Category Archive Mafundisho

JAWA NA UPENDO UNAOTAFUTA.

Wimbo Ulio Bora 3:1-4

[1]Usiku kitandani nalimtafuta mpendwa wa nafsi yangu, Nalimtafuta, nisimpate.

[2]Nikasema, Haya, niondoke nizunguke mjini,  Katika njia zake na viwanjani,

Nimtafute mpendwa wa nafsi yangu. Nikamtafuta, nisimpate.

[3]Walinzi wazungukao mjini waliniona; Je! Mmemwona mpendwa wa nafsi yangu?

[4]Kitambo kidogo tu nikiisha kuwaondokea, Nikamwona mpendwa wa nafsi yangu; Nikamshika, nisimwache tena,  Hata nilipomleta nyumbani mwa mamangu,  Chumbani mwake aliyenizaa.

Kitabu cha wimbo ulio-bora, ni kitabu ambacho huchukiliwa kimwili na watu wengi kana kwamba kiliandikwa mahususi kwa wana-ndoa.. Jambo ambalo sio kweli, Ikumbukwe kuwa dhumuni kuu la biblia ni kutueleza WAZO la Mungu, juu yetu ambalo hilo alilikamilisha kifasaha kupitia Yesu Kristo. Hivyo popote pale unapopasoma kwa namna moja au nyingine inaeleza kusudi la Mungu kwetu, katika kuyatimiza mapenzi yake..

Na ni kawaida yake tangu zamani  kutumia mifano halisi ya namna mbalimbali ili kudhihirisha kusudi lake kamilifu kwetu.

Kwamfano ameweka familia, tujue sifa za wazazi ili tunapomwita Mungu Baba, tujue tabia za ubaba hasaa zipoje…Ameweka mabwana na watumwa ili tunapomwita yeye Bwana tujue sisi tunapaswa tuweje kwake kama watumwa..

Vivyo hivyo ameweka ndoa, na akajifunua kwetu kama mume, na sisi kanisa ni mke wake…Hivyo anataka tujue kama vile upendo wa mke na mume ulivyo ndivyo alivyo yeye kwetu sisi.

Sasa Katika habari hii, tunaona sifa ya upendo ambao Mungu anataka sisi tuuonyeshe kwake, Upendo usio ule wa upande mmoja, bali na upande wa pili, yaani sio  tu yeye kututafuta sisi wakati wote hapana bali Na sisi tumtafute yeye..

Anaeleza kwa mfano wa igizo picha ya  mwanamke ambaye yupo sikuzote na mpenzi Wake kitandani, lakini ikatokea siku moja alipoamka usiku hakumwona kitandani Mwake…

Hivyo hakuweza kuendelea kulala angali mumewe hayupo, ikambidi atoke aanze Kumtafuta usiku ule ule, sio kwa siri Bali hadharani tena sehemu zenye hatari ambazo walinzi tu usiku hupita kufanya doria..Na alipokutana Nao akawauliza juu ya mpenzi wake kama wamemwona, lakini Baadaye kidogo alimwona..akamkumbatia na kurudi naye mpaka mahali pao maalumu.

Ufunuo wake ni upi.

Yapo majira wewe kama mwana wa Mungu utapitia pengine hali fulani ya kushuka viwango kiroho, (ukame wa kiroho)

Lakini ukiwa na upendo wa kweli kwa Mungu wako, ni wazi kuwa hutakaa tu na kusema Mungu nisaidie…Hapana Utachukua tu hatua kama za huyu mwanamke ya kuamka na kuanza kutafuta namna ya kumtafuta mpenzi wako (Kristo) yaani kurejesha viwango vyako vya mwanzoni, hata kwa kugharimika raha, au vitu n.k..

Ndio hapo mtu hutenga muda mwingi wa maombi, mikesha, mifungo n.k.

Na kama vile yule Mwanamke alipowafuata walinzi usiku, kuwauliza habari za mumewe…Ndivyo ilivyo kwa mtu mwenye kiu na pendo na Mungu hataridhika kutembea yeye kama yeye tu, ataulizia msaada mpaka kwa viongozi wake wa kiroho apate mwongozo..(ambayo hufunua wale walinzi). Na hatimaye kufikia kilele cha mahusiano na Mungu wake tena.

Ndugu, kumbuka kuwa furaha, na amani, uzuri wa Kristo sio tu wa kuletewa sikuzote, bali pia wa kutafuta…Ni kweli siku za kwanza za wokovu uliona Kristo akijifunua Kwako kwa namna za ajabu, hata kama hukufanya lolote lakini sasahivi ni kama huoni moto ule ule uliokuwa nao…jua tu si kwamba umetenda dhambi au umemkosea Mungu…hapana ni kwamba Mungu anataka amke sasa mtafuta mpenzi wako..kudhihirisha upendo wa kweli..

Ndicho Yesu alichowaambia wale waandishi na mafarisayo juu ya wanafunzi wake..

Marko 2:18 Nao wanafunzi wake Yohana na Mafarisayo walikuwa wakifunga; basi walikuja, wakamwambia, Kwani wanafunzi wa Yohana na wanafunzi wa Mafarisayo hufunga, bali wanafunzi wako hawafungi?
19 Yesu akawaambia, Walioalikwa arusini wawezaje kufunga maadamu bwana-arusi yupo pamoja nao? Muda wote walipo na bwana-arusi pamoja nao hawawezi kufunga.
20 Lakini siku zitakuja watakapoondolewa bwana-arusi, ndipo watakapofunga siku ile

Ongeza mikesha, mifungo, kusoma Neno sana…Na hatimaye utavipata na furaha yako itazidi ile ya kwanza…

Kwasababu upendo wa kweli hutafuta…

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 11 (Mithali, Wimbo ulio bora, Mhubiri)

Naomba kujua maana ya haya maneno katika biblia..“Siti Msharifu”, “Mitalawanda” na “kulalama”

Mimi ni mweusi-mweusi, lakini ninao uzuri.

Print this post

HEKIMA ILIYO SAHIHI, KATIKA HIMIZO LA UTOAJI SADAKA.

Mfalme mmoja wa Israeli aliyeitwa Yoashi aliingiwa na wazo la kutaka kuikarabati nyumba ya Mungu (Hekalu), na kuamsha tena shughuli za kiibada zilizokuwa zimeharibiwa Na watawala wabovu waliotangulia..

Hivyo kwa kuwa alijua ukarabati unahitaji fedha, alichukua hatua ya kuwatoza watu kodi ya nyumba ya Mungu..Ambayo iliagizwa katika torati na Musa..(2Nyakati 24:9)

Hivyo akawateuwa  Walawi, walisimamie jambo hilo tangu mwanzo hadi mwisho, lakini likawa kama linacheleweshwa…

Mpaka baadaye akawauliza tena, kwanini kazi inacheleweshwa, kwa kuona hakuna chochote kilichofanyika..

Lakini mfalme akaja na mkakati mwingine, ili shughuli hiyo ifanyike kwa haraka na wakati, akaona kuliko Kuwalazimisha watu kulipa kodi ngoja aweke sanduku kubwa katika lango la hekalu na kupiga panda kwa watu wote wa Yuda waje kumtolea Mungu wao kwa hiari, bila shuruti..

Na wazo lile likapendwa na watu wengi, na hatma yake makusanyo yakawa mengi, kila siku mpaka wakapata fedha za kuwaajiri wajenzi ili kulikarabati hekalu, na kutengeneza vyombo vya nyumba ya Mungu.

