Jibu: Mpaka kufikia mwaka 2024 biblia imetafsiriwa kwa lugha 756, hivyo kuna tafsiri Zaidi ya 756 mpaka sasa duniani kote.
Sasa kwa asili biblia iliandikwa kwa lugha kuu tatu, ambazo ni KIEBRANIA (Agano la Kale), lugha ya KIARAMU (Sehemu za Agano la kale na jipya) pamoja na lugha ya KIYUNANI AU KIGIRIKI (Agano jipya), Hizo ndizo lugha kuu tatu zilizoandikia biblia ya kwanza, na haikuandikwa kwa lugha ya kiingereza wala Kiswahili, wala lugha nyingine yoyote tofauti na hizo tatu.
Sasa kuna tafsiri nyingi za biblia siku hizi za leo kwasababu kadhaa, na sababu hizo zipo tatu (3)..
1)Tofauti za lugha, 2) Maendeleo ya Lugha 3) Mitazamo ya kidhehebu.
Hizo ndizo sababu kuu tatu,.. hebu tutazame moja baada ya nyingine.
1. Tofauti za Lugha
Kwasababu biblia kwa asili iliandikwa kwa lugha ya Kiebrania, Kiaramu, na Kigiriki. Zipo jamii za watu zisizozungumza lugha hizo, na kwasababu ni lazima watu wote, ulimwenguni kote walisikie Neno la Mungu, ni lazima tafsiri iwepo,….na watalisikiaje na kulielewa wasipolisikia kwa lugha yao na kulisoma kwa lugha yao?..
Hiyo ndiyo ikawa sababu ya Biblia ya kwanza yenye lugha hizo tatu, kutafsiriwa kwa lugha nyingine mbali mbali ikiwemo lugha yetu ya Kiswahili, Hebu tafakari laiti isingetafsiriwa kwa lugha yetu, biblia kwetu ingekuwa ngumu kiasi gani leo?.. Hivi ilivyo tu tayari ni ngumu!… vipi kama tungekuwa tunaisoma kwa lugha nyingine?? Si hali ingekuwa mbaya Zaidi??…kwasababu ingetupasa tukajifunze kwanza lugha hizo tatu, jambo ambalo lingekuwa gumu sana kwa wengi!.
Kwasababu ya shida hiyo, ndipo Bwana MUNGU wetu kupitia Roho wake Mtakatifu alitangulia kuachilia uwezo wa lugha na tafsiri zake ile siku ya Pentekoste, (soma Matendo 2) kuonyesha kuwa sasa Neno linapaswa lihubiriwe kwa watu wote na lugha zote, na ndipo zikaja tafsiri hizo.
2. Maendeleo ya Lugha.
Hii ni sababu ya pili ya uwepo wa tafsiri nyingi, utaona tayari kuna tafsiri moja ya lugha husika, tuchukue mfano lugha ya Kiswahili, halafu baada ya muda unaona kuna tafsiri nyingine zinaongezeka tofauti na hiyo ya kwanza na tena kwa lugha hiyo hiyo ya Kiswahili.
Sasa hiyo inatokana na kukua kwa lugha, kwani lugha siku zote inakuwa (inaongezeka misemo na maneno), na kwasababu hiyo basi tafsiri nyingi zinatokea na bado zitaendelea kutokea,
3. Mitazamo ya Kidhehebu na Theolojia
Kutokana na ongezeko la Madhehebu mengi yenye itikadi zinazotofautiana, imechangia pakubwa kutokea kwa tafsiri mpya kila siku kulingana na misimamo ya dhehebu husika. Kwani tafsiri nyingine zinaegemea mapokeo ya dhehebu hilo, kwamfano utaona dhehebu la katoliki linatumia biblia yenye vitabu vingine vya Deuterokanoni, ambavyo vinafanya jumla ya vitabu 72, tofauti na Biblia ya asili yenye vitabu 66.
Zipo na sababu nyingine ndogo ndogo ikiwemo mbinu za kutafsiri, kwamba wengine wanatafsiri neno kwa neno, na wengine wanatafsiri sentensi nzima na kuleta maana ya ujumla, na sababu nyingine ni mapendekezo ya lugha laini kwaajili ya watoto, zenye kutumia tafsida na zisizotumia lugha za ukali na kuogopesha. Hizi zote ndizo zinazochangia ongezeko la tafsiri za biblia kila siku.
Lakini swali je! Ni tafsiri ipi iliyo sahihi na isiyo na sumu kwa mkristo?
