Unajua Kwanini Naamani atake kuingia tena katika nyumba ya Rimoni baada ya kuponywa? (2Wafalme 5:18)
Turejee..
2Wafalme 5:18 “Jambo hili Bwana amwachilie mtumwa wako; bwana wangu akiingia nyumbani mwa Rimoni ili aabudu humo, naye akitegemea mkononi mwangu, nami nikijiinama nyumbani mwa Rimoni, hapo ninapojiinama nyumbani mwa Rimoni, Bwana amwachilie mtumwa wako jambo hili”.
Katika kitabu hiki cha 2Wafalme 5, tunasoma uponyaji wa mtu mmoja aliyeitwa Naamani, aliyekuwa Jemedari wa jeshi la mfalme wa Shamu. Lakini huyu Naamani alikuwa ni mtu mwenye ukoma ingawa alikuwa shujaa wa vita.
Siku moja alienda kutafuta uponyaji kutoka kwa Mungu wa Israeli, kupitia taarifa alizozipitia kutoka kwa kijakazi wake aliyekuwa Mwishraeli kwa asili, na alipokutana na Nabii Elisha, kwa uongozo wa Roho wa Mungu aliagizwa akajichovye katika mto Yordani mara saba na ugonjwa wake (wa ukoma) utaondoka.
Mwanzo alikataa lakini baadaye alikubali na Bwana MUNGU akamponya ule ukoma, na ngozi yake ikarudi kama ya mtoto mchanga.
2Wafalme 5:14 “Ndipo akashuka, akajichovya mara saba katika Yordani, sawasawa na neno lake yule mtu wa Mungu; nayo nyama ya mwili wake ikarudi ikawa kama nyama ya mwili wa mtoto mchanga, akawa safi”.
Kwa uponyaji huo alioupata aliahidi kutotoa tena sadaka kwa miungu aliyokuwa anaitumikia hapo mwanzo ambayo haikumsaidia kitu. (na mungu aliyekuwa anamtumikia hapo mwanzo kabla ya kuponywa na Bwana alikuwa anaitwa rimoni) .
2Wafalme 5:17 “Naamani akasema; Kama sivyo, lakini mtumwa wako na apewe mzigo wa udongo wa baghala wawili; kwa maana mtumwa wako hatatoa tena sadaka ya kuteketezwa wala dhabihu kwa miungu mingine, ila kwa Bwana”.
Lakini pamoja na ahadi hiyo, aliona tatizo moja mbele yake..
Alijua atakaporudi kwa mfalme, bado atakuwa chini ya mfalme kama jemedari wake, na mara zote alikuwa anaongozana naye kuingia katika hekalu la mungu rimoni, naye pia alikuwa anasujudu.. Hivyo akajua atakaporudi hiyo desturi itaendelea.
Kwahiyo akatangulia kuomba radhi kwamba endapo jambo hilo likitokea basi Mungu amsamehe (yaani amwachilie), kwasababu hajadhamiria kufanya hivyo isipokuwa tu ni kwa kutimiza matakwa ya mfalme, lakini yeye ndani ya moyo wake au kwa hiari yake mwenyewe hajakusudia kumtolea mungu rimoni sadaka wala kumsujudia..
Hivyo Elisha akamruhusu aende na afanye kama anayoyaona moyoni mwake.
Ni jambo gani tunalojifunza?..
Ni kweli kwa Naamani tunajifunza Imani ya kupokea uponyaji baada ya kukubali mashauri, kwani kitendo cha kuamini tu taarifa kutoka kwa kijakazi, hiyo ni Imani kubwa, (kwamaana si wote wanaweza kuwasikiliza na kuwaamini watu walio chini yao kiuwezo, kielimu na hata kiufahamu), lakini Naamani aliweza hilo..Na hata sisi ili tuvute msaada wa Mungu na muujiza wake ni sharti tuwe watu wa Imani kama Naamani.
Na ndio Bwana YESU anakuja kurejea habari ya Imani yake katika kitabu cha Luka 4:27
Luka 4:27 “Tena, palikuwa na wenye ukoma wengi katika Israeli zamani za nabii Elisha, wala hapana aliyetakaswa ila Naamani, mtu wa Shamu.”
Lakini pamoja na hayo pia, lipo ambalo hatupaswi kujifunza kwa Naamani,..
NAAMANI MOYONI ALIMKIRI MUNGU WA ISRAELI kwa muujiza aliofanyiwa LAKINI KWA MATENDO ALIMTUMIKIA MUNGU RIMONI kwa heshima ya Mfalme.
Kwahiyo alikuwa ni VUGUVUGU..Moyo wake upo kwa Mungu wa Israeli,…lakini viungo vyake na utumishi wake upo kwa rimoni (mungu wa nchi yake).
Mfumo wa nchi yake ulimbana!, kazi aliyoifanya ilimfunga!..ijapokuwa alikuwa anatamani kweli kutotumika katika hekalu la mungu ambaye hakumsaidia, lakini tayari alikuwa ameshafungwa Nira, na hakuwa tayari kuikata hiyo nira.
Katika kitabu kile cha 2Wakorintho 6:15 Neno la Mungu linasema, tusifungwe Nira pamoja na wasioamini kwa jinsi isivyo sawasawa.
2Wakorintho 6:14 “Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? 15 Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? 16 Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. 17 Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha”
2Wakorintho 6:14 “Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?
15 Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini?
16 Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
17 Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha”
Na sisi kama wakristo ni lazima tutoke katika mahekalu ya sanamu, ni lazima tutoke katika kazi zinazotulazimu kusujudia sanamu au kumwabudu shetani, ni lazima tuache makundi yanayoturudisha kumwabudu shetani.
Ni kweli inagharimu, lakini hiyo ndio maana ya “kuubeba msalaba na kujikana nafsi”, kama kazi inakuuzisha pombe, au mwili wako, au inakuabudisha sanamu…IACHEEE!!. Ili uondokane na uvuguvugu. Kwasababu Bwana YESU alisema atawatapika wale wote walio vuguvugu.
Ufunuo 3:15 “Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. 16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa change”.
Ufunuo 3:15 “Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.
16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa change”.
Bwana atusaidie.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
KUWA MAKINI NA MITANDAO, NI SHIMO REFU.
Agano ni nini? na kuna aina ngapi za maagano?
MADHIHIRISHO MATATU YA MUNGU.
Orodha ya Miji ilivyojulikana Agano Jipya na inavyojulikana sasa
JE! NINAWEZA KUPOTEZA FURAHA YA WOKOVU?
Rudi Nyumbani
Print this post