2 Mambo ya Nyakati 24:6-14

[6]Mfalme akamwita Yehoyada mkuu wao, akamwambia, Mbona hukuwataka Walawi waitoze Yuda na Yerusalemu kodi ya Musa mtumishi wa BWANA, na ya kusanyiko la Israeli, kwa ajili ya hema ya ushuhuda?

[7]Kwa kuwa wana wa Athalia, yule mwanamke mwovu, walikuwa wameibomoa nyumba ya Mungu; na vitakatifu vyote vya nyumba ya BWANA wamewapatia mabaali.

[8]Basi mfalme akaamuru, nao wakafanyiza kasha, wakaliweka nje langoni pa nyumba ya BWANA.

[9]Wakapiga mbiu katika Yuda na Yerusalemu, kumletea BWANA kodi aliyoiweka Musa mtumishi wa Mungu, juu ya Israeli jangwani.

[10]Wakafurahi maakida wote na watu wote, wakaleta na kutia ndani ya kasha, hata wakaisha.

[11]Ikawa wakati walipoletewa kasha wasimamizi wa mfalme kwa mkono wa Walawi, nao wakaona ya kwamba kuna fedha nyingi, huja karani wa mfalme, na msimamizi wake kuhani mkuu, wakatoa yaliyomo kashani, kisha hulichukua kasha, na kulirudisha mahali pake. Ndivyo walivyofanya siku kwa siku, wakakusanya fedha tele.

[12]Na mfalme na Yehoyada waliwapa hao waliofanya kazi ya utumishi wa nyumba ya BWANA; nao wakawaajiri waashi na maseremala ili kuitengeza nyumba ya BWANA, na hao pia wafuao chuma na shaba ili kuitengeza nyumba ya BWANA.

[13]Hivyo mafundi wakafanya kazi yao, nao wakaimaliza, wakaisimamisha nyumba ya Mungu kama ilivyopasa, wakaifanya imara.

[14]Nao walipokwisha, wakaleta mbele ya mfalme na Yehoyada fedha iliyobaki, vikafanyizwa kwayo vyombo vya nyumba ya BWANA, vyombo vya utumishi, navyo vya kutolea, na miiko, na vyombo vya dhahabu na fedha. Wakatoa sadaka za kuteketezwa katika nyumba ya BWANA, daima, siku zote za Yehoyada.

Ni nini tunafundishwa Na Roho Mtakatifu..

Utoaji wenye baraka na anaouhitaji Mungu ni ule wa hiyari na sio wa kulazimishwa…kama kanisa la Kristo Lazima tufikie hatua hii, kwamba viongozi hawawashurutishi watu kutoa mchango, mfano Zaka, Kama vile himizo la kodi, kwamba usipotoa unachukuliwa sheria ya kinidhamu …lakini pia watu nao wanawajibika wenyewe kumtolea Mungu kwa uaminifu na moyo..kanisa lifikiapo hatua hii ya kiroho, Mungu huliongezea baraka sana.

Usikubali kukumbushwa-kumbushwa, au kuhimizwa-himizwa kumtolea Mungu, Bali mtolee Mungu zaka zako, sadaka zako, kwa moyo wa furaha, Bwana atakubariki.

2 Wakorintho 9:6-8

[6]Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu.

[7]Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.

[8]Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema;

Bwana awabariki..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Print this post

Fahamu maana ya Mithali 21:3 Kutenda haki na hukumu  Humpendeza BWANA kuliko kutoa sadaka.

SWALI: Nini maana ya Mithali 21:3

[3]Kutenda haki na hukumu  Humpendeza BWANA kuliko kutoa sadaka.

JIBU:

Mstari huo unatufundisha mambo ambayo Mungu huvutiwa nayo zaidi…

Mungu hupendezwa zaidi na sisi tunapoishi maisha ya haki, tunatenda mema, tunawajali wengine, tunaishi sawasawa ni viwango vyake vya kiroho hapa duniani..kwake hiyo ni bora zaidi ya sadaka zetu tumtoleazo.

Sadaka huwakilisha mambo yote Ya kidini tunayoweza kumfanyia Mungu, mfano ibada, fedha, mifungo, maombi, kuhubiri, kuimba n.k

Bwana huvutiwa zaidi na mioyo na tabia zetu, na sio zile Ibada za nje tu..

Haimaanishi kuwa hapendezwi na hivyo vitu hapana…bali hivyo vifanywe baada ya kutii kwanza..

Tunaona jambo kama hilo amelisisitiza sehemu nyingi kwenye maandiko; Tukianzia kwa Sauli alimwambia, hivyo;

1 Samweli 15:22

[22]Naye Samweli akasema,  je! BWANA huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu  Sawasawa na kuitii sauti ya BWANA? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu,  Na kusikia kuliko mafuta ya beberu.

Mika 6:6-8 inasema;

[6]Nimkaribie BWANA na kitu gani, na kuinama mbele za Mungu aliye juu? Je! Nimkaribie na sadaka za kuteketezwa, na ndama za umri wa mwaka mmoja?

[7]Je! BWANA atapendezwa na elfu za kondoo waume, au na elfu kumi za mito ya mafuta? Je! Nimtoe mzaliwa wangu wa kwanza kwa kosa langu, mzao wa mwili wangu kwa dhambi ya roho yangu?

[8]Ee mwanadamu, yeye amekuonyesha yaliyo mema; na BWANA anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako!

Soma pia..

Isaya 1:11-17 – Inasema…Bwana huchukizwa na sadaka za watu wanaishi katika dhambi

Hivyo ni lazima tujiulize Je! tunatenda haki kwa wengine?

Je! Tunatembea kwa unyenyekevu mbele ya Mungu wetu?

Je! tunamtii Mungu, kuliko vitu vingine vyovyote?

Je tunawahurumia wengine…?

Mambo kama haya ndio yenye uzito zaidi kwa Mungu.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

JE NI KUTII AU KUPATA KWANZA MAARIFA?

Maana ya 2Wakorintho 9:11 mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote

MCHE MWORORO.

Print this post

Kijana ni nani kibiblia?

Biblia haitoi umri fulani maalumu kwamba mtu akiufikia huo basi ndio huitwa kijana.. Japokuwa ni mtu ambaye yupo umri wa hapo katikati yaani utoto na utu uzima, lakini hutambulika kwa kuangalia vitu kama hatua za ukuaji wake, uwajibikaji wake na uzoefu wake wa kimaisha.

Kwamfano katika biblia watu hawa walitajwa kama vijana.

  • Ishmaeli (mwanzo 21:14-20)
  • Isaka (Mwanzo 22:5)
  • Yusufu mwanzo 42:22. (Akiwa na miaka 17)
  • Mfalme Sauli (1Samweli 9:2)
  • Timotheo (1Timotheo 4:12)

Na wengine kadha wa kadha..

Yafuatayo ni Mambo ambayo kijana yeyote anatarajiwa awe nayo kibiblia.

1) Awe anamtafuta Mungu Na kulitii Neno la Mungu.

Mhubiri 12:1

[1]Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo. 

Zaburi 119:9

[9]Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako. 

2) Awe na hekima na tabia ya uongozi, (yaani wakati wote ajifunze kuwa kielelezo.)

1 Timotheo 4:12

[12]Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.

3) Awe na nguvu za rohoni, za kumshinda shetani.

