Title February 2024

SADAKA INAHARIBU NGUVU ZA MADHABAHU ZA MASHETANI.

(Masomo maalumu yahusuyo matoleo  na sadaka).


Karibu tujifunze bible, Neno la Mungu wetu lililo mwanga wa Njia yetu na Taa iongozayo miguu yetu (Zab. 119:105).

Kuna umuhimu mkubwa sana wa kutoa Sadaka katika agano jipya, na shetani anafanya kila awezalo kuwazuia watu wasitoe sadaka kwa Mungu, kwani anaijua Nguvu iliyopo katika sadaka kwa mkristo.

Na moja ya njia anayotumia kuwafanya watu wasimtolee Mungu, ni kuwanyanyua watu/watumishi wake ambao watalichafua eneo hilo kwa aidha kuwalazimisha watu, au kuwatapeli, au kutumia uongo kwa kivuli cha biblia.

Na mtu aliye dhaifu kiimani, akishaona kasoro hizo basi moja kwa moja anakata shauri au anaadhimia kutotoa kabisa sadaka mahali popote kwa kuamini kuwa ni utapeli tu ndio unaoendelea, hivyo adui anakuwa ameshinda juu ya huyo mtu katika eneo la utoaji.

Lakini jambo ni moja tu!.. SADAKA INA NGUVU, na kila MKRISTO (pasipo kujali wadhifa wake, iwe mchungaji au mwanafunzi) NI LAZIMA AJIFUNZE KUTOA SADAKA ili KUFUNGUA MILANGO YA BARAKA na KUONDOA VIKWAZO.

Sasa zipo faida nyingi za SADAKA, lakini leo nataka tuizungumzie hii moja, ambayo ni muhimu sana kuijua…Nayo si nyingine Zaidi ya “KUHARIBU NGUVU ZA MADHABAHU”. Si kila madhabahu inaharibiwa kwa kuomba tu!, la! Nyingine ni lazima zihusishe matoleo/Sadaka.

Hebu tusome habari ya Gideoni kidogo.

Waamuzi 6:25 ”kawa usiku uo huo Bwana akamwambia, MTWAE NG’OMBE WA BABA YAKO, yaani ng’ombe wa pili, wa miaka saba, UKAIANGUSHE MADHABAHU YA BAALI, aliyo nayo baba yako, UKAIKATE ASHERA ile iliyo karibu nayo;

26 UKAMJENGEE BWANA, MUNGU WAKO, MADHABAHU juu ya ngome hii, kwa taratibu zake; UKAMTWAE YULE NG’OMBE WA PILI NA KUMTOA AWE SADAKA YA KUTEKETEZWA, kwa kuni za ile Ashera uliyoikata”

Hapo kuna hatua 4 Gideoni alizoambiwa na Mungu azifanye, ambazo zimebeba funzo kubwa..

   1.MTWAE NG’OMBE WA BABA

Kwanini Amtwae Ng’ombe wa Baba yake?.. Kwasababu madhabahu ile ya baali ilikuwa imemshika sana baba yake (ilikuwa na nguvu juu ya nyumba ya baba yake yote). Ikifunua kuwa na sisi tunapotaka kushughulika na madhabahu za mababa, ni lazima tutafute sadaka kwajili yao, tena zile zinazowagusa kama hiyo ya Gideoni.

   2. UKAIANGUSHE MADHABAHU YA BAALI.

Baada ya Gideoni kumtwaa Ng’ombe wa baba yake, hatua iliyofuata ni kuangusha ile madhababu ya baali na ashera iliyomshika baba yake (kwa kuivunja vunja na kuiponda ponda). Na sisi baada ya kuandaa sadaka hatua inayofuata ni kuzivunja hizo madhabahu kwa damu ya YESU kwa njia ya maombi na kwa KUZIONDOA KABISA KIMWILI KAMA ZINAONEKANA..

Kama kuna miti fulani inatumika kiibada hapo ulipo unaikata, kama ni mazindiko yamewekwa juu ya dari unayaondoa, wala usiogope, na tena wakati mwingine usimwambie mtu..wewe yaondoe kimya kimya kama alivyofanya Gideoni..ukienda kutafuta ruhusa hawatakuruhusu..zaidi utanyanyua vita vikali..

Gideoni angeenda kumpa kwanza taarifa baba yake kwamba ile madhabahu ya baali anaenda kuivunja baba yake asingemwelewa kabisa, kwani zile roho zilikuwa zimemshika baba yake na alikuwa anaiogopa sana ile miungu.. Vile vile madhabahu za mababa/na mababu zimewashika na kuwaogopesha wanaoziabudu.

