Kudhihaki kibiblia ni kitendo cha kumbeza au kumkejeli mtu, shetani au Mungu, (maana yake kumfanya yule mtu aonekane hana heshima, au hana maana), dhihaka pia anaambatana na dharau, utani na hata matusi.
Katika Biblia tunaona kuna watu waliwadhihaki wanadamu wenzao, na wengine walimdhihaki ibilisi na ufalme wake, na wako waliojaribu kumdhihaki Mungu wa mbingu na nchi,..kwa ufupi tuitazame mifano hiyo.
1. DHIHAKA KWA MWANADAMU.
Dhihaka ya Ishmaeli kwa Sara.
Tunasoma kipindi Hajiri amempata Ishmaeli kwa Abrahamu, mtoto Ishmaeli alianza kumfanyia dhihaka mamaye mkubwa Sara, na matokeo yako ni kufukuzwa yeye pamoja na mama yake..
Mwanzo 21:9 “Sara akamwona yule mwana wa Hajiri Mmisri, ambaye alimzalia Ibrahimu, anafanya dhihaka.
10 Kwa hiyo akamwambia Ibrahimu, Mfukuze mjakazi huyu na mwanawe, maana mwana wa mjakazi hatarithi pamoja na mwanangu, Isaka”.
Utasoma pia dhihaka za watu kwa watumishi wa Mungu katika 2Nyakati 36:16, Nehemia 4:1, Na pia sehemu nyingine utaona Mungu anawafanyia dhihaka wanadamu wanaoenda kinyume na shauri lake (Soma Zab 2:4 na Zab 59:8).
2. DHIHAKA KWA SHETANI NA UFALME WAKE.
Kuna wakati Nabii Eliya alimdhihaki mungu-baali pamoja na makuhani wake.
1Wafalme 18:27 “Ikawa, wakati wa adhuhuri, Eliya akawafanyia dhihaka, akasema, Mwiteni kwa sauti kuu; maana ni mungu huyo; labda anazungumza, au ana shughuli, au anasafiri, au labda amelala, sharti aamshwe.
28 Wakapiga kelele, wakajikata-kata kwa visu na vyembe kama ilivyo desturi yao, hata damu ikawachuruzika”.
3. DHIHAKA YA WANADAMU KWA MUNGU.
Hakuna mahali popote mwanadamu amefanikiwa kumdhihaki Mungu, kwasababu Mungu hadhihakiwi..
Wagalatia 6:7 “Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.
8 Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele”.
Wapo waliojaribu kumdhihaki Mungu katika biblia lakini walikuja kujua baadaye kuwa Mungu hadhihakiwi.. Mfano wa hao, ni wale watumwa wa mfalme wa Shamu waliomdhihaki Mungu kwa kusema ana uwezo wa kuokoa tu milimani na si nchi tambarare, na matokeo yake waliziona kazi zake.
1Wafalme 20:23 “Basi watumwa wake mfalme wa Shamu wakamwambia, Mungu wao ni mungu wa milima; ndiyo sababu ya kutushinda sisi; lakini na tupigane nao katika nchi tambarare, na hakika tutawashinda wao.
24 Ufanye neno hili; uwaondoe hao wafalme, kila mtu atoke mahali pake, ukaweke majemadari mahali pao.
25 Kisha ujihesabie jeshi, kama jeshi lililokupotea, farasi kwa farasi na gari kwa gari; nasi tutapigana nao katika nchi tambarare, na bila shaka tutawashinda. Akaisikiliza sauti yao, akafanya kama hivyo.
26 Basi ikawa mwakani, Ben-hadadi akawahesabu Washami, akakwea mpaka Afeki ili apigane na Israeli.
27 Wana wa Israeli nao wakahesabiwa, wakapewa vyakula, wakaenda kupigana nao; wakatua wana wa Israeli mbele yao kama vikundi viwili vya wana-mbuzi; bali Washami wakaijaza nchi.
28 Akaja yule mtu wa Mungu, akamwambia mfalme wa Israeli, akasema, Bwana asema hivi, Kwa sababu Washami wamesema, Bwana ni Mungu wa milima wala si Mungu wa nchi tambarare; basi nitawatia makutano haya yote walio wengi mkononi mwako, nanyi mtajua ya kuwa ndimi Bwana.
29 Wakatua kuelekeana muda wa siku saba. Ikawa siku ya saba vikapangwa vita; wana wa Israeli wakawapiga miongoni mwa Washami siku moja watu mia elfu waendao kwa miguu.
30 Lakini waliosalia wakakimbia mpaka Afeki, mjini; na ukuta ukaanguka juu ya watu ishirini na saba elfu waliosalia. Ben-hadadi naye akakimbia, akaingia mjini, katika chumba cha ndani”.
Kwahiyo Mungu hadhihakiwi wala hajaribiwi wala hapimwi, wana wa Israeli jangwani walijaribu kumpima na maandiko yanasema wakayaona matendo yake..
Zaburi 95:8 “Msifanye migumu mioyo yenu; Kama vile huko Meriba Kama siku ya Masa jangwani.
9 Hapo waliponijaribu baba zenu, Wakanipima, wakayaona matendo yangu.
10 Miaka arobaini nalihuzunika na kizazi kile, Nikasema, Hao ni watu waliopotoka mioyo, Hawakuzijua njia zangu.
11 Nikaapa kwa hasira yangu Wasiingie rahani mwangu”.
Kwa hitimisho hatupaswi kudhihakiana sisi kwa sisi, wala kuwadhihaki watumishi wa Mungu, wala tusijaribu kumdhihaki MUNGU wa mbingu na nchi kwani yeye hadhihakiwi, lakini tunaweza kudhubutu kumdhihaki shetani na majeshi yake, kwa lengo la kumpa Mungu utukufu, na si kujiinua sisi, ikiwa tumesimama vyema na MUNGU, lakini kama hatujasimama vyema na Mungu, kumdhihaki shetani ni hatari, na kuleta matokeo kama yale yaliyowateka wana wa Skewa (Soma Matendo 19:13-17).
Pia kama umeokoka Biblia imesema tutapitia vipindi vya dhihaka tu (soma) kama Bwana wetu YESU KRISTO pamoja na wanafunzi wake alidhihakiwa sisi ni akina nani? (soma Luka 22:63, Matendo 2:13 na Waebrania 11:36) lakini yote katika yote tunafundishwa kusamehe, na kuvumilia, kwasababu siku za mwisho ilishatabiriwa kuwa watakuja watu wa kudhihaki wengi (Soma 2Petro 3:3 na Yuda 1:18)
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
HASIRA YA MUNGU KUKUWAKIA, KWA KUTOMZUNGUZIA TU MUNGU IPASAVYO.
NI NANI ALIYEWAONYA KUIKIMBIA HASIRA ITAKAYOKUJA?
Je Daudi aliwachukia viwete na vipofu? (2Samweli 5:6-9)
SWALI: Silaha za Nuru ni zipi?
Warumi 13:12 Usiku umeendelea sana, mchana umekaribia, basi na tuyavue matendo ya giza, na kuzivaa silaha za nuru
JIBU: Ni lazima tufahamu ulimwengu wa roho upo katika pande mbili,
Upande wa Nuru ni wa Kristo (Yohana 1:4-5), na upande wa giza ni wa ibilisi.
Na pande hizi hazijawahi kupatana hata kidogo, na kama hazijawahi kupatana maana yake zipo vitani na kama zipo vitani basi zote zina silaha zake, kuhakikisha zinajilinda, lakini pia kushambulia, ili kuua utawala mwingine. Ndio hapo kwanini tunaambiwa tuzivae silaha za nuru. Maana yake mtu anaweza akawa ni wa nuru lakini akawa hana/hajui kuzitumia silaha za Nuru.
Vifungu vifuatavyo ni kututhibitishia kuwa Nuru na giza vipo katika mapambano;
2Wakorintho 6:14 Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?
Wakolosai 1:12 mkimshukuru Baba, aliyewastahilisha kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu katika nuru.
13 Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake
Sasa silaha za Nuru ambazo mtu akiwa nazo ataweza kujilinda na mashambulizi ya giza, lakini pia ataweza kuushinda ufalme wa giza ni hizi;
Silaha hizi, ndio zile zinazotajwa pia kwenye Waefeso 6:10-18, kama silaha za haki.
Kwa maelezo marefu juu ya silaha hizi, fungua hapa usome >>> Nini maana ya Dirii, Chapeo na Utayari?
Mtu akiwa na mambo haya, ataweza kulishinda Giza, kotekote.. Ambalo, silaha zake ni kama zifuatazo;
Swali ni Je! Umejivika silaha Nuru ?
Ikiwa upo nje ya Kristo, huwezi kusimama, unahitaji wokovu kwanza, ikiwa upo tayari kufanya hivyo wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Silaha za Mkono wa kuume na za mkono wa kushoto ni zipi
Je mapepo yanakufa? Na kama hayafi, tunashindanaje vita vya kiroho?
NGUVU YA “KUKATAA” UNAPOPAMBANA VITA VYA KIROHO
Mfalme mmoja wa Israeli aliyeitwa Yoashiliingiwa na wazo la kutaka kuikarabati nyumba ya Mungu (Hekalu), na kuamsha tena shughuli za kiibada zilizokuwa zimeharibiwa Na watawala wabovu waliotangulia..
Hivyo kwa kuwa alijua ukarabati unahitaji fedha, alichukua hatua ya kuwatoza watu kodi ya nyumba ya Mungu..Ambayo iliagizwa katika torati na Musa..(2Nyakati 24:9)
Hivyo akawateuwa Walawi, walisimamie jambo hilo tangu mwanzo hadi mwisho, lakini likawa kama linacheleweshwa…
Mpaka baadaye akawauliza tena, kwanini kazi inacheleweshwa, kwa kuona hakuna chochote kilichofanyika..
Lakini mfalme akaja na mkakati mwingine, ili shughuli hiyo ifanyike kwa haraka na wakati, akaona kuliko Kuwalazimisha watu kulipa kodi ngoja aweke sanduku kubwa katika lango la hekalu na kupiga panda kwa watu wote wa Yuda waje kumtolea Mungu wao kwa hiari, bila shuruti..
Na wazo lile likapendwa na watu wengi, na hatma yake makusanyo yakawa mengi, kila siku mpaka wakapata fedha za kuwaajiri wajenzi ili kulikarabati hekalu, na kutengeneza vyombo vya nyumba ya Mungu.
2 Mambo ya Nyakati 24:6-14
[6]Mfalme akamwita Yehoyada mkuu wao, akamwambia, Mbona hukuwataka Walawi waitoze Yuda na Yerusalemu kodi ya Musa mtumishi wa BWANA, na ya kusanyiko la Israeli, kwa ajili ya hema ya ushuhuda?
[7]Kwa kuwa wana wa Athalia, yule mwanamke mwovu, walikuwa wameibomoa nyumba ya Mungu; na vitakatifu vyote vya nyumba ya BWANA wamewapatia mabaali.
[8]Basi mfalme akaamuru, nao wakafanyiza kasha, wakaliweka nje langoni pa nyumba ya BWANA.
[9]Wakapiga mbiu katika Yuda na Yerusalemu, kumletea BWANA kodi aliyoiweka Musa mtumishi wa Mungu, juu ya Israeli jangwani.
[10]Wakafurahi maakida wote na watu wote, wakaleta na kutia ndani ya kasha, hata wakaisha.
[11]Ikawa wakati walipoletewa kasha wasimamizi wa mfalme kwa mkono wa Walawi, nao wakaona ya kwamba kuna fedha nyingi, huja karani wa mfalme, na msimamizi wake kuhani mkuu, wakatoa yaliyomo kashani, kisha hulichukua kasha, na kulirudisha mahali pake. Ndivyo walivyofanya siku kwa siku, wakakusanya fedha tele.
[12]Na mfalme na Yehoyada waliwapa hao waliofanya kazi ya utumishi wa nyumba ya BWANA; nao wakawaajiri waashi na maseremala ili kuitengeza nyumba ya BWANA, na hao pia wafuao chuma na shaba ili kuitengeza nyumba ya BWANA.