Mara nyingi kitu cha asili kinakuwa ni bora kuliko kile kilichochujwa Zaidi.. Tafsiri iliyo bora na yenye kufaa kuliko zote ni ile yenye lugha tatu (Kiebrania, Kiaramu na kiyunani), lakini kwasababu ni ngumu sisi kukijua kiyunani, na kiebrania kifasaha, basi tafsiri inayofuata kwa Ubora ni ile ya kwanza kabisa iliyotafsiriwa katika ugha yetu husika, kwamfano kwa sisi tunaozungumza Kiswahili, tafsiri ya kwanza kabisa na bora kwa lugha yetu ni ile ya SWAHILI UNION VERSION (SUV), ambayo ndiyo inayotumika sasa kwa wingi, inayoanza na…
Mwanzo 1:1 “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. 2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.”
Mwanzo 1:1 “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.
2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.”
Hiyo ndiyo tafsiri iliyo bora, tafsiri nyingine zinazofuata baada ya hapo faida yake inakuwa ni ndogo ukilinganisha na hasara…kwani zinabadilishwa maana na zinatengenezwa kwa kuegemea dini Fulani, na katika lugha nyingine ni hivyo hivyo, ile ya kwanza ni bora Zaidi kuliko zilizoendelea kufuata.
Kwahiyo kwa hitimisho, Tafsiri sahihi yenye kumfaa mtu ni ile ya kwanza (yenye kiebrania, kiyunani na kigiriki) ikiwa mtu atakuwa ana uwezo wa kuzielewa lugha hizo, lakini kama hana uwezo basi ile tafsiri ya kwanza kabisa iliyotafsiriwa kwa lugha yake, ni bora Zaidi.
Je umempokea Bwana YESU kikweli kweli?
Je unajua kuwa tunaishi katika siku za kurudi kwa pili kwa Bwana YESU na unyakuo upo karibu?, Je unajua kuwa kama huna Roho Mtakatifu huwezi kuiona mbingu (Warumi 8:9).. sasa kama bado hujaokoka unasubiri nini?,
Warumi 13:11 “Naam, tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini 12 Usiku umeendelea sana, mchana umekaribia, basi na tuyavue matendo ya giza, na kuzivaa silaha za nuru. 13 Kama ilivyohusika na mchana na tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu. 14 Bali mvaeni Bwana Yesu Kristo, wala msiuangalie mwili, hata kuwasha tamaa zake”.
Warumi 13:11 “Naam, tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini
12 Usiku umeendelea sana, mchana umekaribia, basi na tuyavue matendo ya giza, na kuzivaa silaha za nuru.
13 Kama ilivyohusika na mchana na tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu.
14 Bali mvaeni Bwana Yesu Kristo, wala msiuangalie mwili, hata kuwasha tamaa zake”.
Maran atha.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Print this post
SWALI: Naomba kufahamu Biblia unapozungumzia kuhusu kupewa jina jipya inamaanisha nini?
JIBU: Kazi ya jina sio tu kumtambulisha au kumtofautisha mtu mmoja na mwingine. Bali jina linasimama pia kueleza Wasifa wa mtu,
Hivyo jina la mtu linapobadilika, aidha Wasifa pia hubadilika.
Kwamfano Ibrahimu alipobadilishwa jina kutoka Abramu na Kuwa Ibrahimu ni kwasababu alikuwa anaenda kuwa Baba wa mataifa mengi.(Mwanzo 17:5)
Vilevile Sarai kuitwa Sara. Ni kwasababu anaenda kuwa mama wa mataifa mengi..(Mwanzo 17:15)
Sauli kuwa Paulo kwasababu anaenda kuwa mtume kwa mataifa.(Matendo 13:9)
Vivyo hivyo tunaona Mungu katika maandiko Akijitambulisha kwa majina mbalimbali, lengo sio kuonyesha uzuri au upekee wa majina yake hapana bali kutambulisha wasifa wake.
Kwamfano alipojitambulisha kama Yehova rafa, alisimama kama Mungu mponyaji..Yehova yire Mungu atupaye, Yeshua(Yesu), kama Mungu atuokoaye.
Tukirudi kwa wakati wa sasa Biblia Inatuonyesha kuwa Kristo atakaporudi mara ya pili atakuja na jina lingine jipya. Ambalo ndio tunangojea kuona utukufu wake, mamlaka yake na nguvu zake.
Ufunuo wa Yohana 3:12
[12]Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya.
