Nakusalimu katika jina la mwokozi wetu Yesu Kristo, karibu tuyatafakari maneno ya uzima. Leo napenda tujifunze tabia nyingine ya Bwana Yesu. Kwasababu yeye mwenyewe alituambia ‘tujifunze kwake’. Hivyo naamini tuna mengi ya kuyajua kuhusu yeye.
Habari hiyo tunaisoma katika vifungu hivi;
Luka 9:51 Ikawa, siku za kupaa kwake zilipokuwa karibu kutimia, yeye aliukaza uso wake kwenda Yerusalemu;
52 akatuma wajumbe kutangulia mbele ya uso wake; wakaenda wakaingia katika kijiji cha Wasamaria, ili kumtengenezea mahali.
53 Lakini wenyeji hawakumkaribisha kwa vile alivyouelekeza uso wake kwenda Yerusalemu.
54 Wanafunzi wake Yakobo na Yohana walipoona hayo, walisema, Bwana, wataka tuagize moto ushuke kutoka mbinguni, uwaangamize; [kama Eliya naye alivyofanya]?
55 Akawageukia, akawakanya. [Akasema, Hamjui ni roho ya namna gani mliyo nayo.]
56 Kwa maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa. Wakaondoka wakaenda mpaka kijiji kingine.
Kama wewe ni msomaji mzuri wa biblia utakumbuka kuwa kuna wakati ulifika, ilikuwa wazi kwa watu wote, kuwa Yesu anatafutwa ili auawe, (hususani kule Yerusalemu). Na hilo lilimfanya mara kadha wa kadha asitembee kwa uwazi wote mbele ya makutano (Yohana 7:10), kwasababu, saa yake ya kuuawa ilikuwa bado haijafika.
Yohana 11:54 Kwa hiyo Yesu hakutembea tena kwa wazi katikati ya Wayahudi; bali alitoka huko, akaenda mahali karibu na jangwa, mpaka mji uitwao Efraimu; akakaa huko pamoja na wanafunzi wake.
Lakini mambo yalikuja kubadilika baadaye, hilo halikuendelea kwa wakati wote. Alipoona sasa kazi aliyopewa na Mungu ameimaliza, alionyesha tabia nyingine ambayo haikuwa ya kawaida. Biblia inatuambia, “aliukaza uso wake kuelekea Yerusalemu”, kule kule alipokuwa anatafutwa auawe.
Jambo ambalo lilileta mshtuko hata kwa mitume wake;
Yohana 11:7 Kisha, baada ya hayo, akawaambia wanafunzi wake, Twendeni Uyahudi tena.
8 Wale wanafunzi wakamwambia, Rabi, juzijuzi tu Wayahudi walikuwa wakitafuta kukupiga kwa mawe, nawe unakwenda huko tena?
9 Yesu akajibu, Je! Saa za mchana si kumi na mbili? Mtu akienda mchana hajikwai; kwa sababu aiona nuru ya ulimwengu huu.
Walishangaa, ujasiri huo ni wa namna gani? Ni sawa na wanajeshi waliokwenda vitani, halafu maadui wakawaua wanajeshi wote, akabakia mmoja tu, halafu huyo mmoja anasema nitakwenda kupambana na jeshi lote hilo peke yangu sitajificha. Ukweli ni kwamba inahitaji nguvu nyingine ya ziada ndani ya huyo mtu.
Ndivyo ilivyokuwa kwa Bwana Yesu, aliukaza uso wake, kwenda kututetea sisi. Embu Fikiria kama angeulegeza, na kuendelea kuzunguka mahali pengine na sio kule uyahudi(Yerusalemu), wokovu wetu tungeupatia wapi?
Ilibidi, alazamishe mambo, japo mwili wake ulikuwa hautaki, ndio maana akiwa pale bustanini, anaomwomba Baba, akisema ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke, ni kuonyesha kuwa hata mwili wake ulikuwa unagoma kuwepo kule Yerusalemu, na si mwili tu, bado mazingira pia hayakutaka, alipokuwa anakatiza kwa Wasamaria wenyeje wa pale hawakutaka kumruhusu akae kwao, kwasababu waliona kama anawaletea matatizo, ikumbukwe kuwa watu hao hao ndio waliokuwa wanataka kumfanya mfalme hapo mwanzo. Kuonyesha kuwa mazingira yalimgomea. Si mazingira peke yake, hata mitume wake nao, walifanya kama kumsindikiza tu, lakini mioyo yao walishajiandaa kuchukua hatua yoyote lolote litakapotokea, ndio maana pale bustanini, wale watu walipokuja kila mmoja akakimbia na njia yake.
Kwa ufupi kila kitu kilikataa, isipokuwa roho yake tu. Ndio sababu ya kwanini maandiko yanatuambia ‘aliukaza uso wake’ kwasababu haikuwa rahisi, si jambo tena la kuomba, au kubembeleza, au kushawishi, au kusubiri msimu mzuri. Bali ni kujitoa tu wote wote, katika hayo. Watu wengi tunadhani Yesu aliuchukua msalaba wake siku ile alipobebeshwa ule mti, hapana, aliuchukua msalaba wake Kwa kitendo hichi cha kuamua kuukaza uso wake, kuelekea kifoni. Hata aliposema tujitwike misalaba yetu, alilenga, eneo hilo.
Ni nini na sisi tunapaswa tukipokee kwa Bwana Yesu?
Kwa kuwa Roho wake naye yupo ndani yetu, hatuna budi kufahamu kuwa yapo majira katika safari yetu ya wokovu, hatutahitaji mazingira yawe mazuri, ndio tulitimize kusudi la Mungu, au ndugu kutukubalia, au marafiki kuafikiana na sisi, au miili kutuambia sasa ndio wakati, hapana..bali ni kujitwika misalaba yetu, “kwa kukaza nyuso zetu” na kumfuata Yesu.
Tukingoja vikwazo viondoke, au viondoshwe, tutajidanganya, na tutangoja sana, kwani vita vitaendelea kuwepo mpaka mwisho, mapambano hayaishi, tutashinda tu kwa kukaza tu nyuso zetu. Na Bwana atakuwa pamoja na sisi, ijapokuwa itaonekana ni kujipoteza lakini mwisho wake utakuwa ni uzima kama ulivyokuwa kwa Bwana Yesu.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Ni kweli Paulo alipuuzia maonyo aliyopewa ya kwenda Yerusalemu?
Rudi Nyumbani
Msingi ni chimbuko, au mwanzo au kiini cha kitu fulani.
Ni wazi kuwa kila jambo lina msingi wake. taifa lina msingi wake, taasisi ina msingi wake, kabila lina msingi wake vilevile pia imani ina msingi wake.
Hivyo tukirudi katika ukristo. Msingi wa imani yake ni upi?
Msingi wa ukristo ni YESU KRISTO mwenyewe, na kazi yake aliyoikamilisha ya kufa na kufufuka kwake. Na sio kanisa, au dhehebu, au mapokeo fulani, au kikundi fulani cha wanaharakati.
Pasipo Yesu hakuna ukristo.
Yeye anafananishwa na lile jiwe kuu la pembeni, ambalo hakuna mjenzi aliyeweza kusimamisha jengo bila kuliweka hilo.
1 Petro 2:6
[6]Kwa kuwa imeandikwa katika maandiko Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima, Na kila amwaminiye hatatahayarika.
Habari kamili za Yesu, na kazi yake aliyokuja kuifanya duniani unaipata katika kitabu kimoja tu kiitwacho BIBLIA. Hivyo huwezi kutenganisha biblia na Yesu Kristo.
Ili mtu ashawishwe kuipokea imani, ni sharti, aisikie kwanza injili yake ambayo hiyo utaipata katika Neno la Mungu yaani biblia..(Warumi 10:17)
Mpaka mtu aitwe mkristo ni lazima amtambue kwanza Kristo ni nani, na nini amekileta duniani, vinginevyo hawezi kuwa mkristo, hata kama atajiunga na kanisa, au dhehebu na kuyashika mapokeo yote aliyoyakuta huko, au kuisoma biblia yote, huyo bado hajawa mkristo.
