Ni rahisi kudhani kuwa watu wote walio waovu, au wauaji au wanaofanya vitendo vya giza kama vile uchawi ni mambo ambayo walizaliwa kuyapenda, na hiyo wakati mwingine inapelekea hata maombi yetu kwa Mungu tunayoyaelekeza kwao ni ya kifo tu, na si kingine. Lakini hatujui kuwa wengi wao wanaofanya mambo kama hayo mwanzoni hawakuwa na nia ya kuwa wachawi, au wauaji, bali ilitokea kuna wakati waliingiwa na tamaa ya kitu Fulani labda tuseme mali, na ndani ya mawazo yao wanafikiria mali tu na si kingine, huo ndio mtengo mkubwa shetani anaowanasia watu kwasababu biblia ilishasema katika..
1Timotheo 6.10 “Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni KUPENDA FEDHA; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.”
Unaona sasa katika kuhangaika kwao ndio wanajikuta kidogo kidogo wanaanza kwenda kwa waganga, na kule kwa mganga anapewa labda masharti Fulani ambayo yanamgharimu kuwa mshirikina, na kwa jinsi siku zinavyozidi kuendelea, kwa kuwa lengo la shetani ni kumvuta kwake ili awe mtumishi wake wa UHARIBIFU hivyo anampa vitu anavyovihitaji kwa muda na baadaye analazimishwa kuwa mchawi na huko ndiko anapopewa majukumu makubwa hata ya kutoa roho za watu ili tu aendelee kuishi na kwamba asipofanya hivyo yupo katika hatari ya kuuliwa yeye naye, sasa hatua hiyo aliyofikia hata akijaribu kutoka hawezi, haoni pa kukimbilia, hivyo anajikuta anamalizia kuendelea tu hivyo hivyo huku dhamira yake ikiugua kila siku akifahamu kuwa anayofanya sio sahihi, lakini hawezi kutoka kwasababu ameshaingia katika mtego asioweza kujinasua tena..
Na sisi kwa kuwa hatuna jicho lingine la mbali katika ulimwengu wa roho tunawaombea kifo,.Hatujui kuwa chanzo cha mambo yote ni ibilisi. Kadhalika unakuta na mtu mwingine alijiingiza katika kazi za ujambazi, lengo lake halikuwa kuuwa watu, hapana bali ni kupata mali, sasa hajui kuwa kumbe ni lengo la shetani kumfanya awe muuaji, pasipo kufahamu yeye anaingia huko, na mwisho wa siku katika harakati zake za wizi, siku moja pale anapoona kuwa anakaribia kukamwata analazimika kutoa bunduki na kumpiga mtu na kumuua pasipo yeye mwenyewe kupenda kwa lengo la kujilinda. Lakini sisi huku tunasema Yule jambazi ni katili sana, hana hata huruma.
Kadhalika wapo watu wengine ambao sio wachawi na wala sio wafanyaji wa vitendo viovu, lakini shetani naye anafanikiwa kuwanasa katika mitego yake ya uharibifu.
Kwamfano ngoja nikupe kisa kimoja ambacho kimetokea hapa mtaani kwetu wiki hii.
Kuna kijana mmoja mdogo tu kama miaka 18, ni kijana ambaye ni mtulivu, hakuwa mlevi wala mtumiaji wa sigara, wala hakuwa katika vikundi vya vijana waporaji wa mitaani, lakini ghafla siku ya jumapili tulipata habari kuwa amejinyonga kwa kamba ndani kwao. Na kule kwenye msiba kulikuwa na mtu mwingine aliyehudhuria msibani naye anasema ndugu yake wiki hii hii kajinyonga. Sasa Kama ukichunguza watu wa namna hii vyanzo vinavyowapelekea wao mpaka kufikia hatua hiyo ngumu namna hiyo za kujitoa uhai hazijulikani..
Kwamfano huyu kijana wa kwanza alishawahi kujaribu kujiua mara mbili, haukufanikiwa moja alijaribu kumvamia dereva wa dalala ili aachie usukani gari lipinduke watu wafe pamoja naye kwenye gari, lakini alishikiliwa na watu, na baadaye kupigwa sana nusu kuuawa, na mara ya pili tena alikunywa sumu lakini walimuwahi akapona.
Sasa kwa namna ya kawaida kwa nje, ni rahisi kusema hawa watu ni WAJINGA, WAUAJI, au WANA DHAMBI NYINGI, WAKATILI, MASHETANI n.k. pasipo kujua kuwa wamenaswa katika mitego ambayo hawawezi kutoka kiuwepesi kama wewe unavyodhani na ndio maana wamelazimika kufanya hivyo, sio kwa hiari yao bali ni sababu ya vifungo vya giza kutoka kwa yule adui zimewafanya kuwa hivyo au kufanya vitendo kama hivyo.
Nguvu hiyo hiyo ilimnasa hata mmoja wa mtume wa BWANA wetu YESU KRISTO, naye ni Yuda, ambaye yeye ndio kabisa alikuwa anakula na kutembea na Bwana kila mahali je! Si zaidi kutunasa na sisi watu wa kawaida tusipokuwa makini?. kumbuka lengo la Yuda halikuwa kumsaliti Bwana ili auawe, hapana bali lilikuwa ni fedha tu basi, lakini kwasababu shetani alikuwa anaona mbali akijua kabisa Yuda atajutia kwa tendo lile na kisha baadaye amshawishi ajinyonge hivyo akatumia udanganyifu wa mali kumvuta kwake, na aliponaswa, akiona kuwa maji tayari yameshamwagika hayawezi tena kuzoleka. sasa ile nguvu ya adui ndipo ilipoanza kufanya kazi ndani yake kumpa sababu ya yeye kujiondoa uhai wake..Usidhani ni rahisi kujinasua unapofika katika hatua kama hiyo..Ni ngumu sana hapo inahitaji mkono wa Mungu ulio hodari..Lakini Yuda alizidiwa mpaka kufikia hatua ya KUJINYONGA.
Watu wa namna hii wapo wengi, wamenaswa katika mitego ya adui ya namna mbali mbali na hawawezi kutoka, inawezekana wewe unayesoma habari hii ni mmojawapo. Imefika hatua umezama kwenye uchawi na ushirikina wa viwango vya juu na unaona ni ngumu kutoka tena huko, umezama katika uuaji, umetoa mimba nyingi, umeua watu na shetani anakuambia kuwa wewe dhambi yako haiwezi kusameheka tena, na hivyo unahitaji njia ya kuutoa uhai wako, pengine umekata tamaa ya kuishi baada ya kugundua kuwa umeambukizwa ukimwi au unaugonjwa wa kufisha kama saratani, hivyo kila siku unatamani roho yako itoke usiendelee kuishi tena unatamani hata upate ajali ufe. Ndugu usifanye hivyo yupo tabibu anayeweza kuuganga moyo wako na kukufanya kuwa upya tena kana kwamba hukuwahi kutenda dhambi yoyote, kana kwamba hukuwahi kuumwa, au kumkosea Mungu.
Kama yeye mwenyewe anasema WENYE AFYA HAWAHITAJI TABIBU, BALI WALIO HAWAWEZI.(Mathayo 9:12).Huhitaji kudhani kuwa tatizo lako halina mtetezi..Kumbuka moja ya makusudi maalumu Bwana YESU yaliyomleta duniani ni pamoja na hiyo ya kuwaganga waliovunjika mioyo, na waliofungwa kufunguliwa kwao. Na hakuna yoyote mwingine zaidi yake anayeweza kuwa na hiyo Taaluma.
Isaya 61: 1 “Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao”.
Yeye pekee ndiye anayeweza kukupa wewe tumaini la uzima, haijalishi umeasi kiasi gani, haijalishi umefungwa katika vifungo vikubwa kiasi gani haijalishi umeshajiunga katika vikundi vya kichawi (occultic groups) vingi kiasi gani, haijalishi umeloga au umehudhuria kwa waganga wengi kiasi gani, haijalishi umeuwa na umetoa mimba nyingi kiasi gani, haijalishi una ugonjwa wa mauti kiasi gani ambao uliupata kwa kutokana na uzembe wako wa kuzini ovyo, hiyo haijalishi embu soma hapa:
Zaburi 107: 10 “Waliokaa katika giza na uvuli wa mauti, Wamefungwa katika taabu na chuma,
11 KWA SABABU WALIYAASI MANENO YA MUNGU, WAKALIDHARAU SHAURI LAKE ALIYE JUU.
12 Hata akawadhili moyo kwa taabu, Wakajikwaa wala hakuna msaidizi.
13 WAKAMLILIA BWANA KATIKA DHIKI ZAO, AKAWAPONYA NA SHIDA ZAO.
14 ALIWATOA KATIKA GIZA NA UVULI WA MAUTI, AKAYAVUNJA MAFUNGO YAO.
15 Na wamshukuru Bwana kwa fadhili zake, Na maajabu yake kwa wanadamu.
16 Maana ameivunja milango ya shaba, Ameyakata mapingo ya chuma.”
17 WAPUMBAVU, KWA SABABU YA UKOSAJI WAO, Na kwa sababu ya maovu yao, hujitesa.
18 Nafsi zao zachukia kila namna ya chakula, Wameyakaribia malango ya mauti.
19 Wakamlilia Bwana katika dhiki zao, Akawaponya na shida zao.
20 HULITUMA NENO LAKE, HUWAPONYA, HUWATOA KATIKA MAANGAMIZO YAO”.
Bwana leo atalituma Neno lake na kukuponya kama utakuwa tayari kumruhusu yeye ayabadilishe maisha yako. Uwe tu tayari kutubu dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha kabisa, uwe tayari kusema kuanzia leo mimi na ulimwengu basi, mimi na shetani basi, mimi na dhambi basi namgeukia Bwana Yesu, tumaini langu, kisha ukishatubu hatua inayofuata ni kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO ili upate ondoleo la dhambi zako, popote pale upendapo. Na kuanzia hapo na kuendelea Bwana atakupa uwezo wa kipekee wa kumshinda adui, hayo mapepo yaliyokufunga na yaliyokuwa yanakutishia kukuua yataondolewa na YESU mwenyewe,bila hata kutumia nguvu. huo ugonjwa wa mauti wanaosema hauponyeki YESU KRISTO atakuponya, hiyo hofu ya kutokusamehewa iliyo ndani yako na inayokutaka ujiue,jua tu ni ibilisi ndio kaiweka na Yesu pekee ndio ataiondoa.. Hivyo chukua uamuzi sasa maadamu damu ya Yesu ipo kukuganga, usisubiri baadaye au kesho, saa ya wokovu ni sasa.
Mathayo 11:28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; NANYI MTAPATA RAHA NAFSINI MWENU;
30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.”
RAHA YA NAFSI YAKO UTAIPATA KWA YESU TU PEKEE.
Ubarikiwe sana.Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
1 Timotheo 4 : 1 “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;”
Biblia inasema, nyakati za mwisho wengine, watajitenga na IMANI, Imani inayozungumziwa hapo si imani nyingine zaidi ya Imani katika Yesu Kristo.
Mungu alimuumba mwanadamu na sehemu mbili, Sehemu ya Roho na Sehemu ya mwili.
Sehemu ya mwili ndio hii tunayoiona kwa macho, milima, mabonde, miti, nyumba, bahari, wanadamu, wanyama n.k. Na sehemu ya Roho hatuioni kwa macho, imefungwa kwetu wanadamu.
Sehemu hii ya Roho ndio mahali Mungu, anapoonekana, na ndio mahali malaika wanapoonekana na ndio mahali shetani na malaika zake wanapoonekana, ndio mahali vita vinapopiganwa na ndio mahali vyanzo vya mambo yote vinapotokea.
Sasa baada ya Adamu kuanguka, Bwana hajaruhusu tuingie katika ulimwengu wa Roho, hakuruhusu macho yetu ya Roho yafumbuliwe tuone kila kitu kinachoendelea katika ulimwengu wa Roho.Na endapo tungefumbuliwa macho tuone mambo gani yanaendelea katika ulimwengu wa Roho duniani kusingekuwa mahali pa kukalika, kwasababu tungekuwa tunaona mambo mengi mno ya ajabu, na kila siku tungekuwa tunaona mambo mapya. Tungekuwa tunaona mambo mengine ambayo yangekuwa hata hayatusaidii..Ingekuwa ni dunia iliyojaa vurugu mno. Kwasababu ulimwengu wa Roho umejaa mambo mengi.
Tuchukue mfano, wakati ule Nabii Elisha alipomwomba Mungu amfungue macho Yule mtumwa wake, na alipofunguliwa macho aliona kilima chote kimejaa jeshi la malaika wenye upanga..Sasa kumbuka malaika hata siku moja hawapigani na wanadamu, bali wanashindana na majeshi ya mapepo wabaya.. kwahiyo kama kulikuwa na majeshi ya malaika wa mbinguni, ni wazi kuwa yalikuwepo pia majeshi ya mapepo yaliyokuwa tayari kushindana na lile jeshi la malaika, kwahiyo kama Bwana angeruhusu Yule mtu aendelee kuona yale mambo ya rohoni ni wazi kuwa angeona vita viwili vinaendelea, vya kwanza vya malaika na vya pili vya wanadamu.
2 Wafalme 6: 15 “Hata asubuhi na mapema mtumishi wake yule mtu wa Mungu alipoondoka, na kwenda nje, kumbe! Pana jeshi la watu, na farasi na magari, wameuzingira mji ule. Mtumishi wake akamwambia, Ole wetu! Bwana wangu, tufanyeje?
16 Akamjibu, Usiogope; maana walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao.
17 Elisha akaomba, akasema, Ee Bwana, nakusihi, mfumbue macho yake, apate kuona. Bwana akamfumbua macho yule mtumishi; naye akaona; na tazama, kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zote”.
Kwahiyo unaweza ukaona kuwa ulimwengu wa Roho, wa malaika upo, na una mambo mengi mno, yasiyoelezeka na mengine ni magumu kuyatambua, yamekaa kimafumbo jaribu kufikiri Yohana aliyeandika kitabu cha ufunuo anaona malaika wana Uso wa TAI, mwingine ana kichwa cha NDAMA, mwingine ana kichwa kama cha SIMBA na bado wana mabawa, na wana kwato!! Umewahi kujiuliza hivyo viumbe endapo tukiwa tunaviona kila siku duniani kutakuwaje?? Nabii Ezekieli naye alionyeshwa mambo hayo hayo,Nabii Isaya naye alionyeshwa mambo hayo hayo, lakini hawakuyaelewa kwa undani mambo hayo kwasababu ni mambo ya Rohoni.
Kwahiyo ni wazi kuwa Sio mpango wa Mungu, tuwe na uwezo kila dakika kuyaona mambo ya rohoni, vinginevyo maisha yatakuwa hayana maana.
Lakini maandiko yanasema “ Yohana 4.23 Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. 24 MUNGU NI ROHO, NAO WAMWABUDUO YEYE IMEWAPASA KUMWABUDU KATIKA ROHO NA KWELI.”