[13]Hivyo mafundi wakafanya kazi yao, nao wakaimaliza, wakaisimamisha nyumba ya Mungu kama ilivyopasa, wakaifanya imara.
[14]Nao walipokwisha, wakaleta mbele ya mfalme na Yehoyada fedha iliyobaki, vikafanyizwa kwayo vyombo vya nyumba ya BWANA, vyombo vya utumishi, navyo vya kutolea, na miiko, na vyombo vya dhahabu na fedha. Wakatoa sadaka za kuteketezwa katika nyumba ya BWANA, daima, siku zote za Yehoyada.
Utoaji wenye baraka na anaouhitaji Mungu ni ule wa hiyari na sio wa kulazimishwa…kama kanisa la Kristo Lazima tufikie hatua hii, kwamba viongozi hawawashurutishi watu kutoa mchango,mfano Zaka, Kama vile himizo la kodi, kwamba usipotoa unachukuliwa sheria ya kinidhamu …lakini pia watu nao wanawajibika wenyewe kumtolea Mungu kwa uaminifu na moyo..kanisa lifikiapo hatua hii ya kiroho, Mungu huliongezea baraka sana.
Usikubali kukumbushwa-kumbushwa, au kuhimizwa-himizwa kumtolea Mungu, Bali mtolee Mungu zaka zako, sadaka zako, kwa moyo wa furaha, Bwana atakubariki.
2 Wakorintho 9:6-8
[6]Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu.
[7]Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.
[8]Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema;
Bwana awabariki..
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
SWALI: Yuda alimaanisha nini kusema “wokovu ambao ni wetu sisi sote”
Yuda 1:3
[3]Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu.
JIBU: Mwanzo mwa waraka huu, mtume Yuda anaanza kwa kusema maneno hayo “Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote”
Aliowaandikia waraka huu ni watu wote waliomwamini Yesu, (yaani waliookoka) kwamba wokovu huo ni wao Wote.
Anaandika maneno hayo pengine kutokana na dhana iliyokuwepo ya watu kufikiri kuwa wokovu ni wa jamii ya watu fulani tu.. pengine wayahudi, au waliotahiriwa, au mabwana tu..Hapana
Bali Kristo alikivunja kiambazi chote, ili watu wote wastahili kushirikia neema yake sawasawa.
Wagalatia 3:26-28
[26]Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu.
[27]Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo.
[28]Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu.
Jambo hilo kwa mwanzoni lilikuwa ni gumu kupokelewa hata na baadhi ya watakatifu wa Yerusalemu. Utakumbuka walipomwona Petro ametumwa na Roho Mtakatifu kwenda nyumbani mwa Kornelio mtu wa mataifa bado ilikuwa ngumu kupokelewa na wao…kwasababu imani na dini zote walizozijua tangu zamani, zote zilikuwa ni za kitabaka, kibaguzi, kitaifa n.k..na sio za kila mtu.
Kitendo cha Yesu kuwaambia kahubirini habari njema za ufalme kwa mataifa yote, bila kujali lugha, cheo au jinsia hawakuelewa vema..ndio maana siku ile ya pentekoste walikuwepo watu wengi wamekusanyika watu wa kila taifa chini ya jua. Na wote wakajazwa Roho Mtakatifu.(Matendo 2)
Hivyo ujumbe huu ni lazima ukae mioyoni mwetu hata sasa ili tusiwe Na ubaguzi katika kuwavuta watu kwa Kristo, au tusionyeshe upendeleo kwa kundi fulani tu la watu, Mungu hapokei uso wa mwanadamu.. linapokuja suala la wokovu na mema yote ndani yake watu wote wamestahili na ni sawasawa machoni pake, kushiriki vipawa vyote vya Mungu.
Mwingine atasema, huwezi kumjua Mungu mpaka uwe chini ya nabii au kuhani fulani, hilo si sawa..
Lakini jambo lingine la kujifunza ni kuwa ijapokuwa ni wetu sote anasema tuishindanie imani.. kwasababu adui naye yupo kazini kutaka kuwang’oa watu wa Mungu kwenye mstari wa imani ya kweli, na kuwafanya waangukie imani danganyifu, zilizoletwa na watu wanaojiingiza Kwa siri ndani ya kanisa..