Mithali 20:29

[29]Fahari ya vijana ni nguvu zao,..

1 Yohana 2:14

[14]Nimewaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu.

Lakini pia kijana anakabiliwa na tamaa za ujanani kama vile uzinzi, anasa,starehe..hivyo Anatarajiwa azikimbie wakati wote.

2 Timotheo 2:22

[22]Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.

Kutokana na vigezo hivyo tunaweza Kuona ujana pengine huanzia umri wa kubalehe, mpaka wakati mtu anapungua Nguvu zake mwilini.. labda Miaka 12-45…japo yaweza kupungua au kuzidi..

Zingatia:

Ikiwa wewe ni kijana, hakikisha maonyo hayo unayatendea kazi mapema…

Lakini ikiwa wewe ni mzazi na una mtoto, fahamu kuwa siku moja atakuwa kijana,hivyo kabla adui hajamtumia, anza kumjengea misingi mizuri ya kutembea katika Imani ya wokovu, naye hataicha njia hiyo mpaka atakapokuwa mtu mzima

Mithali 22:6

[6]Mlee mtoto katika njia impasayo,

Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

VIJANA NA MAHUSIANO.

Je Bwana YESU alikuwa na amri ya kumwingiza mtu katika ufalme wa MUNGU au hakuwa nayo?

Fahamu maana ya Mithali 10:5 Akusanyaye wakati wa hari ni mwana mwenye hekima; 

Print this post

SAFARI YA KUUONA USO WA MUNGU.

Musa (Mgongo)

Kristo (kioo)

Mbinguni (Dhahiri)


Ilikuwa ni shauku ya Musa kutaka Kuuona uso wa Mungu baada ya muda mrefu kukaa bila kumwona Mungu..

Lakini tukirudi kwenye maandiko yanasema, Mungu alizungumza na Musa uso kwa uso kama mtu anavyozungumza na rafiki yake.

Kutoka 33:11 Naye Bwana akasema na Musa uso kwa uso, kama vile mtu asemavyo na rafiki yake. Kisha akageuka akarejea hata maragoni; bali mtumishi wake Yoshua, mwana wa Nuni, naye ni kijana, hakutoka mle hemani.

Lakini iweje tena, aombe kuuona uso wa Mungu, na Mungu kumwambia huwezi kuuona uso wangu ukaishi?

Kutoka 33:20 Kisha akasema, Huwezi kuniona uso wangu, maana mwanadamu hataniona akaishi.

21 Bwana akasema, Tazama, hapa pana mahali karibu nami, nawe utasimama juu ya mwamba;

22 kisha itakuwa wakati unapopita utukufu wangu, nitakutia katika ufa wa ule mwamba, na kukufunika kwa

mkono wangu hata nitakapokuwa nimekwisha kupita;

23 nami nitaondoa mkono wangu, nawe utaniona nyuma yangu, bali uso wangu hautaonekana

Ukweli ni kwamba kuuona uso wa Mungu, sio kuona mwonekano Fulani, au umbo Fulani la Mungu. Hapana, bali ni kumjua yeye ndani ni nani.. Tangu zamani Mungu alikuwa akijifunua kwa wanadamu kupitia maumbile mbalimbali, ambayo yanaweza kuchukua taswira ya vitu, wanadamu au malaika(huitwa Theofania),. Hivyo kwa namna yoyote ile Mungu anapomtokea mtu kwa namna mojawapo ya hizo na kuisikia sauti yake kama vile mwanadamu mwenzako anavyozungumza na wewe, ni  sawa na kusema Mungu amesema nawe uso kwa uso. Lakini haimaanishi kuwa umeuona uso wake. Kuuona uso wake ni kumjua yeye ni nani.

Sasa Mungu akamwambia, Musa, huwezi kuniona ukaishi, Kwanini amwambie vile, Je! Mungu ni kifo? Hapana, Mungu ni uzima, lakini Musa alikuwa bado hajakamilika kwasababu ya dhambi, hivyo utukufu wa Mungu asingeweza kuustahimili, kwasababu wakati wa kuustahimili ulikuwa bado, kwani ulihitaji kwanza ondoleo la dhambi kabisa.

Hivyo Mungu akamwonyesha sehemu yake ya nyuma (Mgongo). Lakini Uso hakuuona.. Ndipo akamjua Mungu kwa sehemu yeye ni nani..

Alipomwona alishangaa sana, kwa zile tabia na sifa, Mungu alizokuwa nazo, jinsi zilivyo tofauti na mawazo ya wanadamu.. Pengine alijua ataona mafunuo makubwa ya nguvu na uweza, na mamlaka, ya ukuu, na utukufu usioelezeka kibinadamu, lakini alipomwona Mungu alimwona ni mwenye huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema, mwenye hukumu za haki.

Kutoka 34:5-7

5 Bwana akashuka ndani ya lile wingu, akasimama pamoja naye huko, akalitangaza jina la Bwana.

6 Bwana akapita mbele yake, akatangaza, Bwana, Bwana, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si

mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli;

7 mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; wala si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; mwenye kuwapatiliza watoto uovu wa baba

zao, na wana wa wana wao pia, hata kizazi cha tatu na cha nne.

Hata sasa, mtu anayemtambua Mungu kwa namna hii,  basi ameuona mgongo wa Mungu.. Na pale mtu anapoiga tabia hizo basi, amemkaribia Mungu sana.

Lakini safari ya kuuona Uso wa Mungu, ilikuwa bado haijakamilika..

Uso (Katika kioo)

Hivyo wakati ulipofika, Mungu akamtuma mwanawe duniani, (Yesu Kristo), kutuonyesha sasa uso wa Mungu ulivyo..Maandiko yanasema hivyo;

Yohana 1:18 Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua.

Umeona kumbe, hakukuwahi kutokea mtu duniani aliyeuona uso wa Mungu, na moja ya kazi kubwa aliyokuja kuifanya Yesu duniani ni kumfunua Mungu(uso wake) ni nani?

Na kwasababu hakuna mtu mwenye dhambi anayeweza kumwona Mungu akaishi, ilimbidi yeye mwenyewe awe fidia ya dhambi zetu, kwa kufa kwake pale msalabani, ili sisi tuhesabiwe kuwa hatuna dhambi (kwa neema), na ndipo sasa tustahimili kuuona utukufu wa Uso wa Mungu.

Na alipotukamilisha kwa namna hiyo, basi, akatuwezesha pia kumkaribia Mungu tumwone.

Yesu akatufunulia uso wa Mungu, kuwa yeye ni UPENDO. Na upendo wake si ule wa kibinadamu, , kwamba nakupenda kwasababu umenipenda, au umenitendea jambo zuri.. Hapana, bali ni ule usio na sharti wa kuonyesha fadhili hata kwa wanaotuchukia..

Musa, aliishia kujua huruma tu za Mungu  juu juu (kibinadamu), lakini hakujua kuwa hata jino kwa jino, ilikuwa ni makosa, kumwonea mwenzako hasira, au hata kumfolea ilikuwa ni makosa, yanayostahili hukumu,  talaka Mungu hapendezwi nazo.. Musa hakujua kuwa Mungu anataka tumwone yeye kama BABA, ambaye ni ‘ABA’ yaani Baba mwenye mahusiano ya karibu na mwanawe, kama ilivyokuwa kwa Yesu na Mungu,yeye alidhani Mungu ni wa kutoa tu amri, sheria na hukumu, Musa hakujua kuwa mwenye dhambi (mfano wa mzinzi, mwanamke mchawi) hapaswi kutupiwa mawe, bali kuhubiriwa injili ili atubu.. Yote hayo Yesu alikuja kutufunulia, kiufasaha kabisa wala hakutuficha chochote..