Hivyo wewe vaa ujasiri kuwasaidia, kwani baada ya hapo watamshukuru Mungu wako kwa mambo yatakayofanyika baada ya hapo.

  3.UKAMJENGEE BWANA MADHABAHU.

Baada ya Gideoni kuvunja ile madhabahu akaijenga madhabahu ya BWANA pale pale. Na sisi baada ya maombi na kusafisha kila uchafu..tunalisimamisha jina la Bwana mahali pale, kwa kuanzisha ibada, au kanisa…Wengi baada ya maombi hakuna tena kinachoendele, jambo ambalo ni la hatari sana!..

Ni lazima jina la Bwana liendelee kutamkwa mahali pale, ili madhabahu ya adui isisimamishwe tena, kama ni nyumbani au kijijini. (Maombi ya asubuhi na jioni lazima yafanyike, vile vile nyakati za kujifunza Neno la Mungu lazima ziendelee, na watu waendelee kumtafuta Mungu).. Sio kuomba tu na kuacha!.

   4. UKAMTOE NG’OMBE KUWA SADAKA.

Baada ya Gideoni kujenga madhabahu akamtoa yule Ng’ombe wa baba yake awe sadaka na hapo ndipo ukawa mwisho wa Nguvu ya ile madhabahu ya baali kutenda kazi…ikamwachia baba yake moja kwa moja, hata alipokuja na kusikia kuwa ile madhabahu ya ashera imevunjwa na mwanae wala hakuogopa kwani tayari vifungo vya uoga vilikuwa vimeshamwachia…. na hata yeye (Gideoni) naye pia alifunguliwa kwa ujumla.. Na hapo ndio ukawa mwanzo wa ushujaa wa Gideoni!.

Vile vile na sisi tunapomaliza maombi na kuhitimisha kuvunja madhabahu…Ile sadaka inapaswa itumike kujenga kanisa la pale, au kuimarisha ibada za pale, ikiwa na maana kwamba kama fedha basi zitumike kununua biblia, au vitabu vya nyimbo, au kama ni kiwanja kimetolewa kama sadaka basi kitumike kujenga kanisa ili watu wa Mungu waendelee kumwabudu Mungu wa kweli pale.

Lakini ikiwa hakuna namna ya wewe kufika mahali pale ambapo madhabahi hizo zimesimamishwa, aidha kutokana na umbali.. basi baada ya maombi toa sadaka katika madhabahu nyingine yoyote ya Mungu aliye hai na italeta matokeo yale yale. Lakini kumbuka USIOMBE TU, BILA KUTOA!..TOA TOA TOA!!!!!

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

MADHABAHU NI NINI?

YANAYOENDELEA SASA KATIKA MADHABAHU YA MUNGU ROHONI.

UDHAIFU WA SADAKA!

Kwanini madhabahu zilitengenezwa kwa mawe yasiyochongwa?

MAVAZI YA NDANI NA YA NJE.

Rudi Nyumbani

Print this post

MANABII WA BIBLIA (Wanaume)

Manabii Wanaume katika biblia walikuwa wengi kiidadi kuliko manabii wanawake.


UFUATAO NI UFUPISHO KWA NJIA YA JEDWALI:

Kutazama Jadwali zima, basi Slide kuelekea upande wa kushoto.

N/AJINAWAFALME WALIOTAWALA ENZI ZAKEMIJI/MATAIFA ALIYOYATOLEA UNABIIMAJIRA ALIYOTOA UNABII
1.ELIYAAhabu, Ahazia na YoramuISRAELIKabla Israeli haijapelekwa Ashuru
2.ELISHAYoramu, Yehu na YehoahaziISRAELIKabla Israeli haijapelekwa Ashuru
3.YONAYeroboamu wa PiliNINAWI (Ashuru)Kabla Israeli haijapelekwa Ashuru
4.NAHUMUManase, Amosi na YosiaNINAWI (Ashuru)Kabla YUDA haijapelekwa Babeli
5.OBADIASedekiaEDOMUKabla YUDA haijapelekwa Babeli
6.HOSEAYeroboamu wa Pili, Zekaria, Shalumu, Menahemu, Pekahia,Peka na HosheaISRAELIKabla Israeli haijapelekwa Ashuru
7.AMOSIYeroboamu wa PiliISREALIKabla Israeli haijapelekwa Ashuru
8.ISAYAuzia, Yothamu, Ahazi, Hezekia na ManaseYUDAKabla YUDA haijapelekwa Babeli
9.YEREMIAYosia, Yehoahazi,Yehohakimu, Yekonia na Sedekia. YUDAKabla YUDA haijapelekwa Babeli
10.YOELIYoashiYUDAKabla YUDA haijapelekwa Babeli
11.MIKAYothamu, Ahazi, Hezekia na Manase. YUDAKabla YUDA haijapelekwa Babeli
12.HABAKUKIYehoyakimu na YekoniaYUDAKabla YUDA haijapelekwa Babeli
13.SEFANIAAmoni na YosiaYUDAKabla YUDA haijapelekwa Babeli
14.EZEKIELIYekonia na SedekiaYUDA (Ikiwa utumwani Babeli)Wakati YUDA Ikipelekwa utumwani Babeli
15.DANIELIYehohakimu, Yekonia na Sedekia.YUDA (Ikiwa utumwani Babeli)Wakati YUDA ikiwa utumwani Babeli
16.HAGAILiwali ZERUBABELIYUDA (Masalia waliorudi Yerusalemu kutoka utumwani)Baada ya YUDA kutoka utumwani Babeli
17.ZEKARIALiwali ZERUBABELIYUDA (Masalia waliorudi Yerusalemu kutoka utumwani)Baada ya YUDA kutoka utumwani Babeli
18.MALAKILiwali NEHEMIAYUDA (Masalia waliorudi Yerusalemu kutoka utumwani)Baada ya YUDA kutoka utumwani Babeli

