndugu yake.

Sasa WASAMARIA wakati huo hawakuwa watu wa Taifa la Israeli, walikuwa ni watu wa mchanganyiko na watu wa mataifa…Kwahiyo hawakuwa uzao wa Ibrahimu hata kidogo..Lakini Bwana alitoa mfano huo kuonyesha kuwa watu wa mataifa wanaweza kuwa majirani wa kweli kuliko hata hao waisraeli wanaojiona wamestahili kupendana wao kwa wao tu!.

Katika mfano ule tunaona…Alikuja kwanza kuhani ambaye alikuwa myahudi lakini alipita kando hakutaka kumsaidia myahudi mwenzake mtu wa Taifa moja na yeye…Baadaye kidogo alipita Mlawi ambaye alikuwa myahudi pia lakini hakutaka kumsaidia myahudi mwenzake aliyekuwa amepatwa na matatizo…Lakini alipopita Msamaria ambaye hakuwa hata myahudi wala hamjui Mungu wa Israeli, alimsaidia kwa msaada mkubwa Myahudi ambaye alikuwa hata hamjui..Na hivyo huyo Bwana ndiye akasema ni JIRANI mwema anayepaswa kupendwa kama nafsi yake.

Bila shaka baada ya mfano huo, Yule mwanasheria aliondoka kwa hasira kwasababu ni kama aliambiwa amri mpya awapende pia watu wa mataifa aliokuwa anaishi nao, (makafiri) kama nafsi yake.

Na sisi kuna jambo tunaweza kujifunza hapo….Udini na Udhehebu ni mbaya sana, unaweza kutufanya tudhani tunampendeza Mungu kumbe hatumpendezi hata kidogo…Ni mara ngapi umeona watu wanaojiita wakristo wakiwachukia watu wasio wa Imani yao?…Utaona wanatoa mpaka maneno ya laana kwasababu tu sio wakristo kama wao…Wakati hao wanaowashutumu ndio Mungu anawaona ni MAJIRANI ZAO WAZURI kuliko hata wakristo wenzao..

Kama umefanya utafiti, utagundua kuwa fursa nyingi au msaada mwingi, Mungu anawatumia watu wasio wa Kristo au watu wa kiulimwengu kutusaidia kuliko watu wa ki-Mungu, Utaona watu ambao ni wakidunia wakati mwingine ni wakarimu na wanaojali kuliko hata watu wanaomjua Mungu. Hao Bwana anatuambia tuwapende kama nafsi zetu..hao ndio wasamaria wema..ndio majirani zetu, sio wakuwachukia na kuwasema bali kuwapenda kama nafsi zetu….

Sio kwasababu hamjui Mungu wako basi ndio awe sababu ya kuwa adui yako na kusema watu wa imani yangu tu ndio marafiki zangu, wakati mwingine Bwana anawatumia hao watu wasiomjua Mungu wako kukuletea wewe msaada kama ilivyokuwa kwa huyu myahudi aliyeangukia katikati ya wanyanganyi badala asaidiwe na watu wa dini yake na imani yake anakwenda kusaidiwa na watu hata wasioijua Torati..

Biblia imetuonya tu tusichangamane kufuata njia zao zisizofaa, kama ni walevi hatuenendi katika njia zao, kama ni waasherati vivyo hivyo, kama ni wacheza dansi, kama ni waabudu sanamu tusishirikiane nao hata kidogo…lakini sio tusiwapende na kuwachukia, wakitaka kukopa kwako usiwape kisogo, wakikuaribisha kwao usikatae, wakikupa zawadi pokea, wakiumwa uwatembelee… ili kwa matendo yetu mazuri na upendo wetu tuwavute waje upande wetu, na tuonekane tumeweza kuyafanya mapenzi ya Baba yetu aliye mbinguni.

Hivyo jawabu la mambo yote ni upendo, kwetu sisi kwa sisi na kwa wale walio nje.

Bwana atusaidie sote .jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

UPENDO

UMETEKWA NA UPENDO WA KRISTO?

BIBLIA ITUAMBIA TUSALIMIANE KWA BUSU TAKATIFU. HILI BUSU NDIO LIPI?

HAWA ALIPOLAANIWA ALIAMBIWA “TAMAA YAKO ITAKUWA KWA MUMEO”.NI TAMAA IPI INAYOZUNGUMZIWA HAPO?


Rudi Nyumbani

 

Print this post

NITAONGEZAJE NGUVU ZANGU ZA ROHONI?

Hapo nyuma, kabla sijampa Kristo maisha yangu, na wakati ambao bado ni mchanga kabisa wa masuala ya wokovu, niliaminishwa kuwa kigezo kikuu kinachomtambulisha mtu huyu kuwa anazo nguvu nyingi za rohoni ni kiwango chake cha UPAKO, pengine na wewe ulifahamu hivyo au unafahamu hivyo, yaani mtu kuwa na uwezo wa kufanya miujiza,au kuona vitu katika ulimwengu wa roho kama vile mapepo, wachawi,majini, kuona maono, kuota ndoto, kunena sana kwa lugha, au kufanya sana ishara.n.k. Kwamba mtu kama huyo ni mtu mwenye nguvu nyingi sana rohoni na hivyo shetani anamwogopa sana. Jambo hili lilinifanya nione shauku kutatufa Upako kuliko kitu kingine chochote.

Lakini je! Kwa mujibu wa biblia hizo ndizo nguvu za rohoni?. Leo tutajifunza juu ya hilo, na ni kitu gani tufanye ili nguvu zetu za rohoni ziongezeke. Sasa Ili kuelewa nini maana ya nguvu za rohoni, ni vizuri tujifunze kwanza juu ya nguvu nyingine, Tunajua siku zote kitu chochote chenye nguvu huwa kinakuwa na uwezo wa “kuteka na kutawala”, Simba ni mnyama mwenye nguvu na ndio maana ameteka pori lote, hivyo nguvu ya aina yoyote ile huwa inateka na kutawala, tunafahamu pia mtu mwenye nguvu ya kiuchumi huwa anatawala, mwenye nguvu ya kisiasa huwa anateka na kutawala, mwenye nguvu ya kiteknolojia huwa na uwezo pia wa kuteka na kutawala, na ndio maana tunaona mataifa kama Marekani na Ulaya, yanatawala dunia sio kwasababu ni makubwa hapana, bali kwasababu yana nguvu Fulani zinazowazidi wengine.