Kwa jinsi nyingine ni kuwa sisi tumemwona Mungu kupitia Kristo, na kwa kupitia uhalisia wa maisha yake. Tukiyaishi maneno ya Kristo, basi tumemjua Mungu uso wake, kiufasaha kabisa..

Lakini Safari bado inaendelea… Uso wa Mungu katika kilele chake, bado hatujaufikia…

Utauliza kwa namna gani?

Uso dhahiri (mbinguni)

Ni kwamba kwasasa tunauona kwa njia ya KIOO, bado hatujauona kiuhalisia kabisa kwa macho, japo tunaweza kusema kuona kwenye kioo hakuna tofauti na kuona kabisa kwa macho, lakini ladha huwa zinatofautiana, kumwona Raisi kwenye Tv, ni Yule Yule utakayemwona kwa macho, lakini ladha ni tofauti..

Hivyo Kristo alikuwa kama chapa (kioo) ya Mungu yenyewe, duniani..Yaani sisi tayari tumemwona Mungu kupitia Kristo Yesu..

Waebrania 1:3 Yeye kwa kuwa ni mng’ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu;

Ndio maana maandiko bado yanasema, kwasasa tunaona kwa kioo, lakini wakati ule tutamjua sana yeye alivyo..

1Wakorintho 13:12 Maana wakati wa sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule tutaona uso kwa uso; wakati wa sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana kama mimi nami ninavyojuliwa sana.

Wakati wa kuona dhahiri, wema wote wa Mungu, itakuwa ni mbinguni.

Tutamjua katika eneo gani?

Katika eneo lilelile la upendo, (sawasawa na ile 1Wakorintho 13 ilivyokuwa inaeleza habari hiyo tangu juu)

Hapo ndipo tutaufurahia upendo wa Mungu katika namna ambayo hatujawahi kuijua, kwa vile vitu tulivyoandaliwa na yeye mbinguni, milele…

Hivyo, hatuna budi sasa kutembea katika upendo wa Mungu kwasababu yeye ndio huo..

1Yohana 4:16 Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake.

Hitimisho:

Hatua za kuuona  Uso wa Mungu, zilianza, na Musa, (kwa mgongo), zikaja kwa Kristo (kwa kioo), na mwisho mbinguni, (dhahiri).

Je! Umempokea Kristo? Ikiwa bado, fahamu kuwa  huwezi kamwe kumwona Mungu, hata iweje, mpokee leo, akuoshe dhambi zako, kwasababu kumbuka pia alimwambia Musa, hatamwesabia mtu mwovu kuwa hana hatia, yaani kila mmoja atapewa anachostahili. Ukifa katika dhambi zako, hakuna upendo huko kuzimu, hutatolewa huko na kuletwa mbinguni.. kwasababu umechagua mwenyewe giza. Yesu alisema Jehanamu ya moto ipo, na mtu asipomwamini yeye, atakufa katika dhambi zake. Hivyo ndugu, Ingia ndani ya Yesu leo upokee neema, hujui ni lini utaondoka duniani, usiishi tu kama mnyama, tubu dhambi mkimbilie Yesu, akuponye.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

UPENDO NI NINI NA JE! KUNA AINA NGAPI ZA UPENDO?

NI NANI ATAKAYETUTENGA NA UPENDO WA KRISTO?

UFAHAMU UFUNGUO WA KUMPENDA BWANA ZAIDI

Print this post

Je tunajazwaje maarifa ya mapenzi yake? (Wakolosai 1:9)

Wakolosai 1:9

[9]Kwa sababu hiyo sisi nasi, tangu siku ile tuliposikia, hatuachi kufanya maombi na dua kwa ajili yenu, ili mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni;

JIBU:

Vifungu hivyo vinaonyesha kiu ya mtume Paulo juu ya watakatifu wa kanisa la Kolosai, Kwamba wajawe kuyajua mapenzi ya Mungu katika hekima yote na ufahamu wa rohoni.

Alijua ili kanisa liweze kumpendeza Mungu na kusimama ni lazima lijue mapenzi ya Mungu makamilifu.. Hivyo Ikawa shauku yake tangu zamani lijazwe kujua mapenzi hayo.

Mapenzi ya Mungu ni yapi?

Kuna makundi mawili (2), ya mapenzi ya Mungu.

1)Mapenzi Ya daima

2) Mapenzi Ya wakati

Mapenzi ya daima: Ni yale ambayo yapo wakati wote, na kwa wote kwamba kila mwamini lazima ayatimize..mfano wa haya ni..ni kama utakatifu (1Wathesalonike 4:3), kuhubiri Injili, kuishi kwa upendo, kukusanyika pamoja, kudumu katika maombi, kumwabudu Mungu.

Lakini mapenzi ya wakati: Ni yale ambayo Mungu anakusudia uyafanye katika kipindi fulani tu, ni mapenzi yasiyo na mfanano, au mwendelezo fulani.. Kwamfano Mungu anakutaka leo usihubiri, bali uende kumtembelea yatima mmoja kijijini. Mfano wa kama alivyoambiwa Filipo awaache makutano aende jangwani kwa ajili ya yule mtu mmoja mkushi.(matendo Matendo 8:26)

Au wakati mwingine unapitishwa katika jaribu fulani, halafu pasipo kujua kuwa hilo ni darasa la Mungu ili kutumiza kusudi fulani, unajikuta unakemea na kushindana nayo…Ndio maana Bwana Yesu alipoomba juu ya kuondolewa kikombe cha mateso, alimalizia kwa kusema Baba mapenzi yako yatimizwe.

Sasa yote haya yanahitaji hekima na maarifa kuyatambua na kuyatimiliza. Si rahisi kuyatambua kwa akili za kibinadamu au kuyatimiliza.

Lakini Swali linakuja mtu anawezaje kupata maarifa hayo ya mapenzi ya Mungu?

1) Kwa maombi.

Jambo la kwanza Paulo analitaja ni kuomba, aliwaombea watakatifu Wa Kolosai kwasababu alijua uwezekano wa kupokea Maarifa hayo upo katika maombi.

Yakobo 1:5

[5]Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.

Maombi hufungua mlango wa Mungu kuyaingilia maisha yetu na kututia katika kusudi Lake kamilifu. Mungu anafanya kazi ndani yetu kupitia maombi…Bila uombaji haiwezekani kutembea ndani ya mapenzi yote ya Mungu.

2) Neno la Mungu.

Kwa kusoma Neno ndipo unapojua Tabia za Mungu, nini anataka na nini hataki. Sauti ya Mungu, maagizo ya Mungu ya moja kwa moja yasiyohitaji usaidizi ni biblia takatifu.

Zaburi 119:105

[105]Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu.

Mtu ajijengeaye tabia ya kusoma biblia, si rahisi kuanguka au kutoka nje ya mpango wa Mungu. Kwasababu lile neno linakaa ndani yake kama mafuta kumfundisha.

3) Mashauri Ya kikristo.