Mbali na hawa walioorodheshwa katika Jedwali hilo hapo juu, walikuwepo pia Manabii wengine ambao hawakuonekana wakitajwa katika kutoa Nabii za Nchi au Taifa.. Mfano wa hao tunawaona katika Jedwali lifuatalo.

N/AJINAMFALME ALIYETAWALA WAKATI WAKEHALI KIROHOMAREJEO
1.MUSAIsreli wakiwa Misri na JangwaniWA KWELI Kutoka, M/Walawi, Kumbukumbu na Hesabu
2.MIKAYAAhabuWA KWELI1Wafalme 22:13
3.AHIYAYeroboamuWA KWELI1Wafalme 1:45
4.NATHANISauliWA KWELI2Samweli 7:2
5.Nabii wa Yuda (Asiyetajwa jina)Yeroboamu wa KwanzaWA KWELI1Wafalme 13:1-9
6.Nabii MZEE (Asiyetajwa jina)Yeroboamu wa kwanzaMCHANGANYIKO1Wafalme 13:11-14
7. HANANIAYekonia na SedekiaWA UONGOYeremia 28:15-17
8.Manabii 400 (wasiotajwa majina)AhabuWA UONGO1Wafalme 22:6
9.BALAAMUIsraeli wakiwa JangwaniWA UONGO (Mchawi)Yoshua 13:22
10.BAR-YESUNyakati za kanisa la KwanzaWA UONGO (Mchawi)Matendo 13:9
11.AGABONyakati za kanisa la KwanzaWA KWELIMatendo 11:28 na Matendo 21:10

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

MAJINA YA MANABII WANAWAKE

MAJINA YA MITUME WA BWANA YESU

WAFALME NA MALKIA WALIOTAWALA YUDA

WAFALME WALIOTAWALA ISRAELI.

Rudi nyumbani

Print this post

MAJINA YA MANABII WANAWAKE

Orodha ya Manabii wa kike katika biblia.


Jumla ya Manabii wa kike (wanawake) waliotajwa katika biblia ni 11, Kati ya hao manabii Tisa (9) walikuwa wa KWELI na Wawili (2) walikuwa wa UONGO.

LIFUATALO NI JEDWALI LA UFUPISHO..

Kulitazama jedwali zima, basi ‘SLIDE’ kuelekea kushoto.

N/AJINAURAIAHALI ZA KIMWILIHALI YA KIROHOMAREJEO
1.MIRIAMUISRAELIDada wa Musa na HaruniWA KWELIKutoka 15:20
2.DEBORAISRAELIHaijatajwa katika BibliaWA KWELIWaamuzi 4:4
3.HULDAISRAELIMke wa ShalumuWA KWELI2Wafalme 22:14,
2Nyakati 34:22
4.MKE WA ISAYAISRAELIMke wa IsayaWA KWELIIsaya 8:3
5.ANAISRAELIMjaneWA KWELILuka 2:36
6.BINTI WA FILIPOISRAELIBinti wa FilipoWA KWELIMatendo 21:8-9
7.BINTI WA FILIPOISRAELIBinti wa FilipoWA KWELIMatendo 21:8-9
8.BINTI WA FILIPOISRAELIBinti wa FilipoWA KWELIMatendo 21:8-9
9.BINTI WA FILIPOISRAELIBinti wa FilipoWA KWELIMatendo 21:8-9
10.NOADIAISRAELI (Mlawi)HaijatajwaWA UONGONehemia 6:14, Ezra 8:33
11.YEZEBELITIRO (LEBANONI)Mke wa Mfalme AhabuWA UONGO (Mchawi)Ufunuo 2:20

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

Tembelea washirika wetu, www.swisswatch.is best replica watches – viongozi katika viatu vya mtindo!