Jina hili halitakuwa Yesu,tulitumialo sasa ambalo linawasifa wa wokovu, lililojikita katika kiwakomboa na kuwafungua wanadamu katika mauti na vifungo vya kila namna.
Lakini hilo linalokuja litakuwa ni jina lenye uweza Mwingi, la kifalme, la kiutawala zaidi. Wakati huo Kristo hataonekana tena kama mwanakondoo mpole, asimamaye kutuombea kwa Baba N.k..hapana ataonekana katika taswira mpya kabisa ya kifalme, na zaidi ya hapo (Ufunuo 19:11-16), sawasawa na hilo jina lake litakavyokuwa.
Ndio maana kuna umuhimu sana kuokoka sasa, angali neema na msamaha upo katika jina la YESU, kwasababu atakaporudi mara ya pili,na jina jipya hatajua kusamehe ni nini, bali mambo mengine mapya yatakuwa wanaendelea..Usipookoka leo hakuna wokovu siku ya mwisho.
Vilevile wale watakaoshinda Kristo ana ahidi kuwapa majina mapya ya kipekee, ambayo yatawanafisisha kipekee mbele ya Kristo.
Ufunuo wa Yohana 2:17
[17]Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea.
Ndugu Utukufu Unaokuja wa Kristo ni mkuu sana, ni heri ukose vyote sasa, lakini usikose mbingu Mpya na nchi mpya na ile Yerusalemu mpya ishukayo kutoka kwa Baba mbinguni.
Siku hizi ni za mwisho, unyakuo umekaribia sana. Mambo ya umilele yanakaribia kuanza. Bado unaendelea kung’ang’ana na ya kidunia? tubu leo mgeukie Kristo.
Amen.
Majina mbalimbali ya Mungu na maana zake.
JE NI LAZIMA KUBADILISHA JINA BAADA YA KUOKOKA?
Nini maana ya “Heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi”?
SWALI: Je mtu anaweza akawa hajaokoka akaombea mtu na Pepo likamtoka, na pia mtu anaweza akawa ameokoka akaombea mtu na pepo lisitoke ?
JIBU: Kuhusu swali la kwanza linalosema je mtu anaweza akawa hajaokoka kisha akaenda kuombea mtu mwenye pepo na hatimaye likamtoka?
Jibu ni la!, haiwezekani mtu ambaye hajaokoka, akawa na uwezo wa kutoa pepo, kwasababu pale alipo yupo chini ya vifungo vya ibilisi, haiwezekani akaenda kumfungua mtu ambaye ni mfungwa mwenzake, inahitaji mtu aliye huru ndio aweze kufanya hivyo.
Bwana Yesu alisema…
Marko 3:23-27
[23]Akawaita, akawaambia kwa mifano, Awezaje Shetani kumtoa Shetani? [24]Na ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, ufalme huo hauwezi kusimama; [25]na nyumba ikifitinika juu ya nafsi yake, nyumba hiyo haiwezi kusimama. [26]Na kama Shetani ameondoka juu ya nafsi yake, akafitinika, hawezi kusimama, bali huwa na kikomo. [27]Hawezi mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu, na kuviteka vitu vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu; ndipo atakapoiteka nyumba yake.
[23]Akawaita, akawaambia kwa mifano, Awezaje Shetani kumtoa Shetani?
[24]Na ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, ufalme huo hauwezi kusimama;
[25]na nyumba ikifitinika juu ya nafsi yake, nyumba hiyo haiwezi kusimama.
[26]Na kama Shetani ameondoka juu ya nafsi yake, akafitinika, hawezi kusimama, bali huwa na kikomo.
[27]Hawezi mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu, na kuviteka vitu vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu; ndipo atakapoiteka nyumba yake.
Ni hatari huyo mtu akijaribu kufanya hivyo, kwasababu anaweza kukutana na madhara kama yaliyowakuta wale wana wa Skewa.(Matendo 19:13-16).
Kuhusu swali la pili linalouliza Je mtu ambaye ameokoka anaweza akaombea na pepo lisitoke?
Jibu ni ndio Ikiwa mtu huyo anakiwango kidogo cha imani, si mapepo yote yanaweza yakatoka, kwasababu mashetani yanatofautiana kimadaraja (Mathayo 12:43-45), yapo yenye nguvu kubwa ya ukinzani, mengine huitwa wakuu wa giza, mengine wafalme na wenye mamlaka. (Waefeso 6:12)
Hivyo inahitaji nguvu zaidi za kiimani ambazo zinakuja kwa njia ya mifungo na maombi.