Sasa hapa ndipo pa kuzingatia sana, maana pasipoeleweka vizuri, ni rahisi shetani kumzamisha mtu katika MAFUNDISHO YA MASHETANI.
Biblia inasema “saa yaja ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli”
Biblia iliposema “katika roho na kweli” haikumaanisha kuwa itafika wakati tutakuwa tunazama katika ulimwengu wa roho na kufikia kumwona Mungu na malaika, na hatimaye kumwabudu tukiwa tunamwona wazi kama tunavyowaona mwanadamu wenzetu.. Hapana haikumaanisha hivyo…
Na Shetani ndipo alipoanzia hapa kupandikiza mafundisho yake ya mashetani.
Nini maana ya kumwabudu Mungu katika ROHO NA KWELI?
Kabla ya kujua maana ya kumwabudu Mungu katika roho na kweli, hebu turudi nyuma kidogo…Kumbuka kama tulivyosema ulimwengu wa Roho ni ulimwengu wa Malaika, ikiwa na maana kuwa vita vyote na mambo yote yanayoendelea katika ulimwengu wa Roho Mungu huwa anawatumia malaika zake kuyafanikisha, mambo hayo namna ya kuyafanya na jinsi ya kuyafanya hayamuhusu mwanadamu hata kidogo sio sehemu ya mwanadamu..Ni kazi ya malaika Kwamfano Mungu alipomtuma Malaika Gabrieli kwa Mariamu kumpa taarifa za kuzaliwa kwa Mwokozi Bwana Yesu Kristo namna ya kuitengeneza ile mimba tumboni mwa Mariamu pasipo Mwanaume kuhusika haikuwa kazi ya Mariamu, au mwanadamu yoyote yule bali ilikuwa ni kazi ya Malaika wa Mungu katika uwezo wa Roho.
Mungu alipoyaleta yale mapigo yote kwa farao, na kuwaongoza katika lile jangwa kimiujiza haikuwa kazi ya mwanadamu kuyatengeneza yale mapigo..mwanadamu alikuwa na kazi yake tutakuja kuiona mbele kidogo.
Kadhalika kazi ya kuleta tauni katikati ya watu wakati wa Mfalme Daudi haikuwa kazi ya wanadamu bali ilikuwa ni kazi ya Malaika wakifanya kazi katika ulimwengu wa roho..Hao ndio Bwana aliowatia mafuta kuweza kufanya mambo makubwa yasiyowezekana kwa namna ya kawaida.
Sasa mwanadamu ambaye anamcha Mungu hajapewa maarifa hayo, mwanadamu anayemcha Mungu hajapewa uwezo wa kuingia kwenye ulimwengu wa roho na kutengeneza mambo au kuingia na kupambana na roho za malaika walioasi.
Sasa uwezo mwanadamu anayemcha Mungu aliopewa na Mungu ni mwongozo wa namna ya kuwafanya hawa malaika waweze kumhudumia yeye. Mwongozo wa namna ya kutembea na kundi hili la malaika watakatifu.
Ni sawasawa na mwanadamu na Farasi, mwanadamu hajapewa uwezo wa kukimbia kwa kasi kama farasi, hajapewa mapafu kama ya farasi, lakini amepewa uwezo wa kumwongoza Yule farasi amtii yeye ampeleke katika mwendo anaotaka..
Na huo mwongozo mwanadamu aliopewa utakaomsaidia yeye kutembea na malaika walio na nguvu na uwezo katika ulimwengu wa Roho ni BIBLIA TAKATIFU (yaani NENO LA MUNGU). Ni kama tu Mtu asiyekuwa na MANUAL ya kuendesha gari, hataweza kuliendesha gari hilo hata iweje, kadhalika mtu ambaye hajafundishwa namna ya kumpanda farasi na kumwendesha hataweza kumwendesha, badala yake anaweza akajikuta hata akajeruhiwa na Yule farasi farasi.
Naamini kidogo kidogo utakuwa umeshaanza kuelewa nini maana ya kuingia katika ROHO…Kwahiyo maana ya kuingia katika roho sio kugeuka na kuanza kujifananisha na malaika, au mapepo hapana bali ni kuelewa uwezo uliopewa wa kutembea na malaika ambao hao ndio wanaojua namna ya kutengeneza mambo katika ulimwengu wa roho.
Kwasababu hiyo basi Mwanadamu anayemcha Mungu hawezi akajua njama za adui zote na elimu yake kwa mapana na marefu, hawezi akajua idadi ya mapepo yaliyopo, hawezi akajua yanafanyaje fanyaje kazi..malaika watakatifu ndio wanaojua (wamepewa uwezo huo na Mungu mwenyewe) ..Sisi tunachojua tu tukitaka tulindwe na Yule adui Kwanza tumwamini Bwana Yesu Kristo, kisha tukabatizwe kisha tuishi maisha matakatifu na ya uangalifu, tukidumu katika kusali na ushirika. Hiyo inatosha kabisa kuwafanya wale malaika watakatifu watupiganie dhidi ya mapepo wabaya.
Tukitaka tusife tuishi maisha marefu, wale malaika Bwana aliowapaka mafuta katika ulimwengu wa Roho wanajua namna ya kumzuia shetani na mapepo wake wasituguse mpaka tutakapotimiza umri wa kuondoka duniani, hivyo kama maandiko yanavyosema “waheshimu baba yako na mama yako upate siku nyingi na za heri” hivyo wale malaika watakatifu wanatembea na mtu anayelishika neno hilo, na mtu Yule anajikuta anakingiwa na ajali na dhiki za Yule mwovu na kutimiza umri wa maisha yake..Sasa huyu mtu tayari kashaingia katika roho. Anakuwa anamwabudu Mungu katika roho na kweli. Kwasababu maneno ya Yesu Kristo ndio Roho. (Yohana 6:63)
Au mtu wa Mungu anapoumwa wale malaika wanaohusika na uponyaji, waliohusika na kuitengeza mimba ya Mariamu pasipo mwanamume kwa uwezo wa roho ndio hao hao pia wana uwezo wa kuondoa ugonjwa pasipo daktari lakini wanafanya kazi na mtu anayeliaimi neno hili “kwa kupigwa kwake sisi tumepona”.
Kwahiyo hizo ndizo silaha zetu sisi katika ulimwengu wa Roho, kulishika NENO la Mungu pamoja Na kuwa na IMANI katika Neno lake.
Na ndio maana Mtume Paulo alisema katika..
Waefeso 4: 11 “Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.
12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
14 Basi simameni, hali mmejifunga KWELI VIUNONI, na kuvaa dirii ya haki kifuani,
15 na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani;
16 zaidi ya yote mkiitwaa NGAO YA IMANI, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.
17 Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni NENO LA MUNGU;”
Unaona hapo? Ukilijua Neno la Mungu kwa undani,wewe tayari ni Mtu wa rohoni, ambaye unashindana vita visivyoonekana kwa macho na unashinda, hauna haja ya kuona mapepo, hauna haja ya kuona wachawi, hauna haja ya kuona majini, vibwengo, hauna haja ya kumwona hata shetani mwenyewe,..na zaidi ya yote hauna haja ya kuwaona hata malaika..Wao wanafanya kazi zao katika ulimwengu wa roho ambao wewe ndio unaoupalilia kwa kulishika na kuliamini Neno la Mungu..
Sasa mafundisho ya mashetani leo ni yapi?
Mafundisho ya mashetani ni yale yanayokufundisha kwamba unaweza ukaingia katika ulimwengu wa roho na wewe ukashindana na mapepo kama wanavyofanya malaika…Ndio hapo shetani anatumia nguvu kubwa kuwavuta watu wasilijue Neno la Mungu, na kuwafanya wakeshe kutafuta kujua elimu za mapepo, utakuta anawafundisha watu aina za mepepo na majini, na utendaji wao kazi. Wengine wanawafundisha watu wasile vyakula Fulani au wasipande miti Fulani majumbani mwao, kwasababu vina uhusiano wa moja kwa moja na mapepo n.k.
Wengine wanafundisha watu kwamba usiende kuogelewa baharini au mtoni saa 7 au kabla ya kuogelea baharini, kemea kwanza pepo la maji, kwamba kabla ya kupita karibu na makaburi kemea kwanza pepo la mauti lisije likakuingia, unapokaribishwa kwa mtu usiyemjua usile kwanza chakula Fulani, kwamba ukiona mtu kakuamkia na kukuonyesha ishara Fulani, kemea hilo ni pepo la mauti, unapougua kichomi basi umetumiwa jini Fulani n.k..
Unapofika mahali Fulani usipende kutenda wema, nyota yako itachukuliwa n.k nataka nikwambie ndugu hizo zote ni ELIMU ZA MASHETANI.!!
Sisi tuliompa Bwana Yesu Kristo maisha yetu tunafahamu Neno moja tu!! Nalo ni hili “Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, Wala hapana uganga juu ya Israeli. Hesabu 23:23”. Hiyo ndio silaha tuliyo nayo sisi..Ni namna gani inatenda kazi?? Hatujui Malaika ndio wanaojua…wao ndio wanaojua kuna aina ngapi za vibwengo, na wachawi, na mapepo na namna ya kuwashughulikia sisi sio kazi yetu kujua aina za mapepo na utandaji kazi wao…
Tunapotenda wema na kuambiwa nyota zetu zitachukuliwa…hilo hatulijui sisi tunachojua ni kwamba.. “hakuna hata unywele mmoja wa vichwa vyetu utakaopotea, na nywele zetu zote zimehesabiwa Luka 21:18” Ni kwa namna gani hilo linatenda kazi? Hiyo sio kazi yetu kujua, Malaika watakatifu ndio waliobobea katika mambo ya rohoni hao ndio wanazo hizo teknolojia ya kuzihifadhi nyota zetu kama zipo, sisi hatuna huo uwezo. Sisi kazi zetu ni kulishika Neno lake tu!
Biblia inatuonya hizi elimu/mafundisho siku za mwisho yatakuwa mengi, yakiwatoa watu katika Imani lengo ni kuwafanya watu wajitenge na Imani, . Na badala ya kumfungua mtu, utakuta ndio zinamfunga na kumfanya awe mwoga wa wokovu wake, Hata siku moja Mungu hamletei mtu hofu, bali ujasiri, utakuta watu wamehama nyumba zao kwa kuogopa zimezindikwa na wanahubiriwa hivyo na wanaojiiita watumishi. Wengine kila kukicha ni kufundishwa utendaji kazi wa mapepo tu!! Kila kitu kitakachokuja mbele yako ni kukemea, ukiingia hospitali kemea, kabla ya kulala mwaga damu ya Yesu chooni, mapepo yasikuvae, saa kumi jioni majini aina Fulani yanafunguliwa hivyo usipende kula kitu Fulani huo wakati. Na mambo mengine mengi yanayofanana na hayo, kila kitu ni mapepo mapepo tu!!
Dada/Kaka unayesoma haya, tafuta kulijua Neno la Mungu na kuliamini, hayo mengine sio kazi yetu kujua, Mtafute Bwana alisema katika Neno lake Maneno yake ndiyo Roho na Uzima(Yohana 6:64)…na maneno yake sio mengine zaidi ya Biblia takatifu, kwahiyo kwa lugha nyingine unaweza kusema biblia takatifu ndio Roho na uzima..Hivyo kuwa mtu wa rohoni ni kuyaishi na kuyaamini maneno ya Yesu Kristo 100% na si kingine.
Kama unataka leo hii uwe mtu wa rohoni, mtii leo maneno yake anayokuambia, kwa kukusudia kutubu dhambi zako kabisa kwa kumaanisha kuacha uasherati wako, kwa kukusudia kuacha pombe zako, uvaaji wako mbaya {vimini, surali,wigi,wanja,lipstick, herein n.k}, kwa kumaanisha kuacha wizi wako, utukanaji wake, rushwa zako, usengenyaji wako n.k Ili uwe na uhakika wa kuurithi ufalme wa mbinguni na kuruhusu Malaika wa Bwana watembee na wewe siku zote za maisha yako, na kuepukana na mafundisho ya mashetani
Mungu akubariki
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Kama umempa Bwana maisha yako, tafadhali tangaza habari zake kwa kadri uwezavyo kwa watu wengine wasiomjua yeye.
Mada zinazoendana
DHAMBI ILIYOMKOSESHA SHETANI NI IPI?
HUDUMA KUMI (10) ZA SHETANI DUNIANI NI ZIPI?
Wafilipi 4.10 “Nalifurahi sana katika Bwana, kwa kuwa sasa mwisho mmehuisha tena fikira zenu kwa ajili yangu, kama vile mlivyokuwa mkinifikiri hali yangu lakini hamkupata nafasi.
11 Si kwamba nasema haya kwa kuwa nina mahitaji; maana nimejifunza kuwa radhi na hali yo yote niliyo nayo.
12 Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yo yote, na katika mambo yo yote, NIMEFUNDISHWA kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa.
13 Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu”.
Katika maandiko haya Mtume Paulo, anasema AMEFUNDISHWA kushiba na kuona njaa…Hebu litafakari hilo neno kwa undani “NIMEFUNDISHWA”. Kufundishwa maana yake ni kupewa maarifa ambayo ulikuwa huyajui, hivyo ni wazi kuwa Mtume Paulo kuna wakati alikuwa hajafundishwa baadhi ya mambo mpaka ulipofika wakati Fulani wa kupokea mafundisho za dizaini hiyo..
Na moja ya mambo hapa ambayo Mtume Paulo anasema amefundishwa ni hili la “KUSHIBA NA KUONA NJAA”. Ikiwa na maana kuwa kuna wakati Mungu alimpitisha katika kipindi cha uhitaji mkubwa (kipindi kikali cha kuona njaa) ili amfundishe huko.. Na kuna wakati pia Mungu alimpitisha katika kipindi cha kushiba ili pia ajifunze.
Kwahiyo tunaona kuwa mojawapo ya tabia ya Mungu ni kumpitisha Mtu katika VIPINDI VIWILI, vya KUSHIBA na KUONA njaa. Vipindi vya KUPUNGUKIWA na KUWA NA VINGI, Vipindi vya kupandishwa juu na vipindi vya kushushwa.(Mhubiri 3). NIA NA MADHUMUNI YA MUNGU..NI ILI TUFIKIE MAHALI TUWE RADHI NA VITU TULIVYONAVYO. Tufikie mahali tusipepesuka na hali yoyote tutakayokutana nayo katika siku za usoni.
Unajua kuna tabia moja Fulani ambayo baadhi ya majeshi mengi duniani wanayo, pindi wanapomsajili mwanachama mpya katika jeshi huwa wanamchukua Yule mtu kwasababu ndio kajiunga kwa mara ya kwanza,hajui kanuni cha jeshi, wanamchukua na kuanza kumwonea au kumfanyia mambo ya kumuudhi…utaona kafika tu kesho yake, anaanza kupigwapigwa pasipo sababu, pengine ametulia tu hajafanya kosa lolote anajikuta mtu anatokea na kuanza kumtukana pasipo sababu na kumshurutisha kufanya jambo Fulani, utakuta kalala na mtu anakuja kumwamsha na kumpiga bila sababu, na mambo mengi mabaya ya kuudhi hapo hakuna wa kumsaidia. Sasa huo ndio umekuwa utaratifu wa majeshi mengi duniani kufanya hivyo, nia na makusudi yao sio kumtesa Yule mgeni, au kumwonea hapana bali kumtolea ndani yake “ile hasira ya asili (kupanic) ambayo kila mtu anakuwa amezaliwa nayo ” Ili kumpa uwezo wa kustahimili mambo magumu atayoweza kukutana nayo katika vita.