UJUE UCHAWI WA MANABII WA UONGO?.

Wana wa Manabii walikuwa ni watu gani?

JIEPUSHE NA MANENO YA MANABII WA UONGO.

Manabii walisema “Neno la Mungu likanijia” ..Maana ya hili neno ni nini?.

Nini maana ya “Torati na manabii”?

Rudi nyumbani

Print this post

Maana ya Mithali 11:17 Mwenye rehema huitendea mema nafsi yake

Nini maana ya Mithali 11:17 inaposema;

Mwenye rehema huitendea mema nafsi yake; Aliye mkali hujisumbua mwili wake.


JIBU: Mwenye rehema ni mtu wa huruma, mwenye kusamehe, mwenye kuachilia hata kama tendo alilofanyiwa linastahili adhabu kwa yule mwingine.

Biblia inasema mtu kama huyo huipa faida nafsi yake. Huitendea mema nafsi yake. Ambayo huipata kwanza hapa hapa duniani, kwasababu Bwana alisema kipimo kile tupimacho ndicho tutakachopimiwa na watu.

Marko 4:24 Akawaambia, Angalieni msikialo; kipimo kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa, na tena mtazidishiwa.

Maana yake ni anajijengea wigo mpana wa yeye naye kukutana na rehema nyingi mbeleni.

Vilevile anapata faida katika ulimwengu ujao, Bwana  alisema..

Mathayo 5:7 Heri wenye rehema; Maana hao watapata rehema.

Lakini anasema pia, mtu mkali hujisumbua mwili wake. Mtu mkali ni kinyume cha mtu mwenye rehema, ni mtu asiye na huruma, mwenye visasi, asiyejali, mkorofi, akiudhiwa anarudisha Maudhi, akikosewa kidogo, analipiza mara mbili, maneno yake hayana staha, kugombeza wengine kwake ni jambo la kawaida n.k.

Sasa matokeo ya mtu wa namna hii ni kuadhibiwa na Mungu, aidha hapa hapa duniani, au kule aendapo.

Bwana alisema…auaye kwa upanga, atauwa kwa upanga, ukimtendea mtu kwa ukali na wewe ukali utakurudia, ukimpiga mwingine kwasababu kakuudhi kidogo, na wewe utapigwa mahali fulani kwasababu ulimuudhi mwingine.. (hicho huitwa kisasi cha Mungu).

Hivyo tendea mema nafsi yako,lakini pia mwili wako, kwa kumpenda Bwana.Na kuwa mwema.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

KUTUBU SIO KUOMBA REHEMA.(Opens in a new browser tab)

Kiti cha Rehema kilikuwaje? (Kutoka 40:20)

(Opens in a new browser tab)NJIA NYINGINE YA KUPATA REHEMA NA KIBALI KUTOKA KWA MUNGU.(Opens in a new browser tab)

Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?(Opens in a new browser tab)

Rudi nyumbani

Print this post

Fahamu Mithali 20:11 Hata mtoto hujijulisha kwa matendo yake;

SWALI: Nini maana ya Mithali 20:11 inaposema;

Hata mtoto hujijulisha kwa matendo yake; Kwamba kazi yake ni safi, kwamba ni adili.


JIBU:  Mwandishi anatuonyesha kuwa tabia ya mwanadamu yoyote, huwa haijifichi kufuatana na umri wake, kwamba yaweza kukaa ndani  tu kipindi cha utotoni isionekane ikaja kudhihirika ghafla ukubwani. Hapana, anasema “Hata mtoto hujijulisha kwa matendo yake; Kwamba kazi yake ni safi, kwamba ni adili”.

Ikiwa na maana katika utoto ule ule unaweza kuuchunguza mwenendo wa mtoto, ukautambua. Na hiyo itakupa fursa ya kuurekebisha ukiwa ni mbaya, au kuuimarisha ukiwa ni mzuri, akiwa katika vipindi kile kile. Usione mwanao anayotabia ya udokozi, ukasema huyu ni mtoto tu, haelewi anachokifanya. Hapana unapaswa umrekebishe mapema, kwasababu hicho kitu kipo ndani yake, Ukiona mtoto anapenda kutazama biblia, anapenda kukaa kanisani, anapenda kusikiliza nyimbo za injili. Usiseme, huyu ni mtoto, ukampuuzia tu, kwa kuishia  kusema ‘ubarikiwe mwanangu’ kinyume chake, mwendelezee mazingira hayo, kwasababu mwelekeo wa maisha yake, ni huko.