Bwana anafunua mapenzi yake tuwapo katika mabaraza yetu kutafakari maneno yake.. alisema wawili watatu kwa jina lake yupo hapo hapo katikati yao…Wale watu wawili waliokuwa wanakwenda Emau, tunaona walikuwa zaidi ya mmoja, ndipo wakiwa katika kutafakari habari za Kristo, Aliungana nao bila hata wao kujua akaanza kuwafundisha, na mwisho wote kujua mapenzi makamilifu ya Mungu ni nini..(Luka 24)

Na ndio maana hatupaswi kulikwepa kanisa kwasababu huko tunaungana na viungo vingi katika Mwili wa Kristo, na hivyo kujengana na kuonyana. Hatimaye mapenzi ya Mungu yanafunuliwa kwetu.

Hata wakati ule kulipotokea sintofahamu ndani ya kanisa kuhusu vyakula na sheria..baraza lilikalishwa kule Yerusalemu kisha mahojiana mengi yakaendelea …lakini mwishoni Mungu alitoa maarifa kwa kusema wajiepushe.na damu na uasherati lakini sio mataifa watwikwe tena kongwa la torati lililowashinda wao.(Matendo 15 )

Hivyo ni vema kumshirikisha pia mpendwa mwenzako/ kanisa mpango wako, yapo mashauri ya ki-Mungu ndani yao yaliyojaa hekima yatakusaidia.

4) Upambanuzi wa kiroho

Huu ni uwezo wa Mungu ambao mtu humwingia kutokana na kiwango chake cha juu cha ukuaji wa kiroho (Waebrania 5:14).. Bila kutegemea kuomba au kumuuliza Mungu mtu hutambua lililo la kweli na lililo la uongo.. lililosahihi na lisilosahihi, la rohoni au la mwilini, lenye Mwongozo wa ki- Mungu au kibinadamu. Tunaweza kujua mapenzi ya Mungu kwa ujuzi huu, unaozalika kutokana na ukomavu wetu wa kiroho.

Hitimisho:

Hivyo wewe kama mwana wa Mungu, kumbuka ni sharti kutembea ndani ya mapenzi yake…madhara ya kutembea nje ya hayo ndio kama yale aliyoyasema Bwana kwenye Mathayo Mathayo 7:21..

[21]Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Baraka ni nini na kuna aina ngapi za baraka?.

Mwandishi na Uchambuzi wa kitabu cha kwanza cha Petro.(1Petro)

EPUKA KUJIFANYA HUJUI.

Print this post

FUNGUA KINYWA CHA ROHO MTAKATIFU KIHUDUMU.

Ahadi mojawapo ya Roho Mtakatifu Kwa wote waliompokea ni kupewa uwezo wa kuzungumza “ufahamu wa Mungu”, kwa vinywa vyao.

Ufahamu huu unaweza kujifunua katika maumbile mbalimbali aidha kwa kueleza habari zilizopita, au habari zijazo, au zinazoendelea sasa hivi, au kutoa maelekezo, au faraja, au neno la hekima, au maarifa, au uponyaji au baraka..Namna zote hizi kwa lugha rahisi huitwa utabiri / unabii.

Ukiwa kama mwamini ni vema kufahamu sehemu kubwa sana ambayo Roho Mtakatifu anaitumia kuhudumu ni katika vinywa vyetu. Ndio maana siku ile ya kwanza ya pentekoste aliposhuka, alikaa juu ya wale watu kama “ndimi za moto”. Maana yake ni kuwa huduma yake hasaa hujidhihirisha katika ndimi…ndio maana akaweka moto wake juu ya ndimi zao, lugha zao zikabadilishwa wakaanza kunena kwa lugha mpya.

Kwahiyo kinywa cha mtu aliyeokoka, ni kinywa cha Mungu duniani. Usipojifunza kukifungua kinywa chako kiufasaha, ujue hiyo ni namna mojawapo ya kumzimisha Roho Mtakatifu ndani yako.

Watu wengi hawajui kuwa kila mmoja amepewa uwezo wa kutabiri/ kuhutubu na sio suala la huduma fulani ya kinabii tu, hapana utauliza hilo lipo wapi kwenye maandiko? Soma..

Matendo 2:17 wana wenu na binti zenu watatabiri..

Lakini pia 1 Wakorintho 14:31. Inasema..

[31]Kwa maana ninyi nyote mwaweza kuhutubu mmoja mmoja, ili wote wapate kujifunza, na wote wafarijiwe.

Kuhutubu kama ilivyotumika hapo, ni kutabiri/ kusema ufahamu wa Mungu. Jambo ambalo ni la wote sio baadhi.

Sasa unafunguaje kinywa cha Roho Mtakatifu na unafanya hivyo katika mazingira gani?

Usisubiri mpaka karama fulani ije juu yako, yaani kuonyeshwa/kufunuliwa.. hapana…kwasababu tayari una Roho Mtakatifu ndani yako anza kusema maneno yanayolandana na ahadi za Neno la Mungu, bila kufikiri- fikiri

Kwamfano…

Umepelekwa kwenye mashtaka fulani kwa ajili ya Neno. Au unatakiwa uwasilishe hoja, au ufundishe Neno, au uhubiri, au umekwenda mtaani kushuhudia.. usianze kusema mimi nitawezaje kuhubiri, au kujieleza, sijui sheria, sijui vizuri biblia, sijui kupangilia maneno…hupaswi kufikiri hivyo. bali ukumbuke ulishapewa kinywa cha moto, tangu siku ulipoamini, wewe nenda kisha anza kuzungumza huko huko katikati ya maneno yako Roho Mtakatifu ataunganika na wewe.

Mathayo 10:18-20

[18]nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao na kwa mataifa.

[19]Lakini hapo watakapowapeleka, msifikiri-fikiri jinsi mtakavyosema; maana mtapewa saa ile mtakayosema.

[20]Kwa kuwa si ninyi msemao, bali ni Roho wa Baba yenu asemaye ndani yenu.

Mwingine atakuambia mimi siwezi kuomba masafa marefu ninaishiwa na maneno…ndugu hupaswi kukatisha maneno na kuacha Kuomba, ukaenda kulala.. endelea kutafakari huku ukizungumza na Mungu wako Habari mbalimbali za kwenye maandiko, na ghafla tu baada ya muda kidogo utaona unaingia kwenye mkondo fulani wa kimaombi, linatoka neno hili kwenye ufahamu linakuja neno hili la kuombea…ulikuwa umepanga uombe Saa 1, unajikuta unaomba matatu.hapo ni Roho Mtakatifu amekupa Kinywa cha kuomba..na ndani ya maombi hayo ni utabiri tosha, kwasababu sio ufahamu wako, bali ni wa Mungu ndani yako.

Vilevile jifunze kutoa sauti katika uombaji wako wa mara kwa mara..ndio tunafahamu Maombi sio sauti, hata kimoyo- moyo Mungu anasikia, lakini usimzimishe Roho..

Watu wengi wanatamani kunena kwa lugha lakini, wanazuia vinywa vyao kutoa sauti.. wanategemea vipi wanene kwa lugha mpya..unapojiachia Kwenye maombi huku unatoa sauti ni rahisi sana kujazwa Roho Na kuomba kwa lugha.

Eneo lingine labda mtu ni mgonjwa..anahitaji maombi…Fungua kinywa chako kwa ujasiri mtamkie uponyaji…unaweza kudhani ni maneno yako, hujui kumbe Ni Roho Mtakatifu Ameyaingilia na kulifanya tayari kuwa Neno la kinabii la uponyaji, na hatimaye anapokea uponyaji wake saa hiyo hiyo.