Vivyo hivyo na kwa mwenye nguvu za Rohoni, ni lazima mtu awe na uwezo wa kuteka na kutawala, na ndio maana Bwana Yesu alisema maneno haya.

Mathayo 11:12 “Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.”,

 Unaona nguvu anazozizungumzia sasa hapo ni NGUVU ZA ROHONI. Ikiwa na maana kuwa mtu mwenye nguvu nyingi za Rohoni ndiye atakayeweza kuuteka ufalme wa mbinguni, ukiwa na nguvu chache utakuwa mnyonge tu. Na leo nataka ujue hizi nguvu za Rohoni zinapatikana wapi.

Sasa tukirudi kwenye huo huo mstari hapo juu, lazima tujiulize swali moja, ni kwanini Bwana alisema “Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa”, kwanini hakusema tangu siku za Ibrahimu au za Musa hadi sasa? Badala yake anasema “Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa”, . Utagundua kuwa Bwana alitaka tujifunze kitu Fulani kwa Yohana mbatizaji katika masuala ya kupata nguvu za rohoni. Hivyo embu tumwangalie kidogo Yohana alikuwa ni mtu na namna gani tangu utoto wake.

Maandiko yanatuambia:

Luka 1:80 “Yule mtoto akakua, AKAONGEZEKA NGUVU ROHONI, akakaa majangwani hata siku ya kutokea kwake kwa Israeli”.

Unaona kumbe Yohana tangu utoto wake alikuwa akiongeza nguvu rohoni kwa kasi sana, mpaka alipokuwa mtu mzima alipoanza huduma yake. Lakini hakuwahi kufanya muujiza hata mmoja, wala kutoa ishara yoyote kutoka mbinguni kama vile Eliya, Biblia inasema hivyo (Yohana 10:41), Na ndio maana tunasema Upako wowote kulingana na maandiko sio kitambulisho kuwa mtu huyo anazo nguvu za rohoni. Mtu unaweza akawa na uwezo wa kuona maono yote duniani lakini rohoni ukawa mdhaifu kuliko hata mtu aliyempa Kristo maisha yake leo.

Sasa tunaona Yohana alipoteza muda wake mwingi kukaa mbali na makazi ya watu ili tu kuongeza nguvu zake rohoni tangu utoto wake,(baadaye kidogo tutaona ni kitu gani alichokuwa anakifanya alipokuwa anakwenda kule jangwani) mpaka kufikia kilele cha nguvu za rohoni mpaka Bwana Yesu Kumshuhudia vile katika:  

Mathayo 11:11 “Amin, nawaambieni, Hajaondokea mtu katika wazao wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji; 

12 Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.”.

Kwa Nguvu alizokuwa nazo rohoni, hakukuwahi kutokea nabii au mtu yoyote katika agano la kale aliyeweza kumfikia, sio Ibrahimu, sio Musa, sio Eliya, sio Daudi sio mtu yoyote Yule aliyefanya mambo makubwa unayemsoma katika agano la kale aliyeweza kuwa na nguvu zaidi yake (Yohana) kuuteka ule ufalme. Lakini Leo utafahamu SIRI imelala wapi nawe uanze kujishughulisha nayo.

Sasa kumbuka Yohana tangu utoto wake hakuwahi kujishughulisha na jambo lingine zaidi ya kutafuta kumjua huyu MASIHI ALIYETABIRIWA NI NANI?. Ambaye ndiye kiini cha dini yao kiyahudi, ndiye kiini cha wokovu uliokuwa unatarajiwa wa ulimwengu mzima, wakati wengine wanang’ang’ania kukariri torati huyu aling’ang’ania kumtafuta Kristo ambaye Mungu alimshuhudia tangu enzi za kale za manabii. Na hiyo ndiyo iliyomfanya mbinguni aonekane kila siku nguvu zake za rohoni kuongezeka kwa kasi sana.

Alianza kutafuta kwa bidii katika torati habari zake, tangu mwanzo mpaka mwisho, kwa jinsi alivyokuwa anamtafuta kwa bidii akachunguza akaona kuwa kumbe kwa mfano ule ule wa wana wa Israeli walivyookolewa utumwani Misri ndivyo mwokozi atakavyouokoa ulimwengu wote kwa jinsi hiyo hiyo..

Kwa hatua zile tatu, ambapo hatua ya kwanza, ilikuwa ni Yule mwanakondoo kuchinjwa, ili damu ipatikane kwa pigo la mzaliwa wa Kwanza Misri, akajua kumbe damu ilihitajika kufungua vifungo. Na pigo lile lililegeza kweli vifungo vya maadui zao kuwapa ruhusu wa kutoka Misri, lakini lile halikutosha kuwafanya maadui zao wasiwafuatilie, hivyo ilihitajika hatua nyingine ya pili na ndio ile ya nguzo ya moto, ambayo ilikuwa inawatangulia mbele yao sasa ilibidi irudi nyuma yao kuweka wigo wasiwafuate.. Yohana akagundua kumbe moto ulipitia juu yao kuwatakasa pasipo wao kujijua.

Lakini moto ule haukutosha kumaliza kabisa adui yao ulipoondolewa, bado walitaka kuwafuata na ndipo tunaona maji yalifuata kuwatakasa tena, nako ndiko kule kuvuka bahari ya shamu Kubatizwa, na hapo ndipo maadui zao walipomalizwa moja kwa moja walipotoswa na yale maji.

Hatua hizo tatu (yaani damu ya mwana-kondoo, moto-wa-Roho Mtakatifu, na Maji), ndizo Yohana alitambua kuwa Masihi ajaye atazitumia kumkamilisha mwanadamu kwa wokovu wake.