Ni muhimu sana kumtambua Yesu ni nani kwetu. Kumtambua Yesu kama mwana wa Mungu bado inaweza isikupe wokovu, hata kumtambua Yesu kama Mungu bado inaweza isikupe wokovu (ijapokuwa vyote hivyo ni vyeo vyake). Lakini vyeo hivyo sio kiini cha ukristo.
Yesu ni nani na ni nini alikileta duniani?
Yesu ni MKOMBOZI, kama tafsiri ya jina lake linavyojieleza( Mathayo 1:21)
mkombozi wa nini?
Alikuja kutukomboa roho zetu, nafsi zetu na miili yetu, Na kama ilivyo kanuni ya kiroho ili jambo hilo liweze kukamilika ilipasa itolewe kafara isiyo na kasoro yoyote(yaani dhambi). Na aliyeweza kukidhi vigezo hivyo ni Yesu pekee.
Ndio maana ilimgharimu afe, kama fidia ili sisi tupokee ondoleo la dhambi na msamaha wa dhambi kwa kifo chake. Hivyo yoyote anayeamini(yaani anayeupokea wokovu huo aliouleta).
kwa toba ya kweli na ubatizo, Basi anakuwa ameokoka, hivyo ile ghadhabu ya Mungu kwa wenye dhambi wote haiwi tena juu yake, tangu huo wakati anaitwa mbarikiwa, au mkristo, kwasababu dhambi zake zinakuwa zimefutwa kabisa.
Na zaidi ya hayo mtu huyu moja kwa moja anapewa zawadi ya Roho Mtakatifu, ambaye tangu huo wakati na kuendelea anakuwa ndani yake kama msaidizi, kumsaidia madhaifu yake, katika kuomba, kuijua kweli, kumkumbusha aliyoyasema Yesu, kumpasha habari ya mambo yajayo, na kumtia nguvu ya kumtumikia Mungu, pamoja na kumpa nguvu ya kushinda dhambi.
Huyu ndiye mkristo.
Swali ni je! umemwamini ipasavyo? au umempokea kwa namna ile ya kidini?
Usifikiri kuhama dini, wewe ni Kristo, au kuzaliwa kwenye familia ya kikristo wewe ndio mkristo, au kusomea theolojia, hapana hizo ni kampeni tu, ukristo halisi huja kwa kumwelewa Kristo ni nani na ni nini amekifanya kwako.
Ikiwa bado hujaokoka na unataka kumpokea leo ili upate ondoleo la dhambi zako. Basi uamuzi huo ni bora sana kwako. Wasiliana nasi namba uzionazo chini kwa mwongozo wa sala ya toba.
Ubarikiwe.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
+255693036618/ +255789001312
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >>https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Je huduma za mitume na manabii, zinaendelea kufanya kazi hadi sasa?
Rudi Nyumbani
Biblia kitabu kikamilifu, na kitakatifu kimeandikwa na waandishi Zaidi ya 40 kwa Uvuvio wa Roho Mtakatifu. Ndani ya biblia kuna taarifa zinazohusu maisha ya watu zilizobeba sauti ya Mungu nyuma yake, pia kuna taarifa za Mataifa mbalimbali pia zenye kubeba sauti ya Mungu nyuma yake, lakini Zaidi sana kuna Nabii za wakati ujao.
Ifuatayo ni orodha ya waandishi 40 wa Biblia kuanzia Agano la kale hadi Agano jipya.
Agano la kale.
Agano Jipya.
Kwanini waandishi wapo Zaidi ya 40 na si 40 kamili?.. Ni kwasababu biblia pia imewataja wana wa Kora, ambao hatujui walikuwa ni wangapi, zaidi sana yupo mwandishi wa kitabu cha Waebrania, ambaye hajatajwa ni nani, huenda akawa ni Mtume Paulo, lakini kama si yeye bali ni mwingine, basi ataongezeka katika idadi ya walioiandika biblia.
Kumbuka tena, biblia ni kitabu cha Mungu kilichoandikwa na WATU, kwa uvuvio wa ROHO MTAKATIFU, Hivyo maneno yaliyoandikwa ndani ya Biblia, yana uzima.
2Timotheo 3:16 “Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;
17 ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema”.
Shalom.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
KALAMU YENYE UONGO YA WAANDISHI IMEIFANYA KUWA UONGO.
Mwandishi wa kitabu cha Matendo ya mitume.
Mwandishi wa kitabu cha Mithali ni nani?
Hosea 2:13 “Nami nitamwadhibu kwa sababu ya siku za Mabaali, aliowafukizia uvumba; hapo alipojipamba kwa PETE MASIKIONI MWAKE, na kwa vito asema Bwana”.
Kabla ya kuvaa kitu, au kuiga mtindo fulani, hebu tenga muda kwanza kufuatilia asili ya kitu hiko kibiblia, kwasababu kuna vitu vingine asili yake ni mbaya, na isiyo na baraka kwa Mungu.
Hebu jiulize swali hili.. Mungu akuumbe na masikio yaliyo kamili, halafu akwambie au akuruhusu ukayatoboe masikio hayo, eti ili tu upendeze?..hivi jambo hilo ni kweli Mungu kaliagiza au kaliruhusu??.. au ni ujanja tu wa akili za watu! (walionyanyuliwa na ibilisi, Waefeso 4:14).
Sasa sikuhukumu wewe uliyetobolewa masikio, huenda si wewe kwa hiari ulifanya hivyo, bali walikutoboa tu ukiwa mchanga..na pia waliokutoboa huenda nao pia walipokea tu kwa waliotangulia, hivyo huenda kosa si lako wala la wazazi, bali la yule wa kwanza kuanzisha makosa hayo..
Lakini sasa baada ya kuelewa, si sawa kuendeleza hayo makosa kwa vizazi vyako, vile vile si sawa kuweka chuma au dhahabu katika matundu ya masikio yaliyotobolewa, kwani kwa kufanya hivyo bado utakuwa unaendeleza desturi hiyo.
Hebu tusome tena…
Hosea 2:13 “Nami nitamwadhibu kwa sababu ya siku za Mabaali, aliowafukizia uvumba; hapo alipojipamba kwa pete masikioni mwake, na kwa vito asema Bwana”.
Asili ya kujipamba kwa pete za masikioni (yaani kuweka hereni) ilikuwa NI KUJIWEKA TAYARI KWA KUVUKIZA UVUMBA KWA MABAALI… na baali si mwingine zaidi ya shetani mwenyewe/kusifa katika kinyago chake kingine.
Kwahiyo zamani mtu akijipamba kwa kutoboa masikio na kuweka hereni alikuwa aidha ametoka kuvukiza uvumba kwa baali au ndio anaenda kuvukiza uvumba kwa baali, na hereni zamani hazikuwa zinavaliwa tu na wanawake, bali hata na wanaume, na lengo lilikuwa ni hilo hilo kumvukizia uvumba baali.
Labda utauliza ni wapi tena pengine panapoonyesha hereni, zinahusishwa na ibada za miungu..
Mwanzo 35:2 “Yakobo akawaambia watu wa nyumbani mwake, na wote waliokuwa pamoja naye, ONDOENI MIUNGU MIGENI ILIYOKO KWENU, mjisafishe mkabadili nguo zenu. .
4 NAO WAKAMPA YAKOBO MIUNGU MIGENI YOTE ILIYOKUWA MIKONONI MWAO, NA PETE ZILIZOKUWA MASIKIONI MWAO, naye Yakobo akazificha chini ya mwaloni ulioko Shekemu”.