Ndio maana mitume kuna mahali walitoa kweli pepo wengi lakini kuna mahali hawakuweza kwasababu ya uhaba wa maombi. (Mathayo 17:14-21)
Lakini uhalisia ni kuwa mtu yeyote aliyeokoka, haijalishi amedumu sana katika wokovu au ni mchanga. Anayo mamlaka ndani yake ya kutoa pepo lolote lile, isipokuwa anahitaji pia na maombi ile mengine yasishindikane kwake.
MAPEPO YANATAFUTA HIFADHI NDANI YAKO KWA BIDII SANA.
MWANAMKE, USIFUNGUE MLANGO WA MAPEPO KUKUINGIA!.
MAPEPO NI NINI?
WhatsApp
Swali: Maana ya Madhali ni nini kama ilivyotumika hapo katika Zaburi 21:11
Jibu: Turejee…
Zaburi 21:11 “Madhali walinuia kukutenda mabaya, Waliwaza hila wasipate kuitimiza”.
Neno “Madhali” limeonekana mara moja tu kwenye biblia yote, na maana yake ni “Ingawa” Hivyo Kiswahili kingine cha neno “Ingawa” ni “Madhali” …
Kwahiyo maandiko hayo yanaweza kuweleweka pia hivi…“Ingawa walinuia kukutenda mabaya, Waliwaza hila wasipate kuitimiza”.
Madhara yanayonuiwa na watu wabaya, ikiwa tupo ndani ya Kristo, hayataweza kushinda juu yetu, haijalishi yataonekana yamekomaa kiasi gani.
Je umempokea BWANA YESU?..
Unao wokovu ndani yako?
Waebrania 10:37 “Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, Yeye ajaye atakuja, wala hatakawia”.
Maran atha
Swali: Tunasoma Simeoni alipomwona mtoto YESU, Alikiri kuuona Wokovu wa MUNGU, sasa swali ni Wokovu gani huo alioupata?
Jibu: Tuanzie ule mstari wa 25 ili tuweze kuelewa vyema…
Luka 2:25 “Na tazama, pale Yerusalemu palikuwa na mtu, jina lake Simeoni, naye ni mtu mwenye haki, mcha Mungu, akiitarajia faraja ya Israeli; na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake. 26 Naye alikuwa ameonywa na Roho Mtakatifu ya kwamba hataona mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana. 27 Basi akaja hekaluni ameongozwa na Roho; na wale wazazi walipomleta mtoto Yesu ndani, ili wamfanyie kama ilivyokuwa desturi ya sheria, 28 yeye mwenyewe alimpokea mikononi mwake, akamshukuru Mungu, akisema, 29 Sasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako, Kwa amani, kama ulivyosema; 30 KWA KUWA MACHO YANGU YAMEUONA WOKOVU WAKO, 31 Uliouweka tayari machoni pa watu wote; 32 Nuru ya kuwa mwangaza wa Mataifa, Na kuwa utukufu wa watu wako Israeli”
Luka 2:25 “Na tazama, pale Yerusalemu palikuwa na mtu, jina lake Simeoni, naye ni mtu mwenye haki, mcha Mungu, akiitarajia faraja ya Israeli; na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake.
26 Naye alikuwa ameonywa na Roho Mtakatifu ya kwamba hataona mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana.
27 Basi akaja hekaluni ameongozwa na Roho; na wale wazazi walipomleta mtoto Yesu ndani, ili wamfanyie kama ilivyokuwa desturi ya sheria,
28 yeye mwenyewe alimpokea mikononi mwake, akamshukuru Mungu, akisema,
29 Sasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako, Kwa amani, kama ulivyosema;
30 KWA KUWA MACHO YANGU YAMEUONA WOKOVU WAKO,
31 Uliouweka tayari machoni pa watu wote;
32 Nuru ya kuwa mwangaza wa Mataifa, Na kuwa utukufu wa watu wako Israeli”
Sasa hapo hajasema AMEUPATA WOKOVU..La! bali anasema “MACHO YANGU YAMEUONA WOKOVU”.. kuuona wokovu na kuupata wokovu ni vitu viwili tofauti…
Wokovu wa Mungu unapatikana kupitia mmoja tu, naye ni YESU KRISTO (Matendo 4:12),..Baada ya YESU kusulibiwa ndipo watu wakaanza kuupata wokovu, lakini kabla ya hapo waliusikia na kuuona tu,…waliousikia ni manabii wa kale na watu wote wa agano la kale, na waliouona ni watu waliokuwepo kipindi BWANA YESU anazaliwa, na walioupata ni wote waliomwamini baada ya kufufuka kwake.