Sasa hapo ndipo Yohana alipopatia ufunuo wa ubatizo wa Maji akaanza kuufundisha na kuwaambia watu wabatizwe, huku akitazamia kuwa mwanakondoo atakajua ambaye atakamilisha yaliyobakia yaani maji na moto wa Roho Mtakatifu,

Yohana 1:26 “Yohana akawajibu akisema, Mimi nabatiza kwa maji. Katikati yenu amesimama yeye msiyemjua ninyi.

27 Ndiye yule ajaye nyuma yangu, ambaye mimi sistahili kuilegeza gidamu ya kiatu chake.

28 Hayo yalifanyika huko Bethania ng’ambo ya Yordani, alikokuwako Yohana akibatiza.

29 Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, MWANA-KONDOO WA MUNGU, AICHUKUAYE DHAMBI YA ULIMWENGU!

30 HUYU NDIYE NILIYENENA HABARI ZAKE YA KWAMBA, Yuaja mtu nyuma yangu, ambaye amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu.

31 Wala mimi sikumjua; lakini kusudi adhihirishwe kwa Israeli ndiyo maana mimi nalikuja nikibatiza kwa maji.

32 Tena Yohana akashuhudia akisema, Nimemwona Roho akishuka kama hua kutoka mbinguni; naye akakaa juu yake.

33 Wala mimi sikumjua; lakini yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyo aliniambia, Yeye ambaye utamwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu.

34 Nami nimeona, tena nimeshuhudia ya kuwa huyu ni Mwana wa Mungu.

35 Tena siku ya pili yake Yohana alikuwa amesimama pamoja na wawili katika wanafunzi wake.

36 Akamtazama Yesu akitembea, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu!

37 Wale wanafunzi wawili wakamsikia akinena, wakamfuata Yesu”.

(Soma pia Mathayo 3:11)..

Unaona hapo Yohana alimtambua YESU na Kazi yake atakayokuja kuifanya kabla hata hajawasili, alimtengenezea njia, Hivyo mbinguni akaonekana mtu mkuu sana, mwenye nguvu nyingi za rohoni japo duniani watu walimwona maskini amerukwa na akili.

Leo hii nataka nikuambie ndugu usifurahie tu kuwa YESU ameyaokoa maisha yako, halafu ukaridhika, mahali ulipo, unaendelea na mambo yako, YESU KRISTO ni zaidi ya unavyomfikiria, Mungu kaweka Heshima yake yote pale, ndio hekima ya Mungu na NGUVU YA MUNGU (1Wakorintho 1:24), na ndipo utajiri wote, na hazina zote za maarifa zilipolala. Hapo ndipo Yohana alipopatia heshima yake na ukuu wake.

Wakolosai 2:2 “….wakapate utajiri wote wa kufahamu kwa hakika, wapate kujua kabisa siri ya Mungu, yaani, Kristo;

3 ambaye ndani yake yeye hazina zote za hekima na maarifa zimesitirika.”

Kwa mtu Yule leo hii anayejishughulisha kutafuta kumjua YESU usiku na mchana, mtu huyo nguvu zake za rohoni zinaongezeka kwa kasi sana pasipo hata yeye kujijua. Na mwisho wa siku anajikuta anauteka ufalme wa Mbinguni kirahisi kabisa kwasababu amefahamu mahali lulu ya thamani ilipo.

Itafute hii LULU ndugu. Nataka nikuambie vita kubwa ya shetani ipo hapo, watu wasimjue Kristo ni nani hasaa na uweza wake, yeye anataka watu wamwone kama mtu wa kawaida tu, kwasababu anafahamu mtu akishamwelewa vizuri Bwana Yesu ni nani, basi atajijengea daraja zuri mbinguni na atamsababishia madhara makubwa sana katika ufalme wake.

Anza leo mwanzo mpya, maanisha kumfauta Kristo…usitafute upako wala miujiza..Bwana akikujalia hizo ni vizuri lakini sio jawabu la kuwa na nguvu za rohoni…Ikiwa unapenda kuwa mkuu hata zaidi ya Yohana, machoni pa Mungu,wala usijishughulishe na jambo lingine lolote, JISHUGHULISHE KATIKA KUMTAFUTA KRISTO, acha kuzisumbukia karama, acha kutafuta maombezi, acha kukesha kwa ajili ya upako, kesha kwa ajili ya KUMSOMA KRISTO. Sisemi usizitumie hizo karama, hapana zitumie maadamu Mungu kakupa, lakini huku nyuma usisahau kuwa ufalme wa mbinguni unatekwa na wenye nguvu za mafunuo ya YESU Kristo. Tumeaswa tumjua sana Yesu Kristo, Mwana wa Mungu mpaka tufikie kimo cha utimilifu wake.

Waefeso 4:13 “hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani NA KUMFAHAMU SANA MWANA WA MUNGU, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo;”

Unapoyatafakari maandiko, jenga mtazamo wa Kristo ndani yake, wengi wakifungua maandiko wanayatazama kwa sura ya mafanikio ya kidunia, hivyo wanapata ufunuo kulingana na walichokitazamia, lakini ukimsoma Kristo kwa lengo la kutaka kumjua zaidi…atakujaza maarifa na nguvu za rohoni, atajifunua kwako na kuanza kukufundisha kanuni zake zote kwa namna ya ajabu sana.

Ubarikiwe sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Print this post

JINA LA MUNGU NI LIPI?

Shalom mtu wa Mungu. Wengi wanajiuliza swali hili, jina la Mungu hasaa ni lipi kwasababu kwenye biblia tunaona yanatajwa majina mengi tunashindwa kuelewa ni jina lipi la kusimamia. Ni kweli hili ni swali zuri, ambalo mtu aliyemaanisha kweli kumtafuta Mungu atatamani kufahamu jina halisi la Mungu ni lipi?.