Sasa shetani ni yule yule, na ibada zake ni zile zile, hazijabadilika……kama bado yupo kwenye makafara ya mang’ombe mpaka leo, na mambuzi, na bado waganga wake ni wale wale, na mavazi yao ni yale yale, na uchawi wake ni ule ule, unadhani uchawi wake katika HERENI (pete za masikioni) utakuwa umebadilika??.. Jibu ni la! Utakuwa ni ule ule tu.
Tafakari, tafakari mama, tafakari dada, tafakari kaka unayevaa hereni, kuambiwa usivae hereni sio kwamba unawekwa chini ya sheria, hapana!.. bali kinyume chake ndio UNAKUWA HURU… Lakini kuvaa hereni ndio sheria, kwani itakulazimu kila siku kuivaa kabla ya kutoka nje, na kubadilisha aina ya hereni leo hii kesho ile, sasa huoni kama hiyo ndio SHERIA???, na kutokuvaa hereni ndio uhuru??.
Ni kweli ukiacha kuzivaa utaonekana si mrembo kwa baadhi ya watu, lakini utakuwa umejiepusha na ibada za sanamu, ambazo zitakuzalia madhara mengine makubwa kiroho.
Miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu, sawasawa na 1Wakorintho 3:16, na 1Wakorintho 6:19.
Kwa jinsi tunavyozidi kuiweka kuwa mitakatifu, ndivyo Roho Mtakatifu anavyokaa ndani yetu, na ndivyo tunavyomfaidi Roho Mtakatifu kwa matunda yake yaliyotajwa katika Wagalatia 5:22.
Bwana akubariki sana.
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Je unaijua anwani ya msalaba?…na je unajua nguvu yake? Kama bado hujaifahamu basi leo ifahamu na anza kuitumia katika maombi yako, badala ya vitendea kazi vingine kama maji,chumvi na mafuta.
Yohana 19:19 “Naye Pilato akaandika anwani, akaiweka juu ya msalaba, imeandikwa, YESU MNAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI.
20 Basi anwani hiyo waliisoma wengi katika Wayahudi; maana mahali pale aliposulibiwa Yesu palikuwa karibu na mji; nayo iliandikwa kwa Kiebrania, na Kirumi, na Kiyunani”
Jina la YESU WA NAZARETI ndio ANWANI ya maombi ya kila Mkristo.
Umeahi kujiuliza kwanini haijaandikwa YESU MGALILAYA, au YESU MBETHLEHEMU mji ule aliozaliwa, badala yake imeandikwa YESU MNAZARETI?..na tena kwa lugha zote tatu (3), zilizokuu za dunia.
Kuna nini katika Nazareti?
Nazareti ndio mji uliotabiriwa na manabii kubeba utambulisho wa Masihi Mkuu ajaye… hivyo huo ni mji wa UTAMBULISHO KIBIBLIA.
Mathayo 2:23 “akaenda, akakaa katika mji ulioitwa Nazareti; ili litimie neno lililonenwa na manabii, Ataitwa Mnazorayo”.
Kwahiyo tunapotaja jina la YESU na kuelekeza yule wa NAZARETI tumelenga kwenye shabaha yenyewe hivyo mashetani yanaondoka, magonjwa yanaondoka, dhambi inaisha nguvu, kwasababu ndiye Masihi halisi aliyetajwa.
Hebu tulione hili zaidi…
Wakati Bwana YESU anamtokea Sauli alipokuwa anaenda Dameski kwa ajili ya kuwaua wakristo, utaona hakujitambulisha kama YESU wa Galilaya, au YESU aliye mbinguni, badala yake alijitambulisha kama YESU Mnazaeti ijapokuwa yupo mbinguni.
Matendo 22:6 “Ikawa nilipokuwa nikisafiri, nikikaribia Dameski, wakati wa adhuhuri, ghafula nuru kuu ilitoka mbinguni, ikanimulikia pande zote.
7 Nikaanguka nchi, nikasikia sauti ikiniambia, Sauli, Sauli, mbona unaniudhi?
8 Nikajibu, Wewe u nani, Bwana? Akaniambia, MIMI NI YESU MNAZARETI, ambaye wewe unaniudhi”.
Utaona pia Mitume wa Bwana YESU waliitumia hii anwani popote walipokwenda katika huduma zao.
Petro aliitumia alipokutana na yule kiwete aliyezaliwa katika hali ile..
Matendo 3:6 “Lakini Petro akasema, Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende.
7 Akamshika mkono wa kuume, akamwinua, mara nyayo zake na vifundo vya miguu yake vikatiwa nguvu.
8 Akaondoka upesi akasimama, akaanza kwenda; akaingia ndani ya hekalu pamoja nao, akienda, akiruka-ruka, na kumsifu Mungu.
9 Watu wote wakamwona akienda, akimsifu Mungu”.
Soma pia Matendo 2:22, Matendo 3:6, Matendo 4:10, Matendo 10:38, Matendo 26:9, Marko 1:24, Marko 16:6, Marko 10:47, Luka 24:9, Yohana 1:45, utazidi kuona jambo hilo.
Na hiyo pia ndio sababu Mungu aliruhusu Pilato aandike anwani ile juu ya msalaba… “YESU MNAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI”. Kwa lugha zote kuu, ikimaanisha kuwa anwani ya wokovu wa msalaba kwa mataifa yote na lugha zote ni jina la YESU WA NAZARETI.
Matendo 4:12 “Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo”
Maana yake njili inayohubiri msalaba pasipo kuhusisha anwani ya jina la YESU ni uchawi, maombi yoyote yasiyohusisha anwani ya jina la YESU ni unashiri na ibada za sanamu.
Kama anwani hiyo ya jina la YESU WA NAZARETI hata baada ya Bwana kupaa bado anaitumia akiwa mbinguni, sisi ni akina nani tuifanye iieshe matumizi katika zama zetu?, na kuweka mafuta, chumvi, maji au majina yetu kama mbadala??.
Tumia jina la YESU, liamini jina la YESU WA NAZARETI epuka matapeli, na jina la YESU HALIUZWI, EPUKA MATAPELI!.
Maran atha.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Mithali 29:17 “Mrudi mwanao naye atakustarehesha”.
Kumrudi mtoto sio “kumwadhibu tu”. Bali pia kumrekebisha (Kauli zake na njia zake).
Ni kweli maandiko yanaruhusu kumwadhibu mtoto kwa kiboko pale anapokosea, lakini hiyo iwe hatua ya mwisho baada ya kuona harekebishiki kwa maneno..
Katika hatua hiyo maandiko yameruhusu kutumia mapigo kwa huyo mtoto, ili kuiokoa roho yake na kuzimu.
Mithali 23:13 “Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.
14 Utampiga kwa fimbo, Na kumwokoa nafsi yake na Kuzimu”.
Soma pia Mithali 22:15.
Wengi wanaogopa kuwaadhibu watoto wao kwa mapigo wakiamini kuwa watapata madhara ya kisaikolojia na hata kiafya.. pasipo kujua kuwa hapo biblia imesema ukimpiga “hatakufa”..maana yake Mungu atazuia madhara yote ya kiafya, ikiwa lengo lako si lingine zaidi ya kumjenga.
Lakini kabla ya kufikia hatua hiyo ya matumizi ya fimbo, ni muhimu kuanza na maonyo, na makemeo.
Maana yake kama mtoto amekosea kusema ni lazima arekebishwe kusema kwake mapema, kwasababu watoto wanasikia mambo mengi na kuyachukua tu pasipo kupambanua.
Tuliwahi kufanya maombi sehemu fulani, tukakuta mtoto wa miaka 5 anatukana matusi makubwa na anarudia tusi hilo hilo moja, mara ya kwanza tulidhani ni mtoto ana mapepo, lakini baadae tuligundua kuwa hana mapepo na hata matusi aliyokuwa anayatamka alikuwa hajui maana yake, alitamka tu akidhani kuwa ni maneno ya kawaida, pasipo kujua kuwa alikuwa anatukana.