Kwahiyo utaona mara za kwanza anapigwa, na kuanza kunung’unika saa hiyo hiyo, na wakati mwingine kurudisha mapigo au matusi au kununa kwa muda mrefu, na kutengeneza kinyongo lakini siku zinavyozidi kwenda anakuwa anazoea zile hali hivyo hata akifanyiwa hayo mambo mara nyingi vipi anajikuta hapaniki tena kama zamani, anakuwa kawaida, haumii moyo tena kama alivyokuwa anaumia..Hiyo inamsaidia Yule mwanajeshi akiwa vitani atumie AKILI ZAIDI KULIKO HISIA. Kwahiyo hayo ni moja ya mafundisho tu ya majeshi ya watu wa Ulimwengu huu. Hicho ndicho kinachomtofautisha mwanajeshi na raia wa kawaida. Utashangaa ni kwanini anaweza akaona ndugu yake mpendwa vitani labda kaka yake kapigwa risasi na kuuliwa, badala ya kuvunjika moyo na kulia pale, yeye ndio atambeba na kumuhifadhi kisha kuendelea na vita kana kwamba hajafiwa..Lakini ukirudi kwa watu wa kawaida mfano msiba umetokea kidogo tu utaona watu wanaanza kupiga mayowe na wengine hata kukufuru..Ni kwasababu gani? Ni kwasababu hawajafundishwa. Hilo tu.
Lakini Kristo naye ana mafunzo yake, kabla ya kumpeleka mtu, katika vita vya kiroho..Na mojawapo ya mafundisho ndio hayo “KUFUNDISHWA KUONA NJAA na KUSHIBA”.
Wana wa Israeli kabla ya kufika nchi ya Ahadi, Bwana aliwapitisha jangwani na wakati mwingine alikuwa anawaacha waone njaa na kiu kwa muda mrefu ili awafundishe. Ili Watakapoingia nchi ya Kaanani wasilalamike watakapopitia mitikisiko kidogo tu. Walikuwa wanatembe jangwa masiku hawaoni maji.
Kumbukumbu 8: 1 “Amri hii ninayokuamuru leo mtaishika kuitenda, mpate kuishi na kuongezeka, na kuingia katika nchi ile ambayo Bwana aliwaapia baba zenu; nanyi mtaimiliki.
2 Nawe utaikumbuka njia ile yote Bwana, Mungu wako ALIYOKUONGOZA MIAKA HII AROBAINI KATIKA JANGWA, ili akutweze, kukujaribu kuyajua yaliyo moyoni mwako, kwamba utashika amri zake, au sivyo.
3 Akakutweza, AKAKUACHA UONE NJAA, akakulisha kwa mana, usiyoijua wewe wala baba zako hawakuijua; apate kukujulisha ya kuwa MWANADAMU HAISHI KWA MKATE TU, BALI HUISHI KWA KILA LITOKALO KATIKA KINYWA CHA BWANA”.
Unaona! Wana wa Israeli kuna kipindi Mungu aliwaacha makusudi waone njaa lakini walikuwa hawafi wala hawaumwi, Ili wajue tu kuwa Mtu anaweza kuishi bila kula vyakula vya kimwilini na asife bali akaishi kwa Neno la Mungu tu.
Na ndio maana Bwana Yesu naye vivyo hivyo alipokwenda mlimani alifunga siku 40 usiku na mchana bila kula, na mwovu alipomjia na kumjaribu ageuze jiwe kuwa mkate..alimpa jibu lile lile kuwa “MTU HATAISHI KWA MKATE TU BALI KWA KILA NENO LINALOTOKA KATIKA KINYWA CHA BWANA”..Kwasababu gani alimjibu vile ni kwasababu “HUKO NYUMA ALISHAFUNDISHWA KUSHIBA NA KUONA NJAA” kwahiyo kwake yeye AWE NACHO au ASIWE nacho vyote ni sawasawa. Awe na chakula asiwe na chakula kwake yeye ni sawa sawa..Anayaweza mambo yote kwa yeye AMTIAYE Nguvu. Anachojua ni kwamba Mungu hatamtupa kabisa.
Na ndio Mtume Paulo naye, hakuwahi kutamani fungu kutoka kwenye makanisa aliyoyazaa yeye kiroho, ingawa angestahili kupata fungu kutoka huko, lakini badala yake ndio anawaambia watu wa kanisa la Filipi ambalo walitamani sana kumuhudumia kwa mali zao..
“Si kwamba nasema haya kwa kuwa nina mahitaji; MAANA NIMEJIFUNZA KUWA RADHI NA HALI YO YOTE NILIYO NAYO.
12 Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yo yote, na katika mambo yo yote, NIMEFUNDISHWA kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa.
13 Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu”.
Hiyo ina maana kuwa HAHUBIRI INJILI YA KRISTO kwasababu anataka FEDHA, au kwasababu ANA FEDHA, hapana Bali anahubiri injili ya Kristo kwasababu ana NIA YA KRISTO NDANI YAKE, AWAVUTE WENGI KWAKE…AWE NACHO ASIWE NACHO KWAKE YEYE NI SAWASAWA Injili ya KRISTO ataendele kuihubiri.
Na sisi je! Tumefundishwa KUWA RADHI NA VITU TULIVYO NAVYO? Kwamba ifikie mahali hatumfuati Bwana Yesu kwasababu tunatafuta utajiri, au mali kutoka kwake, au hatumfuati kwasababu Tuna mali., Yaani ifikie hatua tunasema TUMEFUNDISHWA KUWA RADHI NA VITU TULIVYO NAVYO. Tumefundishwa kuridhika na vitu tulivyo navyo..viwe vingi au vichache tutamtumikia Bwana, tuwe tuna Elimu tusiwe na Elimu kwetu iwe ni mamoja, tuwe matajiri tuwe maskini Thamani ya Kristo Kwangu ni ile ile. Niwe na chochote nisiwe na chochote tutaihubiri injili ya Kristo.
Kama hatujafunzwa hivyo Basi tumwombe Bwana atufundishe masomo hayo ili tuweze kutembea naye pasipo manung’uniko wala malalamiko Kama alivyotembea na Mtume Paulo..Hiyo itatusaidia sisi tunapopitia vipindi vya kupungukiwa tusijione wanyonge, na kuanza kutanga huku na huko, bali tujue ni vya muda tu, sisi tusonge mbele na Imani mpaka kuja kwake YESU KRISTO ambapo yeye mwenyewe atatufariji kwa taabu zetu hapa duniani.
Tafadhali wahubirie wengine habari njema ya Msalaba kwa kadri uwezavyo.
Ubarikiwe.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
JE! SISI KAMA WAKRISTO NI DHAMBI KUSHEHEREKEA KRISMASI?
YOHANA 3:3 “Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.
4 Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?
5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.
6 Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.
7 Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili.
8 Upepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho.”
Jina la Bwana wetu Yesu Kristo lisifiwe daima, Ni siku nyingine tena Bwana aliyotupa kwa neema zake na leo tutaangalia vifungu hivyo ni kwanini Yesu aliifananisha hali ya mtu aliyezaliwa kwa Roho na kama UPEPO UVUMAO.
Yapo mambo matatu hapo Bwana aliyoyasema kuhusu Upepo,
1) La kwanza ni Upepo Huvuma upendako
2) La pili ni: Sauti yake waisikia (lakini hauuoni)
3) Na la tatu ni Hujui utokako wala unakokwenda.
Na mwisho akamalizia kusema “NDIVYO ILIVYO HALI YAKE MTU ALIYEZALIWA NA ROHO”. Hii ina maana gani? Ni wazi kuwa inamaanisha pale Roho wa Mungu anapoingia ndani ya mtu kwa mara ya kwanza basi hali yake inabadilika na kufanana na tabia inayoweza kulinganishwa na tabia ya upepo.
Tabia hizi ni mara tu baada ya mtu kuzaliwa kwa Roho, kwahiyo tunaweza kusema Upepo huo ni Roho mtakatifu ndani ya mtu. Kwasababu ndiye aliyemfanya kuwa hivyo. Kama tunavyofahamu tabia ya upepo, kwanza ni kitu kisichoweza kuonekana kwa macho lakini utaisikia sauti yake pale unapovuma, au utauhisi katika mwili wako pale unapopita karibu na wewe, lakini usijue chanzo chake ni wapi na hatma ya safari yake itaishia wapi!!.
Kadhalika Roho Mtakatifu anapoingia ndani ya mwamini tabia hizi za upepo wa Roho huingia ndani yake. Pale mtu alipoamua na kudhamiria kweli kumpa Kristo maisha yake. Basi kuanzia huo wakati na kuendelea ndani yake kunakuwa na nguvu isiyojulikana chanzo chake ni nini kwa nje! Watu wa nje wanaweza kushangaa mbona huyu mtu tabia yake imebadilika kwa ghafla hivi,wasijue ni nani aliyembadilisha, wakijaribu kachunguza labda ni dini hawaoni, labda ni dhehebu hawaoni, labda ni mwanadamu hawaoni, na ndio hapo utaona maisha ya yule mtu yanabadilika, pengine mambo aliyokuwa anapenda kuyafanya hapo mwanzo yanageuzwa ghafla, maisha aliyokuwa anaishi nyuma yanageuka ghafla, mara nyingine atajikuta anachukia hata kufanya baadhi ya vitu alivyokuwa anavifanya nyuma, anajikuta kiini cha maisha yake ni kumwangalia Bwana YESU tu mahali popote alipo…Baadhi ya mambo yasiyokuwa na maana yataanza kumkera, anaanza kutokujiona kuwa huru akiwa katika vikao vya usengenyaji, tofauti na alivyokuwa hapo mwanzo..
Hii yote inatokea ni kwasababu yule Roho aliye ndani yake humsukuma kufanya vitu ambavyo hata pengine yeye mwenyewe hajui ni kwanini anavifanya, saa nyingine anaweza akadhani ni kwa akili zake anafanya hivyo.Au ni kwasababu ametokea tu kupenda mwenyewe Lakini ukweli ni kwamba sio yeye anafanya hivyo bali ni Roho wa Mungu ndani yake atembeaye kama upepo usioonekana anamwelekeza asikojua yeye.
Atajikuta anaanza kuchukia kupenda pombe, ambapo hapo mwanzo alikuwa anazitamani, anajikuta kuvaa vimini na suruali anajiona kama yupo uchi au anajiaibisha mbele za watu hivyo anajikuta anaanza kupenda kuvaa sketi ndefu ambazo hapo mwanzo alikuwa akivaa anajiona kama mshamba. Anajikuta anatamani kusoma biblia, au kusikiliza Neno la Mungu sana, ambapo hapo kwanza alikuwa hana mpango navyo. Anajikuta kampani za marafiki wa kidunia ni mzigo mkubwa kwake tofauti na jinsi alivyokuwa nyuma. Anajikuta hata akipitia dhiki kubwa kiasi gani kwa ajili ya imani hapepesuki mpaka watu wa nje! Wanashangaa huyu mtu ni wa dizaini gani. N.k.
Na hata baada ya muda mrefu kupita ukimuuliza ilikuwaje kuwaje ukaweza kuacha dhambi na mambo ya kidunia pamoja na majaribu mazito kiasi kile atakwambia kwa kweli sifahamu nguvu hiyo ilitoka wapi,nilijikuta tu ninamsimamo na maamuzi yangu..nilijikuta tu kuna nguvu fulani ndani yangu ikinisukuma kunipeleka sehemu Fulani,sasa huo ulikuwa ni ule upepo wa Roho ambao ulikuwa unampeleka asikotazamia yeye kwenda,.ataishia kukwambia ni neema za Mungu tu.
Na ndio maana katika siku ile ya Pentekoste Roho aliposhuka kwa watu kwa mara ya kwanza Ishara ya kwanza aliyoshuka nayo ni ishara ya UVUMI WA UPEPO uendao kwa kasi, sio kwasababu Mungu alikuwa anataka kuwaonyesha watu uweza wake wa kuamuru tufani, hapana, bali Upepo ule ulifunua jambo kubwa sana katika roho kwa waumini wa kweli waliokuwa Yerusalemu..na ndio maana ukichunguza kwa makini baada ya pale maisha na mienendo ya mitume ilibadilika ghafla tangu ule wakati, walipokea ujasiri usio wa kawaida kuhubiri injili, walijawa na Imani kwa Mungu, hawakuwaogopa maadui zao tena, na kwenda kujificha kama ilivyokuwa pale mwanzo.. Mara nyingi roho alikuwa akiwatwaa na kuwapeleka wasikojua, na huko wanapofika wanalihubiri Neno la Mungu kwa ushujaa mwingi..Tunamwona mtu kama Filipo alitwaliwa na Roho na kupelekwa kule Roho alipopenda kumpeleka.
Matendo 2:1 “Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja.
2 KUKAJA GHAFULA TOKA MBINGUNI UVUMI KAMA UVUMI WA UPEPO WA NGUVU UKIENDA KASI, UKAIJAZA NYUMBA YOTE WALIYOKUWA WAMEKETI.
3 Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao.
4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka”.
Unaona kulikuwa na Upepo wasiojua ulipotoka ,Ule ulifunua UPEPO WA ROHO, ambao ndio ulioathiri maisha yao kuanzia ule wakati na kuendelea.
Unaona umuhimu kwa kuzaliwa kwa Roho? Leo hii ni kwasababu gani huwezi kushinda tamaa, na dhambi, ni kwasababu moja tu, nayo ni hii HAUJAZALIWA MARA YA PILI hivyo ule upepo wa Roho hauwezi ukawa na nguvu juu ya maisha yako. Haujamkaribisha Roho ndani ya maisha yako. Kama ungekuwa umezaliwa kwa Roho ile nguvu ingekusukuma mahali usipojua kama vile UPEPO uvumapo na usingeona kuwa dhambi ni jambo gumu kuliacha kwasababu ni Roho mwenyewe angekuwa anatenda kazi ndani yako.. Nguvu ile Ingekusukuma kule usikoweza kufika, ingekusukuma kutenda mapenzi ya Mungu na kumtazama Kristo kila wakati.
Kumbuka Nikodemo alikuwa ni Farisayo wa mtu dini sana, anayejua maandiko sana lakini hakuwa amezaliwa mara ya pili, unaona? kumbe unaweza ukawa wa kidini na usiwe na Roho Mtakatifu ndani yako. Ndugu Usiridhike na dhehebu lako, au kanisa lako ukajiona kuwa tayari umekamilika na huku unaona kabisa maisha yako ya kikristo yanadorora siku baada ya siku..Na ndio maana maandiko yanasema, MTU ASIPOZALIWA KWA MAJI NA KWA ROHO HAWEZI KUUINGIA UFALME WA MBINGUNI hapo hata kama uwe unayafahamu maandiko kiasi gani, huwezi kuuingia ufalme wa mbinguni, Bwana Yesu anasema hivyo.