Hili si swali gheni kwetu sisi, ni swali ambalo lilianza kuulizwa na wana wa Israeli tangu zamani kabla hata hawajatolewa katika nchi ya Misri, walikuwa wanajiuliza huyu Mungu wa Ibrahimu, wa Isaka na Yakobo tunayemtumainia siku zote jina lake ni Nani?..Na ndio maana utaona jambo la kwanza ambalo Musa alimuuliza Mungu kabla ya kwenda kuwaokoa wana wa Israeli, ni kuwa “watu hawa wakiniuliza jina lako ni nani niwajibuje”?. Unaona alijua kabisa ndio swali atakalokumbana nalo la kwanza kabla ya mambo mengine kwa wayahudi waliokuwa wanateseka kule Misri. Hivyo leo tutajifunza Jina hasaa la Mungu ni lipi kwa mujibu wa majibu aliyopewa Musa na Mungu katika maandiko… tusome:

Kutoka 3:13 “Musa akamwambia Mungu, Tazama, nitakapofika kwa wana wa Israeli, na kuwaambia, Mungu wa baba zenu amenituma kwenu; nao wakaniuliza, Jina lake n’nani? Niwaambie nini?

14 Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO;akasema,Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli;MIMI NIKO amenituma kwenu.

15 Tena Mungu akamwambia Musa, Waambie wana wa Israeli maneno haya, Bwana, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenituma kwenu; hili ndilo jina langu hata milele, nalo ni kumbukumbu langu hata vizazi vyote.”

Hilo ndilo lilokuwa jibu la Mungu, jina lake wakimuuliza ni MIMI NIKO AMBAYE NIKO, au NITAKUWA KAMA NITAKAVYOKUWA…Lakini leo nataka tujiulize swali moja je hili jina “NITAKUWA KAMA NITAKAVYOKUWA”, Ni jina kweli?. Ukweli ni kwamba hili sio “jina”. Lakini kulikuwa na sababu kubwa Mungu kujitambulisha kwa Musa kwa namna hiyo mwanzoni kabisa, nataka nikuambie na hapo ndipo siri ya jina lake ilipolala.

Aliposema NITAKUWA KAMA NITAKAVYOKUWA…kwa Lugha nyepesi ni sawa na kusema, siku hiyo ikifika Nitajifunua au nitajulikana kama nitakavyokuwa.. hiyo siku ndio litajulikana, kwahiyo hiyo ni kuonyesha kuwa Mungu jina lake la si la mara moja tu kama ya kwetu sisi wanadamu yalivyo, bali linajifunua katika maumbile tofauti kulingana na wakati na majira… Ukimwelewa kwa hapo Mungu basi hutapata shida huko mbeleni.

Na ndio maana kipindi kifupi tu mbeleni mara baada ya Musa kwenda kumwonyesha Farao zile Ishara alizopewa na Mungu, na kukataa kuwaachia wana wa Israeli waende zao, kinyume chake akawazidishia utumwa, mpaka wana wa Israeli wakamnung’unikia Musa, na Musa akarudisha malalamiko yake kwa Mungu, ndipo tunaanza kuona sasa hatua ya kwanza ya “NITAKUWA KAMA NITAKAVYOKUWA” ilipoanza kutenda kazi. Tunaona Mungu alimwambia tena Musa mimi ni YEHOVA.

Kutoka 6:1 “Bwana akamwambia Musa, Sasa utaona nitakavyomtenda Farao; maana kwa mkono hodari atawapa ruhusa kwenda zao, na kwa mkono hodari atawafukuza katika nchi yake.

2 Kisha Mungu akasema na Musa, akamwambia, Mimi ni YEHOVA;

3 nami nilimtokea Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi, bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao.

4 Tena nimelithibitisha agano langu nao, la kuwapa nchi ya Kanaani; nchi ya kukaa kwao hali ya ugeni.

5 Na zaidi ya hayo, nimesikia kuugua kwao wana wa Israeli, ambao Wamisri wanawatumikisha, nami nimelikumbuka agano langu.

6 Basi waambie wana wa Israeli, Mimi ni YEHOVA, nami nitawatoa ninyi mtoke chini ya mizigo ya Wamisri, nami nitawaokoa na utumwa wao, nami nitawakomboa kwa mkono ulionyoshwa, na kwa hukumu kubwa;

7 nami nitawatwaeni kuwa watu wangu, nitakuwa Mungu kwenu; nanyi mtajua ya kuwa mimi ni YEHOVA, Mungu wenu, niwatoaye mtoke chini ya mizigo ya Wamisri.”

Unaona hapo alimtokea Ibrahimu, na Isaka na Yakobo kama Mungu mwenyezi, (EL shadai) ukisoma mwanzo 17:1 utaona..Sasa Kwa utambulisho huu wa kumjua yeye kama mwenye enzi yote, mwenye Nguvu zote na uweza wote, ndio uliowafanya Ibrahimu na Isaka na Yakobo, wamwamini Mungu kwa kiwango kile cha juu namna ile, Unadhani mpaka mtu akuamini hivi hivi tu kuwa utakuja kumfanya kuwa taifa kubwa na mataifa yote duniani yatajibarikia kwako, na huku umeshazeeka, hapo inahitaji Mungu ajifunue kwako kama Mungu-mwenyezi vinginevyo hutaweza kuamini mpaka mwisho..

Lakini sasa Jina hili YEHOVA lilizuka mara baada tu ya Farao kuonyesha kiburi,..Na kama tunavyosoma habari Hiyo hatuna muda wa kuuleza moja moja hapa lakini kwa mapigo yale yaliyomfuata mpaka dakika ya mwisho, tunafahamu sio tu Farao na wayahudi walikiri kuwa Yule ni YEHOVA, bali pia mataifa yote duniani yalimtambua na kumwogopa Mungu kwa jina hilo.

Hata baada ya kuingia nchi ya kaanani Jina hili liliendelea kutumika kwa wana wa Israeli, lilichukua maumbile tofuatitofauti kulingana na wakati waliokuwa wanaupitia:

⧫Mfano utaona Mungu alijifunua kwao kama YEHOVA-RAFA: Maana yake Mungu-Nikuponyaye. (Kutoka 15:26.) Mungu aliwaahidia yale magonjwa yaliyokuwa Misri hayatawapa tena ikiwa watazishika amri zake..

⧫Alijifunua tena kama YEHOVA-NISI: Ikiwa na maana kuwa Mungu ni Bendera yetu (Berani ya vita) (Kutoka 15:26).

⧫Alijifunua tena kama YEHOVA-SHALOMU: Mungu ni Amani (Waamuzi 6:24). Gideoni alijenga madhabahu na kuiita jina hili baada ya kudhani kuwa Mungu angemuua pale alipokutana na malaika.