Sasa mtoto ni kwamba alisikia hayo matusi pengine kwa watoto wenzake anaocheza nao, wasio na maadili na yeye akidhani ni neno la kawaida akalichukua na kulitumia popote alipoona mazingira hayampendezi.
Sasa mzazi hakuchukua jukumu sahihi la kumrekebisha, badala yake tu alianza kumpiga kila alipotaja hilo neno akidhani kuwa anafanya makusudi, na hata sisi tulipofika alitukana na mamaye alimfinya, lakini alipolia bado aliendelea kutukana.
Mama alidhani mtoto anakiburi na mkorofi, kumbe mtoto alilia akijitetea kwa kudhani kuwa lile neno ni sahihi kutamka mahali pale.
Sasa laiti kama mzazi angepata wasaa wa kumketisha na kumwonya na kumwambia anachokisema si sahihi na hakifai, kabla ya mapigo… mtoto angeelewa na kubadilika.
Kwahiyo ni muhimu kuwasikiliza watoto wanasema nini na kuzirekebisha kauli zao mapema,
Ni vizuri kuangalia watoto wako wanachokiangalia na kukikosoa mbele yao kama hakifai…
Pia ni muhimu kufuatilia michezo yao wanayoicheza na kuikemea mapema mbele yao,…..kwani wao ni kuiga tu siku zote…ni vichache wanabuni wenyewe..
Vingi wanaiga kutoka kwa watu pasipo kupambanua, na wanajifunza kutoka kwa watu wanaowazunguka, ikiwemo wanafunzi wenzao mashuleni na pia kupitia Tv.
Kwahiyo kagua maisha ya watoto wako, na “warudi mapema”..wala hawatakuchukia, au kuwashusha kisaikolojia bali utawajenga kwa maisha yao ya baadae..
usipowarudi mapema na wakikua katika misingi hiyo itakuwa ni ngumu kubadilika ukubwani, kwani ile dhambi wameanza kuifanya tangu utotoni na hivyo hawawezi kushawishika kuona madhara yake ukubwani, na ili hali hawakuona madhara yake utotoni.
Mtoto akiwa na kiburi au mtukutu basi mkanye kila wakati, na panapobidi basi tumia kiboko ila usimwache akakua na hiyo tabia.
Na pia akiwa hasikii, tafuta kila namna awe anasikia, usiache na kusema huyu karithi hiyo tabia kwa watu fulani waliotangulia..
Na pia mfundishe kauli za kibiblia, na kuomba, mfundishe
salamu za kibiblia, na misemo ya kibiblia…akue katika hiyo hata kama bado hajaweza kuipambanua lakini mfanye akariri hivyo hivyo kwani itakuja kumsaidia mbeleni kwasababu itakuwa moyoni mwake.
Kwa kumlea hivyo biblia inasema baadaye atakustarehesha..
Mithali 29:17 “Mrudi mwanao naye atakustarehesha”.
Kustarehesha maana yake “hatakuja kukusumbua huko mbeleni”…
Mithali 22:6 “Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee”
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!
WAISRAELI WENGI SANA WANARUDI KWAO SASA.
BASI TUENDELEE KUMJUA MUNGU,NAYE ATATUJILIA KAMA MVUA YA VULI.
Jina tukufu la Bwana YESU KRISTO libarikiwe.
Je umewahi kutafakari kwanini mapigo yote tisa (9) aliyopigwa Farao bado moyo wake ulikuwa mgumu? Na kwanini lile pigo moja la mwisho la kufa wazaliwa wa kwanza ndipo akawaruhusu wana wa Israeli?.
Sasa hakuna mahali popote maandiko yanasema kuwa “Mungu aliufanya moyo wa Farao kuwa mlaini”.
Maana yake Farao aliendelea kuwa na moyo mgumu mpaka alipoingia kwenye ile bahari ya Shamu, na hapo ndio ikawa mwisho wake.
Sasa ni nini kilitokea mpaka Farao akawaachia wana wa Israeli?… Si kingine bali ni ule msiba alioupata,
Na huku bado moyo wake ukiendelea kuwa mgumu, alivunja sheria ya moyo wake na kuwafukuza wana wa Israeli kwa muda. (Lakini moyo wake bado ulikuwa mgumu tu).
Kutoka 11:1 “BWANA akamwambia Musa, Liko pigo moja bado, nitakaloleta juu ya Farao na juu ya Misri; baadaye atawapa ninyi ruhusa mtoke huku; naye hapo atakapowapa ruhusa, atawafukuza mtoke huku kabisa kabisa”
Sasa ni siri gani iliyokuwepo ndani ya wazaliwa wa kwanza wa Misri hata kumfanya Farao awafukuze wana wa Israeli?…Kwani ni wazi kuwa hata Farao angepigwa kwa mapigo gani ya asili asingewaachia wana wa Israeli.
Ila ni nini kilikuwa kwa wazaliwa wa kwanza wa kiMisri?
Kilichokuwa ndani ya wazaliwa wa kwanza wa Misri, ikiwemo mwana wa Farao si kingine zaidi ya “miungu ya kimisri”..
Hivyo kifo cha wazaliwa wa kwanza ilikuwa ni hukumu kubwa kwa miungu yao pamoja kudhalilika kwa miungu yao ambao waliamini ina nguvu nyingi.
Ndio maana MUNGU aliposhuka kuwaharibu wazaliwa wa kwanza pia alisema ataiharibu na miungu yao (ambayo kiuhalisia ilikuwa inaishi ndani ya hao wazaliwa wa kwanza).
Kutoka 12:12 “Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, namij nitawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi BWANA.”
Zamani katika nchi ya Misri na hata katika mataifa mengine ya dunia, wazaliwa wa kwanza wa kiume waliaminika kama miungu ya familia na ya nchi.
Na wanyama wa kwanza kuzaliwa, ndio waliotumika kwa kafara za miungu yao.
Hivyo watoto wote wa kwanza wa kiume walikuwa wanabeba ukuhani wa miungu, na roho zote za miungu zilikuwa zinakaa ndani yao.
Kwahiyo kilichomwumiza zaidi Farao si msiba wa mtoto, bali ni kuhukumiwa kwa miungu yao iliyokuwepo ndani ya wale watoto!!..
Kwaufupi Farao alichanganyikiwa kidogo, hakuelewa ni nini kimetokea katika eneo lake la imani.
Na hata waMisri wote walichanganyikiwa vivyo hivyo, hakuna ambaye hakulia..wote walilia na kuhofu na kutoelewa ni nini cha kufanya, waliyeyuka mpaka kufikia hatua ya wana wa Israeli kuwateka nyara.
Kutoka 12:33 “Wamisri nao wakawahimiza watu, kuwatoa katika nchi kwa haraka, maana walisema, Tumekwisha kufa sote.
34 Watu wakauchukua unga wa mikate yao kabla haijatiwa chachu, na vyombo vyao vya kukandia wakavitia ndani ya nguo zao mabegani.
35 Wana wa Israeli wakafanya kama neno lile la Musa; wakataka kwa Wamisri vyombo vya fedha na vyombo vya dhahabu, na mavazi.
36 BWANA akawajalia kupendelewa na Wamisri hata wakawapa kila walichokitaka. Nao wakawateka Wamisri nyara”
Ni ujumbe gani tunapata hapo?..au ni kitu gani kilichokuwa kimewafunga wana wa Israeli?
Si utajiri wala hazina zilizoko Misri kwamaana Bwana aliuharibu utajiri wake wote kwa zile mvua za mawe na nzige, vile vile si uzuri wa Misri, kwasababu Bwana aliharibu uzuri wake kwa zile mvua za mawe lakini bado wana wa Israeli walikuwa kifungoni.