Lakini Mtu anazaliwaje kwa Roho na kwa Maji?
Ni kwa kukudhamiria kabisa kutubu na kuacha dhambi na maisha ya kale.Wengi hawafanyi hivyo, toba haitoki moyoni bali midomoni na ndio maana inakuwa ngumu Roho wa Mungu kukaa ndani yao. Na maana ya toba sio kuomba msamaha tu, bali ni KUGEUKA AU KUACHA. Hivyo unapogeuka na kukusudia kuacha dhambi hata usiposema kwa mdomo hiyo tayari ni TOBA, Hivyo ukizingatia hayo na Mungu akishaona nia yako yeye mwenyewe atakuosha “roho yako”, kwa maji (ambayo ni DAMU yake na Neno lake) na kukugawia Roho wake ndani yako atakayekuweza kukusaidia kuishinda dhambi siku zote za maisha uliyopo hapa duniani..
Kama maandiko yanavyosema:
Ezekieli 36: 24 “Maana nitawatwaa kati ya mataifa, nami nitawakusanya na kuwatoa katika nchi zote, na kuwarudisha katika nchi yenu wenyewe.
25 Nami NITAWANYUNYIZIA MAJI SAFI, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote.
26 Nami nitawapa ninyi moyo mpya, NAMI NITATIA ROHO MPYA NDANI YENU, NAMI NITATOA MOYO WA JIWE ULIOMO NDANI YA MWILI WENU, NAMI NITAWAPA MOYO WA NYAMA.
27 NAMI NITATIA ROHO YANGU NDANI YENU, NA KUWAENDESHA KATIKA SHERIA ZANGU, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda.
28 Nanyi mtakaa katika nchi ile niliyowapa baba zenu, nanyi mtakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu.”
Hivyo mambo hayo hayatimiliki pasipo kuambatana na ishara ya wazi ya nje kuonyesha kuwa hicho kilichotendeka nje ndicho kilichofanyika rohoni mwako. Kwahiyo ni lazima mtu akazamishwe kwenye MAJI mengi akabatizwe kwa maji tele,kama Bwana alivyoagiza na ni katika JINA LA YESU, kuonyesha kuwa ameoshwa dhambi zake kwa maji ya Roho, kisha ndipo awe na uhakika kuwa amepokea ubatizo wa Roho Mtakatifu ndani yako.
Hivyo ikiwa haujachukua uamuzi huo fanya hivyo haraka, ili neema hii ipate kuwa juu yako. Na ule UPEPO wa ROHO MTAKATIFU utakuvumisha na kukupeleka usikojua wewe, Na mwisho wake utashangaa umetulia mahali Mungu ambapo alikusudia..na utakuwa na uhakika siku ile kunyakuliwa juu kwenda mbinguni kumlaki Bwana, katika upepo huo wa kisulisuli kama Nabii Eliya.
Chukua muda wako kuwahubiria habari njema za wokovu, ndugu zako, marafiki zako na jamaa zako popote pale ulipo, ili na wao wapone, shetani asipate mazao.
Mungu akubariki.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
JIFANYIE RAFIKI KWA MALI YA UDHALIMU.
HISIA YA MUNGU ILIYO MBAYA KULIKO ZOTE
Mwanzo baada ya Adama na Hawa kuasi, Bwana aliwafukuza kutoka uweponi mwake, ndani ya ile bustani ya Mungu (Edeni)..Lakini tunaona baada tu ya kufukuzwa haikuishia hapo, bali tunaona pia ARDHI ililalaaniwa kwa ajili yao. Ikiwa na maana kuwa kila kinachopatikana kutoka ardhini, kitapatikana kwa tabu kuanzia huo wakati na kuendelea..Ilikuwa ni pigo kubwa kwasababu karibia kila kitu kinatoka ardhini, kwasababu hata mwanadamu mwenyewe anatoka ardhini, na ndio maana hata yeye anapatikana kwa uchungu, na kwasababu hiyo Bwana Mungu alimwambia mwanamke atazaa kwa uchungu..Na sio mwanadamu tu, bali hata wanyama na viumbe vyote hiyo laana iliwapata kwasababu nao pia wanatoka ardhini…Hivyo ile laana ya ardhi kulaaniwa NI PANA KIDOGO zaidi ya tunavyoielewa.
Lakini kama tukijifunza kitabu cha Mwanzo kwa undani zaidi, tutazidi kuona kuwa hiyo laana ya ardhi kulaaniwa haikuishia tu pale Adamu aliasi, bali utaona kuwa kwa jinsi muda ulivyokuwa unaenda na maasi yalivyokuwa yanazidi kuongezeka ile laana nayo ilikuwa inajiongeza.. Ndio maana utaona Kaini baada ya kumwua ndugu yake Habili, ile laana ya ardhi kulaaniwa iliongezwa kwake…
Mwanzo 4: 9 “Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?
10 Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako INANILILIA KUTOKA KATIKA ARDHI. 11 Basi sasa, UMELAANIWA WEWE KATIKA ARDHI, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako;
12 UTAKAPOILIMA ARDHI haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani.
13 Kaini akamwambia Bwana, Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki.
14 Tazama, UMENIFUKUZA LEO KATIKA USO WA ARDHI, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua.”
Unaona hapo? Baada ya laana ya kwanza Bwana Mungu aliyomlaani Adamu na uzao wake juu ya ardhi, tunaona Kaini anazidishiwa tena mara mbili baada ya kumwua ndugu yake..hivyo ni laana juu ya laana..
Kwahiyo hali hiyo ya laana kujiongeza juu ya laana iliendelea kwa miaka na miaka kutokana na maasi ya wanadamu…Mpaka ilipofika wakati karibia na gharika Bwana alipomchagua mtu ambaye kwa kupitia yeye ataisimamisha ile laana ya ARDHI KULAANIWA kila kukicha..Na ndio tunasoma Bwana alimnyanyua Nuhu kwa kizazi chake, Mtu mkamilifu na wa Haki, ambaye alipata sana Neema mbele ya Macho ya Mungu..kama tunavyosoma mtoto huyo alipozaliwa tu Baba yake kwa Imani akatoa unabii juu yake na kusema…
Mwanzo 5: 28 “Lameki akaishi miaka mia na themanini na miwili, akazaa mwana.
29 Akamwita jina lake Nuhu, akinena, HUYU NDIYE ATAKAYETUFARIJI KWA KAZI YETU NA KWA TAABU YA MIKONO YETU KATIKA NCHI ALIYOILAANI BWANA.
30 Lameki akaishi baada ya kumzaa Nuhu miaka mia na tisini na mitano, akazaa wana, waume na wake”.
Unaona, tangu Adamu mpaka Kuzaliwa kwa Nuhu, ni takribani zaidi ya miaka 1500 ilipita..kwahiyo kwa kipindi chote hicho matatizo yalikuwa makubwa sana duniani kwasababu ya Ardhi iliyolaaniwa na inayoendelea kulaaniwa kutokana na dhambi zilivyokuwa zinazidi kuongezeka..Kwahiyo Baba yake Nuhu, kabla hajafa alijua atazaliwa mwana ambaye kwa kupitia yeye hiyo laana itasimama na itakuwa faraja kwa vizazi vijavyo..
Na Nuhu alipokuwa mtu mzima, baada ya Baba yake kufa alianza kumtafuta Mungu na kwenda katika njia zake, na kutojichangamana na maasi ya ulimwengu..Na hivyo Bwana akapendezwa naye kuliko watu wote waliokuwa wanaishi duniani kwa wakati huo, kumbuka dunia ya wakati ule ilikuwa na watu wengi kama dunia ya sasa, lakini yeye akakubalika sana machoni pa Bwana.
SASA NI WAKATI GANI? NUHU ALIPOISIMAMISHA HIYO LAANA?.
Kwasababu tunaona Baba yake alishatabiri kuwa yeye ndiye atakayefariji uzao wao katika nchi aliyoilaani Bwana, hivyo ni lazima uje wakati ambapo Bwana ataisimamisha hiyo laana kupitia Nuhu. Na wakati huo sio mwingine zaidi ya WAKATI BAADA YA GHARIKA KUPITA..pale ambapo Nuhu alimtolea Bwana sadaka nzuri iliyompendeza na Bwana akaridhika na sadaka ile na KUAPA KUTOILAANI TENA NCHI kwa namna yoyote ile..Tunasoma hayo katika..
Mwanzo 8: 18 “Basi Nuhu akatoka, yeye, na wanawe, na mkewe, na wake za wanawe pamoja naye;
19 kila mnyama, na kila kitambaacho, na kila ndege, kila kinachokwenda juu ya nchi kwa kabila zao, wakatoka katika safina.
20 Nuhu akamjengea Bwana madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliye safi, na katika kila ndege aliye safi, akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu.
21 Bwana akasikia harufu ya kumridhisha; Bwana akasema moyoni, SITAILAANI NCHI TENA BAADA YA HAYO KWA SABABU YA WANADAMU, MAANA MAWAZO YA MOYO WA MWANADAMU NI MABAYA TANGU UJANA WAKE; wala sitapiga tena baada ya hayo kila kilicho hai kama nilivyofanya. 22 Muda nchi idumupo, majira ya kupanda, na mavuno, wakati wa baridi na wakati wa hari, wakati wa kaskazi na wakati wa kusi, mchana na usiku, havitakoma”.
Unaona hapo? Bwana anasema “sitailaani tena nchi” na sio “sitamlaani tena mwanadamu” nchi na ardhi ni kitu kimoja. Kwahiyo baada ya Nuhu kumtolea Bwana sadaka iliyokubalika mbele zake, Bwana akaisimamisha na ile laana iliyokuwa inaendelea kujiongeza siku baada ya siku.
Mwanzo 9: 8 “Mungu akamwambia Nuhu, na wanawe pamoja naye, akisema, 9 Mimi, tazama, nalithibitisha agano langu nanyi; tena na uzao wenu baada yenu;
10 tena na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, ndege, na mnyama wa kufugwa, na kila mnyama wa mwitu katika nchi pamoja nanyi; wote wanaotoka katika safina, hata kila kilicho hai katika nchi.
11 Na agano langu nitalithibitisha nanyi; WALA KILA CHENYE MWILI HAKITAFUTWA TENA KWA MAJI YA GHARIKA; WALA HAKUTAKUWA TENA GHARIKA, BAADA YA HAYO, KUIHARIBU NCHI.
12 Mungu akasema, Hii ndiyo ishara ya agano nifanyalo kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, kwa vizazi vyote hata milele;
13 Mimi nauweka upinde wangu winguni, nao utakuwa ni ishara ya agano kati yangu na nchi.
14 Hata itakuwa nikitanda mawingu juu ya nchi, upinde utaonekana winguni,
15 nami nitalikumbuka agano langu, lililoko kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili, wala maji hayatakuwa gharika tena kuwaharibu wote wenye mwili.
16 Basi huo upinde utakuwa winguni; nami nitauangalia nipate kulikumbuka agano la milele lililoko kati ya Mungu na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili kilichoko katika nchi.
17 Mungu akamwambia Nuhu, Hii ndiyo ishara ya agano nililoliweka kati yangu na wote wenye mwili walioko katika nchi.”
Lakini tunaona kuwa japokuwa Bwana aliisimamisha ile laana bado kulikuwa na matatizo madogo madogo yaliyoendelea kutokea.. kulikuwepo bado na vipindi vya njaa duniani ingawa mvua badao zilikuwa zinanyesha kwa misimu, bado vilikuwepo, vipindi vya matetemeko, vipindi vya taabu, nyakati za kula kwa jasho n.k Hivyo kwa lugha nyingine ni kwamba Nuhu alisimamisha laana isiendelee lakini hakuiondoa laana kabisa.
Agano Mungu aliloingia na Nuhu, halikutosha kuondoa LAANA YOTE MUNGU aliyoilaani ARDHI, lilikuwa ni agano la kuleta UNAFUU tu wa maisha juu ya wanadamu.
Hivyo ni lazima aje mwingine mfano wa Nuhu ambaye sio tu kuisimamisha laana bali KUIONDOA KABISA LAANA ISIWEPO, dunia irudi katika hali yake ya kwanza, kusiwepo na tabu tena, kusiwepo na kula kwa jasho tena, zisiwepo shida tena n.k Na huyu si mwingine zaidi ya YESU KRISTO.
Na kama tunavyoona ili kwamba Bwana aibariki tena ardhi kama alivyofanya kwa Nuhu, ni lazima gharika ipite Kwanza kuiharibu dunia yote, kisha ndio ije ile baraka na kabla hajaiharibu dunia kwa gharika, alimuhifadhi kwanza Nuhu na wanawe ndani ya safina.
Vivyo hivyo katika siku hizi za mwisho wakati BWANA MUNGU anataka kwenda kuifuta kabisa laana ya DUNIA, ARDHI ILIYOLAANIWA. Bwana Mungu alimnyanyua YESU KRISTO kwa mfano wa Nuhu, ili kwa kupitia yeye Bwana ayarejeshe mambo yote yaliyoharibika, arejeshe dunia iwe kama Edeni, aiondoe laana yote ambayo haikumalizika kuondolewa na Nuhu.
Na ni lazima gharika kwanza ije ili kuondoa waovu wote, ulimwenguni ndipo mambo yote yafanywe kuwa mapya..Hivyo kabla ya Yesu Kristo kuja duniani kurejesha mambo yote, siku zake zitafananishwa kama siku za Nuhu, ataijenga safina ambayo ni NENO LAKE, na kuwaingiza watu wake humo, na kisha kuihukumu dunia kwa moto kama Nuhu alivyoihukumu kwa gharika.
Waebrania 11: 7 “Kwa imani Nuhu akiisha kuonywa na Mungu katika habari za mambo yasiyoonekana bado, kwa jinsi alivyomcha Mungu, aliunda safina, apate kuokoa nyumba yake. Na hivyo AKAUHUKUMU MAKOSA ULIMWENGU, akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani.”
Kwahiyo Yesu Kristo ndiye mhukumu wa ulimwengu na mrithi, ATAKAYETUFARIJI SISI KATIKA ARDHI HII ILIYOLAANIWA NA BWANA, na faraja hiyo haitakuja sasa, bali baada ya ulimwengu huu kuteketezwa, ndipo hapo dunia itarejeshwa na kuwa kama paradiso ya kwanza. Katika utawala wa miaka 1000 na katika umilele.