⧫YEHOVA-MEKADISHKEMU: Bwana atutakasaye (Kutoka 31:13)

⧫YEHOVA-ROHI: Bwana ndiye mchungaji wangu (Zab 23)

⧫YEHOVA-YIRE: Mungu atupaye (Mwanzo 22:14)..

Na mengine mengi hatuaweza kuyataja yote hapa.. Mungu alikuwa akijifunua kwa wana wa Israeli, akionyesha uweza wake na ukuu wake kwao, katika mazingira mbali mbali waliyokuwa wanapitia.

Hivyo hiyo ikaendelea mpaka wakati wa waamuzi,na wafalme na manabii..miaka mingi sana ilipita…

Na ulipofika wakati sasa wa Mungu kuikomboa dunia yote, sio kwa Taifa moja tena kama hapo mwanzo, bali dunia nzima ilimpasa ajichagulie jina la wakati huo.. Haleluya!! Na jina hilo ni lazima libebe sifa zote za majina yaliyotangulia, ili kusudi kwamba kusiwe na kitu chochote cha kando kilichosalia, Jina la dunia nzima…Jina ambalo manabii wa zamani mpaka Musa mwenyewe alitamani lifunuliwe wakati wao lakini ilishindakana…na jina hilo si lingine zaidi ya YESU KRISTO

Tafsiri ya YESU ni “YEHOVA-MWOKOZI” hiyo ndiyo tafsiri yake..Hivyo jina hili limebeba ukombozi mkamilifu wa viumbe vyote, sio wanadamu tu bali mpaka wa wanyama..tabia ya majina yote ya kwanza yamo ndani yake, jina hilo linaponya, linachunga, linatoa Baraka, linahuisha, linaokoa, linashindania vita, linaumba, linafunga, linafungua, linafanya kila kitu..Lile la kwanza lililishia kwa maadui wa mwilini lakini hili limechimba kwenye mizizi kabisa kwenye kiti cha enzi cha shetani huko kuzimu na kumshinda, na kumnyang’anya mamlaka yote na kumpa mwanadamu. Hivyo mwanadamu yoyote akipata ufunuo wa jina hili hakuna jambo lolote litakaloweza kumshinda hapa duniani.

Na ndio maana sasa biblia inasema..Matendo 4:12 “Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.”

Jina hilo ni jina la YESU KRISTO. Utauliza ni wapi tena kwenye maandiko panaposema jina la Yesu ni jina la Mungu…Bwana Yesu alisema maneno haya..

Yohana 5:42 “Walakini nimewajua ninyi ya kuwa hamna upendo wa Mungu ndani yenu.

43 Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, wala ninyi hamnipokei; mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea huyo”.

Hivyo ndugu jina la Mungu Yule ambaye anasema NITAKUWA KAMA NITAKAVYOKUWA sasa ndio hili YESU KRISTO. Uponyaji wako utaupata kwa kupitia hili, kushukuria utashukuria kwa jina hili, kutolea mapepo utatolea kwa jina hili hakuna jina lingine hapo..Vile vile kubatizwa utabatizwa kwa jina hili..Wapo watu wanaobatiza kwa jina la Baba na mwana na Roho Mtakatifu, (Mathayo 28:19). Wanakosa ufunuo Yesu alimaanisha nini pale kusema vile..Hawajui kuwa jina la (Baba na mwana na Roho Mtakatifu) ni jina moja hilo nalo ni jina la YESU. Na ndio maana mitume wote baada ya kulitambua hilo utaona mahali pote walikuwa wanabatiza kwa jina hilo la YESU KRISTO, soma (Mdo 2:38, 8:16, 10:48, 19:5) sehemu zote hizo mitume hawakubatiza kwa vyeo vya Baba na Mwana na Roho Mtakatifu. Bali kwa jina la YESU KRISTO…

Kwa akili ya kawaida tu kwanini pepo ukikemea hulikemei kwa jina la baba na mwana na roho mtakatifu? Badala yake unatumia jina la Yesu, ukiumwa unatumia jina la YESU likuponye iweje leo unapoenda kubatizwa unatua vyeo badala ya JINA?. Ni vizuri tuifahamu kweli na tuifuate, Dini zisitukwamishe.

Natumaini utakuwa umemfahamu MIMI NIKO AMBAYE NIKO kwa sasa jina lake ni lipi?.

Lakini Pia, fahamu kuwa Hili jina la YESU nalo halitadumu milele, kuna wakati unafika Mungu atabalika na kuja na jina jipya, na hilo litatumika katika ule utawala wa miaka 1000, pale Kristo atakapokuwa kama Bwana wa Mabwana na Mfalme wa Wafalme. Jina hilo litakuwa sio la ukombozi tena kama sasa, kwasababu ukombozi utakuwa umekwisha wakati huo…bali litakuwa na tabia nyingine ambazo tutazijua vizuri tukifika huko. Hivyo ni vizuri usiichezee neema tuliyonayo sasa ya ukombozi kupitia jina la Yesu, upo wakati utatamani kuokoka utashindwa kwasababu neema itakuwa imeshaondoka.

Ufunuo19:11 “Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita.

12 Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; NAYE ANA JINA LILILOANDIKWA, ASILOLIJUA MTU ILA YEYE MWENYEWE.

13 Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.

14 Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi.”

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Zinazoendana:

KWANINI YESU ALIMUITA BABA YAKE “ABA”?

JINA LAKO NI LA NANI?

JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?


Rudi Nyumbani

Print this post

UFUNUO: Mlango wa 9.

Shalom.Karibu katika mwendelezo wa kitabu cha Ufunuo, ni vizuri ukakisoma kitabu hichi peke yako kwanza kwa utulivu, na katika uwepo wa Bwana, na kufuatilia mfululizo huu tangu mwanzo ili tunapoendelea katika sura hizi zinazofuata usibakie nyuma twende pamoja.