Wala si ushujaa wa waMisri kwasababu Bwana aliwapiga kwa chawa, na majipu na aliwanyima maji ya kunywa kwa siku saba, hivyo walikuwa dhaifu..lakini bado wana wa Israeli walikuwa kifungoni.
Ni nini kilichokuwa kimewashikilia wana wa Israeli???…..jibu ni “miungu ya kimisri” iliyokuwa inaabudiwa ndani ya watu.
Hiyo ilipopigwa pamoja na makuhani wake (ambao ndio wazaliwa wa kwanza)..vifungo vikalegea, wana wa Israeli wakaachiwa.
Laiti Bwana Mungu angelileta hilo pigo mwanzoni kabla ya yote, Farao angeshaawaachia Israeli kitambo sana pamoja na moyo wake kuwa mgumu, lakini Mungu aliliruhusu liwe mwisho wa kusudi lake maalumu.
Na ukiendelea kusoma mbele utaona Bwana anawapa amri wana wa Israeli wawatakase wazaliwa wa kwanza na kwamba kila mzaliwa wa kwanza atakuwa ni wa Bwana, maana yake atakuwa kuhani wa Bwana kwa lazima (kwasababu kulikuwa na kitu katika wazaliwa wa kwanza).
Maana yake kila mzaliwa wa kwanza wa wana wa Israeli alipaswa kutolewa kwa Bwana kama Hana alivyomtoa Samweli kwa Bwana (hiyo ilikuwa ni amri).
Lakini sheria hiyo ilikuja kubadilika, na ukuhani wa wazaliwa wa kwanza likapewa kabila la Lawi.
Hesabu 3:12 “Mimi, tazama, nimewatwaa Walawi na kuwatoa kati ya wana wa Israeli badala ya wazaliwa wa kwanza wote wafunguao tumbo katika wana wa Israeli; na hao Walawi watakuwa wangu;
13 kwa kuwa hao wazaliwa wa kwanza wote ni wangu; katika siku ile niliyowapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri nikajiwekea wakfu wazaliwa wa kwanza wote wa Israeli, wa wanadamu na wa wanyama; watakuwa wangu; mimi ndimi BWANA”.
Hivyo wazaliwa wa kwanza wa wana wa Israeli wanaozaliwa ilikuwa ni sharti wakombolewe kwa sadaka ili watokane na kiapo hiko cha Bwana cha kuwa makuhani.
Na maana ya kukombolewa si kutolewa katika vifungo vya laana, kama mafundisho ya siku hizi za mwisho yanavyofundisha.
Bali ukombozi ilikiwa ni ile hali ya mtoto kutolewa katika nafasi ya kikuhani ambayo angepaswa kuitumikia maisha yake yote.
Hivyo anapokombolewa anakuwa huru kama watu wengine wasio na utumishi wa kikuhani (kwa ufupi anafunguliwa kutoka katika vifungo vya ukuhani)
Na mtoto wa kwanza asipokombolewa anabaki katika kifungo cha dhambi ya nafasi ya kikuhani.
Sasa swali je hata sasa katika agano jipya tunasheria hizo za kukomboa mzaliwa wa kwanza?.
Jibu ni la!..katika agano jipya hatuna sheria za kumkomboa mzaliwa wa kwanza au wa mwisho, kwasababu sote tuliomwamini Bwana YESU na kutakaswa kwa damu yake tunafanyika kuwa makuhani wa Bwana.
Ufunuo wa Yohana 1:6 “na kutufanya kuwa ufalme, na makuhani kwa Mungu, naye ni Baba yake; utukufu na ukuu una Yeye hata milele na milele. Amina”.
Hivyo sote tunayo huduma ya kikuhani na mbele za Mungu, na ukishakuwa tu kuhani tayari ni mzaliwa wa kwanza pasipo kujali rika…Hivyo kanisa la Kristo ni wazaliwa wa kwanza.
Waebrania 12:23 “mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika”.
Kwahiyo hakuna sadaka yoyote ya ukombozi kwa wazaliwa wa kwanza kwa jinsi ya mwili.
Mafundisho na maombi ya kukombolewa kwa wazaliwa wa kwanza si ya kiMungu, bali ni ya ibilisi.
Ndio tunaweza kuwaombea wazaliwa wetu wa kwanza na kuwaweka wakfu kwa Bwana, dhidi ya roho zinazofuatilia, lakini si kuwakomboa….uwakomboe na nini?…je uwakomboe uwatoe katika ukuhani?…maana ndio lengo la ukombozi hilo kibiblia lililokuwepo juu ya wana wa Israeli juu ya wazaliwa wa kwanza.
Zaidi sana watoto wetu wa kwanza wanapaswa wawe wazaliwa wa kwanza kiroho kwa kumwamini YESU na kutakaswa ndipo wanapofanyika makuhani kama wengine wote waliomwamini YESU.
Mwisho, fahamu kuwa kilichowafuga wana wa Israeli ni miungu ya misri, iliyokuwa inaabimudiwa ndani ya kila kiumbe kilichokuwa cha kwanza.
Hali kadhalika vile vitu vinavyojiinua katika maisha yetu vilivyo vya kwanza ndivyo ni lazima tuwe navyo makini kwani hivyo ibilisi anaweza kuvitumia kama mlango wa kutufunga.
Je cha kwanza kwako ni nini?…je ni kazi uliyonayo?…au ni cheo ulicho nacho?..au ni uzuri au ni Bwana YESU?..
Ni heri BWANA YESU akawa wa kwanza kwako, kwani yeye ndiye njia, kweli na Uzima.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Waliouawa Shitimu kwa pigo walikuwa ni watu Elfu 23 au elfu 24?.
(Ukarimu na maziwa)
Nakusalimu katika jina la Yesu Kristo mwokozi wetu. Karibu tujifunze maneno ya uzima. Haya ni mafunzo maalumu kwa ajili ya wanawake. Ikiwa utatamani kupata mengine mengi basi fungua link hii.. uweze yasoma..
https://wingulamashahidi.org/2021/07/21/masomo-maalumu-kwa-wanawake/
Kama wewe ni msomaji mzuri wa biblia, utakumbuka ile habari ya Debora na Baraka katika kitabu cha waamuzi.
Habari ile inaeleza jinsi Israeli ilivyo nyanyaswa na kutumikishwa na maadui zao wakaanani kwa muda wa miaka ishirini, chini ya mfalme mmoja aliyeitwa Yabini, na jemedari wake mkali aliyeitwa Sisera.(Waamuzi 4)
Watu hawa walikuwa wameendelea sana kivita, hivyo Israeli hawakuweza kufanya lolote isipokuwa kukubali mateso, ndipo wakamlilia Bwana sana. Naye akawasikia akawainulia mtetezi. Ndio huyu Debora nabii pamoja na baraka shujaa wa Israeli.
Sasa huyu Sisera alikuwa ni jemedari kwelikweli, hata Neno la Mungu lilipomjilia Debora, kumwagiza Baraka jemedari wa Israeli, akapange vita nao, bado alisita, na alichofanya ni kuomba Debora aende naye vitani..
Ni jambo ambalo ni kinyume na asili, wanawake kuhusishwa kwenye vita, kwasababu hiyo Debora akapewa Neno na Bwana kwa Baraka..kufuatana na wazo lake la kutaka.mwanamke aende naye vitani..kuwa ushindi huo hautakuwa mkononi mwake bali mkononi mwa mwanamke.
Waamuzi 4:8-9
[8]Baraka akamwambia, Kama utakwenda pamoja nami ndipo nitakwenda; bali kama huendi pamoja nami, mimi siendi.
[9]Basi akasema, Hakika nitakwenda pamoja nawe, lakini safari utakayoiendea haitakupatia heshima wewe; maana BWANA atamwuza Sisera katika mkono wa mwanamke. Debora akainuka, akaenda pamoja na Baraka mpaka Kedeshi.