Ndugu yangu unayesoma haya. Hii dunia haiwezi kufanywa upya kabla maangamizi hayajaja, hii dunia haina muda mrefu kama wengi wanavyodhani, Kristo mfano wa Nuhu anawaingiza wanawe sasa kwenye safina yake aliyoitengeneza yeye mwenyewe (NENO LAKE) na akisha maliza kuwaingiza wote mlango wa neema unafungwa, na kisha ghadhabu ya Mungu kumwagwa ulimwenguni kote. Na anasema kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu ndivyo itakavyokuwa katika siku za kuja kwake mwana wa Adamu, siku za Nuhu watu walikuwa wanakula na kunywa,(anasa), walikuwa wanaoa na kuoana (ndoa za jinsia moja),walikuwa waasherati kama leo, wanaojipenda wenyewe, watu wa fashion, wanawake na wanaume wasiovaa mavazi ya kujisitiri, walikuwepo watu wa dhihaka, wauaji, wasengenyaji, wasiosamehe, wala rushwa, wacheza dansi n.k Ndio hao hao wapo sasa..Tusiangukie katika hilo kundi ndugu yangu. Bwana alimfunulia Mtume Petro mambo hayo yatakayotokea siku hizi za mwisho na kusema..
2 Petro 3: 2-12
“1 Wapenzi, waraka huu ndio wa pili niwaandikiao ninyi; katika zote mbili naziamsha nia zenu safi kwa kuwakumbusha,
2 mpate kuyakumbuka yale maneno yaliyonenwa zamani na manabii watakatifu, na ile amri ya Bwana na Mwokozi iliyoletwa na mitume wenu.
3 Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika siku za mwisho watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe,
4 NA KUSEMA, IKO WAPI AHADI ILE YA KUJA KWAKE? KWA MAANA, TANGU HAPO BABU ZETU WALIPOLALA, VITU VYOTE VINAKAA HALI IYO HIYO, TANGU MWANZO WA KUUMBWA.
5 Maana hufumba macho yao wasione neno hili ya kuwa zilikuwako mbingu tangu zamani, na nchi pia, imefanyizwa kutoka katika maji, na ndani ya maji, kwa neno la Mungu;
6 kwa hayo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji, ikaangamia.
7 Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu.
8 Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba KWA BWANA SIKU MOJA NI KAMA MIAKA ELFU, NA MIAKA ELFU NI KAMA SIKU MOJA.
9 BWANA HAKAWII KUITIMIZA AHADI YAKE, KAMA WENGINE WANAVYOKUDHANI KUKAWIA, BALI HUVUMILIA KWENU, MAANA HAPENDI MTU YE YOTE APOTEE, BALI WOTE WAFIKILIE TOBA.
10 Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.
11 Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa,
12 mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka? “
Unaona hapo juu anavyosema? “BWANA HAKAWII KUITIMIZA AHADI YAKE, KAMA WENGINE WANAVYOKUDHANI KUKAWIA, BALI HUVUMILIA KWENU, MAANA HAPENDI MTU YE YOTE APOTEE, BALI WOTE WAFIKILIE TOBA.”
Anakuvumilia leo ili utubu, ili utubie uasherati wako, ili utubie usengenyaji wako, ili utubie uvaaji wako mbaya, ili utubie dansi zako unazoenda kucheza kila siku, ili utubie kutokusamehe kwako, ili utubie kula kwako rushwa, ili utubie hasira zako zinazowaka pasipo sababu, anataka kukuingiza kwenye safina yake katika dakika hizi za mwisho za majeruhi. Na kutubu sio tu kuomba msamaha, hapana bali maana yake ni KUGEUKA NA KUACHA UNAYOYAFANYA. Na baada tu ya kuamua kwa dhati kugeuka, hatua inayofuata ni ubatizo wa maji mengi, na kwa jina lake YESU (Matendo 2:38).
Hivyo Mgeukie leo YESU. Kwasababu yeye ndiye Mungu aliyemchagua na kumtia mafuta kwa UKOMBOZI, hakuna mwingine zaidi yake, kila kitu kimewekwa chini yake, na yeye ndiye atakayeihukumu hii dunia mfano wa Huhu. Ili ayafanye mambo yote kuwa mapya baada yake, ili siku ile ATUFARIJI tukafurahi naye katika mbingu mpya na chini mpya ambayo itashuka hapa duniani, mahali ambapo tutakuwa na raha milele, mahali ambapo kutakuwa hakuna magonjwa wala njaa, wala shida, wala mauti,wala dhiki, wala maadui..Mahali ambapo tutafutwa machozi yetu na tutakula mema yote ya nchi Bwana aliyotuandalia zaidi hata ya ilivyokuwa pale Edeni.
Bwana akubariki sana.
Tafadhali washirikishe na wengine mambo haya, na Bwana atakubariki.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
MAMBO (2) YATAKAYOKUTENGA NA IMANI SIKU HIZI ZA MWISHO.
Kamusi inatoa tafsiri ya neno “KURITHI” kwamba ni kitendo cha kupokea mali baada ya kifo cha mmiliki wa mali hiyo. Hii ikiwa na maana kuwa mali inapopaswa kurithishwa haiwezi kutoka mikononi mwa mrithishaji mpaka siku atakapokufa mwenyewe. Hivyo yule atakayerithishwa siku zote hapaswi kujimilikisha mali zile hata kama atakuwa anazihudimia kwa kiasi gani, mpaka siku atakapokufa mmiliki mwenyewe ndipo ziwe zake moja kwa moja kihalali.
Na ni lazima pia mrithishaji na mrithishwaji wawe na mahusiano ya kibinafsi na ya kipekee na kama hiyo haitoshi, ni lazima pia waingie katika makubaliano ya kimaagano au ya ki-waraka ili kutambulisha kuwa walidhiana katika mapatano hayo. Haiwezekani mtu kutokea siku ya kifo na kudai urithi kama mmojawapo wa warithishwaji angali hakuwa na mahusiano yoyote na mwenye mali au makubaliano.
Biblia nayo inakubaliana na tafsiri hiyo,Tukisoma:
Waebrania 9:16 “Maana agano la urithi lilipo, lazima IWEPO MAUTI YAKE ALIYELIFANYA.
17 Kwa maana agano la urithi lina nguvu palipotukia kufa kwa mtu; kwa kuwa halina nguvu kabisa, akiwa yu hai yeye aliyelifanya”.
Unaona hapo?. Ni kwanini KIFO kitokee? Ni kwasababu moja tu ili kwamba ile mali iwe ni milki halali ya yule mrithishwaji MILELE. Kwasababu kifo kisipokuwepo inaweza kutokea siku moja pengine yule aliye hai akadai tena mali zake, na kugeuka kuwa sio urithi tena..
Kwasababu sheria moja ya urithi ni lazima uwe ni wa milele.. Na kifo tu pekee ndio kinaweza kuleta hilo jambo. Hivyo tunaweza kusema nguvu ya urithi ni KIFO.
Hayo mambo yanafunua nini rohoni? Kumbuka Mungu alitoa ahadi kuu za urithi kwa watoto wake juu ya nchi aliyowaandalia itakayokuja huko mbeleni. Na tunafahamu kuwa mbingu hizi na dunia hii ni mali ya Mungu sasa?, milima, sayari, nyota, mito , habari mabara n.k vyote hivi ni mali yake.
(Kutoka 19:5).Na mwanadamu aliwekwa ndani yake pale Edeni lakini kwa kutokutii kwake akamruhusu shetani ainyakue mikononi kwake, mpaka kupelekea kuingia katika matatizo tuliyonayo sasa hivyo ikamgharimu Mungu amtume mwanawe mpendwa Yesu Kristo ili aje kuukomboa tena ulimwengu uliokuwa umepotea. Na tunafahamu kuwa ushindi huo ulipatikana pale Kalvari miaka 2000 iliyopita hapo ndipo umiliki wa mbingu hizi na nchi hizi ziliporudi tena kwa Mungu baba kwa kupitia YESU mwokozi wetu.
Hivyo, vitu vyote vilivyopo ulimwenguni sasa vinamilikiwa na YESU KRISTO mwenyewe, isipokuwa huu mfumo wa utawala mbovu wa shetani unaoiharibu dunia sasa kwa kitambo ndio upo mikononi mwa shetani. Lakini kwa kuwa YESU ni mshindi alishapanga siku ya maangamizi ya vitu vyote ili kuitengeneza upya dunia na kuifanya kuwa bustani ya Mungu yenye makao mazuri yasiyoneneka. Matengenezo hayo yataanza katika ule utawala wa miaka 1000, ambapo kila kitu kiovu kitasafishwa na YESU KRISTO atakapokuja kutawala na watakatifu wake hapa duniani.
Sasa hapo ndipo Mungu atakapoutoa ule urithi alioutunza kwa ajili ya watoto wake ambao tangu zamani aliundaa kwa ajili yao, urithi ambao Ibrahimu aliuona tokea mbali ukamfanya mpaka aishi kama mpitaji hapa duniani.
Waebrania 11:8 “Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako.
9 Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile.
10 MAANA ALIKUWA AKIUTAZAMIA MJI WENYE MISINGI, AMBAO MWENYE KUUBUNI NA KUUJENGA NI MUNGU.”
Unaona hapo Yatafakari maneno hayo vizuri “10 MAANA ALIKUWA AKIUTAZAMIA MJI WENYE MISINGI, AMBAO MWENYE KUUBUNI NA KUUJENGA NI MUNGU.”
kama biblia inavyosema katika Mathayo 5: 5 “Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi”.
Ndugu Ipo nchi tutakayokuja kuirithi sisi watoto wa Mungu baada ya utawala huu mbovu wa shetani kuharibiwa kabisa hapo dunia itakapofanywa kuwa upya tena wakati huo ndipo urithi wetu utaachiliwa. Hapo ndio kila mtoto wa Mungu ambaye alijiona kuwa yeye si kitu alipokuwa duniani, aliyejinyima nafsi yake na mambo ya ulimwengu mpaka kuonekana kama ni takataka ya dunia sasa kwa mambo ambayo atakutana nayo huko katika siku hizo, hata kumbuka tena taabu yake aliyoipitia, biblia inasema kama vile mwanamke aliyetoka kujifungua anavyosahau uchungu aliopitia baada ya kuona kiumbe kipya kuja duniani.Ndivyo itakavyokuwa kwa watoto wa Mungu siku ile.
1Petro 1:3 “Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu;
4 TUPATE NA URITHI USIOHARIBIKA, USIO NA UCHAFU, USIONYAUKA, ULIOTUNZWA MBINGUNI KWA AJILI YENU.”
Sasa swali linakuja je! ili Mungu atupe huo urithi wa mbingu mpya na nchi mpya, ambao ametuahidia inampasa na yeye afe ili tuwe na umiliki halali wa urithi huo milele?
Jibu ni hapana, kama tunavyojua kuwa Mungu anaishi milele, hafi, sasa kitakachofanyika ni kuwa MUNGU ATAKUFA KWA HABARI YA UMILIKI WA NCHI HIYO INAYOKUJA, ikiwa na maana kuwa dunia ijayo itakuwa ni MILKI HALILI YA MWANADAMU MILELE.. Yaani mwanadamu atakuwa na maamuzi ya kufanya jambo lolote katika nchi hiyo aliyoandaliwa na Mungu.. Unajua kwasasa huwezi kufanya lolote kwasababu dunia hii ni mali ya Mungu, embu jaribu kufikiria mfano ingekuwa ni mali yako, ungeamua kufanya nini?. Unaona ni kama jambo ambalo haliwezekani lakini itakuwa hivyo.
Mungu wakaandalia watakatifu wake urithi wa milele, siku hiyo Mungu hatawauliza chochote juu ya urithi huo, kana kwamba sio yeye aliyeiumba dunia bali wao..
Jambo pekee litakalofanyika ni kwamba tutamjua yeye katika viwango vingine, Tutamwabudu Mungu katika viwango vingine , mbali ni hivi tunavyovijua mbali na masuala ya mbingu na nchi, mambo ambayo kwasasa hatuwezi kuyastahimili mpaka tutakapofika kule kwanza…siku hizo hatutamwabudu yeye kama tunavyomwabudu sasa, Huko tutakapomjua Mungu kwa mapana na marefu, huko ndiko tutakapomjua Mungu kuwa ni zaidi ya mbingu na nchi, na vitu tunavyoviona Haleluya!.
Ni vizuri tukiyafahamu hayo, ili kusudi kwamba mambo ya ulimwengu huu mabovu ya kitambo tuyaonapo tuone kuwa ni takataka tukifananisha na urithi usioharibika Mungu aliotuandalia huko mbeleni na ndio maana biblia ilikazia sana kusema maneno haya:
Waefeso 1.18 “macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; NA UTAJIRI WA UTUKUFU WA URITHI WAKE KATIKA WATAKATIFU JINSI ULIVYO”
Pia Kumbuka biblia inaposema mbingu mpya na nchi mpya, inamaanisha jambo zaidi ya hii sayari yetu inayojulikana kama dunia..Inamaanisha kuwa ni pamoja na sayari zote, na nyota zote na magimba yote yaliyopo angani. Yote yatakuwa ni makao na urithi Mungu aliwaandalia wanadamu watakatifu.
Sayari hii yetu ni kama makao makuu tu, wanasayansi wanafanya utafiti wa kupata uwezekano wa makazi mapya ya wanadamu katika sayari nyingine, na kweli wameziona lakini hawawezi kuzifikia, kwasababu ni mbali na upeo wa kibinadamu kufika huko. Wanachunguza chunguza uwezekano wa kuishi katika sayari zilizo kando kando ya dunia lakini bado hawataweza kwasababu huo sio urithi wao. Huo ni urithi wa wana wa Mungu Bwana aliowaandalia wale wazishikao amri zake.
Ayubu 9: 7 “Aliamuruye jua, nalo halichomozi; Nazo nyota huzipiga muhuri”.Na pia inasema..
Zaburi 147: 4 “Huihesabu idadi ya nyota, Huzipa zote majina”.
Kitu kikishapewa jina na Mungu mwenyewe inamaanisha kuwa kitu hichi kina uhai, na pia kinakaliwa. Sasa kama nyota zote kazipa majina na kazipiga muhuri itafika wakati kama ilivyokuwa pale mwanzo Nchi ilikuwa ukiwa lakini Roho wa Mungu alipotujua juu ya dunia hii , pakawa mahali pa kukaliwa na watu. Ndivyo itakavyokuwa kwa sayari nyingine na magimba mengine yaliyopo angani.
Ili kusudi kwamba Mungu awe wa milele na asiyeisha, ni lazima awe na urithi ambao kuisha kwake unahitaji umilele. dunia pekee hii haitaweza kustahimili umilele, kwani kuna wakati itafika tutajua kila kitu kilichopo duniani.
Na ndio maana pale anasema macho ya mioyo yetu yatiwe nuru ili tujue utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo;…Zingatia hilo neno UTAJIRI WA UTUKUFU WA URITHI WAKE.. yaani utukufu wa urithi wake una TAJIRI usiopunguka..
Hayo ni machache tu yapo mambo mengi yahusuyo urithi Mungu aliowaandalia watoto wake. Leo hii watu wanajiona kuwa hii dunia ni ya kwao japo si ya kwao, wanajiona kuwa wanaweza kufanya kila kitu, wanajiona kuwa wapo huru kana kwamba hakuna anayewamiliki.. Sasa kama wao kwasasa wanajiona hivyo na hawajijui kuwa wanamilikiwa pasipo wao kujijua kwasababu hii nchi hawajarithishwa wao. Itakuwaje siku hiyo pale Mungu atakapomaliza kuitengeneza upya hii dunia na kuwapa watoto wake..