Ndivyo ilivyokuwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo, tabia zake zilianza kuonekana tangu utotoni, wazazi wake walimstaajabia, kumwona  katika umri ule mdogo, yupo hekaluni, amekaa na waalimu na wakuu wa dini akiwauliza maswali, Kinyume chake wazazi wake hawakumkemea, bali waliyaweka yote mioyoni mwao, na kukubali kuutambua mwelekeo wa mtoto wao.

Hii ni kufundisha nini? 

Lipo funzo la rohoni, lakini pia la mwilini.

La mwilini ni kuwa yatupaswa tuwatazame watoto, bila kupuuzia kitendo chochote wanachokidhihirisha katika umri ule wa chini. Ikiwa ni chema tukipalilie, ikiwa ni kibaya, tukikemee, na kushughulika nacho kwelikweli kabla hakijaweka mizizi. Hivyo hakuna mzazi au mlezi anaweza kusema, huyu mwanangu kabadilika tu ghafla. Ukweli ni kwamba mabadiliko yalianza kuwepo tangu zamani, isipokuwa kwa namna moja au nyingine tulipuuzia, tulipoyaona ndani yao tukadhani ni tabia za utoto tu. Wazazi wanaowajenga wanao katika maadili na vipawa tangu utotoni, ukiwatazama watoto wao wanapokuwa watu wazima, huwa wanakuwa na ufanisi na ujuzi wa hali ya juu sana, zaidi ya wale ambao watajijengea wenyewe wanapokuwa watu wazima. Hivyo mzazi jali maisha ya kiroho ya mwanao.

Vilevile rohoni, wapo ambao ni wachanga kiroho. Ikiwa na maana katika kanisa ni wale ambao wameokoka hivi karibuni. Halikadhalika hawa nao utaweza kutambua karama zao, sio mpaka wawe wakomavu kiroho. Aliye Mwinjilisti, utaona anapenda kushuhudia, lakini pia anauwezo wa kuwavuta wengine kwa Bwana.  Aliye mwalimu, utaona anapenda sana kujifunza, aliye nabii, utaona karama za maono, ndoto, huwa zinamjia mara kwa mara, hata kwa namna ambazo hazielewi elewi, mwimbaji atapenda wakati mwingi kujifunza kuimba hata kama hawezi. Hivyo, kila mmoja wetu, kitu ambacho Mungu amekiweka ndani yake, hujidhihirisha mapema sana pindi ameokoka. Sio mpaka awe amekomaa sana kiroho kama wengi wanavyodhani.

Pindi unapookoka, kipindi hicho hicho karama yako inaanza kufanya kazi, unapachopaswa tu, ni kujishughulisha na utumishi wa Bwana, ndivyo utakavyoruhusu mambo hayo kutokea kwa wepesi na urahisi zaidi?

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine

MZAZI, JALI MAISHA YA KIROHO YA MTOTO WAKO.

(TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!

Uasherati wa Kiroho maana yake nini?(Opens in a new browser tab)(Opens in a new browser tab)

MAANA WEWE, BWANA HUKUWAACHA WAKUTAFUTAO”.(Opens in a new browser tab)

Rudi nyumbani

Print this post

MAJINA YA MITUME WA BWANA YESU

Mitume wa BWANA YESU walikuwa 12, ambapo baadaye walisalia 11 baada ya YUDA ISKARIOTE, aliyemsaliti BWANA kufa kwa kujinyonga!.. Nafasi yake ilichukuliwa na MATHIYA, na hivyo kukamilisha idadi ya Mitume 12

IFUATAZO NI TAKWIMU YA MITUME WA BWANA.

Kutazama column za ziada slide jedwali lifuatalo kuelekea upande wa kushoto.