Na kweli tunaona walipokwenda vitani kupigana nao. Yule Sisera jemedari wao, alifanikiwa kutoroka..Alipokuwa anakimbia alimwona mwanamke mmoja aliyeitwa Yaeli. Mwanamke huyo alimkaribisha kwake kwa ukarimu wa hali ya juu sana. Akampeleka sehemu ya maficho kabisa mahali ambapo si rahisi kugundulika, tena akamfunika ili kumuhakikishia ulinzi wote,
Jambo lile la ukarimu usio wa kawaida lilimtuliza moyo Sisera, akajihisi kama amepona, ndipo akamwomba yule mwanamke maji kidogo anywe. Lakini yule mwanamke bado akaendelea kuonyesha ukarimu wa hali wa juu sana, akaenda kumletea MAZIWA badala ya MAJI.. Pengine akamwambia aah! bwana wangu, maji si mazuri ukiwa umefunguka tangu asubuhi, tena kwenye mbio na pilika pilika za vita, kutumia maji si vizuri kiafya, kunywa kwanza maziwa haya, mwili uchangamke, upate nguvu, ndipo baadaye nitakupa maji unywe.
Sisera kuona vile akaendelea ku-relax, zaidi kuona ukarimu wa ajabu wa yule mwanamke, akafanya kosa akanywa yale maziwa, yakamlewesha kwa haraka mpaka akapotelea usingizini akasahau kabisa kwamba yupo vitani anatafutwa.
Lakini mwanamke Yaeli alipoona shujaa Sisera amelala fofofo, akasema nimempata adui yetu, sasa ninakwenda kumuua kirahisi kabisa.Akaenda kuchukua msumari mrefu, na nyundo. akavielekezea kichwani, akaupigilia ukaingia wote kichwani. Na mwisho wake ukawa umefikia pale pale.
Hata baadaye Baraka anakuja akakuta tayari mtu ameshakuwa marehemu.
Waamuzi 4:17-21
[17]Lakini Sisera akakimbia kwa miguu, akaifikilia hema ya Yaeli mkewe Heberi, Mkeni; kwa maana palikuwa na amani kati ya Yabini, mfalme wa Hazori, na nyumba ya Heberi, Mkeni.
[18]Yaeli akatoka kwenda kumlaki Sisera, akamwambia, Karibu Bwana wangu, karibu kwangu; usiogope. Akakaribia kwake hemani, naye akamfunika kwa bushuti.
[19]Akamwambia, Tafadhali nipe maji kidogo ninywe; maana nina kiu. Akafungua chupa ya maziwa, akampa kunywa, akamfunika.
[20]Naye akamwambia, Simama mlangoni pa hema; kisha itakuwa mtu awaye yote akija na kukuuliza, akisema, Je! Yupo mtu hapa, basi, mjibu, La, hapana.
[21]Ndipo Yaeli, mkewe Heberi, akatwaa kigingi cha hema, akashika nyundo mkononi mwake, akamwendea polepole, akamtia kile kigingi katika kipaji chake, nacho kikapenya, hata kuingia mchangani; kwa maana usingizi mzito ulikuwa umemshika; basi akazimia, akafa.
Ni nini Kristo anataka wanawake wafahamu kwa ushujaa wa Yaeli? (Ni ukarimu na Maziwa)
Kumbuka vita vyetu sisi si juu ya damu na nyama, bali dhidi ya wakuu wa giza hili na ibilisi. Na mtu yeyote ambaye anahubiri injili, mtu huyo ni askari wa Bwana. Mfano wa akina Debora, na Baraka. Haijalishi jinsia yake ni ipi, wote ni watendakazi katika shamba la Bwana.
Lakini kama tunavyojua Mungu ameweka majukumu mbalimbali ndani ya mwili wa Kristo, wewe kama mwanamke hujaitwa kuwa mchungaji, au askofu, lakini umeitwa kuwa shujaa wa kumwangamiza adui kwa karama uliyopewa. Debora na Yaeli hakuwa kama Baraka, maumbile yao hayakuumbwa kusimama na mikuki na ngao, na kukimbizana maporini usiku na mchana na maadui. Hapana.. bali ni kuwa katika utulivu. Na utulivu ukitumiwa vizuri huleta mlipuko mkubwa kuliko wingi wa makombora ya vita.
Aliyemuua shujaa Sisera alikuwa mwanamke, aliyekuwa nabii wa Israeli alikuwa mwanamke. Ushindi ulipatikana kwa mikono ya wanawake. Lakini bila kuvaa suruali, na mitutu vya vita.
Hata leo, ikiwa mwanamke ataitambua vema kazi ya injili kwa kufuata kanuni za kibiblia anaouwezo wa kuwavua watu wengi kwa Kristo zaidi hata ya mhubiri wa kusimama kwenye majukwaa makubwa.
Ukarimu, kwa wenye dhambi, upendo wa waliotekwa na mwovu, pamoja na maziwa (Ndio Neno la Mungu) ni Njia hii ya YAELI, ukiitumia itakufanya uwavute wale watu kwa Kristo wengi, na hatimaye kanisa la Kristo kukua na kuongezeka.
Ni watu wangapi unaweza wafadhili kichakula huku unawahubiria injili, unaweza wapelekea mavazi huku unawafundisha habari za Kristo, unaweza wafadhili kwa chochote huku unawaalika kanisani..kidogo.kidogo, upo kazini kwako, unazungumza nao kwa ukarimu, unawasaidia majukumu ambayo wangepaswa wayafanye wao wenyewe lakini wewe unawasaidia, lengo lako ni uwavute katika imani, huku ukihakikisha unawapa na maziwa, yaani maneno ya faraja ya Mungu,(1Wakorintho 3:2, 1Petro 2:2).
Wewe ni mamantilie, wateja wako, unawapa zaidi ya huduma, huku unawafundisha habari za Kristo, unawaeleza uzuri wa kukusanyika kanisani, n.k.
Ukiendelea hivyo baada ya kipindi fulani utashangaa watu hao wanavutika kwako, na kwa Kristo. Hata yule mpinga-kristo aliyekuwa na moyo mgumu kuliko wote anaokoka, yule boss wako ambaye alikuwa hataki kusikia masuala ya Mungu anaokoka. Wale ambao walirudi nyuma, wanaamka tena.
Onyesha tu ukarimu, lakini usiwe ukarimu wa bure, huo hautazaa chochote bali wenye injili nyuma yake.
Hivyo wewe kama mwanamke/binti wa kikristo simama katika eneo la utulivu, kiasi, kujisitiri, ni ukweli utaziangusha ngome sugu za adui.
1 Petro 3:1-5
[1]Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno;
[2]wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu.
[3]Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi;
[4]bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.
[5]Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
KWANINI DANI ALIKAA KATIKA MERIKEBU.
Maziwa yasiyoghoshiwa ni nini? Kwanini biblia inatumia mfano huo?
Maana ya Mithali 30:33 Kwa maana kupiga maziwa huleta siagi
Rudi Nyumbani
Kibiblia Neno laana linatafsiri kwa namna mbili.
Namna ya kwanza, ni Kupoteza sifa ya kukubaliwa na Mungu kwa jambo lolote lile. Na hii chanzo chake ni lile anguko la mwanadamu tangu mwanzo.
Namna ya pili, ni apizo alitoalo mtu kwa mwenzake au alitoalo Mungu mwenyewe, kwa mwanadamu ili wafikiwe na ubaya fulani, au wakasifikiwe na Mema waliyokusudiwa.
LAANA YA KWANZA:
Sasa laana hii ya kwanza, inazalika kwasababu ya asili yetu, ambayo ilionekana tangu Adamu, kuhasi maagizo ya Mungu, ambayo hata sisi sote tuliopo leo, asili hiyo ipo ndani yetu. Ni sawa na unavyomwona mdudu kama mende, ukimtazama tu tangu akiwa mtoto, utamchukia hata kabla hajaonyesha hali yake ya kupenda uchafu, kwasababu unajua asili hiyo ipo ndani yake. Atakuja kuwa mchafu tu.