WATAKUWA HURU KIASI GANI?..NI ZAIDI YA UHURU unaweza kuudhani. Kwa Mungu hakuna utumwa.
Lakini leo hii tusipoyaona hayo na kuupenda huu ulimwengu uliojaa utumwa wa kila namna, ulimwengu wa kitambo, ambao mwisho wake upo karibu, hatutaki kutazama mambo ya milele yanayodumu, tunapuuzia wokovu, tunadhani kuwa Mungu ni mtu wa kando wa sisi kujiamulia mambo tu, kana kwamba tusipompokea yeye kuna kitu anapungukiwa…Hapana ndugu siku ile tutajuta pale tutakapoona tumekosa urithi huo ulio bora, na wenzetu wanaingia katika raha ya milele na sisi tunaenda katika ziwa la moto.
Siku ile ya hukumu Bwana atakapotenga mbuzi na kondoo, kondoo wake wakiwa upande wake wa kiume na mbuzi (waovu) wakiwa upande wa kushoto atawaambia maneno haya:
Mathayo 25:34 “Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, URITHINI UFALME MLIOWEKEWA TAYARI TANGU KUUMBWA ULIMWENGU;”
Unaona? Wataurithi ufalme Mungu aliwaandalia tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu.Lakini waliosalia wote sehemu yao itakuwa katika lile ziwa la moto. Kama biblia inavyoeleza katika..
1Wakorintho 6:9 “Au hamjui ya kuwa wadhalimu HAWATAURITHI UFALME WA MUNGU? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,
10 wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi.”
Hivyo tuyachunguze maisha yetu leo kama je! kweli tunastahili kupewa urithi huo? Je! tumeshaingia katika agano hilo la kufanyika kuwa warithi wa Baba yetu wa mbinguni?. Kumbuka Agano hilo halifanyiki nje ya Damu ya YESU Kristo. Ikiwa bado haujaokolewa fanya hivyo sasa maadamu neema ipo, uoshwe dhambi zako kwa kutubu na kubatizwa katika ubatizo uliosahihi wa maji mengi katika jina la YESU ili upate ondoleo la dhambi zako. Na ikiwa bado unasua sua njia panda upo vuguvugu ni wakati sasa wa kufanya imara wito wako na uteule wako. Ili urithi huo usikupite.
Bwana akubariki.
Tafadhali Washirikishe wengine habari njema za Yesu Kristo, popote pale ulipo.
Mada Nyinginezo:
TULICHUNGUZE UMBO LA YESU NA MWENENDO WAKE.
Tukisoma Agano la Kale, biblia inaelezea maisha ya watumishi wake, jinsi walivyokuwa na jinsi walivyoishi. Tunajua kabisa wengi maisha yao hayakukamilika, kwasababu torati waliyopewa isingeweza kuwakamilisha na kuwa wakamilifu, Kwasababu torati yenyewe haikutimilika..
Ndio maana utamwona Mtu kama Daudi aliyependwa sana na Mungu, alioa wake wengi, na mwanawe Sulemani alikuwa na wake wengi vile vile. Utamwona Daudi mtu aliyeupendeza Moyo wa Mungu alikuwa anaua, na aliua watu wengi na bado BWANA hakumuhesabia makosa.
Utamwona Daudi hakubatizwa lakini bado alikuwa ni mtu anayeupendeza moyo wa Mungu. Alikuwa anashindana na kuwatakia shari maadui zake, na kuwachukia lakini bado alikuwa ni mteule wa Bwana.
Sasa kwa jicho la haraka haraka unaweza ukasema, kama Daudi alikuwa ana wake wengi, alikuwa anawashambulia na kushindana na maadui zake, alikuwa anaua na bado ni mtumishi wa Mungu, na mimi sio vibaya nikifanya hayo hayo na bado kwani Mungu atakuwa na mimi. Ni rahisi kusema hivyo.
Lakini ningependa ufahamu kitu kimoja, agano la kale(au agano la kwanza) lilikuwa sio utimilifu wa mambo yote…lilikuwa ni muhtasari tu wa Agano halisi la Mungu. Na ndio maana Bwana Yesu alisema katika..
Mathayo 5:17 “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.”
Unaona hapo? Bwana alikuja KUITIMILIZA, yaani kuifanya ieleweke vizuri…yaani ikiwa na maana kuwa, Torati iliposema USIUE, Haikumaanisha tu kumkamata mtu na kuutoa uhai wake bali iliimanisha kwanza USIMCHUKIE KABISA NDUGU YAKO, Vivyo hivyo Torati iliposema USIZINI, Haikumaanisha tu kwenda kufanya zinaa ya nje, hapana bali ilimaanisha pia MTU HATAKIWI KUTAMANI KABISA NDANI YA MOYO WAKO. Kwahiyo unaweza ukaona hapo kutoka “kuzini” mpaka “kutokutamani” huko ni kukitimiliza kile kipengele kilichosalia..kwasababu Torati asili yake ni Rohoni.
Hivyo Daudi na watakatifu wa agano la kale walipokuwa wanaua hawakuwa wanafanya jambo lililosahihi, ingawa kwa wakati ule Bwana aliruhusu wafanye vile kwasababu wakati wa Utimilifu wa Torati, ulikuwa bado haujafika.
Kadhalika Daudi, na Sulemani mwanae, na watakatifu wote wa Agano la kale walipooa wake wengi, walikuwa hawafanyi jambo lililo sahihi machoni pa Bwana, ilikuwa sio mpango kamili wa Mungu wawe na wake na wengi, Lakini Bwana aliliruhusu waendelee kuoa wake wengi na kutoa talaka,hivyo hivyo mpaka UTIMILIFU utakapofika.
Watakatifu wa agano la kale, walikuwa wanaapa, lakini hayakuwa ni mapenzi ya Mungu mwanadamu yeyote aape, lakini Bwana aliwaruhusu waendelee kufanya hivyo mpaka wakati wa Utimilifu utakapofika. Na mara nyingine aliruhusu ifanyike hivyo kwasababu tu ya ugumu wa mioyo yao.
Ndipo wakati wa UTIMILIFU ulipofika, Mungu alimtuma mwanawe mpendwa Yesu Kristo ili kuhubiri UTIMILIFU wote WA TORATI.
Na ndio hapo Bwana Yesu alisema..
Mathayo 5:21 “Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu.
22 Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto”.
Mathayo 5:27“Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; 28 lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake”.
Mathayo 5.33 “Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana nyapo zako;
34 lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu;
35 wala kwa nchi, kwa maana ndiyo pa kuwekea miguu yake; wala kwa Yerusalemu, kwa maana ndio mji wa Mfalme mkuu.
36 Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi.
37 Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu”
Mathayo 5:38“Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino;
39 Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili.”
Kaka/dada unayesoma haya, UMESIKIA kwamba imenenwa unaweza ukaokolewa tu, maadamu unatenda mema, na kuzishika amri 10 za Mungu, lakini Kristo anasema.. Mtu hawezi kuuona ufalme wa mbingu, asipozaliwa mara ya pili.
Na tena umesikia mahali wanasema ubatizo sio wa lazima, mbona hata Daudi hakubatizwa lakini Mungu alimkubali, Ndugu usiamini huo uongo leo KRISTO ANAKUAMBIA… “AAMINIYE NA KUBATIZWA ATAOKOKA ASIYEAMINI ATAHUKUMIWA” (Marko 16:15-16).“
Umeona hapo? Anasema asiyeamini atahukumiwa, Ndugu yangu usipoamini na kubatizwa utahukumiwa, hayo ni maneno ya Mkuu wa Uzima mwenyewe YESU KRISTO, Na yeye hawezi kusema uongo.
Inawezekana mahali Fulani umesikia mtu Fulani akikuambia kwamba unatakiwa umfuate Yesu tu, kwa wepesi usijiweke rehani saana..Lakini yeye anakwambia leo
Luka 9:23-25 “..Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha. Kwa kuwa yamfaa nini mtu kuupata ulimwengu wote, kama akijiangamiza, au kujipoteza mwenyewe?.”
tena umesikia mahali pengine wakisema kuwa ni ruksa kuwa na wake wengi au waume wengi..lakini kristo mtimilifu wa torati anakuagiza leo maneno haya
Luka 19: 9 “nami nawaambia ninyi, kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini…..
7 wakamwambia, jinsi gani basi musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha?
8 akawaambia, musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi”.
Tena umesikia dhehebu Fulani likisema, mtu akifa leo hupitia kwanza TOHARANI kutakaswa dhambi zake kisha atakwenda mbinguni, na wengine wanasema mtu akifa amekufa wala hakuna kiyama ya wafu. Lakini Bwana Yesu anasema “27 Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu;(Waebrania 9:27)”. Unaona? Usidanganyike ndugu kufanya ibada za wafu, au kuwaombea wafu, wala usidanganyike kuwa ukifa leo ni unapotea tu kama wale masadukayo walivyokuwa wanaamini. Fahamu kuwa ukishakufa wewe utakuwa ni wakusubiria hukumu aidha peponi au jehanum, Hivyo usikubali kusikiliza hadithi za kutungwa, zitakazokufanya ustarehe katika dhambi zako ukidhani kuwa kuna nafasi ya pili uko uendako, au kuna kupotea tu hakuna hukumu.
Ndugu, mtii YESU KRISTO leo, usiseme kwasababu Daudi alikuwa na wake wengi, basi na wewe ndio uwe na wake wengi, usiseme kwasababu Daudi hakubatizwa na wewe usiutafute ubatizo leo, usiseme kwasababu Daudi alikuwa anashindana na maadui zake na kuwaua na wewe leo ukatafute kuwaangamiza wale wanaokuchukia.. usifanye hivyo mtimilifu wetu yesu kristo ndiye anayetuagiza tusifanye hivyo. tusishindane na watu waovu, wala tusijilipize kisasi. sio kila njia ya watakatifu wa agano la kale ilikuwa ni kamilifu, mtazame YESU Kristo yeye ndiye njia na kweli na uzima. na ndiye aliyepakwa mafuta kutufundisha maneno ya uzima. huyu yesu kristo ndiye aliyefanyika bora kuliko wanadamu wote na malaika wote..na ndio maana ile sauti ilitoka mbinguni na kusema… “huyu ndiye mwanangu mpendwa wangu msikieni yeye”.
Waebrania 2: 1 “Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi,
2 mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika mwana [yesu kristo], aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.
3 yeye kwa kuwa ni mng’ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa ukuu huko juu;
4 amefanyika bora kupita malaika, kwa kadiri jina alilolirithi lilivyo tukufu kuliko lao.”
Mwamini YESU uokolewe hizi ni saa za majeruhi.
ubarikiwe
tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine na mungu atakubariki.
Mada Nyinginezo:
ROHO YA MPINGA KRISTO IKITENDA KAZI SIKU HIZI ZA MWISHO
NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE.
NJAA inaficha uchungu wa kitu, mtu mwenye njaa hata akipewa mboga iliyochungu kiasi gani, bado ataiona ni tamu tu, kwasababu NJAA ipo ndani yake, lakini kwake yeye aliyeshiba, hata chakula kiungwe kwa viungo vingi kiasi gani bado ataona tu kuna kasoro nyingi ndani yake..Ni kwasababu njaa haipo ndani yake.
Unaweza ukajiuliza ni kwanini Neno la Mungu linafananishwa na ASALI? Sababu ni hizi kwanza Asali ni kitu kitamu kuliko vyakula vyote na matunda yote, pili asali ni chakula kisichoharibika kinadumu milele, ni kitu kisichoisha ubora wake kwa mamilioni na mamilioni ya miaka ipo vile vile tofauti na kitu chochote kile kinachoweza kulika, Bwana anasema:
“Mwanangu, ule asali, kwa maana ni njema, Na sega la asali lililo tamu ulionjapo. 14 Basi utaijua hekima kuwa tamu kwa nafsi yako; Ikiwa umekwisha kuiona; Ndipo itakapofuata thawabu; Wala tumaini lako halitabatilika.” (Mithali 24: 13)”.
Lakini japo asali ni tamu kuliko vitu vyote kamwe hatuwezi kuuona utamu wake pale nafsi zetu zikiwa zimejikinai, tukijiona kuwa tunajua, tumefika, hakuna mtu anayeweza kutuongezea kitu cha ziada katika ukristo wetu ni dini zetu tu, tukijiona kuwa sisi ni bora kuliko wengine,
tunawadharau wengine wote, hatutaki kuwasikiliza wala kuwahudumia?, tunasema wale sio wa dhehebu letu, hivyo hatuwasikilizi hawana chochote cha kutuongezea, n.k. ..
Hapo hata kama tutalifahamu Neno la Mungu kwa wingi kiasi gani, hata kama tutakuwa na mafunuo mengi kiasi gani, hata kama tutahubiri mikutano mingi kiasi gani, hata kama tutawaombea wagonjwa wakapona kiasi gani..ULE UTAMU WA NENO LA MUNGU HATUTAUHISI KAMWE NDANI YETU.
Na ndio hapo mtu wa namna hiyo anaishia kuwa wa kidini tu, kama wale mafarisayo na masadukayo, walivyokuwa kipindi kile cha Yesu. Walimwona Bwana kama mtu asiyekuwa na dini, wala elimu, walimwona Bwana kama mtu mwenye pepo, walimwona Bwana kama mwana wa Seremala maskini tu asiyejua kitu, , hivyo pale alipokuja na Neno la Uzima kutoka kwa Mungu, walimdharau japo waliufahamu kuwa anachosema ni ukweli lakini kwa kuwa waliridhika tu na dini zao na mapokeo yao, walikuwa wameshiba nafsini mwao, wakaupinga wokovu…..kwani hekima inasema:
“Nafsi iliyoshiba hukinai sega la asali; Bali nafsi yenye njaa huona kila kitu kichungu kuwa kitamu.” (Mithali27:7).
Embu leo hii, turuhusu nafsi zetu ziwe na NJAA kwa ajili HAKI na KWELI ya Neno la Mungu Ili endapo maagizo yanayoonekana kuwa ni magumu yatokayo katika Neno la Mungu yatakapokuja mbele yetu tuyaone kuwa ni matamu hata kama yataonekana kuwa ni machungu kwa watu wengine, walioshiba. Pale biblia inapotuagiza mara baada ya kuamini kwetu tukabatizwe kwa kuzamishwa katika maji tele,na katika jina la YESU basi sisi tuwe wepesi wa kutii,maadamu nafsi zetu zina njaa ya haki, hata kama tutaona kisima, au mto au bahari vipo mbali nasi basi tufanye hivyo tu kwasababu Roho zetu zina njaa..Tufanye kama yule Mkushi aliyehitaji kubatizwa akiwa njiani, katika safari yake.