Uwapo na Watoto wako, Acha kuzungumza nao, habari za kidunia dunia tu..wawekee mikono wabariki kwa Imani kama vile Isaka alivyowabariki Yakobo na Esau na maneno yale yakawa kweli. Vivyo hivyo na wewe tabiri juu ya watoto wako unataka wawe nani wawapo watu wazima.

Uwapo kazini na marafiki zako, penda kuzungumza maneno ya ki-Mungu wakati mwingi kwasababu huko huko unabii unaweza kupita bila wewe kujijua… mwangalie kayafa

Yohana 11:49-52

[49]Mtu mmoja miongoni mwao, Kayafa, aliyekuwa Kuhani Mkuu mwaka ule, akawaambia, Ninyi hamjui neno lo lote;

[50]wala hamfikiri ya kwamba yafaa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu, wala lisiangamie taifa zima.

[51]Na neno hilo yeye hakulisema kwa nafsi yake; bali kwa kuwa alikuwa Kuhani Mkuu mwaka ule, alitabiri ya kwamba Yesu atakufa kwa ajili ya taifa hilo.

[52]Wala si kwa ajili ya taifa hilo tu; lakini pamoja na hayo awakusanye watoto wa Mungu waliotawanyika, ili wawe wamoja.

Hivyo kinywa chako ni kinywa cha Roho Mtakatifu usikifunge Bali kijaze Maneno ya Mungu.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

VIASHIRIA VINGINE VYA ROHO MTAKATIFU KUWEPO NDANI YAKO.

TULITAFUTE KWA BIDII TUNDA LA ROHO.

KWA KUWA ROHO BORA ILIKUWA NDANI YAKE.

Print this post

Je mapepo yanakufa? Na kama hayafi, tunashindanaje vita vya kiroho?

SWALI: Je mapepo yanakufa? Na kama hayafi, ni vita ya namna gani tunashindana nayo katika ulimwengu wa Roho?


JIBU: Katika biblia tunaposoma Neno “pepo”, ni vema tufahamu ufunuo wake upo katika namna mbili;

  1. Pepo: Kama malaika muasi
  2. Pepo: Kama pando la malaika muasi

Yote mawili unapaswa kufahamu, Ili ujue ni nani unashughulika naye katika vita hivyo vya kiroho.

Kwamfano, ukisoma ile waefeso 6:12 inayosema kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama, bali juu ya falme na mamlaka na wakuu wa giza hili pamoja na majeshi ya mapepo wabaya.. Sasa hao wanaotajwa hasaa ni malaika waasi.

Lakini hawa malaika waasi, huwa na mapando yao, ambayo huyapanda ndani ya watu, mfano wa hayo ni magonjwa, ukichaa, ububu, udhaifu (Marko 9:25)uuaji, uchungu, majivuno, kiburi, masengenyo n.k.. na haya mapando wakati mwingine huitwa mapepo, kwasababu asili yao ni kutoka kwa hao malaika waasi.

Luka 13:11 Na tazama, palikuwa na mwanamke aliyekuwa na pepo wa udhaifu muda wa miaka kumi na minane, naye amepindana, hawezi kujinyosha kabisa.

Pepo linalozungumziwa hapo, hasaa sio yale mashetani, bali ni pando la udhaifu waliloliweka ndani ya huo mwanamke.

Hizi zote ni kazi za shetani na malaika zake duniani. Sasa mapando haya ndio tunaweza kuyaua (kwa kuyang’oa), lakini sio wale malaika waasi. Ndio maana Bwana Yesu alisema..

Mathayo 15:13 Akajibu, akasema, Kila pando asilolipanda Baba yangu wa mbinguni litang’olewa

Wale malaika waasi (yaani wakuu wa giza, wafalme, majeshi ya mapepo yote)hatuwezi kuwaua, kwa maombi au kwa namna yoyote, isipokuwa tayari wameshawekewa hukumu yao, siku ile ya mwisho ambapo watatupwa wote kwenye lile ziwa la moto.

Na mapando haya, Bwana Yesu alitoa maelezo yake vema, wakati ambapo adui hupandwa ndani ya mtu..

alisema.

Mathayo 13:24 Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake;
25 lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake.
26 Baadaye majani ya ngano yalipomea na kuzaa, yakaonekana na magugu.
27 Watumwa wa mwenye nyumba wakaenda wakamwambia, Bwana, hukupanda mbegu njema katika konde lako? Limepata wapi basi magugu?
28 Akawaambia, Adui ndiye aliyetenda hivi. Watumwa wakamwambia, Basi, wataka twende tukayakusanye?
29 Akasema, La; msije mkakusanya magugu, na kuzing’oa ngano pamoja nayo.
30 Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome; bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu.

Kumbe wakati ambapo watu wamelala, ndipo hupanda mbegu zake. Yaani wakati ambapo watu wamekuwa walegevu kiroho ndipo shetani hupata nguvu ya kuja kupachika, mbegu zake za uharibifu, zitakazokuja kusumbua baadaye. Ndio maana ni lazima ujue kanuni mbalimbali za kumpinga shetani.

Na haya mapando, yanaweza kuwekwa kwa mtu yeyote, hata mtu aliyeokoka, anaweza kuwa nayo. Ndio maana utaona wapo watu wengine wameokoka, lakini wanasumbuliwa na mapepo, kiuhalisia, hawana malaika wale waasi ndani yao, wanayo mapando yao.

Ni sawa, na mtu ambaye anamilika chombo kama komputa, akiwa anaitumia kwa matumizi yake tu ya sikuzote, tu ambayo ni lazima, si rahisi computa hiyo kuvamiwa na virusi, lakini akianza kutembea mitandaoni, kisha kubofya, au kupakua kila kitu anachokiona ni wazi kuwa chombo hicho kipo hatarini kuvamiwa na virusi, na matokeo yake ni kuwa mfumo wote wa kumpyuta unaliwa, au kuharibifu chombo kabisa, ndio maana wanaweka ulinzi (anti-virus) sikuzote,

Vivyo hivyo na maisha ya mwanadamu yakiwa ovyo ovyo, hawezi kukwepa mapando ya mashetani ambayo yamezaa kila mahali. Mtu yeyote ambaye hajaokoka tayari kuna pepo fulani ndani yake.

Kwamfano, mwingine, labda mkristo  ameokoka, halafu akiwa kanisani, anaanza kuruhusu masengenyo kinyume na mchungaji wake, au mama-mchungaji, sasa mtu kama huyo akiwa anaendelea na tabia hiyo..matokeo yake ni kwamba pepo la uchungu litamvaa, ataanza kuwachukia viongozi wake hata bila sababu, na kuzusha vita, na uharibifu hata  wengine. Yeye atadhani ni tabia yake kumbe sio, bali pepo limeshamvaa la uchungu.

Nikupe huu ushuhuda, Kulikuwa na mama mmoja kanisa, kipindi chote ulikuwa ukikutana naye, anamzungumzia vibaya mama mchungaji wa kanisa alilokuwa mwanzo, hapo mwanzo alikuwa vizuri tu kiroho, lakini kwa jinsi siku zilivyozidi kwenda, akiendeleza chuki zake, , hali yake ilikuja kubadilika ghafla, akaomba tumwombee, tulipomwombea alilipuka mapepo, lile pepo likawa linasema “mama mchungaji” yaani asili yangu ni chuki kwa mama mchungaji, tulipolikemea likamwacha akarudia hali yake ya kawaida, akawa mtu mzuri tu.