Sasa utauliza vipi waliokufa katika haki wakati wa agano la kale, je hawakupata wokovu kabisa katika kipindi chao?… Jibu ni kwamba baada ya kufa kwao wokovu wao ulikuwa haujakamilika, lakini KRISTO aliposhuka kuzimu na kuchukua mamlaka yote ya walio hai na waliokufa, ndipo wokovu wao ukakamilika (maana yake wakaupata wokovu).
1Petro 1:10 “Katika habari ya wokovu huo manabii walitafuta-tafuta na kuchunguza-chunguza, ambao walitabiri habari za neema itakayowafikia ninyi. 11 Wakatafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, ambaye alitangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwako baada ya hayo. 12 Wakafunuliwa ya kuwa si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yenu walihudumu katika mambo hayo, ambayo sasa yamehubiriwa kwenu na wale waliowahubiri ninyi Injili kwa Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni. Mambo hayo malaika wanatamani kuyachungulia”.
1Petro 1:10 “Katika habari ya wokovu huo manabii walitafuta-tafuta na kuchunguza-chunguza, ambao walitabiri habari za neema itakayowafikia ninyi.
11 Wakatafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, ambaye alitangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwako baada ya hayo.
12 Wakafunuliwa ya kuwa si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yenu walihudumu katika mambo hayo, ambayo sasa yamehubiriwa kwenu na wale waliowahubiri ninyi Injili kwa Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni. Mambo hayo malaika wanatamani kuyachungulia”.
Kwahiyo Simoni aliuona Wokovu, kwakuwa anayebeba wokovu (YESU KRISTO) yupo pale.
Na wote tunaomwamini sasa, tunapokea wokovu wa roho zetu.
Je umempokea YESU?… Je umeoshwa dhambi zako kwa damu yake?
Matendo 4:12 “Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo”
FAHAMU KANUNI ZA KUZISUBIRIA AHADI ZA MUNGU?
Nini tofauti ya haya maneno. 1) KUOKOKA, 2) WOKOVU, 3) KUONGOKA.?
Kama tunaokolewa kwa neema kwanini wokovu tuupate kwa nguvu?
UKIAMINI NA UKIMKIRI YESU KWA KINYWA CHAKO, UTAOKOKA.
Je mtu anaweza kupoteza wokovu?
Musa alikuwa na sababu kadha wa kadha za yeye kufanye vile, ikiwemo
Kutoka 3:11
[11]Musa akamwambia Mungu, Mimi ni nani, hata niende kwa Farao, nikawatoe wana wa Israeli watoke Misri?
Musa aliogopa, kwenda kuwahubiria watu juu ya Mungu Ambaye hakulijua jina lake, kwani zamani zile, miungu yote ilifahamika kwa majina, hivyo alijiona kama kwenda kuwaambia watu habari za Mungu asiyejulikana jina lake, ni kama anawafedhehi.
Kutoka 3:13 Musa akamwambia Mungu, Tazama, nitakapofika kwa wana wa Israeli, na kuwaambia, Mungu wa baba zenu amenituma kwenu; nao wakaniuliza, Jina lake n’nani? Niwaambie nini?
Kutoka 4:1
[1]Musa akajibu akasema, Lakini, tazama, hawataniamini, wala hawataisikia sauti yangu; maana watasema, BWANA hakukutokea.
Kwasababu alikuwa hana ishara yoyote ya ki-Mungu ndani yake.
Kutoka 4:10
[10]Musa akamwambia BWANA Ee Bwana, mimi si msemaji, tokea zamani, wala tokea hapo uliposema na mtumishi wako; maana mimi si mwepesi wa kusema, na ulimi wangu ni mzito.
Pamoja na Mungu kumwakikishia kuwa atakuwa naye na kumsaidia lakini Musa bado akakataa, ndipo Mungu akaghadhibika na kumletea nduguye Haruni, kama msaidizi wake.