Ndivyo ilivyo kwetu sisi, tayari Mungu alishaona tangu tunazaliwa tutamwasi tu yeye, mfano wa baba yetu Adamu.
Na ndio maana akaandaa mpango wa kuzaliwa upya mara ya pili, kupitia Yesu Kristo. Hivyo mtu yeyote anayezaliwa mara ya pili, anaondolewa katika laana hiyo ya kukataliwa na Mungu, na anakuwa mwana wa Baraka. Laana hii haiwezi kuondoka bila damu ya Yesu.
Hiyo ndio sababu kwanini maandiko yanasema Yesu alifanyika laana kwa ajili yetu. Maana yake, tunapokombolewa na yeye tunafanywa kuwa watu wengine kabisa wenye asili nyingine wasio na laana, wenye kukubaliwa na kupendwa na Mungu.
Wagalatia 3:13 Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti;
14 ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani.
Hivyo wewe uliyeokoka, na kupokea Roho Mtakatifu unaitwa, mbarikiwa, unaitwa mungu duniani, mtoto wa Mungu kwelikweli.
LAANA YA PILI
Lakini laana ya pili, kama tulivyoona ipo katika maapizo ambayo huyatoa Mungu au mwanadamu mwenyewe.
a) Tukianzana na zile zinazonenwa na Mungu
Mungu anaweza kukutamkia laana, hata kama utakuwa umekombolewa na yeye. Unaweza kushiriki mabaya. Laana hizi zinaweza kukufanya usipoteze wokovu wako, lakini zikakukosesha mambo mengi sana duniani.
Mfano wa hizi ndio zile alizowaambia wana wa Israeli, kwamba watakapoacha sheria zake, basi watatawanywa katika mataifa yote, watakuwa mikia na sio vichwa, nchi itazuliwa Baraka zake, wataondokeshewa adui zao N.k. (Kumbukumbu 28)
Mfano pia wa hizi, ndio kama ile aliyoilaani nchi, na nyoka pale Edeni. Akasema itatoa miiba, na nyoka atakwenda kwa tumbo (Mwanzo 3:17). Vilevile ndio ile aliyomwambia Kaini kuwa atakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani (Mwanzo 4:12).
Hata sasa wapo wengi wanaokutana na maapizo hayo ya Mungu kwa kufanya dhambi au makosa ya makusudi. Namna ya kueupuka laana hizi ni kutii agizo la Mungu.
Kwasababu unapozizoelea zitakufanya uangukie kabisa kwenye kundi lile la kwanza la kukataliwa kabisa..la watu ambao hawajaokoka.
Waebrania 6:4 Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu,5 na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo,
6 wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri.
7 Maana nchi inayoinywa mvua inayoinyeshea mara kwa mara, na kuzaa mboga zenye manufaa kwa hao ambao kwa ajili yao yalimwa, hushiriki baraka zitokazo kwa Mungu; 8 bali ikitoa miiba na magugu hukataliwa na kuwa karibu na laana; ambayo mwisho wake ni kuteketezwa.
Kinyume cha laana ni Baraka, unapotii amri za Mungu, umejiwekea mazingira mazuri ya kupokea Baraka.
b) Lakini pia zipo laana zinazonenwa na mwanadamu.
Hizi nazo zimegawanyika katika makundi mawili.
i) Kundi la kwanza ni la watu wa Mungu/wenye haki.
Kwamfano Utakumbuka Hamu alipoona uchi wa baba yake. Nuhu aliulaani uzao wake, Hivyo watu wa Mungu wamepewa mamlaka hiyo, hata sasa, ndio maana Bwana Yesu alisema mtakalolifunga duniani, limefungwa mbinguni, na akatusihi pia tuwe watu wa kubariki kuliko kulaani. (1Petro 3:9)
Unapokosewa na mwenye dhambi epuka kutoa neno la madhara kwake, kwasababu hakika jambo hilo litampata na kumwangamiza kabisa. Ndicho alichokifanya Elisha kwa wale vijana arobaini na wawili waliomdhihaki.
ii) Kundi la pili ni laana zitokazo kwa watu waovu.
Husasani wachawi, nao pia huweza kusema jambo likatokea, Utakumbuka kisa cha Balaamu mchawi, alipoajiriwa na Balaki kwenda kuwalaani Israeli wa Mungu, lakini alishindwa akajikuta anawabariki badala ya kuwalaani.
Akasema hakuna uchawi (Hesabu 23:23).
Ikiwa wewe umeokoka, huna haja ya kuogopa laana za hawa, kwasababu haziwezi kukupata, kwasababu unalindwa na nguvu za Mungu, hizi huwa zinawapata watu ambao wapo nje ya Kristo YESU.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
NUHU WA SASA.
MADHARA YA DHAMBI YA UASHERATI.
KUVUNJA MAAGANO YA UKOO.
Rudi Nyumbani
Wakorintho 2:10 Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu.
11 Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu
Sifa mojawapo ya Roho Mtakatifu, ni kuchunguza, na tunajua mpaka kitu kichunguzwe ni lazima tu kitakuwa kimesitirika, kwa lugha nyingine tunaweza kusema kipo katika mafumbo. Hivyo Roho Mtakatifu anafanya kazi ya kuyachunguza “YOTE”. Akiwa na maana Mafumbo yote, si tu yale yaliyo chini bali pia hata yaliyo kule juu Mungu mwenyewe alipo.
Na leo tutanyambua aina hizo za mafumbo kwa upana, ili tuelewe ni kwa jinsi gani Roho Mtakatifu alivyomsaada mkubwa sana kwetu.
Mafumbo ya Wanadamu:
Ukipokea Roho Mtakatifu, moja kwa moja unaongezewa hekima, ya kuweza kupambanua, na kuhukumu, akili zote za kibinadamu. Wala hakuna litakalokushinda, kwamfano Bwana Yesu alipowekewa mitego mingi na wayahudi ili watafute kosa ndani yake, wapate kumshitaki, hawakuweza kumshinda kwasababu saa ile ile, alielewa vema mawazo yao kwa Roho Mtakatifu aliyekuwa ndani yake.
Kwamfano katika ile habari ya kulipa kodi walipomjaribu, walishindwa kabisa kabisa.
Mathayo 22:15 Ndipo Mafarisayo wakaenda zao, wakafanya shauri, jinsi ya kumtega kwa maneno.
16 Wakatuma kwake wanafunzi wao pamoja na Maherodi, wakasema, Mwalimu, twajua ya kuwa wewe u mtu wa kweli, na njia ya Mungu waifundisha katika kweli, wala hujali cheo cha mtu awaye yote, kwa maana hutazami sura za watu.
17 Basi utuambie, Waonaje? Ni halali kumpa Kaisari kodi, ama sivyo? 18 Lakini Yesu akaufahamu uovu wao, akasema, Mbona mnanijaribu, enyi wanafiki?
19 Nionyesheni fedha ya kodi. Nao wakamletea dinari. 20 Akawaambia, Ni ya nani sanamu hii, na anwani hii?
21 Wakamwambia, Ni ya Kaisari. Akawaambia, Basi, mlipeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na Mungu yaliyo ya Mungu. 22 Waliposikia, walistaajabu, wakamwacha, wakaenda zao
Wakati mwingine walimletea mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, ili wamnase wakashindwa pia, kwasababu Yesu alikuwa na Roho wa Mungu ndani yake(Yohana 8:1-11). Ndio maana Yesu naye akatupa hakikisho hilo kwamba katika kuenenda kuhubiri kwetu, tusihofu watakapotaka kutushitaki, na kutupeleka mabarazani, au mahakamani, kutuhukumu, kwani yeye mwenywe atatupa kinywa cha hekima ambacho watesi wetu hawatatuweza.