Samsoni, alipokwenda kuwashindana na wafilisti, hakushughulika  kwanza na wafilisti, bali mashamba yao ya ngano. (mapando yao). Kwa kuyachoma moto. Vivyo hivyo na sisi ili tuyamalize nguvu haya mashetani, tuangushe ngome zao. Ni lazima fikra zetu hasaa zielekee mapando yao.

NAMNA YA KUSHINDANA VITA VYA KIROHO:

Injili:

Kwamfano kuwaangusha wakuu wa giza sio kuwatumia makombora ya moto hapo angani. Hapana, bali ni kwenda kuhubiri injili ili watu wamsikie Kristo waokoke,

Ndio maana Yesu alipowatuma wanafunzi wake wawili wawili kuhubiri waliporudi Yesu aliwaambia ‘nalimwona shetani akianguka kutoka mbinguni kama umeme’.

Kumbe anguko lake lilikuwa katika kuhubiri na si kumtumia makombora.

Maombi:

Hii ni silaha kubwa, ya kumpinga shetani. Maombi huruhusu, utendaji kazi wa Mungu ndani ya maisha ya mwamini, usipokuwa mwombaji tarajia shetani kuyapangalia maisha yao. Yesu alituagiza tukeshe kuomba tusije ingia majaribuni.

Upendo:

Upendo hupinga, wivu, chuki, uchungu, mashindano, uzinzi, n.k. ambayo haya yote huzaliwa mahali ambapo hapana upendo. Ni lazima kila siku wewe kama mwamini kila siku ujifunze kutendea kazi upendo….ili uondoe mazingira ya mashetani kuangua mayao yao hapo.

Neno:

Ukiwa na Neno la Mungu la kutosha ndani yako, adui hawezi kukushinda. Utakumbuka kule jangwani, shetani alipojaribu kumpandia Kristo maneno ya uongo kwa kupitia biblia, yeye mwenyewe alilitumia Neno la Kweli, kumpinga. Watu wengi wanavamiwa na maroho ya upotevu, kwasababu hawana Neno la Mungu mioyoni mwao. Jifunze kusoma biblia. Ni silaha inayoitwa Upanga.

Imani:

Imani huzaa ujasiri, na ujasiri hutoa mamlaka ndani yako. Biblia huiita imani “Ngao” Shetani anapenda kutumia silaha ya woga, ili kuzimisha utendaji kazi wa Mungu mioyoni mwetu. Hatuna budi kusimama kwa utimilifu wa imani kumtumikia Mungu.

Kukemea:

Fahamu adui ni mpingamizi sikuzote, hapembelezwi, bali analazimishwa kutoka, Yesu alimkemea shetani alipotaka kumjaribu kwa kinywa cha Petro, aliyakemewa mapepo yote sugu, yaliyokuwa ndani ya watu yawatoke. Hivyo na wewe pia ukutanapo na kazi hizi za mwovu, jifunze kutumia kinywa chako, kwa mamlaka uliyopewa na Kristo kukemea haraka sana, kila pepo, au kimelea chochote cha uovu kinachozaliwa na adui.

Hivyo kwa hitimisho ni kuwa, mashetani hawafi, lakini kazi zao zinakufa.. Hatuwaui hao, bali tunaziua kazi zao. Usipoteze muda mwingi kumrushia shetani mabovu hawezi kufa, bali tuma nguvu zako nyingi kurushia mabovu mapanda yake, kwa kanuni hizo tulizojifunza. Utawashinda kabisa kabisa.

Bwana akubariki

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Mbona ni maskini tu huwa ndio wanaolipuka mapepo, na sio matajiri?

MWANAMKE, USIFUNGUE MLANGO WA MAPEPO KUKUINGIA!.

SI MAPEPO YOTE NI YA KULIPUKA.

Kwanini Bwana Yesu, aliruhusu yale mapepo yawaingie nguruwe?

Print this post

LINDA CHEMCHEMI YA MOYO WAKO.

Mithali 4:23 “Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako CHEMCHEMI ZA UZIMA”.

Chemchemi kazi yake ni kutoa “maji ya kunywa” lakini pia maji ya “kustawisha mimea”.

Kama chemchemi ikitoa maji ya chumvi au ya magadi, ni wazi kuwa maji yake hayatafaa kwa matumizi yoyote yale, hivyo mahali hapo hapana uhai, watu hawawezi kuishi wala wanyama wala mimea..

Lakini kama chemchemi ikitoa maji safi yasiyo na magadi wala chumvi, na tena masafi, basi mahali pale kila kitu kitasitawi ikiwemo watu, wanyama na mimea, na hata shughuli zote nyingine za kiuchumi.

Mfano wa maji machungu na yasiyofaa ni yale wana wa Israeli waliyokutana nayo kule ‘Mara’

Kutoka 15:22 “Musa akawaongoza Israeli waende mbele kutoka Bahari ya Shamu, nao wakatokea kwa jangwa la Shuri; wakaenda safari ya siku tatu jangwani wasione maji.

23 Walipofika mahali palipoitwa Mara hawakupata kuyanywa yale maji ya Mara, kwa kuwa yalikuwa machungu; kwa ajili ya hayo jina lake likaitwa Mara.

24 Ndipo watu wakamnung’unikia Musa, wakisema, Tunywe nini?

25 Naye akamlilia Bwana; Bwana akamwonyesha mti, naye akautia katika hayo maji, maji yakawa matamu. Basi akawawekea amri na hukumu huko, akawaonja huko”.

Sasa Biblia inafananisha “Mioyo yetu na chemchemi zinazotoa maji”… Maana yake yanayotoka mioyoni mwetu yanaweza kukuza, kustawisha au kudhoofisha afya zetu, wanyama wetu, mimea yetu…kwaufupi kila kitu kinachotuzunguka ikiwemo kazi zetu, elimu zetu, nafasi zetu, kibali chetu na mambo mengine yote yanategemea sana yanayotoka mioyoni mwetu.

Sasa najua utauliza haya maji machungu au matamu ni nini?.. Turejee maneno ya Bwana Yesu.

Mathayo 12:34 “Enyi wazao wa nyoka, mwawezaje kunena mema, mkiwa wabaya? Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake.

35 Mtu mwema katika akiba njema hutoa mema; na mtu mbaya katika akiba mbaya hutoa mabaya”.

Tusome tena Mathayo 15:18-20…

Mathayo 15:18 “Bali vitokavyo kinywani vyatoka moyoni; navyo ndivyo vimtiavyo mtu unajisi.

19 kwa maana MOYONI hutoka MAWAZO MABAYA, UUAJI, UZINZI, UASHERATI; WIVI, USHUHUDA WA UONGO, NA MATUKANO

20 hayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi…….”.

Umeona hapo?.. kumbe moyoni ndiko kunakotoka matukano, uzinzi, wizi, uongo n.k mambo ambayo ndiyo yanayomtia mtu unajisi, na bila shaka hayo ndiyo Maji machungu yatokayo moyoni kupita kinywani, ambayo hayafai kwa kustawisha chochote…

Wengi wamepoteza na kuharibu maisha yao kwasababu ya uzinzi, na wengine kwasababu ya wizi, na wengine kwasababu ya mauaji, wapo waliopoteza kibali kwa Mungu na kwa watu kwasababu ya wizi, au uzinzi, au mauaji..wapo walipoteza kazi zao za mikono na huduma zao zilizokuwa zenye utukufu kwasababu ya uzinzi, au wizi au matukano..