Hivyo anaeleza mkristo ni wajibu wake, kuilinda imani yake, kwa kuendelea kudumu katika kuomba, upendo, na kujifunza vigezi halisi vya neema ya Mungu, ili asiigeuze kuwa ndio chanzo cha kuishi kwenye dhambi na uovu.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
SWALI: Katika sehemu nyingi kwenye maandiko tunaona, Mungu akiwaagiza watu wake Wamsifu au wamwabudu katika uzuri wa utakatifu, nini maana ya uzuri wa utakatifu?
1 Mambo ya Nyakati 16:29
[29]Mpeni BWANA utukufu wa jina lake; Leteni sadaka, mje mbele zake; Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utakatifu;
Zaburi 29:2
[2]Mpeni BWANA utukufu wa jina lake; Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utautakatifu.
Soma pia..
Zaburi 96:9, 2Nyakati 20:21
JIBU: Kuna mambo mawili hapo.
Jambo la kwanza ni “Uzuri” na jambo la pili ni “utakatifu”
Hasemi tumwabudu Bwana katika utakatifu…hapana bali anasema tumwabudu Bwana katika uzuri wa utakatifu..
Kwa namna nyingine anamaanisha hivi; tuuone uzuri ulio katika utakatifu ndio tumwabudu yeye Katika huo.
Tunaweza tukaujua utakatifu…ambao mfano wake ni kama vile maisha ya upendo, haki, usafi, adabu, amani, utu wema. n.k. Lakini tusione uzuri wa mambo kama hayo mioyoni mwetu au maishani mwetu…wengine wanaona kama utakatifu wa Mungu ni kitu cha kutisha, lakini kumbe Sio..
Siku tukiona uzuri wake ndio hatutakuwa na unafki pale tunapoambiwa tufanye jambo lolote katika utakatifu..
Kwasababu tusipoona hilo, hatma yake huwa ni kutimiza ibada kama tu agizo fulani au utaratibu wa kidini au nidhamu fulani lakini sio katika furaha na faida tuipatayo katika huo utakatifu.
Kwamfano Ibada tu yenyewe ni tendo takatifu lakini je tunaifurahia ibada na kujiona tunanufaika sana mioyoni mwetu katika hizo au tunamtimizia Mungu tu haki yake ya kuabudiwa, lakini hakuna chochote kitufurahishacho ndani yake?
Ibada ifanywayo katika uzuri wa utakatifu ni lazima itaambatana na sifa hizi;
Itakuwa Katika Roho na kweli (Yohana 4:24)
Itafanywa Katika Moyo mweupe( Zaburi 24:3-4). Mfano kusamehe, na amani moyoni.
Itajaa shukrani na kumfurahia Mungu:
Zaburi 139:14
[14]Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa
Kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu,
Itamwadhimisha Mungu na kumfurahia sana, kwa maajabu yake na matendo yake makuu, kwa viwango visivyo vya kawaida
Itaambatana na maisha ya utakatifu:
Warumi 12:1
[1]Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.
Maisha yetu ni ibada tosha, mwonekano wako, uvaaji wako, usemi wako, tabia yako, vitaakisi utakatifu wa Kristo.
Je umeuona uzuri wa Mungu, uzuri wa ibada, uzuri wa kukusanyika, uzuri wa uumbaji wake, ambavyo ndio uzuri wa utakatifu? Kama ni ndio basi utamsifu na kumwabudu pia katika tabia zake.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Nini maana ya kumwabudu Mungu katika Roho na kweli?
Ibada ni nini,Na je ili ikamilike inapaswa iwe na nini na nini?
DHABIHU ZA ROHO NI ZIPI? (1Petro 2:5)
SWALI: Nini maana ya “kupelekea mkono” kama ilivyotumika kwenye maandiko. Esta 2:21
Esta 2:21
[21]Ikawa siku zile, Mordekai alipokuwa akiketi mlangoni pa mfalme, wawili katika wasimamizi wake mfalme, Bigthana na Tereshi, wangoje mlango, walighadhibika, wakataka kumpelekea mikono mfalme Ahasuero.