Jambo ambalo halikuwa mpango wa awali wa Mungu, kwani uongozi wa Haruni hakuwa kusudi kamilifu la Bwana. Sababu kadha wa kadha zilizowapelekea wana wa Israeli kupata adhabu, zilikuwa ni pamoja na uongozi dhaifu wa Haruni. Utakumbuka wakati Musa amepanda juu mlimani kuchukua zile mbao mbili za amri 10, Haruni aliachiwa uongozi kwa muda, watu walipomfuata Kwa ajili ya hatma zao, akasikiliza mapendekezo yao akawaundia sanamu ya ndama ili waiabudu, ikapelekea Mungu kuwaangamiza wana wa Israeli wengi sana, (Kutoka 32:1-6) mzizi huo ni kutokana na kutokutii kwa Musa, halikadhalika sababu ya Musa kutoiona nchi ya ahadi ilichangiwa pia na uongozi hafifu wa Haruni, kwani kule Meriba kosa alilofinya Musa la kuchukua utukufu wa Mungu, alihusika na Haruni pia. (Hesabu 20:10-12)
Hivyo ni wazi kama angekuwa na imani na Mungu, mengi yasingetokea mbeleni. Hata wakati huu wa sasa, wengi wetu tumejikuta katika machaguzi ya pili ya Mungu kwasababu tu, ya kumpotezea imani, kuwa anaweza kutenda kusudi lake lote hata katika Madhaifu yetu.
Mwamini Mungu mtegemee yeye tu.
Shikilia vifungu hivi vikusaidie.
Mithali 3:5
[5]Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;
Isaya 6:8
[8]Kisha nikaisikia sauti ya Bwana, akisema, Nimtume nani, naye ni nani atakayekwenda kwa ajili yetu? Ndipo niliposema, Mimi hapa, nitume mimi.
2 Timotheo 1:7
[7]Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.
Kwanini Mungu alimchagua Musa, na si mtu mwingine?
Je ni sala gani inahitajika kabla ya kumchinja mnyama katika ukristo?
Je maombi ya mlimani yana ulazima wowote kwa mkristo?
Mungu hakumchagua Musa kwasababu ya wema, au kipawa, au ujuzi fulani aliokuwa nao tofauti na wengine. Hapana almchagua ili ‘kutumiza kusudi lake la kuchagua’ ambalo tunalisoma kwa urefu katika (Warumi 9:11-17). Linalomaanisha Mungu humchagua mtu na kumfanya awe kama anavyotaka mwenyewe, na sio kwa jinsi Yule mtu atakavyo. Kwamfano alimchagua Farao, kisha akamwekea moyo mgumu,ili atimize kusudi lake mwenyewe, kujichotea utukufu kwa mapigo yale kumi,aliyoyaachia kwa wamisri, vivyo hivyo na kwa Musa alimchagua na kumpa neema ile kubwa ya hofu ya Ki-Mungu na upole ili atimize kusudi lake la kuwakomboa wana wa Israeli.
Lakini hakuwa na tendo lolote jema alilowahi kutenda lililomshawishi Mungu amchague yeye tofauti na wengine.
Na ndivyo anavyofanya hata sasa kwa wanadamu wote. Tunaokolewa na kutumiwa na Mungu kwa neema tu, na si kwasababu ya matendo Fulani mema tuliyowahi kumtendea Mungu.
Nini tofauti ya Majira na Wakati?
Tofauti ya kazi ya Damu ya Yesu na Jina la Yesu ni ipi?
NAAM, HATA WABAYA KWA SIKU YA UBAYA.
Swali: Je sisi wakristo tunapaswa tuombe sala gani kabla kumchinja mnyama?, maana Imani nyingine tunaona kabla kuchinja wanatanguliza sala.
Jibu: Katika biblia hatujapewa maagizo yoyote ya kuomba sala, au kukiri maneno Fulani kabla ya kumchinja mnyama. Ndio zipo Imani zinazoelekeza kufanya hivyo, lakini si Biblia takatifu.
Maagizo tu yaliyopo katika biblia ni kushukuru kabla ya kula..lakini kupiga sala kabla ya kuchinja hatujapewa kwani hatuendi kutoa sadaka kwa miungu bali ni kwaajili ya kitoweo.
Katika agano la kale, wanyama waliombewa kabla ya kuchinjwa iwapo wanaenda kutolewa kama sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana (dhabihu).
Walawi 4:32 “Naye akileta mwana-kondoo kuwa sadaka ya dhambi, ataleta wa kike mkamilifu. 33 Naye ataweka mkono wake kichwani mwake sadaka ya dhambi, kisha atamchinja awe sadaka ya dhambi, mahali hapo wachinjapo sadaka ya kuteketezwa”.
Walawi 4:32 “Naye akileta mwana-kondoo kuwa sadaka ya dhambi, ataleta wa kike mkamilifu.
33 Naye ataweka mkono wake kichwani mwake sadaka ya dhambi, kisha atamchinja awe sadaka ya dhambi, mahali hapo wachinjapo sadaka ya kuteketezwa”.