Katika sura iliyopita tuliona jinsi wale malaika 7 walivyopewa baragumu zao na  pindi walipozipuliza/kuzipiga ni nini kilitokea, Na tulishaona baragumu nne za mwanzo…kama hujapitia pia ni vizuri ukapitia au bofya hapa⏩ Ufunuo:Mlango wa 8. Na tuliona kuwa baragumu hizo ni kama mwanzo wa utungu tu! Wa vile vitasa saba vitakavyokuja kuachiwa huko mbeleni katika siku ile kuu ya Bwana.…Ni sawa na mtu anayenawa uso kwa muda tu! Lakini baadaye atakuja kuoga mwili mzima.

Vile vile tuliona  pia  hizi baragumu zitaanza kupigwa mara baada ya unyakuo kupita tu! Na zile tatu za kwanza Zitawaathiri sana wayahudi waliyopo Israeli (na watu wanaoishi mashariki ya kati), isipokuwa lile la 4 ambalo litaathiri dunia nzima, kwasababu jua likipigwa ni dunia nzima itaathirika na sio sehemu tu!..na mapigo hayo yatatekelezwa kupitia wale mashahidi wawili waliozungumziwa katika ufunuo 11.

Ufunuo 11:3 “Nami nitawaruhusu mashahidi wangu wawili, nao watatoa unabii siku elfu na mia mbili na sitini, hali wamevikwa magunia.

4 Hao ndio ile mizeituni miwili na vile vinara viwili visimamavyo mbele za Bwana wa nchi.

5 Na mtu akitaka kuwadhuru, moto hutoka katika vinywa vyao na kuwala adui zao. Na mtu akitaka kuwadhuru, hivyo ndivyo impasavyo kuuawa.

6 Hao wana amri ya kuzifunga mbingu, ili mvua isinyeshe katika siku za unabii wao. Nao wana amri juu ya maji kuyageuza kuwa damu, na kuipiga nchi kwa kila pigo, kila watakapo”.

Unaona Mashahidi hawa wawili wataleta mapigo hayo kwa amri ya Bwana kama vile Musa alivyoleta mapigo juu ya Farao kwa Amri ya Bwana.

Na mwishoni mwa sura ya 8, tuliona pia kulikuwa na malaika (Tai) aliyeruka katika anga na kutangaza ole kwa wote wanaokaa juu ya nchi kwasababu ya sauti ya zile baragumu 3 zilizosalia, yaani baragumu la 5,6 na la 7.

Hivyo leo tunaendelea na sura ya 9 kwa Neema za Bwana..ambayo inaelezea juu ya baragumu zilizosalia isipokuwa ile ya saba tu.

Ufunuo 9: 1 “Malaika wa tano akapiga baragumu, nikaona nyota iliyotoka mbinguni, imeanguka juu ya nchi; naye akapewa ufunguo wa shimo la kuzimu.

2 Akalifungua shimo la kuzimu; moshi ukapanda kutoka mle shimoni kama moshi wa tanuru kubwa; jua na anga vikatiwa giza kwa sababu ya ule moshi wa shimoni.

3 Nzige wakatoka katika ule moshi, wakaenda juu ya nchi, wakapewa nguvu kama nguvu waliyo nayo nge wa nchi.

4 Wakaambiwa wasiyadhuru majani ya nchi, wala kitu cho chote kilicho kibichi, wala mti wo wote, ila wale watu wasio na muhuri ya Mungu katika vipaji vya nyuso zao.

5 Wakapewa amri kwamba wasiwaue, bali wateswe miezi mitano. Na maumivu yao yalikuwa kama kuumwa na nge, aumapo mwanadamu.

6 Na siku zile wanadamu watatafuta mauti, wala hawataiona kamwe. Nao watatamani kufa, nayo mauti itawakimbia.

7 Na maumbo ya hao nzige yalikuwa kama farasi waliowekwa tayari kwa vita, na juu ya vichwa vyao kama taji, mfano wa dhahabu, na nyuso zao zilikuwa kama nyuso za wanadamu.

8 Nao walikuwa na nywele kama nywele za wanawake. Na meno yao yalikuwa kama meno ya simba.

9 Nao walikuwa na dirii kifuani kama dirii za chuma. Na sauti ya mabawa yao ilikuwa kama sauti ya magari, ya farasi wengi waendao kasi vitani.

10 Nao wana mikia kama ya nge, na miiba; na nguvu yao ya kuwadhuru wanadamu miezi mitano ilikuwa katika mikia yao.

11 Na juu yao wanaye mfalme, naye ni malaika wa kuzimu, jina lake kwa Kiebrania ni Abadoni, na kwa Kiyunani analo jina lake Apolioni”.

Kama tulivyotangulia kujifunza, Nyota iliyoanguka kutoka mbinguni si kimondo bali ni ‘shetani’ na Ufunuo 12:12 inasema.. “hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. OLE WA NCHI NA BAHARI! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.”

Na pia sehemu nyingine Bwana Yesu anasema: Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme. (Luka10:18)

Ikiwa na maana kuwa kuanguka kwa shetani, na kutupwa chini duniani ni LAANA! Sio kitu kizuri..viumbe vyote vikaavyo baharini vitaathirika na kadhalika vikaavyo juu ya nchi…sasa wanadamu ndio wanaokaa juu ya nchi, hao ndio waathirika wakuu!.

Katika baragumu hili tunaona shetani kama nyota iliyoanguka kutoka juu…akipewa funguo za kuzimu…sasa kumbuka kuzimu zimegawanyika katika sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ni sehemu ambapo roho za watu waliokufa katika dhambi zipo, ni sehemu ya mateso sana, roho za watu hawa zipo zikiwa katika hali ya vifungo, zikiteseka zikingoja ufufuo wa hukumu.

Na sehemu ya pili ya kuzimu, ni sehemu ambayo roho za baadhi ya malaika walioasi mbinguni zimefungiwa…Kumbuka sio mapepo yote yaliyoasi yanatenda kazi leo duniani, hapana, yapo mengine mabaya kuliko haya yaliyopo sasa, ambayo yalifungwa katika hii kuzimu ya pili, kwa makosa yaliyofanya na hata kuna mengine yanaweza  kutupwa huko hata leo, ndio maana utaona kuna yale yaliyomsihi Bwana Yesu asiyapeleke shimoni..Huko shimoni kunakozungumziwa ni “kuzimu ya malaika walioasi’’ ni sehemu ya vifungo vya giza na mateso ambapo roho hizo zimefungwa huko mpaka siku zitakapotupwa katika ziwa la moto…ambapo tutakuja kuona katika ufunuo 20 shetani naye atakuja kutupwa huko na kufungwa kwa miaka 1000.