JIBU:
Kupeleka Mkono, ni neno linalomaanisha “kutaka kudhuru”. Kwamfano katika hiyo habari tunaona Mordekai kama msimamizi wa malangoni pa mfalme aligundua njama za watumishi wenzake wengine ambao walitaka kwenda kumuua mfalme..hatujua aidha kwa kumwekea sumu, au kumchoma upanga, au hatua nyingine yoyote ilitayo madhara.
Kitendo hicho kibiblia, huitwa “kupeleka mkono”
Tunaweza kuona jambo lingine kama hilo, wakati fulani Daudi alimkaribia sana mfalme kwa kiwango ambacho angeweza kumuangamiza kama angetaka..lakini akasema nisinyoshe mkono wangu kwa masihi wa Bwana. Maana yake nisimuue.
1 Samweli 24:4-7
[4]Nao watu wa Daudi wakamwambia, Tazama, hii ndiyo siku ile aliyokuambia BWANA, Angalia, nitamtia adui yako mikononi mwako, nawe utamtenda yo yote utakayoona kuwa mema. Basi Daudi akainuka, akaukata upindo wa vazi lake Sauli kwa siri.
[5]Lakini halafu, moyo wake Daudi ukamchoma, kwa sababu amekata upindo wa vazi lake Sauli.
[6]Akawaambia watu wake, Hasha! Nisimtendee bwana wangu, masihi wa BWANA, neno hili, kuunyosha mkono wangu juu yake, kwa maana yeye ni masihi wa BWANA.
[7]Basi Daudi akawazuia watu wake kwa maneno hayo, asiwaache kumwondokea Sauli. Kisha Sauli akatoka pangoni, akaenda zake.
Bwana akubariki..
Je umempokea Kristo kama Bwana na mwokozi wa maisha yako?
Ikiwa upo tayari kufanya hivyo leo.. basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo mwisho wa makala hii.. Pia kufahamu tafsiri ya maneno mengine ya kibiblia tazama chini.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Uchambuzi wa kitabu cha kwanza cha Paulo kwa Timotheo (1Timotheo)
Kutia mkono chini ya paja kama ishara ya kiapo, kulimaanisha nini?
Mapokeo ni mafundisho, mifumo au taratibu zisizokuwepo ndani ya Biblia zilizotengenezwa na watu na kurithishwa kutoka kizazi hata kizazi.
Yapo mapokeo yaliyo mema na yaliyo hatari kwa Imani.. Mfano ya mapokeo mazuri yasiyo na madhara katika imani kama endapo yakifanyika kwa ufunuo ni pokeo ya kuadhimisha siku ya kufufuka kwa Bwana Yesu.. katika Biblia hakuna agizo la kuadhimisha siku ya kufufuka kwa Bwana, hivyo mtu asiyeadhimisha hafanyi makosa, lakini pia anayeadhimisha kwa ufunuo wa kutafakari ufufuko wake, pia hakosei, hivyo huu ni mfano wa pokeo lisilo la hatari.
Na mfano wa mapokeo ambayo ni hatari na yapo kinyume kabisa na Biblia, ni yale yanayofanyika ndani ya ukatoliki, kama kuadhimisha Ekaristi pamoja na ibada za watakatifu (Hizo hazipo kabisa ndani ya Biblia), na ni hatari kiroho, kwani kuabudu sanamu au kuitumikia Biblia imekataza jambo hilo katika Kutoka 20:4-5.
Pia mfano wa pokeo lingine lililo baya na hatari kiroho ni ubatizo wa watoto.. Pokeo hili ni maarufu sana lakini ni hatari sana, Kwasababu kwenye Biblia hamna mahali popote watoto wadogo walibatizwa, bali tunaona tu waliwekewa mikono na Bwana Yesu.