Yohana 21:12 Lakini, kabla hayo yote hayajatokea, watawakamata na kuwaudhi; watawapeleka mbele ya masinagogi, na kuwaua magerezani, mkipelekwa mbele ya wafalme na maliwali kwa ajili ya jina langu.
13 Na hayo yatakuwa ushuhuda kwenu.
14 Basi, kusudieni mioyoni mwenu, kutofikiri-fikiri kwanza mtakavyojibu;
15 kwa sababu mimi nitawapa kinywa na hekima ambayo watesi wenu wote hawataweza kushindana nayo wala kuipinga.
Lakini pia Roho achunguzaye mafumbo hutupa hekima sio tu ya kutambua lakini pia ya kufanya hukumu sahihi.
Utakumbuka kisa kile cha Sulemani na wale wanawake wawili makahaba, ambao kila mmoja alikuwa ana mng’ang’ania mtoto Yule mmoja wakisema ni wake. Lakini Sulemani alipewa hekima ya kutoa hukumu vema, kwa kuwaambia nileteeni upanga, nimgawanye, ili kila mtu achukue nusu yake. Yule ambaye mtoto si wake akasema na iwe hivyo, lakini Yule mwingine akamwonea huruma. Ndipo Sulemani akatambua kuwa mtoto ni wa Yule mama aliyemwonea huruma (1Wafalme 3:16-28)
Sasa hiyo yote ni kazi ya Roho Mtakatifu ya kuchunguza mafumbo ya wanadamu, na kutupasha habari.
Lakini pia hutumia njia ya maono au ndoto kutufahamisha. Mafumbo yaliyositirika mioyoni mwa watu. Mfano wa Yusufu kwa Farao, na Danieli kwa ile ndoto ya Nebukadreza, Mambo ambayo hata walioziota ndoto zenyewe hawakuzikumbuka wala kujua maana zao, lakini Roho Mtakatifu aliwafunulia.
Hivyo ndivyo Roho Mtakatifu anavyotusaidia kuchunguza mafumbo ya wanadamu.
Mafumbo ya shetani:
Si kawaida ya shetani kujidhihirisha kwa wazi kama wengi wanavyodhani, bali huja kama malaika wa nuru, hivyo kama hujajazwa Roho Mtakatifu vema kamwe huwezi yajua mafumbo yake. Ndicho walichokikosa baadhi ya watakatifu wa kanisa la Thiatira.
Ufunuo 2:24 Lakini nawaambia ninyi wengine mlioko Thiatira, wo wote wasio na mafundisho hayo, wasiozijua fumbo za Shetani, kama vile wasemavyo, Sitaweka juu yenu mzigo mwingine.
25 Ila mlicho nacho kishikeni sana, hata nitakapokuja.
Swali ni je haya Mafumbo ya shetani yanakujaje?
Yapo Manabii wa Uongo:
Manabii hawa wa uongo wamegawanyika katika makundi mawili.
Kundi la watumishi wa Mungu: Hawa ni ambao hawajasimama vema, hivyo wakati mwingine shetani hutumia vivywa vyao au mafundisho yao kupotosha wengine, bila hata ya wao kukusudia wakati mwingine. Mfano wa hawa alikuwa ni Petro, wakati ule aliposimama mbele ya Yesu na kuanza kumkemea kwamba hatakwenda msalabani. Lakini Yesu palepale alitambua si Petro anayezungumza bali ni shetani, akamkea na kumwambia nenda nyuma yangu shetani (Mathayo 16:23).
Mfano wa hawa pia ni wale manabii 400 wa Ahabu. Ambao walimtabiria mfalme kuwa akienda vitani atashinda, kumbe ni pepo la uongo liliwaingia vinywani mwao likawaonyesha maono feki. Matokeo yake yakawa ni mfalme kufa (1Wafalme 22).
Mfano wa watumishi wa namna hii wanaompa shetani nafasi kuwatumia ni wengi sana. Hivyo si kila neno ambalo utaambiwa na kila anayeitwa mtumishi ulipokee tu au uliamini, ukijawa Roho vema utaweza yapambanua vizuri mafumbo haya ya shetani katikati ya vinywa vyao. Atakupa upambanuzi, kwa mafuta aliyoyaweka ndani yako.
Kundi la watumishi wa shetani: Hawa wanajijua kabisa kuwa ni watumishi wa ibilisi, ni wachawi wanaovaa suti na majoho, na kusimama madhabahuni, hawana hata ushirika na Kristo. Kuwatambua hawa Roho alitufundisha, ni kutazama matunda yao. (Mathayo 7:15-20), asilimia kubwa ya hawa wanajigamba kwa vitu, ukubwa. Na mafundisho yao ni ya mwilini. lakini pia kwasababu wana mapepo ya utambuzi hupendelea sana kujitii manabii. Ni wengi leo wanawafuata kwasababu ya kazi hiyo, wakidhani wanatabiriwa na Roho Mtakatifu kumbe ni mizimu. Ukijawa Roho vema utaweza kuzitambua hizo Roho. Kwasababu hazina ushirika hata kidogo na jina la Yesu, au mambo ya rohoni.
Mafumbo ya Mungu.
Mungu pia ana mafumbo yake, ambayo kama huna Roho Mtakatifu huwezi yatambua. Kwamfano Kristo anatembea leo duniani, akiwa na kiu, na njaa na uchi, na anagonga kwenye milango ya watu..Sasa kwasababu wewe hujui unadhani akija kwako atakutokea amevaa mavazi meupe na uso unaong’aa kama jua, hujui kuwa amekuja kama watumishi wa Mungu wa kweli wanaojitaabisha kwa ajili ya roho yako, kukulea na kukulisha neno la Mungu. Lakini wewe unasema hawa ni matapeli, omba omba.
Mathayo 25:31 Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake;
32 na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi;
33 atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto.
34 Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu;
35 kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha;
36 nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia.
37 Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha?
38 Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika?
39 Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia?
40 Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.
Umeona hao wanaozungumziwa hapo, sio wale maskini unaowaona barabarani, au omba-omba, bali ni watendakazi wa Mungu. Hivyo watu wanaoonyosha mikono yao, kuwatengemeza watumishi na madhabahu za kweli za Mungu, wamejaliwa kuyajua mafumbo haya ya Mungu.
Mafumbo ya Mungu yapo mengi sana, ndio siri za ufalme wa mbinguni ambazo zipo ndani ya Yesu Kristo. Ambazo Yesu mwenyewe alizizungumza pia katika Mathayo 13.
Vilevile ukitaka umwone Mungu fumbo lake ni upendo, Ukitaka upewe na Mungu, fumbo lake ni utoe, ukitaka ukwezwe na Mungu fumbo lake ni unyenyekevu.
Kwanini leo utaona mtu anasema sijawahi kumsikia Mungu, na angali Mungu anasema nasi kila siku? Sijawahi kukutana na Mungu, na angali Mungu anakutana nasi kila siku? Sijawahi kuziona nguvu za Mungu, na wakati zipo nasi kila kitu? Ni kwasababu hajajawa vema Roho Mtakatifu, ambaye atamjalia kuujua moyo wa Mungu upo wapi.
Hivyo kwa hitimisho ni kuwa, tunahitaji kujazwa Roho na hiyo inakuja tutengapo muda wetu mwingi kila siku kutafakari sana Neno, pamoja na kuomba kila siku kwa muda usiopungua saa moja , hiyo itakupelekea kujazwa vema Roho, na hatimaye tutaweza kuyachunguza yote, na kuyatambua yote. Na wala hatutashindwa aidha na mwanadamu au shetani.
Ubarikiwe.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
JINSI ROHO MTAKATIFU ANAVYOKUJA JUU YA MTU.
Roho Mtakatifu ni nani?.
ZIFAHAMU KAZI KUU (10) ZA SHETANI DUNIANI.
Rudi Nyumbani