Sasa pia kumbuka shetani alinyanganywa funguo za mauti na kuzimu na Bwana Yesu mwenyewe, kwasababu hapo kwanza alikuwa nazo alikuwa na uwezo wa kuzileta juu roho za watu waliopo kuzimu na baadhi ya mapepo,! Ndio maana unaona aliweza hata kumleta Nabii Samweli juu aliyekuwa amekufa kuzungumza naye. Lakini Baada ya Bwana Yesu kuja, mamlaka yote ya wafu yakawa chini ya Yesu Kristo, hakuna kiumbe chochote hata shetani chenye mamlaka juu ya wafu au roho zilizopo kuzimu au peponi. Lakini tunaona hapa! Shetani anapewa ufunguo za kuzimu…na kama unavyoona ni ANAPEWA!! Ikiwa na maana kuwa hakuwa nazo hapo kabla…alikuwa amenyanganywa lakini hapa anapewa tena kwa muda.. sasa hapewi funguo za kuzimu mahali wanadamu walioasi walipo hapana bali anapewa funguo za kuzimu mahali malaika walioasi walipo?..hizo ni sehemu mbili tofauti.

Na kwasababu ana ghadhabu nyingi na lengo lake ni kuiharibu dunia kwasababu anajua muda wake umeisha….funguo atakazopewa atafungua kuzimu na kuyafungulia mapepo ambayo Bwana Yesu aliyafunga yasifanye kazi duniani kwa kipindi Fulani kwasababu yangeleta uharibifu mkubwa sana ambao haujawahi kuwepo!!..Ndio maana kuna umuhimu mkubwa sana wa kumshukuru Mungu kwaajili ya Yesu Kristo, maana kama si yeye sijui tungekuwa wapi leo. Shetani angetupepeta vya kutosha.

Kwahiyo shetani atapewa funguo na atayafungua hayo mapepo yaliyokuwa kifungoni, ambayo ni mabaya kuliko haya yaliyopo huru sasa duniani..Sasa biblia imeyafananisha hayo mapepo na hao nzige tunaowasoma kwenye sura hii…Kumbuka sio nzige kama nzige hawa wadudu tunaowajua watakaotoka kuzimu hapana! Bali ni maroho! Biblia imefananisha mara nyingi roho chafu na roho za wanyama au wadudu..(Kwamfano Ufunuo 16:13 unaweza ukaona jambo hilo….Inasema:  “Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote…”).

Maumivu yao ni kama ya ng’e..roho hizi zitaleta madhara makubwa katikati ya watu..pigo hili litakuwa ni kwa watu wa dunia nzima…Unajua sasahivi kila uovu Fulani unaasisiwa na roho Fulani (au pepo fulani)..Kwamfano ushoga ni mapepo Fulani ya aina hiyo yanawaingia watu na kuwapeleka kwenye ushoga…yasingekuwepo hayo watu kwa hali ya kawaida wasingeweza kuwa mashoga..kadhalika na usagaji, ufanyaji masturbation, uuaji, wizi, usengenyaji, n.k yote hayo ni mapepo.

Ili kuelewa vizuri kama wewe ni mdadisi wa kifaa kinachoitwa computer au simu, utagundua kuwa unaponunua computer au simu inakuwa na mambo machache sana…ili kuiongezea uwezo inakubidi kudownload baadhi ya programs au softwares ili iweze kwenda kama unavyotaka wewe..utagundua kuwa ili sauti iweze kusikika vizuri, au ili uweze kuongeza milio ya simu, au uweze kuwasiliana na watu kisasa n.k inakubidi udownload applications au software kwenye simu yako au computer yako..sasa hizo applications au softwares unazoziongeza kwenye simu yako ndio mfano wa mapepo ambayo shetani anayaongeza ndani ya watu ili waweze kuwa mashoga, wauaji, wazinzi, walawiti n.k

Sasa katika siku hizo yatakapofunguliwa, zitazalika tabia duniani ambazo hazipo duniani leo…pengine utaanza kuona watu wanaanza kula nyama za watu, au utaanza kuona watu wanaanza kuwa na uwezo wa ajabu wa kipepo, ukatili wa ajabu utaongezeka ambao haujawahi kuonekana hapo kabla, pengine utaona watu wanafanya uzinzi mabarabarani bila aibu,..na kuzuka baadhi ya magonjwa ambayo ni mapya, ya mateso kushinda saratani au ukimwi,..pengine utaanza kuona na wanyama pia wanabadilika tabia, hawafugiki tena, nk n.K, siku hizo ndizo  watu watatamani kufa lakini biblia inasema mauti itawakimbia. Kila mtu ataona hakuna maana ya maisha tena, duniani hakukaliki hofu ya kila kitu.

Na kwenye ule mstari wa mwisho biblia inasema wanaye mfalme naye ni malaika wa kuzimu..jina lake kwa kiebrania ni Abadoni na kwa kiyunani ni Apolioni…Abadoni maana yake ni “MAHALI PA UHARIBIFU”. …na Apolioni maana yake ni “MUHARIBIFU”…Majina yote haya mawili yanamzungumzia ‘shetani’ ambaye ndiye mwaribifu na kila aina ya uharibifu unatoka kwake. Yeye ndiye mfalme wa kuzimu na mfalme wa hawa malaika walioachiwa kutoka kuzimu.

Na ndio maana ni vizuri kutengeneza mambo yako sasa, angali neema ya Kristo ipo, huko mbeleni ni vilio na maombolezo kwa watakaokosa unyakuo.

Tukiendelea na mistari inayofuata biblia inasema…

Ufunuo 9: 12 “Ole wa kwanza umekwisha pita. Tazama, bado ziko ole mbili, zinakuja baadaye.