Sumu ya mapokeo mabaya ni ile Bwana Yesu aliyoionyesha katika Marko 7:7-13, kuhusu “Heshima kwa mzazi”
Marko 7:7 “Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu,
8 Ninyi mwaiacha amri ya Mungu, na kuyashika MAPOKEO YA WANADAMU.
9 Akawaambia, Vema! Mwaikataa amri ya Mungu mpate kuyashika mapokeo yenu.
10 Maana Musa alisema, Waheshimu baba yako na mama yako, na, Amtukanaye babaye au mamaye kufa na afe.
11 Bali ninyi husema, Mtu akimwambia babaye au mamaye, Ni Korbani, yaani, wakfu, kitu changu cho chote kikupasacho kufaidiwa nacho, huwa basi;
12 wala hammruhusu baada ya hayo kumtendea neno babaye au mamaye;
13 huku mkilitangua neno la Mungu kwa MAPOKEO YENU mliyopokeana; tena mwafanya mambo mengi yaliyo sawasawa na hayo”.
Kwahiyo kwa hitimisho ni kwamba tunaweza kuishi bila mapokeo na bado tukamwona Mungu na ni vizuri zaidi kuishi bila mapokeo kwani mapokeo mengi yanawafanya watu kuwa mateka wa elimu za uongo, ndivyo Biblia inavyosema..
Wakolosai 2:8 “Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo.
9 Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili”.
Bwana atusaidie.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Je! taratibu za kufunga ndoa yaani harusi] ni agizo la Mungu au ni mapokeo tu ya kibinadamu?
TOFAUTI KATI MAASKOFU, MASHEMASI, WAZEE WA KANISA NI IPI?
KAMA MKRISTO NI LAZIMA UWE NA DESTURI HII.
Je ni Wokovu gani Simeoni aliouona? (Luka 2:30)
SWALI: Nini maana ya ‘laana ya torati’, ambayo Kristo alikuja kutukomboa kutoka katika hiyo?
Wagalatia 3:13
[13]Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti;
JIBU:
Mungu alimpa Musa Torati ambayo ndani yake haikuwa na baraka tu pale Mtu alipoitii, bali pia ilikuwa na laana nyuma yake pale mtu alipoiasi..
Sasa hizo laana ndio ziliitwa “laana ya torati”, yaani adhabu, hukumu na kutengwa na uso wa Mungu.
Ukisoma Kumbukumbu la torati sura ya 27 – 28 inaeleza kwa undani juu ya baraka na laana mtu azipatapo pale anapoitii Au kunapoikataa torati..
Kwamfano
Kumbukumbu la Torati 27:26 inasema;
[26]Na alaaniwe asiyeyaweka imara maneno ya torati hii kwa kuyafanya. Na watu wote waseme, Amina.
Hivyo wanadamu, wote hawakufanikiwa kuzishika amri zile, na sheria Mungu alizowapa, na matokeo yake ikiwa ni laana juu ya kila mtu.
Warumi 3:10-12,23
[10]kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Hakuna mwenye haki hata mmoja. [11]Hakuna afahamuye; Hakuna amtafutaye Mungu.
[12]Wote wamepotoka, wameoza wote pia; Hakuna mtenda mema, la! Hata mmoja…
[23]kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;
Sasa Kristo alipokuja, alifanywa laana kwa ajili yetu..sawasawa na hiyo Wagalatia 3:13, maana yake aliichukua hukumu yetu ya makosa kwa kupigwa na kufa kwake pale msalabani ili sisi tuponywe..
Warumi 8:1
[1]Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.
Ndio maana mtu yeyote ambaye hajamwamini Kristo bado yupo Chini ya hukumu na adhabu, kwasababu atataka kumpendeza Mungu kwa kutegemea tu nguvu zake mwenye, na hatimaye mwisho wa siku atashindwa..kwasababu hakuna mwanadamu aliyewahi kuishika torati yote…
Atasema haibi, hasemi uongolakini wakati huo huo ana mawazo mabaya, yote hayo ni makosa na dhambi…na mshahara wa dhambi sikuzote ni mauti..(Warumi 6:23)
Umeona umuhimu wa Yesu maishani mwetu?
Unasubiri nini usimwamini, akutoe katika laana hiyo, ili uhesabiwe bure kwa neema yake?