Lakini katika agano jipya dhabihu ya mwili wa YESU ilishatolewa, (hiyo ndio dhabihu kamilifu)…sasa wanyama wanachinjwa kwaajili ya vitoweo, na si kwaajili ya sadaka.. na hakuna sala yoyote inayotangulia, na hata wanaoomba hizo dua bado kuna viumbe vitawafunga katika sheria hiyo, kwamaana samaki au dagaa au wadudu kama kumbikumbi au senene unawaombeaje dua kabla ya kutoa uhai wao?… utaombea dagaa mmoja mmoja??..ni jambo lisilowezekana vinginevyo hatutakula kabisa.
Kwahiyo kwa hitimisho ni kwamba hakuna sala inayotangulia kabla ya kuchinja au kuutoa uhai wa kiumbe chochote kwaajili ya chakula.. Na kufahamu kwa urefu kama wakristo anaruhusiwa kula nyama ya mnyama aliyechinjwa kwa dua, basi fungua hapa >>UKWELI KUHUSU UISLAMU Sehemu ya Pili: (Jiwe/Jabali la Kaaba).
SWALI: Yusufu aliwezaje kutafsiri ndoto? Je ni kwa hekima aliyokuwa nayo au kwa kuangalia ishara fulani, au kwa usomaji wa vitabu, au kwa saikolojia?
JIBU: Biblia inatuonyesha sifa kuu, ya Yusufu iliyokuwa ndani yake ni uwezo wa kutafsiri ndoto.
Lakini swali linaloulizwa je uwezo huo alitolea wapi, ulikuwa ndani yake mwenyewe au ulitoka kwingine.
Tukisoma Mwanzo 41:15, tunaweza kupata majibu;
Farao akamwambia Yusufu, Nimeota ndoto, wala hakuna awezaye kunifasiria; nami nimesikia habari zako, ya kwamba, usikiapo ndoto, waweza kuifasiri.16 Yusufu akamjibu Farao, akisema, Si mimi; Mungu atampa Farao majibu ya amani.
Hapo Yusufu anasema si mimi, Mungu atampa Farao majibu. Kuonyesha kuwa uwezo huo ulitoka kwa Mungu wala sio katika akili zake, elimu , saikolojia , au hekima ya kibinadamu.
Alimtegemea Mungu asilimia mia kumfunulia, mfano tu wa Danieli alipokwenda kuomba juu ya tafsiri ya ndoto ya Nebukadreza katika sala akafunuliwa. Ndivyo ilivyokuwa kwa Yusufu, katika kutafsiri ndoto ya Farao, pamoja na za wale watumishi wawili wa mfalme waliokuwa wanahudumu mezani pa mfalme. Hakubuni tu tafsiri kulingana na mazingira, bali alifunuliwa moja kwa moja aidha kwa ndoto au kuona maono.
Lakini ni kwanini Yusufu apokee neema hiyo kirahisi kwa Mungu, tofauti na wengine.
Jibu lipo katika TABIA yake, Ni wazi Roho ya Mungu huvutika sana katika tabia njema ya mtu. Yusufu tangu udogo alijitahidi kujiepusha na tabia zisizofaa, jambo lililopelekea mpaka ndugu zake kumchukia kwasababu alikuwa anatoa siri za mambo yao mabaya, hata alipouzwa kwa akida wa Farao, bado aliendeleza tabia yake ileile, pale mke wa Potifa alipomtamani akakataa, mwishowe akatupwa gerezani. Kwa njia hiyo Yusufu hakuacha kulitunza joto la ROHO ndani yake. Mfano tu wa Danieli naye, ambaye hakutaka kujitia unajisi kwa vyakula vya kifalme, na ndani yake hakukuonekana kosa lolote (Danieli 6:3).
Akashuhudiwa na mfalme kuwa Roho njema sana, na iliyo bora inakaa ndani yake.
Danieli 5:12 kwa kuwa roho njema kupita kiasi, na maarifa, na ufahamu, na uwezo wa kufasiri ndoto, na kufunua maneno ya fumbo, na kufungua mafundo, zilionekana katika Danieli huyo, ambaye mfalme alimwita Belteshaza. Basi na aitwe Danieli, naye ataionyesha tafsiri.
Hivyo ili na sisi tushiriki sehemu bora na njema za vipawa mbalimbali vya Roho Mtakatifu, hatuna budi kujijenga kimwenendo, katika maisha matakatifu yampendezayo Mungu.
Je! habari ya Yusufu, inabeba ujumbe gani kwa agano jipya?
KWA KUWA ROHO BORA ILIKUWA NDANI YAKE.
WALA HAKUSIMAMA MTU PAMOJA NAYE, YUSUFU ALIPOJITAMBULISHA KWA NDUGUZE
JIBU: Safina ya Nuhu ilikuwa ni mfano wa Meli kubwa iliyojengwa katika deka tatu, ambayo vipimo vyake vilikuwa ni mikono mia tatu urefu wake, na mikono hamsini upana, na mikono thelathini kwenda juu.
Mwanzo 6:13 Mungu akamwambia Nuhu, Mwisho wa kila mwenye mwili umekuja mbele zangu; kwa sababu wameijaza dunia dhuluma, basi nitawaharibu pamoja na dunia.14 Ujifanyie safina ya mti wa mvinje; fanya na vyumba ndani ya safina, ukaifunike ndani na nje kwa lami. 15 Hivi ndivyo utakavyoifanya; mikono mia tatu urefu wa safina, mikono hamsini upana wake, na mikono thelathini kwenda juu kwake.
Ambayo kwa vipimo vya sasa ni sawa na makadirio ya;
> Mita 137 urefu
> Mita 23 upanda
> Mita 14 kimo.
Ukubwa wa ile Safina, kwa sasa tunaweza kuifananisha na hizi meli kubwa za mizigo.
Yapo mambo manne ya kufahamu;
1). Jambo la kwanza ni kuwa hawakuingizwa wengi wengi, bali wawili wawili, na wengine saba saba, hivyo ni idadi ndogo tu ya kila jamii ndio iliyoingizwa.
2) Lakini pia kuna uwezekano Nuhu aliwaingiza wale wadogo wadogo tu, na sio wale wakubwa, Hivyo ikaachilia nafasi ya wanyama wote kujitosheleza ndani ya safina.
3) Tatu alipoambiwa awaingize wanyama kwa “namna” zao, (Mwanzo 6:20). Kwa lugha ya kibiblia si lazima imaanishe kila familia za wanyama ziingie, mfano familia mbalimbali za mbwa, wenye manyoya marefu, wenye asili ya ufupi, wawindaji, n.k. hapana, bali walipoingizwa mbwa, ni namna moja tu, iliwakilisha wote, Na baadaye walipoongozeka waliweza kuonekana wa maumbile tofauti tofauti tena, hilo linawezekana, ni sawa na sisi wanadamu tulitoka katika asili ya baba mmoja na mama mmoja, lakini leo hii kuna waafrika, wazungu, wachina, waarabu n.k. Hivyo ikiwa aliwaingiza kwa njia hiyo basi kisayansi inawezekana kabisa.
4) Lakini hoja ya mwisho iliyo na nguvu kuliko zote, ni kuwa hata kama ni namna zote na familia zao waliingia, bado Mungu anaweza kufanya mambo ambayo mwanadamu hawezi kuyafanya, ikiwa katika uzazi wa mwanaume mmoja Mungu amehifadhi mamilioni ya mbegu za kibinadamu, na ndani ya tumbo la mwanamke mmoja hadi watoto tisa wanakaa kwa ujauzito mmoja. Hivyo hatuwezi kushangaa, Mungu kuvihifadhi viumbe vyote katika meli ile, inayoonekana haijitoshelezi. Kwasababu yeye ni Mungu asiyeshindwa na chochote.
Ni kwa yeye haathiriwi na nafasi ya udogo au ukubwa, kusudi lake litasimama tu. Kwa vile vichache vilivyokuwa kwenye safina, ulimwengu leo umejawa na viumbe vingi na watu wengi. Wengine wanasema mimi nabanwa na muda hivyo siwezi kumtumikia Mungu, mimi nabanwa na masomo hivyo siwezi kufanya kitu kwa Mungu, mimi nimefungwa gerezani, siwezi kulitimiza kusudi lolote la Mungu. Ndugu Neno la Mungu halifungwi.
Ndugu Paulo alifungwa gerezani akazuiwa kwenda kuhubiri injili katika mataifa kama ilivyo desturi yake, lakini akiwa gerezani aliandika nyaraka ambazo mpaka leo hii zinaendelea kuhubiri injili, zaidi hata ya ziara zake.
Amini uweza wote wa Mungu mahali popote ulipo, bila kuathiriwa na mazingira.
NUHU ALIJENGA SAFINA KWA MIAKA MINGAPI?
SAFINA NI NINI?
Mvinje ni mti gani? (Mwanzo 6:14)