13 Malaika wa sita akapiga baragumu, nikasikia sauti moja iliyotoka katika zile pembe za madhabahu ya dhahabu iliyo mbele za Mungu,

14 ikimwambia yule malaika wa sita aliyekuwa na baragumu, Wafungue nao malaika wanne waliofungwa kwenye mto mkubwa Frati.

15 Wale malaika wanne wakafunguliwa, waliokuwa wamewekwa tayari kwa ile saa na siku na mwezi na mwaka, ili kwamba waue theluthi ya wanadamu.

16 Na hesabu ya majeshi ya wapanda farasi ilikuwa elfu ishirini mara elfu kumi; nilisikia hesabu yao.

17 Hiyo ndivyo nilivyowaona hao farasi katika maono yangu, nao waliokaa juu yao, wana dirii kifuani, kama za moto, na za samawi, na za kiberiti; na vichwa vya farasi hao ni kama vichwa vya simba, na katika vinywa vyao hutoka moto na moshi na kiberiti.

18 Theluthi ya wanadamu wakauawa kwa mapigo matatu hayo, kwa moto huo na moshi huo na kiberiti hicho, yaliyotoka katika vinywa vyao.

19 Kwa maana nguvu za hao farasi ni katika vinywa vyao, na katika mikia yao; maana mikia yao ni mfano wa nyoka, ina vichwa, nao wanadhuru kwa hivyo.

20 Na wanadamu waliosalia, wasiouawa kwa mapigo hayo, hawakuzitubia zile kazi za mikono yao, hata wasiwasujudie mashetani, na sanamu za dhahabu na za fedha na za shaba na za mawe na za miti, zisizoweza kuona wala kusikia wala kuenenda.

21 Wala hawakuutubia uuaji wao, wala uchawi wao, wala uasherati wao, wala wivi wao”.

Katika mstari wa 14 tunaona ikitolewa amri ya kufunguliwa kwa wale malaika wanne waliokuwa wamefungwa katika Mto Frati. Na hawa lengo la kuzuiwa katika Mto Frati ni ili wasilete madhara waliyoamriwa kuleta kabla ya wakati kufika, kwamba wakati ukifika waue theluthi ya wanadamu wanaoishi juu ya nchi…Ili tujue hawa malaika ni wapi…turudi nyuma kidogo kwenye ufunuo Mlango wa 7.

Ufunuo 7: 1 “Baada ya hayo nikaona malaika wanne wamesimama katika pembe nne za nchi, wakizizuia pepo nne za nchi, upepo usivume juu ya nchi, wala juu ya bahari, wala juu ya mti wo wote.

2 Nikaona malaika mwingine, akipanda kutoka maawio ya jua, mwenye muhuri ya Mungu aliye hai; akawapigia kelele kwa sauti kuu wale malaika wanne waliopewa kuidhuru nchi na bahari,

3 akisema, Msiidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao”.

Malaika hao wanne waliokuwa wamezuiwa kwenye mto Frati ndio hawa hawa ambao walionekana wamesimama kwenye pepo nne za nchi, wakizizuia pepo nne za nchi, Na pepo hizi nne ni upepo wa KI-SIASA, upepo wa KI-DINIKI-UCHUMI na KI-JESHI. Hizo ndio pepo 4 za nchi.

Malaika hawa waliwekwa kuzuia vita vikuu vya Harmagedoni visitokee juu ya nchi.. Kwahiyo walikuwa wanazuia shughuli zozote za kipepo zisifanye kazi juu ya siasa ya dunia, uchumi wadunia, dini ya dunia wala jeshi la dunia, lakini sasa wakati huu, wataruhusu shetani aingie kuvuruga siasa ya dunia, uchumi, dini pamoja na jeshi…Yale mapepo yaliyotoka kuzimu yatawaingia wanasiasa wa dunia, sasa kuanzia wakati huu kutakuwa hakuna kuelewana duniani, kutakuwa hakuna kuvumiliana tena…mipango ya vita itawekwa, na amani itavurugika kwa kiwango kikubwa sana…Na ndio maana unajiuliza kwanini Leo mataifa makubwa yanagombana lakini hayapigani, nikwasababu malaika hawa wameamuriwa wazuie machafuko, lakini wakati utafika hakutakuwa na kuzuiwa tena, vitendo vitafuata.

Biblia inasema zaidi ya wanajeshi milioni 200 (elfu ishirini mara elfu kumi), watahusika katika mapambano ya vita hiyo ya Harmagedoni… “na vichwa vya farasi hao ni kama vichwa vya simba, na katika vinywa vyao hutoka moto na moshi na kiberiti.” Mstari huu unazungumzia aina za silaha zitakazotumika wakati huo, farasi anawakilisha silaha za kijeshi kama ndege za vita, vifaru, helicopter za mabomu ya atomiki n.k na kama hapo inavyosema katika midomo yao inatoka moto, moshi na kiberiti…inazungumzia mabomu, na makombora yatokayo kwenye vifaru hivyo, ndege hizo, nk na walikuwa na vichwa kama vya simba, kama vile simba angurumapo atafutapo mawindo na silaha hizi zitakuwa na mingurumo zitumiwapo.

Kwahiyo katika baragumu hili la sita ndio utakuwa mwanzo wa maandalizi ya vita ya tatu ya dunia…Vita ya Mungu mwenyezi, (Harmagedoni). Ambayo tutakuja kuisoma vizuri katika Kile kitasa cha sita katika Ufunuo ule mlango wa 16. Wakati huu machafuko ya mataifa yatakuwa mengi sana duniani. 

Kristo yupo mlangoni, umefanya uteule wako na wito wako imara sawasawa na 2 Petro 1:10?. Kama sivyo jitazame mara mbili, kisha chagua mwisho mwema, mambo haya sio hadithi tu za kale ni mambo ambayo yatakuja kutokea dhahiri mbele ya macho ya watu wengi.

Bwana akubariki. Kwa Mwendelezo >>>Ufunuo: Mlango wa 10. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

VIFUNGO VYA GIZA VYA MILELE.

DANIELI: MLANGO WA 1

UMEFUNGWA KATIKA GIZA NA UVULI WA MAUTI?


Rudi Nyumbani:

Print this post