Wapo walioharibu ndoa zao zilizokuwa za heshima na mfano kwasababu ya uzinzi, uongo, na mauaji (utoaji mimba) Kwanini?.. kwasababu chemchemi zao zinatoa maji machungu yanayoua ndoa, kazi, huduma, kibali, heshima na nguvu.

Yakobo 3:8 “Bali ulimi hakuna awezaye kuufuga; ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti.

9 Kwa huo twamhimidi Mungu Baba yetu, na kwa huo twawalaani wanadamu waliofanywa kwa mfano wa Mungu.

10 Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, haifai mambo hayo kuwa hivyo.

11 Je! Chemchemi katika jicho moja hutoa maji matamu na maji machungu?

12 Ndugu zangu, Je! Mtini waweza kuzaa zeituni, au mzabibu kuzaa tini? Kadhalika chemchemi haiwezi kutoa maji ya chumvi na maji matamu”.

Lakini kama moyoni kukitoka mambo masafi, ambayo ni upendo, ukweli, utu wema, uvumilivu (kwa ujumla utakatifu)… hakika hiyo ni chemchemi bora inayostawisha kila kitu, maji yake yatastawisha wokovu, kazi ya Mungu, kazi ya mikono, elimu, heshima, ndoa, nafasi na mambo mengine yote mazuri.

Je wewe chemchemi ya moyo wako inatoa maji ya aina gani?.. machungu au matamu?.. Kama inatoa machungu ipo dawa leo?.. dawa hiyo ni Roho Mtakatifu… Mwamini YESU leo kisha ukabatizwe na Roho Mtakatifu ataingia ndani yako na kukutakasa moyo wako Bureeeee kabisa!

Baada ya hapo ndoa  yako iliyokufa itafufuka upya, huduma yako, kazi yako, elimu yako au kitu kingine cha thamani ulichopewa na Bwana, kitafufuka kwani tayari maji yatokayo ndani yako ni masafi..

Lakini labda tayari chemchemi yako ni safi, nayo inatoa maji masafi.. bado kuna jambo lingine la ziada la kufanya nalo ni KUILINDA chemchemi yako..

Mithali 4:23 “Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako CHEMCHEMI ZA UZIMA”.

Utaulinda moyo wako kwa MAOMBI, kusoma NENO, kujihadhari na ulimwengu na kushiriki ibada pamoja na watu wenye imani moja na wewe kila mara.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Nini maana ya Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu?

Fahamu Maana ya Mithali 15:24 Kwa mtu mwenye akili njia ya uhai huenda juu;

MOYO ULIOELEKEA KWA MUNGU.

JE UPANGA UMEINGIA MOYONI MWAKO?.

JIHADHARI NA MANENO YASIYO NA  MAANA 

Print this post

Je! Ni sahihi kwa mkristo kufundishwa na AI mfano wa Chatgpt, deepseek n.k.

SWALI: Je! Ni sahihi kwa mkristo kujifunza, au kufundishwa na AI (Artificial Inteligence), mfano wa Chatgpt, deepseek n.k.


JIBU: Ili kujibu swali hili ni vema, kutambua mashine hizi za akili bandia (AI), zinafanya kazi gani.

Kwa ufupi ni kuwa AI, inafanya kazi ya kuchakata taarifa nyingi, kutoka katika vyanzo vingi vilivyopo mitandaoni, mfano vitabu, makala, sauti, machapisho n.k, na hivyo inazichanganya taarifa hizo zote kwa kuangalia muktadha unaofanana na kuzifupisha, na kukujibu.

Hivyo kimsingi, ni chombo ambacho kinatoa msaada mkubwa katika ulimwengu wa sasa, na ndio ukweli usiopingika..Kwasababu kinarahisisha utafutaji wa taarifa. Lakini pamoja na hayo haimaanishi kuwa kinatoa kwa ufasaha wote.

Sasa tukija kwenye eneo la kiroho. Je ni vema mkristo kwenda kuuliza AI, au kuandaa maombi au masomo kupitia hiyo, n.k.

Ukweli ni kwamba Imani, sio taarifa, ni zaidi ya taarifa.. Hizi AI, zinatoa tu taarifa lakini hazitoi mafunuo. Hazina pumzi ya Roho Mtakatifu ndani yake.

Ikiwa unataka kuongeza maarifa kwa sehemu fulani zinaweza kukusaidia, lakini sio kukujenga nafsi, kwani inahitaji pumzi ya Mungu na miongozo ya Mungu wewe kujengwa nafsi, na sio taarifa.

Kwamfano ikiwa wewe ni mchungaji halafu, kila inapokaribia jumapili unachowaza ni kwenda chatgpt, kuiambia ikuandalie somo la kufundisha jumapili,  ndugu hapo hesabu kuwa umepotea kama sio kukengeuka… Tumia hiyo kwenye biashara zako, masomo yako,  projekti zao lakini sio kwenye mambo ya kiroho. Hilo liepuke kabisa.

Kufundisha Neno inahitaji ‘Neno’ mwenyewe (Yesu) akae ndani yako, kwasababu ni UHAI sio taarifa (Waebrania 4:12) ndio hapo itakupasa kupiga magoti kwanza uombe, kwa muda mrefu, utafakari moyoni mwako, ukae kwenye utulivu wa kutosha, ndipo Mungu alipande somo lake moyoni mwako. Ambalo yeye mwenyewe anajua litakuwenda kuwagusa vipi watu wake, wenye changamoto mbalimbali, kwamfano, pengine mtu mmoja alikuwa anakaribia kwenda kujinyonga kwasababu ya ugumu wa maisha na mateso fulani, na Mungu kamwona anataka amsaidie, kwa kuliweka somo linalohusiana na mapito ya Ayubu ili ainuliwe imani. Kinyume chake kwasababu ya uvivu wako wewe unakwenda kuiambia chatgpt (akili bandia), ikuandalie somo. Halafu jumapili utakwenda na taarifa zao sio mafunuo. Badala uokoe roho inayokwenda kujinyonga, unaiambia, “leo tunajifunza kanuni kumi za kudumisha ndoa na mahusiano kibiblia”. Hapo unafanya nini sasa?

Au Neno fulani Bwana anataka kukupa la wakati wako, sasa ikiwa unakimbilia AI ikusaidie, hutaki kuchukua muda wako binafsi kutafakari na kuomba ‘jiandae kukutana na ukame wa kiroho.

Visaidizi hivi, hatupaswi kuvifanya ndio sehemu ya imani yetu, kwamba kila kitu tutegemee kule, hivi ni tone dogo sana kati ya bahari kubwa. Roho Mtakatifu alishatuandalia njia zake, kuu za kujengwa na yeye.

Wekeza zaidi, kuomba msaada kwa wakufunzi wako, viongozi wako, ndugu zako katika Kristo, wekeza katika maombi, mifungo, tafakari, na kujisomea mwenyewe Neno.  kwa njia hizi hakika Bwana atasema nawe na kujengwa zaidi kuliko visaidizi. Lakini pia ikiwa pana umuhimu wa kujiongezea taarifa kwa vile unavyovijua, visaidizi hivi vitakufaa (Katika uangalizi maalumu), vinginevyo utajidumaza kiroho.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >>  https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Karismatiki ni nini?

Uinjilisti kama agizo kuu la Bwana.

Vita vya kiroho, na mwamini Mpya.

Print this post