Matendo 8: 35 “Filipo akafunua kinywa chake, naye, akianza kwa andiko lilo hilo, akamhubiri habari njema za Yesu.
36 Wakawa wakiendelea njiani, wakafika mahali penye maji; yule towashi akasema, Tazama, maji haya; ni nini kinachonizuia nisibatizwe?
37 Filipo akasema, Ukiamini kwa moyo wako wote, inawezekana. Akajibu, akanena, Naamini ya kwamba Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu.]
38 Akaamuru lile gari lisimame; wakatelemka wote wawili majini, Filipo na yule towashi; naye akambatiza”.
Tusifanane na hao walioshiba, wameshakinai sega la asali ambao pamoja na elimu zao kubwa za dini wakilijua hilo wamelipuuzia kama jambo lisilo na umuhimu sana.
(Luka 6:21 Heri ninyi mlio na njaa sasa, kwa sababu mtashiba.)
Pale biblia inapotuonya tuvae mavazi ya kujisitiri, na tusivae mavazi yaipasayo jinsia tofauti (kumb 22:5). Basi tuone kuwa hicho ni chakula kitamu kwa kutii haraka sana, kwa kwenda kutupa vimini, na suruali, na kaptura ambazo ni za jinsia tofauti na za kwetu [wanawake]. Sisi tusifanane na hao walioshiba wanaosema Mungu haangalii mavazi bali roho, tukiwaacha wale waliojikinai wanaosema tunaishi chini ya neema na wala sio sheria..Sisi tuziache tu nafsi zetu ziwe na njaa..ndipo tutakapoliona Neno la Mungu ni tamu kwetu.
Tuwe kama Daudi, anasema “MAUSIA YAKO NI MATAMU SANA KWANGU, KUPITA ASALI KINYWANI MWANGU Zaburi 119:103.”
Pale biblia inapotuonya tusiabudu sanamu wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni wala chini duniani, basi moja kwa moja tusijione kuwa dini zetu ni bora kuliko Neno la Mungu, tusione kuwa viongozi wetu wa dini ni bora kuliko Neno la Mungu, tusione kuwa dhehebu letu ni zaidi ya Neno la Mungu na kupuuzia, na kuzidi kuabudu sanamu za wafu na kuzifanyia ibada na kusali rozari za kipagani vitu ambavyo Neno limekataza. Sisi tutii tu hata kama dini zetu zinatukemea. Kwasababu tunataka kwenda mbinguni.
Mathayo 5:6 “Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa.”
Tule asali sana maadamu tuna njaa, lakini ole wetu endapo tumeshiba, kwani ni jambo gani litakalotuburudisha lenye utamu zaidi ya asali?.
Dumu katika Neno la Mungu.
Ubarikiwe DAIMA wewe umtafutaye BWANA.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
Mwanzo Bwana alipowatoa wana wa Israeli katika nchi ya Misri, hakuwakuta ni wakamilifu kwa asilimia zote kama anavyotaka yeye, kwasababu kule Misri walipokuwepo hakukuwa na utaratibu wowote wa kumwabudu Mungu wa kweli, na wala wana wa Israeli walikuwa hawamjui kwa kina Mungu wa Ibrahimu, walikuwa wanayo kama historia vichwani mwao kuwa kipindi Fulani nyuma Mungu alimtokea Baba yao Ibrahimu na kumpa maneno mengi ya Ahadi, walisikia tu kipindi Fulani Mungu, aliipiga dunia kwa njaa lakini alimfunulia Yusufu aliyekuwa mwisraeli kama wao juu ya majanga hayo yatakayokuja..hawakumjua sana kwa undani, Mungu wao ni Mungu wa namna gani…Walimjua tu ni Mungu hodari na atakayekuja kuwaokoa katika matatizo yao basi.
Na kwa jinsi walivyokuwa wanaendelea kukaa katika nchi ya Misri, pasipo kumsikia kwa vizazi vingi, kidogo kidogo walianza kumdhania Mungu wa Yakobo ni kama miungu ya kimisri, walidhani kwamba Mungu wa Yakobo baba yao anaweza akatengenezewa mfano wa kinyago Fulani kama wa-Misri wanavyoifanyia miungu yao. Waliona kwasababu wa-Misri wanatolea dhabihu sanamu zao huku wanaendelea na roho zao mbaya, na bado wanapata mvua nakufanikiwa wakajua na Mungu wa Yakobo yuko hivyo hivyo, wanaweza wakamtolea dhabihu, na sadaka lakini maisha yao yakaendelea kuwa vile vile, wakaendelea kuwa na kiburi chao, matusi yao, malalamiko yao, uuaji wao, n.k.
Hivyo kwasababu waliishi na Wa-Misri kwa muda mrefu, kwa zaidi ya miaka 400, ule utamaduni au ule mfumo wa kuabudu walioutumia wa-Misri, uliwaingia na wao pia kudhani kuwa Mungu wa Israeli naye anaabudiwa kama inavyoabudiwa miungu ya kimisri..
Hata katika maisha ni kawaida kuona mazingira Fulani yakiwaathiri watu Fulani na kudhani watu wote wako kama wao. Utakuta kwamfano familia Fulani ina utaratifu wa kukaa pamoja, na kula pamoja mezani..lakini mmoja wa familia hiyo anatoka na kwenda kutembelea familia nyingine na kutazamia kuikuta familia ile ipo kama ya kwao, badala yake anakuta kila mtu yupo kivyake, baba na mama hawaongei, kila mtu na ratiba zake..lazima itamshangaza kidogo kwasababu amekuta kitu asichokitegemea..
Ndivyo ilivyokuwa kwa Wana wa Israeli, Bwana Mungu wakati anakuja kuwatoa ilikuwa ni shida sana wao kumwelewa na ndio maana tunaona Bwana Mungu aliwapitisha kwanza jangwani kabla ya kuwaingiza nchi ya Ahadi ili awafundishe yeye ni nani, na anataka nini kutoka kwao.
Utaona baada tu ya kutolewa nchi ya Misri, pamoja na kufanyiwa miujiza yote ile, wakaanza kunung’unika na kulalamika, ni kwasababu gani walikuwa wanafanya vile? Ni kwasababu walikuwa hawamjui bado Mungu wa Israeli kuwa hapendi watu wanaonungu’unika, wao walidhani Mungu wa Israeli ni kama miungu ya kimisri ambayo ukiinung’unikia tu haiwezi kufanya lolote, walidhani ni kama ile miungu ya kimisri ambayo ukiilalamikia na kuitukana haikufanyi chochote.
Na ukiendelea mbele zaidi utaona wana wa Israeli wanaanza kufikiria kutengeneza ndama ya kusubu ili iwarudishe Misri, ni kwanini walifanya vile? ni kwasababu walidhani Mungu wa Israeli ni kama miungu ya kimisri, kwamba inafika mahali inashindwa kufanya jambo Fulani, na hivyo kuitafutia njia mbadala.
Na mambo mengine mengi, waliyoyafanya wana wa Israeli yaliyomkasirisha Mungu yalitokana na kutomjua Mungu wa YAKOBO ni nani? Yalitokana na kumdhania Mungu wa Baba yao Ibrahimu ni mfano wa mmojawapo wa miungu ya Misri, isipokuwa yeye ana nguvu kidogo kipita yao.
Kwasababu hiyo basi iliwachukua muda mrefu sana kumjua Mungu wa Israeli ni nani..Mpaka Bwana alipoanza kuwapa sheria ndio kidogo kidogo ndipo Alipoanza kuwaambia yeye ni MUNGU MMOJA, na hakuna mwingine zaidi yake wala wa kufananishwa na yeye, hivyo wasiwe na miungu mingine ya kando ila yeye peke yake. ALIPOANZA KUWAAMBIA YEYE NI MUNGU MTAKATIFU NA HIVYO ANAWATAKA NA WAO WAWE WATAKATIFU KAMA YEYE ALIVYO..
Walawi 11: 45 “Kwa kuwa mimi ni Bwana niliyewaleta kutoka nchi ya Misri, ili kwamba niwe Mungu wenu; BASI MTAKUWA WATAKATIFU, KWA KUWA MIMI NI MTAKATIFU”.
Ndipo walipoanza kumwelewa Mungu kuwa sio kama miungu ya Misri waliyoizoea kwamba unaweza ukaitumikia na bado ukaendelea kuwa mwizi, unaweza ukaitolea dhabihu na bado ukaendelea kuwa mnung’unikaji, unaweza ukaitumikia na bado ukaendelea kuwa muuaji au mwizi unaweza ukaiabudu na kuiimbia na bado ukaendelea kuilalamikia, unaweza ukaifuata na bado ukaendelea kuwa mzinzi, au mlaji rushwa, au mtu mwenye chuki, kwamba unaweza ukawa na miungu mingine midogo midogo mingi ya pembeni ya kukusaidia pale Mungu mkubwa anapokwama, n.k ndipo walipojua kuwa Mungu wa Israeli sio kama walivyokuwa wanamdhania kama miungu ya Misri waliyoizoea Ndipo walipomwelewa vizuri Mungu wa Israeli ni Mungu mtakatifu sana na hana msaidizi na yupo mmoja,Iliwachukua miaka zaidi ya 40 kumwelewa vizuri Mungu wa Israeli..
Na baada akili zao kubadilishwa kumjua Mungu wa kweli ni Mungu wa namna gani, ndipo wakaweza kutembea na Mungu.
Kaka/Dada unayesoma haya..swali ni lile lile “Je! Unamjua Mungu wa kweli??” Kumbuka unaposema umetoka kwenye dhambi ni sawa na Bwana kakutoa nchi ya Misri ambayo ulikuwa ni mtumwa wa dhambi? Lakini je! Baada ya kutoka huko umemfahamu Mungu unayemtumikia?? Au unamchukulia Mungu, kama ile miungu uliyokuwa unaiabudu kabla ya kumpokea yeye??…
Biblia inasema katika agano jipya pia..
1 PERTO 1: 13 “kwa hiyo vifungeni viuno vya nia zenu, na kuwa na kiasi; mkiitumainia kwa utimilifu ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake yesu kristo.
14 kama watoto wa kutii msijifananishe NA TAMAA ZENU ZA KWANZA ZA UJINGA WENU;
15 bali kama yeye ALIYEWAITA ALIVYO MTAKATIFU, NINYI NANYI IWENI WATAKATIFU KATIKA MWENENDO WENU WOTE;
16 kwa maana imeandikwa, MTAKUWA WATAKATIFU KWA KUWA MIMI NI MTAKATIFU.
17 na ikiwa mnamwita baba, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni”.
Huwezi ukasema umetolewa katika utumwa wa dhambi na bado unasujudia sanamu, huwezi ukasema umetolewa katika utumwa wa dhambi na bado ukawa mwasherati, au mlevi, au mtukanaji…Huwezi ukasema umeokolewa kutoka katika utumwa wa dhambi na bado unavaa nguo zinazoonyesha maungo yako, unavaa nguzo zinazo kubana, unavalia vimini, suruali na kupaka wanja..Hizo zote ni tamaduni za miungu ya ki-Misri na huwezi kumtumikia Mungu wa kweli kwa tamaduni za ki-Misri.
Ndugu yangu kama unataka kwenda na Bwana, mtii anayokuambia leo, Geuka upate ufahamu, usidanganyike kwamba Mungu anaangalia roho haangalii mwili, usidanganyike kwamba wanaopaka lipstick,na wanja na wanaovaa hereni, na wigi wataingia mbinguni..Usidanganyike kuwa wanaofanya masturbation, na wanaotazama pornography, na wanaoishi na wanawake/wanaume ambao hawajaoana kuwa wataingia mbinguni, usidanganyike kuwa ukiwa vuguvugu, nusu Mungu nusu ulimwengu, utaingia mbinguni.. Bwana anasema mwenyewe kuwa ATAKUTAPIKA!! Kwasababu yeye ni mtakatifu na hivyo tutakuwa watakatifu kama yeye alivyo..
Waebrania 12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, NA HUO UTAKATIFU, AMBAO HAPANA MTU ATAKAYEMWONA BWANA ASIPOKUWA NAO;”
Ni maombi yangu kuwa utamjua Mungu wa kweli ni nani, kama hujamjua na utachukua uamuzi thabiti wa kumfuata yeye kwa viwango anavyotaka yeye vya UTAKATIFU. Na kama hujabatizwa nakushauri ufanye hivyo mapema, kwasababu ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi, na kwa Jina la Yesu ni wa muhimu sana, katika kuikamilisha safari yako ya wokovu.
Bwana akubariki.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Tafadhali “Share” ujumbe huu kwa wengine na Bwana atakubariki.
Mada Nyinginezo:
TAWI LIZAALO HULISAFISHA ILI LIZIDI KUZAA.
IKO NJIA IONEKANAYO KUWA SAWA MACHONI PA MTU.
Ishara kubwa Bwana Yesu aliyowapa wanafunzi wake ambayo kwa hiyo waliambiwa watakapoiona basi wajue kuwa “muda wa mavuno umekaribia” ni ishara ya MTINI. tukisoma
Mathayo 24:32 inasema “Basi KWA MTINI JIFUNZENI mfano; tawi lake likiisha kuchipuka na kuchanua majani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno u karibu;
33 nanyi kadhalika, myaonapo hayo yote, tambueni ya kuwa yu karibu, milangoni.
Na tunajua kuwa “mtini” alioumaanisha hapo si mwingine zaidi zaidi ya TAIFA LA ISRAELI (Yeremia 24), Ikiwa na maana kuwa tutakapoona taifa la Israeli linaanza kuchipua na kuchanua tena, basi majira ya mwisho wa dunia yamekaribia sana. Kumbuka Mungu katika mpango wake wa wokovu alianza na Israeli na katika kutimiliza atatimiliza na taifa hilo hilo, kwasababu makao ya MFALME YESU atakapokuja kwa mara ya pili kuutawala huu ulimwengu mzima katika nchi ya wenye haki, hayatakuwa katika mojawapo ya nchi hizi za mataifa tulizopo sisi na zitakazokuwepo huko hapana, bali makao yake yake makuu yatakuwa pale Israeli nchi takatifu. Alishuka hapo mara ya kwanza, atashuka hapo hapo mara ya pili. Hivyo ni lazima kwanza pale patakaswe kisha mataifa mengine yafuate kabla ya yeye kuteremka ulimwenguni.
Hivyo Mungu akishamaliza kupatakasa Israeli, ndipo atakapoitumia Israeli kuitakasa dunia nzima kwa fimbo yake. Na ndio maana Mungu alisema hivi juu ya Israeli.
Yeremia 51:20 “ WEWE U RUNGU LANGU NA SILAHA ZANGU ZA VITA; kwa wewe nitawavunja-vunja mataifa; na kwa wewe nitaharibu falme;
21 na kwa wewe nitamvunja-vunja farasi, na yeye ampandaye; na kwa wewe nitalivunja-vunja gari la vita, na yeye achukuliwaye ndani yake;
22 na kwa wewe nitawavunja-vunja mwanamume na mwanamke; na kwa wewe nitawavunja-vunja mzee na mtoto; na kwa wewe nitawavunja-vunja kijana mwanamume na kijana mwanamke;
23 na kwa wewe nitamvunja-vunja mchungaji na kundi lake; na kwa wewe nitamvunja-vunja mkulima na jozi yake ya ng’ombe; na kwa wewe nitawavunja-vunja maliwali na maakida.”