N/AJINAMajina MengineJina la MzaziMji aliotokeakazi aliyokuwa anafanyaVitabu vya biblia alivyoandikaAlivyokufa
1.SIMONI- Kefa/jiwe/Petro
Yona (Mathayo 16:17)Bethsaida ya GalilayaMVUVI2 (1Petro na 2Petro)-Kwa Kusulibiwa kichwa chini miguu juu
2.ANDREAHakunaYonaBethsaida ya GalilayaMVUVIHakuna- Kwa kusulibiwa
3.YAKOBO-BoanergeZebedayo na SalomeBethaida ya GalilayaMVUVIHakuna-Kwa kukatwa kichwa na Herode (Matendo 12:1-2)
4.YOHANA-BoanergeZebedayo na SalomeBethsaida ya GalilayaMVUVI5 (Yohana, Waraka wa Yohana na Ufunuo)- Katika uzee
5.MATHAYO-LawiAlfayo (Marko 2:14)GalilayaMTOZA USHURU1 (Mathayo)-Kwa kuchomwa Mkuki Ethiopia
6.BARTHOLOMAYO- NathanaeliHalijatajwa katika Biblia GalilayaHaijatajwa katika BibliaHakuna- Kwa kusulibiwa
7.TOMASO- PachaHalijatajwa katika BibliaGalilayaMVUVIHakuna-Kwa kuchomwa Mkuki, India
8.FILIPOHakunaHalijatajwa katika BibliaGalilayaHaijatajwa katika BibliaHakuna- Kwa kusulibiwa
9.YAKOBO- Yakobo mdogoAlfayoGalilayaHaijatajwa katika BibliaHakuna-Kwa kupigwa Mawe
10SIMONI- ZeloteHalijatajwa katika BibliaKana ya GalilayaHaijatajwa katika BibliaHakuna- Kwa kusulibishwa
11.THADAYO- YudaYakoboGalilayaHaijatajwa katika BibliaHakuna-Kwa kupigwa Mawe
12.YUDA-IskarioteSimoniKeriothiHaijatajwa katika BibliaHakuna- Kwa kujinyonga
13.MATHIYAHakunaHalijatajwa katika BibliaHaujatajwaHaijatajwa katika BibliaHakuna-Kwa kukatwa kichwa

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

Rudi nyumbani

Print this post

WAFALME WALIOTAWALA ISRAELI.

Wafalme waliotawala ISRAELI, ukiwatoa wale watatu wa Mwanzo (Yaani Sauli, Daudi na Sulemani) walikuwa ni Wafalme 19 tu, na hakukuwa na Malkia aliyetawala Israeli kama ilivyokuwa kwa YUDA.

Kati ya Wafalme hao 19 waliotawala Israeli, hakuna hata mmoja aliyekuwa Mkamilifu mbele za MUNGU katika ukamilifu wote kama ilivyokuwa kwa baadhi ya Wafalme waliotawala YUDA. Isipokuwa Mfalme mmoja tu aliyeitwa YEHU ndiye angalau alionekana kufanya Mema lakini pia alifanya na Mabaya.

UFUATAO NI UFUPISHO KWA NJIA YA TAKWIMU.

JINAMIAKA ALIYOTAWALAMATENDOMAREJEO
1.YEROBOAMU22MABAYA1Wafalme 12:25-33
2.NADABU2MABAYA1Wafalme 15:25-31
3.BAASHA24MABAYA1Wafalme 15:33-16:7
4.ELA 2MABAYA1Wafalme 16:8-14
5.ZIMRI7MABAYA1Wafalme 16:15-20
6.OMRI12MABAYA1Wafalme 16:21-27
7.AHABU22MABAYA1Wafalme 16:29-33
8.AHAZIA2MABAYA1Wafalme 22:51-53
9.YORAMU12MABAYA2 Wafalme 1:17, 3:1-3
10.YEHU28Nusu Mema-
Nusu Mabaya
2 Wafalme 9:30, 10:36
11.YEHOAHAZI17MABAYA2 Wafalme 13:1-9
12.YEHOASHI16MABAYA2 Wafalme 13: 10-25
13.YEROBOAMU II41MABAYA2 Wafalme 14:23-29
14.ZEKARIA6MABAYA2 Wafalme 15:8-12
15.SHALUMUMwezi 1MABAYA2 Wafalme 15:13-16
16.MENAHEMU10MABAYA2 Wafalme 15:17-22
17.PEKAHIA2MABAYA2 Wafalme 15:23-26
18.PEKA20MABAYA2 Wafalme 15:27-31
19.HOSHEA9MABAYA2 Wafalme 17:1-7

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

Rudi nyumbani

Print this post

WAFALME NA MALKIA WALIOTAWALA YUDA

Wafalme waliotawala YUDA ni 19, na Malkia aliyetawala YUDA ni Mmoja (1), hivyo kufanya jumla ya Watawala 20 kupita katika Taifa la Yuda.

Kati ya hao Wafalme 19; waliofanya MEMA ni Wafalme saba (7) tu, wengine 12 waliosalia walifanya Mabaya. Na Malkia Mmoja aliyetawala naye pia alifanya Mabaya, hivyo kufanya jumla ya watawala 13 waliofanya mabaya.

UFUATAO NI UFUPISHO KWA NJIA YA TAKWIMU.

Tafuta jina la Mfalme hapa >>

N/AJINAJINSIAMIAKA ALIYOTAWALAMATENDOMAREJEO
1.REHOBOAMUM17MABAYA1Wafalme 11:42
2.ABIYAM3MABAYA1Wafalme 14:31-15:8
3.ASAM41MEMA 1Wafalme 15:8-24
4.YEHOSHAFATIM25MEMA1Wafalme 22:41-51
5.YEHORAMUM8MABAYA2Wafalme 8:16-24
6.AHAZIAM1 MABAYA2Wafalme 8:24-29
7.ATHALIAK6MABAYA2Wafalme 8:26, 11:1-20
8.YOASHIM40MEMA2Wafalme 11:21,12:1-21
9.AMAZIAM29MEMA2Wafalme 14:1-22
10.UZIAM52Mwanzo Mema-Mwisho-Mabaya2Wafalme 15:1-7
11.YOTHAMUM16MEMA2Wafalme 15:32-38
12.AHAZIM16MABAYA2Wafalme 15:38-16:20
13.HEZEKIAM29MEMA2Wafalme 18:1-20
14.MANASEM55MABAYA2Wafalme 21:1-18
15.AMONI M2MABAYA2Wafalme 21:18-26
16.YOSIAM31MEMA2Wafalme 21:26-23:30
17.YEHOAHAZIMMiezi 3MABAYA2Wafalme 23:30-34
18.YEHOYAKIMUM11MABAYA2Wafalme 23:34- 24:6
19.YEKONIA/
YEHOYAKINI
MMiezi 3MABAYA2Wafalme 24:6-17
20.SEDEKIAM11MABAYA2Wafalme 15:24:17-25:30

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengineyo:

Rudi nyumbani

Print this post

Ni kwa namna gani, haki yetu inapaswa izidi ya mafarisayo?

Bwana alimaanisha nini katika Mathayo 5:20 aliposema..

[20]Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni. 

Ni haki ipi hiyo.

JIBU: Katika andiko hilo tunaona Bwana akiainisha kigezo cha mtu kuingia kwenye ufalme wa Mungu..kwamba kigezo chenyewe ni “HAKI” …

Haki ni kitu kinachomstahilisha mtu kupokea kitu fulani. Kwamfano tunasema mtoto ana haki ya kulindwa…ikiwa na maana kilichomsababishia apate haki ya kulindwa ni ile hali ya utoto wake.

Mfano mwingine, tunasema ni mtu mzima ana haki ya kuoa au kuolewa na mtu amtakaye, katika wakati auchaguaye yeye. Tafsiri yake ni kwamba kinachompa haki ya kuwa hivyo ni kwasababu yeye ni “mtu-mzima”. Angekuwa mtoto asingekuwa na haki hiyo.

Sasa tukirudi katika habari hiyo tunaona kilichowafanya waandishi na mafarisayo wajihesabie haki kwamba wao ni warithi wa ufalme wa mbinguni. Ilikuwa ni kuitimiza sheria kwa matendo yao. Ambayo kimsingi wao wenyewe hawakuweza kuishika..kwa nje walionekana sawa lakini ndani walikuwa mbali na sheria yao. Kwasababu hakuwahi kutokea mtu hata mmoja aliyeweza kumpendeza Mungu kwa matendo yake, yeye mwenyewe.

Hivyo njia yao ya kupata haki, ambayo ni kwa matendo ya sheria haikuwa sawa. Ndipo Yesu akawaambia wanafunzi wake na wale waliomsikia kwamba haki “ yao” isipozidi ya mafarisayo na waandishi kamwe hawataweza kuuingia ufalme wa mbinguni.

Swali je ya kwao inapaswa iweje. Je ya matendo ya sheria zaidi ya yale au vinginevyo?

Haki Yesu aliyoileta ambayo itampelekea mtu kurithi uzima wa milele ni kwa njia yake yeye mwenyewe .Ambayo sisi tunahesabiwa haki kwa kumwamini, kama mwokozi wa maisha yetu. Bila kutegemea matendo yetu ya haki. Yaani ni haki tuipatayo kwa neema.

Hivyo, wote wanaoipokea haki hiyo basi uzima wa milele ni wao. Na kwasababu ndio njia ambayo sisi tutamfikia Mungu. Basi neema yenyewe inatufundisha pia kuyazaa matunda ya Roho. Na hivyo tunaitimiza sheria ya Mungu mioyoni mwetu bila unafiki. Mbali na mafarisayo ambao walitegemea akili zako na nguvu zao.

Hata sasa ikiwa unategemea jitihada zako, zikupe haki mbele za Mungu, ndugu umepotea. Hutaweza Itegemee neema ya Mungu. Na hiyo itakusaidia kuyatimiza hayo mengine kwa Roho Mtakatifu.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

TUNAHESABIWA HAKI BURE KWA NJIA YA IMANI.

FUNDISHO KUU LA NEEMA YA MUNGU KWETU.

Nini maana ya kumsulibisha mwana wa Mungu mara ya pili?

Rudi nyumbani

Print this post

BARAKA ZA WAZAZI KWA WATOTO.

Masomo maalumu kwa wazazi/walezi.

Je unazijua kanuni za kuwabariki watoto wako?.. Wengi tunaijua kanuni moja tu ya kuwatamkia Baraka!..Hiyo ni sahihi kabisa na ipo kibiblia..(kwasababu maneno ya kinywa yana nguvu).

Lakini ni vizuri kufahamu jambo moja, kama Maneno yako hayataambatana na matendo yako, uwezekano wa hayo uliyoyasema kutokea bado utakuwa ni mdogo sana.

Kama unataka mtoto wako apate Baraka zote ulizozitamka juu yake, (na kwa njia ya maombi) ikiwemo Baraka katika kumjua Mungu, kuwa na afya na mafanikio, basi ongezea yafuatayo..

   1.MFUNDISHE SHERIA ZA MUNGU.

Wafundishe watoto wako sheria za Mungu, huku wewe mwenyewe ukiwa kielelezo cha kuzifanya, ili wasione kama ni sheria tu za MUNGU bali hata zako wewe mzazi!.. Mtoto wako anapaswa azione sheria za Mungu kama ni za kwako wewe. Lakini asipoona wewe mwenyewe ukizifanya hata yeye hataweza kukusikiliza wala kuzitenda, hata kama kwa mdomo atakuitikia.

Mithali 1:8 “Mwanangu, yasikilize mafundisho ya baba yako, Wala usiiache sheria ya mama yako,

9 Kwa maana hayo yatakuwa kilemba cha neema kichwani pako, Na mikufu shingoni mwako”.

   2. USIMNYIME MAPIGO.

Yapo makosa yanayoweza kurekebishwa kwa maneno peke yake na mtoto akajengeka na kubadilika, lakini yapo yanayohitaji kurekebishwa kwa maneno pamoja na kiboko, hususani yale ya kujirudia rudia tena ya makusudi.

Biblia inasema ukimpiga hatakufa bali utakuwa umemwokoa roho yake na kuzimu.. (Hapo utakuwa umembariki pakubwa Zaidi ya kumtamkia tu baraka za maneno halafu hufanyi chochote).

Mithali 23:13 “Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.

14 Utampiga kwa fimbo, Na kumwokoa nafsi yake na Kuzimu”.

   3. MFUNDISHE KUSHIKA ELIMU

Badala ya kumtakia tu Baraka kwa kinywa (au kumwombea tu katika chumba chako cha ndani), tenga muda wa kumfundisha Umuhimu wa Elimu (kwanza ya Mungu) na pili ya dunia… Hapo utakuwa umembariki kwa vitendo na si mdomo tu.

Mithali 4:13 “Mkamate sana elimu, usimwache aende zake; Mshike, maana yeye ni uzima wako”

    4. MFUNDISHE KUSHIKA SHERIA ZA NCHI na KUWAHESHIMU WENYE MAMLAKA (Wafalme).

Badala ya kumtamkia tu mafanikio, na kumwombea.. tenga muda kumfundisha umuhimu wa kuwatii wenye mamlaka na kuzingatia sheria ya nchi, hiyo itakuwa Baraka kwake katika siku zijazo za maisha yake.

Mithali 24:21 “Mwanangu, mche Bwana, NA MFALME; Wala usishirikiane na wenye kigeugeu;

    5. MFUNDISHE KATIKA NJIA INAYOMPASA

Ni njia gani inampasa katika umri wake na jinsia yake?.. Je! Katika umri wake huo anapaswa amiliki simu??..je katika umri wake anapaswa asemeshwe maneno hayo unayomsemesha?..je katika umri wake anapaswa atazame hayo anayoyatazama katika TV?.. je katika umri wake huo anapaswa awepo hapo alipo?..anapaswa afanye hicho anachokifanya?.Je! Kwa jinsia yake anapaswa kuvaa hayo mavazi unayomvika??..

Ni muhimu sana kujua mambo yampasayo mwanao/wanao kwa rika walilopo na jinsia zao…

Mithali 22:6 “Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee”

Ukiyafanya hayo na mengine kama hayo pamoja na MAOMBI umwombeayo kila siku, basi utakuwa umembariki mwanao/wanao  kweli kweli.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

JE! UMEYABATILISHA MAMBO YA KITOTO?

FIMBO YA HARUNI!

MANENO YA MUNGU YANAPINDULIWAJE?

NINI TOFAUTI KATI YA MATENDO YA SHERIA NA MATENDO YA IMANI?

MAOMBI YA KUOMBEA WATOTO.

Rudi nyumbani

Print this post