Mpokee sasa akuokoe…bofya hapa kwa mwongozo wa sala hiyo…
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
SWALI: Nini maana ya Mithali 21:3
[3]Kutenda haki na hukumu Humpendeza BWANA kuliko kutoa sadaka.
JIBU:
Mstari huo unatufundisha mambo ambayo Mungu huvutiwa nayo zaidi…
Mungu hupendezwa zaidi na sisi tunapoishi maisha ya haki, tunatenda mema, tunawajali wengine, tunaishi sawasawa ni viwango vyake vya kiroho hapa duniani..kwake hiyo ni bora zaidi ya sadaka zetu tumtoleazo.
Sadaka huwakilisha mambo yote Ya kidini tunayoweza kumfanyia Mungu, mfano ibada, fedha, mifungo, maombi, kuhubiri, kuimba n.k
Bwana huvutiwa zaidi na mioyo na tabia zetu, na sio zile Ibada za nje tu..
Haimaanishi kuwa hapendezwi na hivyo vitu hapana…bali hivyo vifanywe baada ya kutii kwanza..
Tunaona jambo kama hilo amelisisitiza sehemu nyingi kwenye maandiko; Tukianzia kwa Sauli alimwambia, hivyo;
1 Samweli 15:22
[22]Naye Samweli akasema, je! BWANA huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya BWANA? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu.
Mika 6:6-8 inasema;
[6]Nimkaribie BWANA na kitu gani, na kuinama mbele za Mungu aliye juu? Je! Nimkaribie na sadaka za kuteketezwa, na ndama za umri wa mwaka mmoja?
[7]Je! BWANA atapendezwa na elfu za kondoo waume, au na elfu kumi za mito ya mafuta? Je! Nimtoe mzaliwa wangu wa kwanza kwa kosa langu, mzao wa mwili wangu kwa dhambi ya roho yangu?
[8]Ee mwanadamu, yeye amekuonyesha yaliyo mema; na BWANA anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako!
Soma pia..
Isaya 1:11-17 – Inasema…Bwana huchukizwa na sadaka za watu wanaishi katika dhambi
Hivyo ni lazima tujiulize Je! tunatenda haki kwa wengine?
Je! Tunatembea kwa unyenyekevu mbele ya Mungu wetu?
Je! tunamtii Mungu, kuliko vitu vingine vyovyote?
Je tunawahurumia wengine…?
Mambo kama haya ndio yenye uzito zaidi kwa Mungu.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Maana ya 2Wakorintho 9:11 mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote
katika agano jipya wapo watu wanne ambao wametajwa kwa jina la Yohana.. Wawili kati ya hao ndio hujulikana sana…ambao ni Yohana mbatizaji na Yohana mtume wa Yesu ..hawa wametajwa Sehemu nyingi katika agano jipya..
Mfano vifungu ambavyo utamsoma Yohana mbatizaji ni kama vifuatavyo:
Hivi ni vifungu vinavyomtaja Yohana Mtume;
Na ndiye mwandishi wa injili ya Yohana, pia na nyaraka zote tatu (1,2, 3 Yohana, ) pamoja na kitabu cha Ufunuo.
Yohana mwingine ni Marko, ndiye mwandishi wa kitabu cha Marko,..anatajwa katika kitabu cha Matendo 12:12, 13:5, Wakolosai 4:10
Na ndiye aliyekuwa Msaidizi wa Paulo na Barnaba katika ziara zao za kupeleka injili kwa mataifa.
Yohana mwingine ni Baba wa Simoni Petro anatajwa katika;
Yohana 1:42
[42]Akampeleka kwa Yesu. Naye Yesu akamtazama, akasema, Wewe u Simoni, mwana wa Yohana; nawe utaitwa Kefa (tafsiri yake Petro, au Jiwe).
Soma pia Yohana 21:15-27
Hivyo jumla Yao ni wanne…
Je ungependa kufahamu Zaidi watu wengine Katika biblia? Kama ni ndio basi jiunge tazama chini kwa makala nyingine..
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Maherodi walikuwa ni akina nani, Na kazi yao ilikuwa ni ipi?
Kwanini nguo za waliomwua Stefano ziwekwe miguuni mwa Sauli?.