Unaona?. Sasa kulingana na unabii wa kibiblia katika hatua tuliyopo sasa tunatazamia kushuhudia VITA KUU MBILI KUBWA zitakazopiganwa pale Israeli kabla ya mambo yote kuisha. Vita ya kwanza ni ile inayozungumziwa katika Ezekieli 38-39, ambayo ndio itakayofuata muda mfupi ujao Na vita ya pili ni ile ya HAR-MAGEDONI (Ufunuo 16:16), hiyo itakayokuja kuhitimisha utawala mbovu wa huu ulimwengu, inajulikana kama vita ya Mungu mwenyezi.
VITA YA ULIYOZUNGUMZIWA KATIKA EZEKIELI 38-39.
Siku zote Mungu kabla hajafanya jambo kubwa litakaloleta madhara huwa anatanguliza kwanza madogo madogo ili kuwakumbusha watu wachukue tahadhara kwani makubwa zaidi ya hayo yanakuja mbeleni. Na ndio maana Bwana Yesu alisema, kutakuwa na vita, na tetesi za vita, kutakuwa na njaa na matetemeko ya ardhi, hayo yote ni MWANZO WA UTUNGU, Unaona Hapo utungu wenyewe bado haujafika. Ukifika inamaanisha maafa yatakuwa makubwa zaidi kuliko haya tuyaonayo. Na ukitazama kwa ukaribu haya matetemeko ya ardhi tunayoyaona ulimwenguni na kusema ni makubwa, yanayoangamiza maelfu haya yote si kitu, Yapo matetemeko hasa yatakayokuja siku ile ya mwisho hii dunia itakapoikiswa pale visiwa na milima vitakapohama kwa nguvu ya tetemeko la ardhi ambalo Mungu atalileta mwenyewe duniani kote, na mvua ya mawe makubwa sana ambayo haijawahi kunyesha tangu ulimwengu kuumbwa, hapo ndipo wanadamu wote waliosalia wakati huo watalia na kuomba milima iwaangukie wajisitiri mbali na hasira ya Mungu. Ni mambo ya kutisha sana.
Ufunuo 6.12 “Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu,
13 na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi.
14 Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake.
15 Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima,
16 wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo.
17 Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?”
Vivyo hivyo na kwenye suala la magonjwa na vita. Magonjwa yaliyopo leo yanatabika na homa zake ni za wastani, kadhalika na yanapatikana maeneo Fulani Fulani tu sio kila mahali haya yote ni mwanzo wa utungu,lakini yale yatakayoletwa na Mungu katika siku ile ya ghadhabu ya hasira yake, biblia inasema kutakuwa na jipu baya na bovu juu ya watu wote ulimwenguni walioipokea ile chapa ya mnyama. Jaribu kufikiri ukimwi na kansa,au ebola ni magonjwa yanayoogopeka, Lakini biblia hayajayaona hayo, mpaka kulizungumzia hili jipu bovu tu lenyewe…ni baya kiasi gani mpaka wanadamu watamtukana Mungu kwa maumivu ya ugonjwa huo. Sio kutamani kuwepo huko ndugu.
Sasa tukirudi kwenye suala la vita. Leo Tunaweza kushuhudia vita ya kwanza na vya pili vya dunia vilivyoua watu zaidi ya watu milioni 80, huo ni mwanzo tu wa utungu, na lakini ipo vita itakayopiganwa siku za mwisho ambayo ndio ile ya mwisho inayojulikana kama HAR-MAGEDONI. Watu watakaouawa ni idadi kubwa mito ya damu itabubujika Israeli kwa wingi wa watu watakaouawa.
Sasa tuitazame Israeli kama jinsi ilivyofananishwa na mtini kuchipuka kwake, ambako kulikuwa ni mwaka 1948.
Tunaona kuwa tangu huo wakati Israeli ilipokuwa Taifa huru tena, mvutano mkubwa ulianza kujitokeza mashariki ya kati na duniani kote kwa ujumla. Nchi za kiharabu zikiigombani Israeli na mataifa mengine yakizisapoti.Mpaka kupeleka Israeli kuwa na maadui wengi pande zake zote. Watu wasifahamu kuwa jambo hilo linatoka kwa Bwana mwenyewe ili kuonyesha kuwa moja ya hizi siku mataifa yote yatahukumiwa na rungu la Bwana Israeli.
Hiyo Iliendelea hivyo hivyo mpaka kupelekea mwaka 1967 mataifa yote ya urabuni yakiongozwa na Syria kujikusanya kwa ajili ya kuipoteza Israeli katika ramani ya dunia. Lakini jambo hilo kama tunavyosoma katika historia, Israeli ilizipiga silaha zao za vita na vita kuisha ndani ya siku 6 tu. Kupeleka mpaka Israeli kuteka sehemu ya kubwa ya taifa lake ambalo hapo kabla lilikuwa haliyamiliki pamoja na nchi za kando kando.
Sasa hayo nayo ni mwanzo wa utungu ili kutupa sisi picha ya mambo yatakayokuja kutoka siku za hivi karibuni. Hii ilikuwa ni mataifa ya uarabuni lakini siku zinakuja mataifa yote ulimwenguni yataungana kwenda kupigana na Israeli hiyo ndiyo vita ya Har-magedoni.
Hivyo tukisoma kitabu cha Ezekieli 28-39, tunaona vita nyingine hapa ukiwa na muda wako mwenyewe unaweza kusoma sura zote mbili upate kuiona habari nzima ni vita ambayo itapiganwa tena kipindi hichi karibu na unyakuo kutokea. Embu Tusome mistari michache tu ya mwanzo.
Ezekieli 38
EZEKIELI: MLANGO 38
1 Neno la Bwana likanijia, kusema,
2 Mwanadamu, kaza uso wako, umwelekee Gogu, wa nchi ya Magogu, mkuu wa Roshi, Mesheki, na Tubali, ukatabiri juu yake,
3 useme, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni juu yako, Ewe Gogu, mkuu wa Roshi, na Mesheki, na Tubali;
4 nami nitakugeuza na kutia kulabu katika mataya yako, nami nitakutoa, pamoja na jeshi lako lote, farasi na hao wapandao farasi, wote wamevaa silaha za namna zote, jeshi kubwa sana, wenye ngao na kigao, wote wakishika upanga;
5 Uajemi, na Kushi, na Putu, pamoja nao; wote wana ngao na chapeo;
6 Gomeri, na vikosi vyake vyote; nyumba ya Togarma, pande za mwisho za kaskazini, na vikosi vyake vyote; naam, watu wengi pamoja nawe.
7 Ujiweke tayari, naam, jiweke tayari, wewe na majeshi yako yote waliokukusanyikia, nawe uwe jemadari wao.
8 NA BAADA YA SIKU NYINGI UTAJILIWA; KATIKA MIAKA YA MWISHO, UTAINGIA NCHI ILIYORUDISHIWA HALI YAKE YA KWANZA, BAADA YA KUPIGWA KWA UPANGA, ILIYOKUSANYWA TOKA KABILA NYINGI ZA WATU, juu ya milima ya Israeli, iliyokuwa ukiwa wa daima; lakini imetolewa katika kabila za watu, nao watakaa salama salimini wote pia.
9 Nawe utapaa juu, utakuja kama tufani, utakuwa kama wingu kuifunika nchi, wewe, na vikosi vyako vyote, na kabila nyingi za watu pamoja nawe.
10 BWANA MUNGU ASEMA HIVI; ITAKUWA KATIKA SIKU HIYO, MAWAZO YATAINGIA MOYONI MWAKO, NAWE UTAKUSUDIA KUSUDI BAYA;
11 nawe utasema, Nitapanda juu niiendee nchi yenye vijiji visivyo na maboma; nitawaendea watu wanaostarehe, wanaokaa salama, wote wakikaa pasipo kuta, ambao hawana makomeo wala malango;
12 ili kuteka mateka, na kuwinda mawindo; uugeuze mkono wako juu ya mahali palipoharibika, ambapo sasa panakaliwa na watu, na juu ya watu waliokusanyika toka mataifa, waliopata ng’ombe na mali, wakaao katikati ya dunia.
13 Sheba, na Dedani, na wafanya biashara wa Tarshishi, pamoja na wana-simba wake wote, watakuambia, Je! Umekuja kuteka mateka? Umekusanya jeshi lako, ili kuwinda mawindo? Kuchukua fedha na dhahabu, kuchukua ng’ombe na mali, kuteka mateka mengi sana?
14 Basi, mwanadamu, tabiri, umwambie Gogu, Bwana MUNGU asema hivi; Katika siku ile watu wangu, Israeli, watakapokaa salama, hutapata habari?
15 Nawe utakuja kutoka mahali pako, kutoka pande za mwisho za kaskazini, wewe, na watu wa kabila nyingi pamoja nawe, wote wamepanda farasi, kusanyiko kubwa, na jeshi kuu;
16 NAWE UTAPANDA JUU UWAJILIE WATU WANGU, ISRAELI, KAMA WINGU KUIFUNIKA NCHI; ITAKUWA KATIKA SIKU ZA MWISHO, NITAKULETA UPIGANE NA NCHI YANGU, ILI MATAIFA WANIJUE, nitakapotakaswa kwako, Ewe Gogu, mbele ya macho yao.
17 Bwana MUNGU asema hivi; Je! Wewe ndiwe niliyemnena zamani za kale, kwa vinywa vya watumishi wangu, manabii wa Israeli, waliotabiri siku zile kwa muda wa miaka mingi, ya kwamba nitakuleta upigane nao?
18 Itakuwa katika siku hiyo, Gogu atakapokuja kupigana na nchi ya Israeli, asema Bwana MUNGU, ghadhabu yangu itapanda katika mianzi ya pua yangu.
19 Kwa maana katika wivu wangu, na katika moto wa ghadhabu yangu, nimenena, Hakika katika siku ile kutakuwako tetemeko kubwa katika nchi ya Israeli;
20 hata samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama wa kondeni, na vitu vyote vitambaavyo juu ya nchi, na wanadamu wote walio juu ya uso wa nchi, watatetemeka mbele ya uso wangu; nayo milima itatupwa chini, na magenge yataanguka, na kila ukuta utaanguka chini.
21 Nami nitaita upanga, uje juu yake katika milima yangu yote, asema Bwana MUNGU; nao upanga wa kila mtu utakuwa juu ya ndugu yake.
22 Nami nitamhukumu kwa tauni, na kwa damu; nami nitanyesha mvua ifurikayo, na mvua ya mawe makubwa sana, na moto na kiberiti juu yake, na vikosi vyake, na watu wa kabila nyingi walio pamoja naye.
23 Nami nitajitukuza, na kujitakasa, na kujidhihirisha, mbele ya macho ya mataifa mengi; nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana”.
Sasa Nchi ya Magogu, biblia inayoitaja hapo ni eneo linalojulikana kama URUSI kwasasa. Hivyo nchi hii leo tunaoina ni nchi yenye nguvu sana kiasi kwamba inalitishia hata taifa la Marekani kwa nguvu zake na ukuu wake. Lakini biblia inasema siku moja mawazo yataliingia hili taifa ili kwenda kuishambulia Israeli. Na kibaya zaidi halitashuka peke yake, hapana bali litashuka na majeshi ya mataifa mengine mengi kama tunavyoyasoma hapo juu. Na mengi ya hayo yatakuwa na haya mataifa ya kiharabu, ambayo hayo kimsingi ni maadui wa Israeli tangu zamani, pamoja na nchi nyingi zilizokando kando ya Urusi.
Wote watapanga vita kuiendea ile nchi ndogo sana Israeli. Kama tunavyoona hata sasa Taifa linaloongoza kuwa na maadui wengi duniani ni taifa la Israeli, hivyo Urusi kwa kujipendekeza na kujionyesha kuwa yeye anayo nguvu na kwamba anaweza kuwasaidia watu waliwashindwa ISRAELI. Yeye naye siku hiyo atapanga vita na mabomu yake ya Atomiki ili kwenda kulisambaratisha taifa lile. Hawajui kuwa hapo ndipo Mungu alipokusudia uwe mwisho wa mataifa hayo yote chini ya jua. Siku hiyo Urusi itapotezwa kwenye ramani ya dunia, kwasababu Bwana atakuwa upande wa Israeli. Na wa-Rusi siku hiyo watasoma maandiko haya ya Ezekieli na kutambua kuwa unabii huo ulikuwa unawahusu wao.
Kumbuka vita hiyo japo itauwa watu wengi sana kiasi kwamba biblia inasema mizoga yao itakuwa inazikwa kwa muda wa miezi 7 ikikusanywa tu, na silaha zao zitakuwa zikitumika kama kuni kwa muda wa miaka 7, lakini huo utakuwa ni mwanzo tu wa utungu. Vita yenyewe kuu bado. Vita ya Har-magedoni ambayo itahusisha mataifa yote ulimwenguni.
Tutakuja kuizungumzia vizuri vita hii [Har-Magedoni] katika makala nyingine. Lakini tufahamu kuwa vita inayozungumziwa katika Ezekieli 38-39 ipo mbioni kutokea, kama tunavyoona sasahivi mvutano ulivyo mkubwa mashariki ya kati na ishara kuwa vita vinajiandaa kupiganwa muda wowote. Hivyo ndivyo Mungu anavyozidi kuitasa Israeli kidogo kidogo, Na ndivyo pia wanavyojiandaa kumpokea Masiya wao.
Swali tujiulize wakati sasahivi neema inarudi Israeli, mimi na wewe mpaka mambo hayo yatakapotokea tutakuwa wapi? Kumbuka ndugu tuliambiwa tukiyaona hayo yanaanza kutokea basi tunyanyue vichwa vyetu, kwa kuwa ukombozi wetu umekaribia. Ikiwa na maana UNYAKUO wetu upo karibu.
Kristo yupo mlangoni ndugu. Unasubiri nini usiufanye leo wito wako na uteule wako imara?. Walioishi kipindi chote cha nyuma kuanzia miaka ya 1900 kurudi nyuma mpaka kipindi cha kanisa la kwanza hawakukishuhudia kitu hichi sisi tunachokishuhudia leo yaani taifa huru la Israeli. Na biblia ilishasema kizazi hiki hakitapita, sasa unasubiri nini usiushindanie wokovu katika muda huu mfupi uliobaki?.
Ungependa mambo hayo yakukute kwa ghafla, Bwana amesema dunia hii itaangamizwa kwasababu ya maovu yake. Na wenye haki watapata kwa Mungu waepushwe nayo.. je! Na wewe ungependa uwe miongoni mwa watakaoharibiwa katika ile siku ya Bwana? Kama sivyo mgeukie Kristo, ambaye yeye ndio safina pekee iliyothibitishwa na Mbingu kwa wokovu wa mwanadamu.
Bwana akubariki.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP