Maana ya Mithali 11:17 Mwenye rehema huitendea mema nafsi yake

Maana ya Mithali 11:17 Mwenye rehema huitendea mema nafsi yake

Nini maana ya Mithali 11:17 inaposema;

Mwenye rehema huitendea mema nafsi yake; Aliye mkali hujisumbua mwili wake.


JIBU: Mwenye rehema ni mtu wa huruma, mwenye kusamehe, mwenye kuachilia hata kama tendo alilofanyiwa linastahili adhabu kwa yule mwingine.

Biblia inasema mtu kama huyo huipa faida nafsi yake. Huitendea mema nafsi yake. Ambayo huipata kwanza hapa hapa duniani, kwasababu Bwana alisema kipimo kile tupimacho ndicho tutakachopimiwa na watu.

Marko 4:24 Akawaambia, Angalieni msikialo; kipimo kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa, na tena mtazidishiwa.

Maana yake ni anajijengea wigo mpana wa yeye naye kukutana na rehema nyingi mbeleni.

Vilevile anapata faida katika ulimwengu ujao, Bwana  alisema..

Mathayo 5:7 Heri wenye rehema; Maana hao watapata rehema.

Lakini anasema pia, mtu mkali hujisumbua mwili wake. Mtu mkali ni kinyume cha mtu mwenye rehema, ni mtu asiye na huruma, mwenye visasi, asiyejali, mkorofi, akiudhiwa anarudisha Maudhi, akikosewa kidogo, analipiza mara mbili, maneno yake hayana staha, kugombeza wengine kwake ni jambo la kawaida n.k.

Sasa matokeo ya mtu wa namna hii ni kuadhibiwa na Mungu, aidha hapa hapa duniani, au kule aendapo.

Bwana alisema…auaye kwa upanga, atauwa kwa upanga, ukimtendea mtu kwa ukali na wewe ukali utakurudia, ukimpiga mwingine kwasababu kakuudhi kidogo, na wewe utapigwa mahali fulani kwasababu ulimuudhi mwingine.. (hicho huitwa kisasi cha Mungu).

Hivyo tendea mema nafsi yako,lakini pia mwili wako, kwa kumpenda Bwana.Na kuwa mwema.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

KUTUBU SIO KUOMBA REHEMA.(Opens in a new browser tab)

Kiti cha Rehema kilikuwaje? (Kutoka 40:20)

(Opens in a new browser tab)NJIA NYINGINE YA KUPATA REHEMA NA KIBALI KUTOKA KWA MUNGU.(Opens in a new browser tab)

Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?(Opens in a new browser tab)

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments